<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?>
<!DOCTYPE ThML PUBLIC 
    "-//CCEL/DTD Theological Markup Language//EN"
    "http://www.ccel.org/dtd/ThML10.dtd">
    
<!-- Copyright Christian Classics Ethereal Library -->
<ThML>
<ThML.head>
<generalInfo>
  <description>
	This Bible translation was converted automatically from data
	files made available by the Unbound Bible project.  Book 
	names, introductions, titles, paragraphs, and the like were 
	not available, so standard English names have been used.  
	Therefore this file would benefit from additional work by 
	someone who has access to a print edition.
	</description>
  <pubHistory />
  <comments />
</generalInfo>
<printSourceInfo>
  <published />
</printSourceInfo>
<electronicEdInfo>
  <publisherID>ccel</publisherID>
  <authorID>bible</authorID>
  <bookID>sw</bookID>
  <workID>sw</workID>
  <bkgID>holy_bible_swahili_new_testament_(bible)</bkgID>
  <version>1.0</version>
  <series />
  <editorialComments />
  <revisionHistory>Converted from Unbound Bible text files 2002-12-31</revisionHistory>
  <status />
  <DC>
    <DC.Title>The Holy Bible: Swahili New Testament</DC.Title>
    <DC.Title sub="short">Swahili Bible</DC.Title>
    <DC.Title sub="authTitle">Swahili Bible</DC.Title>
    <DC.Creator sub="Author">Anonymous</DC.Creator>
    <DC.Creator sub="Author" scheme="file-as">Anonymous</DC.Creator>
    <DC.Publisher>Grand Rapids, MI: Christian Classics Ethereal Library</DC.Publisher>
    <DC.Subject scheme="ccel">All; Bible; New Testament</DC.Subject>
    <DC.Subject scheme="LCCN" />
    <DC.Date sub="Created">2002-12-31</DC.Date>
    <DC.Type>Text.Bible</DC.Type>
    <DC.Format scheme="IMT">text/xml</DC.Format>
    <DC.Identifier scheme="URL">/ccel/bible/sw.html</DC.Identifier>
    <DC.Identifier scheme="osisID">Bible</DC.Identifier>
    <DC.Source>The Unbound Bible</DC.Source>
    <DC.Source scheme="URL">http://unbound.biola.edu</DC.Source>
    <DC.Language scheme="ISO639-3">swa</DC.Language>
    <DC.Rights>Public Domain</DC.Rights>
  </DC>
</electronicEdInfo>





<style type="text/css">
</style>

<style type="text/xcss">
</style>


</ThML.head>
<ThML.body>

<div1 title="Title Page" progress="0.09%" prev="toc" next="NT" id="i">
<h2 id="i-p0.1">Holy Bible</h2>
<h1 id="i-p0.2">Swahili New Testament</h1>
</div1>

<div1 title="New Testament" progress="0.09%" prev="i" next="Matt" id="NT">
<h1 id="NT-p0.1">New Testament</h1>

<div2 title="Matthew" progress="0.09%" prev="NT" next="Matt.1" id="Matt">
<h2 id="Matt-p0.1">Matthew</h2>

<div3 title="Matthew 1" progress="0.09%" prev="Matt" next="Matt.2" id="Matt.1">
<h3 id="Matt.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Matt.1-p1">
<scripture passage="Matt 1:1" parsed="|Matt|1|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.1" />
<sup>1</sup>Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake:
<scripture passage="Matt 1:2" parsed="|Matt|1|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.2" />
<sup>2</sup>Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake,
<scripture passage="Matt 1:3" parsed="|Matt|1|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.3" />
<sup>3</sup>Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
<scripture passage="Matt 1:4" parsed="|Matt|1|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.4" />
<sup>4</sup>Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa Salmoni,
<scripture passage="Matt 1:5" parsed="|Matt|1|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.5" />
<sup>5</sup>Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu). Boazi na Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi, Obedi alimzaa Yese,
<scripture passage="Matt 1:6" parsed="|Matt|1|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.6" />
<sup>6</sup>naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa mke wa Uria).
<scripture passage="Matt 1:7" parsed="|Matt|1|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.7" />
<sup>7</sup>Solomoni alimzaa Rehoboamu, Rehoboamu alimzaa Abiya, Abiya alimzaa Asa,
<scripture passage="Matt 1:8" parsed="|Matt|1|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.8" />
<sup>8</sup>Asa alimzaa Yehoshafati, Yehoshafati alimzaa Yoramu, Yoramu alimzaa Uzia,
<scripture passage="Matt 1:9" parsed="|Matt|1|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.9" />
<sup>9</sup>Uzia alimzaa Yothamu, Yothamu alimzaa Ahazi, Ahazi alimzaa Hezekia,
<scripture passage="Matt 1:10" parsed="|Matt|1|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.10" />
<sup>10</sup>Hezekia alimzaa Manase, Manase alimzaa Amoni, Amoni alimzaa Yosia,
<scripture passage="Matt 1:11" parsed="|Matt|1|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.11" />
<sup>11</sup>Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni.
<scripture passage="Matt 1:12" parsed="|Matt|1|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.12" />
<sup>12</sup>Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli alimzaa Zerobabeli,
<scripture passage="Matt 1:13" parsed="|Matt|1|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.13" />
<sup>13</sup>Zerobabeli alimzaa Abiudi, Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaa Azori,
<scripture passage="Matt 1:14" parsed="|Matt|1|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.14" />
<sup>14</sup>Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaa Akimu, Akimu alimzaa Eliudi,
<scripture passage="Matt 1:15" parsed="|Matt|1|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.15" />
<sup>15</sup>Eliudi alimzaa Eleazeri, Eleazeri alimzaa Mathani, Mathani alimzaa Yakobo,
<scripture passage="Matt 1:16" parsed="|Matt|1|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.16" />
<sup>16</sup>Yakobo alimzaa Yosefu, aliyekuwa mume wake Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.
<scripture passage="Matt 1:17" parsed="|Matt|1|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.17" />
<sup>17</sup>Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo.
<scripture passage="Matt 1:18" parsed="|Matt|1|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.18" />
<sup>18</sup>Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Matt 1:19" parsed="|Matt|1|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.19" />
<sup>19</sup>Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.
<scripture passage="Matt 1:20" parsed="|Matt|1|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.20" />
<sup>20</sup>Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, "Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Matt 1:21" parsed="|Matt|1|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.21" />
<sup>21</sup>Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao."
<scripture passage="Matt 1:22" parsed="|Matt|1|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.22" />
<sup>22</sup>Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:
<scripture passage="Matt 1:23" parsed="|Matt|1|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.23" />
<sup>23</sup>"Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa Emanueli" (maana yake, "Mungu yu pamoja nasi").
<scripture passage="Matt 1:24" parsed="|Matt|1|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.24" />
<sup>24</sup>Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani.
<scripture passage="Matt 1:25" parsed="|Matt|1|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.1.25" />
<sup>25</sup>Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 2" progress="0.37%" prev="Matt.1" next="Matt.3" id="Matt.2">
<h3 id="Matt.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Matt.2-p1">
<scripture passage="Matt 2:1" parsed="|Matt|2|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.1" />
<sup>1</sup>Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu,
<scripture passage="Matt 2:2" parsed="|Matt|2|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.2" />
<sup>2</sup>wakauliza, "Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu."
<scripture passage="Matt 2:3" parsed="|Matt|2|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.3" />
<sup>3</sup>Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu.
<scripture passage="Matt 2:4" parsed="|Matt|2|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.4" />
<sup>4</sup>Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria, akawauliza, "Kristo atazaliwa wapi?"
<scripture passage="Matt 2:5" parsed="|Matt|2|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.5" />
<sup>5</sup>Nao wakamjibu, "Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:
<scripture passage="Matt 2:6" parsed="|Matt|2|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.6" />
<sup>6</sup>`Ewe Bethlehemu katika nchi ya Yuda, kwa vyovyote wewe si mdogo kabisa kati ya viongozi wa Yuda; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu, Israeli."`
<scripture passage="Matt 2:7" parsed="|Matt|2|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.7" />
<sup>7</sup>Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza wakati hasa ile nyota ilipowatokea.
<scripture passage="Matt 2:8" parsed="|Matt|2|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.8" />
<sup>8</sup>Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, "Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu."
<scripture passage="Matt 2:9" parsed="|Matt|2|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.9" />
<sup>9</sup>Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
<scripture passage="Matt 2:10" parsed="|Matt|2|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.10" />
<sup>10</sup>Walipoiona hiyo nyota, walifurahi mno.
<scripture passage="Matt 2:11" parsed="|Matt|2|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.11" />
<sup>11</sup>Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane. ic
<scripture passage="Matt 2:12" parsed="|Matt|2|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.12" />
<sup>12</sup>Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode; hivyo wakarudi makwao kwa njia nyingine.
<scripture passage="Matt 2:13" parsed="|Matt|2|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.13" />
<sup>13</sup>Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode anakusudia kumwua huyu mtoto."
<scripture passage="Matt 2:14" parsed="|Matt|2|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.14" />
<sup>14</sup>Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akaondoka usiku, akaenda Misri.
<scripture passage="Matt 2:15" parsed="|Matt|2|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.15" />
<sup>15</sup>Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: "Nilimwita Mwanangu kutoka Misri."
<scripture passage="Matt 2:16" parsed="|Matt|2|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.16" />
<sup>16</sup>Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa wamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuru watoto wote wa kiume mjini Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake wauawe. Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale wataalamu wa nyota.
<scripture passage="Matt 2:17" parsed="|Matt|2|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.17" />
<sup>17</sup>Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia:
<scripture passage="Matt 2:18" parsed="|Matt|2|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.18" />
<sup>18</sup>"Sauti imesikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki."
<scripture passage="Matt 2:19" parsed="|Matt|2|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.19" />
<sup>19</sup>Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri,
<scripture passage="Matt 2:20" parsed="|Matt|2|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.20" />
<sup>20</sup>akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa."
<scripture passage="Matt 2:21" parsed="|Matt|2|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.21" />
<sup>21</sup>Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli.
<scripture passage="Matt 2:22" parsed="|Matt|2|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.22" />
<sup>22</sup>Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya,
<scripture passage="Matt 2:23" parsed="|Matt|2|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.2.23" />
<sup>23</sup>akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: "Ataitwa Mnazare."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 3" progress="0.69%" prev="Matt.2" next="Matt.4" id="Matt.3">
<h3 id="Matt.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Matt.3-p1">
<scripture passage="Matt 3:1" parsed="|Matt|3|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.1" />
<sup>1</sup>Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:
<scripture passage="Matt 3:2" parsed="|Matt|3|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.2" />
<sup>2</sup>"Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia."
<scripture passage="Matt 3:3" parsed="|Matt|3|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.3" />
<sup>3</sup>Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake."`
<scripture passage="Matt 3:4" parsed="|Matt|3|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.4" />
<sup>4</sup>Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
<scripture passage="Matt 3:5" parsed="|Matt|3|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.5" />
<sup>5</sup>Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
<scripture passage="Matt 3:6" parsed="|Matt|3|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.6" />
<sup>6</sup>wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
<scripture passage="Matt 3:7" parsed="|Matt|3|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.7" />
<sup>7</sup>Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
<scripture passage="Matt 3:8" parsed="|Matt|3|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.8" />
<sup>8</sup>Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
<scripture passage="Matt 3:9" parsed="|Matt|3|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.9" />
<sup>9</sup>Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, `Baba yetu ni Abrahamu!` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
<scripture passage="Matt 3:10" parsed="|Matt|3|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.10" />
<sup>10</sup>Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
<scripture passage="Matt 3:11" parsed="|Matt|3|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.11" />
<sup>11</sup>Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
<scripture passage="Matt 3:12" parsed="|Matt|3|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.12" />
<sup>12</sup>Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika." ic
<scripture passage="Matt 3:13" parsed="|Matt|3|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.13" />
<sup>13</sup>Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
<scripture passage="Matt 3:14" parsed="|Matt|3|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.14" />
<sup>14</sup>Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, "Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe."
<scripture passage="Matt 3:15" parsed="|Matt|3|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.15" />
<sup>15</sup>Lakini Yesu akamjibu, "Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka." Hapo Yohane akakubali.
<scripture passage="Matt 3:16" parsed="|Matt|3|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.16" />
<sup>16</sup>Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake.
<scripture passage="Matt 3:17" parsed="|Matt|3|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.3.17" />
<sup>17</sup>Sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 4" progress="0.91%" prev="Matt.3" next="Matt.5" id="Matt.4">
<h3 id="Matt.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Matt.4-p1">
<scripture passage="Matt 4:1" parsed="|Matt|4|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.1" />
<sup>1</sup>Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
<scripture passage="Matt 4:2" parsed="|Matt|4|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.2" />
<sup>2</sup>Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
<scripture passage="Matt 4:3" parsed="|Matt|4|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.3" />
<sup>3</sup>Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate."
<scripture passage="Matt 4:4" parsed="|Matt|4|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.4" />
<sup>4</sup>Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."`
<scripture passage="Matt 4:5" parsed="|Matt|4|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.5" />
<sup>5</sup>Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
<scripture passage="Matt 4:6" parsed="|Matt|4|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.6" />
<sup>6</sup>akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: `Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."`
<scripture passage="Matt 4:7" parsed="|Matt|4|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.7" />
<sup>7</sup>Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: `Usimjaribu Bwana, Mungu wako."`
<scripture passage="Matt 4:8" parsed="|Matt|4|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.8" />
<sup>8</sup>Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
<scripture passage="Matt 4:9" parsed="|Matt|4|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.9" />
<sup>9</sup>akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."
<scripture passage="Matt 4:10" parsed="|Matt|4|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.10" />
<sup>10</sup>Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."`
<scripture passage="Matt 4:11" parsed="|Matt|4|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.11" />
<sup>11</sup>Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
<scripture passage="Matt 4:12" parsed="|Matt|4|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.12" />
<sup>12</sup>Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.
<scripture passage="Matt 4:13" parsed="|Matt|4|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.13" />
<sup>13</sup>Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
<scripture passage="Matt 4:14" parsed="|Matt|4|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.14" />
<sup>14</sup>Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
<scripture passage="Matt 4:15" parsed="|Matt|4|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.15" />
<sup>15</sup>"Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng`ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
<scripture passage="Matt 4:16" parsed="|Matt|4|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.16" />
<sup>16</sup>Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!"
<scripture passage="Matt 4:17" parsed="|Matt|4|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.17" />
<sup>17</sup>Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!"
<scripture passage="Matt 4:18" parsed="|Matt|4|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.18" />
<sup>18</sup>Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
<scripture passage="Matt 4:19" parsed="|Matt|4|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.19" />
<sup>19</sup>Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."
<scripture passage="Matt 4:20" parsed="|Matt|4|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.20" />
<sup>20</sup>Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ic
<scripture passage="Matt 4:21" parsed="|Matt|4|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.21" />
<sup>21</sup>Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,
<scripture passage="Matt 4:22" parsed="|Matt|4|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.22" />
<sup>22</sup>nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
<scripture passage="Matt 4:23" parsed="|Matt|4|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.23" />
<sup>23</sup>Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
<scripture passage="Matt 4:24" parsed="|Matt|4|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.24" />
<sup>24</sup>Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
<scripture passage="Matt 4:25" parsed="|Matt|4|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.4.25" />
<sup>25</sup>Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng`ambo ya mto Yordani, walimfuata.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 5" progress="1.20%" prev="Matt.4" next="Matt.6" id="Matt.5">
<h3 id="Matt.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Matt.5-p1">
<scripture passage="Matt 5:1" parsed="|Matt|5|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
<scripture passage="Matt 5:2" parsed="|Matt|5|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.2" />
<sup>2</sup>naye akaanza kuwafundisha:
<scripture passage="Matt 5:3" parsed="|Matt|5|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.3" />
<sup>3</sup>"Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
<scripture passage="Matt 5:4" parsed="|Matt|5|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.4" />
<sup>4</sup>Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
<scripture passage="Matt 5:5" parsed="|Matt|5|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.5" />
<sup>5</sup>Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
<scripture passage="Matt 5:6" parsed="|Matt|5|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.6" />
<sup>6</sup>Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
<scripture passage="Matt 5:7" parsed="|Matt|5|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.7" />
<sup>7</sup>Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
<scripture passage="Matt 5:8" parsed="|Matt|5|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.8" />
<sup>8</sup>Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
<scripture passage="Matt 5:9" parsed="|Matt|5|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.9" />
<sup>9</sup>Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
<scripture passage="Matt 5:10" parsed="|Matt|5|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.10" />
<sup>10</sup>Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
<scripture passage="Matt 5:11" parsed="|Matt|5|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.11" />
<sup>11</sup>"Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
<scripture passage="Matt 5:12" parsed="|Matt|5|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.12" />
<sup>12</sup>Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
<scripture passage="Matt 5:13" parsed="|Matt|5|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.13" />
<sup>13</sup>"Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
<scripture passage="Matt 5:14" parsed="|Matt|5|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.14" />
<sup>14</sup>"Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
<scripture passage="Matt 5:15" parsed="|Matt|5|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.15" />
<sup>15</sup>Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
<scripture passage="Matt 5:16" parsed="|Matt|5|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.16" />
<sup>16</sup>Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."
<scripture passage="Matt 5:17" parsed="|Matt|5|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.17" />
<sup>17</sup>"Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
<scripture passage="Matt 5:18" parsed="|Matt|5|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.18" />
<sup>18</sup>Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
<scripture passage="Matt 5:19" parsed="|Matt|5|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.19" />
<sup>19</sup>Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 5:20" parsed="|Matt|5|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.20" />
<sup>20</sup>Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 5:21" parsed="|Matt|5|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.21" />
<sup>21</sup>"Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: `Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.`
<scripture passage="Matt 5:22" parsed="|Matt|5|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.22" />
<sup>22</sup>Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: `Pumbavu` atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
<scripture passage="Matt 5:23" parsed="|Matt|5|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.23" />
<sup>23</sup>Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
<scripture passage="Matt 5:24" parsed="|Matt|5|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.24" />
<sup>24</sup>iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
<scripture passage="Matt 5:25" parsed="|Matt|5|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.25" />
<sup>25</sup>"Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
<scripture passage="Matt 5:26" parsed="|Matt|5|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.26" />
<sup>26</sup>Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
<scripture passage="Matt 5:27" parsed="|Matt|5|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.27" />
<sup>27</sup>"Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: `Usizini!`
<scripture passage="Matt 5:28" parsed="|Matt|5|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.28" />
<sup>28</sup>Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
<scripture passage="Matt 5:29" parsed="|Matt|5|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.29" />
<sup>29</sup>Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling`oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.
<scripture passage="Matt 5:30" parsed="|Matt|5|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.30" />
<sup>30</sup>Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.
<scripture passage="Matt 5:31" parsed="|Matt|5|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.31" />
<sup>31</sup>"Ilikwisha semwa pia: `Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.`
<scripture passage="Matt 5:32" parsed="|Matt|5|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.32" />
<sup>32</sup>Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
<scripture passage="Matt 5:33" parsed="|Matt|5|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.33" />
<sup>33</sup>"Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: `Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.`
<scripture passage="Matt 5:34" parsed="|Matt|5|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.34" />
<sup>34</sup>Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
<scripture passage="Matt 5:35" parsed="|Matt|5|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.35" />
<sup>35</sup>wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
<scripture passage="Matt 5:36" parsed="|Matt|5|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.36" />
<sup>36</sup>Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
<scripture passage="Matt 5:37" parsed="|Matt|5|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.37" />
<sup>37</sup>Ukisema, `Ndiyo`, basi iwe `Ndiyo`; ukisema `Siyo`, basi iwe kweli `Siyo`. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
<scripture passage="Matt 5:38" parsed="|Matt|5|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.38" />
<sup>38</sup>"Mmesikia kwamba ilisemwa: `Jicho kwa jicho, jino kwa jino.`
<scripture passage="Matt 5:39" parsed="|Matt|5|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.39" />
<sup>39</sup>Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
<scripture passage="Matt 5:40" parsed="|Matt|5|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.40" />
<sup>40</sup>Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
<scripture passage="Matt 5:41" parsed="|Matt|5|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.41" />
<sup>41</sup>Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
<scripture passage="Matt 5:42" parsed="|Matt|5|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.42" />
<sup>42</sup>Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.
<scripture passage="Matt 5:43" parsed="|Matt|5|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.43" />
<sup>43</sup>"Mmesikia kwamba ilisemwa: `Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.`
<scripture passage="Matt 5:44" parsed="|Matt|5|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.44" />
<sup>44</sup>Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi
<scripture passage="Matt 5:45" parsed="|Matt|5|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.45" />
<sup>45</sup>ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
<scripture passage="Matt 5:46" parsed="|Matt|5|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.46" />
<sup>46</sup>Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
<scripture passage="Matt 5:47" parsed="|Matt|5|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.47" />
<sup>47</sup>Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
<scripture passage="Matt 5:48" parsed="|Matt|5|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.5.48" />
<sup>48</sup>Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 6" progress="1.72%" prev="Matt.5" next="Matt.7" id="Matt.6">
<h3 id="Matt.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Matt.6-p1">
<scripture passage="Matt 6:1" parsed="|Matt|6|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.1" />
<sup>1</sup>"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.
<scripture passage="Matt 6:2" parsed="|Matt|6|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.2" />
<sup>2</sup>"Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
<scripture passage="Matt 6:3" parsed="|Matt|6|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.3" />
<sup>3</sup>Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata rafiki yako asijue ufanyalo.
<scripture passage="Matt 6:4" parsed="|Matt|6|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.4" />
<sup>4</sup>Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
<scripture passage="Matt 6:5" parsed="|Matt|6|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.5" />
<sup>5</sup>"Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
<scripture passage="Matt 6:6" parsed="|Matt|6|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.6" />
<sup>6</sup>Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
<scripture passage="Matt 6:7" parsed="|Matt|6|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.7" />
<sup>7</sup>"Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
<scripture passage="Matt 6:8" parsed="|Matt|6|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.8" />
<sup>8</sup>Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba.
<scripture passage="Matt 6:9" parsed="|Matt|6|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.9" />
<sup>9</sup>Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: `Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.
<scripture passage="Matt 6:10" parsed="|Matt|6|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.10" />
<sup>10</sup>Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
<scripture passage="Matt 6:11" parsed="|Matt|6|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.11" />
<sup>11</sup>Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.
<scripture passage="Matt 6:12" parsed="|Matt|6|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.12" />
<sup>12</sup>Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
<scripture passage="Matt 6:13" parsed="|Matt|6|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.13" />
<sup>13</sup>Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.`<i>fa</i> na utukufu, hata milele. Amina.
<scripture passage="Matt 6:14" parsed="|Matt|6|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.14" />
<sup>14</sup>"Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia.
<scripture passage="Matt 6:15" parsed="|Matt|6|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.15" />
<sup>15</sup>Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
<scripture passage="Matt 6:16" parsed="|Matt|6|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.16" />
<sup>16</sup>"Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
<scripture passage="Matt 6:17" parsed="|Matt|6|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.17" />
<sup>17</sup>Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako,
<scripture passage="Matt 6:18" parsed="|Matt|6|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.18" />
<sup>18</sup>ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika atakutuza.
<scripture passage="Matt 6:19" parsed="|Matt|6|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.19" />
<sup>19</sup>"Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
<scripture passage="Matt 6:20" parsed="|Matt|6|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.20" />
<sup>20</sup>Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.
<scripture passage="Matt 6:21" parsed="|Matt|6|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.21" />
<sup>21</sup>Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
<scripture passage="Matt 6:22" parsed="|Matt|6|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.22" />
<sup>22</sup>"Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga.
<scripture passage="Matt 6:23" parsed="|Matt|6|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.23" />
<sup>23</sup>Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa katika giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza la kutisha mno.
<scripture passage="Matt 6:24" parsed="|Matt|6|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.24" />
<sup>24</sup>"Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
<scripture passage="Matt 6:25" parsed="|Matt|6|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.25" />
<sup>25</sup>"Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
<scripture passage="Matt 6:26" parsed="|Matt|6|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.26" />
<sup>26</sup>Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao?
<scripture passage="Matt 6:27" parsed="|Matt|6|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.27" />
<sup>27</sup>Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
<scripture passage="Matt 6:28" parsed="|Matt|6|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.28" />
<sup>28</sup>"Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
<scripture passage="Matt 6:29" parsed="|Matt|6|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.29" />
<sup>29</sup>Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
<scripture passage="Matt 6:30" parsed="|Matt|6|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.30" />
<sup>30</sup>Ikiwa basi Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyi watu wenye imani haba!
<scripture passage="Matt 6:31" parsed="|Matt|6|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.31" />
<sup>31</sup>"Basi, msiwe na wasiwasi: `Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!`
<scripture passage="Matt 6:32" parsed="|Matt|6|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.32" />
<sup>32</sup>Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.
<scripture passage="Matt 6:33" parsed="|Matt|6|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.33" />
<sup>33</sup>Bali, zingatieni kwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo mengine yote mtapewa kwa ziada.
<scripture passage="Matt 6:34" parsed="|Matt|6|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.6.34" />
<sup>34</sup>Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 7" progress="2.12%" prev="Matt.6" next="Matt.8" id="Matt.7">
<h3 id="Matt.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Matt.7-p1">
<scripture passage="Matt 7:1" parsed="|Matt|7|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.1" />
<sup>1</sup>"Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
<scripture passage="Matt 7:2" parsed="|Matt|7|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.2" />
<sup>2</sup>kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.
<scripture passage="Matt 7:3" parsed="|Matt|7|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.3" />
<sup>3</sup>Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
<scripture passage="Matt 7:4" parsed="|Matt|7|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.4" />
<sup>4</sup>Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, `Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako`, wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
<scripture passage="Matt 7:5" parsed="|Matt|7|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.5" />
<sup>5</sup>Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
<scripture passage="Matt 7:6" parsed="|Matt|7|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.6" />
<sup>6</sup>"Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua ninyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.
<scripture passage="Matt 7:7" parsed="|Matt|7|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.7" />
<sup>7</sup>"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
<scripture passage="Matt 7:8" parsed="|Matt|7|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.8" />
<sup>8</sup>Maana, aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye hufunguliwa.
<scripture passage="Matt 7:9" parsed="|Matt|7|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.9" />
<sup>9</sup>Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe?
<scripture passage="Matt 7:10" parsed="|Matt|7|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.10" />
<sup>10</sup>Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka?
<scripture passage="Matt 7:11" parsed="|Matt|7|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.11" />
<sup>11</sup>Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba.
<scripture passage="Matt 7:12" parsed="|Matt|7|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.12" />
<sup>12</sup>"Watendeeni wengine yale mnayotaka wao wawatendee ninyi. Hii ndiyo maana ya Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.
<scripture passage="Matt 7:13" parsed="|Matt|7|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.13" />
<sup>13</sup>"Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi.
<scripture passage="Matt 7:14" parsed="|Matt|7|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.14" />
<sup>14</sup>Lakini njia inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
<scripture passage="Matt 7:15" parsed="|Matt|7|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.15" />
<sup>15</sup>"Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
<scripture passage="Matt 7:16" parsed="|Matt|7|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.16" />
<sup>16</sup>Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!
<scripture passage="Matt 7:17" parsed="|Matt|7|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.17" />
<sup>17</sup>Basi, mti mwema huzaa matunda mema, na mti mbaya huzaa matunda mabaya.
<scripture passage="Matt 7:18" parsed="|Matt|7|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.18" />
<sup>18</sup>Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema.
<scripture passage="Matt 7:19" parsed="|Matt|7|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.19" />
<sup>19</sup>Kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa motoni.
<scripture passage="Matt 7:20" parsed="|Matt|7|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.20" />
<sup>20</sup>Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. ic
<scripture passage="Matt 7:21" parsed="|Matt|7|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.21" />
<sup>21</sup>"Si kila aniambiaye, `Bwana, Bwana,` ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
<scripture passage="Matt 7:22" parsed="|Matt|7|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.22" />
<sup>22</sup>Wengi wataniambia Siku ile ya hukumu: `Bwana, Bwana! kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi.`
<scripture passage="Matt 7:23" parsed="|Matt|7|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.23" />
<sup>23</sup>Hapo nitawaambia: `Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.`
<scripture passage="Matt 7:24" parsed="|Matt|7|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.24" />
<sup>24</sup>"Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
<scripture passage="Matt 7:25" parsed="|Matt|7|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.25" />
<sup>25</sup>Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
<scripture passage="Matt 7:26" parsed="|Matt|7|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.26" />
<sup>26</sup>"Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
<scripture passage="Matt 7:27" parsed="|Matt|7|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.27" />
<sup>27</sup>Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena kwa kishindo kikubwa."
<scripture passage="Matt 7:28" parsed="|Matt|7|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.28" />
<sup>28</sup>Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake.
<scripture passage="Matt 7:29" parsed="|Matt|7|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.7.29" />
<sup>29</sup>Hakuwa kama walimu wao wa Sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 8" progress="2.45%" prev="Matt.7" next="Matt.9" id="Matt.8">
<h3 id="Matt.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Matt.8-p1">
<scripture passage="Matt 8:1" parsed="|Matt|8|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata.
<scripture passage="Matt 8:2" parsed="|Matt|8|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.2" />
<sup>2</sup>Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, "Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!"
<scripture passage="Matt 8:3" parsed="|Matt|8|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.3" />
<sup>3</sup>Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, "Nataka! Takasika." Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
<scripture passage="Matt 8:4" parsed="|Matt|8|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.4" />
<sup>4</sup>Kisha Yesu akamwambia, "Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona."
<scripture passage="Matt 8:5" parsed="|Matt|8|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.5" />
<sup>5</sup>Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, ofisa mmoja Mroma alimwendea, akamsihi
<scripture passage="Matt 8:6" parsed="|Matt|8|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.6" />
<sup>6</sup>akisema, "Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana."
<scripture passage="Matt 8:7" parsed="|Matt|8|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.7" />
<sup>7</sup>Yesu akamwambia, "Nitakuja kumponya."
<scripture passage="Matt 8:8" parsed="|Matt|8|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.8" />
<sup>8</sup>Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
<scripture passage="Matt 8:9" parsed="|Matt|8|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.9" />
<sup>9</sup>Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, `Nenda!` naye huenda; na mwingine, `Njoo!` naye huja; na mtumishi wangu, `Fanya kitu hiki!` naye hufanya."
<scripture passage="Matt 8:10" parsed="|Matt|8|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.10" />
<sup>10</sup>Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, "Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii.
<scripture passage="Matt 8:11" parsed="|Matt|8|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.11" />
<sup>11</sup>Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 8:12" parsed="|Matt|8|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.12" />
<sup>12</sup>Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno."
<scripture passage="Matt 8:13" parsed="|Matt|8|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.13" />
<sup>13</sup>Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, "Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini." Na mtumishi wake akapona saa ileile.
<scripture passage="Matt 8:14" parsed="|Matt|8|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.14" />
<sup>14</sup>Yesu alifika nyumbani kwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, ana homa kali.
<scripture passage="Matt 8:15" parsed="|Matt|8|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.15" />
<sup>15</sup>Basi, Yesu akamgusa huyo mama mkono, na homa ikamwacha; akasimama, akamtumikia.
<scripture passage="Matt 8:16" parsed="|Matt|8|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.16" />
<sup>16</sup>Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
<scripture passage="Matt 8:17" parsed="|Matt|8|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.17" />
<sup>17</sup>Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: "Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu."
<scripture passage="Matt 8:18" parsed="|Matt|8|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.18" />
<sup>18</sup>Yesu alipoona kundi la watu limemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake waende ng`ambo ya ziwa.
<scripture passage="Matt 8:19" parsed="|Matt|8|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.19" />
<sup>19</sup>Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, "Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako."
<scripture passage="Matt 8:20" parsed="|Matt|8|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.20" />
<sup>20</sup>Yesu akamjibu, "Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia."
<scripture passage="Matt 8:21" parsed="|Matt|8|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.21" />
<sup>21</sup>Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu."
<scripture passage="Matt 8:22" parsed="|Matt|8|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.22" />
<sup>22</sup>Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao."
<scripture passage="Matt 8:23" parsed="|Matt|8|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.23" />
<sup>23</sup>Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye.
<scripture passage="Matt 8:24" parsed="|Matt|8|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.24" />
<sup>24</sup>Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi.
<scripture passage="Matt 8:25" parsed="|Matt|8|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.25" />
<sup>25</sup>Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe, tunaangamia!"
<scripture passage="Matt 8:26" parsed="|Matt|8|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.26" />
<sup>26</sup>Yesu akawaambia, "Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?" Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.
<scripture passage="Matt 8:27" parsed="|Matt|8|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.27" />
<sup>27</sup>Watu wakashangaa, wakasema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!"
<scripture passage="Matt 8:28" parsed="|Matt|8|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.28" />
<sup>28</sup>Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi,<i>fb</i> ng`ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita katika njia hiyo.
<scripture passage="Matt 8:29" parsed="|Matt|8|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.29" />
<sup>29</sup>Nao wakaanza kupiga kelele, "Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?"
<scripture passage="Matt 8:30" parsed="|Matt|8|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.30" />
<sup>30</sup>Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa.
<scripture passage="Matt 8:31" parsed="|Matt|8|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.31" />
<sup>31</sup>Basi, hao pepo wakamsihi, "Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale."
<scripture passage="Matt 8:32" parsed="|Matt|8|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.32" />
<sup>32</sup>Yesu akawaambia, "Haya, nendeni." Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.
<scripture passage="Matt 8:33" parsed="|Matt|8|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.33" />
<sup>33</sup>Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
<scripture passage="Matt 8:34" parsed="|Matt|8|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.8.34" />
<sup>34</sup>Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 9" progress="2.85%" prev="Matt.8" next="Matt.10" id="Matt.9">
<h3 id="Matt.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Matt.9-p1">
<scripture passage="Matt 9:1" parsed="|Matt|9|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake.
<scripture passage="Matt 9:2" parsed="|Matt|9|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.2" />
<sup>2</sup>Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako."
<scripture passage="Matt 9:3" parsed="|Matt|9|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.3" />
<sup>3</sup>Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, "Mtu huyu anamkufuru Mungu!"
<scripture passage="Matt 9:4" parsed="|Matt|9|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.4" />
<sup>4</sup>Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, "Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
<scripture passage="Matt 9:5" parsed="|Matt|9|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.5" />
<sup>5</sup>Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, `Umesamehewa dhambi zako`, au kusema, `Simama, utembee`?
<scripture passage="Matt 9:6" parsed="|Matt|9|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.6" />
<sup>6</sup>Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani." Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako."
<scripture passage="Matt 9:7" parsed="|Matt|9|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.7" />
<sup>7</sup>Huyo mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akaenda nyumbani kwake.
<scripture passage="Matt 9:8" parsed="|Matt|9|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.8" />
<sup>8</sup>Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
<scripture passage="Matt 9:9" parsed="|Matt|9|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.9" />
<sup>9</sup>Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, "Nifuate." Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
<scripture passage="Matt 9:10" parsed="|Matt|9|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.10" />
<sup>10</sup>Yesu alipokuwa nyumbani<i>fc</i> ameketi kula chakula, watoza ushuru wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
<scripture passage="Matt 9:11" parsed="|Matt|9|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.11" />
<sup>11</sup>Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, "Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?"
<scripture passage="Matt 9:12" parsed="|Matt|9|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.12" />
<sup>12</sup>Yesu aliwasikia, akasema, "Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.
<scripture passage="Matt 9:13" parsed="|Matt|9|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.13" />
<sup>13</sup>Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: `Nataka huruma, wala si dhabihu.` Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi."
<scripture passage="Matt 9:14" parsed="|Matt|9|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.14" />
<sup>14</sup>Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?"
<scripture passage="Matt 9:15" parsed="|Matt|9|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.15" />
<sup>15</sup>Yesu akawajibu, "Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
<scripture passage="Matt 9:16" parsed="|Matt|9|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.16" />
<sup>16</sup>"Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
<scripture passage="Matt 9:17" parsed="|Matt|9|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.17" />
<sup>17</sup>Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama."
<scripture passage="Matt 9:18" parsed="|Matt|9|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.18" />
<sup>18</sup>Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, "Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi."
<scripture passage="Matt 9:19" parsed="|Matt|9|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.19" />
<sup>19</sup>Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake, akamfuata.
<scripture passage="Matt 9:20" parsed="|Matt|9|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.20" />
<sup>20</sup>Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
<scripture passage="Matt 9:21" parsed="|Matt|9|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.21" />
<sup>21</sup>Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: "Nikigusa tu vazi lake, nitapona."
<scripture passage="Matt 9:22" parsed="|Matt|9|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.22" />
<sup>22</sup>Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, "Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya." Mama huyo akapona saa ileile.
<scripture passage="Matt 9:23" parsed="|Matt|9|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.23" />
<sup>23</sup>Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
<scripture passage="Matt 9:24" parsed="|Matt|9|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.24" />
<sup>24</sup>akasema, "Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu." Nao wakamcheka.
<scripture passage="Matt 9:25" parsed="|Matt|9|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.25" />
<sup>25</sup>Basi, umati wa watu ulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshika huyo msichana mkono, naye akasimama.
<scripture passage="Matt 9:26" parsed="|Matt|9|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.26" />
<sup>26</sup>Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote.
<scripture passage="Matt 9:27" parsed="|Matt|9|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.27" />
<sup>27</sup>Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, "Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
<scripture passage="Matt 9:28" parsed="|Matt|9|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.28" />
<sup>28</sup>Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, "Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?" Nao wakamjibu, "Naam, Mheshimiwa."
<scripture passage="Matt 9:29" parsed="|Matt|9|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.29" />
<sup>29</sup>Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, "Na iwe kwenu kama mnavyoamini."
<scripture passage="Matt 9:30" parsed="|Matt|9|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.30" />
<sup>30</sup>Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: "Msimwambie mtu yeyote jambo hili."
<scripture passage="Matt 9:31" parsed="|Matt|9|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.31" />
<sup>31</sup>Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile yote.
<scripture passage="Matt 9:32" parsed="|Matt|9|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.32" />
<sup>32</sup>Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
<scripture passage="Matt 9:33" parsed="|Matt|9|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.33" />
<sup>33</sup>Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, "Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!"
<scripture passage="Matt 9:34" parsed="|Matt|9|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.34" />
<sup>34</sup>Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, "Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya."
<scripture passage="Matt 9:35" parsed="|Matt|9|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.35" />
<sup>35</sup>Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
<scripture passage="Matt 9:36" parsed="|Matt|9|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.36" />
<sup>36</sup>Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
<scripture passage="Matt 9:37" parsed="|Matt|9|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.37" />
<sup>37</sup>Hapo akawaambia wanafunzi wake, "Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache.
<scripture passage="Matt 9:38" parsed="|Matt|9|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.9.38" />
<sup>38</sup>Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 10" progress="3.33%" prev="Matt.9" next="Matt.11" id="Matt.10">
<h3 id="Matt.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Matt.10-p1">
<scripture passage="Matt 10:1" parsed="|Matt|10|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
<scripture passage="Matt 10:2" parsed="|Matt|10|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.2" />
<sup>2</sup>Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni aitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;
<scripture passage="Matt 10:3" parsed="|Matt|10|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.3" />
<sup>3</sup>Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
<scripture passage="Matt 10:4" parsed="|Matt|10|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.4" />
<sup>4</sup>Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
<scripture passage="Matt 10:5" parsed="|Matt|10|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.5" />
<sup>5</sup>Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: "Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.
<scripture passage="Matt 10:6" parsed="|Matt|10|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.6" />
<sup>6</sup>Ila nendeni kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo.
<scripture passage="Matt 10:7" parsed="|Matt|10|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.7" />
<sup>7</sup>Mnapokwenda hubirini hivi: `Ufalme wa mbinguni umekaribia.`
<scripture passage="Matt 10:8" parsed="|Matt|10|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.8" />
<sup>8</sup>Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.
<scripture passage="Matt 10:9" parsed="|Matt|10|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.9" />
<sup>9</sup>Msichukue mifukoni mwenu dhahabu, wala fedha, wala sarafu za shaba.
<scripture passage="Matt 10:10" parsed="|Matt|10|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.10" />
<sup>10</sup>Msichukue mkoba wa kuombea njiani, wala koti la ziada, wala viatu, wala fimbo. Maana mfanyakazi anastahili riziki yake.
<scripture passage="Matt 10:11" parsed="|Matt|10|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.11" />
<sup>11</sup>"Mkiingia katika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtu yeyote aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeni naye mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
<scripture passage="Matt 10:12" parsed="|Matt|10|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.12" />
<sup>12</sup>Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake.
<scripture passage="Matt 10:13" parsed="|Matt|10|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.13" />
<sup>13</sup>Kama wenyeji wa nyumba hiyo wakiipokea salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei, basi amani yenu itawarudia ninyi.
<scripture passage="Matt 10:14" parsed="|Matt|10|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.14" />
<sup>14</sup>Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakung`uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.
<scripture passage="Matt 10:15" parsed="|Matt|10|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.15" />
<sup>15</sup>Kweli nawaambieni, Siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.
<scripture passage="Matt 10:16" parsed="|Matt|10|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.16" />
<sup>16</sup>"Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
<scripture passage="Matt 10:17" parsed="|Matt|10|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.17" />
<sup>17</sup>Jihadharini na watu, maana watawapeleka ninyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
<scripture passage="Matt 10:18" parsed="|Matt|10|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.18" />
<sup>18</sup>Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
<scripture passage="Matt 10:19" parsed="|Matt|10|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.19" />
<sup>19</sup>Basi, watakapowapeleka ninyi mahakamani, msiwe na wasiwasi mtasema nini au namna gani; wakati utakapofika, mtapewa la kusema.
<scripture passage="Matt 10:20" parsed="|Matt|10|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.20" />
<sup>20</sup>Maana si ninyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
<scripture passage="Matt 10:21" parsed="|Matt|10|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.21" />
<sup>21</sup>"Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe, nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
<scripture passage="Matt 10:22" parsed="|Matt|10|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.22" />
<sup>22</sup>Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
<scripture passage="Matt 10:23" parsed="|Matt|10|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.23" />
<sup>23</sup>"Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.
<scripture passage="Matt 10:24" parsed="|Matt|10|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.24" />
<sup>24</sup>"Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.
<scripture passage="Matt 10:25" parsed="|Matt|10|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.25" />
<sup>25</sup>Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
<scripture passage="Matt 10:26" parsed="|Matt|10|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.26" />
<sup>26</sup>"Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na kila kilichofichwa kitafichuliwa.
<scripture passage="Matt 10:27" parsed="|Matt|10|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.27" />
<sup>27</sup>Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong`onezwa, litangazeni hadharani.
<scripture passage="Matt 10:28" parsed="|Matt|10|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.28" />
<sup>28</sup>Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.
<scripture passage="Matt 10:29" parsed="|Matt|10|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.29" />
<sup>29</sup>Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakini hata mmoja wao haanguki chini bila kibali cha Baba yenu.
<scripture passage="Matt 10:30" parsed="|Matt|10|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.30" />
<sup>30</sup>Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
<scripture passage="Matt 10:31" parsed="|Matt|10|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.31" />
<sup>31</sup>Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamani kuliko shomoro wengi. ic
<scripture passage="Matt 10:32" parsed="|Matt|10|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.32" />
<sup>32</sup>"Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
<scripture passage="Matt 10:33" parsed="|Matt|10|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.33" />
<sup>33</sup>Lakini yeyote atakayenikana hadharani, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
<scripture passage="Matt 10:34" parsed="|Matt|10|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.34" />
<sup>34</sup>"Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
<scripture passage="Matt 10:35" parsed="|Matt|10|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.35" />
<sup>35</sup>Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake.
<scripture passage="Matt 10:36" parsed="|Matt|10|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.36" />
<sup>36</sup>Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
<scripture passage="Matt 10:37" parsed="|Matt|10|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.37" />
<sup>37</sup>"Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
<scripture passage="Matt 10:38" parsed="|Matt|10|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.38" />
<sup>38</sup>Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili.
<scripture passage="Matt 10:39" parsed="|Matt|10|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.39" />
<sup>39</sup>Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
<scripture passage="Matt 10:40" parsed="|Matt|10|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.40" />
<sup>40</sup>"Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
<scripture passage="Matt 10:41" parsed="|Matt|10|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.41" />
<sup>41</sup>Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii, atapokea tuzo la nabii. Anayemkaribisha mtu mwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokea tuzo la mtu mwema.
<scripture passage="Matt 10:42" parsed="|Matt|10|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.10.42" />
<sup>42</sup>Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwe kupata tuzo lake."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 11" progress="3.80%" prev="Matt.10" next="Matt.12" id="Matt.11">
<h3 id="Matt.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Matt.11-p1">
<scripture passage="Matt 11:1" parsed="|Matt|11|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzi kumi na wawili maagizo, alitoka hapo, akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
<scripture passage="Matt 11:2" parsed="|Matt|11|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.2" />
<sup>2</sup>Yohane mbatizaji akiwa gerezani alipata habari juu ya matendo ya Kristo. Basi, Yohane akawatuma wanafunzi wake,
<scripture passage="Matt 11:3" parsed="|Matt|11|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.3" />
<sup>3</sup>wamwulize: "Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?"
<scripture passage="Matt 11:4" parsed="|Matt|11|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.4" />
<sup>4</sup>Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona:
<scripture passage="Matt 11:5" parsed="|Matt|11|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.5" />
<sup>5</sup>vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa na viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
<scripture passage="Matt 11:6" parsed="|Matt|11|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.6" />
<sup>6</sup>Heri mtu yule asiyekuwa na mashaka nami."
<scripture passage="Matt 11:7" parsed="|Matt|11|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.7" />
<sup>7</sup>Basi, hao wajumbe wa Yohane walipokuwa wanakwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu habari za Yohane: "Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
<scripture passage="Matt 11:8" parsed="|Matt|11|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.8" />
<sup>8</sup>Lakini mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumtazama mtu aliyevaa mavazi maridadi? Watu wanaovaa mavazi maridadi hukaa katika nyumba za wafalme.
<scripture passage="Matt 11:9" parsed="|Matt|11|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.9" />
<sup>9</sup>Basi, mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.
<scripture passage="Matt 11:10" parsed="|Matt|11|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.10" />
<sup>10</sup>"Huyu ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: `Tazama, hapa namtuma mjumbe wangu, asema Bwana, akutangulie na kukutayarishia njia yako.`
<scripture passage="Matt 11:11" parsed="|Matt|11|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.11" />
<sup>11</sup>Kweli nawaambieni, miongoni mwa watoto wote wa watu, hajatokea aliye mkuu kuliko Yohane mbatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni, ni mkubwa kuliko yeye.
<scripture passage="Matt 11:12" parsed="|Matt|11|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.12" />
<sup>12</sup>Tangu wakati wa Yohane mbatizaji mpaka leo hii, Ufalme wa mbinguni unashambuliwa vikali, na watu wakali wanajaribu kuunyakua kwa nguvu.
<scripture passage="Matt 11:13" parsed="|Matt|11|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.13" />
<sup>13</sup>Mafundisho yote ya manabii na sheria yalibashiri juu ya nyakati hizi.
<scripture passage="Matt 11:14" parsed="|Matt|11|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.14" />
<sup>14</sup>Kama mwaweza kukubali basi, Yohane ndiye Eliya ambaye angekuja.
<scripture passage="Matt 11:15" parsed="|Matt|11|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.15" />
<sup>15</sup>Mwenye masikio na asikie!
<scripture passage="Matt 11:16" parsed="|Matt|11|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.16" />
<sup>16</sup>"Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja kwa kingine:
<scripture passage="Matt 11:17" parsed="|Matt|11|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.17" />
<sup>17</sup>`Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza; tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!`
<scripture passage="Matt 11:18" parsed="|Matt|11|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.18" />
<sup>18</sup>Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: `Amepagawa na pepo.`
<scripture passage="Matt 11:19" parsed="|Matt|11|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.19" />
<sup>19</sup>Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: `Mtazameni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wahalifu!` Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake."
<scripture passage="Matt 11:20" parsed="|Matt|11|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.20" />
<sup>20</sup>Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kubadili nia zao mbaya:
<scripture passage="Matt 11:21" parsed="|Matt|11|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.21" />
<sup>21</sup>"Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia na kujipaka majivu zamani, ili kuonyesha kwamba wametubu.
<scripture passage="Matt 11:22" parsed="|Matt|11|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.22" />
<sup>22</sup>Hata hivyo nawaambieni, Siku ya hukumu, ninyi mtapata adhabu kubwa kuliko Tiro na Sidoni.
<scripture passage="Matt 11:23" parsed="|Matt|11|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.23" />
<sup>23</sup>Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka Kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
<scripture passage="Matt 11:24" parsed="|Matt|11|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.24" />
<sup>24</sup>Lakini nawaambieni, Siku ya hukumu itakuwa nafuu zaidi kwa watu wa Sodoma, kuliko kwako wewe."
<scripture passage="Matt 11:25" parsed="|Matt|11|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.25" />
<sup>25</sup>Wakati huo Yesu alisema, "Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima mambo haya, ukawafumbulia watoto wadogo.
<scripture passage="Matt 11:26" parsed="|Matt|11|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.26" />
<sup>26</sup>Naam Baba, ndivyo ilivyokupendeza.
<scripture passage="Matt 11:27" parsed="|Matt|11|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.27" />
<sup>27</sup>"Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumjulisha.
<scripture passage="Matt 11:28" parsed="|Matt|11|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.28" />
<sup>28</sup>Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
<scripture passage="Matt 11:29" parsed="|Matt|11|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.29" />
<sup>29</sup>Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu.
<scripture passage="Matt 11:30" parsed="|Matt|11|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.11.30" />
<sup>30</sup>Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 12" progress="4.16%" prev="Matt.11" next="Matt.13" id="Matt.12">
<h3 id="Matt.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Matt.12-p1">
<scripture passage="Matt 12:1" parsed="|Matt|12|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.1" />
<sup>1</sup>Wakati huo, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano siku ya Sabato. Basi, wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakala punje zake.
<scripture passage="Matt 12:2" parsed="|Matt|12|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.2" />
<sup>2</sup>Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, "Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato."
<scripture passage="Matt 12:3" parsed="|Matt|12|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa?
<scripture passage="Matt 12:4" parsed="|Matt|12|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.4" />
<sup>4</sup>Yeye aliingia katika Nyumba ya Mungu pamoja na wenzake, wakala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
<scripture passage="Matt 12:5" parsed="|Matt|12|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.5" />
<sup>5</sup>Au je, hamjasoma katika Sheria kwamba kila siku ya Sabato makuhani huivunja Sheria Hekaluni, lakini hawafikiriwi kuwa na hatia?
<scripture passage="Matt 12:6" parsed="|Matt|12|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.6" />
<sup>6</sup>Basi, nawaambieni kwamba hapa pana kikuu<i>fd</i> kuliko Hekalu.
<scripture passage="Matt 12:7" parsed="|Matt|12|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.7" />
<sup>7</sup>Kama tu mngejua maana ya maneno haya: `Nataka huruma wala si dhabihu`, hamngewahukumu watu wasio na hatia.
<scripture passage="Matt 12:8" parsed="|Matt|12|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.8" />
<sup>8</sup>Maana Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato."
<scripture passage="Matt 12:9" parsed="|Matt|12|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.9" />
<sup>9</sup>Yesu alitoka hapo, akaenda katika sunagogi lao.
<scripture passage="Matt 12:10" parsed="|Matt|12|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.10" />
<sup>10</sup>Kulikuwa na mtu mmoja mwenye mkono uliopooza. Basi, watu wakamwuliza Yesu, "Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato?" Walimwuliza hivyo wapate kisa cha kumshtaki.
<scripture passage="Matt 12:11" parsed="|Matt|12|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.11" />
<sup>11</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Tuseme mmoja wenu ana kondoo wake ambaye ametumbukia shimoni; je, hatamshika na kumtoa humo siku ya Sabato?
<scripture passage="Matt 12:12" parsed="|Matt|12|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.12" />
<sup>12</sup>Mtu ana thamani kuliko kondoo! Basi, ni halali kutenda mema siku ya Sabato."
<scripture passage="Matt 12:13" parsed="|Matt|12|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.13" />
<sup>13</sup>Kisha akamwambia yule mtu, "Nyosha mkono wako." Akaunyosha, nao ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.
<scripture passage="Matt 12:14" parsed="|Matt|12|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.14" />
<sup>14</sup>Basi, Mafarisayo wakatoka nje, wakashauriana jinsi watakavyomwangamiza Yesu.
<scripture passage="Matt 12:15" parsed="|Matt|12|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.15" />
<sup>15</sup>Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,
<scripture passage="Matt 12:16" parsed="|Matt|12|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.16" />
<sup>16</sup>akawaamuru wasiwaambie watu habari zake,
<scripture passage="Matt 12:17" parsed="|Matt|12|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.17" />
<sup>17</sup>ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie:
<scripture passage="Matt 12:18" parsed="|Matt|12|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.18" />
<sup>18</sup>"Hapa ni mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka Roho yangu juu yake, naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.
<scripture passage="Matt 12:19" parsed="|Matt|12|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.19" />
<sup>19</sup>Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika barabarani.
<scripture passage="Matt 12:20" parsed="|Matt|12|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.20" />
<sup>20</sup>Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi ufukao moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
<scripture passage="Matt 12:21" parsed="|Matt|12|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.21" />
<sup>21</sup>Katika jina lake mataifa yatakuwa na tumaini."
<scripture passage="Matt 12:22" parsed="|Matt|12|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.22" />
<sup>22</sup>Hapo watu wakamletea Yesu kipofu mmoja ambaye alikuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Yesu akamponya hata, akaweza kusema na kuona.
<scripture passage="Matt 12:23" parsed="|Matt|12|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.23" />
<sup>23</sup>Umati wote wa watu ulishangaa ukasema, "Je, huenda ikawa huyu ndiye Mwana wa Daudi?"
<scripture passage="Matt 12:24" parsed="|Matt|12|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.24" />
<sup>24</sup>Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, wakasema, "Mtu huyu anawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo."
<scripture passage="Matt 12:25" parsed="|Matt|12|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.25" />
<sup>25</sup>Yesu, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, "Ufalme wowote uliogawanyika makundimakundi yanayopingana, hauwezi kudumu, na mji wowote au jamaa yoyote iliyogawanyika makundimakundi yanayopingana, itaanguka.
<scripture passage="Matt 12:26" parsed="|Matt|12|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.26" />
<sup>26</sup>Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamaje?
<scripture passage="Matt 12:27" parsed="|Matt|12|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.27" />
<sup>27</sup>Ninyi mnasema ati nawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli; je, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo wao ndio watakaowahukumu ninyi.
<scripture passage="Matt 12:28" parsed="|Matt|12|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.28" />
<sup>28</sup>Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
<scripture passage="Matt 12:29" parsed="|Matt|12|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.29" />
<sup>29</sup>"Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang`anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyang`anya mali yake.
<scripture passage="Matt 12:30" parsed="|Matt|12|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.30" />
<sup>30</sup>"Yeyote asiyejiunga nami, anapingana nami; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
<scripture passage="Matt 12:31" parsed="|Matt|12|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.31" />
<sup>31</sup>Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Matt 12:32" parsed="|Matt|12|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.32" />
<sup>32</sup>Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.
<scripture passage="Matt 12:33" parsed="|Matt|12|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.33" />
<sup>33</sup>"Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mema; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
<scripture passage="Matt 12:34" parsed="|Matt|12|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.34" />
<sup>34</sup>Enyi kizazi cha nyoka! Mnawezaje kusema mambo mema hali ninyi ni waovu? Maana mtu husema kutokana na yale yaliyojaa moyoni.
<scripture passage="Matt 12:35" parsed="|Matt|12|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.35" />
<sup>35</sup>Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.
<scripture passage="Matt 12:36" parsed="|Matt|12|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.36" />
<sup>36</sup>"Basi, nawaambieni, Siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema.
<scripture passage="Matt 12:37" parsed="|Matt|12|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.37" />
<sup>37</sup>Maana kwa maneno yako, utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako, utahukumiwa kuwa na hatia."
<scripture passage="Matt 12:38" parsed="|Matt|12|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.38" />
<sup>38</sup>Kisha baadhi ya walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamwambia Yesu, "Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako."
<scripture passage="Matt 12:39" parsed="|Matt|12|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.39" />
<sup>39</sup>Naye akawajibu, "Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara; hamtapewa ishara nyingine, ila tu ile ishara ya nabii Yona.
<scripture passage="Matt 12:40" parsed="|Matt|12|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.40" />
<sup>40</sup>Jinsi Yona alivyokaa siku tatu kutwa kucha tumboni mwa nyangumi, ndivyo naye Mwana wa Mtu atakavyokaa ndani ya ardhi siku tatu kutwa kucha.
<scripture passage="Matt 12:41" parsed="|Matt|12|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.41" />
<sup>41</sup>Watu wa Ninewi watatokea siku ya hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!
<scripture passage="Matt 12:42" parsed="|Matt|12|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.42" />
<sup>42</sup>Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna kikuu<i>fe</i> kuliko Solomoni.
<scripture passage="Matt 12:43" parsed="|Matt|12|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.43" />
<sup>43</sup>"Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzika asipate.
<scripture passage="Matt 12:44" parsed="|Matt|12|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.44" />
<sup>44</sup>Hapo hujisemea: `Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka.` Lakini anaporudi na kuikuta tupu, imefagiwa na kupambwa,
<scripture passage="Matt 12:45" parsed="|Matt|12|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.45" />
<sup>45</sup>huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu."
<scripture passage="Matt 12:46" parsed="|Matt|12|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.46" />
<sup>46</sup>Yesu alikuwa bado anasema na umati wa watu wakati mama yake na ndugu zake walipofika na kusimama nje, wakitaka kusema naye.
<scripture passage="Matt 12:47" parsed="|Matt|12|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.47" />
<sup>47</sup>Basi, mtu mmoja akamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kusema nawe."
<scripture passage="Matt 12:48" parsed="|Matt|12|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.48" />
<sup>48</sup>Lakini Yesu akamjibu mtu huyo, "Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni kina nani?"
<scripture passage="Matt 12:49" parsed="|Matt|12|49|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.49" />
<sup>49</sup>Kisha akaunyosha mkono wake kuelekea wanafunzi wake, akasema, "Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu!
<scripture passage="Matt 12:50" parsed="|Matt|12|50|0|0" osisRef="Bible:Matt.12.50" />
<sup>50</sup>Maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 13" progress="4.78%" prev="Matt.12" next="Matt.14" id="Matt.13">
<h3 id="Matt.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Matt.13-p1">
<scripture passage="Matt 13:1" parsed="|Matt|13|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.1" />
<sup>1</sup>Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.
<scripture passage="Matt 13:2" parsed="|Matt|13|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.2" />
<sup>2</sup>Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
<scripture passage="Matt 13:3" parsed="|Matt|13|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.3" />
<sup>3</sup>naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
<scripture passage="Matt 13:4" parsed="|Matt|13|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.4" />
<sup>4</sup>Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
<scripture passage="Matt 13:5" parsed="|Matt|13|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.5" />
<sup>5</sup>Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
<scripture passage="Matt 13:6" parsed="|Matt|13|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.6" />
<sup>6</sup>Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
<scripture passage="Matt 13:7" parsed="|Matt|13|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.7" />
<sup>7</sup>Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.
<scripture passage="Matt 13:8" parsed="|Matt|13|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.8" />
<sup>8</sup>Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.
<scripture passage="Matt 13:9" parsed="|Matt|13|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.9" />
<sup>9</sup>Mwenye masikio na asikie!"
<scripture passage="Matt 13:10" parsed="|Matt|13|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.10" />
<sup>10</sup>Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, "Kwa nini unasema na watu kwa mifano?"
<scripture passage="Matt 13:11" parsed="|Matt|13|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.11" />
<sup>11</sup>Yesu akawajibu, "Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
<scripture passage="Matt 13:12" parsed="|Matt|13|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.12" />
<sup>12</sup>Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
<scripture passage="Matt 13:13" parsed="|Matt|13|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.13" />
<sup>13</sup>Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
<scripture passage="Matt 13:14" parsed="|Matt|13|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.14" />
<sup>14</sup>Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: `Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
<scripture passage="Matt 13:15" parsed="|Matt|13|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.15" />
<sup>15</sup>Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.`
<scripture passage="Matt 13:16" parsed="|Matt|13|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.16" />
<sup>16</sup>"Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
<scripture passage="Matt 13:17" parsed="|Matt|13|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.17" />
<sup>17</sup>Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
<scripture passage="Matt 13:18" parsed="|Matt|13|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.18" />
<sup>18</sup>"Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
<scripture passage="Matt 13:19" parsed="|Matt|13|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.19" />
<sup>19</sup>Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake.
<scripture passage="Matt 13:20" parsed="|Matt|13|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.20" />
<sup>20</sup>Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huo na mara akaupokea kwa furaha.
<scripture passage="Matt 13:21" parsed="|Matt|13|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.21" />
<sup>21</sup>Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara.
<scripture passage="Matt 13:22" parsed="|Matt|13|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.22" />
<sup>22</sup>Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda.
<scripture passage="Matt 13:23" parsed="|Matt|13|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.23" />
<sup>23</sup>Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini."
<scripture passage="Matt 13:24" parsed="|Matt|13|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.24" />
<sup>24</sup>Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
<scripture passage="Matt 13:25" parsed="|Matt|13|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.25" />
<sup>25</sup>Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake.
<scripture passage="Matt 13:26" parsed="|Matt|13|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.26" />
<sup>26</sup>Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza kuonekana.
<scripture passage="Matt 13:27" parsed="|Matt|13|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.27" />
<sup>27</sup>Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, `Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa magugu yametoka wapi?`
<scripture passage="Matt 13:28" parsed="|Matt|13|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.28" />
<sup>28</sup>Yeye akawajibu, `Adui ndiye aliyefanya hivyo.` Basi, watumishi wake wakamwuliza, `Je, unataka twende tukayang`oe`
<scripture passage="Matt 13:29" parsed="|Matt|13|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.29" />
<sup>29</sup>Naye akawajibu, `La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang`oa na ngano pia.
<scripture passage="Matt 13:30" parsed="|Matt|13|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.30" />
<sup>30</sup>Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu."`
<scripture passage="Matt 13:31" parsed="|Matt|13|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.31" />
<sup>31</sup>Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake.
<scripture passage="Matt 13:32" parsed="|Matt|13|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.32" />
<sup>32</sup>Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake."
<scripture passage="Matt 13:33" parsed="|Matt|13|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.33" />
<sup>33</sup>Yesu akawaambia mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka."
<scripture passage="Matt 13:34" parsed="|Matt|13|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.34" />
<sup>34</sup>Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
<scripture passage="Matt 13:35" parsed="|Matt|13|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.35" />
<sup>35</sup>ili jambo lililonenwa na nabii litimie: "Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu."
<scripture passage="Matt 13:36" parsed="|Matt|13|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.36" />
<sup>36</sup>Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani."
<scripture passage="Matt 13:37" parsed="|Matt|13|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.37" />
<sup>37</sup>Yesu akawaambia, "Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
<scripture passage="Matt 13:38" parsed="|Matt|13|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.38" />
<sup>38</sup>Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.
<scripture passage="Matt 13:39" parsed="|Matt|13|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.39" />
<sup>39</sup>Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.
<scripture passage="Matt 13:40" parsed="|Matt|13|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.40" />
<sup>40</sup>Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati;
<scripture passage="Matt 13:41" parsed="|Matt|13|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.41" />
<sup>41</sup>Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu,
<scripture passage="Matt 13:42" parsed="|Matt|13|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.42" />
<sup>42</sup>na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga meno.
<scripture passage="Matt 13:43" parsed="|Matt|13|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.43" />
<sup>43</sup>Kisha, wale wema watang`ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi, kama mna masikio!
<scripture passage="Matt 13:44" parsed="|Matt|13|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.44" />
<sup>44</sup>"Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
<scripture passage="Matt 13:45" parsed="|Matt|13|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.45" />
<sup>45</sup>"Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
<scripture passage="Matt 13:46" parsed="|Matt|13|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.46" />
<sup>46</sup>Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile.
<scripture passage="Matt 13:47" parsed="|Matt|13|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.47" />
<sup>47</sup>"Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
<scripture passage="Matt 13:48" parsed="|Matt|13|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.48" />
<sup>48</sup>Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.
<scripture passage="Matt 13:49" parsed="|Matt|13|49|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.49" />
<sup>49</sup>Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema,
<scripture passage="Matt 13:50" parsed="|Matt|13|50|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.50" />
<sup>50</sup>na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno."
<scripture passage="Matt 13:51" parsed="|Matt|13|51|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.51" />
<sup>51</sup>Yesu akawauliza, "Je, mmeelewa mambo haya yote?" Wakamjibu, "Naam."
<scripture passage="Matt 13:52" parsed="|Matt|13|52|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.52" />
<sup>52</sup>Naye akawaambia, "Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale."
<scripture passage="Matt 13:53" parsed="|Matt|13|53|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.53" />
<sup>53</sup>Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo,
<scripture passage="Matt 13:54" parsed="|Matt|13|54|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.54" />
<sup>54</sup>akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, "Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
<scripture passage="Matt 13:55" parsed="|Matt|13|55|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.55" />
<sup>55</sup>Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
<scripture passage="Matt 13:56" parsed="|Matt|13|56|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.56" />
<sup>56</sup>Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?"
<scripture passage="Matt 13:57" parsed="|Matt|13|57|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.57" />
<sup>57</sup>Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, "Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!"
<scripture passage="Matt 13:58" parsed="|Matt|13|58|0|0" osisRef="Bible:Matt.13.58" />
<sup>58</sup>Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 14" progress="5.46%" prev="Matt.13" next="Matt.15" id="Matt.14">
<h3 id="Matt.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Matt.14-p1">
<scripture passage="Matt 14:1" parsed="|Matt|14|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.1" />
<sup>1</sup>Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu.
<scripture passage="Matt 14:2" parsed="|Matt|14|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.2" />
<sup>2</sup>Basi, akawaambia watumishi wake, "Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake."
<scripture passage="Matt 14:3" parsed="|Matt|14|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.3" />
<sup>3</sup>Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa ni
<scripture passage="Matt 14:4" parsed="|Matt|14|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.4" />
<sup>4</sup>kwamba alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!"
<scripture passage="Matt 14:5" parsed="|Matt|14|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.5" />
<sup>5</sup>Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii.
<scripture passage="Matt 14:6" parsed="|Matt|14|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.6" />
<sup>6</sup>Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,
<scripture passage="Matt 14:7" parsed="|Matt|14|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.7" />
<sup>7</sup>hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba.
<scripture passage="Matt 14:8" parsed="|Matt|14|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.8" />
<sup>8</sup>Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, "Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji."
<scripture passage="Matt 14:9" parsed="|Matt|14|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.9" />
<sup>9</sup>Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.
<scripture passage="Matt 14:10" parsed="|Matt|14|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.10" />
<sup>10</sup>Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane.
<scripture passage="Matt 14:11" parsed="|Matt|14|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.11" />
<sup>11</sup>Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake.
<scripture passage="Matt 14:12" parsed="|Matt|14|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.12" />
<sup>12</sup>Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
<scripture passage="Matt 14:13" parsed="|Matt|14|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.13" />
<sup>13</sup>Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini.
<scripture passage="Matt 14:14" parsed="|Matt|14|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.14" />
<sup>14</sup>Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.
<scripture passage="Matt 14:15" parsed="|Matt|14|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.15" />
<sup>15</sup>Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula."
<scripture passage="Matt 14:16" parsed="|Matt|14|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.16" />
<sup>16</sup>Yesu akawaambia, "Si lazima waende, wapeni ninyi chakula."
<scripture passage="Matt 14:17" parsed="|Matt|14|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.17" />
<sup>17</sup>Lakini wao wakamwambia, "Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili."
<scripture passage="Matt 14:18" parsed="|Matt|14|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.18" />
<sup>18</sup>Yesu akawaambia, "Nileteeni hapa."
<scripture passage="Matt 14:19" parsed="|Matt|14|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.19" />
<sup>19</sup>Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
<scripture passage="Matt 14:20" parsed="|Matt|14|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.20" />
<sup>20</sup>Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.
<scripture passage="Matt 14:21" parsed="|Matt|14|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.21" />
<sup>21</sup>Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
<scripture passage="Matt 14:22" parsed="|Matt|14|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.22" />
<sup>22</sup>Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng`ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.
<scripture passage="Matt 14:23" parsed="|Matt|14|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.23" />
<sup>23</sup>Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake,
<scripture passage="Matt 14:24" parsed="|Matt|14|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.24" />
<sup>24</sup>na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
<scripture passage="Matt 14:25" parsed="|Matt|14|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.25" />
<sup>25</sup>Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.
<scripture passage="Matt 14:26" parsed="|Matt|14|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.26" />
<sup>26</sup>Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, "Ni mzimu!" Wakapiga kelele kwa hofu.
<scripture passage="Matt 14:27" parsed="|Matt|14|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.27" />
<sup>27</sup>Mara, Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"
<scripture passage="Matt 14:28" parsed="|Matt|14|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.28" />
<sup>28</sup>Petro akamwambia, "Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako."
<scripture passage="Matt 14:29" parsed="|Matt|14|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.29" />
<sup>29</sup>Yesu akasema, "Haya, njoo." Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
<scripture passage="Matt 14:30" parsed="|Matt|14|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.30" />
<sup>30</sup>Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, "Bwana, niokoe!"
<scripture passage="Matt 14:31" parsed="|Matt|14|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.31" />
<sup>31</sup>Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, "Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?"
<scripture passage="Matt 14:32" parsed="|Matt|14|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.
<scripture passage="Matt 14:33" parsed="|Matt|14|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.33" />
<sup>33</sup>Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, "Hakika wewe ni Mwana wa Mungu."
<scripture passage="Matt 14:34" parsed="|Matt|14|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.34" />
<sup>34</sup>Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.
<scripture passage="Matt 14:35" parsed="|Matt|14|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.35" />
<sup>35</sup>Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,
<scripture passage="Matt 14:36" parsed="|Matt|14|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.14.36" />
<sup>36</sup>wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusa walipona.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 15" progress="5.84%" prev="Matt.14" next="Matt.16" id="Matt.15">
<h3 id="Matt.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Matt.15-p1">
<scripture passage="Matt 15:1" parsed="|Matt|15|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.1" />
<sup>1</sup>Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza,
<scripture passage="Matt 15:2" parsed="|Matt|15|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.2" />
<sup>2</sup>"Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!"
<scripture passage="Matt 15:3" parsed="|Matt|15|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawajibu, "Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?
<scripture passage="Matt 15:4" parsed="|Matt|15|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.4" />
<sup>4</sup>Mungu amesema: `Waheshimu baba yako na mama yako,` na `Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe`.
<scripture passage="Matt 15:5" parsed="|Matt|15|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.5" />
<sup>5</sup>Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: `Kitu hiki nimemtolea Mungu,`
<scripture passage="Matt 15:6" parsed="|Matt|15|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.6" />
<sup>6</sup>basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.
<scripture passage="Matt 15:7" parsed="|Matt|15|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.7" />
<sup>7</sup>Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
<scripture passage="Matt 15:8" parsed="|Matt|15|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.8" />
<sup>8</sup>`Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
<scripture passage="Matt 15:9" parsed="|Matt|15|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.9" />
<sup>9</sup>Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu."`
<scripture passage="Matt 15:10" parsed="|Matt|15|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.10" />
<sup>10</sup>Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, "Sikilizeni na muelewe!
<scripture passage="Matt 15:11" parsed="|Matt|15|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.11" />
<sup>11</sup>Kitu kinachomtia mtu najisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi."
<scripture passage="Matt 15:12" parsed="|Matt|15|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.12" />
<sup>12</sup>Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, "Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?"
<scripture passage="Matt 15:13" parsed="|Matt|15|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.13" />
<sup>13</sup>Lakini yeye akawajibu, "Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakuupanda, utang`olewa.
<scripture passage="Matt 15:14" parsed="|Matt|15|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.14" />
<sup>14</sup>Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni."
<scripture passage="Matt 15:15" parsed="|Matt|15|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.15" />
<sup>15</sup>Petro akadakia, "Tufafanulie huo mfano."
<scripture passage="Matt 15:16" parsed="|Matt|15|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.16" />
<sup>16</sup>Yesu akasema, "Hata nyinyi hamwelewi?
<scripture passage="Matt 15:17" parsed="|Matt|15|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.17" />
<sup>17</sup>Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutupwa nje chooni?
<scripture passage="Matt 15:18" parsed="|Matt|15|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.18" />
<sup>18</sup>Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.
<scripture passage="Matt 15:19" parsed="|Matt|15|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.19" />
<sup>19</sup>Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.
<scripture passage="Matt 15:20" parsed="|Matt|15|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.20" />
<sup>20</sup>Hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi. Lakini kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu najisi."
<scripture passage="Matt 15:21" parsed="|Matt|15|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.21" />
<sup>21</sup>Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni.
<scripture passage="Matt 15:22" parsed="|Matt|15|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.22" />
<sup>22</sup>Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo."
<scripture passage="Matt 15:23" parsed="|Matt|15|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.23" />
<sup>23</sup>Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi, wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Mwambie aende zake kwa maana anatufuatafuata akipiga kelele."
<scripture passage="Matt 15:24" parsed="|Matt|15|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.24" />
<sup>24</sup>Yesu akajibu, "Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo."
<scripture passage="Matt 15:25" parsed="|Matt|15|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.25" />
<sup>25</sup>Hapo huyo mama akaja, akapiga magoti mbele yake, akasema, "Mheshimiwa, nisaidie."
<scripture passage="Matt 15:26" parsed="|Matt|15|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.26" />
<sup>26</sup>Yesu akamjibu, "Si sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
<scripture passage="Matt 15:27" parsed="|Matt|15|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.27" />
<sup>27</sup>Huyo mama akajibu, "Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao."
<scripture passage="Matt 15:28" parsed="|Matt|15|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.28" />
<sup>28</sup>Hapo Yesu akamjibu, "Mama, imani yako ni kubwa; basi, ufanyiwe kama unavyotaka." Yule binti yake akapona tangu saa hiyo wakati huohuo.
<scripture passage="Matt 15:29" parsed="|Matt|15|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.29" />
<sup>29</sup>Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwa Galilaya, akapanda mlimani, akaketi.
<scripture passage="Matt 15:30" parsed="|Matt|15|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.30" />
<sup>30</sup>Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
<scripture passage="Matt 15:31" parsed="|Matt|15|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.31" />
<sup>31</sup>Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamsifu Mungu wa Israeli.
<scripture passage="Matt 15:32" parsed="|Matt|15|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.32" />
<sup>32</sup>Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, "Nawaonea watu hawa huruma kwa sababu kwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende bila kula wasije wakazimia njiani."
<scripture passage="Matt 15:33" parsed="|Matt|15|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.33" />
<sup>33</sup>Wanafunzi wakamwambia, "Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?"
<scripture passage="Matt 15:34" parsed="|Matt|15|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Wakamjibu, "Saba na visamaki vichache."
<scripture passage="Matt 15:35" parsed="|Matt|15|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.35" />
<sup>35</sup>Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini.
<scripture passage="Matt 15:36" parsed="|Matt|15|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.36" />
<sup>36</sup>Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
<scripture passage="Matt 15:37" parsed="|Matt|15|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.37" />
<sup>37</sup>Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya makombo, wakajaza vikapu saba.
<scripture passage="Matt 15:38" parsed="|Matt|15|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.38" />
<sup>38</sup>Hao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.
<scripture passage="Matt 15:39" parsed="|Matt|15|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.15.39" />
<sup>39</sup>Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la Magadani.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 16" progress="6.25%" prev="Matt.15" next="Matt.17" id="Matt.16">
<h3 id="Matt.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Matt.16-p1">
<scripture passage="Matt 16:1" parsed="|Matt|16|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.1" />
<sup>1</sup>Mafarisayo na Masadukayo walimwendea Yesu, na kwa kumjaribu, wakamwomba afanye ishara itokayo mbinguni.
<scripture passage="Matt 16:2" parsed="|Matt|16|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.2" />
<sup>2</sup>Lakini Yesu akawajibu, "Wakati wa jioni ukifika ninyi husema: `Hali ya hewa itakuwa nzuri kwa maana anga ni jekundu!`
<scripture passage="Matt 16:3" parsed="|Matt|16|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.3" />
<sup>3</sup>Na alfajiri mwasema: `Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda!` Basi, ninyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.
<scripture passage="Matt 16:4" parsed="|Matt|16|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.4" />
<sup>4</sup>Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara yoyote isipokuwa tu ile ya Yona." Basi, akawaacha, akaenda zake.
<scripture passage="Matt 16:5" parsed="|Matt|16|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.5" />
<sup>5</sup>Wanafunzi wake walipokwisha vukia upande wa pili wa ziwa, walijikuta wamesahau kuchukua mikate.
<scripture passage="Matt 16:6" parsed="|Matt|16|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.6" />
<sup>6</sup>Yesu akawaambia, "Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!"
<scripture passage="Matt 16:7" parsed="|Matt|16|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.7" />
<sup>7</sup>Lakini wao wakawa wanajadiliana: "Anasema hivyo kwa kuwa hatukuchukua mikate."
<scripture passage="Matt 16:8" parsed="|Matt|16|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.8" />
<sup>8</sup>Yesu alijua mawazo yao, akawaambia, "Enyi watu wenye imani haba! Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate?
<scripture passage="Matt 16:9" parsed="|Matt|16|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.9" />
<sup>9</sup>Je, hamjaelewa bado? Je, hamkumbuki nilipoimega ile mikate mitano kwa ajili ya wale watu elfu tano? Je, mlijaza vikapu vingapi vya makombo?
<scripture passage="Matt 16:10" parsed="|Matt|16|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.10" />
<sup>10</sup>Au, ile mikate saba waliyogawiwa wale watu elfu nne, je, mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?
<scripture passage="Matt 16:11" parsed="|Matt|16|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.11" />
<sup>11</sup>Inawezekanaje hamwelewi ya kwamba sikuwa nikisema juu ya mikate? Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!"
<scripture passage="Matt 16:12" parsed="|Matt|16|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.12" />
<sup>12</sup>Hapo wanafunzi wakafahamu kwamba aliwaambia wajihadhari siyo na chachu ya mikate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
<scripture passage="Matt 16:13" parsed="|Matt|16|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.13" />
<sup>13</sup>Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?"
<scripture passage="Matt 16:14" parsed="|Matt|16|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.14" />
<sup>14</sup>Wakamjibu, "Wengine wanasema kuwa ni Yohane mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii."
<scripture passage="Matt 16:15" parsed="|Matt|16|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.15" />
<sup>15</sup>Yesu akawauliza, "Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?"
<scripture passage="Matt 16:16" parsed="|Matt|16|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.16" />
<sup>16</sup>Simoni Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai."
<scripture passage="Matt 16:17" parsed="|Matt|16|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.17" />
<sup>17</sup>Yesu akasema, "Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si binadamu aliyekufunulia ukweli huu, ila Baba yangu aliye mbinguni.
<scripture passage="Matt 16:18" parsed="|Matt|16|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.18" />
<sup>18</sup>Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba<i>ff</i> huu nitalijenga kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda.
<scripture passage="Matt 16:19" parsed="|Matt|16|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.19" />
<sup>19</sup>Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni."
<scripture passage="Matt 16:20" parsed="|Matt|16|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.20" />
<sup>20</sup>Kisha akawaonya wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.
<scripture passage="Matt 16:21" parsed="|Matt|16|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.21" />
<sup>21</sup>Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake: "Ni lazima mimi niende Yerusalemu, na huko nikapate mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Nitauawa, na siku ya tatu nitafufuliwa."
<scripture passage="Matt 16:22" parsed="|Matt|16|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.22" />
<sup>22</sup>Hapo Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea: "Isiwe hivyo Bwana! Jambo hili halitakupata!"
<scripture passage="Matt 16:23" parsed="|Matt|16|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.23" />
<sup>23</sup>Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, "Ondoka mbele yangu Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungu bali ni ya kibinadamu!"
<scripture passage="Matt 16:24" parsed="|Matt|16|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.24" />
<sup>24</sup>Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kama mtu yeyote anataka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
<scripture passage="Matt 16:25" parsed="|Matt|16|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.25" />
<sup>25</sup>Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza;
<scripture passage="Matt 16:26" parsed="|Matt|16|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.26" />
<sup>26</sup>lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
<scripture passage="Matt 16:27" parsed="|Matt|16|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.27" />
<sup>27</sup>Maana, Mwana wa Mtu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika wake, na hapo ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.
<scripture passage="Matt 16:28" parsed="|Matt|16|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.16.28" />
<sup>28</sup>Kweli nawaambieni, wako wengine papahapa ambao hawatakufa kabla ya kumwona Mwana wa Mtu akija katika Ufalme wake."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 17" progress="6.61%" prev="Matt.16" next="Matt.18" id="Matt.17">
<h3 id="Matt.17-p0.1">Chapter 17</h3>
<p id="Matt.17-p1">
<scripture passage="Matt 17:1" parsed="|Matt|17|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.1" />
<sup>1</sup>Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.
<scripture passage="Matt 17:2" parsed="|Matt|17|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.2" />
<sup>2</sup>Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang`aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
<scripture passage="Matt 17:3" parsed="|Matt|17|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.3" />
<sup>3</sup>Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
<scripture passage="Matt 17:4" parsed="|Matt|17|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.4" />
<sup>4</sup>Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."
<scripture passage="Matt 17:5" parsed="|Matt|17|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.5" />
<sup>5</sup>Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni."
<scripture passage="Matt 17:6" parsed="|Matt|17|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.6" />
<sup>6</sup>Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
<scripture passage="Matt 17:7" parsed="|Matt|17|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.7" />
<sup>7</sup>Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, "Simameni, msiogope!"
<scripture passage="Matt 17:8" parsed="|Matt|17|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.8" />
<sup>8</sup>Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.
<scripture passage="Matt 17:9" parsed="|Matt|17|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.9" />
<sup>9</sup>Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: "Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu."
<scripture passage="Matt 17:10" parsed="|Matt|17|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.10" />
<sup>10</sup>Kisha wanafunzi wakamwuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliya aje?"
<scripture passage="Matt 17:11" parsed="|Matt|17|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.11" />
<sup>11</sup>Yesu akawajibu, "Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
<scripture passage="Matt 17:12" parsed="|Matt|17|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.12" />
<sup>12</sup>Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao."
<scripture passage="Matt 17:13" parsed="|Matt|17|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.13" />
<sup>13</sup>Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji.
<scripture passage="Matt 17:14" parsed="|Matt|17|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.14" />
<sup>14</sup>Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia magoti,
<scripture passage="Matt 17:15" parsed="|Matt|17|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.15" />
<sup>15</sup>akasema, "Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
<scripture passage="Matt 17:16" parsed="|Matt|17|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.16" />
<sup>16</sup>Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya."
<scripture passage="Matt 17:17" parsed="|Matt|17|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.17" />
<sup>17</sup>Yesu akajibu, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto."
<scripture passage="Matt 17:18" parsed="|Matt|17|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.18" />
<sup>18</sup>Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo.
<scripture passage="Matt 17:19" parsed="|Matt|17|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.19" />
<sup>19</sup>Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, "Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?"
<scripture passage="Matt 17:20" parsed="|Matt|17|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.20" />
<sup>20</sup>Yesu akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: `Toka hapa uende pale,` nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu."<i>fg</i> kuondolewa ila kwa sala na kufunga."
<scripture passage="Matt 17:21" parsed="|Matt|17|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.21" />
<sup>21</sup>missing
<scripture passage="Matt 17:22" parsed="|Matt|17|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.22" />
<sup>22</sup>Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, "Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu.
<scripture passage="Matt 17:23" parsed="|Matt|17|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.23" />
<sup>23</sup>Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa." Wanafunzi wakahuzunika mno.
<scripture passage="Matt 17:24" parsed="|Matt|17|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.24" />
<sup>24</sup>Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?"
<scripture passage="Matt 17:25" parsed="|Matt|17|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.25" />
<sup>25</sup>Petro akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?"
<scripture passage="Matt 17:26" parsed="|Matt|17|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.26" />
<sup>26</sup>Petro akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya basi, wananchi hawahusiki.
<scripture passage="Matt 17:27" parsed="|Matt|17|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.17.27" />
<sup>27</sup>Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 18" progress="6.93%" prev="Matt.17" next="Matt.19" id="Matt.18">
<h3 id="Matt.18-p0.1">Chapter 18</h3>
<p id="Matt.18-p1">
<scripture passage="Matt 18:1" parsed="|Matt|18|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.1" />
<sup>1</sup>Wakati ule wanafunzi walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni?"
<scripture passage="Matt 18:2" parsed="|Matt|18|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.2" />
<sup>2</sup>Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamisha kati yao,
<scripture passage="Matt 18:3" parsed="|Matt|18|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.3" />
<sup>3</sup>kisha akasema, "Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 18:4" parsed="|Matt|18|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.4" />
<sup>4</sup>Yeyote anayejinyenyekesha kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 18:5" parsed="|Matt|18|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.5" />
<sup>5</sup>Yeyote anayemkaribisha mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi.
<scripture passage="Matt 18:6" parsed="|Matt|18|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.6" />
<sup>6</sup>"Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
<scripture passage="Matt 18:7" parsed="|Matt|18|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.7" />
<sup>7</sup>Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
<scripture passage="Matt 18:8" parsed="|Matt|18|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.8" />
<sup>8</sup>"Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili.
<scripture passage="Matt 18:9" parsed="|Matt|18|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.9" />
<sup>9</sup>Na kama jicho lako likikukosesha, ling`oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
<scripture passage="Matt 18:10" parsed="|Matt|18|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.10" />
<sup>10</sup>"Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Nawaambieni, malaika wao huko mbinguni wako daima mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.<i>fh</i>
<scripture passage="Matt 18:11" parsed="|Matt|18|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.11" />
<sup>11</sup>missing
<scripture passage="Matt 18:12" parsed="|Matt|18|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.12" />
<sup>12</sup>Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yule aliyepotea.
<scripture passage="Matt 18:13" parsed="|Matt|18|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.13" />
<sup>13</sup>Akimpata, nawaambieni kweli, humfurahia huyo kuliko awafurahiavyo wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
<scripture passage="Matt 18:14" parsed="|Matt|18|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.14" />
<sup>14</sup>Hali kadhalika, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa wadogo apotee.
<scripture passage="Matt 18:15" parsed="|Matt|18|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.15" />
<sup>15</sup>"Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
<scripture passage="Matt 18:16" parsed="|Matt|18|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.16" />
<sup>16</sup>Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
<scripture passage="Matt 18:17" parsed="|Matt|18|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.17" />
<sup>17</sup>Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.
<scripture passage="Matt 18:18" parsed="|Matt|18|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.18" />
<sup>18</sup>"Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.
<scripture passage="Matt 18:19" parsed="|Matt|18|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.19" />
<sup>19</sup>Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
<scripture passage="Matt 18:20" parsed="|Matt|18|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.20" />
<sup>20</sup>Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao."
<scripture passage="Matt 18:21" parsed="|Matt|18|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.21" />
<sup>21</sup>Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, "Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?"
<scripture passage="Matt 18:22" parsed="|Matt|18|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.22" />
<sup>22</sup>Yesu akamjibu, "Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
<scripture passage="Matt 18:23" parsed="|Matt|18|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.23" />
<sup>23</sup>Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
<scripture passage="Matt 18:24" parsed="|Matt|18|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.24" />
<sup>24</sup>Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
<scripture passage="Matt 18:25" parsed="|Matt|18|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.25" />
<sup>25</sup>Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe.
<scripture passage="Matt 18:26" parsed="|Matt|18|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.26" />
<sup>26</sup>Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, `Unisubiri nami nitakulipa deni lote.`
<scripture passage="Matt 18:27" parsed="|Matt|18|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.27" />
<sup>27</sup>Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
<scripture passage="Matt 18:28" parsed="|Matt|18|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.28" />
<sup>28</sup>"Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, `Lipa deni lako!`
<scripture passage="Matt 18:29" parsed="|Matt|18|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.29" />
<sup>29</sup>Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, `Unisubiri nami nitalipa deni langu lote.`
<scripture passage="Matt 18:30" parsed="|Matt|18|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.30" />
<sup>30</sup>Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
<scripture passage="Matt 18:31" parsed="|Matt|18|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.31" />
<sup>31</sup>"Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
<scripture passage="Matt 18:32" parsed="|Matt|18|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.32" />
<sup>32</sup>Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, `Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
<scripture passage="Matt 18:33" parsed="|Matt|18|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.33" />
<sup>33</sup>Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?`
<scripture passage="Matt 18:34" parsed="|Matt|18|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.34" />
<sup>34</sup>"Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
<scripture passage="Matt 18:35" parsed="|Matt|18|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.18.35" />
<sup>35</sup>Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 19" progress="7.34%" prev="Matt.18" next="Matt.20" id="Matt.19">
<h3 id="Matt.19-p0.1">Chapter 19</h3>
<p id="Matt.19-p1">
<scripture passage="Matt 19:1" parsed="|Matt|19|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, alitoka Galilaya, akaenda katika mkoa wa Yudea, ng`ambo ya mto Yordani.
<scripture passage="Matt 19:2" parsed="|Matt|19|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.2" />
<sup>2</sup>Watu wengi walimfuata huko, naye akawaponya.
<scripture passage="Matt 19:3" parsed="|Matt|19|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.3" />
<sup>3</sup>Mafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, "Je, ni halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?"
<scripture passage="Matt 19:4" parsed="|Matt|19|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.4" />
<sup>4</sup>Yesu akawajibu, "Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke,
<scripture passage="Matt 19:5" parsed="|Matt|19|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.5" />
<sup>5</sup>na akasema: `Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?`
<scripture passage="Matt 19:6" parsed="|Matt|19|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.6" />
<sup>6</sup>Kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe."
<scripture passage="Matt 19:7" parsed="|Matt|19|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.7" />
<sup>7</sup>Lakini wao wakamwuliza, "Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamke apewe hati ya talaka na kuachwa?"
<scripture passage="Matt 19:8" parsed="|Matt|19|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.8" />
<sup>8</sup>Yesu akawajibu, "Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
<scripture passage="Matt 19:9" parsed="|Matt|19|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.9" />
<sup>9</sup>Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini."
<scripture passage="Matt 19:10" parsed="|Matt|19|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.10" />
<sup>10</sup>Wanafunzi wake wakamwambia, "Ikiwa mambo ya mume na mkewe ni hivyo, ni afadhali kutooa kabisa."
<scripture passage="Matt 19:11" parsed="|Matt|19|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.11" />
<sup>11</sup>Yesu akawaambia, "Si wote wanaoweza kulipokea fundisho hili, isipokuwa tu wale waliojaliwa na Mungu.
<scripture passage="Matt 19:12" parsed="|Matt|19|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.12" />
<sup>12</sup>Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee."
<scripture passage="Matt 19:13" parsed="|Matt|19|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.13" />
<sup>13</sup>Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
<scripture passage="Matt 19:14" parsed="|Matt|19|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.14" />
<sup>14</sup>Yesu akasema, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie; maana Ufalme wa mbinguni ni wa watu walio kama watoto hawa."
<scripture passage="Matt 19:15" parsed="|Matt|19|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.15" />
<sup>15</sup>Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo.
<scripture passage="Matt 19:16" parsed="|Matt|19|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.16" />
<sup>16</sup>Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, "Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uzima wa milele?"
<scripture passage="Matt 19:17" parsed="|Matt|19|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.17" />
<sup>17</sup>Yesu akamwambia, "Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uzima, shika amri."
<scripture passage="Matt 19:18" parsed="|Matt|19|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.18" />
<sup>18</sup>Yule mtu akamwuliza, "Amri zipi?" Yesu akasema, "Usiue, usizini, usiibe, usitoe ushahidi wa uongo,
<scripture passage="Matt 19:19" parsed="|Matt|19|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.19" />
<sup>19</sup>waheshimu baba yako na mama yako; na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
<scripture passage="Matt 19:20" parsed="|Matt|19|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.20" />
<sup>20</sup>Huyo kijana akamwambia, "Hayo yote nimeyazingatia tangu utoto wangu; sasa nifanye nini zaidi?"
<scripture passage="Matt 19:21" parsed="|Matt|19|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.21" />
<sup>21</sup>Yesu akamwambia, "Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako uwape maskini hiyo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate."
<scripture passage="Matt 19:22" parsed="|Matt|19|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.22" />
<sup>22</sup>Huyo kijana aliposikia hayo, alienda zake akiwa mwenye huzuni, maana alikuwa na mali nyingi.
<scripture passage="Matt 19:23" parsed="|Matt|19|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.23" />
<sup>23</sup>Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kweli nawaambieni, itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.
<scripture passage="Matt 19:24" parsed="|Matt|19|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.24" />
<sup>24</sup>Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
<scripture passage="Matt 19:25" parsed="|Matt|19|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.25" />
<sup>25</sup>Wale wanafunzi waliposikia hivyo walishangaa, wakamwuliza, "Ni nani basi, awezaye kuokoka?"
<scripture passage="Matt 19:26" parsed="|Matt|19|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.26" />
<sup>26</sup>Yesu akawatazama, akasema, "Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana."
<scripture passage="Matt 19:27" parsed="|Matt|19|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.27" />
<sup>27</sup>Kisha Petro akasema, "Na sisi je? Tumeacha yote tukakufuata; tutapata nini basi?"
<scripture passage="Matt 19:28" parsed="|Matt|19|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.28" />
<sup>28</sup>Yesu akawaambia, "Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake katika ulimwengu mpya, ninyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
<scripture passage="Matt 19:29" parsed="|Matt|19|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.29" />
<sup>29</sup>Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uzima wa milele.
<scripture passage="Matt 19:30" parsed="|Matt|19|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.19.30" />
<sup>30</sup>Lakini walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 20" progress="7.71%" prev="Matt.19" next="Matt.21" id="Matt.20">
<h3 id="Matt.20-p0.1">Chapter 20</h3>
<p id="Matt.20-p1">
<scripture passage="Matt 20:1" parsed="|Matt|20|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.1" />
<sup>1</sup>"Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu, ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake.
<scripture passage="Matt 20:2" parsed="|Matt|20|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.2" />
<sup>2</sup>Akapatana nao kuwalipa dinari moja kwa siku, kisha akawapeleka katika shamba lake la mizabibu.
<scripture passage="Matt 20:3" parsed="|Matt|20|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.3" />
<sup>3</sup>Akatoka mnamo saa tatu asubuhi, akaona watu wengine wamesimama sokoni, hawana kazi.
<scripture passage="Matt 20:4" parsed="|Matt|20|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.4" />
<sup>4</sup>Akawaambia, `Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.`
<scripture passage="Matt 20:5" parsed="|Matt|20|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.5" />
<sup>5</sup>Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo.
<scripture passage="Matt 20:6" parsed="|Matt|20|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.6" />
<sup>6</sup>Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, `Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?`
<scripture passage="Matt 20:7" parsed="|Matt|20|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.7" />
<sup>7</sup>Wakamjibu: `Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri.` Yeye akawaambia, `Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu.`
<scripture passage="Matt 20:8" parsed="|Matt|20|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.8" />
<sup>8</sup>"Kulipokuchwa, huyo mwenye shamba alimwambia mtunza hazina wake, `Waite wafanyakazi ukawalipe mshahara wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho, na kumalizia na wale wa kwanza.`
<scripture passage="Matt 20:9" parsed="|Matt|20|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.9" />
<sup>9</sup>Basi, wakaja wale walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakapokea kila mmoja dinari moja.
<scripture passage="Matt 20:10" parsed="|Matt|20|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.10" />
<sup>10</sup>Wale wa kwanza walipofika, walikuwa wanadhani watapewa zaidi; lakini hata wao wakapewa kila mmoja dinari moja.
<scripture passage="Matt 20:11" parsed="|Matt|20|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.11" />
<sup>11</sup>Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnung`unikia yule bwana.
<scripture passage="Matt 20:12" parsed="|Matt|20|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.12" />
<sup>12</sup>Wakasema, `Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?`
<scripture passage="Matt 20:13" parsed="|Matt|20|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.13" />
<sup>13</sup>"Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, `Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana nami mshahara wa denari moja?
<scripture passage="Matt 20:14" parsed="|Matt|20|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.14" />
<sup>14</sup>Chukua haki yako, uende zako. Napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
<scripture passage="Matt 20:15" parsed="|Matt|20|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.15" />
<sup>15</sup>Je, sina haki ya kufanya na mali yangu nipendavyo? Je, unaona kijicho kwa kuwa mimi ni mwema?"`
<scripture passage="Matt 20:16" parsed="|Matt|20|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.16" />
<sup>16</sup>Yesu akamaliza kwa kusema, "Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho."
<scripture passage="Matt 20:17" parsed="|Matt|20|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.17" />
<sup>17</sup>Yesu alipokuwa anakwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
<scripture passage="Matt 20:18" parsed="|Matt|20|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.18" />
<sup>18</sup>"Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe.
<scripture passage="Matt 20:19" parsed="|Matt|20|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.19" />
<sup>19</sup>Watamkabidhi kwa watu wa mataifa mengine ili adhihakiwe, apigwe viboko na kusulubiwa; lakini siku ya tatu atafufuliwa."
<scripture passage="Matt 20:20" parsed="|Matt|20|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.20" />
<sup>20</sup>Hapo mama yao wana wa Zebedayo alimjia Yesu pamoja na wanawe, akapiga magoti mbele yake na kumwomba kitu.
<scripture passage="Matt 20:21" parsed="|Matt|20|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.21" />
<sup>21</sup>Yesu akamwuliza, "Unataka nini?" Huyo mama akamwambia, "Ahidi kwamba katika Ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto."
<scripture passage="Matt 20:22" parsed="|Matt|20|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.22" />
<sup>22</sup>Yesu akajibu, "Hamjui mnaomba nini. Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa mimi?" Wakamjibu, "Tunaweza."
<scripture passage="Matt 20:23" parsed="|Matt|20|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.23" />
<sup>23</sup>Yesu akawaambia, "Kweli mtakunywa kikombe changu, lakini kuketi kulia au kushoto kwangu si kazi yangu kupanga; jambo hilo watapewa wale waliowekewa tayari na Baba yangu."
<scripture passage="Matt 20:24" parsed="|Matt|20|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.24" />
<sup>24</sup>Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakawakasirikia hao ndugu wawili.
<scripture passage="Matt 20:25" parsed="|Matt|20|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.25" />
<sup>25</sup>Hivyo Yesu akawaita, akawaambia, "Mnajua kwamba watawala wa mataifa hutawala watu wao kwa mabavu na wakuu hao huwamiliki watu wao.
<scripture passage="Matt 20:26" parsed="|Matt|20|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.26" />
<sup>26</sup>Lakini kwenu isiwe hivyo, ila yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote;
<scripture passage="Matt 20:27" parsed="|Matt|20|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.27" />
<sup>27</sup>na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.
<scripture passage="Matt 20:28" parsed="|Matt|20|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.28" />
<sup>28</sup>Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi."
<scripture passage="Matt 20:29" parsed="|Matt|20|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.29" />
<sup>29</sup>Yesu alipokuwa anaondoka mjini Yeriko, umati wa watu ulimfuata.
<scripture passage="Matt 20:30" parsed="|Matt|20|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.30" />
<sup>30</sup>Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
<scripture passage="Matt 20:31" parsed="|Matt|20|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.31" />
<sup>31</sup>Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
<scripture passage="Matt 20:32" parsed="|Matt|20|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.32" />
<sup>32</sup>Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
<scripture passage="Matt 20:33" parsed="|Matt|20|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.33" />
<sup>33</sup>Wakamjibu, "Mheshimiwa, tunaomba macho yetu yafumbuliwe."
<scripture passage="Matt 20:34" parsed="|Matt|20|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.20.34" />
<sup>34</sup>Basi, Yesu akawaonea huruma, akawagusa macho yao, na papo hapo wakaweza kuona, wakamfuata.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 21" progress="8.11%" prev="Matt.20" next="Matt.22" id="Matt.21">
<h3 id="Matt.21-p0.1">Chapter 21</h3>
<p id="Matt.21-p1">
<scripture passage="Matt 21:1" parsed="|Matt|21|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.1" />
<sup>1</sup>Yesu na wanafunzi wake walipokaribia Yerusalemu na kufika Bethfage katika mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
<scripture passage="Matt 21:2" parsed="|Matt|21|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.2" />
<sup>2</sup>akawaambia, "Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu na mtamkuta punda amefungwa na mtoto wake. Wafungueni mkawalete kwangu.
<scripture passage="Matt 21:3" parsed="|Matt|21|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.3" />
<sup>3</sup>Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, `Bwana anawahitaji,` naye atawaachieni mara."
<scripture passage="Matt 21:4" parsed="|Matt|21|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.4" />
<sup>4</sup>Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii yatimie:
<scripture passage="Matt 21:5" parsed="|Matt|21|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.5" />
<sup>5</sup>"Uambieni mji wa Sioni: Tazama, Mfalme wako anakujia! Ni mpole na amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda."
<scripture passage="Matt 21:6" parsed="|Matt|21|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.6" />
<sup>6</sup>Hivyo, wale wanafunzi walienda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza.
<scripture passage="Matt 21:7" parsed="|Matt|21|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.7" />
<sup>7</sup>Wakamleta yule punda na mtoto wake, wakatandika nguo zao juu yao na Yesu akaketi juu yake.
<scripture passage="Matt 21:8" parsed="|Matt|21|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.8" />
<sup>8</sup>Umati mkubwa wa watu ukatandaza nguo zao barabarani, na watu wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani.
<scripture passage="Matt 21:9" parsed="|Matt|21|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.9" />
<sup>9</sup>Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaaza sauti: "Hosana Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Hosana Mungu juu mbinguni!"
<scripture passage="Matt 21:10" parsed="|Matt|21|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.10" />
<sup>10</sup>Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, "Huyu ni nani?"
<scripture passage="Matt 21:11" parsed="|Matt|21|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.11" />
<sup>11</sup>Watu katika ule umati wakasema, "Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti katika mkoa wa Galilaya."
<scripture passage="Matt 21:12" parsed="|Matt|21|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.12" />
<sup>12</sup>Basi, Yesu akaingia Hekaluni, akawafukuza nje watu waliokuwa wanauza na kununua vitu ndani ya Hekalu; akazipindua meza za wale waliokuwa wanavunja fedha, na viti vya wale waliokuwa wanauza njiwa.
<scripture passage="Matt 21:13" parsed="|Matt|21|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.13" />
<sup>13</sup>Akawaambia, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala.` Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi."
<scripture passage="Matt 21:14" parsed="|Matt|21|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.14" />
<sup>14</sup>Vipofu na vilema walimwendea huko Hekaluni, naye Yesu akawaponya.
<scripture passage="Matt 21:15" parsed="|Matt|21|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.15" />
<sup>15</sup>Basi, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaaza sauti zao Hekaluni wakisema: "Sifa kwa Mwana wa Daudi," wakakasirika.
<scripture passage="Matt 21:16" parsed="|Matt|21|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.16" />
<sup>16</sup>Hivyo wakamwambia, "Je, husikii wanachosema?" Yesu akawajibu, "Naam, nasikia! Je hamjasoma Maandiko haya Matakatifu? `Kwa vinywa vya watoto wadogo na wanyonyao unajipatia sifa kamilifu."`
<scripture passage="Matt 21:17" parsed="|Matt|21|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.17" />
<sup>17</sup>Basi, akawaacha, akatoka nje ya mji na kwenda Bethania, akalala huko.
<scripture passage="Matt 21:18" parsed="|Matt|21|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.18" />
<sup>18</sup>Yesu alipokuwa anarudi mjini asubuhi na mapema, aliona njaa.
<scripture passage="Matt 21:19" parsed="|Matt|21|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.19" />
<sup>19</sup>Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauma chochote ila majani matupu. Basi akauambia, "Usizae tena matunda milele!" Papo hapo huo mtini ukanyauka.
<scripture passage="Matt 21:20" parsed="|Matt|21|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.20" />
<sup>20</sup>Wanafunzi walipouona walishangaa wakisema, "Kwa nini mtini huu umenyauka ghafla?"
<scripture passage="Matt 21:21" parsed="|Matt|21|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.21" />
<sup>21</sup>Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani bila kuwa na mashaka, mnaweza si tu kufanya hivyo, bali hata mkiuambia mlima huu: `Ng`oka ukajitose baharini,` itafanyika hivyo.
<scripture passage="Matt 21:22" parsed="|Matt|21|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.22" />
<sup>22</sup>Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba katika sala, mtapata."
<scripture passage="Matt 21:23" parsed="|Matt|21|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.23" />
<sup>23</sup>Yesu aliingia Hekaluni, akawa anafundisha. Alipokuwa akifundisha, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani amekupa mamlaka haya?"
<scripture passage="Matt 21:24" parsed="|Matt|21|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.24" />
<sup>24</sup>Yesu akawajibu, "Na mimi nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, basi nami nitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.
<scripture passage="Matt 21:25" parsed="|Matt|21|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.25" />
<sup>25</sup>Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa nani? Je, yalitoka mbinguni ama kwa watu?" Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi: "Tukisema, `Yalitoka mbinguni`, atatuuliza, `Basi, mbona hamkumsadiki?`
<scripture passage="Matt 21:26" parsed="|Matt|21|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.26" />
<sup>26</sup>Na tukisema, `Yalitoka kwa watu,` tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii."
<scripture passage="Matt 21:27" parsed="|Matt|21|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.27" />
<sup>27</sup>Basi, wakamjibu, "Hatujui!" Naye Yesu akawaambia, "Nami pia sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.
<scripture passage="Matt 21:28" parsed="|Matt|21|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.28" />
<sup>28</sup>"Ninyi mnaonaje; mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwambia yule wa kwanza, `Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu.`
<scripture passage="Matt 21:29" parsed="|Matt|21|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.29" />
<sup>29</sup>Yule kijana akamwambia, `Sitaki!` Lakini baadaye akabadili nia, akaenda kufanya kazi.
<scripture passage="Matt 21:30" parsed="|Matt|21|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.30" />
<sup>30</sup>Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, `Naam baba!` Lakini hakwenda kazini.
<scripture passage="Matt 21:31" parsed="|Matt|21|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.31" />
<sup>31</sup>Je, ni nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba yake?" Wakamjibu, "Yule mtoto wa kwanza." Basi, Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, watoza ushuru na waasherati wataingia katika Ufalme wa Mungu kabla yenu.
<scripture passage="Matt 21:32" parsed="|Matt|21|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.32" />
<sup>32</sup>Maana Yohane alikuja kwenu akawaonyesha njia njema ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote ninyi hamkubadili mioyo yenu, na hamkusadiki."
<scripture passage="Matt 21:33" parsed="|Matt|21|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.33" />
<sup>33</sup>Yesu akasema, "Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda nchi ya mbali.
<scripture passage="Matt 21:34" parsed="|Matt|21|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.34" />
<sup>34</sup>Wakati wa mavuno ulipofika, aliwatuma watumishi wake kwa wale wakulima, ili wakachukue sehemu ya mavuno yake.
<scripture passage="Matt 21:35" parsed="|Matt|21|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.35" />
<sup>35</sup>Wale wakulima wakawakamata hao watumishi; mmoja wakampiga, mwingine wakamwua na mwingine wakampiga mawe.
<scripture passage="Matt 21:36" parsed="|Matt|21|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.36" />
<sup>36</sup>Huyo mtu akawatuma tena watumishi wengine, wengi kuliko wa safari ya kwanza. Wale wakulima wakawatendea namna ileile.
<scripture passage="Matt 21:37" parsed="|Matt|21|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.37" />
<sup>37</sup>Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: `Watamheshimu mwanangu.`
<scripture passage="Matt 21:38" parsed="|Matt|21|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.38" />
<sup>38</sup>Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: `Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake!`
<scripture passage="Matt 21:39" parsed="|Matt|21|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.39" />
<sup>39</sup>Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua.
<scripture passage="Matt 21:40" parsed="|Matt|21|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.40" />
<sup>40</sup>"Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?"
<scripture passage="Matt 21:41" parsed="|Matt|21|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.41" />
<sup>41</sup>Wao wakamjibu, "Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wa mavuno."
<scripture passage="Matt 21:42" parsed="|Matt|21|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.42" />
<sup>42</sup>Hapo Yesu akawaambia, "Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? `Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!`
<scripture passage="Matt 21:43" parsed="|Matt|21|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.43" />
<sup>43</sup>"Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wa mataifa mengine wenye kutoa matunda yake."<i>fi</i> likimwangukia mtu yeyote, litamponda."
<scripture passage="Matt 21:44" parsed="|Matt|21|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.44" />
<sup>44</sup>missing
<scripture passage="Matt 21:45" parsed="|Matt|21|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.45" />
<sup>45</sup>Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia hiyo mifano yake walitambua kwamba alikuwa anawasema wao.
<scripture passage="Matt 21:46" parsed="|Matt|21|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.21.46" />
<sup>46</sup>Kwa hiyo wakawa wanatafuta njia ya kumtia nguvuni, lakini waliwaogopa watu kwa sababu wao walimtambua yeye kuwa nabii.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 22" progress="8.71%" prev="Matt.21" next="Matt.24" id="Matt.22">
<h3 id="Matt.22-p0.1">Chapter 22</h3>
<p id="Matt.22-p1">
<scripture passage="Matt 22:1" parsed="|Matt|22|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.1" />
<sup>1</sup>Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:

<sup>1</sup>Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,
<scripture passage="Matt 22:2" parsed="|Matt|22|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.2" />
<sup>2</sup>"Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.

<sup>2</sup>"Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose.
<scripture passage="Matt 22:3" parsed="|Matt|22|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.3" />
<sup>3</sup>Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.

<sup>3</sup>Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
<scripture passage="Matt 22:4" parsed="|Matt|22|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.4" />
<sup>4</sup>Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, `Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng`ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.`

<sup>4</sup>Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
<scripture passage="Matt 22:5" parsed="|Matt|22|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.5" />
<sup>5</sup>Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,

<sup>5</sup>Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
<scripture passage="Matt 22:6" parsed="|Matt|22|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.6" />
<sup>6</sup>na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.

<sup>6</sup>Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi.
<scripture passage="Matt 22:7" parsed="|Matt|22|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.7" />
<sup>7</sup>Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.

<sup>7</sup>Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: `Mwalimu.`
<scripture passage="Matt 22:8" parsed="|Matt|22|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.8" />
<sup>8</sup>Kisha akawaambia watumishi wake: `Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.

<sup>8</sup>Lakini ninyi msiitwe kamwe `Mwalimu,` maana mwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote ni ndugu.
<scripture passage="Matt 22:9" parsed="|Matt|22|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.9" />
<sup>9</sup>Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.`

<sup>9</sup>Wala msimwite mtu yeyote `Baba` hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni.
<scripture passage="Matt 22:10" parsed="|Matt|22|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.10" />
<sup>10</sup>Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.

<sup>10</sup>Wala msiitwe `Viongozi,` maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo.
<scripture passage="Matt 22:11" parsed="|Matt|22|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.11" />
<sup>11</sup>"Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.

<sup>11</sup>Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.
<scripture passage="Matt 22:12" parsed="|Matt|22|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.12" />
<sup>12</sup>Mfalme akamwuliza, `Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi?` Lakini yeye akakaa kimya.

<sup>12</sup>Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
<scripture passage="Matt 22:13" parsed="|Matt|22|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.13" />
<sup>13</sup>Hapo mfalme akawaambia watumishi, `Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno."`

<sup>13</sup>"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.<i>fj</i> wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
<scripture passage="Matt 22:14" parsed="|Matt|22|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.14" />
<sup>14</sup>Yesu akamaliza kwa kusema, "Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa."

<sup>14</sup>missing
<scripture passage="Matt 22:15" parsed="|Matt|22|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.15" />
<sup>15</sup>Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake.

<sup>15</sup>"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.
<scripture passage="Matt 22:16" parsed="|Matt|22|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.16" />
<sup>16</sup>Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.

<sup>16</sup>"Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika.
<scripture passage="Matt 22:17" parsed="|Matt|22|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.17" />
<sup>17</sup>Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?"

<sup>17</sup>Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?
<scripture passage="Matt 22:18" parsed="|Matt|22|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.18" />
<sup>18</sup>Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, "Enyi

<sup>18</sup>Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
<scripture passage="Matt 22:19" parsed="|Matt|22|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.19" />
<sup>19</sup>Nionyesheni fedha ya kulipia kodi." Nao wakamtolea sarafu ya fedha. sarafu ya fedha.

<sup>19</sup>Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu?
<scripture passage="Matt 22:20" parsed="|Matt|22|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.20" />
<sup>20</sup>Basi, Yesu akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?"

<sup>20</sup>Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake.
<scripture passage="Matt 22:21" parsed="|Matt|22|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.21" />
<sup>21</sup>Wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Hapo Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu."

<sup>21</sup>Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake.
<scripture passage="Matt 22:22" parsed="|Matt|22|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.22" />
<sup>22</sup>Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.

<sup>22</sup>Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake.
<scripture passage="Matt 22:23" parsed="|Matt|22|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.23" />
<sup>23</sup>Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemao kwamba wafu hawafufuki.

<sup>23</sup>Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
<scripture passage="Matt 22:24" parsed="|Matt|22|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.24" />
<sup>24</sup>Basi, wakamwambia, "Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.

<sup>24</sup>Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia! ic
<scripture passage="Matt 22:25" parsed="|Matt|22|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.25" />
<sup>25</sup>Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.

<sup>25</sup>"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang`anyi na uchoyo.
<scripture passage="Matt 22:26" parsed="|Matt|22|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.26" />
<sup>26</sup>Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.

<sup>26</sup>Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
<scripture passage="Matt 22:27" parsed="|Matt|22|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.27" />
<sup>27</sup>Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.

<sup>27</sup>"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
<scripture passage="Matt 22:28" parsed="|Matt|22|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.28" />
<sup>28</sup>Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa."

<sup>28</sup>Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
<scripture passage="Matt 22:29" parsed="|Matt|22|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.29" />
<sup>29</sup>Yesu akawajibu, "Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!

<sup>29</sup>"Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
<scripture passage="Matt 22:30" parsed="|Matt|22|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.30" />
<sup>30</sup>Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama malaika mbinguni.

<sup>30</sup>Mwasema: `Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!`
<scripture passage="Matt 22:31" parsed="|Matt|22|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.31" />
<sup>31</sup>Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu?

<sup>31</sup>Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua manabii.
<scripture passage="Matt 22:32" parsed="|Matt|22|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.32" />
<sup>32</sup>Aliwaambia, `Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo!` Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."

<sup>32</sup>Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!
<scripture passage="Matt 22:33" parsed="|Matt|22|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.33" />
<sup>33</sup>Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.

<sup>33</sup>Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?
<scripture passage="Matt 22:34" parsed="|Matt|22|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.34" />
<sup>34</sup>Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja.

<sup>34</sup>Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
<scripture passage="Matt 22:35" parsed="|Matt|22|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.35" />
<sup>35</sup>Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,

<sup>35</sup>Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
<scripture passage="Matt 22:36" parsed="|Matt|22|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.36" />
<sup>36</sup>"Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?"

<sup>36</sup>Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya.
<scripture passage="Matt 22:37" parsed="|Matt|22|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.37" />
<sup>37</sup>Yesu akamjibu, "`Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.`

<sup>37</sup>"Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
<scripture passage="Matt 22:38" parsed="|Matt|22|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.38" />
<sup>38</sup>Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.

<sup>38</sup>Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.
<scripture passage="Matt 22:39" parsed="|Matt|22|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.39" />
<sup>39</sup>Ya pili inafanana na hiyo: `Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.`

<sup>39</sup>Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: `Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."` ic
<scripture passage="Matt 22:40" parsed="|Matt|22|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.40" />
<sup>40</sup>Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili."
<scripture passage="Matt 22:41" parsed="|Matt|22|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.41" />
<sup>41</sup>Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,
<scripture passage="Matt 22:42" parsed="|Matt|22|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.42" />
<sup>42</sup>"Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?" Wakamjibu, "Wa Daudi."
<scripture passage="Matt 22:43" parsed="|Matt|22|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.43" />
<sup>43</sup>Yesu akawaambia, "Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:
<scripture passage="Matt 22:44" parsed="|Matt|22|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.44" />
<sup>44</sup>`Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.`
<scripture passage="Matt 22:45" parsed="|Matt|22|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.45" />
<sup>45</sup>Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo `Bwana,` anawezaje kuwa mwanawe?"
<scripture passage="Matt 22:46" parsed="|Matt|22|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.22.46" />
<sup>46</sup>Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 24" progress="9.63%" prev="Matt.22" next="Matt.25" id="Matt.24">
<h3 id="Matt.24-p0.1">Chapter 24</h3>
<p id="Matt.24-p1">
<scripture passage="Matt 24:1" parsed="|Matt|24|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.1" />
<sup>1</sup>Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu.
<scripture passage="Matt 24:2" parsed="|Matt|24|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.2" />
<sup>2</sup>Yesu akawaambia, "Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa."
<scripture passage="Matt 24:3" parsed="|Matt|24|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.3" />
<sup>3</sup>Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, "Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?"
<scripture passage="Matt 24:4" parsed="|Matt|24|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.4" />
<sup>4</sup>Yesu akawajibu, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
<scripture passage="Matt 24:5" parsed="|Matt|24|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.5" />
<sup>5</sup>Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: `Mimi ndiye Kristo,` nao watawapotosha watu wengi.
<scripture passage="Matt 24:6" parsed="|Matt|24|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.6" />
<sup>6</sup>Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
<scripture passage="Matt 24:7" parsed="|Matt|24|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.7" />
<sup>7</sup>Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
<scripture passage="Matt 24:8" parsed="|Matt|24|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.8" />
<sup>8</sup>Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.
<scripture passage="Matt 24:9" parsed="|Matt|24|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.9" />
<sup>9</sup>"Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.
<scripture passage="Matt 24:10" parsed="|Matt|24|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.10" />
<sup>10</sup>Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
<scripture passage="Matt 24:11" parsed="|Matt|24|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.11" />
<sup>11</sup>Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
<scripture passage="Matt 24:12" parsed="|Matt|24|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.12" />
<sup>12</sup>Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
<scripture passage="Matt 24:13" parsed="|Matt|24|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.13" />
<sup>13</sup>Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.
<scripture passage="Matt 24:14" parsed="|Matt|24|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.14" />
<sup>14</sup>Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
<scripture passage="Matt 24:15" parsed="|Matt|24|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.15" />
<sup>15</sup>"Basi, mtakapoona `Chukizo Haribifu` lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
<scripture passage="Matt 24:16" parsed="|Matt|24|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.16" />
<sup>16</sup>hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
<scripture passage="Matt 24:17" parsed="|Matt|24|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.17" />
<sup>17</sup>Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake.
<scripture passage="Matt 24:18" parsed="|Matt|24|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.18" />
<sup>18</sup>Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
<scripture passage="Matt 24:19" parsed="|Matt|24|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.19" />
<sup>19</sup>Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
<scripture passage="Matt 24:20" parsed="|Matt|24|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.20" />
<sup>20</sup>Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato!
<scripture passage="Matt 24:21" parsed="|Matt|24|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.21" />
<sup>21</sup>Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
<scripture passage="Matt 24:22" parsed="|Matt|24|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.22" />
<sup>22</sup>Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
<scripture passage="Matt 24:23" parsed="|Matt|24|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.23" />
<sup>23</sup>"Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: `Kristo yuko hapa` au `Yuko pale,` msimsadiki.
<scripture passage="Matt 24:24" parsed="|Matt|24|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.24" />
<sup>24</sup>Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu.
<scripture passage="Matt 24:25" parsed="|Matt|24|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.25" />
<sup>25</sup>Sikilizeni, nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati.
<scripture passage="Matt 24:26" parsed="|Matt|24|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.26" />
<sup>26</sup>Basi, wakiwaambieni, `Tazameni, yuko jangwani,` msiende huko; au, `Tazameni, amejificha ndani,` msisadiki;
<scripture passage="Matt 24:27" parsed="|Matt|24|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.27" />
<sup>27</sup>maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
<scripture passage="Matt 24:28" parsed="|Matt|24|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.28" />
<sup>28</sup>Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
<scripture passage="Matt 24:29" parsed="|Matt|24|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.29" />
<sup>29</sup>"Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
<scripture passage="Matt 24:30" parsed="|Matt|24|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.30" />
<sup>30</sup>Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi.
<scripture passage="Matt 24:31" parsed="|Matt|24|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.31" />
<sup>31</sup>Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu.
<scripture passage="Matt 24:32" parsed="|Matt|24|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.32" />
<sup>32</sup>"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
<scripture passage="Matt 24:33" parsed="|Matt|24|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.33" />
<sup>33</sup>Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.<i>fk</i>
<scripture passage="Matt 24:34" parsed="|Matt|24|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.34" />
<sup>34</sup>Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
<scripture passage="Matt 24:35" parsed="|Matt|24|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.35" />
<sup>35</sup>Naam, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
<scripture passage="Matt 24:36" parsed="|Matt|24|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.36" />
<sup>36</sup>"Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake ndiye ajuaye.
<scripture passage="Matt 24:37" parsed="|Matt|24|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.37" />
<sup>37</sup>Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
<scripture passage="Matt 24:38" parsed="|Matt|24|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.38" />
<sup>38</sup>Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina.
<scripture passage="Matt 24:39" parsed="|Matt|24|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.39" />
<sup>39</sup>Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja.
<scripture passage="Matt 24:40" parsed="|Matt|24|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.40" />
<sup>40</sup>Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
<scripture passage="Matt 24:41" parsed="|Matt|24|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.41" />
<sup>41</sup>Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
<scripture passage="Matt 24:42" parsed="|Matt|24|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.42" />
<sup>42</sup>Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.
<scripture passage="Matt 24:43" parsed="|Matt|24|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.43" />
<sup>43</sup>Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
<scripture passage="Matt 24:44" parsed="|Matt|24|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.44" />
<sup>44</sup>Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia."
<scripture passage="Matt 24:45" parsed="|Matt|24|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.45" />
<sup>45</sup>Yesu akaendelea kusema, "Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake?
<scripture passage="Matt 24:46" parsed="|Matt|24|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.46" />
<sup>46</sup>Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo.
<scripture passage="Matt 24:47" parsed="|Matt|24|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.47" />
<sup>47</sup>Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote.
<scripture passage="Matt 24:48" parsed="|Matt|24|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.48" />
<sup>48</sup>Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: `Bwana wangu anakawia kurudi,`
<scripture passage="Matt 24:49" parsed="|Matt|24|49|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.49" />
<sup>49</sup>kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi,
<scripture passage="Matt 24:50" parsed="|Matt|24|50|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.50" />
<sup>50</sup>bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua.
<scripture passage="Matt 24:51" parsed="|Matt|24|51|0|0" osisRef="Bible:Matt.24.51" />
<sup>51</sup>Atamkatilia mbali na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 25" progress="10.17%" prev="Matt.24" next="Matt.26" id="Matt.25">
<h3 id="Matt.25-p0.1">Chapter 25</h3>
<p id="Matt.25-p1">
<scripture passage="Matt 25:1" parsed="|Matt|25|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.1" />
<sup>1</sup>"Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.
<scripture passage="Matt 25:2" parsed="|Matt|25|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.2" />
<sup>2</sup>Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.
<scripture passage="Matt 25:3" parsed="|Matt|25|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.3" />
<sup>3</sup>Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.
<scripture passage="Matt 25:4" parsed="|Matt|25|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.4" />
<sup>4</sup>Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.
<scripture passage="Matt 25:5" parsed="|Matt|25|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.5" />
<sup>5</sup>Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote walisinzia, wakalala.
<scripture passage="Matt 25:6" parsed="|Matt|25|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.6" />
<sup>6</sup>Usiku wa manane kukawa na kelele: `Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.`
<scripture passage="Matt 25:7" parsed="|Matt|25|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.7" />
<sup>7</sup>Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
<scripture passage="Matt 25:8" parsed="|Matt|25|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.8" />
<sup>8</sup>Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: `Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.`
<scripture passage="Matt 25:9" parsed="|Matt|25|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.9" />
<sup>9</sup>Lakini wale wenye busara wakawaambia, `Hayatatutosha sisi na ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!`
<scripture passage="Matt 25:10" parsed="|Matt|25|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.10" />
<sup>10</sup>Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.
<scripture passage="Matt 25:11" parsed="|Matt|25|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.11" />
<sup>11</sup>Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: `Bwana, bwana, tufungulie!`
<scripture passage="Matt 25:12" parsed="|Matt|25|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.12" />
<sup>12</sup>Lakini yeye akawajibu, `Nawaambieni kweli, siwajui ninyi."`
<scripture passage="Matt 25:13" parsed="|Matt|25|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.13" />
<sup>13</sup>Kisha Yesu akasema, "Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.
<scripture passage="Matt 25:14" parsed="|Matt|25|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.14" />
<sup>14</sup>"Itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng`ambo: aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.
<scripture passage="Matt 25:15" parsed="|Matt|25|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.15" />
<sup>15</sup>Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja sarafu tano za fedha ziitwazo talanta, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri.
<scripture passage="Matt 25:16" parsed="|Matt|25|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.16" />
<sup>16</sup>Mara yule aliyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano.
<scripture passage="Matt 25:17" parsed="|Matt|25|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.17" />
<sup>17</sup>Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili.
<scripture passage="Matt 25:18" parsed="|Matt|25|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.18" />
<sup>18</sup>Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaenda akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake.
<scripture passage="Matt 25:19" parsed="|Matt|25|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.19" />
<sup>19</sup>"Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake.
<scripture passage="Matt 25:20" parsed="|Matt|25|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.20" />
<sup>20</sup>Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akaja amechukua zile talanta tano faida, akamwambia, `Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.`
<scripture passage="Matt 25:21" parsed="|Matt|25|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.21" />
<sup>21</sup>Bwana wake akamwambia, `Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.`
<scripture passage="Matt 25:22" parsed="|Matt|25|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.22" />
<sup>22</sup>"Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, `Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.`
<scripture passage="Matt 25:23" parsed="|Matt|25|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.23" />
<sup>23</sup>Bwana wake akamwambia, `Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.`
<scripture passage="Matt 25:24" parsed="|Matt|25|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.24" />
<sup>24</sup>"Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaja, akasema, `Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya.
<scripture passage="Matt 25:25" parsed="|Matt|25|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.25" />
<sup>25</sup>Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.`
<scripture passage="Matt 25:26" parsed="|Matt|25|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.26" />
<sup>26</sup>"Bwana wake akamwambia, `Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya.
<scripture passage="Matt 25:27" parsed="|Matt|25|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.27" />
<sup>27</sup>Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake!
<scripture passage="Matt 25:28" parsed="|Matt|25|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.28" />
<sup>28</sup>Basi, mnyang`anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi.
<scripture passage="Matt 25:29" parsed="|Matt|25|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.29" />
<sup>29</sup>Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
<scripture passage="Matt 25:30" parsed="|Matt|25|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.30" />
<sup>30</sup>Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.`
<scripture passage="Matt 25:31" parsed="|Matt|25|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.31" />
<sup>31</sup>"Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu,
<scripture passage="Matt 25:32" parsed="|Matt|25|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.32" />
<sup>32</sup>na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
<scripture passage="Matt 25:33" parsed="|Matt|25|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.33" />
<sup>33</sup>Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.
<scripture passage="Matt 25:34" parsed="|Matt|25|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.34" />
<sup>34</sup>"Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, `Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
<scripture passage="Matt 25:35" parsed="|Matt|25|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.35" />
<sup>35</sup>Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
<scripture passage="Matt 25:36" parsed="|Matt|25|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.36" />
<sup>36</sup>nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.`
<scripture passage="Matt 25:37" parsed="|Matt|25|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.37" />
<sup>37</sup>Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme `Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?
<scripture passage="Matt 25:38" parsed="|Matt|25|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.38" />
<sup>38</sup>Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika?
<scripture passage="Matt 25:39" parsed="|Matt|25|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.39" />
<sup>39</sup>Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?`
<scripture passage="Matt 25:40" parsed="|Matt|25|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.40" />
<sup>40</sup>Mfalme atawajibu, `Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.`
<scripture passage="Matt 25:41" parsed="|Matt|25|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.41" />
<sup>41</sup>"Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, `Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
<scripture passage="Matt 25:42" parsed="|Matt|25|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.42" />
<sup>42</sup>Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji.
<scripture passage="Matt 25:43" parsed="|Matt|25|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.43" />
<sup>43</sup>Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.`
<scripture passage="Matt 25:44" parsed="|Matt|25|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.44" />
<sup>44</sup>"Hapo nao watajibu, `Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukuja kukuhudumia?`
<scripture passage="Matt 25:45" parsed="|Matt|25|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.45" />
<sup>45</sup>Naye atawajibu, `Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.`
<scripture passage="Matt 25:46" parsed="|Matt|25|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.25.46" />
<sup>46</sup>Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uzima wa milele."
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 26" progress="10.70%" prev="Matt.25" next="Matt.27" id="Matt.26">
<h3 id="Matt.26-p0.1">Chapter 26</h3>
<p id="Matt.26-p1">
<scripture passage="Matt 26:1" parsed="|Matt|26|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,
<scripture passage="Matt 26:2" parsed="|Matt|26|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.2" />
<sup>2</sup>"Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe."
<scripture passage="Matt 26:3" parsed="|Matt|26|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.3" />
<sup>3</sup>Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, Kuhani Mkuu.
<scripture passage="Matt 26:4" parsed="|Matt|26|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.4" />
<sup>4</sup>Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
<scripture passage="Matt 26:5" parsed="|Matt|26|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.5" />
<sup>5</sup>Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
<scripture passage="Matt 26:6" parsed="|Matt|26|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.6" />
<sup>6</sup>Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,
<scripture passage="Matt 26:7" parsed="|Matt|26|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.7" />
<sup>7</sup>mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
<scripture passage="Matt 26:8" parsed="|Matt|26|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.8" />
<sup>8</sup>Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, "Ya nini hasara hii?
<scripture passage="Matt 26:9" parsed="|Matt|26|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.9" />
<sup>9</sup>Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha."
<scripture passage="Matt 26:10" parsed="|Matt|26|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.10" />
<sup>10</sup>Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, "Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.
<scripture passage="Matt 26:11" parsed="|Matt|26|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.11" />
<sup>11</sup>Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
<scripture passage="Matt 26:12" parsed="|Matt|26|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.12" />
<sup>12</sup>Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.
<scripture passage="Matt 26:13" parsed="|Matt|26|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.13" />
<sup>13</sup>Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye."
<scripture passage="Matt 26:14" parsed="|Matt|26|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.14" />
<sup>14</sup>Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu,
<scripture passage="Matt 26:15" parsed="|Matt|26|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.15" />
<sup>15</sup>akawaambia, "Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?" Wakamhesabia sarafu thelathini za fedha;
<scripture passage="Matt 26:16" parsed="|Matt|26|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.16" />
<sup>16</sup>na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.
<scripture passage="Matt 26:17" parsed="|Matt|26|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.17" />
<sup>17</sup>Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, "Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?"
<scripture passage="Matt 26:18" parsed="|Matt|26|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.18" />
<sup>18</sup>Yeye akawajibu, "Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie: `Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu."`
<scripture passage="Matt 26:19" parsed="|Matt|26|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.19" />
<sup>19</sup>Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka.
<scripture passage="Matt 26:20" parsed="|Matt|26|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.20" />
<sup>20</sup>Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
<scripture passage="Matt 26:21" parsed="|Matt|26|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.21" />
<sup>21</sup>Walipokuwa wakila, Yesu akasema, "Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti."
<scripture passage="Matt 26:22" parsed="|Matt|26|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.22" />
<sup>22</sup>Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja, "Bwana! Je, ni mimi?"
<scripture passage="Matt 26:23" parsed="|Matt|26|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.23" />
<sup>23</sup>Yesu akajibu, "Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti.<i>fm</i>
<scripture passage="Matt 26:24" parsed="|Matt|26|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.24" />
<sup>24</sup>Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa."
<scripture passage="Matt 26:25" parsed="|Matt|26|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.25" />
<sup>25</sup>Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, "Mwalimu! Je, ni mimi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema."
<scripture passage="Matt 26:26" parsed="|Matt|26|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.26" />
<sup>26</sup>Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, "Twaeni mle; huu ni mwili wangu."
<scripture passage="Matt 26:27" parsed="|Matt|26|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.27" />
<sup>27</sup>Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema, "Nyweni nyote;
<scripture passage="Matt 26:28" parsed="|Matt|26|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.28" />
<sup>28</sup>maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano,<i>fn</i> damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi.
<scripture passage="Matt 26:29" parsed="|Matt|26|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.29" />
<sup>29</sup>Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu."
<scripture passage="Matt 26:30" parsed="|Matt|26|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.30" />
<sup>30</sup>Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
<scripture passage="Matt 26:31" parsed="|Matt|26|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.31" />
<sup>31</sup>Kisha Yesu akawaambia, "Usiku huu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema: `Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.`
<scripture passage="Matt 26:32" parsed="|Matt|26|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.32" />
<sup>32</sup>Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya."
<scripture passage="Matt 26:33" parsed="|Matt|26|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.33" />
<sup>33</sup>Petro akamwambia Yesu "Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe."
<scripture passage="Matt 26:34" parsed="|Matt|26|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.34" />
<sup>34</sup>Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
<scripture passage="Matt 26:35" parsed="|Matt|26|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.35" />
<sup>35</sup>Petro akamwambia, "Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakukana kamwe." Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
<scripture passage="Matt 26:36" parsed="|Matt|26|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.36" />
<sup>36</sup>Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali."
<scripture passage="Matt 26:37" parsed="|Matt|26|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.37" />
<sup>37</sup>Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko.
<scripture passage="Matt 26:38" parsed="|Matt|26|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.38" />
<sup>38</sup>Hapo akawaambia, "Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami."
<scripture passage="Matt 26:39" parsed="|Matt|26|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.39" />
<sup>39</sup>Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: "Baba yangu, kama inawezekana, aacha kikombe<i>fo</i> hiki cha mateso kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe."
<scripture passage="Matt 26:40" parsed="|Matt|26|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.40" />
<sup>40</sup>Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, "Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
<scripture passage="Matt 26:41" parsed="|Matt|26|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.41" />
<sup>41</sup>Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu."
<scripture passage="Matt 26:42" parsed="|Matt|26|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.42" />
<sup>42</sup>Akaenda tena mara ya pili akasali: "Baba yangu, kama haiwezekani kikombe<i>fp</i> hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako yafanyike."
<scripture passage="Matt 26:43" parsed="|Matt|26|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.43" />
<sup>43</sup>Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
<scripture passage="Matt 26:44" parsed="|Matt|26|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.44" />
<sup>44</sup>Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno yaleyale.
<scripture passage="Matt 26:45" parsed="|Matt|26|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.45" />
<sup>45</sup>Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, "Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
<scripture passage="Matt 26:46" parsed="|Matt|26|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.46" />
<sup>46</sup>Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti."
<scripture passage="Matt 26:47" parsed="|Matt|26|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.47" />
<sup>47</sup>Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao, mara akaja Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili. Pamoja naye walikuja watu wengi wenye mapanga na marungu ambao walitumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
<scripture passage="Matt 26:48" parsed="|Matt|26|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.48" />
<sup>48</sup>Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: "Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni."
<scripture passage="Matt 26:49" parsed="|Matt|26|49|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.49" />
<sup>49</sup>Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, "Shikamoo, Mwalimu!" Kisha akambusu.
<scripture passage="Matt 26:50" parsed="|Matt|26|50|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.50" />
<sup>50</sup>Yesu akamwambia, "Rafiki, fanya ulichokuja kufanya." Hapo wale watu wakaja, wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
<scripture passage="Matt 26:51" parsed="|Matt|26|51|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.51" />
<sup>51</sup>Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono, akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
<scripture passage="Matt 26:52" parsed="|Matt|26|52|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.52" />
<sup>52</sup>Hapo Yesu akamwambia, "Rudisha upanga wako alani, maana yeyote anayeutumia upanga, atakufa kwa upanga.
<scripture passage="Matt 26:53" parsed="|Matt|26|53|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.53" />
<sup>53</sup>Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
<scripture passage="Matt 26:54" parsed="|Matt|26|54|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.54" />
<sup>54</sup>Lakini yatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayo kwamba ndivyo inavyopaswa kuwa?"
<scripture passage="Matt 26:55" parsed="|Matt|26|55|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.55" />
<sup>55</sup>Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, "Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba mimi ni mnyang`anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
<scripture passage="Matt 26:56" parsed="|Matt|26|56|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.56" />
<sup>56</sup>Lakini haya yote yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie." Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
<scripture passage="Matt 26:57" parsed="|Matt|26|57|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.57" />
<sup>57</sup>Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu wa Sheria na wazee.
<scripture passage="Matt 26:58" parsed="|Matt|26|58|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.58" />
<sup>58</sup>Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
<scripture passage="Matt 26:59" parsed="|Matt|26|59|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.59" />
<sup>59</sup>Basi, makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu wapate kumwua,
<scripture passage="Matt 26:60" parsed="|Matt|26|60|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.60" />
<sup>60</sup>lakini hawakupata ushahidi wowote, ingawa walikuja mashahidi wengi wa uongo. Mwishowe wakaja mashahidi wawili,
<scripture passage="Matt 26:61" parsed="|Matt|26|61|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.61" />
<sup>61</sup>wakasema, "Mtu huyu alisema: `Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu."`
<scripture passage="Matt 26:62" parsed="|Matt|26|62|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.62" />
<sup>62</sup>Kuhani Mkuu akasimama, akamwuliza Yesu, "Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?"
<scripture passage="Matt 26:63" parsed="|Matt|26|63|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.63" />
<sup>63</sup>Lakini Yesu akakaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, "Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!"
<scripture passage="Matt 26:64" parsed="|Matt|26|64|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.64" />
<sup>64</sup>Yesu akamwambia, "Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu sasa mtamwona Mwana wa Mtu ameketi upande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu ya mawingu ya mbinguni."
<scripture passage="Matt 26:65" parsed="|Matt|26|65|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.65" />
<sup>65</sup>Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, "Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
<scripture passage="Matt 26:66" parsed="|Matt|26|66|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.66" />
<sup>66</sup>Ninyi mwaonaje?" Wao wakamjibu, "Anastahili kufa!"
<scripture passage="Matt 26:67" parsed="|Matt|26|67|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.67" />
<sup>67</sup>Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi,
<scripture passage="Matt 26:68" parsed="|Matt|26|68|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.68" />
<sup>68</sup>wakasema, "Haya Kristo, tutabirie; ni nani amekupiga!"
<scripture passage="Matt 26:69" parsed="|Matt|26|69|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.69" />
<sup>69</sup>Petro alikuwa ameketi nje uani. Basi, mtumishi mmoja wa kike akamwendea, akasema, "Wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya."
<scripture passage="Matt 26:70" parsed="|Matt|26|70|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.70" />
<sup>70</sup>Petro akakana mbele ya wote akisema, "Sijui hata unasema nini."
<scripture passage="Matt 26:71" parsed="|Matt|26|71|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.71" />
<sup>71</sup>Alipokuwa akitoka mlangoni, mtumishi mwingine wa kike akamwona, akawaambia wale waliokuwa pale, "Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti."
<scripture passage="Matt 26:72" parsed="|Matt|26|72|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.72" />
<sup>72</sup>Petro akakana tena kwa kiapo: "Simjui mtu huyo."
<scripture passage="Matt 26:73" parsed="|Matt|26|73|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.73" />
<sup>73</sup>Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, "Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha."
<scripture passage="Matt 26:74" parsed="|Matt|26|74|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.74" />
<sup>74</sup>Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, "Simjui mtu huyo!" Mara jogoo akawika.
<scripture passage="Matt 26:75" parsed="|Matt|26|75|0|0" osisRef="Bible:Matt.26.75" />
<sup>75</sup>Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Basi, akatoka nje akalia sana.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 27" progress="11.54%" prev="Matt.26" next="Matt.28" id="Matt.27">
<h3 id="Matt.27-p0.1">Chapter 27</h3>
<p id="Matt.27-p1">
<scripture passage="Matt 27:1" parsed="|Matt|27|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.1" />
<sup>1</sup>Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
<scripture passage="Matt 27:2" parsed="|Matt|27|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.2" />
<sup>2</sup>Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.
<scripture passage="Matt 27:3" parsed="|Matt|27|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.3" />
<sup>3</sup>Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha.
<scripture passage="Matt 27:4" parsed="|Matt|27|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.4" />
<sup>4</sup>Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako."
<scripture passage="Matt 27:5" parsed="|Matt|27|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.5" />
<sup>5</sup>Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.
<scripture passage="Matt 27:6" parsed="|Matt|27|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.6" />
<sup>6</sup>Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, "Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu."
<scripture passage="Matt 27:7" parsed="|Matt|27|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.7" />
<sup>7</sup>Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
<scripture passage="Matt 27:8" parsed="|Matt|27|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.8" />
<sup>8</sup>Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
<scripture passage="Matt 27:9" parsed="|Matt|27|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.9" />
<sup>9</sup>Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: "Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,
<scripture passage="Matt 27:10" parsed="|Matt|27|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.10" />
<sup>10</sup>wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza."
<scripture passage="Matt 27:11" parsed="|Matt|27|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.11" />
<sup>11</sup>Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, "Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamwambia, "Wewe umesema."
<scripture passage="Matt 27:12" parsed="|Matt|27|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.12" />
<sup>12</sup>Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
<scripture passage="Matt 27:13" parsed="|Matt|27|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.13" />
<sup>13</sup>Hivyo Pilato akamwuliza, "Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?"
<scripture passage="Matt 27:14" parsed="|Matt|27|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.14" />
<sup>14</sup>Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.
<scripture passage="Matt 27:15" parsed="|Matt|27|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.15" />
<sup>15</sup>Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
<scripture passage="Matt 27:16" parsed="|Matt|27|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.16" />
<sup>16</sup>Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
<scripture passage="Matt 27:17" parsed="|Matt|27|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.17" />
<sup>17</sup>Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, "Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba<i>fq</i> ama Yesu aitwae Kristo?"
<scripture passage="Matt 27:18" parsed="|Matt|27|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.18" />
<sup>18</sup>Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.
<scripture passage="Matt 27:19" parsed="|Matt|27|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.19" />
<sup>19</sup>Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: "Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."
<scripture passage="Matt 27:20" parsed="|Matt|27|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.20" />
<sup>20</sup>Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.
<scripture passage="Matt 27:21" parsed="|Matt|27|21|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.21" />
<sup>21</sup>Mkuu wa mkoa akawauliza, "Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?" Wakamjibu, "Baraba!"
<scripture passage="Matt 27:22" parsed="|Matt|27|22|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.22" />
<sup>22</sup>Pilato akawauliza, "Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?" Wote wakasema, "Asulubiwe!"
<scripture passage="Matt 27:23" parsed="|Matt|27|23|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.23" />
<sup>23</sup>Pilato akauliza, "Kwa nini? Amefanya kosa gani?" Wao wakazidi kupaaza sauti: "Asulubiwe!"
<scripture passage="Matt 27:24" parsed="|Matt|27|24|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.24" />
<sup>24</sup>Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, "Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe."
<scripture passage="Matt 27:25" parsed="|Matt|27|25|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.25" />
<sup>25</sup>Watu wote wakasema, "Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!"
<scripture passage="Matt 27:26" parsed="|Matt|27|26|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.26" />
<sup>26</sup>Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.
<scripture passage="Matt 27:27" parsed="|Matt|27|27|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.27" />
<sup>27</sup>Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.
<scripture passage="Matt 27:28" parsed="|Matt|27|28|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.28" />
<sup>28</sup>Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
<scripture passage="Matt 27:29" parsed="|Matt|27|29|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.29" />
<sup>29</sup>Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!"
<scripture passage="Matt 27:30" parsed="|Matt|27|30|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.30" />
<sup>30</sup>Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
<scripture passage="Matt 27:31" parsed="|Matt|27|31|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.31" />
<sup>31</sup>Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
<scripture passage="Matt 27:32" parsed="|Matt|27|32|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.32" />
<sup>32</sup>Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
<scripture passage="Matt 27:33" parsed="|Matt|27|33|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.33" />
<sup>33</sup>Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la kichwa,"
<scripture passage="Matt 27:34" parsed="|Matt|27|34|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.34" />
<sup>34</sup>wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
<scripture passage="Matt 27:35" parsed="|Matt|27|35|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.35" />
<sup>35</sup>Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
<scripture passage="Matt 27:36" parsed="|Matt|27|36|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.36" />
<sup>36</sup>Wakaketi, wakawa wanamchunga.
<scripture passage="Matt 27:37" parsed="|Matt|27|37|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.37" />
<sup>37</sup>Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."
<scripture passage="Matt 27:38" parsed="|Matt|27|38|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.38" />
<sup>38</sup>Wanyang`anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
<scripture passage="Matt 27:39" parsed="|Matt|27|39|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.39" />
<sup>39</sup>Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,
<scripture passage="Matt 27:40" parsed="|Matt|27|40|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.40" />
<sup>40</sup>"Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!"
<scripture passage="Matt 27:41" parsed="|Matt|27|41|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.41" />
<sup>41</sup>Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,
<scripture passage="Matt 27:42" parsed="|Matt|27|42|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.42" />
<sup>42</sup>"Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
<scripture passage="Matt 27:43" parsed="|Matt|27|43|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.43" />
<sup>43</sup>Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka."
<scripture passage="Matt 27:44" parsed="|Matt|27|44|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.44" />
<sup>44</sup>Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
<scripture passage="Matt 27:45" parsed="|Matt|27|45|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.45" />
<sup>45</sup>Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
<scripture passage="Matt 27:46" parsed="|Matt|27|46|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.46" />
<sup>46</sup>Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
<scripture passage="Matt 27:47" parsed="|Matt|27|47|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.47" />
<sup>47</sup>Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, "Anamwita Eliya."
<scripture passage="Matt 27:48" parsed="|Matt|27|48|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.48" />
<sup>48</sup>Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
<scripture passage="Matt 27:49" parsed="|Matt|27|49|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.49" />
<sup>49</sup>Wengine wakasema, "Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa."
<scripture passage="Matt 27:50" parsed="|Matt|27|50|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.50" />
<sup>50</sup>Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.
<scripture passage="Matt 27:51" parsed="|Matt|27|51|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.51" />
<sup>51</sup>Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
<scripture passage="Matt 27:52" parsed="|Matt|27|52|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.52" />
<sup>52</sup>makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;
<scripture passage="Matt 27:53" parsed="|Matt|27|53|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.53" />
<sup>53</sup>nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.
<scripture passage="Matt 27:54" parsed="|Matt|27|54|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.54" />
<sup>54</sup>Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, "Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu."
<scripture passage="Matt 27:55" parsed="|Matt|27|55|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.55" />
<sup>55</sup>Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
<scripture passage="Matt 27:56" parsed="|Matt|27|56|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.56" />
<sup>56</sup>Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
<scripture passage="Matt 27:57" parsed="|Matt|27|57|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.57" />
<sup>57</sup>Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
<scripture passage="Matt 27:58" parsed="|Matt|27|58|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.58" />
<sup>58</sup>Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.
<scripture passage="Matt 27:59" parsed="|Matt|27|59|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.59" />
<sup>59</sup>Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
<scripture passage="Matt 27:60" parsed="|Matt|27|60|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.60" />
<sup>60</sup>akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
<scripture passage="Matt 27:61" parsed="|Matt|27|61|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.61" />
<sup>61</sup>Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.
<scripture passage="Matt 27:62" parsed="|Matt|27|62|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.62" />
<sup>62</sup>Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
<scripture passage="Matt 27:63" parsed="|Matt|27|63|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.63" />
<sup>63</sup>Wakasema, "Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, `Baada ya siku tatu nitafufuka.`
<scripture passage="Matt 27:64" parsed="|Matt|27|64|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.64" />
<sup>64</sup>Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali."
<scripture passage="Matt 27:65" parsed="|Matt|27|65|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.65" />
<sup>65</sup>Pilato akawaambia, "Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo."
<scripture passage="Matt 27:66" parsed="|Matt|27|66|0|0" osisRef="Bible:Matt.27.66" />
<sup>66</sup>Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.
</p>
</div3>

<div3 title="Matthew 28" progress="12.24%" prev="Matt.27" next="Mark" id="Matt.28">
<h3 id="Matt.28-p0.1">Chapter 28</h3>
<p id="Matt.28-p1">
<scripture passage="Matt 28:1" parsed="|Matt|28|1|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.1" />
<sup>1</sup>Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
<scripture passage="Matt 28:2" parsed="|Matt|28|2|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.2" />
<sup>2</sup>Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
<scripture passage="Matt 28:3" parsed="|Matt|28|3|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.3" />
<sup>3</sup>Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
<scripture passage="Matt 28:4" parsed="|Matt|28|4|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.4" />
<sup>4</sup>Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa.
<scripture passage="Matt 28:5" parsed="|Matt|28|5|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.5" />
<sup>5</sup>Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, "Ninyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
<scripture passage="Matt 28:6" parsed="|Matt|28|6|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.6" />
<sup>6</sup>Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
<scripture passage="Matt 28:7" parsed="|Matt|28|7|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.7" />
<sup>7</sup>Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni."
<scripture passage="Matt 28:8" parsed="|Matt|28|8|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.8" />
<sup>8</sup>Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
<scripture passage="Matt 28:9" parsed="|Matt|28|9|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.9" />
<sup>9</sup>Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: "Salamu." Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
<scripture passage="Matt 28:10" parsed="|Matt|28|10|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.10" />
<sup>10</sup>Kisha Yesu akawaambia, "Msiogope! Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, na huko wataniona."
<scripture passage="Matt 28:11" parsed="|Matt|28|11|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.11" />
<sup>11</sup>Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
<scripture passage="Matt 28:12" parsed="|Matt|28|12|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.12" />
<sup>12</sup>Basi, wakakutana pamoja na wazee, na baada ya kushauriana, wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha
<scripture passage="Matt 28:13" parsed="|Matt|28|13|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.13" />
<sup>13</sup>wakisema, "Ninyi mtasema hivi: `Wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba sisi tukiwa tumelala.`
<scripture passage="Matt 28:14" parsed="|Matt|28|14|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.14" />
<sup>14</sup>Na kama mkuu wa mkoa akijua jambo hili, sisi tutasema naye na kuhakikisha kuwa ninyi hamtapata matatizo."
<scripture passage="Matt 28:15" parsed="|Matt|28|15|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.15" />
<sup>15</sup>Wale walinzi wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Habari hiyo imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.
<scripture passage="Matt 28:16" parsed="|Matt|28|16|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.16" />
<sup>16</sup>Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.
<scripture passage="Matt 28:17" parsed="|Matt|28|17|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.17" />
<sup>17</sup>Walipomwona, wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka.
<scripture passage="Matt 28:18" parsed="|Matt|28|18|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.18" />
<sup>18</sup>Yesu akaja karibu, akawaambia, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
<scripture passage="Matt 28:19" parsed="|Matt|28|19|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.19" />
<sup>19</sup>Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Matt 28:20" parsed="|Matt|28|20|0|0" osisRef="Bible:Matt.28.20" />
<sup>20</sup>Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati."
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Mark" progress="12.47%" prev="Matt.28" next="Mark.1" id="Mark">
<h2 id="Mark-p0.1">Mark</h2>

<div3 title="Mark 1" progress="12.47%" prev="Mark" next="Mark.2" id="Mark.1">
<h3 id="Mark.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Mark.1-p1">
<scripture passage="Mark 1:1" parsed="|Mark|1|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.1" />
<sup>1</sup>Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.<i>fa</i>
<scripture passage="Mark 1:2" parsed="|Mark|1|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.2" />
<sup>2</sup>Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.
<scripture passage="Mark 1:3" parsed="|Mark|1|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.3" />
<sup>3</sup>Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake."`
<scripture passage="Mark 1:4" parsed="|Mark|1|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.4" />
<sup>4</sup>Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
<scripture passage="Mark 1:5" parsed="|Mark|1|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.5" />
<sup>5</sup>Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
<scripture passage="Mark 1:6" parsed="|Mark|1|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.6" />
<sup>6</sup>Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
<scripture passage="Mark 1:7" parsed="|Mark|1|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.7" />
<sup>7</sup>Naye alihubiri akisema, "Baada yangu anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake.
<scripture passage="Mark 1:8" parsed="|Mark|1|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.8" />
<sup>8</sup>Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu."
<scripture passage="Mark 1:9" parsed="|Mark|1|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.9" />
<sup>9</sup>Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa na Yohane katika mto Yordani.
<scripture passage="Mark 1:10" parsed="|Mark|1|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.10" />
<sup>10</sup>Mara tu alipotoka majini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishuka juu yake kama njiwa.
<scripture passage="Mark 1:11" parsed="|Mark|1|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.11" />
<sup>11</sup>Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."
<scripture passage="Mark 1:12" parsed="|Mark|1|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.12" />
<sup>12</sup>Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani,
<scripture passage="Mark 1:13" parsed="|Mark|1|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.13" />
<sup>13</sup>akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamtumikia.
<scripture passage="Mark 1:14" parsed="|Mark|1|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.14" />
<sup>14</sup>Yohane alipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu, akisema,
<scripture passage="Mark 1:15" parsed="|Mark|1|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.15" />
<sup>15</sup>"Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!"
<scripture passage="Mark 1:16" parsed="|Mark|1|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.16" />
<sup>16</sup>Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
<scripture passage="Mark 1:17" parsed="|Mark|1|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.17" />
<sup>17</sup>Yesu akawaambia, "Nifuateni nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."
<scripture passage="Mark 1:18" parsed="|Mark|1|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.18" />
<sup>18</sup>Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
<scripture passage="Mark 1:19" parsed="|Mark|1|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.19" />
<sup>19</sup>Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao pia walikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.
<scripture passage="Mark 1:20" parsed="|Mark|1|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.20" />
<sup>20</sup>Yesu akawaita mara, nao wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi, wakamfuata.
<scripture passage="Mark 1:21" parsed="|Mark|1|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.21" />
<sup>21</sup>Wakafika mjini Kafarnaumu, na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katika Sunagogi, akaanza kufundisha.
<scripture passage="Mark 1:22" parsed="|Mark|1|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.22" />
<sup>22</sup>Watu wote waliomsikia walishangazwa na mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kama walimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenye mamlaka.
<scripture passage="Mark 1:23" parsed="|Mark|1|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.23" />
<sup>23</sup>Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu,
<scripture passage="Mark 1:24" parsed="|Mark|1|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.24" />
<sup>24</sup>akapaaza sauti, "Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!"
<scripture passage="Mark 1:25" parsed="|Mark|1|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.25" />
<sup>25</sup>Yesu akamkemea, "Nyamaza! Mtoke mtu huyu."
<scripture passage="Mark 1:26" parsed="|Mark|1|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.26" />
<sup>26</sup>Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.
<scripture passage="Mark 1:27" parsed="|Mark|1|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.27" />
<sup>27</sup>Watu wote wakashangaa, wakaulizana, "Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!"
<scripture passage="Mark 1:28" parsed="|Mark|1|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.28" />
<sup>28</sup>Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahali katika wilaya ya Galilaya.
<scripture passage="Mark 1:29" parsed="|Mark|1|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.29" />
<sup>29</sup>Wakatoka katika sunagogi, wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao.
<scripture passage="Mark 1:30" parsed="|Mark|1|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.30" />
<sup>30</sup>Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
<scripture passage="Mark 1:31" parsed="|Mark|1|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.31" />
<sup>31</sup>Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono, akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
<scripture passage="Mark 1:32" parsed="|Mark|1|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.32" />
<sup>32</sup>Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwa wote na watu waliopagawa na pepo.
<scripture passage="Mark 1:33" parsed="|Mark|1|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.33" />
<sup>33</sup>Watu wote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango.
<scripture passage="Mark 1:34" parsed="|Mark|1|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.34" />
<sup>34</sup>Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
<scripture passage="Mark 1:35" parsed="|Mark|1|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.35" />
<sup>35</sup>Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali.
<scripture passage="Mark 1:36" parsed="|Mark|1|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.36" />
<sup>36</sup>Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta.
<scripture passage="Mark 1:37" parsed="|Mark|1|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.37" />
<sup>37</sup>Walipomwona wakamwambia, "Kila mtu anakutafuta."
<scripture passage="Mark 1:38" parsed="|Mark|1|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.38" />
<sup>38</sup>Yesu akawaambia, "Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo."
<scripture passage="Mark 1:39" parsed="|Mark|1|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.39" />
<sup>39</sup>Basi, akaenda kila mahali Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.
<scripture passage="Mark 1:40" parsed="|Mark|1|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.40" />
<sup>40</sup>Mtu mmoja mwenye ukoma alimwendea Yesu, akapiga magoti, akamwomba, "Ukitaka, waweza kunitakasa!"
<scripture passage="Mark 1:41" parsed="|Mark|1|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.41" />
<sup>41</sup>Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, "Nataka, takasika!"
<scripture passage="Mark 1:42" parsed="|Mark|1|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.42" />
<sup>42</sup>Mara ukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika.
<scripture passage="Mark 1:43" parsed="|Mark|1|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.43" />
<sup>43</sup>Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi na kumwonya vikali,
<scripture passage="Mark 1:44" parsed="|Mark|1|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.44" />
<sup>44</sup>"Usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani; kisha utoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona."
<scripture passage="Mark 1:45" parsed="|Mark|1|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.1.45" />
<sup>45</sup>Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 2" progress="12.95%" prev="Mark.1" next="Mark.3" id="Mark.2">
<h3 id="Mark.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Mark.2-p1">
<scripture passage="Mark 2:1" parsed="|Mark|2|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.1" />
<sup>1</sup>Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani.
<scripture passage="Mark 2:2" parsed="|Mark|2|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.2" />
<sup>2</sup>Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,
<scripture passage="Mark 2:3" parsed="|Mark|2|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.3" />
<sup>3</sup>wakati mtu mmoja aliyepooza alipoletwa kwake akiwa amechukuliwa na watu wanne.
<scripture passage="Mark 2:4" parsed="|Mark|2|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.4" />
<sup>4</sup>Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya dari iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
<scripture passage="Mark 2:5" parsed="|Mark|2|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.5" />
<sup>5</sup>Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Mwanangu, umesamehewa dhambi zako."
<scripture passage="Mark 2:6" parsed="|Mark|2|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.6" />
<sup>6</sup>Baadhi ya walimu wa Sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao,
<scripture passage="Mark 2:7" parsed="|Mark|2|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.7" />
<sup>7</sup>"Anathubutuje kusema hivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake."
<scripture passage="Mark 2:8" parsed="|Mark|2|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.8" />
<sup>8</sup>Yesu alitambua mara mawazo yao, akawaambia, "Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu?
<scripture passage="Mark 2:9" parsed="|Mark|2|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.9" />
<sup>9</sup>Ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, `Umesamehewa dhambi zako`, au kumwambia, `Inuka! Chukua mkeka wako utembee?`
<scripture passage="Mark 2:10" parsed="|Mark|2|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.10" />
<sup>10</sup>Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani." Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza,
<scripture passage="Mark 2:11" parsed="|Mark|2|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.11" />
<sup>11</sup>"Nakwambia simama, chukua mkeka wako uende nyumbani!"
<scripture passage="Mark 2:12" parsed="|Mark|2|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.12" />
<sup>12</sup>Mara, watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka, akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wote wakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, "Hatujapata kamwe kuona jambo kama hili."
<scripture passage="Mark 2:13" parsed="|Mark|2|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.13" />
<sup>13</sup>Yesu alikwenda tena kando ya ziwa. Umati wa watu ukamwendea, naye akaanza kuwafundisha.
<scripture passage="Mark 2:14" parsed="|Mark|2|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.14" />
<sup>14</sup>Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, "Nifuate!" Lawi akasimama, akamfuata.
<scripture passage="Mark 2:15" parsed="|Mark|2|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.15" />
<sup>15</sup>Baadaye, Yesu alikuwa amekaa mezani, nyumbani kwa Lawi, kula chakula. Watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuwa wamemfuata Yesu na wengi wao wakawa wamekaa mezani pamoja naye na wanafunzi wake.
<scripture passage="Mark 2:16" parsed="|Mark|2|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.16" />
<sup>16</sup>Basi, baadhi ya walimu wa Sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watoza ushuru, wakawauliza wanafunzi wake, "Kwa nini anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?"
<scripture passage="Mark 2:17" parsed="|Mark|2|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.17" />
<sup>17</sup>Yesu alipowasikia, akawaambia, "Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi."
<scripture passage="Mark 2:18" parsed="|Mark|2|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.18" />
<sup>18</sup>Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, "Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?"
<scripture passage="Mark 2:19" parsed="|Mark|2|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.19" />
<sup>19</sup>Yesu akajibu, "Walioalikwa harusini wanawezaje kufunga kama bwana harusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana harusi hawawezi kufunga.
<scripture passage="Mark 2:20" parsed="|Mark|2|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.20" />
<sup>20</sup>Lakini wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
<scripture passage="Mark 2:21" parsed="|Mark|2|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.21" />
<sup>21</sup>"Hakuna mtu anayekata kiraka kutoka katika nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama akifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
<scripture passage="Mark 2:22" parsed="|Mark|2|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.22" />
<sup>22</sup>Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai itavipasua hivyo viriba, nayo divai pamoja na hivyo viriba vitaharibika. Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!"
<scripture passage="Mark 2:23" parsed="|Mark|2|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.23" />
<sup>23</sup>Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano.
<scripture passage="Mark 2:24" parsed="|Mark|2|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.24" />
<sup>24</sup>Mafarisayo wakawaambia, "Tazama! Kwa nini wanafanya jambo ambalo si halali kufanya wakati wa Sabato?"
<scripture passage="Mark 2:25" parsed="|Mark|2|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.25" />
<sup>25</sup>Yesu akawajibu, "Je, hamjapata kusoma juu ya kile alichofanya Daudi wakati alipohitaji chakula? Yeye pamoja na wenzake waliona njaa,
<scripture passage="Mark 2:26" parsed="|Mark|2|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.26" />
<sup>26</sup>naye akaingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa Kuhani Mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake."
<scripture passage="Mark 2:27" parsed="|Mark|2|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.27" />
<sup>27</sup>Basi, Yesu akawaambia, "Sabato iliwekwa kwa ajili ya binadamu na si binadamu kwa ajili ya Sabato!
<scripture passage="Mark 2:28" parsed="|Mark|2|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.2.28" />
<sup>28</sup>Kwa hiyo, Mwana wa Mtu ni Bwana hata wa Sabato."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 3" progress="13.35%" prev="Mark.2" next="Mark.4" id="Mark.3">
<h3 id="Mark.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Mark.3-p1">
<scripture passage="Mark 3:1" parsed="|Mark|3|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza.
<scripture passage="Mark 3:2" parsed="|Mark|3|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.2" />
<sup>2</sup>Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki.
<scripture passage="Mark 3:3" parsed="|Mark|3|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.3" />
<sup>3</sup>Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, "Njoo hapa katikati."
<scripture passage="Mark 3:4" parsed="|Mark|3|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.4" />
<sup>4</sup>Kisha, akawauliza, "Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao hawakusema neno.
<scripture passage="Mark 3:5" parsed="|Mark|3|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.5" />
<sup>5</sup>Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, "Nyosha mkono wako!" Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
<scripture passage="Mark 3:6" parsed="|Mark|3|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.6" />
<sup>6</sup>Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.
<scripture passage="Mark 3:7" parsed="|Mark|3|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.7" />
<sup>7</sup>Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea,
<scripture passage="Mark 3:8" parsed="|Mark|3|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.8" />
<sup>8</sup>Idumea, ng`ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
<scripture passage="Mark 3:9" parsed="|Mark|3|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.9" />
<sup>9</sup>Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
<scripture passage="Mark 3:10" parsed="|Mark|3|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.10" />
<sup>10</sup>Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa.
<scripture passage="Mark 3:11" parsed="|Mark|3|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.11" />
<sup>11</sup>Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, "Wewe ni Mwana wa Mungu!"
<scripture passage="Mark 3:12" parsed="|Mark|3|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.12" />
<sup>12</sup>Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.
<scripture passage="Mark 3:13" parsed="|Mark|3|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.13" />
<sup>13</sup>Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea,
<scripture passage="Mark 3:14" parsed="|Mark|3|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.14" />
<sup>14</sup>naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume,<i>fb</i> wakae naye, awatume kuhubiri
<scripture passage="Mark 3:15" parsed="|Mark|3|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.15" />
<sup>15</sup>na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo.
<scripture passage="Mark 3:16" parsed="|Mark|3|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.16" />
<sup>16</sup>Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro),
<scripture passage="Mark 3:17" parsed="|Mark|3|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.17" />
<sup>17</sup>Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake "wanangurumo"),
<scripture passage="Mark 3:18" parsed="|Mark|3|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.18" />
<sup>18</sup>Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na
<scripture passage="Mark 3:19" parsed="|Mark|3|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.19" />
<sup>19</sup>Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
<scripture passage="Mark 3:20" parsed="|Mark|3|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.20" />
<sup>20</sup>Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.
<scripture passage="Mark 3:21" parsed="|Mark|3|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.21" />
<sup>21</sup>Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu.
<scripture passage="Mark 3:22" parsed="|Mark|3|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.22" />
<sup>22</sup>Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, "Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo."
<scripture passage="Mark 3:23" parsed="|Mark|3|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.23" />
<sup>23</sup>Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano,"Shetani anawezaje kumfukuza Shetani?
<scripture passage="Mark 3:24" parsed="|Mark|3|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.24" />
<sup>24</sup>Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.
<scripture passage="Mark 3:25" parsed="|Mark|3|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.25" />
<sup>25</sup>Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.
<scripture passage="Mark 3:26" parsed="|Mark|3|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.26" />
<sup>26</sup>Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.
<scripture passage="Mark 3:27" parsed="|Mark|3|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.27" />
<sup>27</sup>"Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang`anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang`anya mali yake.
<scripture passage="Mark 3:28" parsed="|Mark|3|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.28" />
<sup>28</sup>"Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;
<scripture passage="Mark 3:29" parsed="|Mark|3|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.29" />
<sup>29</sup>lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele."
<scripture passage="Mark 3:30" parsed="|Mark|3|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.30" />
<sup>30</sup>Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu.")
<scripture passage="Mark 3:31" parsed="|Mark|3|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.31" />
<sup>31</sup>Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona.
<scripture passage="Mark 3:32" parsed="|Mark|3|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.32" />
<sup>32</sup>Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona."
<scripture passage="Mark 3:33" parsed="|Mark|3|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.33" />
<sup>33</sup>Yesu akawaambia, "Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?"
<scripture passage="Mark 3:34" parsed="|Mark|3|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.34" />
<sup>34</sup>Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, "Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.
<scripture passage="Mark 3:35" parsed="|Mark|3|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.3.35" />
<sup>35</sup>Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 4" progress="13.72%" prev="Mark.3" next="Mark.5" id="Mark.4">
<h3 id="Mark.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Mark.4-p1">
<scripture passage="Mark 4:1" parsed="|Mark|4|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.1" />
<sup>1</sup>Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
<scripture passage="Mark 4:2" parsed="|Mark|4|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.2" />
<sup>2</sup>Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia,
<scripture passage="Mark 4:3" parsed="|Mark|4|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.3" />
<sup>3</sup>"Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
<scripture passage="Mark 4:4" parsed="|Mark|4|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.4" />
<sup>4</sup>Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
<scripture passage="Mark 4:5" parsed="|Mark|4|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.5" />
<sup>5</sup>Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
<scripture passage="Mark 4:6" parsed="|Mark|4|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.6" />
<sup>6</sup>Jua lilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
<scripture passage="Mark 4:7" parsed="|Mark|4|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.7" />
<sup>7</sup>Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
<scripture passage="Mark 4:8" parsed="|Mark|4|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.8" />
<sup>8</sup>Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia."
<scripture passage="Mark 4:9" parsed="|Mark|4|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.9" />
<sup>9</sup>Kisha akawaambia, "Mwenye masikio na asikie!"
<scripture passage="Mark 4:10" parsed="|Mark|4|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.10" />
<sup>10</sup>Yesu alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliomsikia walimwendea pamoja na wale kumi na wawili, wakamwuliza juu ya hiyo mifano.
<scripture passage="Mark 4:11" parsed="|Mark|4|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.11" />
<sup>11</sup>Naye akawaambia, "Ninyi mmejaliwa kujua siri ya Utawala wa Mungu, lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwa mifano,
<scripture passage="Mark 4:12" parsed="|Mark|4|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.12" />
<sup>12</sup>ili, `Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe."`
<scripture passage="Mark 4:13" parsed="|Mark|4|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.13" />
<sup>13</sup>Basi, Yesu akawauliza, "Je, ninyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote?
<scripture passage="Mark 4:14" parsed="|Mark|4|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.14" />
<sup>14</sup>Mpanzi hupanda neno la Mungu.
<scripture passage="Mark 4:15" parsed="|Mark|4|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.15" />
<sup>15</sup>Watu wengine ni kama wale walio njiani ambapo mbegu zilianguka. Hawa hulisikia hilo neno lakini mara Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
<scripture passage="Mark 4:16" parsed="|Mark|4|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.16" />
<sup>16</sup>Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu wanapolisikia hilo neno hulipokea kwa furaha.
<scripture passage="Mark 4:17" parsed="|Mark|4|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.17" />
<sup>17</sup>Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno mara wanakata tamaa.
<scripture passage="Mark 4:18" parsed="|Mark|4|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.18" />
<sup>18</sup>Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaolisikia hilo neno,
<scripture passage="Mark 4:19" parsed="|Mark|4|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.19" />
<sup>19</sup>lakini wasiwasi wa ulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namna huwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda.
<scripture passage="Mark 4:20" parsed="|Mark|4|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.20" />
<sup>20</sup>Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea, wakazaa matunda: wengine thelathini, wengine sitini na wengine mia moja."
<scripture passage="Mark 4:21" parsed="|Mark|4|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.21" />
<sup>21</sup>Yesu akaendelea kuwaambia, "Je, watu huwasha taa wakaileta ndani na kuifunika kwa pishi au kuiweka mvunguni? La! Huiweka juu ya kinara.
<scripture passage="Mark 4:22" parsed="|Mark|4|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.22" />
<sup>22</sup>Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
<scripture passage="Mark 4:23" parsed="|Mark|4|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.23" />
<sup>23</sup>Mwenye masikio na asikie!"
<scripture passage="Mark 4:24" parsed="|Mark|4|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.24" />
<sup>24</sup>Akawaambia pia, "Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
<scripture passage="Mark 4:25" parsed="|Mark|4|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.25" />
<sup>25</sup>Aliye na kitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa."
<scripture passage="Mark 4:26" parsed="|Mark|4|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.26" />
<sup>26</sup>Yesu akaendelea kusema, "Ufalme wa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegu shambani.
<scripture passage="Mark 4:27" parsed="|Mark|4|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.27" />
<sup>27</sup>Usiku hulala, mchana yu macho na wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika.
<scripture passage="Mark 4:28" parsed="|Mark|4|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.28" />
<sup>28</sup>Udongo wenyewe huiwezesha mimea kukua na kuzaa matunda: kwanza huchipua jani changa, kisha suke, na mwishowe nafaka ndani ya suke.
<scripture passage="Mark 4:29" parsed="|Mark|4|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.29" />
<sup>29</sup>Nafaka inapoiva, huyo mtu huanza kutumia mundu wake, maana wakati wa mavuno umefika."
<scripture passage="Mark 4:30" parsed="|Mark|4|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.30" />
<sup>30</sup>Tena, Yesu akasema, "Tuufananishe Utawala wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani?
<scripture passage="Mark 4:31" parsed="|Mark|4|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.31" />
<sup>31</sup>Ni kama mbegu ya haradali ambayo ni ndogo kuliko mbegu zote.
<scripture passage="Mark 4:32" parsed="|Mark|4|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.32" />
<sup>32</sup>Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake."
<scripture passage="Mark 4:33" parsed="|Mark|4|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.33" />
<sup>33</sup>Yesu aliwahubiria ujumbe wake kwa mifano mingine mingi ya namna hiyo; aliongea nao kadiri walivyoweza kusikia.
<scripture passage="Mark 4:34" parsed="|Mark|4|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.34" />
<sup>34</sup>Hakuongea nao chochote bila kutumia mifano; lakini alipokuwa pamoja na wanafunzi wake peke yao alikuwa akiwafafanulia kila kitu.
<scripture passage="Mark 4:35" parsed="|Mark|4|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.35" />
<sup>35</sup>Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Tuvuke ziwa, twende ng`ambo."
<scripture passage="Mark 4:36" parsed="|Mark|4|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.36" />
<sup>36</sup>Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Palikuwapo pia mashua nyingine hapo.
<scripture passage="Mark 4:37" parsed="|Mark|4|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.37" />
<sup>37</sup>Basi, dhoruba kali ikaanza kuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikaanza kujaa maji.
<scripture passage="Mark 4:38" parsed="|Mark|4|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.38" />
<sup>38</sup>Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, "Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?"
<scripture passage="Mark 4:39" parsed="|Mark|4|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.39" />
<sup>39</sup>Basi, akaamka, akaukemea ule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa, "Kimya! Tulia!" Hapo upepo ukakoma, kukawa shwari kabisa.
<scripture passage="Mark 4:40" parsed="|Mark|4|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.40" />
<sup>40</sup>Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?"
<scripture passage="Mark 4:41" parsed="|Mark|4|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.4.41" />
<sup>41</sup>Nao wakaogopa sana, wakawa wanaulizana, "Huyu ni nani basi, hata upepo na mawimbi vinamtii?"
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 5" progress="14.18%" prev="Mark.4" next="Mark.6" id="Mark.5">
<h3 id="Mark.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Mark.5-p1">
<scripture passage="Mark 5:1" parsed="|Mark|5|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.1" />
<sup>1</sup>Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase, ng`ambo ya ziwa.
<scripture passage="Mark 5:2" parsed="|Mark|5|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.2" />
<sup>2</sup>Mara tu Yesu aliposhuka mashuani, mtu mmoja aliyepagawa na pepo mchafu alitoka makaburini, akakutana naye.
<scripture passage="Mark 5:3" parsed="|Mark|5|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.3" />
<sup>3</sup>Mtu huyo alikuwa akiishi makaburini wala hakuna mtu aliyeweza tena kumfunga kwa minyororo.
<scripture passage="Mark 5:4" parsed="|Mark|5|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.4" />
<sup>4</sup>Mara nyingi walimfunga kwa pingu na minyororo lakini kila mara aliweza kuikata hiyo minyororo na kuzivunja hizo pingu, wala hakuna mtu aliyeweza kumzuia.
<scripture passage="Mark 5:5" parsed="|Mark|5|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.5" />
<sup>5</sup>Mchana na usiku alikaa makaburini na milimani akipaaza sauti na kujikatakata kwa mawe.
<scripture passage="Mark 5:6" parsed="|Mark|5|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.6" />
<sup>6</sup>Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia, akamwinamia
<scripture passage="Mark 5:7" parsed="|Mark|5|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.7" />
<sup>7</sup>akisema kwa sauti kubwa, "Una shauri gani nami, wewe Yesu Mwana wa Mungu aliye juu? Kwa jina la Mungu, nakusihi usinitese!"
<scripture passage="Mark 5:8" parsed="|Mark|5|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.8" />
<sup>8</sup>Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, "Pepo mchafu, mtoke mtu huyu.")
<scripture passage="Mark 5:9" parsed="|Mark|5|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.9" />
<sup>9</sup>Basi, Yesu akamwuliza, "Jina lako nani?" Naye akajibu, "Jina langu ni `Jeshi`, maana sisi tu wengi."
<scripture passage="Mark 5:10" parsed="|Mark|5|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.10" />
<sup>10</sup>Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepo katika nchi ile.
<scripture passage="Mark 5:11" parsed="|Mark|5|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.11" />
<sup>11</sup>Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe malishoni kwenye mteremko wa mlima.
<scripture passage="Mark 5:12" parsed="|Mark|5|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.12" />
<sup>12</sup>Basi, hao pepo wakamsihi, "Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie."
<scripture passage="Mark 5:13" parsed="|Mark|5|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.13" />
<sup>13</sup>Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
<scripture passage="Mark 5:14" parsed="|Mark|5|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.14" />
<sup>14</sup>Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
<scripture passage="Mark 5:15" parsed="|Mark|5|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.15" />
<sup>15</sup>Wakamwendea Yesu, wakamwona na mtu yuleyule aliyekuwa amepagawa na jeshi la pepo ameketi chini, amevaa nguo na ana akili yake sawa, wakaogopa.
<scripture passage="Mark 5:16" parsed="|Mark|5|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.16" />
<sup>16</sup>Watu walishuhudia tukio hilo wakaeleza wengine mambo yaliyompata huyo mtu aliyekuwa amepagawa na pepo na juu ya wale nguruwe.
<scripture passage="Mark 5:17" parsed="|Mark|5|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.17" />
<sup>17</sup>Basi, wakaanza kumwomba aondoke katika nchi yao.
<scripture passage="Mark 5:18" parsed="|Mark|5|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.18" />
<sup>18</sup>Yesu alipokuwa anapanda mashuani, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akamwomba amruhusu kwenda naye.
<scripture passage="Mark 5:19" parsed="|Mark|5|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.19" />
<sup>19</sup>Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, "Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma."
<scripture passage="Mark 5:20" parsed="|Mark|5|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.20" />
<sup>20</sup>Basi, huyo mtu akaenda, akaanza kutangaza huko Dekapoli mambo yote Yesu aliyomtendea; watu wote wakashangaa.
<scripture passage="Mark 5:21" parsed="|Mark|5|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.21" />
<sup>21</sup>Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
<scripture passage="Mark 5:22" parsed="|Mark|5|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.22" />
<sup>22</sup>Hapo akaja mmojawapo wa maofisa wa sunagogi, jina lake Yairo. Alipomwona Yesu, akajitupa mbele ya miguu yake,
<scripture passage="Mark 5:23" parsed="|Mark|5|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.23" />
<sup>23</sup>akamsihi akisema, "Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi."
<scripture passage="Mark 5:24" parsed="|Mark|5|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.24" />
<sup>24</sup>Basi, Yesu akaondoka pamoja naye. Watu wengi sana wakamfuata, wakawa wanamsonga kila upande.
<scripture passage="Mark 5:25" parsed="|Mark|5|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.25" />
<sup>25</sup>Mmojawapo alikuwa mwanamke mwenye ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili.
<scripture passage="Mark 5:26" parsed="|Mark|5|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.26" />
<sup>26</sup>Mwanamke huyo alikuwa amekwisha sumbuka sana kuwaendea waganga wengi. Na ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote, hakupata nafuu bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
<scripture passage="Mark 5:27" parsed="|Mark|5|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.27" />
<sup>27</sup>Alikuwa amesikia habari za Yesu, na hivyo akaupenya msongamano wa watu kutoka nyuma, akagusa vazi lake.
<scripture passage="Mark 5:28" parsed="|Mark|5|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.28" />
<sup>28</sup>Alifanya hivyo, maana alijisemea, "Nikigusa tu vazi lake, nitapona."
<scripture passage="Mark 5:29" parsed="|Mark|5|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.29" />
<sup>29</sup>Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ameponywa ugonjwa wake.
<scripture passage="Mark 5:30" parsed="|Mark|5|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.30" />
<sup>30</sup>Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, "Nani aliyegusa mavazi yangu?"
<scripture passage="Mark 5:31" parsed="|Mark|5|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.31" />
<sup>31</sup>Wanafunzi wake wakamjibu, "Unaona jinsi watu wanavyokusonga; mbona wauliza nani aliyekugusa?"
<scripture passage="Mark 5:32" parsed="|Mark|5|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.32" />
<sup>32</sup>Lakini Yesu akaendelea kutazama amwone huyo aliyefanya hivyo.
<scripture passage="Mark 5:33" parsed="|Mark|5|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.33" />
<sup>33</sup>Hapo huyo mwanamke, akifahamu yaliyompata, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa chini mbele ya Yesu na kusema ukweli wote.
<scripture passage="Mark 5:34" parsed="|Mark|5|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.34" />
<sup>34</sup>Yesu akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako."
<scripture passage="Mark 5:35" parsed="|Mark|5|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.35" />
<sup>35</sup>Yesu alipokuwa bado anaongea, watu walifika kutoka nyumbani kwa yule ofisa wa sunagogi, wakamwambia, "Binti yako amekwisha kufa. Ya nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?"
<scripture passage="Mark 5:36" parsed="|Mark|5|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.36" />
<sup>36</sup>Lakini, bila kujali walichosema, Yesu akamwambia mkuu wa sunagogi, "Usiogope, amini tu."
<scripture passage="Mark 5:37" parsed="|Mark|5|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.37" />
<sup>37</sup>Wala hakumruhusu mtu yeyote kufuatana naye ila Petro, Yakobo na Yohane nduguye Yakobo.
<scripture passage="Mark 5:38" parsed="|Mark|5|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.38" />
<sup>38</sup>Wakafika nyumbani kwa ofisa wa sunagogi naye Yesu akasikia makelele, kilio na maombolezo mengi.
<scripture passage="Mark 5:39" parsed="|Mark|5|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.39" />
<sup>39</sup>Akaingia ndani, akawaambia, "Mbona mnapiga kelele na kulia? Msichana hakufa, amelala tu."
<scripture passage="Mark 5:40" parsed="|Mark|5|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.40" />
<sup>40</sup>Lakini wao wakamcheka. Basi, akawaondoa wote nje, akawachukua baba na mama ya huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
<scripture passage="Mark 5:41" parsed="|Mark|5|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.41" />
<sup>41</sup>Kisha akamshika mkono, akamwambia, "Talitha, kumi," maana yake, "Msichana, nakwambia, amka!"
<scripture passage="Mark 5:42" parsed="|Mark|5|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.42" />
<sup>42</sup>Mara msichana akasimama, akaanza kutembea. (Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili.) Hapo watu wakashangaa kupita kiasi.
<scripture passage="Mark 5:43" parsed="|Mark|5|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.5.43" />
<sup>43</sup>Yesu akawakataza sana wasimjulishe mtu jambo hilo. Kisha akawaambia wampe huyo msichana chakula.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 6" progress="14.67%" prev="Mark.5" next="Mark.7" id="Mark.6">
<h3 id="Mark.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Mark.6-p1">
<scripture passage="Mark 6:1" parsed="|Mark|6|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliondoka hapo akaenda katika kijiji chake, akifuatwa na wanafunzi wake.
<scripture passage="Mark 6:2" parsed="|Mark|6|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.2" />
<sup>2</sup>Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, "Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
<scripture passage="Mark 6:3" parsed="|Mark|6|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.3" />
<sup>3</sup>Je, huyu si yule seremala mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni; Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?" Basi, wakawa na mashaka naye. ic\is Ndani ya Sunagogi (Marko 6:2)\ie
<scripture passage="Mark 6:4" parsed="|Mark|6|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.4" />
<sup>4</sup>Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake."
<scripture passage="Mark 6:5" parsed="|Mark|6|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.5" />
<sup>5</sup>Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya.
<scripture passage="Mark 6:6" parsed="|Mark|6|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.6" />
<sup>6</sup>Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya pale karibu akiwafundisha watu.
<scripture passage="Mark 6:7" parsed="|Mark|6|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.7" />
<sup>7</sup>Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili, akaanza kuwatuma wawiliwawili. Aliwapa uwezo wa kuwatoa pepo wachafu,
<scripture passage="Mark 6:8" parsed="|Mark|6|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.8" />
<sup>8</sup>na kuwaamuru, "Msichukue chochote mnapokwenda isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni.
<scripture passage="Mark 6:9" parsed="|Mark|6|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.9" />
<sup>9</sup>Vaeni viatu lakini msivae kanzu mbili."
<scripture passage="Mark 6:10" parsed="|Mark|6|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.10" />
<sup>10</sup>Tena aliwaambia, "Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
<scripture passage="Mark 6:11" parsed="|Mark|6|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.11" />
<sup>11</sup>Mahali popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na kuyakung`uta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao."
<scripture passage="Mark 6:12" parsed="|Mark|6|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.12" />
<sup>12</sup>Basi, wakaondoka, wakahubiri watu watubu.
<scripture passage="Mark 6:13" parsed="|Mark|6|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.13" />
<sup>13</sup>Waliwafukuza pepo wengi wabaya; wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.
<scripture passage="Mark 6:14" parsed="|Mark|6|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.14" />
<sup>14</sup>Basi, mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilienea kila mahali. Baadhi ya watu walikuwa wakisema, "Yohane Mbatizaji amefufuka kutoka wafu, ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake."
<scripture passage="Mark 6:15" parsed="|Mark|6|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.15" />
<sup>15</sup>Wengine walisema, "Mtu huyu ni Eliya." Wengine walisema, "Huyu ni nabii kama mmojawapo wa manabii wa kale."
<scripture passage="Mark 6:16" parsed="|Mark|6|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.16" />
<sup>16</sup>Lakini Herode alipopata habari hizi alisema, "Huyu ni Yohane! Nilimkata kichwa, lakini amefufuka."
<scripture passage="Mark 6:17" parsed="|Mark|6|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.17" />
<sup>17</sup>Hapo awali Herode mwenyewe alikuwa ameamuru Yohane atiwe nguvuni, akamfunga gerezani. Herode alifanya hivyo kwa sababu ya Herodia ambaye Herode alimwoa ingawaje alikuwa mke wa Filipo, ndugu yake.
<scripture passage="Mark 6:18" parsed="|Mark|6|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.18" />
<sup>18</sup>Yohane alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kumchukua mke wa ndugu yako."
<scripture passage="Mark 6:19" parsed="|Mark|6|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.19" />
<sup>19</sup>Basi Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumwua, asiweze.
<scripture passage="Mark 6:20" parsed="|Mark|6|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.20" />
<sup>20</sup>Herode alimwogopa Yohane kwa maana alijua kwamba yeye ni mtu mwema na mtakatifu, na hivyo akamlinda. Herode alipenda kumsikiliza Yohane, ingawaje baada ya kumsikiliza, alifadhaika sana.
<scripture passage="Mark 6:21" parsed="|Mark|6|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.21" />
<sup>21</sup>Ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
<scripture passage="Mark 6:22" parsed="|Mark|6|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.22" />
<sup>22</sup>Basi, binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, "Niombe chochote utakacho, nami nitakupa."
<scripture passage="Mark 6:23" parsed="|Mark|6|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.23" />
<sup>23</sup>Tena akamwapia, "Chochote utakachoniomba, nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu."
<scripture passage="Mark 6:24" parsed="|Mark|6|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.24" />
<sup>24</sup>Hapo huyo msichana akatoka, akamwuliza mama yake, "Niombe nini?" Naye akamjibu, "Kichwa cha Yohane mbatizaji."
<scripture passage="Mark 6:25" parsed="|Mark|6|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.25" />
<sup>25</sup>Msichana akamrudia mfalme mbio akamwomba, "Nataka unipe sasa hivi katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji."
<scripture passage="Mark 6:26" parsed="|Mark|6|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.26" />
<sup>26</sup>Mfalme akahuzunika sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake, na kwa ajili ya wale wageni wake karamuni, hakutaka kumkatalia.
<scripture passage="Mark 6:27" parsed="|Mark|6|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.27" />
<sup>27</sup>Basi, mfalme akamwamuru askari kukileta kichwa cha Yohane. Askari akaenda, akamkata kichwa Yohane mle gerezani,
<scripture passage="Mark 6:28" parsed="|Mark|6|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.28" />
<sup>28</sup>akakileta katika sinia, akampa msichana naye msichana akampa mama yake.
<scripture passage="Mark 6:29" parsed="|Mark|6|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.29" />
<sup>29</sup>Wanafunzi wa Yohane walipopata habari, walikwenda wakachukua mwili wake, wakauzika kaburini.
<scripture passage="Mark 6:30" parsed="|Mark|6|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.30" />
<sup>30</sup>Wale mitume walirudi, wakakusanyika mbele ya Yesu wakamwarifu yote waliyotenda na kufundisha.
<scripture passage="Mark 6:31" parsed="|Mark|6|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.31" />
<sup>31</sup>Alisema hivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mno walikuwa wanafika hapo na kuondoka hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasi ya kula chakula. Basi, Yesu akawaambia, "Twendeni peke yetu mahali pa faragha kula chakula, mkapumzike kidogo."
<scripture passage="Mark 6:32" parsed="|Mark|6|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.32" />
<sup>32</sup>Basi, Wakaondoka peke yao kwa mashua, wakaenda mahali pa faragha.
<scripture passage="Mark 6:33" parsed="|Mark|6|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.33" />
<sup>33</sup>Lakini watu wengi waliwaona wakienda, wakawatambua. Hivyo wengi wakatoka katika kila mji, wakakimbilia huko Yesu na wanafunzi wake walikokuwa wanakwenda, wakawatangulia kufika.
<scripture passage="Mark 6:34" parsed="|Mark|6|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.34" />
<sup>34</sup>Waliposhuka pwani, Yesu aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji. Akaanza kuwafundisha mambo mengi.
<scripture passage="Mark 6:35" parsed="|Mark|6|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.35" />
<sup>35</sup>Saa za mchana zilikwisha pita. Basi, wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwambia, "Hapa ni nyikani, na sasa kunakuchwa.
<scripture passage="Mark 6:36" parsed="|Mark|6|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.36" />
<sup>36</sup>Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue chakula."
<scripture passage="Mark 6:37" parsed="|Mark|6|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.37" />
<sup>37</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Wapeni ninyi chakula." Nao wakamwuliza, "Je, twende kununua mikate kwa fedha dinari mia mbili, na kuwapa chakula?"
<scripture passage="Mark 6:38" parsed="|Mark|6|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.38" />
<sup>38</sup>Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame." Walipokwisha tazama, wakamwambia, "Kuna mikate mitano na samaki wawili." ic\is Mikate na samaki (Marko 6:38)\ie
<scripture passage="Mark 6:39" parsed="|Mark|6|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.39" />
<sup>39</sup>Basi, Yesu akawaamuru wanafunzi wawaketishe watu wote makundimakundi penye nyasi.
<scripture passage="Mark 6:40" parsed="|Mark|6|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.40" />
<sup>40</sup>Nao wakaketi makundimakundi ya watu mia moja na ya watu hamsini.
<scripture passage="Mark 6:41" parsed="|Mark|6|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.41" />
<sup>41</sup>Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.
<scripture passage="Mark 6:42" parsed="|Mark|6|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.42" />
<sup>42</sup>Watu wote wakala, wakashiba.
<scripture passage="Mark 6:43" parsed="|Mark|6|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.43" />
<sup>43</sup>Wakaokota mabaki ya mikate na samaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
<scripture passage="Mark 6:44" parsed="|Mark|6|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.44" />
<sup>44</sup>Nao waliokula hiyo mikate walikuwa wanaume elfu tano.
<scripture passage="Mark 6:45" parsed="|Mark|6|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.45" />
<sup>45</sup>Mara Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie kwenda Bethsaida, ng`ambo ya ziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu.
<scripture passage="Mark 6:46" parsed="|Mark|6|46|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.46" />
<sup>46</sup>Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali.
<scripture passage="Mark 6:47" parsed="|Mark|6|47|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.47" />
<sup>47</sup>Ilipokuwa jioni, mashua ilikuwa katikati ya ziwa, naye alikuwa peke yake katika nchi kavu.
<scripture passage="Mark 6:48" parsed="|Mark|6|48|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.48" />
<sup>48</sup>Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea akitembea juu ya maji. Alitaka kuwapita.
<scripture passage="Mark 6:49" parsed="|Mark|6|49|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.49" />
<sup>49</sup>Lakini walimwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu, wakapiga yowe.
<scripture passage="Mark 6:50" parsed="|Mark|6|50|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.50" />
<sup>50</sup>Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"
<scripture passage="Mark 6:51" parsed="|Mark|6|51|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.51" />
<sup>51</sup>Kisha akapanda mashuani walimokuwa, na upepo ukatulia. Nao wakashangaa sana.
<scripture passage="Mark 6:52" parsed="|Mark|6|52|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.52" />
<sup>52</sup>maana hawakuwa bado wameelewa maana ya ile mikate. Akili zao zilikuwa bado zimepumbazika.
<scripture passage="Mark 6:53" parsed="|Mark|6|53|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.53" />
<sup>53</sup>Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.
<scripture passage="Mark 6:54" parsed="|Mark|6|54|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.54" />
<sup>54</sup>Walipotoka mashuani, mara watu wakamtambua Yesu.
<scripture passage="Mark 6:55" parsed="|Mark|6|55|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.55" />
<sup>55</sup>Basi, kwa haraka wakazunguka katika nchi ile yote, wakaanza kuwachukua wagonjwa wamelala juu ya mikeka yao, wakawapeleka kila mahali waliposikia Yesu yupo.
<scripture passage="Mark 6:56" parsed="|Mark|6|56|0|0" osisRef="Bible:Mark.6.56" />
<sup>56</sup>Kila mahali Yesu alipokwenda, vijijini, mijini, au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa uwanjani, wakamsihi waguse walau pindo la vazi lake. Nao wote waliomgusa walipona.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 7" progress="15.34%" prev="Mark.6" next="Mark.8" id="Mark.7">
<h3 id="Mark.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Mark.7-p1">
<scripture passage="Mark 7:1" parsed="|Mark|7|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.1" />
<sup>1</sup>Baadhi ya Mafarisayo na walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu.
<scripture passage="Mark 7:2" parsed="|Mark|7|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.2" />
<sup>2</sup>Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.
<scripture passage="Mark 7:3" parsed="|Mark|7|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.3" />
<sup>3</sup>Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.
<scripture passage="Mark 7:4" parsed="|Mark|7|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.4" />
<sup>4</sup>Tena hawali kitu chochote kutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza.<i>fc</i> Kuna pia desturi nyingine walizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
<scripture passage="Mark 7:5" parsed="|Mark|7|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.5" />
<sup>5</sup>Basi, Mafarisayo na walimu wa Sheria wakamwuliza Yesu, "Mbona wanafunzi wako hawayajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu, bali hula chakula kwa mikono najisi?"
<scripture passage="Mark 7:6" parsed="|Mark|7|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.6" />
<sup>6</sup>Yesu akawajibu, "Wanafiki ninyi! Nabii Isaya alitabiri ukweli juu yenu alipoandika: `Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno matupu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
<scripture passage="Mark 7:7" parsed="|Mark|7|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.7" />
<sup>7</sup>Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.`
<scripture passage="Mark 7:8" parsed="|Mark|7|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.8" />
<sup>8</sup>Ninyi mnaiacha amri ya Mungu na kushikilia maagizo ya watu."
<scripture passage="Mark 7:9" parsed="|Mark|7|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.9" />
<sup>9</sup>Yesu akaendelea kusema, "Ninyi mnajua kuepa kwa ujanja sheria ya Mungu kwa ajili ya kufuata mapokeo yenu.
<scripture passage="Mark 7:10" parsed="|Mark|7|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.10" />
<sup>10</sup>Maana Mose aliamuru: `Waheshimu baba yako na mama yako,` na, `Anayemlaani baba au mama, lazima afe.`
<scripture passage="Mark 7:11" parsed="|Mark|7|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.11" />
<sup>11</sup>Lakini ninyi mwafundisha, `Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani ni zawadi kwa Mungu),
<scripture passage="Mark 7:12" parsed="|Mark|7|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.12" />
<sup>12</sup>basi, halazimiki tena kuwasaidia wazazi wake.`
<scripture passage="Mark 7:13" parsed="|Mark|7|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.13" />
<sup>13</sup>Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa ajili ya mafundisho mnayopokezana. Tena mnafanya mambo mengi ya namna hiyo."
<scripture passage="Mark 7:14" parsed="|Mark|7|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.14" />
<sup>14</sup>Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, "Nisikilizeni nyote, mkaelewe.
<scripture passage="Mark 7:15" parsed="|Mark|7|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.15" />
<sup>15</sup>Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu toka nje ambacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakini kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia mtu najisi."<i>fd</i>
<scripture passage="Mark 7:16" parsed="|Mark|7|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.16" />
<sup>16</sup>missing
<scripture passage="Mark 7:17" parsed="|Mark|7|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.17" />
<sup>17</sup>Alipouacha umati wa watu na kuingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza maana ya huo mfano.
<scripture passage="Mark 7:18" parsed="|Mark|7|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.18" />
<sup>18</sup>Naye akawaambia, "Je, hata ninyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu toka nje hakiwezi kumtia unajisi,
<scripture passage="Mark 7:19" parsed="|Mark|7|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.19" />
<sup>19</sup>kwa maana hakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?" (Kwa kusema hivyo, Yesu alivihalalisha vyakula vyote.)
<scripture passage="Mark 7:20" parsed="|Mark|7|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.20" />
<sup>20</sup>Akaendelea kusema, "Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.
<scripture passage="Mark 7:21" parsed="|Mark|7|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.21" />
<sup>21</sup>Kwa maana kutoka ndani, katika moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji,
<scripture passage="Mark 7:22" parsed="|Mark|7|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.22" />
<sup>22</sup>uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu.
<scripture passage="Mark 7:23" parsed="|Mark|7|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.23" />
<sup>23</sup>Maovu hayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu najisi."
<scripture passage="Mark 7:24" parsed="|Mark|7|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.24" />
<sup>24</sup>Yesu aliondoka hapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
<scripture passage="Mark 7:25" parsed="|Mark|7|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.25" />
<sup>25</sup>Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
<scripture passage="Mark 7:26" parsed="|Mark|7|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.26" />
<sup>26</sup>Mama huyo alikuwa Mgiriki, mwenyeji wa Sirofoinike. Basi, akamwomba Yesu amtoe binti yake pepo mchafu.
<scripture passage="Mark 7:27" parsed="|Mark|7|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.27" />
<sup>27</sup>Yesu akamwambia, "Kwanza watoto washibe; kwa maana si vizuri kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
<scripture passage="Mark 7:28" parsed="|Mark|7|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.28" />
<sup>28</sup>Lakini huyo mama akasema, "Sawa, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto."
<scripture passage="Mark 7:29" parsed="|Mark|7|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.29" />
<sup>29</sup>Yesu akamwambia, "Kwa sababu ya neno hilo, nenda. Pepo amemtoka binti yako!"
<scripture passage="Mark 7:30" parsed="|Mark|7|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.30" />
<sup>30</sup>Basi, akaenda nyumbani kwake, akamkuta mtoto amelala kitandani, na pepo amekwisha mtoka.
<scripture passage="Mark 7:31" parsed="|Mark|7|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.31" />
<sup>31</sup>Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
<scripture passage="Mark 7:32" parsed="|Mark|7|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakamletea bubu-kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
<scripture passage="Mark 7:33" parsed="|Mark|7|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.33" />
<sup>33</sup>Yesu akamtenga na umati wa watu, akamtia vidole masikioni, akatema mate na kumgusa ulimi.
<scripture passage="Mark 7:34" parsed="|Mark|7|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.34" />
<sup>34</sup>Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, "Efatha," maana yake, "Funguka."
<scripture passage="Mark 7:35" parsed="|Mark|7|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.35" />
<sup>35</sup>Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukafunguliwa, akaanza kusema sawasawa.
<scripture passage="Mark 7:36" parsed="|Mark|7|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.36" />
<sup>36</sup>Yesu akawaamuru wasimwambie mtu juu ya jambo hilo. Lakini kadiri alivyowakataza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari hiyo.
<scripture passage="Mark 7:37" parsed="|Mark|7|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.7.37" />
<sup>37</sup>Watu walishangaa sana, wakasema, "Amefanya yote vyema: amewajalia viziwi kusikia, na bubu kusema!"
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 8" progress="15.75%" prev="Mark.7" next="Mark.9" id="Mark.8">
<h3 id="Mark.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Mark.8-p1">
<scripture passage="Mark 8:1" parsed="|Mark|8|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.1" />
<sup>1</sup>Wakati huo umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena, na hawakuwa na chakula. Basi, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia,
<scripture passage="Mark 8:2" parsed="|Mark|8|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.2" />
<sup>2</sup>"Nawahurumia watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu, wala hawana chakula.
<scripture passage="Mark 8:3" parsed="|Mark|8|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.3" />
<sup>3</sup>Nikiwaacha waende nyumbani wakiwa na njaa watazimia njiani, maana baadhi yao wametoka mbali."
<scripture passage="Mark 8:4" parsed="|Mark|8|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.4" />
<sup>4</sup>Wanafunzi wake wakamwuliza, "Hapa nyikani itapatikana wapi mikate ya kuwashibisha watu hawa wote?"
<scripture passage="Mark 8:5" parsed="|Mark|8|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.5" />
<sup>5</sup>Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Nao wakamjibu, "Saba."
<scripture passage="Mark 8:6" parsed="|Mark|8|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.6" />
<sup>6</sup>Basi, akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu, nao wakawagawia.
<scripture passage="Mark 8:7" parsed="|Mark|8|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.7" />
<sup>7</sup>Walikuwa pia na visamaki vichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.
<scripture passage="Mark 8:8" parsed="|Mark|8|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.8" />
<sup>8</sup>Watu wakala, wakashiba. Wakaokota mabaki yaliyosalia wakajaza makapu saba.
<scripture passage="Mark 8:9" parsed="|Mark|8|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.9" />
<sup>9</sup>Nao waliokula walikuwa watu wapatao elfu nne. Yesu akawaaga,
<scripture passage="Mark 8:10" parsed="|Mark|8|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.10" />
<sup>10</sup>na mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya ya Dalmanutha.
<scripture passage="Mark 8:11" parsed="|Mark|8|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.11" />
<sup>11</sup>Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka awafanyie ishara kuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni.
<scripture passage="Mark 8:12" parsed="|Mark|8|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.12" />
<sup>12</sup>Yesu akahuzunika rohoni, akasema, "Mbona kizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote!"
<scripture passage="Mark 8:13" parsed="|Mark|8|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.13" />
<sup>13</sup>Basi, akawaacha, akapanda tena mashua, akaanza safari kwenda ng`ambo ya pili ya ziwa.
<scripture passage="Mark 8:14" parsed="|Mark|8|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.14" />
<sup>14</sup>Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate; walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua.
<scripture passage="Mark 8:15" parsed="|Mark|8|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.15" />
<sup>15</sup>Yesu akawaonya, "Angalieni sana! Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode."
<scripture passage="Mark 8:16" parsed="|Mark|8|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.16" />
<sup>16</sup>Wanafunzi wakaanza kujadiliana wao kwa wao, "Anasema hivyo kwa kuwa hatuna mikate."
<scripture passage="Mark 8:17" parsed="|Mark|8|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.17" />
<sup>17</sup>Yesu alitambua hayo, akawaambia, "Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu, wala hamjaelewa? Je, mioyo yenu imeshupaa?
<scripture passage="Mark 8:18" parsed="|Mark|8|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.18" />
<sup>18</sup>Je, Mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki
<scripture passage="Mark 8:19" parsed="|Mark|8|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.19" />
<sup>19</sup>wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu elfu tano? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki ya makombo?" Wakamjibu, "Kumi na viwili."
<scripture passage="Mark 8:20" parsed="|Mark|8|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.20" />
<sup>20</sup>"Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu elfu nne, mlikusanya makapu mangapi ya makombo?" Wakamjibu, "Saba."
<scripture passage="Mark 8:21" parsed="|Mark|8|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.21" />
<sup>21</sup>Basi, akawaambia, "Na bado hamjaelewa?"
<scripture passage="Mark 8:22" parsed="|Mark|8|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.22" />
<sup>22</sup>Yesu alifika Bethsaida pamoja na wanafunzi wake. Huko watu wakamletea kipofu mmoja, wakamwomba amguse.
<scripture passage="Mark 8:23" parsed="|Mark|8|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.23" />
<sup>23</sup>Yesu akamshika mkono huyo kipofu, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, "Je, unaweza kuona kitu?"
<scripture passage="Mark 8:24" parsed="|Mark|8|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.24" />
<sup>24</sup>Huyo kipofu akatazama, akasema, "Ninawaona watu wanaoonekana kama miti inayotembea."
<scripture passage="Mark 8:25" parsed="|Mark|8|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.25" />
<sup>25</sup>Kisha Yesu akamwekea tena mikono machoni, naye akakaza macho, uwezo wake wa kuona ukamrudia, akaona kila kitu sawasawa.
<scripture passage="Mark 8:26" parsed="|Mark|8|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.26" />
<sup>26</sup>Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, "Usirudi kijijini!"
<scripture passage="Mark 8:27" parsed="|Mark|8|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.27" />
<sup>27</sup>Kisha Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika vijiji vya Kaisarea Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu aliwauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema mimi ni nani?"
<scripture passage="Mark 8:28" parsed="|Mark|8|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.28" />
<sup>28</sup>Wakamjibu, "Wengine wanasema wewe ni Yohane Mbatizaji, wengine Eliya na wengine mmojawapo wa manabii."
<scripture passage="Mark 8:29" parsed="|Mark|8|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.29" />
<sup>29</sup>Naye akawauliza, "Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?" Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo."
<scripture passage="Mark 8:30" parsed="|Mark|8|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.30" />
<sup>30</sup>Kisha Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.
<scripture passage="Mark 8:31" parsed="|Mark|8|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.31" />
<sup>31</sup>Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake: "Ni lazima Mwana wa Mtu apatwe na mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Atauawa na baada ya siku tatu atafufuka."
<scripture passage="Mark 8:32" parsed="|Mark|8|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.32" />
<sup>32</sup>Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Basi, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea.
<scripture passage="Mark 8:33" parsed="|Mark|8|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.33" />
<sup>33</sup>Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, "Ondoka mbele yangu, Shetani! Fikira zako si za kimungu ila ni za kibinadamu!"
<scripture passage="Mark 8:34" parsed="|Mark|8|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.34" />
<sup>34</sup>Kisha akauita umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
<scripture passage="Mark 8:35" parsed="|Mark|8|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.35" />
<sup>35</sup>Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa.
<scripture passage="Mark 8:36" parsed="|Mark|8|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.36" />
<sup>36</sup>Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake?
<scripture passage="Mark 8:37" parsed="|Mark|8|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.37" />
<sup>37</sup>Ama mtu atatoa kitu gani badala ya maisha yake?
<scripture passage="Mark 8:38" parsed="|Mark|8|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.8.38" />
<sup>38</sup>Mtu yeyote katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu anayenionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 9" progress="16.18%" prev="Mark.8" next="Mark.10" id="Mark.9">
<h3 id="Mark.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Mark.9-p1">
<scripture passage="Mark 9:1" parsed="|Mark|9|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.1" />
<sup>1</sup>Yesu akaendelea kuwaambia, "Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa enzi."
<scripture passage="Mark 9:2" parsed="|Mark|9|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.2" />
<sup>2</sup>Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
<scripture passage="Mark 9:3" parsed="|Mark|9|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.3" />
<sup>3</sup>mavazi yake yakang`aa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe.
<scripture passage="Mark 9:4" parsed="|Mark|9|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.4" />
<sup>4</sup>Eliya na Mose wakawatokea, wakazungumza na Yesu.
<scripture passage="Mark 9:5" parsed="|Mark|9|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.5" />
<sup>5</sup>Petro akamwambia Yesu, "Mwalimu, ni vizuri sana kwamba tuko hapa. Basi, afadhali tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."
<scripture passage="Mark 9:6" parsed="|Mark|9|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.6" />
<sup>6</sup>Yeye na wenzake waliogopa hata hakujua la kusema.
<scripture passage="Mark 9:7" parsed="|Mark|9|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.7" />
<sup>7</sup>Kisha likatokea wingu likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu, "Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni."
<scripture passage="Mark 9:8" parsed="|Mark|9|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.8" />
<sup>8</sup>Mara wanafunzi hao wakatazama tena, lakini hawakumwona mtu mwingine, ila Yesu peke yake pamoja nao.
<scripture passage="Mark 9:9" parsed="|Mark|9|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.9" />
<sup>9</sup>Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka kutoka wafu.
<scripture passage="Mark 9:10" parsed="|Mark|9|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.10" />
<sup>10</sup>Basi, wakashika agizo hilo, lakini wakawa wanajadiliana wao kwa wao maana ya kufufuka kutoka wafu.
<scripture passage="Mark 9:11" parsed="|Mark|9|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.11" />
<sup>11</sup>Wakamwuliza Yesu, "Mbona walimu wa Sheria wanasema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?"
<scripture passage="Mark 9:12" parsed="|Mark|9|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.12" />
<sup>12</sup>Naye akawajibu, "Naam, Eliya anakuja kwanza kutayarisha yote. Hata hivyo, kwa nini basi imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Mwana wa Mtu atapatwa na mateso mengi na kudharauliwa?
<scripture passage="Mark 9:13" parsed="|Mark|9|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.13" />
<sup>13</sup>Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyotaka kama ilivyoandikwa juu yake."
<scripture passage="Mark 9:14" parsed="|Mark|9|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.14" />
<sup>14</sup>Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliona umati mkubwa wa watu hapo. Na baadhi ya walimu wa Sheria walikuwa wanajadiliana nao.
<scripture passage="Mark 9:15" parsed="|Mark|9|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.15" />
<sup>15</sup>Mara tu ule umati wa watu ulipomwona, wote walishangaa sana, wakamkimbilia wamsalimu.
<scripture passage="Mark 9:16" parsed="|Mark|9|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.16" />
<sup>16</sup>Yesu akawauliza, "Mnajadiliana nini nao?"
<scripture passage="Mark 9:17" parsed="|Mark|9|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.17" />
<sup>17</sup>Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, "Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
<scripture passage="Mark 9:18" parsed="|Mark|9|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.18" />
<sup>18</sup>Kila mara anapomvamia, humwangusha chini na kumfanya atokwe na povu kinywani, akisaga meno na kuwa mkavu mwili wote. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo lakini hawakuweza."
<scripture passage="Mark 9:19" parsed="|Mark|9|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.19" />
<sup>19</sup>Yesu akawaambia, "Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kwangu."
<scripture passage="Mark 9:20" parsed="|Mark|9|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.20" />
<sup>20</sup>Wakampeleka. Mara tu huyo pepo alipomwona Yesu, alimtia mtoto kifafa, naye mtoto akaanguka chini, akagaagaa na kutoka povu kinywani. Yesu akamwuliza baba yake huyo mtoto,
<scripture passage="Mark 9:21" parsed="|Mark|9|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.21" />
<sup>21</sup>"Amepatwa na mambo hayo tangu lini?" Naye akamjibu, "Tangu utoto wake.
<scripture passage="Mark 9:22" parsed="|Mark|9|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.22" />
<sup>22</sup>Na mara nyingi pepo huyo amemwangusha motoni na majini, ili amwangamize kabisa. Basi, ikiwa waweza, utuhurumie na kutusaidia!"
<scripture passage="Mark 9:23" parsed="|Mark|9|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.23" />
<sup>23</sup>Yesu akamwambia, "Eti ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani."
<scripture passage="Mark 9:24" parsed="|Mark|9|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.24" />
<sup>24</sup>Hapo, huyo baba akalia kwa sauti, "Naamini! Lakini imani yangu haitoshi, nisaidie!"
<scripture passage="Mark 9:25" parsed="|Mark|9|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.25" />
<sup>25</sup>Yesu alipouona umati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimkemea yule pepo mchafu, "Pepo unayemfanya huyu mtoto kuwa bubu-kiziwi, nakuamuru, mtoke mtoto huyu wala usimwingie tena!"
<scripture passage="Mark 9:26" parsed="|Mark|9|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.26" />
<sup>26</sup>Hapo huyo pepo alipaaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto alionekana kama maiti, hata wengine walisema, "Amekufa!"
<scripture passage="Mark 9:27" parsed="|Mark|9|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.27" />
<sup>27</sup>Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.
<scripture passage="Mark 9:28" parsed="|Mark|9|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.28" />
<sup>28</sup>Yesu alipoingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza kwa faragha, "Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa?"
<scripture passage="Mark 9:29" parsed="|Mark|9|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.29" />
<sup>29</sup>Naye akawaambia, "Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala tu."
<scripture passage="Mark 9:30" parsed="|Mark|9|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.30" />
<sup>30</sup>Yesu na wanafunzi wake waliondoka hapo, wakaendelea na safari kupitia wilaya ya Galilaya. Yesu hakupenda watu wajue alipokuwa,
<scripture passage="Mark 9:31" parsed="|Mark|9|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.31" />
<sup>31</sup>kwa sababu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, "Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu ambao watamuua; lakini siku ya tatu baada ya kuuawa atafufuka."
<scripture passage="Mark 9:32" parsed="|Mark|9|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.32" />
<sup>32</sup>Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo. Wakaogopa kumwuliza.
<scripture passage="Mark 9:33" parsed="|Mark|9|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.33" />
<sup>33</sup>Basi, walifika Kafarnaumu. Na alipokuwa nyumbani, aliwauliza, "Mlikuwa mnajadiliana nini njiani?"
<scripture passage="Mark 9:34" parsed="|Mark|9|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.34" />
<sup>34</sup>Lakini wao wakanyamaza, maana njiani walikuwa wamebishana ni nani aliye mkuu kati yao.
<scripture passage="Mark 9:35" parsed="|Mark|9|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.35" />
<sup>35</sup>Yesu akaketi chini, akawaita wale kumi na wawili, akawaambia, "Yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho na kuwa mtumishi wa wote."
<scripture passage="Mark 9:36" parsed="|Mark|9|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.36" />
<sup>36</sup>Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kati yao, akamku mbatia, halafu akawaambia,
<scripture passage="Mark 9:37" parsed="|Mark|9|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.37" />
<sup>37</sup>"Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma."
<scripture passage="Mark 9:38" parsed="|Mark|9|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.38" />
<sup>38</sup>Yohane akamwambia, "Mwalimu, tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu."
<scripture passage="Mark 9:39" parsed="|Mark|9|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.39" />
<sup>39</sup>Lakini Yesu akasema, "Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya muujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
<scripture passage="Mark 9:40" parsed="|Mark|9|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.40" />
<sup>40</sup>Maana, asiyepingana nasi, yuko upande wetu.
<scripture passage="Mark 9:41" parsed="|Mark|9|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.41" />
<sup>41</sup>Mtu yeyote atakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
<scripture passage="Mark 9:42" parsed="|Mark|9|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.42" />
<sup>42</sup>"Mtu yeyote atakayemfanya mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingekuwa afadhali kwa mtu huyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa la kusagia na kutupwa baharini.
<scripture passage="Mark 9:43" parsed="|Mark|9|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.43" />
<sup>43</sup>Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia kwenye uzima bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu.<i>fe</i>
<scripture passage="Mark 9:44" parsed="|Mark|9|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.44" />
<sup>44</sup>missing
<scripture passage="Mark 9:45" parsed="|Mark|9|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.45" />
<sup>45</sup>Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uzima bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.<i>ff</i>
<scripture passage="Mark 9:46" parsed="|Mark|9|46|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.46" />
<sup>46</sup>missing
<scripture passage="Mark 9:47" parsed="|Mark|9|47|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.47" />
<sup>47</sup>Na jicho lako likikukosesha, ling`oe! Afadhali kuingia katika utawala wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
<scripture passage="Mark 9:48" parsed="|Mark|9|48|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.48" />
<sup>48</sup>Humo wadudu wake hawafi, na moto hauzimiki. ic\is Mawe ya kusagia (Marko 9:42)\ie moto hauzimiki. moto hauzimiki.
<scripture passage="Mark 9:49" parsed="|Mark|9|49|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.49" />
<sup>49</sup>"Maana kila mmoja atakolezwa kwa moto.
<scripture passage="Mark 9:50" parsed="|Mark|9|50|0|0" osisRef="Bible:Mark.9.50" />
<sup>50</sup>Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu na kudumisha amani kati yenu."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 10" progress="16.77%" prev="Mark.9" next="Mark.11" id="Mark.10">
<h3 id="Mark.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Mark.10-p1">
<scripture passage="Mark 10:1" parsed="|Mark|10|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.1" />
<sup>1</sup>Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata ng`ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
<scripture passage="Mark 10:2" parsed="|Mark|10|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.2" />
<sup>2</sup>Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, "Je, ni halali mtu kumpa talaka mkewe?"
<scripture passage="Mark 10:3" parsed="|Mark|10|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawajibu, "Mose aliwapa maagizo gani?"
<scripture passage="Mark 10:4" parsed="|Mark|10|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.4" />
<sup>4</sup>Nao wakasema, "Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha."
<scripture passage="Mark 10:5" parsed="|Mark|10|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.5" />
<sup>5</sup>Yesu akawaambia, "Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
<scripture passage="Mark 10:6" parsed="|Mark|10|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.6" />
<sup>6</sup>Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke.
<scripture passage="Mark 10:7" parsed="|Mark|10|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.7" />
<sup>7</sup>Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe,
<scripture passage="Mark 10:8" parsed="|Mark|10|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.8" />
<sup>8</sup>nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.
<scripture passage="Mark 10:9" parsed="|Mark|10|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.9" />
<sup>9</sup>Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe."
<scripture passage="Mark 10:10" parsed="|Mark|10|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.10" />
<sup>10</sup>Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo.
<scripture passage="Mark 10:11" parsed="|Mark|10|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.11" />
<sup>11</sup>Naye akawaambia, "Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe.
<scripture passage="Mark 10:12" parsed="|Mark|10|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.12" />
<sup>12</sup>Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini."
<scripture passage="Mark 10:13" parsed="|Mark|10|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.13" />
<sup>13</sup>Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
<scripture passage="Mark 10:14" parsed="|Mark|10|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.14" />
<sup>14</sup>Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa.
<scripture passage="Mark 10:15" parsed="|Mark|10|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.15" />
<sup>15</sup>Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia katika Ufalme huo."
<scripture passage="Mark 10:16" parsed="|Mark|10|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.16" />
<sup>16</sup>Kisha akawapokea watoto hao, akawawekea mikono, akawabariki.
<scripture passage="Mark 10:17" parsed="|Mark|10|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.17" />
<sup>17</sup>Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?"
<scripture passage="Mark 10:18" parsed="|Mark|10|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.18" />
<sup>18</sup>Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake.
<scripture passage="Mark 10:19" parsed="|Mark|10|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.19" />
<sup>19</sup>Unazijua amri: `Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba na mama yako."`
<scripture passage="Mark 10:20" parsed="|Mark|10|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.20" />
<sup>20</sup>Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu."
<scripture passage="Mark 10:21" parsed="|Mark|10|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.21" />
<sup>21</sup>Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate."
<scripture passage="Mark 10:22" parsed="|Mark|10|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.22" />
<sup>22</sup>Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi.
<scripture passage="Mark 10:23" parsed="|Mark|10|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.23" />
<sup>23</sup>Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!"
<scripture passage="Mark 10:24" parsed="|Mark|10|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.24" />
<sup>24</sup>Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, "Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu!
<scripture passage="Mark 10:25" parsed="|Mark|10|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.25" />
<sup>25</sup>Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Mark 10:26" parsed="|Mark|10|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.26" />
<sup>26</sup>Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?"
<scripture passage="Mark 10:27" parsed="|Mark|10|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.27" />
<sup>27</sup>Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana."
<scripture passage="Mark 10:28" parsed="|Mark|10|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.28" />
<sup>28</sup>Petro akamwambia, "Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!"
<scripture passage="Mark 10:29" parsed="|Mark|10|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.29" />
<sup>29</sup>Yesu akasema, "Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema,
<scripture passage="Mark 10:30" parsed="|Mark|10|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.30" />
<sup>30</sup>atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele.
<scripture passage="Mark 10:31" parsed="|Mark|10|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.31" />
<sup>31</sup>Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."
<scripture passage="Mark 10:32" parsed="|Mark|10|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.32" />
<sup>32</sup>Basi, walikuwa njiani kwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
<scripture passage="Mark 10:33" parsed="|Mark|10|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.33" />
<sup>33</sup>"Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe na kumkabidhi kwa watu wa mataifa.
<scripture passage="Mark 10:34" parsed="|Mark|10|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.34" />
<sup>34</sup>Nao watamdhihaki; watamtemea mate, watampiga mijeledi na kumwua. Na baada ya siku tatu atafufuka."
<scripture passage="Mark 10:35" parsed="|Mark|10|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.35" />
<sup>35</sup>Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba."
<scripture passage="Mark 10:36" parsed="|Mark|10|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.36" />
<sup>36</sup>Yesu akawauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
<scripture passage="Mark 10:37" parsed="|Mark|10|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.37" />
<sup>37</sup>Wakamjibu, "Uturuhusu tuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wa Ufalme wako."
<scripture passage="Mark 10:38" parsed="|Mark|10|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.38" />
<sup>38</sup>Yesu akawaambia, "Hamjui mnachoomba! Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa, au kubatizwa kama nitakavyobatizwa?"
<scripture passage="Mark 10:39" parsed="|Mark|10|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.39" />
<sup>39</sup>Wakamjibu, "Tunaweza." Yesu akawaambia, "Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli, na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa.
<scripture passage="Mark 10:40" parsed="|Mark|10|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.40" />
<sup>40</sup>Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga, bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa."
<scripture passage="Mark 10:41" parsed="|Mark|10|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.41" />
<sup>41</sup>Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane.
<scripture passage="Mark 10:42" parsed="|Mark|10|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.42" />
<sup>42</sup>Yesu akawaita, akawaambia, "Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
<scripture passage="Mark 10:43" parsed="|Mark|10|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.43" />
<sup>43</sup>Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu, sharti awe mtumishi wenu.
<scripture passage="Mark 10:44" parsed="|Mark|10|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.44" />
<sup>44</sup>Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote.
<scripture passage="Mark 10:45" parsed="|Mark|10|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.45" />
<sup>45</sup>Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi."
<scripture passage="Mark 10:46" parsed="|Mark|10|46|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.46" />
<sup>46</sup>Basi, wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwa anatoka katika mji huo akiwa na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mwombaji aitwaye Bartimayo mwana wa Timayo alikuwa ameketi kando ya barabara.
<scripture passage="Mark 10:47" parsed="|Mark|10|47|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.47" />
<sup>47</sup>Aliposikia kwamba ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita mahali hapo, alianza kupaaza sauti, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
<scripture passage="Mark 10:48" parsed="|Mark|10|48|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.48" />
<sup>48</sup>Watu wengi walimkemea ili anyamaze, lakini yeye akazidi kupaaza sauti, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
<scripture passage="Mark 10:49" parsed="|Mark|10|49|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.49" />
<sup>49</sup>Yesu alisimama, akasema, "Mwiteni." Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, "Jipe moyo! Simama, anakuita."
<scripture passage="Mark 10:50" parsed="|Mark|10|50|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.50" />
<sup>50</sup>Naye akatupilia mbali vazi lake, akaruka juu, akamwendea Yesu.
<scripture passage="Mark 10:51" parsed="|Mark|10|51|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.51" />
<sup>51</sup>Yesu akamwuliza, "Unataka nikufanyie nini?" Huyo kipofu akamwambia, "Mwalimu, naomba nipate kuona."
<scripture passage="Mark 10:52" parsed="|Mark|10|52|0|0" osisRef="Bible:Mark.10.52" />
<sup>52</sup>Yesu akamwambia, "Nenda, imani yako imekuponya." Mara huyo kipofu akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 11" progress="17.35%" prev="Mark.10" next="Mark.12" id="Mark.11">
<h3 id="Mark.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Mark.11-p1">
<scripture passage="Mark 11:1" parsed="|Mark|11|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.1" />
<sup>1</sup>Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu walifika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni. Hapo aliwatuma wawili wa wanafunzi wake,
<scripture passage="Mark 11:2" parsed="|Mark|11|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.2" />
<sup>2</sup>akawaambia, "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwana punda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
<scripture passage="Mark 11:3" parsed="|Mark|11|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.3" />
<sup>3</sup>Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnafanya hivyo?` Mwambieni, `Bwana anamhitaji na atamrudisha hapa mara."` ic\is Bethania (Marko 11:1)\ie
<scripture passage="Mark 11:4" parsed="|Mark|11|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.4" />
<sup>4</sup>Basi, wakaenda, wakamkuta mwana punda barabarani amefungwa mlangoni. Walipokuwa wakimfungua,
<scripture passage="Mark 11:5" parsed="|Mark|11|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.5" />
<sup>5</sup>baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza "Kwa nini mnamfungua huyo mwana punda?"
<scripture passage="Mark 11:6" parsed="|Mark|11|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.6" />
<sup>6</sup>Wanafunzi wakajibu kama Yesu alivyokuwa amewaambia; nao wakawaacha waende zao.
<scripture passage="Mark 11:7" parsed="|Mark|11|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.7" />
<sup>7</sup>Wakampelekea Yesu huyo mwana punda. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana punda, na Yesu akaketi juu yake.
<scripture passage="Mark 11:8" parsed="|Mark|11|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.8" />
<sup>8</sup>Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani; wengine wakatandaza matawi ya miti waliyoyakata mashambani.
<scripture passage="Mark 11:9" parsed="|Mark|11|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.9" />
<sup>9</sup>Watu wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao wakisema, "Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!
<scripture passage="Mark 11:10" parsed="|Mark|11|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.10" />
<sup>10</sup>Ubarikiwe Ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!"
<scripture passage="Mark 11:11" parsed="|Mark|11|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.11" />
<sup>11</sup>Yesu aliingia mjini Yerusalemu akaenda moja kwa moja mpaka Hekaluni, akatazama kila kitu kwa makini. Lakini kwa vile ilikwisha kuwa jioni, akaenda Bethania pamoja na wale kumi na wawili.
<scripture passage="Mark 11:12" parsed="|Mark|11|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.12" />
<sup>12</sup>Kesho yake, walipokuwa wanatoka Bethania, Yesu aliona njaa.
<scripture passage="Mark 11:13" parsed="|Mark|11|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.13" />
<sup>13</sup>Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila majani matupu, kwa vile hayakuwa majira ya mtini kuzaa matunda.
<scripture passage="Mark 11:14" parsed="|Mark|11|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.14" />
<sup>14</sup>Hapo akauambia mtini, "Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako." Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
<scripture passage="Mark 11:15" parsed="|Mark|11|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.15" />
<sup>15</sup>Basi, wakafika Yerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza nje watu waliokuwa wanauza na kununua vitu humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilishana fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
<scripture passage="Mark 11:16" parsed="|Mark|11|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.16" />
<sup>16</sup>Hakumruhusu mtu yeyote kupitia Hekaluni akichukua kitu.
<scripture passage="Mark 11:17" parsed="|Mark|11|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.17" />
<sup>17</sup>Kisha akawafundisha, "Imeandikwa: `Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote!` Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi!"
<scripture passage="Mark 11:18" parsed="|Mark|11|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.18" />
<sup>18</sup>Makuhani wakuu na walimu wa Sheria waliposikia hayo, walianza kutafuta njia ya kumwangamiza. Lakini walimwogopa kwa sababu umati wa watu ulishangazwa na mafundisho yake.
<scripture passage="Mark 11:19" parsed="|Mark|11|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.19" />
<sup>19</sup>Ilipokuwa jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini.
<scripture passage="Mark 11:20" parsed="|Mark|11|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.20" />
<sup>20</sup>Asubuhi na mapema, walipokuwa wanapita, waliuona ule mtini umenyauka wote, hata mizizi.
<scripture passage="Mark 11:21" parsed="|Mark|11|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.21" />
<sup>21</sup>Petro aliukumbuka, akamwambia Yesu, "Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani, umenyauka!"
<scripture passage="Mark 11:22" parsed="|Mark|11|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.22" />
<sup>22</sup>Yesu akawaambia, "Mwaminini Mungu.
<scripture passage="Mark 11:23" parsed="|Mark|11|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.23" />
<sup>23</sup>Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: `Ng`oka ukajitose baharini` bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
<scripture passage="Mark 11:24" parsed="|Mark|11|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.24" />
<sup>24</sup>Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.
<scripture passage="Mark 11:25" parsed="|Mark|11|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.25" />
<sup>25</sup>Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.<i>fg</i> hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."
<scripture passage="Mark 11:26" parsed="|Mark|11|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.26" />
<sup>26</sup>missing
<scripture passage="Mark 11:27" parsed="|Mark|11|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.27" />
<sup>27</sup>Basi, wakafika tena Yerusalemu. Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walimwendea,
<scripture passage="Mark 11:28" parsed="|Mark|11|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.28" />
<sup>28</sup>wakamwuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani aliyekupa mamlaka ya kufanya mambo haya?"
<scripture passage="Mark 11:29" parsed="|Mark|11|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.29" />
<sup>29</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, na pia nitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
<scripture passage="Mark 11:30" parsed="|Mark|11|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.30" />
<sup>30</sup>Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka mbinguni ama kwa watu? Nijibuni."
<scripture passage="Mark 11:31" parsed="|Mark|11|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.31" />
<sup>31</sup>Wakaanza kujadiliana, "Tukisema, `Yalitoka mbinguni`, atatuuliza, `Basi, mbona hamkumsadiki?`
<scripture passage="Mark 11:32" parsed="|Mark|11|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.32" />
<sup>32</sup>Na tukisema, `Yalitoka kwa watu..."` (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.)
<scripture passage="Mark 11:33" parsed="|Mark|11|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.11.33" />
<sup>33</sup>Basi, wakamjibu Yesu, "Sisi hatujui." Naye Yesu akawaambia, "Nami pia sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 12" progress="17.75%" prev="Mark.11" next="Mark.13" id="Mark.12">
<h3 id="Mark.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Mark.12-p1">
<scripture passage="Mark 12:1" parsed="|Mark|12|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.1" />
<sup>1</sup>Yesu alianza kusema nao kwa mifano: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
<scripture passage="Mark 12:2" parsed="|Mark|12|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.2" />
<sup>2</sup>Wakati wa mavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima akamletee sehemu ya mazao ya shamba lake.
<scripture passage="Mark 12:3" parsed="|Mark|12|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.3" />
<sup>3</sup>Wale wakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
<scripture passage="Mark 12:4" parsed="|Mark|12|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.4" />
<sup>4</sup>Akatuma tena mtumishi mwingine; huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.
<scripture passage="Mark 12:5" parsed="|Mark|12|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.5" />
<sup>5</sup>Mwenye shamba akatuma mtumishi mwingine tena, na huyo wakamuua. Wengine wengi waliotumwa, baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa.
<scripture passage="Mark 12:6" parsed="|Mark|12|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.6" />
<sup>6</sup>Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishowe akamtuma huyo akisema, `Watamheshimu mwanangu.`
<scripture passage="Mark 12:7" parsed="|Mark|12|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.7" />
<sup>7</sup>Lakini hao wakulima wakaambiana, `Huyu ndiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu!`
<scripture passage="Mark 12:8" parsed="|Mark|12|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.8" />
<sup>8</sup>Kwa hiyo wakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu. ic Mnara ndani ya shamba la mizabibu (Marko 12:1)
<scripture passage="Mark 12:9" parsed="|Mark|12|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.9" />
<sup>9</sup>"Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na kulikodisha hilo shamba la mizabibu kwa watu wengine.
<scripture passage="Mark 12:10" parsed="|Mark|12|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.10" />
<sup>10</sup>Je, hamjasoma Maandiko haya? `Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.
<scripture passage="Mark 12:11" parsed="|Mark|12|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.11" />
<sup>11</sup>Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu."`
<scripture passage="Mark 12:12" parsed="|Mark|12|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.12" />
<sup>12</sup>Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walifahamu ya kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtia nguvuni, lakini waliogopa umati wa watu. Basi, wakamwacha wakaenda zao.
<scripture passage="Mark 12:13" parsed="|Mark|12|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.13" />
<sup>13</sup>Basi, baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake.
<scripture passage="Mark 12:14" parsed="|Mark|12|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.14" />
<sup>14</sup>Wakamwendea, wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?"
<scripture passage="Mark 12:15" parsed="|Mark|12|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.15" />
<sup>15</sup>Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, "Mbona mnanijaribu? Nionyesheni sarafu."
<scripture passage="Mark 12:16" parsed="|Mark|12|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.16" />
<sup>16</sup>Wakamwonyesha. Naye akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?" Wakamjibu, "Ni ya Kaisari."
<scripture passage="Mark 12:17" parsed="|Mark|12|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.17" />
<sup>17</sup>Basi, Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yake Mungu." Wakashangazwa sana naye.
<scripture passage="Mark 12:18" parsed="|Mark|12|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.18" />
<sup>18</sup>Masadukayo wasemao kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza,
<scripture passage="Mark 12:19" parsed="|Mark|12|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.19" />
<sup>19</sup>"Mwalimu, Mose alituagiza hivi: `Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane amzalie watoto ndugu yake marehemu.`
<scripture passage="Mark 12:20" parsed="|Mark|12|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.20" />
<sup>20</sup>Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
<scripture passage="Mark 12:21" parsed="|Mark|12|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.21" />
<sup>21</sup>Ndugu wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu hali kadhalika.
<scripture passage="Mark 12:22" parsed="|Mark|12|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.22" />
<sup>22</sup>Wote saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa.
<scripture passage="Mark 12:23" parsed="|Mark|12|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.23" />
<sup>23</sup>Basi, siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa."
<scripture passage="Mark 12:24" parsed="|Mark|12|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.24" />
<sup>24</sup>Yesu akawaambia, "Ninyi mmekosea sana, kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu.
<scripture passage="Mark 12:25" parsed="|Mark|12|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.25" />
<sup>25</sup>Maana wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni.
<scripture passage="Mark 12:26" parsed="|Mark|12|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.26" />
<sup>26</sup>Lakini kuhusu kufufuliwa kwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemu inayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto? Mungu alimwambia Mose, `Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.`
<scripture passage="Mark 12:27" parsed="|Mark|12|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.27" />
<sup>27</sup>Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Ninyi mmekosea sana!"
<scripture passage="Mark 12:28" parsed="|Mark|12|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.28" />
<sup>28</sup>Mmojawapo wa walimu wa Sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza, "Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?"
<scripture passage="Mark 12:29" parsed="|Mark|12|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.29" />
<sup>29</sup>Yesu akamjibu, "Ya kwanza ndiyo hii: `Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake Bwana.
<scripture passage="Mark 12:30" parsed="|Mark|12|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.30" />
<sup>30</sup>Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.`
<scripture passage="Mark 12:31" parsed="|Mark|12|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.31" />
<sup>31</sup>Na ya pili ndiyo hii: `Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.` Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi."
<scripture passage="Mark 12:32" parsed="|Mark|12|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.32" />
<sup>32</sup>Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia, "Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
<scripture passage="Mark 12:33" parsed="|Mark|12|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.33" />
<sup>33</sup>Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko dhabihu na sadaka zote za kuteketezwa."
<scripture passage="Mark 12:34" parsed="|Mark|12|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.34" />
<sup>34</sup>Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwa ujasiri, akamwambia, "Wewe huko mbali na Ufalme wa Mungu." Baada ya hayo, hakuna mtu aliyethubutu tena kumwuliza kitu.
<scripture passage="Mark 12:35" parsed="|Mark|12|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.35" />
<sup>35</sup>Wakati Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
<scripture passage="Mark 12:36" parsed="|Mark|12|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.36" />
<sup>36</sup>Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: `Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako."`
<scripture passage="Mark 12:37" parsed="|Mark|12|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.37" />
<sup>37</sup>"Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?" Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
<scripture passage="Mark 12:38" parsed="|Mark|12|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.38" />
<sup>38</sup>Katika mafundisho yake, Yesu alisema, "Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi,
<scripture passage="Mark 12:39" parsed="|Mark|12|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.39" />
<sup>39</sup>na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
<scripture passage="Mark 12:40" parsed="|Mark|12|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.40" />
<sup>40</sup>Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!"
<scripture passage="Mark 12:41" parsed="|Mark|12|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.41" />
<sup>41</sup>Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina ya Hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi.
<scripture passage="Mark 12:42" parsed="|Mark|12|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.42" />
<sup>42</sup>Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha.
<scripture passage="Mark 12:43" parsed="|Mark|12|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.43" />
<sup>43</sup>Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, "Kweli nawaambieni, huyu mama mjane maskini ametoa zaidi kuliko wengine wote waliotia fedha katika sanduku la hazina.
<scripture passage="Mark 12:44" parsed="|Mark|12|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.12.44" />
<sup>44</sup>Maana wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi."
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 13" progress="18.33%" prev="Mark.12" next="Mark.14" id="Mark.13">
<h3 id="Mark.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Mark.13-p1">
<scripture passage="Mark 13:1" parsed="|Mark|13|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, "Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!"
<scripture passage="Mark 13:2" parsed="|Mark|13|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.2" />
<sup>2</sup>Yesu akamwambia, "Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa."
<scripture passage="Mark 13:3" parsed="|Mark|13|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.3" />
<sup>3</sup>Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
<scripture passage="Mark 13:4" parsed="|Mark|13|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.4" />
<sup>4</sup>"Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?"
<scripture passage="Mark 13:5" parsed="|Mark|13|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.5" />
<sup>5</sup>Yesu akaanza kuwaambia, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
<scripture passage="Mark 13:6" parsed="|Mark|13|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.6" />
<sup>6</sup>Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, `Mimi ndiye!` nao watawapotosha watu wengi.
<scripture passage="Mark 13:7" parsed="|Mark|13|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.7" />
<sup>7</sup>Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
<scripture passage="Mark 13:8" parsed="|Mark|13|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.8" />
<sup>8</sup>Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
<scripture passage="Mark 13:9" parsed="|Mark|13|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.9" />
<sup>9</sup>"Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
<scripture passage="Mark 13:10" parsed="|Mark|13|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.10" />
<sup>10</sup>Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
<scripture passage="Mark 13:11" parsed="|Mark|13|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.11" />
<sup>11</sup>Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Mark 13:12" parsed="|Mark|13|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.12" />
<sup>12</sup>Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
<scripture passage="Mark 13:13" parsed="|Mark|13|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.13" />
<sup>13</sup>Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
<scripture passage="Mark 13:14" parsed="|Mark|13|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.14" />
<sup>14</sup>"Mtakapoona `Chukizo Haribifu` limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
<scripture passage="Mark 13:15" parsed="|Mark|13|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.15" />
<sup>15</sup>Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
<scripture passage="Mark 13:16" parsed="|Mark|13|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.16" />
<sup>16</sup>Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
<scripture passage="Mark 13:17" parsed="|Mark|13|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.17" />
<sup>17</sup>Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
<scripture passage="Mark 13:18" parsed="|Mark|13|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.18" />
<sup>18</sup>Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
<scripture passage="Mark 13:19" parsed="|Mark|13|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.19" />
<sup>19</sup>Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
<scripture passage="Mark 13:20" parsed="|Mark|13|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.20" />
<sup>20</sup>Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
<scripture passage="Mark 13:21" parsed="|Mark|13|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.21" />
<sup>21</sup>"Basi mtu akiwaambieni, `Tazama, Kristo yupo hapa!` au `Yupo pale!` msimsadiki.
<scripture passage="Mark 13:22" parsed="|Mark|13|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.22" />
<sup>22</sup>Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
<scripture passage="Mark 13:23" parsed="|Mark|13|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.23" />
<sup>23</sup>Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
<scripture passage="Mark 13:24" parsed="|Mark|13|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.24" />
<sup>24</sup>"Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
<scripture passage="Mark 13:25" parsed="|Mark|13|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.25" />
<sup>25</sup>Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
<scripture passage="Mark 13:26" parsed="|Mark|13|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.26" />
<sup>26</sup>Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
<scripture passage="Mark 13:27" parsed="|Mark|13|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.27" />
<sup>27</sup>Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
<scripture passage="Mark 13:28" parsed="|Mark|13|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.28" />
<sup>28</sup>"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
<scripture passage="Mark 13:29" parsed="|Mark|13|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.29" />
<sup>29</sup>Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
<scripture passage="Mark 13:30" parsed="|Mark|13|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.30" />
<sup>30</sup>Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
<scripture passage="Mark 13:31" parsed="|Mark|13|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.31" />
<sup>31</sup>Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
<scripture passage="Mark 13:32" parsed="|Mark|13|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.32" />
<sup>32</sup>"Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
<scripture passage="Mark 13:33" parsed="|Mark|13|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.33" />
<sup>33</sup>Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
<scripture passage="Mark 13:34" parsed="|Mark|13|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.34" />
<sup>34</sup>Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
<scripture passage="Mark 13:35" parsed="|Mark|13|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.35" />
<sup>35</sup>Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
<scripture passage="Mark 13:36" parsed="|Mark|13|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.36" />
<sup>36</sup>Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
<scripture passage="Mark 13:37" parsed="|Mark|13|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.13.37" />
<sup>37</sup>Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!"
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 14" progress="18.74%" prev="Mark.13" next="Mark.15" id="Mark.14">
<h3 id="Mark.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Mark.14-p1">
<scripture passage="Mark 14:1" parsed="|Mark|14|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.1" />
<sup>1</sup>Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
<scripture passage="Mark 14:2" parsed="|Mark|14|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.2" />
<sup>2</sup>Lakini walisema, "Tusimtie nguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia."
<scripture passage="Mark 14:3" parsed="|Mark|14|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.3" />
<sup>3</sup>Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
<scripture passage="Mark 14:4" parsed="|Mark|14|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.4" />
<sup>4</sup>Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika wakajisemea, "Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
<scripture passage="Mark 14:5" parsed="|Mark|14|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.5" />
<sup>5</sup>Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha denari mia tatu, wakapewa maskini!" Wakamkemea huyo mama.
<scripture passage="Mark 14:6" parsed="|Mark|14|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.6" />
<sup>6</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Mwacheni; kwa nini mnamsumbua? Amenitendea jambo jema.
<scripture passage="Mark 14:7" parsed="|Mark|14|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.7" />
<sup>7</sup>Maskini mnao daima pamoja nanyi; mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
<scripture passage="Mark 14:8" parsed="|Mark|14|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.8" />
<sup>8</sup>Yeye amefanya alivyoweza; ameupaka mwili wangu marashi kuutayarisha kwa maziko.
<scripture passage="Mark 14:9" parsed="|Mark|14|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.9" />
<sup>9</sup>Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa ajili ya kumkumbuka."
<scripture passage="Mark 14:10" parsed="|Mark|14|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.10" />
<sup>10</sup>Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alienda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
<scripture passage="Mark 14:11" parsed="|Mark|14|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.11" />
<sup>11</sup>Makuhani wakuu waliposikia habari hiyo, walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Basi, Yuda akaanza kutafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.
<scripture passage="Mark 14:12" parsed="|Mark|14|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.12" />
<sup>12</sup>Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, "Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?"
<scripture passage="Mark 14:13" parsed="|Mark|14|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.13" />
<sup>13</sup>Basi Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake akiwaambia, "Nendeni mjini, nanyi mtakutana na mtu anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni
<scripture passage="Mark 14:14" parsed="|Mark|14|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.14" />
<sup>14</sup>mpaka katika nyumba atakayoingia, mkamwambie mwenye nyumba, `Mwalimu anasema: wapi chumba changu ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?`
<scripture passage="Mark 14:15" parsed="|Mark|14|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.15" />
<sup>15</sup>Naye atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo."
<scripture passage="Mark 14:16" parsed="|Mark|14|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.16" />
<sup>16</sup>Wanafunzi wakaondoka, wakaenda mjini, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Wakaandaa karamu ya Pasaka.
<scripture passage="Mark 14:17" parsed="|Mark|14|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.17" />
<sup>17</sup>Ilipokuwa jioni, Yesu alifika pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
<scripture passage="Mark 14:18" parsed="|Mark|14|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.18" />
<sup>18</sup>Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, "Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti."
<scripture passage="Mark 14:19" parsed="|Mark|14|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.19" />
<sup>19</sup>Hapo wanafunzi wake wakaanza kuhuzunika, wakamwuliza mmojammoja, "Je, ni mimi?"
<scripture passage="Mark 14:20" parsed="|Mark|14|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.20" />
<sup>20</sup>Yesu akawaambia, "Ni mmoja wenu ninyi kumi na wawili, anayechovya mkate pamoja nami katika bakuli.
<scripture passage="Mark 14:21" parsed="|Mark|14|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.21" />
<sup>21</sup>Kweli Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yanavyosema juu yake; lakini, ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa!"
<scripture passage="Mark 14:22" parsed="|Mark|14|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.22" />
<sup>22</sup>Walipokuwa wanakula, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake akisema, "Twaeni; huu ni mwili wangu."
<scripture passage="Mark 14:23" parsed="|Mark|14|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.23" />
<sup>23</sup>Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa; nao wote wakanywa katika kikombe hicho.
<scripture passage="Mark 14:24" parsed="|Mark|14|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.24" />
<sup>24</sup>Akawaambia, "Hii ni damu yangu inayothibitisha agano la Mungu, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi.
<scripture passage="Mark 14:25" parsed="|Mark|14|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.25" />
<sup>25</sup>Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upya katika Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Mark 14:26" parsed="|Mark|14|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.26" />
<sup>26</sup>Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
<scripture passage="Mark 14:27" parsed="|Mark|14|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.27" />
<sup>27</sup>Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami; maana Maandiko Matakatifu yasema: `Nitampiga mchungaji nao kondoo watatawanyika.`
<scripture passage="Mark 14:28" parsed="|Mark|14|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.28" />
<sup>28</sup>Lakini nikisha fufuka, nitawatangulieni kule Galilaya."
<scripture passage="Mark 14:29" parsed="|Mark|14|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.29" />
<sup>29</sup>Petro akamwambia "Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakukana kamwe!"
<scripture passage="Mark 14:30" parsed="|Mark|14|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.30" />
<sup>30</sup>Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu."
<scripture passage="Mark 14:31" parsed="|Mark|14|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.31" />
<sup>31</sup>Lakini Petro akasisitiza, "Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakuacha kamwe." Wanafunzi wote pia wakasema vivyo hivyo.
<scripture passage="Mark 14:32" parsed="|Mark|14|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakafika katika bustani iitwayo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa wakati mimi nasali."
<scripture passage="Mark 14:33" parsed="|Mark|14|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.33" />
<sup>33</sup>Kisha akawachukua Petro, Yakobo na Yohane; akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.
<scripture passage="Mark 14:34" parsed="|Mark|14|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.34" />
<sup>34</sup>Akawaambia, "Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe."
<scripture passage="Mark 14:35" parsed="|Mark|14|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.35" />
<sup>35</sup>Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi, akasali kwamba, kama ingewezekana, asiipitie saa hiyo ya mateso.
<scripture passage="Mark 14:36" parsed="|Mark|14|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.36" />
<sup>36</sup>Akasema, "Baba yangu, kwako mambo yote yanawezekana. Uniondolee kikombe hiki; lakini isiwe kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe." ic\is Bustani ya Gethsemane (Marko 14:32)\ie
<scripture passage="Mark 14:37" parsed="|Mark|14|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.37" />
<sup>37</sup>Kisha akarudi kwa wanafunzi wale watatu, akawakuta wamelala. Basi, akamwuliza Petro, "Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?"
<scripture passage="Mark 14:38" parsed="|Mark|14|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.38" />
<sup>38</sup>Kisha akawaambia, "Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
<scripture passage="Mark 14:39" parsed="|Mark|14|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.39" />
<sup>39</sup>Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale.
<scripture passage="Mark 14:40" parsed="|Mark|14|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.40" />
<sup>40</sup>Kisha akarudi tena, akawakuta wamelala. Macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Hawakujua la kumjibu.
<scripture passage="Mark 14:41" parsed="|Mark|14|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.41" />
<sup>41</sup>Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, "Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
<scripture passage="Mark 14:42" parsed="|Mark|14|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.42" />
<sup>42</sup>Amkeni, twendeni zetu. Tazameni, yule atakayenisaliti amekaribia."
<scripture passage="Mark 14:43" parsed="|Mark|14|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.43" />
<sup>43</sup>Yesu alipokuwa bado anasema, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee.
<scripture passage="Mark 14:44" parsed="|Mark|14|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.44" />
<sup>44</sup>Msaliti Yuda alikuwa amewapa ishara: "Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni, mkampeleke chini ya ulinzi."
<scripture passage="Mark 14:45" parsed="|Mark|14|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.45" />
<sup>45</sup>Yuda alipofika tu, alimwendea Yesu moja kwa moja, akasema, "Mwalimu!" Kisha akambusu.
<scripture passage="Mark 14:46" parsed="|Mark|14|46|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.46" />
<sup>46</sup>Basi, hao watu wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
<scripture passage="Mark 14:47" parsed="|Mark|14|47|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.47" />
<sup>47</sup>Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
<scripture passage="Mark 14:48" parsed="|Mark|14|48|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.48" />
<sup>48</sup>Yesu akawaambia, "Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang`anyi?
<scripture passage="Mark 14:49" parsed="|Mark|14|49|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.49" />
<sup>49</sup>Kila siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini sasa lazima Maandiko Matakatifu yatimie."
<scripture passage="Mark 14:50" parsed="|Mark|14|50|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.50" />
<sup>50</sup>Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
<scripture passage="Mark 14:51" parsed="|Mark|14|51|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.51" />
<sup>51</sup>Kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata.
<scripture passage="Mark 14:52" parsed="|Mark|14|52|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.52" />
<sup>52</sup>Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ile shuka, akakimbia uchi.
<scripture passage="Mark 14:53" parsed="|Mark|14|53|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.53" />
<sup>53</sup>Basi, wakampeleka Yesu kwa Kuhani Mkuu ambapo makuhani wakuu wote, wazee na walimu wa Sheria walikuwa wamekutanika.
<scripture passage="Mark 14:54" parsed="|Mark|14|54|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.54" />
<sup>54</sup>Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ya wa Kuhani Mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
<scripture passage="Mark 14:55" parsed="|Mark|14|55|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.55" />
<sup>55</sup>Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakupata.
<scripture passage="Mark 14:56" parsed="|Mark|14|56|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.56" />
<sup>56</sup>Watu wengi walitoa ushahidi wa uongo juu ya Yesu, lakini ushahidi wao haukupatana.
<scripture passage="Mark 14:57" parsed="|Mark|14|57|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.57" />
<sup>57</sup>Kisha wengine walisimama, wakatoa ushahidi wa uongo wakisema:
<scripture passage="Mark 14:58" parsed="|Mark|14|58|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.58" />
<sup>58</sup>"Tulimsikia mtu huyu akisema, `Nitaliharibu Hekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono."`
<scripture passage="Mark 14:59" parsed="|Mark|14|59|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.59" />
<sup>59</sup>Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukupatana.
<scripture passage="Mark 14:60" parsed="|Mark|14|60|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.60" />
<sup>60</sup>Basi, Kuhani Mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, "Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?"
<scripture passage="Mark 14:61" parsed="|Mark|14|61|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.61" />
<sup>61</sup>Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, "Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?"
<scripture passage="Mark 14:62" parsed="|Mark|14|62|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.62" />
<sup>62</sup>Yesu akajibu, "Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenyezi, akija katika mawingu ya mbinguni."
<scripture passage="Mark 14:63" parsed="|Mark|14|63|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.63" />
<sup>63</sup>Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema, "Tuna haja gani tena ya mashahidi?
<scripture passage="Mark 14:64" parsed="|Mark|14|64|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.64" />
<sup>64</sup>Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?" Wote wakaamua kwamba anastahili kuuawa.
<scripture passage="Mark 14:65" parsed="|Mark|14|65|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.65" />
<sup>65</sup>Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, "Bashiri ni nani aliyekupiga!" Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
<scripture passage="Mark 14:66" parsed="|Mark|14|66|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.66" />
<sup>66</sup>Petro alipokuwa bado chini ukumbini, mmoja wa wajakazi wa kuhani Mkuu alikuja.
<scripture passage="Mark 14:67" parsed="|Mark|14|67|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.67" />
<sup>67</sup>Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama, akamwambia, "Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti."
<scripture passage="Mark 14:68" parsed="|Mark|14|68|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.68" />
<sup>68</sup>Lakini Petro akakana, "Sijui, wala sielewi unayosema!" Kisha Petro akaondoka, akaenda nje uani. Hapo jogoo akawika.
<scripture passage="Mark 14:69" parsed="|Mark|14|69|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.69" />
<sup>69</sup>Yule mjakazi alipomwona tena Petro, akaanza tena kuwaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, "Mtu huyu ni mmoja wao."
<scripture passage="Mark 14:70" parsed="|Mark|14|70|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.70" />
<sup>70</sup>Petro akakana tena. Baadaye kidogo, watu waliokuwa wamesimama hapo wakamwambia Petro, "Hakika wewe ni mmoja wao, maana wewe ni Mgalilaya."
<scripture passage="Mark 14:71" parsed="|Mark|14|71|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.71" />
<sup>71</sup>Lakini Petro akaanza kulaani na kuapa akisema, "Mimi simjui mtu huyu mnayesema habari zake."
<scripture passage="Mark 14:72" parsed="|Mark|14|72|0|0" osisRef="Bible:Mark.14.72" />
<sup>72</sup>Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: "Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu." Petro akabubujika machozi.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 15" progress="19.58%" prev="Mark.14" next="Mark.16" id="Mark.15">
<h3 id="Mark.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Mark.15-p1">
<scripture passage="Mark 15:1" parsed="|Mark|15|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.1" />
<sup>1</sup>Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
<scripture passage="Mark 15:2" parsed="|Mark|15|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.2" />
<sup>2</sup>Pilato akamwuliza Yesu, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akajibu, "Wewe umesema."
<scripture passage="Mark 15:3" parsed="|Mark|15|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.3" />
<sup>3</sup>Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
<scripture passage="Mark 15:4" parsed="|Mark|15|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.4" />
<sup>4</sup>Pilato akamwuliza tena Yesu, "Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako."
<scripture passage="Mark 15:5" parsed="|Mark|15|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.5" />
<sup>5</sup>Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
<scripture passage="Mark 15:6" parsed="|Mark|15|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.6" />
<sup>6</sup>Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
<scripture passage="Mark 15:7" parsed="|Mark|15|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.7" />
<sup>7</sup>Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
<scripture passage="Mark 15:8" parsed="|Mark|15|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.8" />
<sup>8</sup>Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
<scripture passage="Mark 15:9" parsed="|Mark|15|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.9" />
<sup>9</sup>Pilato akawauliza, "Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?"
<scripture passage="Mark 15:10" parsed="|Mark|15|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.10" />
<sup>10</sup>Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
<scripture passage="Mark 15:11" parsed="|Mark|15|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.11" />
<sup>11</sup>Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
<scripture passage="Mark 15:12" parsed="|Mark|15|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.12" />
<sup>12</sup>Pilato akawauliza tena, "Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?"
<scripture passage="Mark 15:13" parsed="|Mark|15|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.13" />
<sup>13</sup>Watu wote wakapaaza sauti tena: "Msulubishe!"
<scripture passage="Mark 15:14" parsed="|Mark|15|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.14" />
<sup>14</sup>Lakini Pilato akawauliza, "Kwa nini! Amefanya kosa gani?" Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, "Msulubishe!"
<scripture passage="Mark 15:15" parsed="|Mark|15|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.15" />
<sup>15</sup>Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
<scripture passage="Mark 15:16" parsed="|Mark|15|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.16" />
<sup>16</sup>Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
<scripture passage="Mark 15:17" parsed="|Mark|15|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.17" />
<sup>17</sup>Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
<scripture passage="Mark 15:18" parsed="|Mark|15|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.18" />
<sup>18</sup>Wakaanza kumsalimu, "Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!"
<scripture passage="Mark 15:19" parsed="|Mark|15|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.19" />
<sup>19</sup>Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
<scripture passage="Mark 15:20" parsed="|Mark|15|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.20" />
<sup>20</sup>Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
<scripture passage="Mark 15:21" parsed="|Mark|15|21|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.21" />
<sup>21</sup>Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
<scripture passage="Mark 15:22" parsed="|Mark|15|22|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.22" />
<sup>22</sup>Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la Kichwa."
<scripture passage="Mark 15:23" parsed="|Mark|15|23|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.23" />
<sup>23</sup>Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
<scripture passage="Mark 15:24" parsed="|Mark|15|24|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.24" />
<sup>24</sup>Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
<scripture passage="Mark 15:25" parsed="|Mark|15|25|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.25" />
<sup>25</sup>Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
<scripture passage="Mark 15:26" parsed="|Mark|15|26|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.26" />
<sup>26</sup>Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: "Mfalme wa Wayahudi."
<scripture passage="Mark 15:27" parsed="|Mark|15|27|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.27" />
<sup>27</sup>Pamoja naye waliwasulubisha wanyang`anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.<i>fh</i> Matakatifu yanayosema, "Aliwekwa kundi moja na waovu."
<scripture passage="Mark 15:28" parsed="|Mark|15|28|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.28" />
<sup>28</sup>missing
<scripture passage="Mark 15:29" parsed="|Mark|15|29|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.29" />
<sup>29</sup>Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, "Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
<scripture passage="Mark 15:30" parsed="|Mark|15|30|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.30" />
<sup>30</sup>Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!"
<scripture passage="Mark 15:31" parsed="|Mark|15|31|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.31" />
<sup>31</sup>Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
<scripture passage="Mark 15:32" parsed="|Mark|15|32|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.32" />
<sup>32</sup>Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini." Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
<scripture passage="Mark 15:33" parsed="|Mark|15|33|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.33" />
<sup>33</sup>Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
<scripture passage="Mark 15:34" parsed="|Mark|15|34|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.34" />
<sup>34</sup>Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
<scripture passage="Mark 15:35" parsed="|Mark|15|35|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.35" />
<sup>35</sup>Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, "Sikiliza! Anamwita Eliya!"
<scripture passage="Mark 15:36" parsed="|Mark|15|36|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.36" />
<sup>36</sup>Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, "Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!"
<scripture passage="Mark 15:37" parsed="|Mark|15|37|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.37" />
<sup>37</sup>Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
<scripture passage="Mark 15:38" parsed="|Mark|15|38|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.38" />
<sup>38</sup>Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
<scripture passage="Mark 15:39" parsed="|Mark|15|39|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.39" />
<sup>39</sup>Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, "Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!"
<scripture passage="Mark 15:40" parsed="|Mark|15|40|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.40" />
<sup>40</sup>Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
<scripture passage="Mark 15:41" parsed="|Mark|15|41|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.41" />
<sup>41</sup>Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
<scripture passage="Mark 15:42" parsed="|Mark|15|42|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.42" />
<sup>42</sup>Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
<scripture passage="Mark 15:43" parsed="|Mark|15|43|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.43" />
<sup>43</sup>Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
<scripture passage="Mark 15:44" parsed="|Mark|15|44|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.44" />
<sup>44</sup>Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
<scripture passage="Mark 15:45" parsed="|Mark|15|45|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.45" />
<sup>45</sup>Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
<scripture passage="Mark 15:46" parsed="|Mark|15|46|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.46" />
<sup>46</sup>Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
<scripture passage="Mark 15:47" parsed="|Mark|15|47|0|0" osisRef="Bible:Mark.15.47" />
<sup>47</sup>Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.
</p>
</div3>

<div3 title="Mark 16" progress="20.09%" prev="Mark.15" next="Luke" id="Mark.16">
<h3 id="Mark.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Mark.16-p1">
<scripture passage="Mark 16:1" parsed="|Mark|16|1|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.1" />
<sup>1</sup>Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.
<scripture passage="Mark 16:2" parsed="|Mark|16|2|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.2" />
<sup>2</sup>Basi, alfajiri na mapema siku ya Jumapili, jua lilipoanza kuchomoza, walienda kaburini.
<scripture passage="Mark 16:3" parsed="|Mark|16|3|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.3" />
<sup>3</sup>Nao wakawa wanaambiana, "Nani atakayetuondolea lile jiwe mlangoni mwa kaburi?"
<scripture passage="Mark 16:4" parsed="|Mark|16|4|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.4" />
<sup>4</sup>Lakini walipotazama, waliona jiwe limekwisha ondolewa. (Nalo lilikuwa kubwa mno.)
<scripture passage="Mark 16:5" parsed="|Mark|16|5|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.5" />
<sup>5</sup>Walipoingia kaburini, walimwona kijana mmoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wa kulia; wakashangaa sana.
<scripture passage="Mark 16:6" parsed="|Mark|16|6|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.6" />
<sup>6</sup>Lakini huyo kijana akawaambia, "Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwa wamemlaza.
<scripture passage="Mark 16:7" parsed="|Mark|16|7|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.7" />
<sup>7</sup>Nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro ya kwamba anawatangulieni kule Galilaya. Huko mtamwona kama alivyowaambieni."
<scripture passage="Mark 16:8" parsed="|Mark|16|8|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.8" />
<sup>8</sup>Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. [[[
<scripture passage="Mark 16:9" parsed="|Mark|16|9|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.9" />
<sup>9</sup>Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionyesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo saba.
<scripture passage="Mark 16:10" parsed="|Mark|16|10|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.10" />
<sup>10</sup>Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia.
<scripture passage="Mark 16:11" parsed="|Mark|16|11|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.11" />
<sup>11</sup>Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini.
<scripture passage="Mark 16:12" parsed="|Mark|16|12|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.12" />
<sup>12</sup>Baadaye Yesu aliwatokea wanafunzi wawili akiwa na sura nyingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda shambani.
<scripture passage="Mark 16:13" parsed="|Mark|16|13|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.13" />
<sup>13</sup>Nao pia wakaenda wakawaambia wenzao. Hata hivyo hawakuamini.
<scripture passage="Mark 16:14" parsed="|Mark|16|14|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.14" />
<sup>14</sup>Mwishowe, Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka.
<scripture passage="Mark 16:15" parsed="|Mark|16|15|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.15" />
<sup>15</sup>Basi, akawaambia, "Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu.
<scripture passage="Mark 16:16" parsed="|Mark|16|16|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.16" />
<sup>16</sup>Anayeamini na kubatizwa ataokolewa; asiyeamini atahukumiwa.
<scripture passage="Mark 16:17" parsed="|Mark|16|17|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.17" />
<sup>17</sup>Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.
<scripture passage="Mark 16:18" parsed="|Mark|16|18|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.18" />
<sup>18</sup>Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona."
<scripture passage="Mark 16:19" parsed="|Mark|16|19|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.19" />
<sup>19</sup>Basi, Bwana Yesu alipokwisha sema nao, akachukuliwa mbinguni, akaketi upande wa kulia wa Mungu.
<scripture passage="Mark 16:20" parsed="|Mark|16|20|0|0" osisRef="Bible:Mark.16.20" />
<sup>20</sup>Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao.]<i>fi</i>
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Luke" progress="20.32%" prev="Mark.16" next="Luke.1" id="Luke">
<h2 id="Luke-p0.1">Luke</h2>

<div3 title="Luke 1" progress="20.33%" prev="Luke" next="Luke.2" id="Luke.1">
<h3 id="Luke.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Luke.1-p1">
<scripture passage="Luke 1:1" parsed="|Luke|1|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.1" />
<sup>1</sup>Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu.
<scripture passage="Luke 1:2" parsed="|Luke|1|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.2" />
<sup>2</sup>Waliandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo.
<scripture passage="Luke 1:3" parsed="|Luke|1|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.3" />
<sup>3</sup>Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,
<scripture passage="Luke 1:4" parsed="|Luke|1|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.4" />
<sup>4</sup>ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa.
<scripture passage="Luke 1:5" parsed="|Luke|1|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.5" />
<sup>5</sup>Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
<scripture passage="Luke 1:6" parsed="|Luke|1|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.6" />
<sup>6</sup>Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
<scripture passage="Luke 1:7" parsed="|Luke|1|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.7" />
<sup>7</sup>Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana.
<scripture passage="Luke 1:8" parsed="|Luke|1|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.8" />
<sup>8</sup>Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu,
<scripture passage="Luke 1:9" parsed="|Luke|1|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.9" />
<sup>9</sup>Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani.
<scripture passage="Luke 1:10" parsed="|Luke|1|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.10" />
<sup>10</sup>Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani.
<scripture passage="Luke 1:11" parsed="|Luke|1|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.11" />
<sup>11</sup>Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.
<scripture passage="Luke 1:12" parsed="|Luke|1|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.12" />
<sup>12</sup>Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
<scripture passage="Luke 1:13" parsed="|Luke|1|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.13" />
<sup>13</sup>Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.
<scripture passage="Luke 1:14" parsed="|Luke|1|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.14" />
<sup>14</sup>Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake.
<scripture passage="Luke 1:15" parsed="|Luke|1|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.15" />
<sup>15</sup>Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
<scripture passage="Luke 1:16" parsed="|Luke|1|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.16" />
<sup>16</sup>Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao.
<scripture passage="Luke 1:17" parsed="|Luke|1|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.17" />
<sup>17</sup>Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake."
<scripture passage="Luke 1:18" parsed="|Luke|1|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.18" />
<sup>18</sup>Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu."
<scripture passage="Luke 1:19" parsed="|Luke|1|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.19" />
<sup>19</sup>Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema.
<scripture passage="Luke 1:20" parsed="|Luke|1|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.20" />
<sup>20</sup>Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia."
<scripture passage="Luke 1:21" parsed="|Luke|1|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.21" />
<sup>21</sup>Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.
<scripture passage="Luke 1:22" parsed="|Luke|1|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.22" />
<sup>22</sup>Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
<scripture passage="Luke 1:23" parsed="|Luke|1|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.23" />
<sup>23</sup>Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani.
<scripture passage="Luke 1:24" parsed="|Luke|1|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.24" />
<sup>24</sup>Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema:
<scripture passage="Luke 1:25" parsed="|Luke|1|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.25" />
<sup>25</sup>"Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu."
<scripture passage="Luke 1:26" parsed="|Luke|1|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.26" />
<sup>26</sup>Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya,
<scripture passage="Luke 1:27" parsed="|Luke|1|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.27" />
<sup>27</sup>kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi.
<scripture passage="Luke 1:28" parsed="|Luke|1|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.28" />
<sup>28</sup>Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe."
<scripture passage="Luke 1:29" parsed="|Luke|1|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.29" />
<sup>29</sup>Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini?
<scripture passage="Luke 1:30" parsed="|Luke|1|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.30" />
<sup>30</sup>Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.
<scripture passage="Luke 1:31" parsed="|Luke|1|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.31" />
<sup>31</sup>Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu.
<scripture passage="Luke 1:32" parsed="|Luke|1|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.32" />
<sup>32</sup>Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.
<scripture passage="Luke 1:33" parsed="|Luke|1|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.33" />
<sup>33</sup>Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho."
<scripture passage="Luke 1:34" parsed="|Luke|1|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.34" />
<sup>34</sup>Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?"
<scripture passage="Luke 1:35" parsed="|Luke|1|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.35" />
<sup>35</sup>Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.
<scripture passage="Luke 1:36" parsed="|Luke|1|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.36" />
<sup>36</sup>Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa.
<scripture passage="Luke 1:37" parsed="|Luke|1|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.37" />
<sup>37</sup>Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu."
<scripture passage="Luke 1:38" parsed="|Luke|1|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.38" />
<sup>38</sup>Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake.
<scripture passage="Luke 1:39" parsed="|Luke|1|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.39" />
<sup>39</sup>Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yuda.
<scripture passage="Luke 1:40" parsed="|Luke|1|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.40" />
<sup>40</sup>Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti.
<scripture passage="Luke 1:41" parsed="|Luke|1|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.41" />
<sup>41</sup>Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu,
<scripture passage="Luke 1:42" parsed="|Luke|1|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.42" />
<sup>42</sup>akasema kwa sauti kubwa, "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.
<scripture passage="Luke 1:43" parsed="|Luke|1|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.43" />
<sup>43</sup>Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
<scripture passage="Luke 1:44" parsed="|Luke|1|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.44" />
<sup>44</sup>Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
<scripture passage="Luke 1:45" parsed="|Luke|1|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.45" />
<sup>45</sup>Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokwambia."
<scripture passage="Luke 1:46" parsed="|Luke|1|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.46" />
<sup>46</sup>Naye Maria akasema,
<scripture passage="Luke 1:47" parsed="|Luke|1|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.47" />
<sup>47</sup>"Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
<scripture passage="Luke 1:48" parsed="|Luke|1|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.48" />
<sup>48</sup>Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
<scripture passage="Luke 1:49" parsed="|Luke|1|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.49" />
<sup>49</sup>Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu, jina lake ni takatifu.
<scripture passage="Luke 1:50" parsed="|Luke|1|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.50" />
<sup>50</sup>Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi.
<scripture passage="Luke 1:51" parsed="|Luke|1|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.51" />
<sup>51</sup>Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
<scripture passage="Luke 1:52" parsed="|Luke|1|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.52" />
<sup>52</sup>amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu.
<scripture passage="Luke 1:53" parsed="|Luke|1|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.53" />
<sup>53</sup>Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
<scripture passage="Luke 1:54" parsed="|Luke|1|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.54" />
<sup>54</sup>Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.
<scripture passage="Luke 1:55" parsed="|Luke|1|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.55" />
<sup>55</sup>Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele."
<scripture passage="Luke 1:56" parsed="|Luke|1|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.56" />
<sup>56</sup>Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.
<scripture passage="Luke 1:57" parsed="|Luke|1|57|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.57" />
<sup>57</sup>Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.
<scripture passage="Luke 1:58" parsed="|Luke|1|58|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.58" />
<sup>58</sup>Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.
<scripture passage="Luke 1:59" parsed="|Luke|1|59|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.59" />
<sup>59</sup>Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya.
<scripture passage="Luke 1:60" parsed="|Luke|1|60|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.60" />
<sup>60</sup>Lakini mama yake akasema, "La, sivyo, bali ataitwa Yohane."
<scripture passage="Luke 1:61" parsed="|Luke|1|61|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.61" />
<sup>61</sup>Wakamwambia, "Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?"
<scripture passage="Luke 1:62" parsed="|Luke|1|62|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.62" />
<sup>62</sup>Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.
<scripture passage="Luke 1:63" parsed="|Luke|1|63|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.63" />
<sup>63</sup>Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: "Yohane ndilo jina lake." Wote wakastaajabu.
<scripture passage="Luke 1:64" parsed="|Luke|1|64|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.64" />
<sup>64</sup>Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.
<scripture passage="Luke 1:65" parsed="|Luke|1|65|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.65" />
<sup>65</sup>Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
<scripture passage="Luke 1:66" parsed="|Luke|1|66|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.66" />
<sup>66</sup>Wote waliosikia mambo hayo waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: "Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?" Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.
<scripture passage="Luke 1:67" parsed="|Luke|1|67|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.67" />
<sup>67</sup>Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu:
<scripture passage="Luke 1:68" parsed="|Luke|1|68|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.68" />
<sup>68</sup>"Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.
<scripture passage="Luke 1:69" parsed="|Luke|1|69|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.69" />
<sup>69</sup>Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake.
<scripture passage="Luke 1:70" parsed="|Luke|1|70|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.70" />
<sup>70</sup>Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu,
<scripture passage="Luke 1:71" parsed="|Luke|1|71|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.71" />
<sup>71</sup>kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
<scripture passage="Luke 1:72" parsed="|Luke|1|72|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.72" />
<sup>72</sup>Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu.
<scripture passage="Luke 1:73" parsed="|Luke|1|73|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.73" />
<sup>73</sup>Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisi
<scripture passage="Luke 1:74" parsed="|Luke|1|74|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.74" />
<sup>74</sup>tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu,
<scripture passage="Luke 1:75" parsed="|Luke|1|75|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.75" />
<sup>75</sup>kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu.
<scripture passage="Luke 1:76" parsed="|Luke|1|76|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.76" />
<sup>76</sup>Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
<scripture passage="Luke 1:77" parsed="|Luke|1|77|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.77" />
<sup>77</sup>kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao.
<scripture passage="Luke 1:78" parsed="|Luke|1|78|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.78" />
<sup>78</sup>Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,
<scripture passage="Luke 1:79" parsed="|Luke|1|79|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.79" />
<sup>79</sup>na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani."
<scripture passage="Luke 1:80" parsed="|Luke|1|80|0|0" osisRef="Bible:Luke.1.80" />
<sup>80</sup>Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionyesha rasmi kwa watu wa Israeli.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 2" progress="21.10%" prev="Luke.1" next="Luke.3" id="Luke.2">
<h3 id="Luke.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Luke.2-p1">
<scripture passage="Luke 2:1" parsed="|Luke|2|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.1" />
<sup>1</sup>Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote chini ya utawala wake wajiandikishe.
<scripture passage="Luke 2:2" parsed="|Luke|2|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.2" />
<sup>2</sup>Kuandikishwa huku kulikuwa mara ya kwanza, wakati Kirenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria.
<scripture passage="Luke 2:3" parsed="|Luke|2|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.3" />
<sup>3</sup>Basi, wote waliohusika walikwenda kujiandikisha, kila mtu katika mji wake.
<scripture passage="Luke 2:4" parsed="|Luke|2|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.4" />
<sup>4</sup>Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya. Kwa kuwa alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yuda alikozaliwa Mfalme Daudi.
<scripture passage="Luke 2:5" parsed="|Luke|2|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.5" />
<sup>5</sup>Alikwenda kujiandikisha pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mja mzito.
<scripture passage="Luke 2:6" parsed="|Luke|2|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.6" />
<sup>6</sup>Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,
<scripture passage="Luke 2:7" parsed="|Luke|2|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.7" />
<sup>7</sup>akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
<scripture passage="Luke 2:8" parsed="|Luke|2|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.8" />
<sup>8</sup>Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.
<scripture passage="Luke 2:9" parsed="|Luke|2|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.9" />
<sup>9</sup>Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
<scripture passage="Luke 2:10" parsed="|Luke|2|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.10" />
<sup>10</sup>Malaika akawaambia, "Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kuu kwa watu wote.
<scripture passage="Luke 2:11" parsed="|Luke|2|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.11" />
<sup>11</sup>Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.
<scripture passage="Luke 2:12" parsed="|Luke|2|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.12" />
<sup>12</sup>Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini."
<scripture passage="Luke 2:13" parsed="|Luke|2|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.13" />
<sup>13</sup>Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema:
<scripture passage="Luke 2:14" parsed="|Luke|2|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.14" />
<sup>14</sup>"Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!"
<scripture passage="Luke 2:15" parsed="|Luke|2|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.15" />
<sup>15</sup>Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: "Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha."
<scripture passage="Luke 2:16" parsed="|Luke|2|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.16" />
<sup>16</sup>Basi, wakaenda mbio, wakamkuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga amelazwa horini.
<scripture passage="Luke 2:17" parsed="|Luke|2|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.17" />
<sup>17</sup>Hao wachungaji walipomwona mtoto huyo wakawajulisha wote habari waliyokuwa wamesikia juu yake.
<scripture passage="Luke 2:18" parsed="|Luke|2|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.18" />
<sup>18</sup>Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na wachungaji.
<scripture passage="Luke 2:19" parsed="|Luke|2|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.19" />
<sup>19</sup>Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake.
<scripture passage="Luke 2:20" parsed="|Luke|2|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.20" />
<sup>20</sup>Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
<scripture passage="Luke 2:21" parsed="|Luke|2|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.21" />
<sup>21</sup>Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
<scripture passage="Luke 2:22" parsed="|Luke|2|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.22" />
<sup>22</sup>Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana.
<scripture passage="Luke 2:23" parsed="|Luke|2|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.23" />
<sup>23</sup>Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana."
<scripture passage="Luke 2:24" parsed="|Luke|2|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.24" />
<sup>24</sup>Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana.
<scripture passage="Luke 2:25" parsed="|Luke|2|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.25" />
<sup>25</sup>Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.
<scripture passage="Luke 2:26" parsed="|Luke|2|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.26" />
<sup>26</sup>Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Masiha wa Bwana.
<scripture passage="Luke 2:27" parsed="|Luke|2|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.27" />
<sup>27</sup>Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria,
<scripture passage="Luke 2:28" parsed="|Luke|2|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.28" />
<sup>28</sup>Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu na kusema:
<scripture passage="Luke 2:29" parsed="|Luke|2|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.29" />
<sup>29</sup>"Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani.
<scripture passage="Luke 2:30" parsed="|Luke|2|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.30" />
<sup>30</sup>Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako,
<scripture passage="Luke 2:31" parsed="|Luke|2|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.31" />
<sup>31</sup>ambao umeutayarisha mbele ya watu wote:
<scripture passage="Luke 2:32" parsed="|Luke|2|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.32" />
<sup>32</sup>Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli."
<scripture passage="Luke 2:33" parsed="|Luke|2|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.33" />
<sup>33</sup>Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto.
<scripture passage="Luke 2:34" parsed="|Luke|2|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.34" />
<sup>34</sup>Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
<scripture passage="Luke 2:35" parsed="|Luke|2|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.35" />
<sup>35</sup>na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako."
<scripture passage="Luke 2:36" parsed="|Luke|2|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.36" />
<sup>36</sup>Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa.
<scripture passage="Luke 2:37" parsed="|Luke|2|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.37" />
<sup>37</sup>Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana.
<scripture passage="Luke 2:38" parsed="|Luke|2|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.38" />
<sup>38</sup>Saa hiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na akaeleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 2:39" parsed="|Luke|2|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.39" />
<sup>39</sup>Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya.
<scripture passage="Luke 2:40" parsed="|Luke|2|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.40" />
<sup>40</sup>Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa pamoja naye.
<scripture passage="Luke 2:41" parsed="|Luke|2|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.41" />
<sup>41</sup>Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka.
<scripture passage="Luke 2:42" parsed="|Luke|2|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.42" />
<sup>42</sup>Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi.
<scripture passage="Luke 2:43" parsed="|Luke|2|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.43" />
<sup>43</sup>Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari.
<scripture passage="Luke 2:44" parsed="|Luke|2|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.44" />
<sup>44</sup>Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
<scripture passage="Luke 2:45" parsed="|Luke|2|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.45" />
<sup>45</sup>Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta.
<scripture passage="Luke 2:46" parsed="|Luke|2|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.46" />
<sup>46</sup>Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
<scripture passage="Luke 2:47" parsed="|Luke|2|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.47" />
<sup>47</sup>Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima.
<scripture passage="Luke 2:48" parsed="|Luke|2|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.48" />
<sup>48</sup>Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, "Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni."
<scripture passage="Luke 2:49" parsed="|Luke|2|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.49" />
<sup>49</sup>Yeye akawajibu, "Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?"
<scripture passage="Luke 2:50" parsed="|Luke|2|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.50" />
<sup>50</sup>Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia.
<scripture passage="Luke 2:51" parsed="|Luke|2|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.51" />
<sup>51</sup>Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake.
<scripture passage="Luke 2:52" parsed="|Luke|2|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.2.52" />
<sup>52</sup>Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 3" progress="21.68%" prev="Luke.2" next="Luke.4" id="Luke.3">
<h3 id="Luke.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Luke.3-p1">
<scripture passage="Luke 3:1" parsed="|Luke|3|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.1" />
<sup>1</sup>Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
<scripture passage="Luke 3:2" parsed="|Luke|3|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.2" />
<sup>2</sup>na Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati huo ndipo neno la Mungu lilipomjia Yohane, mwana wa Zakariya, kule jangwani.
<scripture passage="Luke 3:3" parsed="|Luke|3|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.3" />
<sup>3</sup>Basi, Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto Yordani, akihubiri watu watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
<scripture passage="Luke 3:4" parsed="|Luke|3|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.4" />
<sup>4</sup>Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
<scripture passage="Luke 3:5" parsed="|Luke|3|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.5" />
<sup>5</sup>Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
<scripture passage="Luke 3:6" parsed="|Luke|3|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.6" />
<sup>6</sup>Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu."`
<scripture passage="Luke 3:7" parsed="|Luke|3|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.7" />
<sup>7</sup>Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
<scripture passage="Luke 3:8" parsed="|Luke|3|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.8" />
<sup>8</sup>Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: `Sisi ni watoto wa Abrahamu.` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
<scripture passage="Luke 3:9" parsed="|Luke|3|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.9" />
<sup>9</sup>Lakini, sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni."
<scripture passage="Luke 3:10" parsed="|Luke|3|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.10" />
<sup>10</sup>Umati wa watu ukamwuliza, "Tufanye nini basi?"
<scripture passage="Luke 3:11" parsed="|Luke|3|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.11" />
<sup>11</sup>Akawajibu, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo."
<scripture passage="Luke 3:12" parsed="|Luke|3|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.12" />
<sup>12</sup>Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, "Mwalimu, tufanye nini?"
<scripture passage="Luke 3:13" parsed="|Luke|3|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.13" />
<sup>13</sup>Naye akawaambia, "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."
<scripture passage="Luke 3:14" parsed="|Luke|3|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.14" />
<sup>14</sup>Nao askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye nini?" Naye akawajibu, "Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu."
<scripture passage="Luke 3:15" parsed="|Luke|3|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.15" />
<sup>15</sup>Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
<scripture passage="Luke 3:16" parsed="|Luke|3|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.16" />
<sup>16</sup>Hapo Yohane akawaambia wote, "Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
<scripture passage="Luke 3:17" parsed="|Luke|3|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.17" />
<sup>17</sup>Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto usiozimika."
<scripture passage="Luke 3:18" parsed="|Luke|3|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.18" />
<sup>18</sup>Hivyo, pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu akiwahubiria Habari Njema.
<scripture passage="Luke 3:19" parsed="|Luke|3|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.19" />
<sup>19</sup>Lakini Yohane alimgombeza Herode, mkuu wa mkoa, kwa sababu alikuwa amemchukua Herodia, mke wa ndugu yake, na kumfanya mke wake; na pia kwa ajili ya mabaya yote aliyokuwa amefanya.
<scripture passage="Luke 3:20" parsed="|Luke|3|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.20" />
<sup>20</sup>Kisha Herode akazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohane gerezani.
<scripture passage="Luke 3:21" parsed="|Luke|3|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.21" />
<sup>21</sup>Watu wote walipokuwa wamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akisali, mbingu zilifunguka,
<scripture passage="Luke 3:22" parsed="|Luke|3|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.22" />
<sup>22</sup>na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."
<scripture passage="Luke 3:23" parsed="|Luke|3|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.23" />
<sup>23</sup>Yesu alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
<scripture passage="Luke 3:24" parsed="|Luke|3|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.24" />
<sup>24</sup>Heli alikuwa mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yanai, mwana wa Yosefu,
<scripture passage="Luke 3:25" parsed="|Luke|3|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.25" />
<sup>25</sup>mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Hesli, mwana wa Nagai,
<scripture passage="Luke 3:26" parsed="|Luke|3|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.26" />
<sup>26</sup>mwana wa Maathi, mwana wa Matathia, mwana wa Shemeni, mwana wa Yoseki, mwana wa Yuda,
<scripture passage="Luke 3:27" parsed="|Luke|3|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.27" />
<sup>27</sup>mwana wa Yohanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
<scripture passage="Luke 3:28" parsed="|Luke|3|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.28" />
<sup>28</sup>mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
<scripture passage="Luke 3:29" parsed="|Luke|3|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.29" />
<sup>29</sup>mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Mathati, mwana wa Lawi,
<scripture passage="Luke 3:30" parsed="|Luke|3|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.30" />
<sup>30</sup>mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliakimu,
<scripture passage="Luke 3:31" parsed="|Luke|3|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.31" />
<sup>31</sup>mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
<scripture passage="Luke 3:32" parsed="|Luke|3|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.32" />
<sup>32</sup>mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
<scripture passage="Luke 3:33" parsed="|Luke|3|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.33" />
<sup>33</sup>mwana wa Aminadabu, mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana wa Hesroni, mwana wa Feresi, mwana wa Yuda,
<scripture passage="Luke 3:34" parsed="|Luke|3|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.34" />
<sup>34</sup>mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Abrahamu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
<scripture passage="Luke 3:35" parsed="|Luke|3|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.35" />
<sup>35</sup>mwana wa Serugi, mwana wa Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
<scripture passage="Luke 3:36" parsed="|Luke|3|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.36" />
<sup>36</sup>mwana wa Kainani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Noa, mwana wa Lameki,
<scripture passage="Luke 3:37" parsed="|Luke|3|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.37" />
<sup>37</sup>mwana wa Mathusala, mwana wa Henoki, mwana wa Yaredi, mwana wa Mahalaleli, mwana wa Kenani,
<scripture passage="Luke 3:38" parsed="|Luke|3|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.3.38" />
<sup>38</sup>mwana wa Enosi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, aliyekuwa wa Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 4" progress="22.13%" prev="Luke.3" next="Luke.5" id="Luke.4">
<h3 id="Luke.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Luke.4-p1">
<scripture passage="Luke 4:1" parsed="|Luke|4|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.1" />
<sup>1</sup>Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
<scripture passage="Luke 4:2" parsed="|Luke|4|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.2" />
<sup>2</sup>Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.
<scripture passage="Luke 4:3" parsed="|Luke|4|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.3" />
<sup>3</sup>Ndipo Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate."
<scripture passage="Luke 4:4" parsed="|Luke|4|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.4" />
<sup>4</sup>Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Mtu haishi kwa mkate tu."`
<scripture passage="Luke 4:5" parsed="|Luke|4|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.5" />
<sup>5</sup>Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
<scripture passage="Luke 4:6" parsed="|Luke|4|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.6" />
<sup>6</sup>"Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
<scripture passage="Luke 4:7" parsed="|Luke|4|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.7" />
<sup>7</sup>Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."
<scripture passage="Luke 4:8" parsed="|Luke|4|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.8" />
<sup>8</sup>Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."`
<scripture passage="Luke 4:9" parsed="|Luke|4|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.9" />
<sup>9</sup>Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu,
<scripture passage="Luke 4:10" parsed="|Luke|4|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.10" />
<sup>10</sup>kwa maana imeandikwa: `Atawaamuru malaika wake wakulinde,`
<scripture passage="Luke 4:11" parsed="|Luke|4|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.11" />
<sup>11</sup>na tena, `Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe."`
<scripture passage="Luke 4:12" parsed="|Luke|4|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.12" />
<sup>12</sup>Lakini Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Usimjaribu Bwana Mungu wako."`
<scripture passage="Luke 4:13" parsed="|Luke|4|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.13" />
<sup>13</sup>Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
<scripture passage="Luke 4:14" parsed="|Luke|4|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.14" />
<sup>14</sup>Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
<scripture passage="Luke 4:15" parsed="|Luke|4|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.15" />
<sup>15</sup>Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.
<scripture passage="Luke 4:16" parsed="|Luke|4|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.16" />
<sup>16</sup>Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti.
<scripture passage="Luke 4:17" parsed="|Luke|4|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.17" />
<sup>17</sup>Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:
<scripture passage="Luke 4:18" parsed="|Luke|4|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.18" />
<sup>18</sup>"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,
<scripture passage="Luke 4:19" parsed="|Luke|4|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.19" />
<sup>19</sup>na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."
<scripture passage="Luke 4:20" parsed="|Luke|4|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.20" />
<sup>20</sup>Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.
<scripture passage="Luke 4:21" parsed="|Luke|4|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.21" />
<sup>21</sup>Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo."
<scripture passage="Luke 4:22" parsed="|Luke|4|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.22" />
<sup>22</sup>Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?"
<scripture passage="Luke 4:23" parsed="|Luke|4|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.23" />
<sup>23</sup>Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: `Mganga jiponye mwenyewe`, na pia mtasema: `Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako."`
<scripture passage="Luke 4:24" parsed="|Luke|4|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.24" />
<sup>24</sup>Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake.
<scripture passage="Luke 4:25" parsed="|Luke|4|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.25" />
<sup>25</sup>Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
<scripture passage="Luke 4:26" parsed="|Luke|4|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.26" />
<sup>26</sup>Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni.
<scripture passage="Luke 4:27" parsed="|Luke|4|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.27" />
<sup>27</sup>Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria."
<scripture passage="Luke 4:28" parsed="|Luke|4|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.28" />
<sup>28</sup>Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana.
<scripture passage="Luke 4:29" parsed="|Luke|4|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.29" />
<sup>29</sup>Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.
<scripture passage="Luke 4:30" parsed="|Luke|4|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.30" />
<sup>30</sup>Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.
<scripture passage="Luke 4:31" parsed="|Luke|4|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.31" />
<sup>31</sup>Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.
<scripture passage="Luke 4:32" parsed="|Luke|4|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.32" />
<sup>32</sup>Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.
<scripture passage="Luke 4:33" parsed="|Luke|4|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.33" />
<sup>33</sup>Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:
<scripture passage="Luke 4:34" parsed="|Luke|4|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.34" />
<sup>34</sup>"We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!"
<scripture passage="Luke 4:35" parsed="|Luke|4|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.35" />
<sup>35</sup>Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata kidogo.
<scripture passage="Luke 4:36" parsed="|Luke|4|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.36" />
<sup>36</sup>Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!"
<scripture passage="Luke 4:37" parsed="|Luke|4|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.37" />
<sup>37</sup>Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.
<scripture passage="Luke 4:38" parsed="|Luke|4|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.38" />
<sup>38</sup>Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.
<scripture passage="Luke 4:39" parsed="|Luke|4|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.39" />
<sup>39</sup>Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.
<scripture passage="Luke 4:40" parsed="|Luke|4|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.40" />
<sup>40</sup>Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote.
<scripture passage="Luke 4:41" parsed="|Luke|4|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.41" />
<sup>41</sup>Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.
<scripture passage="Luke 4:42" parsed="|Luke|4|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.42" />
<sup>42</sup>Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
<scripture passage="Luke 4:43" parsed="|Luke|4|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.43" />
<sup>43</sup>Lakini yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo."
<scripture passage="Luke 4:44" parsed="|Luke|4|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.4.44" />
<sup>44</sup>Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 5" progress="22.63%" prev="Luke.4" next="Luke.6" id="Luke.5">
<h3 id="Luke.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Luke.5-p1">
<scripture passage="Luke 5:1" parsed="|Luke|5|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.1" />
<sup>1</sup>Siku moja Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu.
<scripture passage="Luke 5:2" parsed="|Luke|5|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.2" />
<sup>2</sup>Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa; wavuvi wenyewe walikuwa wametoka, wanaosha nyavu zao.
<scripture passage="Luke 5:3" parsed="|Luke|5|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.3" />
<sup>3</sup>Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
<scripture passage="Luke 5:4" parsed="|Luke|5|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.4" />
<sup>4</sup>Alipomaliza kufundisha, akamwambia Simoni, "Peleka mashua mpaka kilindini, mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki."
<scripture passage="Luke 5:5" parsed="|Luke|5|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.5" />
<sup>5</sup>Simoni akamjibu, "Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usiku kucha bila kupata kitu, lakini kwa kuwa umesema, nitatupa nyavu."
<scripture passage="Luke 5:6" parsed="|Luke|5|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.6" />
<sup>6</sup>Baada ya kufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hata nyavu zao zikaanza kukatika.
<scripture passage="Luke 5:7" parsed="|Luke|5|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.7" />
<sup>7</sup>Wakawaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine waje kuwasaidia. Wakaja, wakazijaza mashua zote mbili samaki, hata karibu zingezama.
<scripture passage="Luke 5:8" parsed="|Luke|5|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.8" />
<sup>8</sup>Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema, "Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!"
<scripture passage="Luke 5:9" parsed="|Luke|5|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.9" />
<sup>9</sup>Simoni pamoja na wenzake wote walishangaa kwa kupata samaki wengi vile.
<scripture passage="Luke 5:10" parsed="|Luke|5|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.10" />
<sup>10</sup>Hali kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa wavuvi wenzake Simoni. Yesu akamwambia Simoni, "Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu."
<scripture passage="Luke 5:11" parsed="|Luke|5|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.11" />
<sup>11</sup>Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata.
<scripture passage="Luke 5:12" parsed="|Luke|5|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.12" />
<sup>12</sup>Ikawa, Yesu alipokuwa katika mmojawapo wa miji ya huko, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamwona. Basi, mtu huyo akaanguka kifudifudi akamwomba Yesu: "Mheshimiwa, ukitaka, waweza kunitakasa."
<scripture passage="Luke 5:13" parsed="|Luke|5|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.13" />
<sup>13</sup>Yesu akaunyosha mkono wake, akamgusa na kusema, "Nataka, takasika!" Mara ule ukoma ukamwacha.
<scripture passage="Luke 5:14" parsed="|Luke|5|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.14" />
<sup>14</sup>Yesu akamwamuru: "Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama inavyotakiwa na Sheria ya Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona."
<scripture passage="Luke 5:15" parsed="|Luke|5|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.15" />
<sup>15</sup>Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
<scripture passage="Luke 5:16" parsed="|Luke|5|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.16" />
<sup>16</sup>Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko.
<scripture passage="Luke 5:17" parsed="|Luke|5|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.17" />
<sup>17</sup>Siku moja Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na walimu wa Sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponyea wagonjwa.
<scripture passage="Luke 5:18" parsed="|Luke|5|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.18" />
<sup>18</sup>Mara watu wakaja wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani wamweke mbele ya Yesu.
<scripture passage="Luke 5:19" parsed="|Luke|5|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.19" />
<sup>19</sup>Lakini kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya dari, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
<scripture passage="Luke 5:20" parsed="|Luke|5|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.20" />
<sup>20</sup>Yesu alipoona jinsi walivyokuwa na imani kubwa, akamwambia huyo mtu, "Rafiki, umesamehewa dhambi zako."
<scripture passage="Luke 5:21" parsed="|Luke|5|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.21" />
<sup>21</sup>Walimu wa Sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: "Nani huyu anayemkufuru Mungu kwa maneno yake? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!"
<scripture passage="Luke 5:22" parsed="|Luke|5|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.22" />
<sup>22</sup>Yesu alitambua mawazo yao, akawauliza, "Mnawaza nini mioyoni mwenu?
<scripture passage="Luke 5:23" parsed="|Luke|5|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.23" />
<sup>23</sup>Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, `Umesamehewa dhambi,` au kusema, `Simama utembee`?
<scripture passage="Luke 5:24" parsed="|Luke|5|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.24" />
<sup>24</sup>Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kusamehe dhambi duniani." Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Simama, chukua kitanda chako uende zako nyumbani."
<scripture passage="Luke 5:25" parsed="|Luke|5|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.25" />
<sup>25</sup>Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda zake nyumbani huku akimtukuza Mungu.
<scripture passage="Luke 5:26" parsed="|Luke|5|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.26" />
<sup>26</sup>Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: "Tumeona maajabu leo."
<scripture passage="Luke 5:27" parsed="|Luke|5|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.27" />
<sup>27</sup>Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtoza ushuru mmoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, "Nifuate!"
<scripture passage="Luke 5:28" parsed="|Luke|5|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.28" />
<sup>28</sup>Lawi akaacha yote, akamfuata.
<scripture passage="Luke 5:29" parsed="|Luke|5|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.29" />
<sup>29</sup>Kisha Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake; na kundi kubwa la watoza ushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja nao.
<scripture passage="Luke 5:30" parsed="|Luke|5|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.30" />
<sup>30</sup>Mafarisayo na walimu wa Sheria wakawanung`unikia wafuasi wake wakisema: "Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?"
<scripture passage="Luke 5:31" parsed="|Luke|5|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.31" />
<sup>31</sup>Yesu akawajibu, "Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.
<scripture passage="Luke 5:32" parsed="|Luke|5|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.32" />
<sup>32</sup>Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, ili wapate kutubu."
<scripture passage="Luke 5:33" parsed="|Luke|5|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.33" />
<sup>33</sup>Watu wengine wakamwambia Yesu, "Wafuasi wa Yohane mbatizaji hufunga mara nyingi na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa."
<scripture passage="Luke 5:34" parsed="|Luke|5|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawajibu, "Je, mnaweza kuwataka wale walioalikwa arusini wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao?
<scripture passage="Luke 5:35" parsed="|Luke|5|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.35" />
<sup>35</sup>Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao, na wakati huo ndipo watakapofunga."
<scripture passage="Luke 5:36" parsed="|Luke|5|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.36" />
<sup>36</sup>Yesu akawaambia mfano huu: "Hakuna mtu akataye kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu; kama akifanya hivyo, atakuwa amelikata hilo vazi jipya, na hicho kiraka hakitachukuana na hilo vazi kuukuu.
<scripture passage="Luke 5:37" parsed="|Luke|5|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.37" />
<sup>37</sup>Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; kwani hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, divai itamwagika, na viriba vitaharibika.
<scripture passage="Luke 5:38" parsed="|Luke|5|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.38" />
<sup>38</sup>Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!
<scripture passage="Luke 5:39" parsed="|Luke|5|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.5.39" />
<sup>39</sup>Wala hakuna mtu ambaye hutamani kunywa divai mpya baada ya kunywa ya zamani, kwani husema: `Ile ya zamani ni nzuri zaidi."`
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 6" progress="23.14%" prev="Luke.5" next="Luke.7" id="Luke.6">
<h3 id="Luke.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Luke.6-p1">
<scripture passage="Luke 6:1" parsed="|Luke|6|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.1" />
<sup>1</sup>Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
<scripture passage="Luke 6:2" parsed="|Luke|6|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.2" />
<sup>2</sup>Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, "Mbona mnafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato?"
<scripture passage="Luke 6:3" parsed="|Luke|6|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa?
<scripture passage="Luke 6:4" parsed="|Luke|6|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.4" />
<sup>4</sup>Yeye aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, ni makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kula mikate hiyo."
<scripture passage="Luke 6:5" parsed="|Luke|6|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.5" />
<sup>5</sup>Hivyo akawaambia, "Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato."
<scripture passage="Luke 6:6" parsed="|Luke|6|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.6" />
<sup>6</sup>Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia katika sunagogi, akafundisha. Mle ndani mlikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza.
<scripture passage="Luke 6:7" parsed="|Luke|6|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.7" />
<sup>7</sup>Walimu wa Sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisingizio cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
<scripture passage="Luke 6:8" parsed="|Luke|6|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.8" />
<sup>8</sup>Lakini Yesu alijua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, "Inuka, simama katikati." Yule mtu akaenda akasimama katikati.
<scripture passage="Luke 6:9" parsed="|Luke|6|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.9" />
<sup>9</sup>Kisha Yesu akawaambia, "Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?"
<scripture passage="Luke 6:10" parsed="|Luke|6|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.10" />
<sup>10</sup>Baada ya kuwatazama wote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu, "Nyosha mkono wako." Naye akafanya hivyo, na mkono wake ukawa mzima tena.
<scripture passage="Luke 6:11" parsed="|Luke|6|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.11" />
<sup>11</sup>Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu.
<scripture passage="Luke 6:12" parsed="|Luke|6|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.12" />
<sup>12</sup>Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akimwomba Mungu.
<scripture passage="Luke 6:13" parsed="|Luke|6|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.13" />
<sup>13</sup>Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
<scripture passage="Luke 6:14" parsed="|Luke|6|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.14" />
<sup>14</sup>Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo,
<scripture passage="Luke 6:15" parsed="|Luke|6|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.15" />
<sup>15</sup>Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zelote),
<scripture passage="Luke 6:16" parsed="|Luke|6|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.16" />
<sup>16</sup>Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.
<scripture passage="Luke 6:17" parsed="|Luke|6|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.17" />
<sup>17</sup>Baada ya kushuka mlimani pamoja na mitume, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
<scripture passage="Luke 6:18" parsed="|Luke|6|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.18" />
<sup>18</sup>Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu.
<scripture passage="Luke 6:19" parsed="|Luke|6|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.19" />
<sup>19</sup>Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponya wote.
<scripture passage="Luke 6:20" parsed="|Luke|6|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.20" />
<sup>20</sup>Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema: "Heri ninyi mlio maskini, maana Ufalme wa Mungu ni wenu.
<scripture passage="Luke 6:21" parsed="|Luke|6|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.21" />
<sup>21</sup>Heri ninyi mnaosikia njaa sasa, maana baadaye mtashiba. Heri ninyi mnaolia sasa, maana baadaye mtacheka kwa furaha.
<scripture passage="Luke 6:22" parsed="|Luke|6|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.22" />
<sup>22</sup>"Heri yenu ninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu!
<scripture passage="Luke 6:23" parsed="|Luke|6|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.23" />
<sup>23</sup>Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
<scripture passage="Luke 6:24" parsed="|Luke|6|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.24" />
<sup>24</sup>Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu.
<scripture passage="Luke 6:25" parsed="|Luke|6|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.25" />
<sup>25</sup>Ole wenu ninyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia.
<scripture passage="Luke 6:26" parsed="|Luke|6|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.26" />
<sup>26</sup>Ole wenu ninyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.
<scripture passage="Luke 6:27" parsed="|Luke|6|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.27" />
<sup>27</sup>"Lakini nawaambieni ninyi mnaonisikiliza: wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni.
<scripture passage="Luke 6:28" parsed="|Luke|6|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.28" />
<sup>28</sup>Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.
<scripture passage="Luke 6:29" parsed="|Luke|6|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.29" />
<sup>29</sup>Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang`anya koti lako mwachie pia shati lako.
<scripture passage="Luke 6:30" parsed="|Luke|6|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.30" />
<sup>30</sup>Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang`anya mali yako usimtake akurudishie.
<scripture passage="Luke 6:31" parsed="|Luke|6|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.31" />
<sup>31</sup>Watendeeni wengine kama mnavyotaka wawatendee ninyi.
<scripture passage="Luke 6:32" parsed="|Luke|6|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.32" />
<sup>32</sup>"Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
<scripture passage="Luke 6:33" parsed="|Luke|6|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.33" />
<sup>33</sup>Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo!
<scripture passage="Luke 6:34" parsed="|Luke|6|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.34" />
<sup>34</sup>Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!
<scripture passage="Luke 6:35" parsed="|Luke|6|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.35" />
<sup>35</sup>Ila nyinyi wapendeni adui zenu, na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia malipo, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya.
<scripture passage="Luke 6:36" parsed="|Luke|6|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.36" />
<sup>36</sup>Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.
<scripture passage="Luke 6:37" parsed="|Luke|6|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.37" />
<sup>37</sup>"Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
<scripture passage="Luke 6:38" parsed="|Luke|6|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.38" />
<sup>38</sup>Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho ambacho Mungu atatumia kwenu."
<scripture passage="Luke 6:39" parsed="|Luke|6|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.39" />
<sup>39</sup>Akawaambia mfano huu: "Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni.
<scripture passage="Luke 6:40" parsed="|Luke|6|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.40" />
<sup>40</sup>Mwanafunzi hamshindi mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimu huwa kama mwalimu wake.
<scripture passage="Luke 6:41" parsed="|Luke|6|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.41" />
<sup>41</sup>Unawezaje kukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwenzio, usione boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe?
<scripture passage="Luke 6:42" parsed="|Luke|6|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.42" />
<sup>42</sup>Au, unawezaje kumwambia mwenzako, `Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako,` na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako.
<scripture passage="Luke 6:43" parsed="|Luke|6|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.43" />
<sup>43</sup>"Mti mwema hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri.
<scripture passage="Luke 6:44" parsed="|Luke|6|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.44" />
<sup>44</sup>Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
<scripture passage="Luke 6:45" parsed="|Luke|6|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.45" />
<sup>45</sup>Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
<scripture passage="Luke 6:46" parsed="|Luke|6|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.46" />
<sup>46</sup>"Mbona mwaniita `Bwana, Bwana,` na huku hamtimizi yale ninayosema?
<scripture passage="Luke 6:47" parsed="|Luke|6|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.47" />
<sup>47</sup>Nitawapeni mfano unaofaa kuonyesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:
<scripture passage="Luke 6:48" parsed="|Luke|6|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.48" />
<sup>48</sup>Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
<scripture passage="Luke 6:49" parsed="|Luke|6|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.6.49" />
<sup>49</sup>Lakini yeyote anayesikia maneno yangu lakini asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!"
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 7" progress="23.79%" prev="Luke.6" next="Luke.8" id="Luke.7">
<h3 id="Luke.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Luke.7-p1">
<scripture passage="Luke 7:1" parsed="|Luke|7|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.1" />
<sup>1</sup>Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu.
<scripture passage="Luke 7:2" parsed="|Luke|7|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.2" />
<sup>2</sup>Huko kulikuwa na jemadari mmoja Mroma ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu kufa.
<scripture passage="Luke 7:3" parsed="|Luke|7|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.3" />
<sup>3</sup>Yule jemadari aliposikia habari za Yesu, aliwatuma wazee fulani Wayahudi waende kumwomba aje amponye mtumishi wake.
<scripture passage="Luke 7:4" parsed="|Luke|7|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.4" />
<sup>4</sup>Walipofika kwa Yesu, walimsihi sana, wakasema: "Huyu anastahili afanyiwe jambo hilo,
<scripture passage="Luke 7:5" parsed="|Luke|7|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.5" />
<sup>5</sup>maana analipenda taifa letu, na ndiye aliyetujengea lile sunagogi."
<scripture passage="Luke 7:6" parsed="|Luke|7|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.6" />
<sup>6</sup>Basi, Yesu akaenda pamoja nao. Alipokuwa karibu kufika nyumbani kwa yule jemadari Mroma, yule jemadari aliwatuma marafiki zake wamwambie Yesu: "Bwana, usijisumbue zaidi, maana mimi sistahili uingie nyumbani mwangu.
<scripture passage="Luke 7:7" parsed="|Luke|7|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.7" />
<sup>7</sup>Ndio maana sikujiona nastahili hata kuja kwako; amuru tu, na mtumishi wangu atapona.
<scripture passage="Luke 7:8" parsed="|Luke|7|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.8" />
<sup>8</sup>Mimi pia ni mtu niliye chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, `Nenda!`, naye huenda; namwambia mwingine, `Njoo!` naye huja; na nikimwambia mtumishi wangu, `Fanya hiki!`, hufanya."
<scripture passage="Luke 7:9" parsed="|Luke|7|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.9" />
<sup>9</sup>Yesu aliposikia hayo, alishangaa; halafu akauelekea ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akasema, "Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli."
<scripture passage="Luke 7:10" parsed="|Luke|7|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.10" />
<sup>10</sup>Wale watu walipowasili nyumbani walimkuta yule mtumishi hajambo kabisa.
<scripture passage="Luke 7:11" parsed="|Luke|7|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.11" />
<sup>11</sup>Baadaye kidogo Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake pamoja na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
<scripture passage="Luke 7:12" parsed="|Luke|7|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.12" />
<sup>12</sup>Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya kijana mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
<scripture passage="Luke 7:13" parsed="|Luke|7|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.13" />
<sup>13</sup>Bwana alipomwona mama huyo, alimwonea huruma, akamwambia, "Usilie."
<scripture passage="Luke 7:14" parsed="|Luke|7|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.14" />
<sup>14</sup>Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wanalichukua wakasimama. Halafu akasema, "Kijana! Nakuamuru, amka!"
<scripture passage="Luke 7:15" parsed="|Luke|7|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.15" />
<sup>15</sup>Yule aliyekufa akaketi, akaanza kuongea. Na Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
<scripture passage="Luke 7:16" parsed="|Luke|7|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.16" />
<sup>16</sup>Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema: "Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake."
<scripture passage="Luke 7:17" parsed="|Luke|7|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.17" />
<sup>17</sup>Habari hizo zikaenea kote katika Uyahudi na katika nchi za jirani.
<scripture passage="Luke 7:18" parsed="|Luke|7|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.18" />
<sup>18</sup>Wanafunzi wa Yohane walimpa habari Yohane juu ya mambo hayo yote. Naye Yohane, baada ya kuwaita wawili kati ya wanafunzi wake,
<scripture passage="Luke 7:19" parsed="|Luke|7|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.19" />
<sup>19</sup>aliwatuma kwa Bwana wamwulize: "Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?"
<scripture passage="Luke 7:20" parsed="|Luke|7|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.20" />
<sup>20</sup>Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, "Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: `Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?"`
<scripture passage="Luke 7:21" parsed="|Luke|7|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.21" />
<sup>21</sup>Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponya watu wengi waliokuwa wanateseka kwa magonjwa na waliopagawa na pepo wabaya, akawawezesha vipofu wengi kuona tena.
<scripture passage="Luke 7:22" parsed="|Luke|7|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.22" />
<sup>22</sup>Basi, Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari njema.
<scripture passage="Luke 7:23" parsed="|Luke|7|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.23" />
<sup>23</sup>Heri mtu yule ambaye hana mashaka nami!"
<scripture passage="Luke 7:24" parsed="|Luke|7|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.24" />
<sup>24</sup>Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: "Mlikwenda kule jangwani, hivi mlitaka kuona kitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa na upepo?
<scripture passage="Luke 7:25" parsed="|Luke|7|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.25" />
<sup>25</sup>Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia mavazi maridadi? La hasha! Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
<scripture passage="Luke 7:26" parsed="|Luke|7|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.26" />
<sup>26</sup>Basi, niambieni, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.
<scripture passage="Luke 7:27" parsed="|Luke|7|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.27" />
<sup>27</sup>Huyu Yohane ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: `Hapa ni mtumishi wangu, asema Bwana; ninamtuma akutangulie, akutayarishie njia."`
<scripture passage="Luke 7:28" parsed="|Luke|7|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.28" />
<sup>28</sup>Yesu akamalizia kwa kusema, "Nawaambieni, kati ya binadamu wote hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkubwa zaidi kuliko yeye."
<scripture passage="Luke 7:29" parsed="|Luke|7|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.29" />
<sup>29</sup>Waliposikia hayo watu wote na watoza ushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
<scripture passage="Luke 7:30" parsed="|Luke|7|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.30" />
<sup>30</sup>Lakini Mafarisayo na walimu wa Sheria walikataa mpango wa Mungu uliowahusu wakakataa kubatizwa na Yohane.
<scripture passage="Luke 7:31" parsed="|Luke|7|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.31" />
<sup>31</sup>Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani?
<scripture passage="Luke 7:32" parsed="|Luke|7|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.32" />
<sup>32</sup>Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: `Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza! Tumeomboleza, lakini hamkulia!`
<scripture passage="Luke 7:33" parsed="|Luke|7|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.33" />
<sup>33</sup>Kwa maana Yohane alikuja, yeye alifunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: `Amepagawa na pepo!`
<scripture passage="Luke 7:34" parsed="|Luke|7|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.34" />
<sup>34</sup>Akaja Mwana wa Mtu; anakula na kunywa, mkasema: `Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!`
<scripture passage="Luke 7:35" parsed="|Luke|7|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.35" />
<sup>35</sup>Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali."
<scripture passage="Luke 7:36" parsed="|Luke|7|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.36" />
<sup>36</sup>Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
<scripture passage="Luke 7:37" parsed="|Luke|7|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.37" />
<sup>37</sup>Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja aliyekuwa anaishi maisha mabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
<scripture passage="Luke 7:38" parsed="|Luke|7|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.38" />
<sup>38</sup>Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
<scripture passage="Luke 7:39" parsed="|Luke|7|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.39" />
<sup>39</sup>Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, "Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi."
<scripture passage="Luke 7:40" parsed="|Luke|7|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.40" />
<sup>40</sup>Yesu akamwambia huyo Mfarisayo, "Simoni, ninacho kitu cha kukwambia." Naye Simoni akamwambia, "Ndio Mwalimu, sema." Yesu akasema,
<scripture passage="Luke 7:41" parsed="|Luke|7|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.41" />
<sup>41</sup>"Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa dinari mia tano, na mwingine hamsini.
<scripture passage="Luke 7:42" parsed="|Luke|7|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.42" />
<sup>42</sup>Waliposhindwa kulipa madeni yao, huyo mtu aliwasamehe wote wawili. Sasa ni yupi kati ya hao wawili atampenda zaidi huyo bwana?"
<scripture passage="Luke 7:43" parsed="|Luke|7|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.43" />
<sup>43</sup>Simoni akamjibu, "Ni dhahiri kwamba yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi atampenda zaidi yule bwana." Yesu akamwambia, "Sawa."
<scripture passage="Luke 7:44" parsed="|Luke|7|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.44" />
<sup>44</sup>Halafu akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, "Unamwona huyu mwanamke, sivyo? Basi, mimi nilipoingia hapa nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu yangu; lakini mwanamke huyu ameniosha miguu yangu kwa machozi yake na kunipangusa kwa nywele zake.
<scripture passage="Luke 7:45" parsed="|Luke|7|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.45" />
<sup>45</sup>Wewe hukunisalimu kwa kunibusu, lakini huyu mwanamke tangu nilipoingia hapa amekuwa akiibusu miguu yangu.
<scripture passage="Luke 7:46" parsed="|Luke|7|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.46" />
<sup>46</sup>Wewe hukunionyesha ukarimu wako kwa kunipaka mafuta kichwani, lakini huyu mwanamke amefanya hivyo kwa kunipaka mafuta miguu yangu.
<scripture passage="Luke 7:47" parsed="|Luke|7|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.47" />
<sup>47</sup>Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo."
<scripture passage="Luke 7:48" parsed="|Luke|7|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.48" />
<sup>48</sup>Basi, Yesu akamwambia yule mwanamke, "Umesamehewa dhambi zako."
<scripture passage="Luke 7:49" parsed="|Luke|7|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.49" />
<sup>49</sup>Na hapo wale waliokuwa pamoja naye mezani wakaulizana, "Ni mtu wa namna gani huyu awezaye kusamehe dhambi?"
<scripture passage="Luke 7:50" parsed="|Luke|7|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.7.50" />
<sup>50</sup>Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, "Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani."
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 8" progress="24.46%" prev="Luke.7" next="Luke.9" id="Luke.8">
<h3 id="Luke.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Luke.8-p1">
<scripture passage="Luke 8:1" parsed="|Luke|8|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, Yesu alipitia katika miji na vijiji akitangaza Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
<scripture passage="Luke 8:2" parsed="|Luke|8|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.2" />
<sup>2</sup>Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba;
<scripture passage="Luke 8:3" parsed="|Luke|8|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.3" />
<sup>3</sup>Yoana, mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.
<scripture passage="Luke 8:4" parsed="|Luke|8|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.4" />
<sup>4</sup>Kundi kubwa la watu lilikuwa linakusanyika, na watu walikuwa wanamjia Yesu kutoka kila mji. Naye akawaambia mfano huu:
<scripture passage="Luke 8:5" parsed="|Luke|8|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.5" />
<sup>5</sup>"Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda zile mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga, na ndege wakazila.
<scripture passage="Luke 8:6" parsed="|Luke|8|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.6" />
<sup>6</sup>Nyingine zilianguka penye mawe, na baada ya kuota zikanyauka kwa kukosa maji.
<scripture passage="Luke 8:7" parsed="|Luke|8|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.7" />
<sup>7</sup>Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
<scripture passage="Luke 8:8" parsed="|Luke|8|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.8" />
<sup>8</sup>Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa asilimia mia." Baada ya kusema hayo, akapaaza sauti, akasema, "Mwenye masikio na asikie!"
<scripture passage="Luke 8:9" parsed="|Luke|8|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.9" />
<sup>9</sup>Wanafunzi wake wakamwuliza Yesu maana ya mfano huo.
<scripture passage="Luke 8:10" parsed="|Luke|8|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.10" />
<sup>10</sup>Naye akajibu, "Ninyi mmejaliwa kujua siri za Ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
<scripture passage="Luke 8:11" parsed="|Luke|8|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.11" />
<sup>11</sup>"Basi, maana ya mfano huu ni hii: mbegu ni neno la Mungu.
<scripture passage="Luke 8:12" parsed="|Luke|8|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.12" />
<sup>12</sup>Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini na hivyo wakaokoka.
<scripture passage="Luke 8:13" parsed="|Luke|8|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.13" />
<sup>13</sup>Zile zilizoanguka penye mawe zinaonyesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Hata hivyo, kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
<scripture passage="Luke 8:14" parsed="|Luke|8|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.14" />
<sup>14</sup>Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu wale wanaosikia lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi, mali na anasa za maisha, na hawazai matunda yakakomaa.
<scripture passage="Luke 8:15" parsed="|Luke|8|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.15" />
<sup>15</sup>Na zile zilizoanguka kwenye udongo mzuri ndio watu wale wanaolisikia lile neno, wakalizingatia kwa moyo mwema na wa utii. Hao huvumilia mpaka wakazaa matunda.
<scripture passage="Luke 8:16" parsed="|Luke|8|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.16" />
<sup>16</sup>"Watu hawawashi taa na kuifunika kwa chombo au kuiweka mvunguni. Lakini huiweka juu ya kinara ili watu wanapoingia ndani wapate kuona mwanga.
<scripture passage="Luke 8:17" parsed="|Luke|8|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.17" />
<sup>17</sup>"Chochote kilichofichwa kitafichuliwa na siri yoyote itagunduliwa na kujulikana hadharani.
<scripture passage="Luke 8:18" parsed="|Luke|8|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.18" />
<sup>18</sup>"Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani kuwa anacho, kitachukuliwa."
<scripture passage="Luke 8:19" parsed="|Luke|8|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.19" />
<sup>19</sup>Hapo mama na ndugu zake Yesu wakamjia, lakini hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu.
<scripture passage="Luke 8:20" parsed="|Luke|8|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.20" />
<sup>20</sup>Yesu akapewa habari kwamba mama na ndugu zake walikuwa nje, wanataka kumwona.
<scripture passage="Luke 8:21" parsed="|Luke|8|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.21" />
<sup>21</sup>Lakini Yesu akawaambia watu wote, "Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika."
<scripture passage="Luke 8:22" parsed="|Luke|8|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.22" />
<sup>22</sup>Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvuke ziwa twende mpaka ng`ambo." Basi, wakaanza safari.
<scripture passage="Luke 8:23" parsed="|Luke|8|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.23" />
<sup>23</sup>Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
<scripture passage="Luke 8:24" parsed="|Luke|8|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.24" />
<sup>24</sup>Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, "Bwana, Bwana! Tunaangamia!" Yesu akaamka, akaikemea dhoruba na mawimbi, navyo vikatulia, kukawa shwari.
<scripture passage="Luke 8:25" parsed="|Luke|8|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.25" />
<sup>25</sup>Kisha akawaambia, "Iko wapi imani yenu?" Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, "Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?"
<scripture passage="Luke 8:26" parsed="|Luke|8|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.26" />
<sup>26</sup>Wakaendelea na safari, wakafika pwani ya nchi ya Wagerase inayokabiliana na Galilaya, ng`ambo ya ziwa.
<scripture passage="Luke 8:27" parsed="|Luke|8|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.27" />
<sup>27</sup>Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo, hakuwa anavaa nguo, wala hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.
<scripture passage="Luke 8:28" parsed="|Luke|8|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.28" />
<sup>28</sup>Alipomwona Yesu, alipiga kelele na kujitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kubwa "We, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!"
<scripture passage="Luke 8:29" parsed="|Luke|8|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.29" />
<sup>29</sup>Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikwishamwambia huyo pepo mchafu amtoke mtu huyo. Pepo huyo mchafu alikuwa anamvamia mtu huyo mara nyingi, na ingawa watu walimweka ndani na kumfunga kwa minyororo na pingu, lakini kila mara alivivunja vifungo hivyo, akakimbizwa na pepo huyo mchafu hadi jangwani.
<scripture passage="Luke 8:30" parsed="|Luke|8|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.30" />
<sup>30</sup>Basi, Yesu akamwuliza, "Jina lako nani?" Yeye akajibu, "Jina langu ni `Jeshi"`--kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
<scripture passage="Luke 8:31" parsed="|Luke|8|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.31" />
<sup>31</sup>Hao pepo wakamsihi asiwaamuru wamtoke na kwenda kwenye shimo lisilo na mwisho. ic
<scripture passage="Luke 8:32" parsed="|Luke|8|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.32" />
<sup>32</sup>Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
<scripture passage="Luke 8:33" parsed="|Luke|8|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.33" />
<sup>33</sup>Kwa hiyo pepo hao wakamtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nao wakaporomoka kwenye ule mteremko mkali, wakatumbukia ziwani, wakazama majini.
<scripture passage="Luke 8:34" parsed="|Luke|8|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.34" />
<sup>34</sup>Wale wachungaji walipoona yote yaliyotokea walikimbia, wakaenda kuwapa watu habari, mjini na mashambani.
<scripture passage="Luke 8:35" parsed="|Luke|8|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.35" />
<sup>35</sup>Watu wakaja kuona yaliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na pepo ameketi karibu na Yesu, amevaa nguo, ana akili zake, wakaogopa.
<scripture passage="Luke 8:36" parsed="|Luke|8|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.36" />
<sup>36</sup>Wale watu walioshuhudia tukio hilo waliwaeleza hao jinsi yule mtu alivyoponywa.
<scripture passage="Luke 8:37" parsed="|Luke|8|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.37" />
<sup>37</sup>Wakazi wa nchi ya Gerase walishikwa na hofu kubwa. Kwa hiyo wakamwomba Yesu aondoke, aende zake. Hivyo Yesu alipanda tena mashua, akaondoka.
<scripture passage="Luke 8:38" parsed="|Luke|8|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.38" />
<sup>38</sup>Yule mtu aliyetokwa na wale pepo akamsihi aende pamoja naye. Lakini Yesu hakumruhusu, bali akamwambia,
<scripture passage="Luke 8:39" parsed="|Luke|8|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.39" />
<sup>39</sup>"Rudi nyumbani ukaeleze yote Mungu aliyokutendea." Basi, yule mtu akaenda akitangaza kila mahali katika mji ule mambo yote Yesu aliyomtendea.
<scripture passage="Luke 8:40" parsed="|Luke|8|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.40" />
<sup>40</sup>Yesu aliporudi upande mwingine wa ziwa, kundi la watu lilimkaribisha, kwa maana wote walikuwa wanamngojea.
<scripture passage="Luke 8:41" parsed="|Luke|8|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.41" />
<sup>41</sup>Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,
<scripture passage="Luke 8:42" parsed="|Luke|8|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.42" />
<sup>42</sup>kwa kuwa binti yake wa pekee, mwana wa pekee mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa mahututi. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
<scripture passage="Luke 8:43" parsed="|Luke|8|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.43" />
<sup>43</sup>Kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
<scripture passage="Luke 8:44" parsed="|Luke|8|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.44" />
<sup>44</sup>Huyo mwanamke alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake. Papo hapo akaponywa ugonjwa wake wa kutokwa damu.
<scripture passage="Luke 8:45" parsed="|Luke|8|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.45" />
<sup>45</sup>Yesu akasema, "Ni nani aliyenigusa?" Wote wakasema kwamba hapakuwa na mtu aliyemgusa. Naye Petro akasema, "Mwalimu, umati wa watu umekuzunguka na kukusonga!"
<scripture passage="Luke 8:46" parsed="|Luke|8|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.46" />
<sup>46</sup>Lakini Yesu akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, maana nimehisi nguvu imenitoka."
<scripture passage="Luke 8:47" parsed="|Luke|8|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.47" />
<sup>47</sup>Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponyeshwa mara moja.
<scripture passage="Luke 8:48" parsed="|Luke|8|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.48" />
<sup>48</sup>Yesu akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."
<scripture passage="Luke 8:49" parsed="|Luke|8|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.49" />
<sup>49</sup>Alipokuwa bado akiongea, Yairo akaletewa habari kutoka nyumbani: "Binti yako ameshakufa, ya nini kumsumbua Mwalimu zaidi?"
<scripture passage="Luke 8:50" parsed="|Luke|8|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.50" />
<sup>50</sup>Yesu aliposikia hayo akamwambia Yairo, "Usiogope; amini tu, naye atapona."
<scripture passage="Luke 8:51" parsed="|Luke|8|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.51" />
<sup>51</sup>Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
<scripture passage="Luke 8:52" parsed="|Luke|8|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.52" />
<sup>52</sup>Watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili yake. Lakini Yesu akawaambia, "Msilie, kwa maana mtoto hajafa, amelala tu!"
<scripture passage="Luke 8:53" parsed="|Luke|8|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.53" />
<sup>53</sup>Nao wakamcheka kwa sababu walijua kwamba alikuwa amekufa.
<scripture passage="Luke 8:54" parsed="|Luke|8|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.54" />
<sup>54</sup>Lakini Yesu akamshika mkono akasema, "Mtoto amka!"
<scripture passage="Luke 8:55" parsed="|Luke|8|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.55" />
<sup>55</sup>Roho yake ikamrudia, akaamka mara. Yesu akaamuru wampe chakula.
<scripture passage="Luke 8:56" parsed="|Luke|8|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.8.56" />
<sup>56</sup>Wazazi wake walishangaa, lakini Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote hayo yaliyotendeka.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 9" progress="25.22%" prev="Luke.8" next="Luke.10" id="Luke.9">
<h3 id="Luke.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Luke.9-p1">
<scripture passage="Luke 9:1" parsed="|Luke|9|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo juu ya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
<scripture passage="Luke 9:2" parsed="|Luke|9|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.2" />
<sup>2</sup>Halafu akawatuma waende kuhubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
<scripture passage="Luke 9:3" parsed="|Luke|9|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.3" />
<sup>3</sup>Akawaambia, "Mnaposafiri msichukue chochote: msichukue fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.
<scripture passage="Luke 9:4" parsed="|Luke|9|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.4" />
<sup>4</sup>Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka mtakapoondoka katika kijiji hicho.
<scripture passage="Luke 9:5" parsed="|Luke|9|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.5" />
<sup>5</sup>Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kung`uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao."
<scripture passage="Luke 9:6" parsed="|Luke|9|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.6" />
<sup>6</sup>Basi, wakaanza safari, wakapitia vijijini wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa kila mahali.
<scripture passage="Luke 9:7" parsed="|Luke|9|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.7" />
<sup>7</sup>Sasa, mtawala Herode, alipata habari za mambo yote yaliyokuwa yanatendeka, akawa na wasiwasi kwa vile walikuwa wakisema: "Yohane amefufuka kutoka wafu!"
<scripture passage="Luke 9:8" parsed="|Luke|9|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.8" />
<sup>8</sup>Wengine walisema kwamba Eliya ametokea, na wengine walisema kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amerudi duniani.
<scripture passage="Luke 9:9" parsed="|Luke|9|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.9" />
<sup>9</sup>Lakini Herode akasema, "Huyo Yohane nilimkata kichwa; sasa ni nani huyu ninayesikia habari zake?" Akawa na hamu ya kumwona.
<scripture passage="Luke 9:10" parsed="|Luke|9|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.10" />
<sup>10</sup>Wale mitume waliporudi, walimweleza yote waliyoyafanya. Yesu akawachukua, wakaenda peke yao mjini Bethsaida.
<scripture passage="Luke 9:11" parsed="|Luke|9|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.11" />
<sup>11</sup>Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
<scripture passage="Luke 9:12" parsed="|Luke|9|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.12" />
<sup>12</sup>Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, "Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani."
<scripture passage="Luke 9:13" parsed="|Luke|9|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.13" />
<sup>13</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Wapeni ninyi chakula." Wakamjibu, "Hatuna chochote ila mikate mitano na samaki wawili. Labda twende wenyewe tukawanunulie chakula watu wote hawa!"
<scripture passage="Luke 9:14" parsed="|Luke|9|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.14" />
<sup>14</sup>(Walikuwepo pale wanaume wapatao elfu tano.) Basi, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Waambieni watu waketi katika makundi ya watu hamsinihamsini."
<scripture passage="Luke 9:15" parsed="|Luke|9|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.15" />
<sup>15</sup>Wanafunzi wakafanya walivyoambiwa, wakawaketisha wote.
<scripture passage="Luke 9:16" parsed="|Luke|9|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.16" />
<sup>16</sup>Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu.
<scripture passage="Luke 9:17" parsed="|Luke|9|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.17" />
<sup>17</sup>Wakala wote, wakashiba; wakakusanya makombo ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
<scripture passage="Luke 9:18" parsed="|Luke|9|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.18" />
<sup>18</sup>Siku moja, Yesu alikuwa anasali peke yake, na wanafunzi wake walikuwa karibu. Basi, akawauliza, "Eti watu wanasema mimi ni nani?"
<scripture passage="Luke 9:19" parsed="|Luke|9|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.19" />
<sup>19</sup>Nao wakamjibu, "Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya, hali wengine wanasema kuwa wewe ni mmoja wa manabii wa kale ambaye amefufuka."
<scripture passage="Luke 9:20" parsed="|Luke|9|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.20" />
<sup>20</sup>Hapo akawauliza, "Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo wa Mungu."
<scripture passage="Luke 9:21" parsed="|Luke|9|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.21" />
<sup>21</sup>Halafu Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hiyo.
<scripture passage="Luke 9:22" parsed="|Luke|9|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.22" />
<sup>22</sup>Akaendelea kusema: "Ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria; atauawa, lakini siku ya tatu atafufuliwa."
<scripture passage="Luke 9:23" parsed="|Luke|9|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.23" />
<sup>23</sup>Kisha akawaambia watu wote, "Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane nafsi yake, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate.
<scripture passage="Luke 9:24" parsed="|Luke|9|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.24" />
<sup>24</sup>Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza; lakini atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
<scripture passage="Luke 9:25" parsed="|Luke|9|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.25" />
<sup>25</sup>Je, kuna faida gani mtu kuupata utajiri wote wa dunia kwa kujipoteza au kujiangamiza yeye mwenyewe?
<scripture passage="Luke 9:26" parsed="|Luke|9|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.26" />
<sup>26</sup>Mtu akinionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
<scripture passage="Luke 9:27" parsed="|Luke|9|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.27" />
<sup>27</sup>Nawaambieni kweli, kuna wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Luke 9:28" parsed="|Luke|9|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.28" />
<sup>28</sup>Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu aliwachukua Petro, Yohane na Yakobo, akaenda nao mlimani kusali.
<scripture passage="Luke 9:29" parsed="|Luke|9|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.29" />
<sup>29</sup>Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung`aa sana.
<scripture passage="Luke 9:30" parsed="|Luke|9|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.30" />
<sup>30</sup>Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao ni Mose na Eliya,
<scripture passage="Luke 9:31" parsed="|Luke|9|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.31" />
<sup>31</sup>ambao walitokea wakiwa wenye utukufu, wakazungumza naye juu ya kifo chake ambacho angekikamilisha huko Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 9:32" parsed="|Luke|9|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.32" />
<sup>32</sup>Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye.
<scripture passage="Luke 9:33" parsed="|Luke|9|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.33" />
<sup>33</sup>Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri kwamba tupo hapa: basi, tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."--Kwa kweli hakujua anasema nini.
<scripture passage="Luke 9:34" parsed="|Luke|9|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.34" />
<sup>34</sup>Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
<scripture passage="Luke 9:35" parsed="|Luke|9|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.35" />
<sup>35</sup>Sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ndiye Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni."
<scripture passage="Luke 9:36" parsed="|Luke|9|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.36" />
<sup>36</sup>Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake. Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.
<scripture passage="Luke 9:37" parsed="|Luke|9|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.37" />
<sup>37</sup>Kesho yake walipokuwa wakishuka kutoka kule mlimani, kundi kubwa la watu lilikutana na Yesu.
<scripture passage="Luke 9:38" parsed="|Luke|9|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.38" />
<sup>38</sup>Hapo, mtu mmoja katika lile kundi akapaaza sauti, akasema, "Mwalimu! Ninakusihi umwangalie mwanangu--mwanangu wa pekee!
<scripture passage="Luke 9:39" parsed="|Luke|9|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.39" />
<sup>39</sup>Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.
<scripture passage="Luke 9:40" parsed="|Luke|9|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.40" />
<sup>40</sup>Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza."
<scripture passage="Luke 9:41" parsed="|Luke|9|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.41" />
<sup>41</sup>Yesu akasema, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini?" Kisha akamwambia huyo mtu, "Mlete mtoto wako hapa."
<scripture passage="Luke 9:42" parsed="|Luke|9|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.42" />
<sup>42</sup>Wakati mtoto huyo alipokuwa anamjia Yesu, yule pepo alimwangusha chini na kumtia kifafa. Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu akamponya mtoto na kumkabidhi kwa baba yake.
<scripture passage="Luke 9:43" parsed="|Luke|9|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.43" />
<sup>43</sup>Watu wote wakashangazwa na uwezo mkuu wa Mungu. Wale watu walipokuwa bado wanashangaa juu ya mambo yote aliyofanya, Yesu aliwaambia wanafunzi wake,
<scripture passage="Luke 9:44" parsed="|Luke|9|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.44" />
<sup>44</sup>"Tegeni masikio, myasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu."
<scripture passage="Luke 9:45" parsed="|Luke|9|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.45" />
<sup>45</sup>Lakini wao hawakuelewa maana ya usemi huo. Jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao ili wasitambue; nao wakaogopa kumwuliza juu ya msemo huo.
<scripture passage="Luke 9:46" parsed="|Luke|9|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.46" />
<sup>46</sup>Kukatokea majadiliano kati ya wale wanafunzi kuhusu nani kati yao aliyekuwa mkuu zaidi.
<scripture passage="Luke 9:47" parsed="|Luke|9|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.47" />
<sup>47</sup>Yesu aliyajua mawazo yaliyokuwa mioyoni mwao; basi akamchukua mtoto mdogo akamweka karibu naye,
<scripture passage="Luke 9:48" parsed="|Luke|9|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.48" />
<sup>48</sup>akawaambia, "Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkubwa kuliko wote."
<scripture passage="Luke 9:49" parsed="|Luke|9|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.49" />
<sup>49</sup>Yohane alidakia na kusema, "Bwana, tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jina lako nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu."
<scripture passage="Luke 9:50" parsed="|Luke|9|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.50" />
<sup>50</sup>Lakini Yesu akamwambia, "Msimkataze; kwani asiyepingana nanyi yuko upande wenu."
<scripture passage="Luke 9:51" parsed="|Luke|9|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.51" />
<sup>51</sup>Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 9:52" parsed="|Luke|9|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.52" />
<sup>52</sup>Basi, akawatuma wajumbe wamtangulie, nao wakaenda wakaingia kijiji kimoja cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
<scripture passage="Luke 9:53" parsed="|Luke|9|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.53" />
<sup>53</sup>Lakini wenyeji wa hapo hawakutaka kumpokea kwa sababu alikuwa anaelekea Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 9:54" parsed="|Luke|9|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.54" />
<sup>54</sup>Basi, wanafunzi wake, kina Yohane na Yakobo, walipoona hayo, wakasema, "Bwana, wataka tuamuru moto ushuke kutoka mbinguni uwateketeze?"
<scripture passage="Luke 9:55" parsed="|Luke|9|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.55" />
<sup>55</sup>Lakini yeye akawageukia, akawakemea.<i>fa</i>
<scripture passage="Luke 9:56" parsed="|Luke|9|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.56" />
<sup>56</sup>Wakatoka, wakaenda kijiji kingine. gani mliyo nayo; kwa maana Mwana wa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya watu, bali kuyaokoa."
<scripture passage="Luke 9:57" parsed="|Luke|9|57|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.57" />
<sup>57</sup>Walipokuwa wakisafiri njiani, mtu mmoja akamwambia Yesu, "Nitakufuata kokote utakakokwenda."
<scripture passage="Luke 9:58" parsed="|Luke|9|58|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.58" />
<sup>58</sup>Yesu akasema, "Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia."
<scripture passage="Luke 9:59" parsed="|Luke|9|59|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.59" />
<sup>59</sup>Kisha akamwambia mtu mwingine, "Nifuate." Lakini huyo akasema, "Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu."
<scripture passage="Luke 9:60" parsed="|Luke|9|60|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.60" />
<sup>60</sup>Yesu akamwambia, "Waache wafu wazike wafu wao; bali wewe nenda ukatangaze Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Luke 9:61" parsed="|Luke|9|61|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.61" />
<sup>61</sup>Na mtu mwingine akamwambia, "Nitakufuata, lakini niruhusu kwanza nikawaage wale walio nyumbani kwangu."
<scripture passage="Luke 9:62" parsed="|Luke|9|62|0|0" osisRef="Bible:Luke.9.62" />
<sup>62</sup>Yesu akamwambia, "Yeyote anayeshika jembe tayari kulima na huku anaangalia nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu."
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 10" progress="26.01%" prev="Luke.9" next="Luke.11" id="Luke.10">
<h3 id="Luke.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Luke.10-p1">
<scripture passage="Luke 10:1" parsed="|Luke|10|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
<scripture passage="Luke 10:2" parsed="|Luke|10|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.2" />
<sup>2</sup>Akawaambia, "Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
<scripture passage="Luke 10:3" parsed="|Luke|10|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.3" />
<sup>3</sup>Sasa nendeni; fahamuni kwamba ninawatuma ninyi kama kondoo wanaokwenda kati ya mbwa mwitu.
<scripture passage="Luke 10:4" parsed="|Luke|10|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.4" />
<sup>4</sup>Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani.
<scripture passage="Luke 10:5" parsed="|Luke|10|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.5" />
<sup>5</sup>Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: `Amani iwe katika nyumba hii!`
<scripture passage="Luke 10:6" parsed="|Luke|10|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.6" />
<sup>6</sup>Kama akiwako mwenye kupenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
<scripture passage="Luke 10:7" parsed="|Luke|10|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.7" />
<sup>7</sup>Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
<scripture passage="Luke 10:8" parsed="|Luke|10|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.8" />
<sup>8</sup>Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni.
<scripture passage="Luke 10:9" parsed="|Luke|10|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.9" />
<sup>9</sup>Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieni watu: `Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu.`
<scripture passage="Luke 10:10" parsed="|Luke|10|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.10" />
<sup>10</sup>Lakini mkiingia katika mji wowote, wasipowakaribisheni, tokeni; nanyi mpitapo katika barabara zao semeni:
<scripture passage="Luke 10:11" parsed="|Luke|10|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.11" />
<sup>11</sup>`Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu tunawakung`utieni. Lakini, jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.`
<scripture passage="Luke 10:12" parsed="|Luke|10|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.12" />
<sup>12</sup>Hakika nawaambieni, siku ile mji huo utapata adhabu kubwa zaidi kuliko ile ya watu wa Sodoma.
<scripture passage="Luke 10:13" parsed="|Luke|10|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.13" />
<sup>13</sup>"Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo, na kukaa katika majivu kuonyesha kwamba wametubu.
<scripture passage="Luke 10:14" parsed="|Luke|10|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.14" />
<sup>14</sup>Hata hivyo, Siku ya Hukumu ninyi mtapata adhabu kubwa zaidi kuliko ile ya watu wa Tiro na Sidoni.
<scripture passage="Luke 10:15" parsed="|Luke|10|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.15" />
<sup>15</sup>Na wewe Kafarnaumu, unataka kujikweza mpaka mbinguni? La; utaporomoshwa mpaka Kuzimu."
<scripture passage="Luke 10:16" parsed="|Luke|10|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.16" />
<sup>16</sup>Halafu akasema, "Anayewasikiliza ninyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi. Yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma."
<scripture passage="Luke 10:17" parsed="|Luke|10|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.17" />
<sup>17</sup>Baadaye, wale sabini na wawili walirudi wamejaa furaha, wakisema, "Bwana, hata pepo wametutii tulipolitaja jina lako."
<scripture passage="Luke 10:18" parsed="|Luke|10|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.18" />
<sup>18</sup>Yeye akawaambia, "Nilimwona Shetani jinsi alivyokuwa anaporomoka kama umeme kutoka mbinguni.
<scripture passage="Luke 10:19" parsed="|Luke|10|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.19" />
<sup>19</sup>Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng`e, na uwezo juu ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.
<scripture passage="Luke 10:20" parsed="|Luke|10|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.20" />
<sup>20</sup>Hata hivyo, msifurahi kwa sababu pepo wamewatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni." ic
<scripture passage="Luke 10:21" parsed="|Luke|10|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.21" />
<sup>21</sup>Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, "Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza."
<scripture passage="Luke 10:22" parsed="|Luke|10|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.22" />
<sup>22</sup>Kisha akasema, "Baba yangu ameweka yote mikononi mwangu. Hakuna amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala amjuaye Baba ni nani ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anataka kumfunulia hayo."
<scripture passage="Luke 10:23" parsed="|Luke|10|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.23" />
<sup>23</sup>Halafu akawaelekea wafuasi wake akawaambia, "Heri wanaoona yale mnayoyaona ninyi!
<scripture passage="Luke 10:24" parsed="|Luke|10|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.24" />
<sup>24</sup>Hakika, manabii na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona ninyi wasiyaone, na kusikia yale mnayoyasikia wasiyasikie."
<scripture passage="Luke 10:25" parsed="|Luke|10|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.25" />
<sup>25</sup>Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, "Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?"
<scripture passage="Luke 10:26" parsed="|Luke|10|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.26" />
<sup>26</sup>Yesu akamwuliza, "Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?"
<scripture passage="Luke 10:27" parsed="|Luke|10|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.27" />
<sup>27</sup>Akamjibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
<scripture passage="Luke 10:28" parsed="|Luke|10|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.28" />
<sup>28</sup>Yesu akawaambia, "Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi."
<scripture passage="Luke 10:29" parsed="|Luke|10|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.29" />
<sup>29</sup>Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, "Na jirani yangu ni nani?"
<scripture passage="Luke 10:30" parsed="|Luke|10|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.30" />
<sup>30</sup>Yesu akamjibu, "Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyang`anya mali yake na kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu.
<scripture passage="Luke 10:31" parsed="|Luke|10|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.31" />
<sup>31</sup>Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
<scripture passage="Luke 10:32" parsed="|Luke|10|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.32" />
<sup>32</sup>Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali akamwona, akapita kando.
<scripture passage="Luke 10:33" parsed="|Luke|10|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.33" />
<sup>33</sup>Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma.
<scripture passage="Luke 10:34" parsed="|Luke|10|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.34" />
<sup>34</sup>Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai; na kuyafunga halafu akampandisha juu ya punda wake akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamuuguza.
<scripture passage="Luke 10:35" parsed="|Luke|10|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.35" />
<sup>35</sup>Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, `Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi."`
<scripture passage="Luke 10:36" parsed="|Luke|10|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.36" />
<sup>36</sup>Kisha Yesu akauliza, "Kati ya hao watatu, ni yupi aliyeonyesha kuwa jirani yake yule aliyevamiwa na majambazi?"
<scripture passage="Luke 10:37" parsed="|Luke|10|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.37" />
<sup>37</sup>Yule mwalimu wa Sheria akamjibu, "Ni yule aliyemwonea huruma." Yesu akamwambia, "Nenda ukafanye vivyo hivyo."
<scripture passage="Luke 10:38" parsed="|Luke|10|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.38" />
<sup>38</sup>Walipokuwa safarini, waliingia katika kijiji kimoja na mwanamke mmoja, aitwaye Martha, alimkaribisha nyumbani kwake.
<scripture passage="Luke 10:39" parsed="|Luke|10|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.39" />
<sup>39</sup>Martha alikuwa na dada yake aitwaye Maria; huyu aliketi karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
<scripture passage="Luke 10:40" parsed="|Luke|10|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.40" />
<sup>40</sup>Lakini Martha alikuwa anashughulika na mambo mengi. Basi, akamwendea Yesu, akamwambia, "Bwana, hivi hujali kwamba dada yangu ameniacha nishughulike peke yangu? Mwambie basi, anisaidie."
<scripture passage="Luke 10:41" parsed="|Luke|10|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.41" />
<sup>41</sup>Lakini Bwana akamjibu, "Martha, Martha, unahangaika na kusumbuka kwa mambo mengi.
<scripture passage="Luke 10:42" parsed="|Luke|10|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.10.42" />
<sup>42</sup>Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho hakuna mtu atakayemnyag`anya."
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 11" progress="26.54%" prev="Luke.10" next="Luke.12" id="Luke.11">
<h3 id="Luke.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Luke.11-p1">
<scripture passage="Luke 11:1" parsed="|Luke|11|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.1" />
<sup>1</sup>Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akisali. Alipomaliza kusali, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, "Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kama Yohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake."
<scripture passage="Luke 11:2" parsed="|Luke|11|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.2" />
<sup>2</sup>Yesu akawaambia, "Mnaposali, semeni: `Baba! Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike.
<scripture passage="Luke 11:3" parsed="|Luke|11|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.3" />
<sup>3</sup>Utupe daima chakula chetu cha kila siku.
<scripture passage="Luke 11:4" parsed="|Luke|11|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.4" />
<sup>4</sup>Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu."`
<scripture passage="Luke 11:5" parsed="|Luke|11|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.5" />
<sup>5</sup>Kisha akawaambia, "Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: `Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
<scripture passage="Luke 11:6" parsed="|Luke|11|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.6" />
<sup>6</sup>kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.`
<scripture passage="Luke 11:7" parsed="|Luke|11|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.7" />
<sup>7</sup>Naye, akiwa ndani angemjibu: `Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!`
<scripture passage="Luke 11:8" parsed="|Luke|11|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.8" />
<sup>8</sup>Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji.
<scripture passage="Luke 11:9" parsed="|Luke|11|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.9" />
<sup>9</sup>Kwa hiyo, ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa.
<scripture passage="Luke 11:10" parsed="|Luke|11|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.10" />
<sup>10</sup>Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye hufunguliwa.
<scripture passage="Luke 11:11" parsed="|Luke|11|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.11" />
<sup>11</sup>Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?
<scripture passage="Luke 11:12" parsed="|Luke|11|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.12" />
<sup>12</sup>Na kama akimwomba yai, je, atampa ng`e?
<scripture passage="Luke 11:13" parsed="|Luke|11|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.13" />
<sup>13</sup>Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba."
<scripture passage="Luke 11:14" parsed="|Luke|11|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.14" />
<sup>14</sup>Siku moja Yesu alikuwa anamfukuza pepo aliyemfanya mtu mmoja kuwa bubu. Basi, huyo pepo alipomtoka, yule mtu akaweza kuongea hata umati wa watu ukashangaa.
<scripture passage="Luke 11:15" parsed="|Luke|11|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.15" />
<sup>15</sup>Lakini baadhi ya watu hao wakasema, "Anamfukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo."
<scripture passage="Luke 11:16" parsed="|Luke|11|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.16" />
<sup>16</sup>Wengine, wakimjaribu, wakamtaka afanye ishara kuonyesha kama alikuwa na idhini kutoka mbinguni.
<scripture passage="Luke 11:17" parsed="|Luke|11|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.17" />
<sup>17</sup>Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, "Ufalme wowote uliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yeyote inayofarakana huangamia.
<scripture passage="Luke 11:18" parsed="|Luke|11|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.18" />
<sup>18</sup>Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje? Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
<scripture passage="Luke 11:19" parsed="|Luke|11|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.19" />
<sup>19</sup>Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu ninyi.
<scripture passage="Luke 11:20" parsed="|Luke|11|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.20" />
<sup>20</sup>Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Mungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
<scripture passage="Luke 11:21" parsed="|Luke|11|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.21" />
<sup>21</sup>"Mtu mwenye nguvu anapolinda jumba lake kwa silaha, mali yake yote iko salama.
<scripture passage="Luke 11:22" parsed="|Luke|11|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.22" />
<sup>22</sup>Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
<scripture passage="Luke 11:23" parsed="|Luke|11|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.23" />
<sup>23</sup>Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
<scripture passage="Luke 11:24" parsed="|Luke|11|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.24" />
<sup>24</sup>"Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu fulani, huzururazurura jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata, hujisemea: `Nitarudi kwenye makao yangu nilikotoka.`
<scripture passage="Luke 11:25" parsed="|Luke|11|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.25" />
<sup>25</sup>Anaporudi, huikuta ile nyumba imefagiwa na kupambwa.
<scripture passage="Luke 11:26" parsed="|Luke|11|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.26" />
<sup>26</sup>Basi, huenda na kuwachukua pepo wengine saba waovu zaidi kuliko yeye; wote huenda na kumwingia mtu yule. Hivyo, basi hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya zaidi kuliko pale mwanzo."
<scripture passage="Luke 11:27" parsed="|Luke|11|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.27" />
<sup>27</sup>Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu, akasema kwa sauti kubwa: "Heri tumbo lililokuzaa, na maziwa yaliyokunyonyesha!"
<scripture passage="Luke 11:28" parsed="|Luke|11|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.28" />
<sup>28</sup>Lakini Yesu akasema, "Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika."
<scripture passage="Luke 11:29" parsed="|Luke|11|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.29" />
<sup>29</sup>Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, "Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona.
<scripture passage="Luke 11:30" parsed="|Luke|11|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.30" />
<sup>30</sup>Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana wa Mtu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki.
<scripture passage="Luke 11:31" parsed="|Luke|11|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.31" />
<sup>31</sup>Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atashuhudia kwamba kina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni; kumbe hapa pana mkuu zaidi kuliko Solomoni.
<scripture passage="Luke 11:32" parsed="|Luke|11|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.32" />
<sup>32</sup>Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, na watashuhudia kwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu wa Ninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona!
<scripture passage="Luke 11:33" parsed="|Luke|11|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.33" />
<sup>33</sup>"Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa pishi, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
<scripture passage="Luke 11:34" parsed="|Luke|11|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.34" />
<sup>34</sup>Jicho lako ni kama taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.
<scripture passage="Luke 11:35" parsed="|Luke|11|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.35" />
<sup>35</sup>Uwe mwangalifu basi mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.
<scripture passage="Luke 11:36" parsed="|Luke|11|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.36" />
<sup>36</sup>Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utang`aa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake."
<scripture passage="Luke 11:37" parsed="|Luke|11|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.37" />
<sup>37</sup>Yesu alipokuwa akiongea, Mfarisayo mmoja alimkaribisha chakula nyumbani kwake, naye akaenda, akaketi kula chakula.
<scripture passage="Luke 11:38" parsed="|Luke|11|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.38" />
<sup>38</sup>Huyo Mfarisayo alistaajabu kuona kwamba alikula chakula bila kunawa.
<scripture passage="Luke 11:39" parsed="|Luke|11|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.39" />
<sup>39</sup>Bwana akamwambia, "Ninyi Mafarisayo huosha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu.
<scripture passage="Luke 11:40" parsed="|Luke|11|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.40" />
<sup>40</sup>Wapumbavu ninyi! Je, aliyetengeneza nje si ndiye aliyetengeneza ndani pia?
<scripture passage="Luke 11:41" parsed="|Luke|11|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.41" />
<sup>41</sup>Toeni kwa maskini vile vitu vilivyomo ndani, na vingine vyote vitakuwa halali kwenu.
<scripture passage="Luke 11:42" parsed="|Luke|11|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.42" />
<sup>42</sup>"Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoza watu zaka hata juu ya majani ya kukolezea chakula, mchicha na majani mengine, na huku hamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu. Mambo haya iliwapasa muwe mmeyazingatia bila kuyasahau yale mengine.
<scripture passage="Luke 11:43" parsed="|Luke|11|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.43" />
<sup>43</sup>"Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima hadharani.
<scripture passage="Luke 11:44" parsed="|Luke|11|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.44" />
<sup>44</sup>Ole wenu, kwa sababu mko kama makaburi yaliyofichika; watu hutembea juu yake bila kufahamu."
<scripture passage="Luke 11:45" parsed="|Luke|11|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.45" />
<sup>45</sup>Mmoja wa walimu wa Sheria akamwambia, "Mwalimu, maneno yako yanatukashifu na sisi pia."
<scripture passage="Luke 11:46" parsed="|Luke|11|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.46" />
<sup>46</sup>Yesu akamjibu, "Na ninyi walimu wa Sheria, ole wenu; maana mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshi hata kidole kuwasaidia.
<scripture passage="Luke 11:47" parsed="|Luke|11|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.47" />
<sup>47</sup>Ole wenu, kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii wale ambao wazee wenu waliwaua.
<scripture passage="Luke 11:48" parsed="|Luke|11|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.48" />
<sup>48</sup>Kwa hiyo mnashuhudia na kukubaliana na matendo ya wazee wenu; maana wao waliwaua hao manabii, nanyi mnajenga makaburi yao.
<scripture passage="Luke 11:49" parsed="|Luke|11|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.49" />
<sup>49</sup>Kwa hiyo, Hekima ya Mungu ilisema hivi: `Nitawapelekea manabii na mitume, lakini watawaua baadhi yao, na kuwatesa wengine.`
<scripture passage="Luke 11:50" parsed="|Luke|11|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.50" />
<sup>50</sup>Matokeo yake ni kwamba kizazi hiki kitaadhibiwa kwa sababu ya damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa ulimwengu;
<scripture passage="Luke 11:51" parsed="|Luke|11|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.51" />
<sup>51</sup>tangu kumwagwa damu ya Abeli mpaka kifo cha Zakariya ambaye walimuua kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, hakika kizazi hiki kitaadhibiwa kwa matendo haya.
<scripture passage="Luke 11:52" parsed="|Luke|11|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.52" />
<sup>52</sup>"Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia waliokuwa wanaingia wasiingie."
<scripture passage="Luke 11:53" parsed="|Luke|11|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.53" />
<sup>53</sup>Alipokuwa akitoka pale, wale Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kumshambulia vikali na kumsonga kwa maswali mengi
<scripture passage="Luke 11:54" parsed="|Luke|11|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.11.54" />
<sup>54</sup>ili wapate kumnasa kwa maneno yake.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 12" progress="27.21%" prev="Luke.11" next="Luke.13" id="Luke.12">
<h3 id="Luke.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Luke.12-p1">
<scripture passage="Luke 12:1" parsed="|Luke|12|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.1" />
<sup>1</sup>Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, "Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.
<scripture passage="Luke 12:2" parsed="|Luke|12|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.2" />
<sup>2</sup>Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichika kitafichuliwa.
<scripture passage="Luke 12:3" parsed="|Luke|12|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.3" />
<sup>3</sup>Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonong`ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
<scripture passage="Luke 12:4" parsed="|Luke|12|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.4" />
<sup>4</sup>"Nawaambieni ninyi rafiki zangu: msiwaogope wale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi.
<scripture passage="Luke 12:5" parsed="|Luke|12|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.5" />
<sup>5</sup>Nitawaonyesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.
<scripture passage="Luke 12:6" parsed="|Luke|12|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.6" />
<sup>6</sup>Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
<scripture passage="Luke 12:7" parsed="|Luke|12|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.7" />
<sup>7</sup>Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope, basi, ninyi mna thamani zaidi kuliko shomoro wengi!
<scripture passage="Luke 12:8" parsed="|Luke|12|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.8" />
<sup>8</sup>"Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.
<scripture passage="Luke 12:9" parsed="|Luke|12|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.9" />
<sup>9</sup>Lakini, mtu yeyote anayenikana mbele ya watu, naye atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
<scripture passage="Luke 12:10" parsed="|Luke|12|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.10" />
<sup>10</sup>"Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa; lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
<scripture passage="Luke 12:11" parsed="|Luke|12|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.11" />
<sup>11</sup>"Watakapowapeleka ninyi mbele ya masunagogi na mbele ya wakuu na watawala msiwe na wasiwasi juu ya jinsi mtakavyojitetea au jinsi mtakavyosema.
<scripture passage="Luke 12:12" parsed="|Luke|12|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.12" />
<sup>12</sup>Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile mnachopaswa kusema."
<scripture passage="Luke 12:13" parsed="|Luke|12|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.13" />
<sup>13</sup>Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, "Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba."
<scripture passage="Luke 12:14" parsed="|Luke|12|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.14" />
<sup>14</sup>Yesu akamjibu, "Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi mwamuzi au msuluhishi kati yenu?"
<scripture passage="Luke 12:15" parsed="|Luke|12|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.15" />
<sup>15</sup>Basi, akawaambia wote, "Jihadharini na kila aina ya tamaa; maana uzima wa mtu hautegemei wingi wa vitu alivyo navyo."
<scripture passage="Luke 12:16" parsed="|Luke|12|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.16" />
<sup>16</sup>Kisha akawaambia mfano: "Kulikuwa na tajiri mmoja ambaye shamba lake lilizaa mavuno mengi.
<scripture passage="Luke 12:17" parsed="|Luke|12|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.17" />
<sup>17</sup>Tajiri huyo akafikiri moyoni mwake: `Nitafanyaje nami sina mahali pa kuhifadhia mavuno yangu?
<scripture passage="Luke 12:18" parsed="|Luke|12|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.18" />
<sup>18</sup>Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, na humo nitahifadhi mavuno yangu yote na mali yangu.
<scripture passage="Luke 12:19" parsed="|Luke|12|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.19" />
<sup>19</sup>Hapo nitaweza kuiambia roho yangu: sasa unayo akiba ya matumizi kwa miaka na miaka. Ponda mali, ule, unywe na kufurahi.`
<scripture passage="Luke 12:20" parsed="|Luke|12|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.20" />
<sup>20</sup>Lakini Mungu akamwambia: `Mpumbavu wewe; leo usiku roho yako itachukuliwa. Na vitu vile vyote ulivyojilundikia vitakuwa vya nani?"`
<scripture passage="Luke 12:21" parsed="|Luke|12|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.21" />
<sup>21</sup>Yesu akamaliza kwa kusema "Ndivyo ilivyo kwa mtu anayejilundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu."
<scripture passage="Luke 12:22" parsed="|Luke|12|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.22" />
<sup>22</sup>Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kwa sababu hiyo nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula mnachohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu.
<scripture passage="Luke 12:23" parsed="|Luke|12|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.23" />
<sup>23</sup>Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, na mwili ni bora kuliko mavazi.
<scripture passage="Luke 12:24" parsed="|Luke|12|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.24" />
<sup>24</sup>Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Ninyi mna thamani zaidi kuliko ndege!
<scripture passage="Luke 12:25" parsed="|Luke|12|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.25" />
<sup>25</sup>Ni nani kati yenu kwa kuwa na wasiwasi anaweza kuongeza urefu wa maisha yake?
<scripture passage="Luke 12:26" parsed="|Luke|12|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.26" />
<sup>26</sup>Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini kuwa na wasiwasi juu ya yale mengine?
<scripture passage="Luke 12:27" parsed="|Luke|12|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.27" />
<sup>27</sup>Angalieni maua jinsi yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayafumi. Hata hivyo, nawahakikishieni kwamba hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
<scripture passage="Luke 12:28" parsed="|Luke|12|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.28" />
<sup>28</sup>Lakini, kama Mungu hulivika vizuri jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatawafanyia ninyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!
<scripture passage="Luke 12:29" parsed="|Luke|12|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.29" />
<sup>29</sup>"Basi, msivurugike akili, mkihangaika daima juu ya mtakachokula au mtakachokunywa.
<scripture passage="Luke 12:30" parsed="|Luke|12|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.30" />
<sup>30</sup>Kwa maana hayo yote ndiyo yanayohangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
<scripture passage="Luke 12:31" parsed="|Luke|12|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.31" />
<sup>31</sup>Shughulikieni kwanza Ufalme wa Mungu, na hayo yote mtapewa kwa ziada.
<scripture passage="Luke 12:32" parsed="|Luke|12|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.32" />
<sup>32</sup>"Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni Ufalme.
<scripture passage="Luke 12:33" parsed="|Luke|12|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.33" />
<sup>33</sup>Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
<scripture passage="Luke 12:34" parsed="|Luke|12|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.34" />
<sup>34</sup>Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
<scripture passage="Luke 12:35" parsed="|Luke|12|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.35" />
<sup>35</sup>"Muwe tayari! Jifungeni mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka;
<scripture passage="Luke 12:36" parsed="|Luke|12|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.36" />
<sup>36</sup>muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka arusini, ili wamfungulie mara atakapobisha hodi.
<scripture passage="Luke 12:37" parsed="|Luke|12|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.37" />
<sup>37</sup>Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
<scripture passage="Luke 12:38" parsed="|Luke|12|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.38" />
<sup>38</sup>Heri yao watumishi hao ikiwa bwana wao atawakuta wanakesha hata ikiwa atarudi usiku wa manane au alfajiri.
<scripture passage="Luke 12:39" parsed="|Luke|12|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.39" />
<sup>39</sup>Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua saa ambayo mwizi atakuja, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
<scripture passage="Luke 12:40" parsed="|Luke|12|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.40" />
<sup>40</sup>Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia."
<scripture passage="Luke 12:41" parsed="|Luke|12|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.41" />
<sup>41</sup>Petro akamwambia, "Bwana, mfano huo ni kwa ajili yetu tu, au ni kwa ajili ya watu wote?"
<scripture passage="Luke 12:42" parsed="|Luke|12|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.42" />
<sup>42</sup>Bwana akajibu, "Ni nani basi, mtumishi aliye mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?
<scripture passage="Luke 12:43" parsed="|Luke|12|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.43" />
<sup>43</sup>Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.
<scripture passage="Luke 12:44" parsed="|Luke|12|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.44" />
<sup>44</sup>Hakika atampa madaraka juu ya mali yake yote.
<scripture passage="Luke 12:45" parsed="|Luke|12|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.45" />
<sup>45</sup>Lakini, kama mtumishi huyo atafikiri moyoni mwake: na kusema: `Bwana wangu amekawia sana kurudi` halafu aanze kuwapiga watumishi wenzake, wa kiume au wa kike, na kula, kunywa na kulewa,
<scripture passage="Luke 12:46" parsed="|Luke|12|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.46" />
<sup>46</sup>bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamkatilia mbali na kumweka fungu moja na wasioamini.<i>fb</i>
<scripture passage="Luke 12:47" parsed="|Luke|12|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.47" />
<sup>47</sup>Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
<scripture passage="Luke 12:48" parsed="|Luke|12|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.48" />
<sup>48</sup>Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atatakiwa vingi; aliyekabidhiwa vingi zaidi atatakiwa kutoa vingi zaidi.
<scripture passage="Luke 12:49" parsed="|Luke|12|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.49" />
<sup>49</sup>"Nimekuja kuwasha moto duniani, laiti ungekuwa umewaka tayari!
<scripture passage="Luke 12:50" parsed="|Luke|12|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.50" />
<sup>50</sup>Ninao ubatizo ambao inanipasa niupokee; jinsi gani ninavyohangaika mpaka ukamilike!
<scripture passage="Luke 12:51" parsed="|Luke|12|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.51" />
<sup>51</sup>Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Hata kidogo; si amani bali utengano.
<scripture passage="Luke 12:52" parsed="|Luke|12|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.52" />
<sup>52</sup>Na tangu sasa, jamaa ya watu watano itagawanyika; watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu.
<scripture passage="Luke 12:53" parsed="|Luke|12|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.53" />
<sup>53</sup>Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mama mkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mama mkwe wake."
<scripture passage="Luke 12:54" parsed="|Luke|12|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.54" />
<sup>54</sup>Yesu akayaambia tena makundi ya watu, "Mnapoona mawingu yakitokea upande wa magharibi, mara mwasema: `Mvua itanyesha`, na kweli hunyesha.
<scripture passage="Luke 12:55" parsed="|Luke|12|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.55" />
<sup>55</sup>Mnapoona upepo wa kusi unavuma, mwasema `Kutakuwa na hali ya joto` na ndivyo inavyokuwa.
<scripture passage="Luke 12:56" parsed="|Luke|12|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.56" />
<sup>56</sup>Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia dunia na anga; kwa nini basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?
<scripture passage="Luke 12:57" parsed="|Luke|12|57|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.57" />
<sup>57</sup>"Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya?
<scripture passage="Luke 12:58" parsed="|Luke|12|58|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.58" />
<sup>58</sup>Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
<scripture passage="Luke 12:59" parsed="|Luke|12|59|0|0" osisRef="Bible:Luke.12.59" />
<sup>59</sup>Hakika hutatoka huko nakwambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho."
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 13" progress="27.92%" prev="Luke.12" next="Luke.14" id="Luke.13">
<h3 id="Luke.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Luke.13-p1">
<scripture passage="Luke 13:1" parsed="|Luke|13|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.1" />
<sup>1</sup>Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
<scripture passage="Luke 13:2" parsed="|Luke|13|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.2" />
<sup>2</sup>Naye Yesu akawaambia, "Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo?
<scripture passage="Luke 13:3" parsed="|Luke|13|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.3" />
<sup>3</sup>Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao.
<scripture passage="Luke 13:4" parsed="|Luke|13|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.4" />
<sup>4</sup>Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
<scripture passage="Luke 13:5" parsed="|Luke|13|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.5" />
<sup>5</sup>Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao."
<scripture passage="Luke 13:6" parsed="|Luke|13|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.6" />
<sup>6</sup>Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: "Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
<scripture passage="Luke 13:7" parsed="|Luke|13|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.7" />
<sup>7</sup>Basi, akamwambia mfanyakazi wake: `Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?`
<scripture passage="Luke 13:8" parsed="|Luke|13|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.8" />
<sup>8</sup>Lakini naye akamjibu: `Bwana, tuuache tena mwaka huu; nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea.
<scripture passage="Luke 13:9" parsed="|Luke|13|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.9" />
<sup>9</sup>Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata."`
<scripture passage="Luke 13:10" parsed="|Luke|13|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.10" />
<sup>10</sup>Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato.
<scripture passage="Luke 13:11" parsed="|Luke|13|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.11" />
<sup>11</sup>Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
<scripture passage="Luke 13:12" parsed="|Luke|13|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.12" />
<sup>12</sup>Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, "Mama, umeponywa ugonjwa wako."
<scripture passage="Luke 13:13" parsed="|Luke|13|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.13" />
<sup>13</sup>Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu.
<scripture passage="Luke 13:14" parsed="|Luke|13|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.14" />
<sup>14</sup>Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, "Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato."
<scripture passage="Luke 13:15" parsed="|Luke|13|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.15" />
<sup>15</sup>Hapo Bwana akamjibu, "Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng`ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
<scripture passage="Luke 13:16" parsed="|Luke|13|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.16" />
<sup>16</sup>Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?"
<scripture passage="Luke 13:17" parsed="|Luke|13|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.17" />
<sup>17</sup>Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.
<scripture passage="Luke 13:18" parsed="|Luke|13|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.18" />
<sup>18</sup>Yesu akauliza: "Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini?
<scripture passage="Luke 13:19" parsed="|Luke|13|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.19" />
<sup>19</sup>NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake."
<scripture passage="Luke 13:20" parsed="|Luke|13|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.20" />
<sup>20</sup>Tena akauliza: "Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini?
<scripture passage="Luke 13:21" parsed="|Luke|13|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.21" />
<sup>21</sup>Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote."
<scripture passage="Luke 13:22" parsed="|Luke|13|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.22" />
<sup>22</sup>Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
<scripture passage="Luke 13:23" parsed="|Luke|13|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.23" />
<sup>23</sup>Mtu mmoja akamwuliza, "Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?"
<scripture passage="Luke 13:24" parsed="|Luke|13|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.24" />
<sup>24</sup>Yesu akawaambia, "Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.
<scripture passage="Luke 13:25" parsed="|Luke|13|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.25" />
<sup>25</sup>"Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Ninyi mtasimama nje na kuanza kupiga hodi mkisema: `Bwana, tufungulie mlango.` Lakini yeye atawajibu: `Sijui mmetoka wapi.`
<scripture passage="Luke 13:26" parsed="|Luke|13|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.26" />
<sup>26</sup>Nanyi mtaanza kumwambia: `Sisi ndio wale tuliokula na kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu.`
<scripture passage="Luke 13:27" parsed="|Luke|13|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.27" />
<sup>27</sup>Lakini yeye atasema: `Sijui ninyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu.`
<scripture passage="Luke 13:28" parsed="|Luke|13|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.28" />
<sup>28</sup>Ndipo mtakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo, na manabii wote wapo katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje!
<scripture passage="Luke 13:29" parsed="|Luke|13|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.29" />
<sup>29</sup>Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Ufalme wa Mungu.
<scripture passage="Luke 13:30" parsed="|Luke|13|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.30" />
<sup>30</sup>Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa kwanza watakuwa wa mwisho."
<scripture passage="Luke 13:31" parsed="|Luke|13|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.31" />
<sup>31</sup>Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, "Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua."
<scripture passage="Luke 13:32" parsed="|Luke|13|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.32" />
<sup>32</sup>Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: `Leo na kesho ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu.`
<scripture passage="Luke 13:33" parsed="|Luke|13|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.33" />
<sup>33</sup>Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 13:34" parsed="|Luke|13|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.34" />
<sup>34</sup>"Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, Lakini wewe umekataa.
<scripture passage="Luke 13:35" parsed="|Luke|13|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.13.35" />
<sup>35</sup>Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Naam, hakika nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: `Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."`
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 14" progress="28.40%" prev="Luke.13" next="Luke.15" id="Luke.14">
<h3 id="Luke.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Luke.14-p1">
<scripture passage="Luke 14:1" parsed="|Luke|14|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.1" />
<sup>1</sup>Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
<scripture passage="Luke 14:2" parsed="|Luke|14|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.2" />
<sup>2</sup>Mbele yake Yesu palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa kuvimba mwili.
<scripture passage="Luke 14:3" parsed="|Luke|14|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, "Je, ni halali au la kumponya mtu siku ya sabato?"
<scripture passage="Luke 14:4" parsed="|Luke|14|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.4" />
<sup>4</sup>Lakini wao wakakaa kimya. Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya, akamwacha aende zake.
<scripture passage="Luke 14:5" parsed="|Luke|14|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.5" />
<sup>5</sup>Halafu akawaambia, "Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng`ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?"
<scripture passage="Luke 14:6" parsed="|Luke|14|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.6" />
<sup>6</sup>Nao hawakuweza kumjibu swali hilo.
<scripture passage="Luke 14:7" parsed="|Luke|14|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.7" />
<sup>7</sup>Yesu aliona jinsi wale walioalikwa walivyokuwa wanajichagulia nafasi za heshima, akawaambia mfano:
<scripture passage="Luke 14:8" parsed="|Luke|14|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.8" />
<sup>8</sup>"Kama mtu akikualika arusini, usiketi mahali pa heshima isije ikawa amealikwa mwingine mheshimiwa kuliko wewe;
<scripture passage="Luke 14:9" parsed="|Luke|14|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.9" />
<sup>9</sup>na mwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na kukwambia: `Mwachie huyu nafasi.` Hapo utaaibika mbele ya wote na kulazimika kwenda kuchukua nafasi ya mwisho.
<scripture passage="Luke 14:10" parsed="|Luke|14|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.10" />
<sup>10</sup>Bali ukialikwa kwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ili mwenyeji wako atakapokuja akwambie: `Rafiki, njoo hapa mbele, mahali pazuri zaidi.` Hapo utakuwa umeheshimika mbele ya wote wanaoketi pamoja nawe.
<scripture passage="Luke 14:11" parsed="|Luke|14|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.11" />
<sup>11</sup>Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha, atakwezwa."
<scripture passage="Luke 14:12" parsed="|Luke|14|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.12" />
<sup>12</sup>Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, "Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri, wasije nao wakakualika nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.
<scripture passage="Luke 14:13" parsed="|Luke|14|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.13" />
<sup>13</sup>Badala yake, unapofanya karamu, waalike maskini, vilema viwete na vipofu,
<scripture passage="Luke 14:14" parsed="|Luke|14|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.14" />
<sup>14</sup>nawe utakuwa umepata baraka, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa. Maana Mungu atakupa tuzo lako wakati watu wema watakapofufuka."
<scripture passage="Luke 14:15" parsed="|Luke|14|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.15" />
<sup>15</sup>Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, "Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Luke 14:16" parsed="|Luke|14|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.16" />
<sup>16</sup>Yesu akamjibu, "Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi.
<scripture passage="Luke 14:17" parsed="|Luke|14|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.17" />
<sup>17</sup>Wakati wa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wake awaambie walioalikwa, `Njoni, kila kitu ni tayari.`
<scripture passage="Luke 14:18" parsed="|Luke|14|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.18" />
<sup>18</sup>Lakini wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: `Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.`
<scripture passage="Luke 14:19" parsed="|Luke|14|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.19" />
<sup>19</sup>Mwingine akasema: `Nimenunua ng`ombe jozi tano wa kulima; sasa nimo njiani kwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.`
<scripture passage="Luke 14:20" parsed="|Luke|14|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.20" />
<sup>20</sup>Na mwingine akasema: `Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.`
<scripture passage="Luke 14:21" parsed="|Luke|14|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.21" />
<sup>21</sup>Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: `Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na waliolemaa.`
<scripture passage="Luke 14:22" parsed="|Luke|14|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.22" />
<sup>22</sup>Baadaye, mtumishi huyo akasema: `Bwana mambo yamefanyika kama ulivyoamuru, lakini bado iko nafasi.`
<scripture passage="Luke 14:23" parsed="|Luke|14|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.23" />
<sup>23</sup>Yule bwana akamwambia mtumishi: `Nenda katika barabara na vichochoro vya mji uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.
<scripture passage="Luke 14:24" parsed="|Luke|14|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.24" />
<sup>24</sup>Kwa maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeonja karamu yangu."`
<scripture passage="Luke 14:25" parsed="|Luke|14|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.25" />
<sup>25</sup>Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi, akawageukia akawaambia,
<scripture passage="Luke 14:26" parsed="|Luke|14|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.26" />
<sup>26</sup>"Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
<scripture passage="Luke 14:27" parsed="|Luke|14|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.27" />
<sup>27</sup>Mtu asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
<scripture passage="Luke 14:28" parsed="|Luke|14|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.28" />
<sup>28</sup>Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
<scripture passage="Luke 14:29" parsed="|Luke|14|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.29" />
<sup>29</sup>La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka
<scripture passage="Luke 14:30" parsed="|Luke|14|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.30" />
<sup>30</sup>wakisema: `Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.`
<scripture passage="Luke 14:31" parsed="|Luke|14|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.31" />
<sup>31</sup>"Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfu ishirini?
<scripture passage="Luke 14:32" parsed="|Luke|14|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.32" />
<sup>32</sup>Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
<scripture passage="Luke 14:33" parsed="|Luke|14|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.33" />
<sup>33</sup>Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho.
<scripture passage="Luke 14:34" parsed="|Luke|14|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.34" />
<sup>34</sup>"Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini?
<scripture passage="Luke 14:35" parsed="|Luke|14|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.14.35" />
<sup>35</sup>Haifai kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia mbali. Sikieni basi, kama mna masikio!"
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 15" progress="28.82%" prev="Luke.14" next="Luke.16" id="Luke.15">
<h3 id="Luke.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Luke.15-p1">
<scripture passage="Luke 15:1" parsed="|Luke|15|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.1" />
<sup>1</sup>Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.
<scripture passage="Luke 15:2" parsed="|Luke|15|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.2" />
<sup>2</sup>Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung`unika: "Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao."
<scripture passage="Luke 15:3" parsed="|Luke|15|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawajibu kwa mfano:
<scripture passage="Luke 15:4" parsed="|Luke|15|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.4" />
<sup>4</sup>"Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
<scripture passage="Luke 15:5" parsed="|Luke|15|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.5" />
<sup>5</sup>Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.
<scripture passage="Luke 15:6" parsed="|Luke|15|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.6" />
<sup>6</sup>Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake akiwaambia, `Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.`
<scripture passage="Luke 15:7" parsed="|Luke|15|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.7" />
<sup>7</sup>Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu. ic
<scripture passage="Luke 15:8" parsed="|Luke|15|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.8" />
<sup>8</sup>"Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
<scripture passage="Luke 15:9" parsed="|Luke|15|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.9" />
<sup>9</sup>Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake akisema, `Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.`
<scripture passage="Luke 15:10" parsed="|Luke|15|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.10" />
<sup>10</sup>Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu."
<scripture passage="Luke 15:11" parsed="|Luke|15|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.11" />
<sup>11</sup>Yesu akaendelea kusema, "Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana wawili.
<scripture passage="Luke 15:12" parsed="|Luke|15|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.12" />
<sup>12</sup>Yule mdogo, alimwambia baba yake: `Baba, nipe urithi wangu.` Naye akawagawia mali yake.
<scripture passage="Luke 15:13" parsed="|Luke|15|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.13" />
<sup>13</sup>Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.
<scripture passage="Luke 15:14" parsed="|Luke|15|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.14" />
<sup>14</sup>Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika.
<scripture passage="Luke 15:15" parsed="|Luke|15|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.15" />
<sup>15</sup>Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.
<scripture passage="Luke 15:16" parsed="|Luke|15|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.16" />
<sup>16</sup>Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.
<scripture passage="Luke 15:17" parsed="|Luke|15|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.17" />
<sup>17</sup>Alipoanza kupata akili akafikiri: `Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
<scripture passage="Luke 15:18" parsed="|Luke|15|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.18" />
<sup>18</sup>Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.
<scripture passage="Luke 15:19" parsed="|Luke|15|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.19" />
<sup>19</sup>Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.`
<scripture passage="Luke 15:20" parsed="|Luke|15|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.20" />
<sup>20</sup>Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
<scripture passage="Luke 15:21" parsed="|Luke|15|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.21" />
<sup>21</sup>"Mwanawe akamwambia: `Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.`
<scripture passage="Luke 15:22" parsed="|Luke|15|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.22" />
<sup>22</sup>Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: `Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!
<scripture passage="Luke 15:23" parsed="|Luke|15|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.23" />
<sup>23</sup>Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!
<scripture passage="Luke 15:24" parsed="|Luke|15|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.24" />
<sup>24</sup>Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.` Wakaanza kufanya sherehe.
<scripture passage="Luke 15:25" parsed="|Luke|15|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.25" />
<sup>25</sup>"Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani akasikia vifijo na ngoma.
<scripture passage="Luke 15:26" parsed="|Luke|15|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.26" />
<sup>26</sup>Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: `Kuna nini?`
<scripture passage="Luke 15:27" parsed="|Luke|15|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.27" />
<sup>27</sup>Huyo mtumishi akamwambia: `Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.`
<scripture passage="Luke 15:28" parsed="|Luke|15|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.28" />
<sup>28</sup>Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.
<scripture passage="Luke 15:29" parsed="|Luke|15|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.29" />
<sup>29</sup>Lakini yeye akamjibu: `Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
<scripture passage="Luke 15:30" parsed="|Luke|15|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.30" />
<sup>30</sup>Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.`
<scripture passage="Luke 15:31" parsed="|Luke|15|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.31" />
<sup>31</sup>Baba yake akamjibu: `Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako.
<scripture passage="Luke 15:32" parsed="|Luke|15|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.15.32" />
<sup>32</sup>Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana."`
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 16" progress="29.18%" prev="Luke.15" next="Luke.17" id="Luke.16">
<h3 id="Luke.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Luke.16-p1">
<scripture passage="Luke 16:1" parsed="|Luke|16|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliwaambia wanafunzi wake: "Tajiri mmoja alikuwa na karani wake. Huyu karani alichongewa kwamba alitumia ovyo mali ya tajiri wake.
<scripture passage="Luke 16:2" parsed="|Luke|16|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.2" />
<sup>2</sup>Yule tajiri akamwita akamwambia: `Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.`
<scripture passage="Luke 16:3" parsed="|Luke|16|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.3" />
<sup>3</sup>Yule karani akafikiri: `Bwana wangu amenifukuza kazi ya ukarani; nitafanya nini? Kwenda kulima siwezi; kwenda kuombaomba kama maskini ni aibu.
<scripture passage="Luke 16:4" parsed="|Luke|16|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.4" />
<sup>4</sup>Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.`
<scripture passage="Luke 16:5" parsed="|Luke|16|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.5" />
<sup>5</sup>Basi, akawaita wadeni wa bwana wake, mmoja mmoja, akamwambia yule wa kwanza: `Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?`
<scripture passage="Luke 16:6" parsed="|Luke|16|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.6" />
<sup>6</sup>Yeye akamjibu: `Mapipa mia ya mafuta ya zeituni.` Yule karani akamwambia: `Chukua hati yako ya deni, keti haraka, andika hamsini.`
<scripture passage="Luke 16:7" parsed="|Luke|16|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.7" />
<sup>7</sup>Kisha akamwuliza mdeni mwingine: `Wewe unadaiwa kiasi gani?` Yeye akamjibu: `Magunia mia ya ngano.` Yule karani akamwambia: `Chukua hati yako ya deni, andika themanini.`
<scripture passage="Luke 16:8" parsed="|Luke|16|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.8" />
<sup>8</sup>"Basi, yule bwana akamsifu huyo karani asiye mwaminifu, kwa kuwa alitumia busara. Kwa maana watu wa dunia hii wana busara zaidi na mambo yao kuliko watu wa mwanga."
<scripture passage="Luke 16:9" parsed="|Luke|16|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.9" />
<sup>9</sup>Naye Yesu akaendelea kusema, "Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, mweze kupokewa nao katika makao ya milele.
<scripture passage="Luke 16:10" parsed="|Luke|16|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.10" />
<sup>10</sup>Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
<scripture passage="Luke 16:11" parsed="|Luke|16|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.11" />
<sup>11</sup>Kama basi, ninyi si hamjawa waaminifu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli?
<scripture passage="Luke 16:12" parsed="|Luke|16|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.12" />
<sup>12</sup>Na kama hamjakuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewakabidhi mali yenu wenyewe?
<scripture passage="Luke 16:13" parsed="|Luke|16|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.13" />
<sup>13</sup>"Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali."
<scripture passage="Luke 16:14" parsed="|Luke|16|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.14" />
<sup>14</sup>Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, kwa vile wao walikuwa wanapenda sana fedha, wakamdharau Yesu.
<scripture passage="Luke 16:15" parsed="|Luke|16|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.15" />
<sup>15</sup>Hapo akawaambia, "Ninyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka.
<scripture passage="Luke 16:16" parsed="|Luke|16|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.16" />
<sup>16</sup>"Sheria na maandishi ya manabii vilikuweko mpaka wakati wa Yohane mbatizaji. Tangu hapo, Ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.
<scripture passage="Luke 16:17" parsed="|Luke|16|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.17" />
<sup>17</sup>Lakini ni rahisi zaidi mbingu na dunia kupita, kuliko hata herufi moja ya Sheria kufutwa.
<scripture passage="Luke 16:18" parsed="|Luke|16|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.18" />
<sup>18</sup>"Yeyote anayemwacha mke wake na kuoa mwingine, anazini; na yeyote anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
<scripture passage="Luke 16:19" parsed="|Luke|16|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.19" />
<sup>19</sup>"Palikuwa na mtu mmoja tajiri, ambaye alikuwa anavaa mavazi ya bei kubwa sana ya rangi ya zambarau, na ya kitani safi, na kufanya sherehe kila siku.
<scripture passage="Luke 16:20" parsed="|Luke|16|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.20" />
<sup>20</sup>Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri.
<scripture passage="Luke 16:21" parsed="|Luke|16|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.21" />
<sup>21</sup>Lazaro alitamani kula makombo yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba vidonda vyake!
<scripture passage="Luke 16:22" parsed="|Luke|16|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.22" />
<sup>22</sup>"Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua, wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.
<scripture passage="Luke 16:23" parsed="|Luke|16|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.23" />
<sup>23</sup>Huyo tajiri, alikuwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
<scripture passage="Luke 16:24" parsed="|Luke|16|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.24" />
<sup>24</sup>Basi, akaita kwa sauti: `Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.`
<scripture passage="Luke 16:25" parsed="|Luke|16|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.25" />
<sup>25</sup>Lakini Abrahamu akamjibu: `Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa.
<scripture passage="Luke 16:26" parsed="|Luke|16|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.26" />
<sup>26</sup>Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze.`
<scripture passage="Luke 16:27" parsed="|Luke|16|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.27" />
<sup>27</sup>Huyo aliyekuwa tajiri akasema: `Basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu,
<scripture passage="Luke 16:28" parsed="|Luke|16|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.28" />
<sup>28</sup>maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso.`
<scripture passage="Luke 16:29" parsed="|Luke|16|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.29" />
<sup>29</sup>Lakini Abrahamu akamwambia: `Ndugu zako wanao Mose na manabii; waache wawasikilize hao.`
<scripture passage="Luke 16:30" parsed="|Luke|16|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.30" />
<sup>30</sup>Lakini yeye akasema: `Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka kutoka wafu na kuwaendea, watatubu.`
<scripture passage="Luke 16:31" parsed="|Luke|16|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.16.31" />
<sup>31</sup>Naye Abrahamu akasema: `Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu."`
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 17" progress="29.62%" prev="Luke.16" next="Luke.18" id="Luke.17">
<h3 id="Luke.17-p0.1">Chapter 17</h3>
<p id="Luke.17-p1">
<scripture passage="Luke 17:1" parsed="|Luke|17|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.1" />
<sup>1</sup>Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
<scripture passage="Luke 17:2" parsed="|Luke|17|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.2" />
<sup>2</sup>Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
<scripture passage="Luke 17:3" parsed="|Luke|17|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.3" />
<sup>3</sup>Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.
<scripture passage="Luke 17:4" parsed="|Luke|17|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.4" />
<sup>4</sup>Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema `Nimetubu`, lazima umsamehe."
<scripture passage="Luke 17:5" parsed="|Luke|17|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.5" />
<sup>5</sup>Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani."
<scripture passage="Luke 17:6" parsed="|Luke|17|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.6" />
<sup>6</sup>Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: `Ng`oka ukajipandikize baharini`, nao ungewatii.
<scripture passage="Luke 17:7" parsed="|Luke|17|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.7" />
<sup>7</sup>"Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: `Haraka, njoo ule chakula?`
<scripture passage="Luke 17:8" parsed="|Luke|17|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.8" />
<sup>8</sup>La! Atamwambia: `Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.`
<scripture passage="Luke 17:9" parsed="|Luke|17|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.9" />
<sup>9</sup>Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?
<scripture passage="Luke 17:10" parsed="|Luke|17|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.10" />
<sup>10</sup>Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: `Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."`
<scripture passage="Luke 17:11" parsed="|Luke|17|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.11" />
<sup>11</sup>Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya.
<scripture passage="Luke 17:12" parsed="|Luke|17|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.12" />
<sup>12</sup>Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
<scripture passage="Luke 17:13" parsed="|Luke|17|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.13" />
<sup>13</sup>Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee huruma!"
<scripture passage="Luke 17:14" parsed="|Luke|17|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.14" />
<sup>14</sup>Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
<scripture passage="Luke 17:15" parsed="|Luke|17|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.15" />
<sup>15</sup>Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
<scripture passage="Luke 17:16" parsed="|Luke|17|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.16" />
<sup>16</sup>Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
<scripture passage="Luke 17:17" parsed="|Luke|17|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.17" />
<sup>17</sup>Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
<scripture passage="Luke 17:18" parsed="|Luke|17|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.18" />
<sup>18</sup>Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?"
<scripture passage="Luke 17:19" parsed="|Luke|17|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.19" />
<sup>19</sup>Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya."
<scripture passage="Luke 17:20" parsed="|Luke|17|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.20" />
<sup>20</sup>Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
<scripture passage="Luke 17:21" parsed="|Luke|17|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.21" />
<sup>21</sup>Wala hakuna atakayeweza kusema, `Uko hapa`, au `Uko pale`. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu."
<scripture passage="Luke 17:22" parsed="|Luke|17|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.22" />
<sup>22</sup>Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
<scripture passage="Luke 17:23" parsed="|Luke|17|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.23" />
<sup>23</sup>Na watu watawaambieni: `Tazameni yuko hapa`; ninyi msitoke wala msiwafuate.
<scripture passage="Luke 17:24" parsed="|Luke|17|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.24" />
<sup>24</sup>Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
<scripture passage="Luke 17:25" parsed="|Luke|17|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.25" />
<sup>25</sup>Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.
<scripture passage="Luke 17:26" parsed="|Luke|17|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.26" />
<sup>26</sup>Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.
<scripture passage="Luke 17:27" parsed="|Luke|17|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.27" />
<sup>27</sup>Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
<scripture passage="Luke 17:28" parsed="|Luke|17|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.28" />
<sup>28</sup>Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
<scripture passage="Luke 17:29" parsed="|Luke|17|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.29" />
<sup>29</sup>Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
<scripture passage="Luke 17:30" parsed="|Luke|17|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.30" />
<sup>30</sup>Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.
<scripture passage="Luke 17:31" parsed="|Luke|17|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.31" />
<sup>31</sup>"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
<scripture passage="Luke 17:32" parsed="|Luke|17|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.32" />
<sup>32</sup>Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
<scripture passage="Luke 17:33" parsed="|Luke|17|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.33" />
<sup>33</sup>Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.
<scripture passage="Luke 17:34" parsed="|Luke|17|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.34" />
<sup>34</sup>Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.
<scripture passage="Luke 17:35" parsed="|Luke|17|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.35" />
<sup>35</sup>Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."<i>fc</i> atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie
<scripture passage="Luke 17:36" parsed="|Luke|17|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.36" />
<sup>36</sup>missing
<scripture passage="Luke 17:37" parsed="|Luke|17|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.17.37" />
<sup>37</sup>Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia."
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 18" progress="30.00%" prev="Luke.17" next="Luke.19" id="Luke.18">
<h3 id="Luke.18-p0.1">Chapter 18</h3>
<p id="Luke.18-p1">
<scripture passage="Luke 18:1" parsed="|Luke|18|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.1" />
<sup>1</sup>Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa.
<scripture passage="Luke 18:2" parsed="|Luke|18|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.2" />
<sup>2</sup>Alisema: "Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
<scripture passage="Luke 18:3" parsed="|Luke|18|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.3" />
<sup>3</sup>Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake.
<scripture passage="Luke 18:4" parsed="|Luke|18|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.4" />
<sup>4</sup>Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini, mwishowe akajisemea: `Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu,
<scripture passage="Luke 18:5" parsed="|Luke|18|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.5" />
<sup>5</sup>lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!"`
<scripture passage="Luke 18:6" parsed="|Luke|18|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.6" />
<sup>6</sup>Basi, Bwana akaendelea kusema, "Sikieni jinsi alivyosema huyo hakimu mbaya.
<scripture passage="Luke 18:7" parsed="|Luke|18|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.7" />
<sup>7</sup>Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza?
<scripture passage="Luke 18:8" parsed="|Luke|18|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.8" />
<sup>8</sup>Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?"
<scripture passage="Luke 18:9" parsed="|Luke|18|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.9" />
<sup>9</sup>Halafu Yesu aliwaambia pia mfano wa wale ambao walijiona kuwa wema na kuwadharau wengine.
<scripture passage="Luke 18:10" parsed="|Luke|18|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.10" />
<sup>10</sup>"Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru.
<scripture passage="Luke 18:11" parsed="|Luke|18|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.11" />
<sup>11</sup>Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: `Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
<scripture passage="Luke 18:12" parsed="|Luke|18|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.12" />
<sup>12</sup>Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.`
<scripture passage="Luke 18:13" parsed="|Luke|18|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.13" />
<sup>13</sup>Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: `Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.`
<scripture passage="Luke 18:14" parsed="|Luke|18|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.14" />
<sup>14</sup>Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa."
<scripture passage="Luke 18:15" parsed="|Luke|18|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.15" />
<sup>15</sup>Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali.
<scripture passage="Luke 18:16" parsed="|Luke|18|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.16" />
<sup>16</sup>Lakini Yesu akawaita kwake akisema: "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa.
<scripture passage="Luke 18:17" parsed="|Luke|18|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.17" />
<sup>17</sup>Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika Ufalme huo."
<scripture passage="Luke 18:18" parsed="|Luke|18|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.18" />
<sup>18</sup>Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele?"
<scripture passage="Luke 18:19" parsed="|Luke|18|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.19" />
<sup>19</sup>Yesu akamwambia, "Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake.
<scripture passage="Luke 18:20" parsed="|Luke|18|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.20" />
<sup>20</sup>Unazijua amri: `Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo; waheshimu baba yako na mama yako."`
<scripture passage="Luke 18:21" parsed="|Luke|18|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.21" />
<sup>21</sup>Yeye akasema, "Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu."
<scripture passage="Luke 18:22" parsed="|Luke|18|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.22" />
<sup>22</sup>Yesu aliposikia hayo akamwambia, "Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate."
<scripture passage="Luke 18:23" parsed="|Luke|18|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.23" />
<sup>23</sup>Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana.
<scripture passage="Luke 18:24" parsed="|Luke|18|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.24" />
<sup>24</sup>Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, "Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
<scripture passage="Luke 18:25" parsed="|Luke|18|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.25" />
<sup>25</sup>Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Luke 18:26" parsed="|Luke|18|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.26" />
<sup>26</sup>Wale watu waliposikia hayo, wakasema, "Nani basi, atakayeokolewa?"
<scripture passage="Luke 18:27" parsed="|Luke|18|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.27" />
<sup>27</sup>Yesu akajibu, "Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu."
<scripture passage="Luke 18:28" parsed="|Luke|18|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.28" />
<sup>28</sup>Naye Petro akamwuliza, "Na sisi je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!"
<scripture passage="Luke 18:29" parsed="|Luke|18|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.29" />
<sup>29</sup>Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
<scripture passage="Luke 18:30" parsed="|Luke|18|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.30" />
<sup>30</sup>atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa milele wakati ujao."
<scripture passage="Luke 18:31" parsed="|Luke|18|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.31" />
<sup>31</sup>Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, "Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
<scripture passage="Luke 18:32" parsed="|Luke|18|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.32" />
<sup>32</sup>Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate.
<scripture passage="Luke 18:33" parsed="|Luke|18|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.33" />
<sup>33</sup>Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka."
<scripture passage="Luke 18:34" parsed="|Luke|18|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.34" />
<sup>34</sup>Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
<scripture passage="Luke 18:35" parsed="|Luke|18|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.35" />
<sup>35</sup>Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba.
<scripture passage="Luke 18:36" parsed="|Luke|18|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.36" />
<sup>36</sup>Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, "Kuna nini?"
<scripture passage="Luke 18:37" parsed="|Luke|18|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.37" />
<sup>37</sup>Wakamwambia, "Yesu wa Nazareti anapita."
<scripture passage="Luke 18:38" parsed="|Luke|18|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.38" />
<sup>38</sup>Naye akapaza sauti akisema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
<scripture passage="Luke 18:39" parsed="|Luke|18|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.39" />
<sup>39</sup>Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: "Mwana wa Daudi, nihurumie;"
<scripture passage="Luke 18:40" parsed="|Luke|18|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.40" />
<sup>40</sup>Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
<scripture passage="Luke 18:41" parsed="|Luke|18|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.41" />
<sup>41</sup>"Unataka nikufanyie nini?" Naye akamjibu, "Bwana, naomba nipate kuona tena."
<scripture passage="Luke 18:42" parsed="|Luke|18|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.42" />
<sup>42</sup>Yesu akamwambia, "Ona! Imani yako imekuponya."
<scripture passage="Luke 18:43" parsed="|Luke|18|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.18.43" />
<sup>43</sup>Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 19" progress="30.48%" prev="Luke.18" next="Luke.20" id="Luke.19">
<h3 id="Luke.19-p0.1">Chapter 19</h3>
<p id="Luke.19-p1">
<scripture passage="Luke 19:1" parsed="|Luke|19|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.
<scripture passage="Luke 19:2" parsed="|Luke|19|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.2" />
<sup>2</sup>Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
<scripture passage="Luke 19:3" parsed="|Luke|19|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.3" />
<sup>3</sup>Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.
<scripture passage="Luke 19:4" parsed="|Luke|19|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.4" />
<sup>4</sup>Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.
<scripture passage="Luke 19:5" parsed="|Luke|19|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.5" />
<sup>5</sup>Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako."
<scripture passage="Luke 19:6" parsed="|Luke|19|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.6" />
<sup>6</sup>Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.
<scripture passage="Luke 19:7" parsed="|Luke|19|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.7" />
<sup>7</sup>Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung`unika wakisema, "Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi."
<scripture passage="Luke 19:8" parsed="|Luke|19|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.8" />
<sup>8</sup>Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang`anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne."
<scripture passage="Luke 19:9" parsed="|Luke|19|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.9" />
<sup>9</sup>Yesu akamwambia, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
<scripture passage="Luke 19:10" parsed="|Luke|19|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.10" />
<sup>10</sup>Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea." ic
<scripture passage="Luke 19:11" parsed="|Luke|19|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.11" />
<sup>11</sup>Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)
<scripture passage="Luke 19:12" parsed="|Luke|19|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.12" />
<sup>12</sup>Hivyo akawaambia, "Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
<scripture passage="Luke 19:13" parsed="|Luke|19|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.13" />
<sup>13</sup>Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: `Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.`
<scripture passage="Luke 19:14" parsed="|Luke|19|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.14" />
<sup>14</sup>Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende wakaseme: `Hatumtaki huyu atutawale.`
<scripture passage="Luke 19:15" parsed="|Luke|19|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.15" />
<sup>15</sup>"Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze kujua kila mmoja amepata faida gani.
<scripture passage="Luke 19:16" parsed="|Luke|19|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.16" />
<sup>16</sup>Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: `Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.`
<scripture passage="Luke 19:17" parsed="|Luke|19|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.17" />
<sup>17</sup>Naye akamwambia: `Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!`
<scripture passage="Luke 19:18" parsed="|Luke|19|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.18" />
<sup>18</sup>Mtumishi wa pili akaja, akasema: `Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.`
<scripture passage="Luke 19:19" parsed="|Luke|19|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.19" />
<sup>19</sup>Naye akamwambia pia: `Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji mitano.`
<scripture passage="Luke 19:20" parsed="|Luke|19|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.20" />
<sup>20</sup>"Mtumishi mwingine akaja, akasema: `Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa,
<scripture passage="Luke 19:21" parsed="|Luke|19|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.21" />
<sup>21</sup>kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.`
<scripture passage="Luke 19:22" parsed="|Luke|19|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.22" />
<sup>22</sup>Naye akamwambia: `Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na kuchuma nisichopanda.
<scripture passage="Luke 19:23" parsed="|Luke|19|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.23" />
<sup>23</sup>Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?`
<scripture passage="Luke 19:24" parsed="|Luke|19|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.24" />
<sup>24</sup>Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: `Mnyang`anyeni hizo fedha, mkampe yule aliyepata faida mara kumi.`
<scripture passage="Luke 19:25" parsed="|Luke|19|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.25" />
<sup>25</sup>Nao wakamwambia: `Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi hicho mara kumi!`
<scripture passage="Luke 19:26" parsed="|Luke|19|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.26" />
<sup>26</sup>Naye akawajibu: `Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
<scripture passage="Luke 19:27" parsed="|Luke|19|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.27" />
<sup>27</sup>Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu."`
<scripture passage="Luke 19:28" parsed="|Luke|19|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.28" />
<sup>28</sup>Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 19:29" parsed="|Luke|19|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.29" />
<sup>29</sup>Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
<scripture passage="Luke 19:30" parsed="|Luke|19|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.30" />
<sup>30</sup>akawaambia: "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.
<scripture passage="Luke 19:31" parsed="|Luke|19|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.31" />
<sup>31</sup>Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, `Bwana ana haja naye."`
<scripture passage="Luke 19:32" parsed="|Luke|19|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.
<scripture passage="Luke 19:33" parsed="|Luke|19|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.33" />
<sup>33</sup>Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza, "Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?"
<scripture passage="Luke 19:34" parsed="|Luke|19|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.34" />
<sup>34</sup>Nao wakawajibu, "Bwana anamhitaji."
<scripture passage="Luke 19:35" parsed="|Luke|19|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.35" />
<sup>35</sup>Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.
<scripture passage="Luke 19:36" parsed="|Luke|19|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.36" />
<sup>36</sup>Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
<scripture passage="Luke 19:37" parsed="|Luke|19|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.37" />
<sup>37</sup>Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;
<scripture passage="Luke 19:38" parsed="|Luke|19|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.38" />
<sup>38</sup>wakawa wanasema: "Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!"
<scripture passage="Luke 19:39" parsed="|Luke|19|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.39" />
<sup>39</sup>Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu, "Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!"
<scripture passage="Luke 19:40" parsed="|Luke|19|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.40" />
<sup>40</sup>Yesu akawajibu, "Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti."
<scripture passage="Luke 19:41" parsed="|Luke|19|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.41" />
<sup>41</sup>Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia
<scripture passage="Luke 19:42" parsed="|Luke|19|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.42" />
<sup>42</sup>akisema: "Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.
<scripture passage="Luke 19:43" parsed="|Luke|19|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.43" />
<sup>43</sup>Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.
<scripture passage="Luke 19:44" parsed="|Luke|19|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.44" />
<sup>44</sup>Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa."
<scripture passage="Luke 19:45" parsed="|Luke|19|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.45" />
<sup>45</sup>Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiashara
<scripture passage="Luke 19:46" parsed="|Luke|19|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.46" />
<sup>46</sup>akisema, "Imeandikwa: `Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala`; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi."
<scripture passage="Luke 19:47" parsed="|Luke|19|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.47" />
<sup>47</sup>Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,
<scripture passage="Luke 19:48" parsed="|Luke|19|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.19.48" />
<sup>48</sup>lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 20" progress="31.02%" prev="Luke.19" next="Luke.21" id="Luke.20">
<h3 id="Luke.20-p0.1">Chapter 20</h3>
<p id="Luke.20-p1">
<scripture passage="Luke 20:1" parsed="|Luke|20|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.1" />
<sup>1</sup>Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika,
<scripture passage="Luke 20:2" parsed="|Luke|20|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.2" />
<sup>2</sup>wakasema, "Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?"
<scripture passage="Luke 20:3" parsed="|Luke|20|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.3" />
<sup>3</sup>Yesu akawaambia, "Na mimi nitawaulizeni swali:
<scripture passage="Luke 20:4" parsed="|Luke|20|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.4" />
<sup>4</sup>mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?"
<scripture passage="Luke 20:5" parsed="|Luke|20|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.5" />
<sup>5</sup>Lakini wao wakajadiliana hivi: "Tukisema yalitoka mbinguni, yeye atatuuliza: `Mbona hamkumsadiki?`
<scripture passage="Luke 20:6" parsed="|Luke|20|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.6" />
<sup>6</sup>Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii."
<scripture passage="Luke 20:7" parsed="|Luke|20|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.7" />
<sup>7</sup>Basi, wakamwambia, "Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi."
<scripture passage="Luke 20:8" parsed="|Luke|20|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.8" />
<sup>8</sup>Yesu akawaambia, "Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."
<scripture passage="Luke 20:9" parsed="|Luke|20|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.9" />
<sup>9</sup>Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
<scripture passage="Luke 20:10" parsed="|Luke|20|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.10" />
<sup>10</sup>Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.
<scripture passage="Luke 20:11" parsed="|Luke|20|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.11" />
<sup>11</sup>Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.
<scripture passage="Luke 20:12" parsed="|Luke|20|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.12" />
<sup>12</sup>Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.
<scripture passage="Luke 20:13" parsed="|Luke|20|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.13" />
<sup>13</sup>Yule mwenye shamba akafikiri: `Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.`
<scripture passage="Luke 20:14" parsed="|Luke|20|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.14" />
<sup>14</sup>Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: `Huyu ndiye mrithi. Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.`
<scripture passage="Luke 20:15" parsed="|Luke|20|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.15" />
<sup>15</sup>Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua." Yesu akauliza, "Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?
<scripture passage="Luke 20:16" parsed="|Luke|20|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.16" />
<sup>16</sup>Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na atawapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu." Watu waliposikia maneno hayo, walisema: "Hasha! Yasitukie hata kidogo!"
<scripture passage="Luke 20:17" parsed="|Luke|20|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.17" />
<sup>17</sup>Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, "Maandiko haya Matakatifu yana maana gani basi? `Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!`
<scripture passage="Luke 20:18" parsed="|Luke|20|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.18" />
<sup>18</sup>Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo, atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamsaga kabisa."
<scripture passage="Luke 20:19" parsed="|Luke|20|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.19" />
<sup>19</sup>Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
<scripture passage="Luke 20:20" parsed="|Luke|20|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.20" />
<sup>20</sup>Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali.
<scripture passage="Luke 20:21" parsed="|Luke|20|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.21" />
<sup>21</sup>Hao wapelelezi wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
<scripture passage="Luke 20:22" parsed="|Luke|20|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.22" />
<sup>22</sup>Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipa kodi kwa Kaisari!"
<scripture passage="Luke 20:23" parsed="|Luke|20|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.23" />
<sup>23</sup>Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
<scripture passage="Luke 20:24" parsed="|Luke|20|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.24" />
<sup>24</sup>"Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?"
<scripture passage="Luke 20:25" parsed="|Luke|20|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.25" />
<sup>25</sup>Nao wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Mungu vilivyo vyake Mungu."
<scripture passage="Luke 20:26" parsed="|Luke|20|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.26" />
<sup>26</sup>Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
<scripture passage="Luke 20:27" parsed="|Luke|20|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.27" />
<sup>27</sup>Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu, wakasema:
<scripture passage="Luke 20:28" parsed="|Luke|20|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.28" />
<sup>28</sup>"Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.
<scripture passage="Luke 20:29" parsed="|Luke|20|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.29" />
<sup>29</sup>Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bila kuacha mtoto.
<scripture passage="Luke 20:30" parsed="|Luke|20|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.30" />
<sup>30</sup>Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;
<scripture passage="Luke 20:31" parsed="|Luke|20|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.31" />
<sup>31</sup>na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba--wote walikufa bila kuacha watoto.
<scripture passage="Luke 20:32" parsed="|Luke|20|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.32" />
<sup>32</sup>Mwishowe akafa pia yule mwanamke.
<scripture passage="Luke 20:33" parsed="|Luke|20|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.33" />
<sup>33</sup>Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa na wote saba."
<scripture passage="Luke 20:34" parsed="|Luke|20|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawaambia, "Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;
<scripture passage="Luke 20:35" parsed="|Luke|20|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.35" />
<sup>35</sup>lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.
<scripture passage="Luke 20:36" parsed="|Luke|20|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.36" />
<sup>36</sup>Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.
<scripture passage="Luke 20:37" parsed="|Luke|20|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.37" />
<sup>37</sup>Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
<scripture passage="Luke 20:38" parsed="|Luke|20|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.38" />
<sup>38</sup>Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye."
<scripture passage="Luke 20:39" parsed="|Luke|20|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.39" />
<sup>39</sup>Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, "Mwalimu, umejibu vema kabisa."
<scripture passage="Luke 20:40" parsed="|Luke|20|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.40" />
<sup>40</sup>Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.
<scripture passage="Luke 20:41" parsed="|Luke|20|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.41" />
<sup>41</sup>Yesu akawauliza, "Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
<scripture passage="Luke 20:42" parsed="|Luke|20|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.42" />
<sup>42</sup>Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: `Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia
<scripture passage="Luke 20:43" parsed="|Luke|20|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.43" />
<sup>43</sup>mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.`
<scripture passage="Luke 20:44" parsed="|Luke|20|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.44" />
<sup>44</sup>Ikiwa Daudi anamwita yeye, `Bwana,` basi atakuwaje mwanawe?"
<scripture passage="Luke 20:45" parsed="|Luke|20|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.45" />
<sup>45</sup>Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,
<scripture passage="Luke 20:46" parsed="|Luke|20|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.46" />
<sup>46</sup>"Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
<scripture passage="Luke 20:47" parsed="|Luke|20|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.20.47" />
<sup>47</sup>Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!"
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 21" progress="31.55%" prev="Luke.20" next="Luke.22" id="Luke.21">
<h3 id="Luke.21-p0.1">Chapter 21</h3>
<p id="Luke.21-p1">
<scripture passage="Luke 21:1" parsed="|Luke|21|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.1" />
<sup>1</sup>Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya Hekalu,
<scripture passage="Luke 21:2" parsed="|Luke|21|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.2" />
<sup>2</sup>akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili ndogo.
<scripture passage="Luke 21:3" parsed="|Luke|21|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.3" />
<sup>3</sup>Basi, akasema, "Nawaambieni kweli, mama huyu mjane ametia zaidi katika hazina kuliko wote.
<scripture passage="Luke 21:4" parsed="|Luke|21|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.4" />
<sup>4</sup>Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi."
<scripture passage="Luke 21:5" parsed="|Luke|21|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.5" />
<sup>5</sup>Baadhi ya wanafunzi walikuwa wanazungumza juu ya Hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe ya thamani, pamoja na sadaka zilizotolewa kwa Mungu. Yesu akasema,
<scripture passage="Luke 21:6" parsed="|Luke|21|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.6" />
<sup>6</sup>"Haya yote mnayoyaona--zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa."
<scripture passage="Luke 21:7" parsed="|Luke|21|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.7" />
<sup>7</sup>Basi, wakamwuliza, "Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonyesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?"
<scripture passage="Luke 21:8" parsed="|Luke|21|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.8" />
<sup>8</sup>Yesu akawajibu, "Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: `Mimi ndiye`, na, `Wakati ule umekaribia`. Lakini ninyi msiwafuate!
<scripture passage="Luke 21:9" parsed="|Luke|21|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.9" />
<sup>9</sup>Basi, mtakaposikia habari za vita na misukosuko, msitishike; maana ni lazima hayo yatokee kwanza, lakini mwisho wa yote, bado."
<scripture passage="Luke 21:10" parsed="|Luke|21|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.10" />
<sup>10</sup>Halafu akaendelea kusema: "Taifa moja litapigana na taifa lingine, na ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine.
<scripture passage="Luke 21:11" parsed="|Luke|21|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.11" />
<sup>11</sup>Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, kutakuwa na njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
<scripture passage="Luke 21:12" parsed="|Luke|21|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.12" />
<sup>12</sup>Lakini kabla ya kutokea hayo yote, watawatieni nguvuni, watawatesa na kuwapelekeni katika masunagogi na kuwatia gerezani; mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu.
<scripture passage="Luke 21:13" parsed="|Luke|21|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.13" />
<sup>13</sup>Hii itawapeni fursa ya kushuhudia Habari Njema.
<scripture passage="Luke 21:14" parsed="|Luke|21|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.14" />
<sup>14</sup>Muwe na msimamo huu mioyoni mwenu: hakuna kufikiria kabla ya wakati juu ya jinsi mtakavyojitetea,
<scripture passage="Luke 21:15" parsed="|Luke|21|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.15" />
<sup>15</sup>kwa sababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasaha wa maneno na hekima, hivyo kwamba zenu hawataweza kustahimili wala kupinga.
<scripture passage="Luke 21:16" parsed="|Luke|21|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.16" />
<sup>16</sup>Wazazi wenu, ndugu, jamaa na rafiki zenu watawasaliti ninyi; na baadhi yenu mtauawa.
<scripture passage="Luke 21:17" parsed="|Luke|21|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.17" />
<sup>17</sup>Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu.
<scripture passage="Luke 21:18" parsed="|Luke|21|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.18" />
<sup>18</sup>Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea.
<scripture passage="Luke 21:19" parsed="|Luke|21|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.19" />
<sup>19</sup>Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.
<scripture passage="Luke 21:20" parsed="|Luke|21|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.20" />
<sup>20</sup>"Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo mtambue ya kwamba wakati umefika ambapo mji huo utaharibiwa.
<scripture passage="Luke 21:21" parsed="|Luke|21|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.21" />
<sup>21</sup>Hapo walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini.
<scripture passage="Luke 21:22" parsed="|Luke|21|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.22" />
<sup>22</sup>Kwa maana siku hizo ni siku za adhabu, ili yote yaliyoandikwa yatimie.
<scripture passage="Luke 21:23" parsed="|Luke|21|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.23" />
<sup>23</sup>Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
<scripture passage="Luke 21:24" parsed="|Luke|21|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.24" />
<sup>24</sup>Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
<scripture passage="Luke 21:25" parsed="|Luke|21|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.25" />
<sup>25</sup>"Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota. Mataifa duniani yatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasi kutokana na mshindo wa mawimbi ya bahari.
<scripture passage="Luke 21:26" parsed="|Luke|21|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.26" />
<sup>26</sup>Watu watazirai kwa sababu ya uoga, wakitazamia mambo yatakayoupata ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
<scripture passage="Luke 21:27" parsed="|Luke|21|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.27" />
<sup>27</sup>Halafu, watamwona Mwana wa Mtu akija katika wingu, mwenye nguvu na utukufu mwingi.
<scripture passage="Luke 21:28" parsed="|Luke|21|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.28" />
<sup>28</sup>Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia."
<scripture passage="Luke 21:29" parsed="|Luke|21|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.29" />
<sup>29</sup>Kisha akawaambia mfano: "Angalieni mtini na miti mingine yote.
<scripture passage="Luke 21:30" parsed="|Luke|21|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.30" />
<sup>30</sup>Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
<scripture passage="Luke 21:31" parsed="|Luke|21|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.31" />
<sup>31</sup>Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.
<scripture passage="Luke 21:32" parsed="|Luke|21|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.32" />
<sup>32</sup>Nawaambieni hakika, kizazi hiki cha sasa hakitapita kabla ya hayo yote kutendeka.
<scripture passage="Luke 21:33" parsed="|Luke|21|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.33" />
<sup>33</sup>Mbingu na dunia vitapita, lakini maneno yangu hayatapita.
<scripture passage="Luke 21:34" parsed="|Luke|21|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.34" />
<sup>34</sup>"Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, Siku ile itawajieni ghafla.
<scripture passage="Luke 21:35" parsed="|Luke|21|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.35" />
<sup>35</sup>Kwa maana itawajia kama mtego, wote wanaoishi duniani pote.
<scripture passage="Luke 21:36" parsed="|Luke|21|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.36" />
<sup>36</sup>Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu."
<scripture passage="Luke 21:37" parsed="|Luke|21|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.37" />
<sup>37</sup>Wakati wa mchana, siku hizo, Yesu alikuwa akifundisha watu Hekaluni; lakini usiku alikuwa akienda katika mlima wa Mizeituni na kukaa huko.
<scripture passage="Luke 21:38" parsed="|Luke|21|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.21.38" />
<sup>38</sup>Watu wote walikuwa wanakwenda Hekaluni asubuhi na mapema, wapate kumsikiliza.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 22" progress="31.98%" prev="Luke.21" next="Luke.23" id="Luke.22">
<h3 id="Luke.22-p0.1">Chapter 22</h3>
<p id="Luke.22-p1">
<scripture passage="Luke 22:1" parsed="|Luke|22|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.1" />
<sup>1</sup>Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.
<scripture passage="Luke 22:2" parsed="|Luke|22|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.2" />
<sup>2</sup>Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.
<scripture passage="Luke 22:3" parsed="|Luke|22|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.3" />
<sup>3</sup>Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.
<scripture passage="Luke 22:4" parsed="|Luke|22|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.4" />
<sup>4</sup>Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa Hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao.
<scripture passage="Luke 22:5" parsed="|Luke|22|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.5" />
<sup>5</sup>Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha.
<scripture passage="Luke 22:6" parsed="|Luke|22|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.6" />
<sup>6</sup>Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua.
<scripture passage="Luke 22:7" parsed="|Luke|22|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.7" />
<sup>7</sup>Basi, siku ya Mikate Isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa.
<scripture passage="Luke 22:8" parsed="|Luke|22|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.8" />
<sup>8</sup>Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, "Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka."
<scripture passage="Luke 22:9" parsed="|Luke|22|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.9" />
<sup>9</sup>Nao wakamwuliza, "Unataka tuiandae wapi?"
<scripture passage="Luke 22:10" parsed="|Luke|22|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.10" />
<sup>10</sup>Akawaambia, "Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia.
<scripture passage="Luke 22:11" parsed="|Luke|22|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.11" />
<sup>11</sup>Mwambieni mwenye nyumba: `Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?`
<scripture passage="Luke 22:12" parsed="|Luke|22|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.12" />
<sup>12</sup>Naye atawaonyesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo."
<scripture passage="Luke 22:13" parsed="|Luke|22|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.13" />
<sup>13</sup>Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.
<scripture passage="Luke 22:14" parsed="|Luke|22|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.14" />
<sup>14</sup>Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.
<scripture passage="Luke 22:15" parsed="|Luke|22|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.15" />
<sup>15</sup>Akawaambia, "Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.
<scripture passage="Luke 22:16" parsed="|Luke|22|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.16" />
<sup>16</sup>Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Luke 22:17" parsed="|Luke|22|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.17" />
<sup>17</sup>Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema, "Pokeeni, mgawanye ninyi kwa ninyi.
<scripture passage="Luke 22:18" parsed="|Luke|22|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.18" />
<sup>18</sup>Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja."
<scripture passage="Luke 22:19" parsed="|Luke|22|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.19" />
<sup>19</sup>Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, "Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka."
<scripture passage="Luke 22:20" parsed="|Luke|22|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.20" />
<sup>20</sup>Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.<i>fd</i>
<scripture passage="Luke 22:21" parsed="|Luke|22|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.21" />
<sup>21</sup>"Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani.
<scripture passage="Luke 22:22" parsed="|Luke|22|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.22" />
<sup>22</sup>Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole wake mtu anayemsaliti."
<scripture passage="Luke 22:23" parsed="|Luke|22|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.23" />
<sup>23</sup>Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya jambo hilo.
<scripture passage="Luke 22:24" parsed="|Luke|22|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.24" />
<sup>24</sup>Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko wengine.
<scripture passage="Luke 22:25" parsed="|Luke|22|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.25" />
<sup>25</sup>Yesu akawaambia, "Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu.
<scripture passage="Luke 22:26" parsed="|Luke|22|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.26" />
<sup>26</sup>Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi.
<scripture passage="Luke 22:27" parsed="|Luke|22|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.27" />
<sup>27</sup>Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
<scripture passage="Luke 22:28" parsed="|Luke|22|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.28" />
<sup>28</sup>"Ninyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu;
<scripture passage="Luke 22:29" parsed="|Luke|22|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.29" />
<sup>29</sup>na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyo hivyo nami nitawakabidhi ninyi Ufalme.
<scripture passage="Luke 22:30" parsed="|Luke|22|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.30" />
<sup>30</sup>Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na mtaketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
<scripture passage="Luke 22:31" parsed="|Luke|22|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.31" />
<sup>31</sup>"Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta ninyi kama mtu anavyopepeta ngano.
<scripture passage="Luke 22:32" parsed="|Luke|22|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.32" />
<sup>32</sup>Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako."
<scripture passage="Luke 22:33" parsed="|Luke|22|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.33" />
<sup>33</sup>Naye Petro akamjibu, "Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa."
<scripture passage="Luke 22:34" parsed="|Luke|22|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.34" />
<sup>34</sup>Yesu akamjibu, "Nakwambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu."
<scripture passage="Luke 22:35" parsed="|Luke|22|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.35" />
<sup>35</sup>Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, "Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?" Wakajibu, "La."
<scripture passage="Luke 22:36" parsed="|Luke|22|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.36" />
<sup>36</sup>Naye akawaambia, "Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga, auze koti lake anunue mmoja.
<scripture passage="Luke 22:37" parsed="|Luke|22|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.37" />
<sup>37</sup>Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: `Aliwekwa kundi moja na wahalifu,` ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake."
<scripture passage="Luke 22:38" parsed="|Luke|22|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.38" />
<sup>38</sup>Nao wakasema, "Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili." Naye akasema, "Basi!"
<scripture passage="Luke 22:39" parsed="|Luke|22|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.39" />
<sup>39</sup>Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata.
<scripture passage="Luke 22:40" parsed="|Luke|22|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.40" />
<sup>40</sup>Alipofika huko akawaambia, "Salini, msije mkaingia katika kishawishi."
<scripture passage="Luke 22:41" parsed="|Luke|22|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.41" />
<sup>41</sup>Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali:
<scripture passage="Luke 22:42" parsed="|Luke|22|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.42" />
<sup>42</sup>"Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu."
<scripture passage="Luke 22:43" parsed="|Luke|22|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.43" />
<sup>43</sup>Hapo, malaika kutoka mbinguni, akamtokea ili kumtia moyo.
<scripture passage="Luke 22:44" parsed="|Luke|22|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.44" />
<sup>44</sup>Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.<i>fe</i> ic
<scripture passage="Luke 22:45" parsed="|Luke|22|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.45" />
<sup>45</sup>Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni.
<scripture passage="Luke 22:46" parsed="|Luke|22|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.46" />
<sup>46</sup>Akawaambia, "Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi."
<scripture passage="Luke 22:47" parsed="|Luke|22|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.47" />
<sup>47</sup>Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
<scripture passage="Luke 22:48" parsed="|Luke|22|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.48" />
<sup>48</sup>Lakini Yesu akamwambia, "Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa kumbusu?"
<scripture passage="Luke 22:49" parsed="|Luke|22|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.49" />
<sup>49</sup>Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, "Bwana, tutumie panga zetu?"
<scripture passage="Luke 22:50" parsed="|Luke|22|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.50" />
<sup>50</sup>Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
<scripture passage="Luke 22:51" parsed="|Luke|22|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.51" />
<sup>51</sup>Hapo, Yesu akasema, "Acha! Hii inatosha." Akaligusa sikio la mtu huyo akaliponya.
<scripture passage="Luke 22:52" parsed="|Luke|22|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.52" />
<sup>52</sup>Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: "Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang`anyi?
<scripture passage="Luke 22:53" parsed="|Luke|22|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.53" />
<sup>53</sup>Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku Hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza."
<scripture passage="Luke 22:54" parsed="|Luke|22|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.54" />
<sup>54</sup>Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali.
<scripture passage="Luke 22:55" parsed="|Luke|22|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.55" />
<sup>55</sup>Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja Petro akiwa miongoni mwao.
<scripture passage="Luke 22:56" parsed="|Luke|22|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.56" />
<sup>56</sup>Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, "Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu."
<scripture passage="Luke 22:57" parsed="|Luke|22|57|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.57" />
<sup>57</sup>Lakini Petro akakana akisema, "Wee! simjui mimi."
<scripture passage="Luke 22:58" parsed="|Luke|22|58|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.58" />
<sup>58</sup>Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, "Wewe ni mmoja wao." Lakini Petro akajibu "Bwana we; si mimi!"
<scripture passage="Luke 22:59" parsed="|Luke|22|59|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.59" />
<sup>59</sup>Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, "Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati."
<scripture passage="Luke 22:60" parsed="|Luke|22|60|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.60" />
<sup>60</sup>Lakini Petro akasema, "Bwana wee; sijui hata unachosema!" Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
<scripture passage="Luke 22:61" parsed="|Luke|22|61|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.61" />
<sup>61</sup>Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: "Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
<scripture passage="Luke 22:62" parsed="|Luke|22|62|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.62" />
<sup>62</sup>Hapo akatoka nje, akalia sana.
<scripture passage="Luke 22:63" parsed="|Luke|22|63|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.63" />
<sup>63</sup>Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki.
<scripture passage="Luke 22:64" parsed="|Luke|22|64|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.64" />
<sup>64</sup>Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, "Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri tuone!"
<scripture passage="Luke 22:65" parsed="|Luke|22|65|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.65" />
<sup>65</sup>Wakamtolea maneno mengi ya matusi.
<scripture passage="Luke 22:66" parsed="|Luke|22|66|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.66" />
<sup>66</sup>Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
<scripture passage="Luke 22:67" parsed="|Luke|22|67|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.67" />
<sup>67</sup>Nao wakamwambia, "Twambie! Je, wewe ndiwe Kristo?" Lakini Yesu akawaambia, "Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki;
<scripture passage="Luke 22:68" parsed="|Luke|22|68|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.68" />
<sup>68</sup>na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu.
<scripture passage="Luke 22:69" parsed="|Luke|22|69|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.69" />
<sup>69</sup>Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi."
<scripture passage="Luke 22:70" parsed="|Luke|22|70|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.70" />
<sup>70</sup>Hapo wote wakasema, "Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?" Naye akasema, "Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye."
<scripture passage="Luke 22:71" parsed="|Luke|22|71|0|0" osisRef="Bible:Luke.22.71" />
<sup>71</sup>Nao wakasema, "Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe."sw4323
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 23" progress="32.73%" prev="Luke.22" next="Luke.24" id="Luke.23">
<h3 id="Luke.23-p0.1">Chapter 23</h3>
<p id="Luke.23-p1">
<scripture passage="Luke 23:1" parsed="|Luke|23|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.1" />
<sup>1</sup>Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.
<scripture passage="Luke 23:2" parsed="|Luke|23|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.2" />
<sup>2</sup>Wakaanza kumshtaki wakisema: "Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni Kristo, Mfalme."
<scripture passage="Luke 23:3" parsed="|Luke|23|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.3" />
<sup>3</sup>Pilato akamwuliza Yesu, "Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema."
<scripture passage="Luke 23:4" parsed="|Luke|23|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.4" />
<sup>4</sup>Pilato akawaambia makuhani wakuu na umati wa watu, "Sioni kosa lolote katika mtu huyu."
<scripture passage="Luke 23:5" parsed="|Luke|23|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.5" />
<sup>5</sup>Lakini wao wakasisitiza wakisema: "Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika nchi yote ya Yudea; alianza Galilaya, na sasa yuko hapa."
<scripture passage="Luke 23:6" parsed="|Luke|23|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.6" />
<sup>6</sup>Pilato aliposikia hayo, akauliza, "Je, mtu huyu ni mwenyeji wa Galilaya?"
<scripture passage="Luke 23:7" parsed="|Luke|23|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.7" />
<sup>7</sup>Alipojua kwamba Yesu alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 23:8" parsed="|Luke|23|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.8" />
<sup>8</sup>Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza.
<scripture passage="Luke 23:9" parsed="|Luke|23|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.9" />
<sup>9</sup>Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno.
<scripture passage="Luke 23:10" parsed="|Luke|23|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.10" />
<sup>10</sup>Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakajitokeza mbele, wakatoa mashtaka yao kwa nguvu sana.
<scripture passage="Luke 23:11" parsed="|Luke|23|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.11" />
<sup>11</sup>Basi, herode pamoja na maaskari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
<scripture passage="Luke 23:12" parsed="|Luke|23|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.12" />
<sup>12</sup>Herode na Pilato, ambao hapo awali walikuwa maadui, tangu siku hiyo wakawa marafiki.
<scripture passage="Luke 23:13" parsed="|Luke|23|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.13" />
<sup>13</sup>Basi, Pilato akaitisha mkutano wa makuhani wakuu, viongozi na watu,
<scripture passage="Luke 23:14" parsed="|Luke|23|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.14" />
<sup>14</sup>akawaambia, "Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.
<scripture passage="Luke 23:15" parsed="|Luke|23|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.15" />
<sup>15</sup>Wala si mimi tu, bali hata Herode hakuona kosa lolote, kwa maana amemrudisha kwangu. Ni dhahiri kwamba mtu huyu hakufanya chochote kinachostahili adhabu ya kifo.
<scripture passage="Luke 23:16" parsed="|Luke|23|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.16" />
<sup>16</sup>Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia."<i>ff</i> mmoja.
<scripture passage="Luke 23:17" parsed="|Luke|23|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.17" />
<sup>17</sup>missing
<scripture passage="Luke 23:18" parsed="|Luke|23|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.18" />
<sup>18</sup>Lakini wote wakapiga kelele pamoja: "Mwondoe huyo, utufungulie Baraba!"
<scripture passage="Luke 23:19" parsed="|Luke|23|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.19" />
<sup>19</sup>Baraba alikuwa ametiwa ndani kwa kusababisha uasi katika mji na pia kwa sababu ya kuua.)
<scripture passage="Luke 23:20" parsed="|Luke|23|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.20" />
<sup>20</sup>Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena;
<scripture passage="Luke 23:21" parsed="|Luke|23|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.21" />
<sup>21</sup>lakini wao wakapiga kelele: "Msulubishe, msulubishe!"
<scripture passage="Luke 23:22" parsed="|Luke|23|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.22" />
<sup>22</sup>Pilato akawaambia mara ya tatu, "Amefanya kosa gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie."
<scripture passage="Luke 23:23" parsed="|Luke|23|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.23" />
<sup>23</sup>Lakini wao wakazidi kupiga kelele kwa nguvu sana, kwamba Yesu ni lazima asulubiwe. Mwishowe, sauti zao zikashinda.
<scripture passage="Luke 23:24" parsed="|Luke|23|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.24" />
<sup>24</sup>Basi, Pilato akaamua kwamba matakwa yao yatimizwe.
<scripture passage="Luke 23:25" parsed="|Luke|23|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.25" />
<sup>25</sup>Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
<scripture passage="Luke 23:26" parsed="|Luke|23|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.26" />
<sup>26</sup>Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
<scripture passage="Luke 23:27" parsed="|Luke|23|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.27" />
<sup>27</sup>Watu, umati kwa umati, walimfuata; miongoni mwao wakiwemo wanawake waliokuwa wanaomboleza na kumlilia.
<scripture passage="Luke 23:28" parsed="|Luke|23|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.28" />
<sup>28</sup>Yesu akawageukia, akasema, "Enyi kina mama wa Yerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya watoto wenu.
<scripture passage="Luke 23:29" parsed="|Luke|23|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.29" />
<sup>29</sup>Maana, hakika siku zitakuja ambapo watasema: `Heri yao wale walio tasa, ambao hawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto!`
<scripture passage="Luke 23:30" parsed="|Luke|23|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.30" />
<sup>30</sup>Wakati huo, ndipo watu wataanza kuiambia milima: `Tuangukieni!` na vilima, `Tufunikeni!`
<scripture passage="Luke 23:31" parsed="|Luke|23|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.31" />
<sup>31</sup>Kwa maana, kama watu wanautendea mti mbichi namna hiyo, itakuwaje kwa mti mkavu?"
<scripture passage="Luke 23:32" parsed="|Luke|23|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.32" />
<sup>32</sup>Waliwachukua pia watu wengine wawili, wahalifu, wauawe pamoja naye.
<scripture passage="Luke 23:33" parsed="|Luke|23|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.33" />
<sup>33</sup>Walipofika mahali paitwapo, "Fuvu la Kichwa," ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
<scripture passage="Luke 23:34" parsed="|Luke|23|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.34" />
<sup>34</sup>Yesu akasema, "Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya." Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
<scripture passage="Luke 23:35" parsed="|Luke|23|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.35" />
<sup>35</sup>Watu wakawa wamesimama pale wakitazama. Nao viongozi wakamdhihaki wakisema: "Amewaokoa wengine; sasa na ajiokoe mwenyewe, kama yeye ndiye Kristo, mteule wa Mungu!"
<scripture passage="Luke 23:36" parsed="|Luke|23|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.36" />
<sup>36</sup>Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki
<scripture passage="Luke 23:37" parsed="|Luke|23|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.37" />
<sup>37</sup>wakisema: "Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe."
<scripture passage="Luke 23:38" parsed="|Luke|23|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.38" />
<sup>38</sup>Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake: "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi."
<scripture passage="Luke 23:39" parsed="|Luke|23|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.39" />
<sup>39</sup>Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: "Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia."
<scripture passage="Luke 23:40" parsed="|Luke|23|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.40" />
<sup>40</sup>Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: "Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.
<scripture passage="Luke 23:41" parsed="|Luke|23|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.41" />
<sup>41</sup>Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya."
<scripture passage="Luke 23:42" parsed="|Luke|23|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.42" />
<sup>42</sup>Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako."
<scripture passage="Luke 23:43" parsed="|Luke|23|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.43" />
<sup>43</sup>Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi."
<scripture passage="Luke 23:44" parsed="|Luke|23|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.44" />
<sup>44</sup>Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likafunika nchi yote mpaka saa tisa,
<scripture passage="Luke 23:45" parsed="|Luke|23|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.45" />
<sup>45</sup>na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka vipande viwili.
<scripture passage="Luke 23:46" parsed="|Luke|23|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.46" />
<sup>46</sup>Yesu akalia kwa sauti kubwa: "Baba, naiweka roho yangu mikononi mwako." Alipokwisha sema hayo, akakata roho. ic
<scripture passage="Luke 23:47" parsed="|Luke|23|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.47" />
<sup>47</sup>Hapo, yule jemadari alipoona yaliyotukia akamsifu Mungu akisema: "Hakika huyu alikuwa mtu mwema."
<scripture passage="Luke 23:48" parsed="|Luke|23|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.48" />
<sup>48</sup>Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
<scripture passage="Luke 23:49" parsed="|Luke|23|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.49" />
<sup>49</sup>Marafiki zake wote pamoja na wale wanawake walioandamana naye kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali kutazama tukio hilo.
<scripture passage="Luke 23:50" parsed="|Luke|23|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.50" />
<sup>50</sup>Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yosefu, mwenyeji wa kijiji kimoja cha Wayahudi kiitwacho Armathaya. Alikuwa mtu mwema anayeheshimika;
<scripture passage="Luke 23:51" parsed="|Luke|23|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.51" />
<sup>51</sup>Alikuwa akitazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.
<scripture passage="Luke 23:52" parsed="|Luke|23|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.52" />
<sup>52</sup>Basi, yeye alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
<scripture passage="Luke 23:53" parsed="|Luke|23|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.53" />
<sup>53</sup>Kisha, akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
<scripture passage="Luke 23:54" parsed="|Luke|23|54|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.54" />
<sup>54</sup>Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
<scripture passage="Luke 23:55" parsed="|Luke|23|55|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.55" />
<sup>55</sup>Wale wanawake walioandamana na Yesu kutoka Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa
<scripture passage="Luke 23:56" parsed="|Luke|23|56|0|0" osisRef="Bible:Luke.23.56" />
<sup>56</sup>Halafu, walirudi nyumbani, wakatayarisha manukato na marashi kuyapaka mwili wa Yesu. Siku ya Sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria.
</p>
</div3>

<div3 title="Luke 24" progress="33.37%" prev="Luke.23" next="John" id="Luke.24">
<h3 id="Luke.24-p0.1">Chapter 24</h3>
<p id="Luke.24-p1">
<scripture passage="Luke 24:1" parsed="|Luke|24|1|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.1" />
<sup>1</sup>Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyotayarisha.
<scripture passage="Luke 24:2" parsed="|Luke|24|2|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.2" />
<sup>2</sup>Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi.
<scripture passage="Luke 24:3" parsed="|Luke|24|3|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.3" />
<sup>3</sup>Walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu.
<scripture passage="Luke 24:4" parsed="|Luke|24|4|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.4" />
<sup>4</sup>Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung`aa sana, wakasimama karibu nao.
<scripture passage="Luke 24:5" parsed="|Luke|24|5|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.5" />
<sup>5</sup>Hao wanawake wakaingiwa na hofu, wakainama chini. Ndipo wale watu wakawaambia, "Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu?
<scripture passage="Luke 24:6" parsed="|Luke|24|6|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.6" />
<sup>6</sup>Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni aliyowaambieni alipokuwa kule Galilaya:
<scripture passage="Luke 24:7" parsed="|Luke|24|7|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.7" />
<sup>7</sup>`Ni lazima Mwana wa Mtu atolewe kwa watu waovu, nao watamsulubisha, na siku ya tatu atafufuka."`
<scripture passage="Luke 24:8" parsed="|Luke|24|8|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.8" />
<sup>8</sup>Hapo wanawake wakayakumbuka maneno yake,
<scripture passage="Luke 24:9" parsed="|Luke|24|9|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.9" />
<sup>9</sup>wakarudi kutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumi na mmoja na wengine habari za mambo hayo yote.
<scripture passage="Luke 24:10" parsed="|Luke|24|10|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.10" />
<sup>10</sup>Hao waliotoa habari hizo kwa mitume ni: Maria Magdalene, Yoana na Maria mama wa Yakobo, pamoja na wanawake wengine walioandamana nao.
<scripture passage="Luke 24:11" parsed="|Luke|24|11|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.11" />
<sup>11</sup>Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini.
<scripture passage="Luke 24:12" parsed="|Luke|24|12|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.12" />
<sup>12</sup>Lakini Petro alitoka, akaenda mbio hadi kaburini. Alipoinama kuchungulia ndani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbani huku akiwa anashangaa juu ya hayo yaliyotokea.
<scripture passage="Luke 24:13" parsed="|Luke|24|13|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.13" />
<sup>13</sup>Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu.
<scripture passage="Luke 24:14" parsed="|Luke|24|14|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.14" />
<sup>14</sup>Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia.
<scripture passage="Luke 24:15" parsed="|Luke|24|15|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.15" />
<sup>15</sup>Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea, akatembea pamoja nao.
<scripture passage="Luke 24:16" parsed="|Luke|24|16|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.16" />
<sup>16</sup>Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua.
<scripture passage="Luke 24:17" parsed="|Luke|24|17|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.17" />
<sup>17</sup>Akawauliza, "Mnazungumza nini huku mnatembea?" Nao wakasimama kimya, nyuso zao wamezikunja kwa huzuni.
<scripture passage="Luke 24:18" parsed="|Luke|24|18|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.18" />
<sup>18</sup>Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, "Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?"
<scripture passage="Luke 24:19" parsed="|Luke|24|19|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.19" />
<sup>19</sup>Naye akawajibu, "Mambo gani?" Wao wakamjibu, "Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
<scripture passage="Luke 24:20" parsed="|Luke|24|20|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.20" />
<sup>20</sup>Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha.
<scripture passage="Luke 24:21" parsed="|Luke|24|21|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.21" />
<sup>21</sup>Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiye angeikomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka.
<scripture passage="Luke 24:22" parsed="|Luke|24|22|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.22" />
<sup>22</sup>Tena, wanawake wengine wa kwetu wametushtua. Walikwenda kaburini mapema asubuhi,
<scripture passage="Luke 24:23" parsed="|Luke|24|23|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.23" />
<sup>23</sup>wasiukute mwili wake. Wakarudi wakasema kwamba walitokewa na malaika waliowaambia kwamba alikuwa hai.
<scripture passage="Luke 24:24" parsed="|Luke|24|24|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.24" />
<sup>24</sup>Wengine wetu walikwenda kaburini wakashuhudia yale waliyosema hao wanawake; ila yeye hawakumwona."
<scripture passage="Luke 24:25" parsed="|Luke|24|25|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.25" />
<sup>25</sup>Kisha Yesu akawaambia, "Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii?
<scripture passage="Luke 24:26" parsed="|Luke|24|26|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.26" />
<sup>26</sup>Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?"
<scripture passage="Luke 24:27" parsed="|Luke|24|27|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.27" />
<sup>27</sup>Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.
<scripture passage="Luke 24:28" parsed="|Luke|24|28|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.28" />
<sup>28</sup>Walipokikaribia kile kijiji walikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari;
<scripture passage="Luke 24:29" parsed="|Luke|24|29|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.29" />
<sup>29</sup>lakini wao wakamsihi wakisema, "Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia." Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao.
<scripture passage="Luke 24:30" parsed="|Luke|24|30|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.30" />
<sup>30</sup>Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
<scripture passage="Luke 24:31" parsed="|Luke|24|31|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.31" />
<sup>31</sup>Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.
<scripture passage="Luke 24:32" parsed="|Luke|24|32|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakaambiana, "Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?"
<scripture passage="Luke 24:33" parsed="|Luke|24|33|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.33" />
<sup>33</sup>Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu: wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika
<scripture passage="Luke 24:34" parsed="|Luke|24|34|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.34" />
<sup>34</sup>wakisema, "Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni."
<scripture passage="Luke 24:35" parsed="|Luke|24|35|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.35" />
<sup>35</sup>Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.
<scripture passage="Luke 24:36" parsed="|Luke|24|36|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.36" />
<sup>36</sup>Wanafunzi wote wawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia "Amani kwenu."
<scripture passage="Luke 24:37" parsed="|Luke|24|37|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.37" />
<sup>37</sup>Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.
<scripture passage="Luke 24:38" parsed="|Luke|24|38|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.38" />
<sup>38</sup>Lakini yeye akawaambia, "Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na mashaka mioyoni mwenu?
<scripture passage="Luke 24:39" parsed="|Luke|24|39|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.39" />
<sup>39</sup>Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo."
<scripture passage="Luke 24:40" parsed="|Luke|24|40|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.40" />
<sup>40</sup>Baada ya kusema hayo, akawaonyesha mikono na miguu.
<scripture passage="Luke 24:41" parsed="|Luke|24|41|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.41" />
<sup>41</sup>Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, "Mnacho chakula chochote hapa?"
<scripture passage="Luke 24:42" parsed="|Luke|24|42|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.42" />
<sup>42</sup>Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
<scripture passage="Luke 24:43" parsed="|Luke|24|43|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.43" />
<sup>43</sup>Akakichukua, akala, wote wakimwona.
<scripture passage="Luke 24:44" parsed="|Luke|24|44|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.44" />
<sup>44</sup>Halafu akawaambia, "Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika Sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi."
<scripture passage="Luke 24:45" parsed="|Luke|24|45|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.45" />
<sup>45</sup>Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko Matakatifu.
<scripture passage="Luke 24:46" parsed="|Luke|24|46|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.46" />
<sup>46</sup>Akawaambia, "Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka wafu,
<scripture passage="Luke 24:47" parsed="|Luke|24|47|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.47" />
<sup>47</sup>na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia na Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu na kusamehewa dhambi.
<scripture passage="Luke 24:48" parsed="|Luke|24|48|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.48" />
<sup>48</sup>Ninyi ni mashahidi wa mambo hayo.
<scripture passage="Luke 24:49" parsed="|Luke|24|49|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.49" />
<sup>49</sup>Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu."
<scripture passage="Luke 24:50" parsed="|Luke|24|50|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.50" />
<sup>50</sup>Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.
<scripture passage="Luke 24:51" parsed="|Luke|24|51|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.51" />
<sup>51</sup>Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.
<scripture passage="Luke 24:52" parsed="|Luke|24|52|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.52" />
<sup>52</sup>Wao wakamwabudu, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:
<scripture passage="Luke 24:53" parsed="|Luke|24|53|0|0" osisRef="Bible:Luke.24.53" />
<sup>53</sup>wakakaa muda wote Hekaluni wakimsifu Mungu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="John" progress="33.91%" prev="Luke.24" next="John.1" id="John">
<h2 id="John-p0.1">John</h2>

<div3 title="John 1" progress="33.91%" prev="John" next="John.2" id="John.1">
<h3 id="John.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="John.1-p1">
<scripture passage="John 1:1" parsed="|John|1|1|0|0" osisRef="Bible:John.1.1" />
<sup>1</sup>Hapo Mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu.
<scripture passage="John 1:2" parsed="|John|1|2|0|0" osisRef="Bible:John.1.2" />
<sup>2</sup>Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu.
<scripture passage="John 1:3" parsed="|John|1|3|0|0" osisRef="Bible:John.1.3" />
<sup>3</sup>Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
<scripture passage="John 1:4" parsed="|John|1|4|0|0" osisRef="Bible:John.1.4" />
<sup>4</sup>Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.
<scripture passage="John 1:5" parsed="|John|1|5|0|0" osisRef="Bible:John.1.5" />
<sup>5</sup>Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda.
<scripture passage="John 1:6" parsed="|John|1|6|0|0" osisRef="Bible:John.1.6" />
<sup>6</sup>Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane,
<scripture passage="John 1:7" parsed="|John|1|7|0|0" osisRef="Bible:John.1.7" />
<sup>7</sup>ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini.
<scripture passage="John 1:8" parsed="|John|1|8|0|0" osisRef="Bible:John.1.8" />
<sup>8</sup>Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga.
<scripture passage="John 1:9" parsed="|John|1|9|0|0" osisRef="Bible:John.1.9" />
<sup>9</sup>Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote.
<scripture passage="John 1:10" parsed="|John|1|10|0|0" osisRef="Bible:John.1.10" />
<sup>10</sup>Basi, Neno alikuwako ulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
<scripture passage="John 1:11" parsed="|John|1|11|0|0" osisRef="Bible:John.1.11" />
<sup>11</sup>Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea.
<scripture passage="John 1:12" parsed="|John|1|12|0|0" osisRef="Bible:John.1.12" />
<sup>12</sup>Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu.
<scripture passage="John 1:13" parsed="|John|1|13|0|0" osisRef="Bible:John.1.13" />
<sup>13</sup>Hawa wamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao.
<scripture passage="John 1:14" parsed="|John|1|14|0|0" osisRef="Bible:John.1.14" />
<sup>14</sup>Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli.
<scripture passage="John 1:15" parsed="|John|1|15|0|0" osisRef="Bible:John.1.15" />
<sup>15</sup>Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, "Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: `Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa."`
<scripture passage="John 1:16" parsed="|John|1|16|0|0" osisRef="Bible:John.1.16" />
<sup>16</sup>Kutokana na ukamilifu wake sisi tumepokea neema mfululizo.
<scripture passage="John 1:17" parsed="|John|1|17|0|0" osisRef="Bible:John.1.17" />
<sup>17</sup>Maana Mungu alitoa Sheria kwa njia ya Mose, lakini neema na kweli vimekuja kwa njia ya Kristo.
<scripture passage="John 1:18" parsed="|John|1|18|0|0" osisRef="Bible:John.1.18" />
<sup>18</sup>Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote ule. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.
<scripture passage="John 1:19" parsed="|John|1|19|0|0" osisRef="Bible:John.1.19" />
<sup>19</sup>Huu ndio ushahidi Yohane alioutoa wakati viongozi wa Wayahudi kule Yerusalemu walipowatuma makuhani wa Walawi kwake wamwulize: "Wewe u nani?"
<scripture passage="John 1:20" parsed="|John|1|20|0|0" osisRef="Bible:John.1.20" />
<sup>20</sup>Yohane hakukataa kujibu swali hilo, bali alisema waziwazi, "Mimi siye Kristo."
<scripture passage="John 1:21" parsed="|John|1|21|0|0" osisRef="Bible:John.1.21" />
<sup>21</sup>Hapo wakamwuliza, "Basi, wewe ni nani? Je, wewe ni Eliya?" Yohane akajibu, "La, mimi siye." Wakamwuliza, "Je, wewe ni yule nabii?" Yohane akawajibu, "La!"
<scripture passage="John 1:22" parsed="|John|1|22|0|0" osisRef="Bible:John.1.22" />
<sup>22</sup>Nao wakamwuliza, "Basi, wewe ni nani? Wasema nini juu yako mwenyewe? Tuambie, ili tuwapelekee jibu wale waliotutuma."
<scripture passage="John 1:23" parsed="|John|1|23|0|0" osisRef="Bible:John.1.23" />
<sup>23</sup>Yohane akawajibu, "Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: `Sauti ya mtu imesikika jangwani: Nyoosheni njia ya Bwana."`
<scripture passage="John 1:24" parsed="|John|1|24|0|0" osisRef="Bible:John.1.24" />
<sup>24</sup>Hao watu walikuwa wametumwa na Mafarisayo.
<scripture passage="John 1:25" parsed="|John|1|25|0|0" osisRef="Bible:John.1.25" />
<sup>25</sup>Basi, wakamwuliza Yohane, "Kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala yule nabii, mbona wabatiza?"
<scripture passage="John 1:26" parsed="|John|1|26|0|0" osisRef="Bible:John.1.26" />
<sup>26</sup>Yohane akawajibu, "Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.
<scripture passage="John 1:27" parsed="|John|1|27|0|0" osisRef="Bible:John.1.27" />
<sup>27</sup>Huyo anakuja baada yangu, lakini mimi sistahili hata kumfungua kamba za viatu vyake."
<scripture passage="John 1:28" parsed="|John|1|28|0|0" osisRef="Bible:John.1.28" />
<sup>28</sup>Mambo haya yalifanyika huko Bethania, ng`ambo ya mto Yordani ambako Yohane alikuwa anabatiza.
<scripture passage="John 1:29" parsed="|John|1|29|0|0" osisRef="Bible:John.1.29" />
<sup>29</sup>Kesho yake, Yohane alimwona Yesu akimjia, akasema, "Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu!
<scripture passage="John 1:30" parsed="|John|1|30|0|0" osisRef="Bible:John.1.30" />
<sup>30</sup>Huyu ndiye niliyesema juu yake: `Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!`
<scripture passage="John 1:31" parsed="|John|1|31|0|0" osisRef="Bible:John.1.31" />
<sup>31</sup>Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja kubatiza kwa maji ili watu wa Israeli wapate kumjua."
<scripture passage="John 1:32" parsed="|John|1|32|0|0" osisRef="Bible:John.1.32" />
<sup>32</sup>Huu ndio ushahidi Yohane alioutoa: "Nilimwona Roho akishuka kama njiwa kutoka mbinguni na kutua juu yake.
<scripture passage="John 1:33" parsed="|John|1|33|0|0" osisRef="Bible:John.1.33" />
<sup>33</sup>Mimi sikumjua, lakini yule aliyenituma nikabatize watu kwa maji alikuwa ameniambia: `Mtu yule utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye anayebatiza kwa Roho Mtakatifu.`
<scripture passage="John 1:34" parsed="|John|1|34|0|0" osisRef="Bible:John.1.34" />
<sup>34</sup>Mimi nimeona na ninawaambieni kwamba huyu ndiye Mwana wa Mungu."
<scripture passage="John 1:35" parsed="|John|1|35|0|0" osisRef="Bible:John.1.35" />
<sup>35</sup>Kesho yake, Yohane alikuwa tena mahali hapo pamoja na wanafunzi wake wawili.
<scripture passage="John 1:36" parsed="|John|1|36|0|0" osisRef="Bible:John.1.36" />
<sup>36</sup>Alipomwona Yesu akipita akasema, "Tazameni! Huyu ndiye Mwana-kondoo wa Mungu."
<scripture passage="John 1:37" parsed="|John|1|37|0|0" osisRef="Bible:John.1.37" />
<sup>37</sup>Hao wanafunzi walimsikia Yohane akisema maneno hayo, wakamfuata Yesu.
<scripture passage="John 1:38" parsed="|John|1|38|0|0" osisRef="Bible:John.1.38" />
<sup>38</sup>Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, "Mnatafuta nini?" Nao wakamjibu, "Rabi (yaani Mwalimu), unakaa wapi?"
<scripture passage="John 1:39" parsed="|John|1|39|0|0" osisRef="Bible:John.1.39" />
<sup>39</sup>Yesu akawaambia, "Njoni, nanyi mtaona." Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
<scripture passage="John 1:40" parsed="|John|1|40|0|0" osisRef="Bible:John.1.40" />
<sup>40</sup>Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa hao wawili waliokuwa wamemsikia Yohane akisema hivyo, wakamfuata Yesu.
<scripture passage="John 1:41" parsed="|John|1|41|0|0" osisRef="Bible:John.1.41" />
<sup>41</sup>Andrea alimkuta kwanza Simoni, ndugu yake, akamwambia, "Tumemwona Masiha" (maana yake Kristo).
<scripture passage="John 1:42" parsed="|John|1|42|0|0" osisRef="Bible:John.1.42" />
<sup>42</sup>Kisha akampeleka Simoni kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama Simoni akasema, "Wewe ni Simoni mwana wa Yohane. Sasa utaitwa Kefa." (maana yake ni Petro, yaani, "Mwamba.")
<scripture passage="John 1:43" parsed="|John|1|43|0|0" osisRef="Bible:John.1.43" />
<sup>43</sup>Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, "Nifuate."
<scripture passage="John 1:44" parsed="|John|1|44|0|0" osisRef="Bible:John.1.44" />
<sup>44</sup>Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andrea na Petro.
<scripture passage="John 1:45" parsed="|John|1|45|0|0" osisRef="Bible:John.1.45" />
<sup>45</sup>Naye Filipo akamkuta Nathanieli, akamwambia, "Tumemwona yule ambaye Mose aliandika juu yake katika kitabu cha Sheria, na ambaye manabii waliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutoka Nazareti."
<scripture passage="John 1:46" parsed="|John|1|46|0|0" osisRef="Bible:John.1.46" />
<sup>46</sup>Naye Nathanieli akamwuliza Filipo, "Je, kitu chema chaweza kutoka Nazareti?" Filipo akamwambia, "Njoo uone."
<scripture passage="John 1:47" parsed="|John|1|47|0|0" osisRef="Bible:John.1.47" />
<sup>47</sup>Yesu alipomwona Nathanieli akimjia alisema juu yake, "Tazameni! Huyo ni Mwisraeli halisi: hamna hila ndani yake."
<scripture passage="John 1:48" parsed="|John|1|48|0|0" osisRef="Bible:John.1.48" />
<sup>48</sup>Naye Nathanieli akamwuliza, "Umepataje kunijua?" Yesu akamwambia, "Ulipokuwa chini ya mtini hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona."
<scripture passage="John 1:49" parsed="|John|1|49|0|0" osisRef="Bible:John.1.49" />
<sup>49</sup>Hapo Nathanieli akamwambia, "Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu. Wewe ni Mfalme wa Israeli!"
<scripture passage="John 1:50" parsed="|John|1|50|0|0" osisRef="Bible:John.1.50" />
<sup>50</sup>Yesu akamwambia, "Je, umeamini kwa kuwa nimekwambia kwamba nilikuona chini ya mtini? Utaona makubwa zaidi kuliko haya."
<scripture passage="John 1:51" parsed="|John|1|51|0|0" osisRef="Bible:John.1.51" />
<sup>51</sup>Yesu akaendelea kusema, "Nawaambieni kweli, mtaona mbingu zinafunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Mtu."
</p>
</div3>

<div3 title="John 2" progress="34.48%" prev="John.1" next="John.3" id="John.2">
<h3 id="John.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="John.2-p1">
<scripture passage="John 2:1" parsed="|John|2|1|0|0" osisRef="Bible:John.2.1" />
<sup>1</sup>Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo,
<scripture passage="John 2:2" parsed="|John|2|2|0|0" osisRef="Bible:John.2.2" />
<sup>2</sup>naye Yesu alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
<scripture passage="John 2:3" parsed="|John|2|3|0|0" osisRef="Bible:John.2.3" />
<sup>3</sup>Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, "Hawana divai!"
<scripture passage="John 2:4" parsed="|John|2|4|0|0" osisRef="Bible:John.2.4" />
<sup>4</sup>Yesu akamjibu, "Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado."
<scripture passage="John 2:5" parsed="|John|2|5|0|0" osisRef="Bible:John.2.5" />
<sup>5</sup>Hapo mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambieni, fanyeni."
<scripture passage="John 2:6" parsed="|John|2|6|0|0" osisRef="Bible:John.2.6" />
<sup>6</sup>Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
<scripture passage="John 2:7" parsed="|John|2|7|0|0" osisRef="Bible:John.2.7" />
<sup>7</sup>Yesu akawaambia, "Ijazeni mitungi hiyo maji." Nao wakaijaza mpaka juu.
<scripture passage="John 2:8" parsed="|John|2|8|0|0" osisRef="Bible:John.2.8" />
<sup>8</sup>Kisha akawaambia, "Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu."
<scripture passage="John 2:9" parsed="|John|2|9|0|0" osisRef="Bible:John.2.9" />
<sup>9</sup>Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi,
<scripture passage="John 2:10" parsed="|John|2|10|0|0" osisRef="Bible:John.2.10" />
<sup>10</sup>akamwambia, "Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!"
<scripture passage="John 2:11" parsed="|John|2|11|0|0" osisRef="Bible:John.2.11" />
<sup>11</sup>Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
<scripture passage="John 2:12" parsed="|John|2|12|0|0" osisRef="Bible:John.2.12" />
<sup>12</sup>Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.
<scripture passage="John 2:13" parsed="|John|2|13|0|0" osisRef="Bible:John.2.13" />
<sup>13</sup>Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.
<scripture passage="John 2:14" parsed="|John|2|14|0|0" osisRef="Bible:John.2.14" />
<sup>14</sup>Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng`ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
<scripture passage="John 2:15" parsed="|John|2|15|0|0" osisRef="Bible:John.2.15" />
<sup>15</sup>Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng`ombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.
<scripture passage="John 2:16" parsed="|John|2|16|0|0" osisRef="Bible:John.2.16" />
<sup>16</sup>Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, "Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!"
<scripture passage="John 2:17" parsed="|John|2|17|0|0" osisRef="Bible:John.2.17" />
<sup>17</sup>Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: "Upendo wangu kwa nyumba yako waniua."
<scripture passage="John 2:18" parsed="|John|2|18|0|0" osisRef="Bible:John.2.18" />
<sup>18</sup>Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, "Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?"
<scripture passage="John 2:19" parsed="|John|2|19|0|0" osisRef="Bible:John.2.19" />
<sup>19</sup>Yesu akawaambia, "Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu."
<scripture passage="John 2:20" parsed="|John|2|20|0|0" osisRef="Bible:John.2.20" />
<sup>20</sup>Hapo Wayahudi wakasema, "Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?"
<scripture passage="John 2:21" parsed="|John|2|21|0|0" osisRef="Bible:John.2.21" />
<sup>21</sup>Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake.
<scripture passage="John 2:22" parsed="|John|2|22|0|0" osisRef="Bible:John.2.22" />
<sup>22</sup>Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.
<scripture passage="John 2:23" parsed="|John|2|23|0|0" osisRef="Bible:John.2.23" />
<sup>23</sup>Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizozifanya.
<scripture passage="John 2:24" parsed="|John|2|24|0|0" osisRef="Bible:John.2.24" />
<sup>24</sup>Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote.
<scripture passage="John 2:25" parsed="|John|2|25|0|0" osisRef="Bible:John.2.25" />
<sup>25</sup>Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.
</p>
</div3>

<div3 title="John 3" progress="34.76%" prev="John.2" next="John.4" id="John.3">
<h3 id="John.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="John.3-p1">
<scripture passage="John 3:1" parsed="|John|3|1|0|0" osisRef="Bible:John.3.1" />
<sup>1</sup>Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo.
<scripture passage="John 3:2" parsed="|John|3|2|0|0" osisRef="Bible:John.3.2" />
<sup>2</sup>Siku moja alimwendea Yesu usiku, akamwambia, "Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye."
<scripture passage="John 3:3" parsed="|John|3|3|0|0" osisRef="Bible:John.3.3" />
<sup>3</sup>Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme wa Mungu."
<scripture passage="John 3:4" parsed="|John|3|4|0|0" osisRef="Bible:John.3.4" />
<sup>4</sup>Nikodemo akamwuliza, "Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa mara ya pili!"
<scripture passage="John 3:5" parsed="|John|3|5|0|0" osisRef="Bible:John.3.5" />
<sup>5</sup>Yesu akamjibu, "Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.
<scripture passage="John 3:6" parsed="|John|3|6|0|0" osisRef="Bible:John.3.6" />
<sup>6</sup>Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho.
<scripture passage="John 3:7" parsed="|John|3|7|0|0" osisRef="Bible:John.3.7" />
<sup>7</sup>Usistaajabu kwamba nimekwambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya.
<scripture passage="John 3:8" parsed="|John|3|8|0|0" osisRef="Bible:John.3.8" />
<sup>8</sup>Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho."
<scripture passage="John 3:9" parsed="|John|3|9|0|0" osisRef="Bible:John.3.9" />
<sup>9</sup>Nikodemo akamwuliza, "Mambo haya yanawezekanaje?"
<scripture passage="John 3:10" parsed="|John|3|10|0|0" osisRef="Bible:John.3.10" />
<sup>10</sup>Yesu akamjibu, "Je, wewe ni mwalimu katika Israel na huyajui mambo haya?
<scripture passage="John 3:11" parsed="|John|3|11|0|0" osisRef="Bible:John.3.11" />
<sup>11</sup>Kweli nakwambia, sisi twasema tunayoyajua na kushuhudia tuliyoyaona, lakini ninyi hamkubali ujumbe wetu.
<scripture passage="John 3:12" parsed="|John|3|12|0|0" osisRef="Bible:John.3.12" />
<sup>12</sup>Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyi hamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya mbinguni?
<scripture passage="John 3:13" parsed="|John|3|13|0|0" osisRef="Bible:John.3.13" />
<sup>13</sup>Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu ambaye ameshuka kutoka mbinguni.
<scripture passage="John 3:14" parsed="|John|3|14|0|0" osisRef="Bible:John.3.14" />
<sup>14</sup>"Kama vile Mose alivyomwinua juu nyoka wa shaba kule jangwani, naye Mwana wa Mtu atainuliwa juu vivyo hivyo,
<scripture passage="John 3:15" parsed="|John|3|15|0|0" osisRef="Bible:John.3.15" />
<sup>15</sup>ili kila anayemwamini awe na uzima wa milele.
<scripture passage="John 3:16" parsed="|John|3|16|0|0" osisRef="Bible:John.3.16" />
<sup>16</sup>Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
<scripture passage="John 3:17" parsed="|John|3|17|0|0" osisRef="Bible:John.3.17" />
<sup>17</sup>Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe ulimwengu.
<scripture passage="John 3:18" parsed="|John|3|18|0|0" osisRef="Bible:John.3.18" />
<sup>18</sup>"Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu.
<scripture passage="John 3:19" parsed="|John|3|19|0|0" osisRef="Bible:John.3.19" />
<sup>19</sup>Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu.
<scripture passage="John 3:20" parsed="|John|3|20|0|0" osisRef="Bible:John.3.20" />
<sup>20</sup>Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe.
<scripture passage="John 3:21" parsed="|John|3|21|0|0" osisRef="Bible:John.3.21" />
<sup>21</sup>Lakini mwenye kuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu."
<scripture passage="John 3:22" parsed="|John|3|22|0|0" osisRef="Bible:John.3.22" />
<sup>22</sup>Baada ya hayo, Yesu alifika mkoani Yudea pamoja na wanafunzi wake. Alikaa huko pamoja nao kwa muda, akibatiza watu.
<scripture passage="John 3:23" parsed="|John|3|23|0|0" osisRef="Bible:John.3.23" />
<sup>23</sup>Yohane pia alikuwa akibatiza watu huko Ainoni, karibu na Salemu, maana huko kulikuwa na maji mengi. Watu walimwendea, naye akawabatiza.
<scripture passage="John 3:24" parsed="|John|3|24|0|0" osisRef="Bible:John.3.24" />
<sup>24</sup>Wakati huo Yohane alikuwa bado hajafungwa gerezani.)
<scripture passage="John 3:25" parsed="|John|3|25|0|0" osisRef="Bible:John.3.25" />
<sup>25</sup>Ubishi ulitokea kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohane na Myahudi mmoja kuhusu desturi za kutawadha.
<scripture passage="John 3:26" parsed="|John|3|26|0|0" osisRef="Bible:John.3.26" />
<sup>26</sup>Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, "Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng`ambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea."
<scripture passage="John 3:27" parsed="|John|3|27|0|0" osisRef="Bible:John.3.27" />
<sup>27</sup>Yohane akawaambia, "Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu.
<scripture passage="John 3:28" parsed="|John|3|28|0|0" osisRef="Bible:John.3.28" />
<sup>28</sup>Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: `Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!`
<scripture passage="John 3:29" parsed="|John|3|29|0|0" osisRef="Bible:John.3.29" />
<sup>29</sup>Bibiarusi ni wake bwanaarusi, lakini rafiki yake bwana arusi, anayesimama na kusikiliza, hufurahi sana anapomsikia bwana arusi akisema. Ndivyo furaha yangu ilivyokamilishwa.
<scripture passage="John 3:30" parsed="|John|3|30|0|0" osisRef="Bible:John.3.30" />
<sup>30</sup>Ni lazima yeye azidi kuwa maarufu, na mimi nipungue.
<scripture passage="John 3:31" parsed="|John|3|31|0|0" osisRef="Bible:John.3.31" />
<sup>31</sup>"Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.
<scripture passage="John 3:32" parsed="|John|3|32|0|0" osisRef="Bible:John.3.32" />
<sup>32</sup>Yeye husema yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna mtu anayekubali ujumbe wake.
<scripture passage="John 3:33" parsed="|John|3|33|0|0" osisRef="Bible:John.3.33" />
<sup>33</sup>Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli.
<scripture passage="John 3:34" parsed="|John|3|34|0|0" osisRef="Bible:John.3.34" />
<sup>34</sup>Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.
<scripture passage="John 3:35" parsed="|John|3|35|0|0" osisRef="Bible:John.3.35" />
<sup>35</sup>Baba anampenda Mwana na amemkabidhi vitu vyote.
<scripture passage="John 3:36" parsed="|John|3|36|0|0" osisRef="Bible:John.3.36" />
<sup>36</sup>Anayemwamini Mwana anao uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatakuwa na uzima wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake."
</p>
</div3>

<div3 title="John 4" progress="35.15%" prev="John.3" next="John.5" id="John.4">
<h3 id="John.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="John.4-p1">
<scripture passage="John 4:1" parsed="|John|4|1|0|0" osisRef="Bible:John.4.1" />
<sup>1</sup>Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane.
<scripture passage="John 4:2" parsed="|John|4|2|0|0" osisRef="Bible:John.4.2" />
<sup>2</sup>Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.)
<scripture passage="John 4:3" parsed="|John|4|3|0|0" osisRef="Bible:John.4.3" />
<sup>3</sup>Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;
<scripture passage="John 4:4" parsed="|John|4|4|0|0" osisRef="Bible:John.4.4" />
<sup>4</sup>na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
<scripture passage="John 4:5" parsed="|John|4|5|0|0" osisRef="Bible:John.4.5" />
<sup>5</sup>Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
<scripture passage="John 4:6" parsed="|John|4|6|0|0" osisRef="Bible:John.4.6" />
<sup>6</sup>Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
<scripture passage="John 4:7" parsed="|John|4|7|0|0" osisRef="Bible:John.4.7" />
<sup>7</sup>Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, "Nipatie maji ninywe."
<scripture passage="John 4:8" parsed="|John|4|8|0|0" osisRef="Bible:John.4.8" />
<sup>8</sup>(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
<scripture passage="John 4:9" parsed="|John|4|9|0|0" osisRef="Bible:John.4.9" />
<sup>9</sup>Lakini huyo mwanamke akamwambia, "Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?" (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.)
<scripture passage="John 4:10" parsed="|John|4|10|0|0" osisRef="Bible:John.4.10" />
<sup>10</sup>Yesu akamjibu, "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: `Nipatie maji ninywe,` ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai."
<scripture passage="John 4:11" parsed="|John|4|11|0|0" osisRef="Bible:John.4.11" />
<sup>11</sup>Huyo mama akasema, "Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai?
<scripture passage="John 4:12" parsed="|John|4|12|0|0" osisRef="Bible:John.4.12" />
<sup>12</sup>Au, labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki."
<scripture passage="John 4:13" parsed="|John|4|13|0|0" osisRef="Bible:John.4.13" />
<sup>13</sup>Yesu akamjibu, "Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena.
<scripture passage="John 4:14" parsed="|John|4|14|0|0" osisRef="Bible:John.4.14" />
<sup>14</sup>Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uzima na kumpatia uzima wa milele."
<scripture passage="John 4:15" parsed="|John|4|15|0|0" osisRef="Bible:John.4.15" />
<sup>15</sup>Huyo mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; nisije tena mpaka hapa kuteka maji."
<scripture passage="John 4:16" parsed="|John|4|16|0|0" osisRef="Bible:John.4.16" />
<sup>16</sup>Yesu akamwambia, "Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa."
<scripture passage="John 4:17" parsed="|John|4|17|0|0" osisRef="Bible:John.4.17" />
<sup>17</sup>Huyo mwanamke akamwambia, "Mimi sina mume." Yesu akamwambia, "Umesema kweli, kwamba huna mume.
<scripture passage="John 4:18" parsed="|John|4|18|0|0" osisRef="Bible:John.4.18" />
<sup>18</sup>Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishi naye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli."
<scripture passage="John 4:19" parsed="|John|4|19|0|0" osisRef="Bible:John.4.19" />
<sup>19</sup>Huyo Mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, naona ya kuwa wewe u nabii.
<scripture passage="John 4:20" parsed="|John|4|20|0|0" osisRef="Bible:John.4.20" />
<sup>20</sup>Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudu Mungu ni kule Yerusalemu."
<scripture passage="John 4:21" parsed="|John|4|21|0|0" osisRef="Bible:John.4.21" />
<sup>21</sup>Yesu akamwambia, "Niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu.
<scripture passage="John 4:22" parsed="|John|4|22|0|0" osisRef="Bible:John.4.22" />
<sup>22</sup>Ninyi Wasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi.
<scripture passage="John 4:23" parsed="|John|4|23|0|0" osisRef="Bible:John.4.23" />
<sup>23</sup>Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.
<scripture passage="John 4:24" parsed="|John|4|24|0|0" osisRef="Bible:John.4.24" />
<sup>24</sup>Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake."
<scripture passage="John 4:25" parsed="|John|4|25|0|0" osisRef="Bible:John.4.25" />
<sup>25</sup>Huyo mama akamwambia, "Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu."
<scripture passage="John 4:26" parsed="|John|4|26|0|0" osisRef="Bible:John.4.26" />
<sup>26</sup>Yesu akamwambia, "Mimi ninayesema nawe, ndiye."
<scripture passage="John 4:27" parsed="|John|4|27|0|0" osisRef="Bible:John.4.27" />
<sup>27</sup>Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: "Unataka nini?" au, "Kwa nini unaongea na mwanamke?"
<scripture passage="John 4:28" parsed="|John|4|28|0|0" osisRef="Bible:John.4.28" />
<sup>28</sup>Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu,
<scripture passage="John 4:29" parsed="|John|4|29|0|0" osisRef="Bible:John.4.29" />
<sup>29</sup>"Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?"
<scripture passage="John 4:30" parsed="|John|4|30|0|0" osisRef="Bible:John.4.30" />
<sup>30</sup>Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.
<scripture passage="John 4:31" parsed="|John|4|31|0|0" osisRef="Bible:John.4.31" />
<sup>31</sup>Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: "Mwalimu, ule chakula."
<scripture passage="John 4:32" parsed="|John|4|32|0|0" osisRef="Bible:John.4.32" />
<sup>32</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi."
<scripture passage="John 4:33" parsed="|John|4|33|0|0" osisRef="Bible:John.4.33" />
<sup>33</sup>Wanafunzi wake wakaulizana, "Je, kuna mtu aliyemletea chakula?"
<scripture passage="John 4:34" parsed="|John|4|34|0|0" osisRef="Bible:John.4.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.
<scripture passage="John 4:35" parsed="|John|4|35|0|0" osisRef="Bible:John.4.35" />
<sup>35</sup>Ninyi mwasema: `Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika!` Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.
<scripture passage="John 4:36" parsed="|John|4|36|0|0" osisRef="Bible:John.4.36" />
<sup>36</sup>Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.
<scripture passage="John 4:37" parsed="|John|4|37|0|0" osisRef="Bible:John.4.37" />
<sup>37</sup>Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: `Mmoja hupanda na mwingine huvuna.`
<scripture passage="John 4:38" parsed="|John|4|38|0|0" osisRef="Bible:John.4.38" />
<sup>38</sup>Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao."
<scripture passage="John 4:39" parsed="|John|4|39|0|0" osisRef="Bible:John.4.39" />
<sup>39</sup>Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: "Ameniambia mambo yote niliyofanya."
<scripture passage="John 4:40" parsed="|John|4|40|0|0" osisRef="Bible:John.4.40" />
<sup>40</sup>Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili.
<scripture passage="John 4:41" parsed="|John|4|41|0|0" osisRef="Bible:John.4.41" />
<sup>41</sup>Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbe wake.
<scripture passage="John 4:42" parsed="|John|4|42|0|0" osisRef="Bible:John.4.42" />
<sup>42</sup>Wakamwambia yule mama, "Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu."
<scripture passage="John 4:43" parsed="|John|4|43|0|0" osisRef="Bible:John.4.43" />
<sup>43</sup>Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya.
<scripture passage="John 4:44" parsed="|John|4|44|0|0" osisRef="Bible:John.4.44" />
<sup>44</sup>Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, "Nabii hapati heshima katika nchi yake."
<scripture passage="John 4:45" parsed="|John|4|45|0|0" osisRef="Bible:John.4.45" />
<sup>45</sup>Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
<scripture passage="John 4:46" parsed="|John|4|46|0|0" osisRef="Bible:John.4.46" />
<sup>46</sup>Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
<scripture passage="John 4:47" parsed="|John|4|47|0|0" osisRef="Bible:John.4.47" />
<sup>47</sup>Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
<scripture passage="John 4:48" parsed="|John|4|48|0|0" osisRef="Bible:John.4.48" />
<sup>48</sup>Yesu akamwambia, "Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!"
<scripture passage="John 4:49" parsed="|John|4|49|0|0" osisRef="Bible:John.4.49" />
<sup>49</sup>Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa."
<scripture passage="John 4:50" parsed="|John|4|50|0|0" osisRef="Bible:John.4.50" />
<sup>50</sup>Yesu akamwambia, "Nenda tu, mwanao yu mzima." Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
<scripture passage="John 4:51" parsed="|John|4|51|0|0" osisRef="Bible:John.4.51" />
<sup>51</sup>Alipokuwa bado njiani, watumishi wake walikutana naye, wakamwambia kwamba mwanawe alikuwa mzima.
<scripture passage="John 4:52" parsed="|John|4|52|0|0" osisRef="Bible:John.4.52" />
<sup>52</sup>Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, "Jana saa saba mchana, homa ilimwacha."
<scripture passage="John 4:53" parsed="|John|4|53|0|0" osisRef="Bible:John.4.53" />
<sup>53</sup>Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: "Mwanao yu mzima." Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
<scripture passage="John 4:54" parsed="|John|4|54|0|0" osisRef="Bible:John.4.54" />
<sup>54</sup>Hii ilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudea kwenda Galilaya.
</p>
</div3>

<div3 title="John 5" progress="35.74%" prev="John.4" next="John.6" id="John.5">
<h3 id="John.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="John.5-p1">
<scripture passage="John 5:1" parsed="|John|5|1|0|0" osisRef="Bible:John.5.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akaenda Yerusalemu.
<scripture passage="John 5:2" parsed="|John|5|2|0|0" osisRef="Bible:John.5.2" />
<sup>2</sup>Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, kulikuwa na bwawa la maji liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa na baraza tano zenye matao.
<scripture passage="John 5:3" parsed="|John|5|3|0|0" osisRef="Bible:John.5.3" />
<sup>3</sup>Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: vipofu, viwete na waliopooza.<i>fa</i>
<scripture passage="John 5:4" parsed="|John|5|4|0|0" osisRef="Bible:John.5.4" />
<sup>4</sup>missing

<sup>4</sup>maana mara kwa mara malaika alishuka majini nyakati fulani na kuyatibua. Mtu yeyote aliyekuwa wa kwanza kuingia majini baada ya maji kutibuliwa, alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao.
<scripture passage="John 5:5" parsed="|John|5|5|0|0" osisRef="Bible:John.5.5" />
<sup>5</sup>Basi, hapo palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane.
<scripture passage="John 5:6" parsed="|John|5|6|0|0" osisRef="Bible:John.5.6" />
<sup>6</sup>Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, "Je, wataka kupona?"
<scripture passage="John 5:7" parsed="|John|5|7|0|0" osisRef="Bible:John.5.7" />
<sup>7</sup>Naye akajibu, "Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia."
<scripture passage="John 5:8" parsed="|John|5|8|0|0" osisRef="Bible:John.5.8" />
<sup>8</sup>Yesu akamwambia, "Inuka, chukua mkeka wako utembee."
<scripture passage="John 5:9" parsed="|John|5|9|0|0" osisRef="Bible:John.5.9" />
<sup>9</sup>Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.
<scripture passage="John 5:10" parsed="|John|5|10|0|0" osisRef="Bible:John.5.10" />
<sup>10</sup>Kwa hiyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia huyo mtu aliyeponywa, "Leo ni Sabato, si halali kubeba mkeka wako."
<scripture passage="John 5:11" parsed="|John|5|11|0|0" osisRef="Bible:John.5.11" />
<sup>11</sup>Lakini yeye akawaambia, "Yule mtu aliyeniponya ndiye aliyeniambia: `Chukua mkeka wako, tembea."`
<scripture passage="John 5:12" parsed="|John|5|12|0|0" osisRef="Bible:John.5.12" />
<sup>12</sup>Nao wakamwuliza, "Huyo mtu aliyekwambia: `Chukua mkeka wako, tembea,` ni nani?"
<scripture passage="John 5:13" parsed="|John|5|13|0|0" osisRef="Bible:John.5.13" />
<sup>13</sup>Lakini yeye hakumjua huyo mtu aliyemponya, maana Yesu alikuwa amekwisha ondoka mahali hapo, kwani palikuwa na umati mkubwa wa watu.
<scripture passage="John 5:14" parsed="|John|5|14|0|0" osisRef="Bible:John.5.14" />
<sup>14</sup>Basi, baadaye Yesu alimkuta huyo aliyeponywa Hekaluni, akamwambia, "Sasa umepona; usitende dhambi tena, usije ukapatwa na jambo baya zaidi."
<scripture passage="John 5:15" parsed="|John|5|15|0|0" osisRef="Bible:John.5.15" />
<sup>15</sup>Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.
<scripture passage="John 5:16" parsed="|John|5|16|0|0" osisRef="Bible:John.5.16" />
<sup>16</sup>Kwa vile Yesu alifanya jambo hilo siku ya Sabato, Wayahudi walianza kumdhulumu.
<scripture passage="John 5:17" parsed="|John|5|17|0|0" osisRef="Bible:John.5.17" />
<sup>17</sup>Basi, Yesu akawaambia, "Baba yangu anafanya kazi daima, nami pia nafanya kazi."
<scripture passage="John 5:18" parsed="|John|5|18|0|0" osisRef="Bible:John.5.18" />
<sup>18</sup>Kwa sababu ya maneno haya, viongozi wa Wayahudi walizidi kutafuta njia ya kumwua Yesu: si kwa kuwa aliivunja Sheria ya Sabato tu, bali pia kwa kuwa alisema kwamba Mungu ni Baba yake, na hivyo akajifanya sawa na Mungu.
<scripture passage="John 5:19" parsed="|John|5|19|0|0" osisRef="Bible:John.5.19" />
<sup>19</sup>Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
<scripture passage="John 5:20" parsed="|John|5|20|0|0" osisRef="Bible:John.5.20" />
<sup>20</sup>Baba ampenda Mwana, na humwonyesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonyesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.
<scripture passage="John 5:21" parsed="|John|5|21|0|0" osisRef="Bible:John.5.21" />
<sup>21</sup>Kama vile Baba huwafufua wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uzima wale anaopenda.
<scripture passage="John 5:22" parsed="|John|5|22|0|0" osisRef="Bible:John.5.22" />
<sup>22</sup>Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuli yote ya hukumu amemkabidhi Mwana,
<scripture passage="John 5:23" parsed="|John|5|23|0|0" osisRef="Bible:John.5.23" />
<sup>23</sup>ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba ambaye amemtuma.
<scripture passage="John 5:24" parsed="|John|5|24|0|0" osisRef="Bible:John.5.24" />
<sup>24</sup>"Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifo na kuingia katika uzima.
<scripture passage="John 5:25" parsed="|John|5|25|0|0" osisRef="Bible:John.5.25" />
<sup>25</sup>Kweli nawaambieni, wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia, wataishi.
<scripture passage="John 5:26" parsed="|John|5|26|0|0" osisRef="Bible:John.5.26" />
<sup>26</sup>Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanawe kuwa asili ya uhai.
<scripture passage="John 5:27" parsed="|John|5|27|0|0" osisRef="Bible:John.5.27" />
<sup>27</sup>Tena amempa mamlaka ya kuhukumu kwa sababu yeye ni Mwana wa Mtu.
<scripture passage="John 5:28" parsed="|John|5|28|0|0" osisRef="Bible:John.5.28" />
<sup>28</sup>Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake,
<scripture passage="John 5:29" parsed="|John|5|29|0|0" osisRef="Bible:John.5.29" />
<sup>29</sup>nao watafufuka: wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.
<scripture passage="John 5:30" parsed="|John|5|30|0|0" osisRef="Bible:John.5.30" />
<sup>30</sup>"Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule aliyenituma.
<scripture passage="John 5:31" parsed="|John|5|31|0|0" osisRef="Bible:John.5.31" />
<sup>31</sup>Nikijishuhudia mimi mwenyewe, ushahidi wangu hauwezi kukubaliwa kuwa wa kweli.
<scripture passage="John 5:32" parsed="|John|5|32|0|0" osisRef="Bible:John.5.32" />
<sup>32</sup>Lakini yuko mwingine ambaye hutoa ushahidi juu yangu, nami najua kwamba yote anayosema juu yangu ni ya kweli.
<scripture passage="John 5:33" parsed="|John|5|33|0|0" osisRef="Bible:John.5.33" />
<sup>33</sup>Ninyi mlituma ujumbe kwa Yohane naye aliushuhudia ukweli.
<scripture passage="John 5:34" parsed="|John|5|34|0|0" osisRef="Bible:John.5.34" />
<sup>34</sup>Si kwamba mimi nautegemea ushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ili mpate kuokolewa.
<scripture passage="John 5:35" parsed="|John|5|35|0|0" osisRef="Bible:John.5.35" />
<sup>35</sup>Yohane alikuwa kama taa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwa kitambo.
<scripture passage="John 5:36" parsed="|John|5|36|0|0" osisRef="Bible:John.5.36" />
<sup>36</sup>Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.
<scripture passage="John 5:37" parsed="|John|5|37|0|0" osisRef="Bible:John.5.37" />
<sup>37</sup>Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,
<scripture passage="John 5:38" parsed="|John|5|38|0|0" osisRef="Bible:John.5.38" />
<sup>38</sup>na ujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma.
<scripture passage="John 5:39" parsed="|John|5|39|0|0" osisRef="Bible:John.5.39" />
<sup>39</sup>Ninyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uzima wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!
<scripture passage="John 5:40" parsed="|John|5|40|0|0" osisRef="Bible:John.5.40" />
<sup>40</sup>Hata hivyo, ninyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima. ic
<scripture passage="John 5:41" parsed="|John|5|41|0|0" osisRef="Bible:John.5.41" />
<sup>41</sup>"Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu.
<scripture passage="John 5:42" parsed="|John|5|42|0|0" osisRef="Bible:John.5.42" />
<sup>42</sup>Lakini nawajua ninyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu.
<scripture passage="John 5:43" parsed="|John|5|43|0|0" osisRef="Bible:John.5.43" />
<sup>43</sup>Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea.
<scripture passage="John 5:44" parsed="|John|5|44|0|0" osisRef="Bible:John.5.44" />
<sup>44</sup>Mwawezaje kuamini, hali ninyi mnapenda kupokea sifa kutoka kwenu ninyi wenyewe, wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu?
<scripture passage="John 5:45" parsed="|John|5|45|0|0" osisRef="Bible:John.5.45" />
<sup>45</sup>Msifikiri kwamba mimi nitawashtaki kwa Baba. Mose ambaye ninyi mmemtumainia ndiye atakayewashtaki.
<scripture passage="John 5:46" parsed="|John|5|46|0|0" osisRef="Bible:John.5.46" />
<sup>46</sup>Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia; maana Mose aliandika juu yangu.
<scripture passage="John 5:47" parsed="|John|5|47|0|0" osisRef="Bible:John.5.47" />
<sup>47</sup>Lakini hamuyaamini yale aliyoandika, mtawezaje basi, kuamini maneno yangu?"
</p>
</div3>

<div3 title="John 6" progress="36.29%" prev="John.5" next="John.7" id="John.6">
<h3 id="John.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="John.6-p1">
<scripture passage="John 6:1" parsed="|John|6|1|0|0" osisRef="Bible:John.6.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa Tiberia).
<scripture passage="John 6:2" parsed="|John|6|2|0|0" osisRef="Bible:John.6.2" />
<sup>2</sup>Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa.
<scripture passage="John 6:3" parsed="|John|6|3|0|0" osisRef="Bible:John.6.3" />
<sup>3</sup>Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake.
<scripture passage="John 6:4" parsed="|John|6|4|0|0" osisRef="Bible:John.6.4" />
<sup>4</sup>Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia.
<scripture passage="John 6:5" parsed="|John|6|5|0|0" osisRef="Bible:John.6.5" />
<sup>5</sup>Basi, Yesu na alipotazama na kuona umati wa watu ukija kwake, alimwambia Filipo, "Tununue wapi mikate ili watu hawa wapate kula?"
<scripture passage="John 6:6" parsed="|John|6|6|0|0" osisRef="Bible:John.6.6" />
<sup>6</sup>Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.)
<scripture passage="John 6:7" parsed="|John|6|7|0|0" osisRef="Bible:John.6.7" />
<sup>7</sup>Filipo akamjibu, "Mikate ya denari mia mbili za fedha haiwatoshi watu hawa hata kama ila mmoja atapata kipande kidogo tu!"
<scripture passage="John 6:8" parsed="|John|6|8|0|0" osisRef="Bible:John.6.8" />
<sup>8</sup>Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,
<scripture passage="John 6:9" parsed="|John|6|9|0|0" osisRef="Bible:John.6.9" />
<sup>9</sup>"Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?"
<scripture passage="John 6:10" parsed="|John|6|10|0|0" osisRef="Bible:John.6.10" />
<sup>10</sup>Yesu akasema, "Waketisheni watu." Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume elfu tano.
<scripture passage="John 6:11" parsed="|John|6|11|0|0" osisRef="Bible:John.6.11" />
<sup>11</sup>Yesu akaitwaa ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia watu waliokuwa wameketi; akafanya vivyo hivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
<scripture passage="John 6:12" parsed="|John|6|12|0|0" osisRef="Bible:John.6.12" />
<sup>12</sup>Watu waliposhiba Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Kusanyeni vipande vilivyobaki visipotee."
<scripture passage="John 6:13" parsed="|John|6|13|0|0" osisRef="Bible:John.6.13" />
<sup>13</sup>Basi, wakakusanya vipande vya mikate ya shayiri walivyobakiza wale watu waliokula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
<scripture passage="John 6:14" parsed="|John|6|14|0|0" osisRef="Bible:John.6.14" />
<sup>14</sup>Watu walipoiona ishara hiyo aliyoifanya Yesu, wakasema, "Hakika huyu ndiye nabii anayekuja ulimwenguni."
<scripture passage="John 6:15" parsed="|John|6|15|0|0" osisRef="Bible:John.6.15" />
<sup>15</sup>Yesu akajua ya kuwa watu walitaka kumchukua wamfanye mfalme, akaondoka tena, akaenda mlimani peke yake. ic
<scripture passage="John 6:16" parsed="|John|6|16|0|0" osisRef="Bible:John.6.16" />
<sup>16</sup>Ilipokuwa jioni wanafunzi wake waliteremka hadi ziwani,
<scripture passage="John 6:17" parsed="|John|6|17|0|0" osisRef="Bible:John.6.17" />
<sup>17</sup>wakapanda mashua ili wavuke kwenda Kafarnaumu. Giza lilikuwa limeingia, na Yesu alikuwa hajawafikia bado.
<scripture passage="John 6:18" parsed="|John|6|18|0|0" osisRef="Bible:John.6.18" />
<sup>18</sup>Ziwa likaanza kuchafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma.
<scripture passage="John 6:19" parsed="|John|6|19|0|0" osisRef="Bible:John.6.19" />
<sup>19</sup>Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
<scripture passage="John 6:20" parsed="|John|6|20|0|0" osisRef="Bible:John.6.20" />
<sup>20</sup>Yesu akawaambia, "Ni mimi, msiogope!"
<scripture passage="John 6:21" parsed="|John|6|21|0|0" osisRef="Bible:John.6.21" />
<sup>21</sup>Walifurahi kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walipokuwa wanakwenda.
<scripture passage="John 6:22" parsed="|John|6|22|0|0" osisRef="Bible:John.6.22" />
<sup>22</sup>Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
<scripture passage="John 6:23" parsed="|John|6|23|0|0" osisRef="Bible:John.6.23" />
<sup>23</sup>Mashua nyingine kutoka Tiberia zilifika mahali hapo watu walipokula ile mikate, Bwana alipokwisha mshukuru Mungu.
<scripture passage="John 6:24" parsed="|John|6|24|0|0" osisRef="Bible:John.6.24" />
<sup>24</sup>Basi, hao watu walipogundua kwamba Yesu na wanafunzi wake hawakuwapo mahali hapo, walipanda mashua, wakaenda Kafarnaumu wakimtafuta.
<scripture passage="John 6:25" parsed="|John|6|25|0|0" osisRef="Bible:John.6.25" />
<sup>25</sup>Wale watu walipomkuta Yesu ng`ambo ya pili wa ziwa walimwuliza, "Mwalimu, ulifika lini hapa?"
<scripture passage="John 6:26" parsed="|John|6|26|0|0" osisRef="Bible:John.6.26" />
<sup>26</sup>Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.
<scripture passage="John 6:27" parsed="|John|6|27|0|0" osisRef="Bible:John.6.27" />
<sup>27</sup>Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishugulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uzima wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho."
<scripture passage="John 6:28" parsed="|John|6|28|0|0" osisRef="Bible:John.6.28" />
<sup>28</sup>Wao wakamwuliza, "Tufanye nini ili tuweze kuzitenda kazi za Mungu?"
<scripture passage="John 6:29" parsed="|John|6|29|0|0" osisRef="Bible:John.6.29" />
<sup>29</sup>Yesu akawajibu, "Hii ndiyo kazi anayotaka Mungu muifanye: kumwamini yule aliyemtuma."
<scripture passage="John 6:30" parsed="|John|6|30|0|0" osisRef="Bible:John.6.30" />
<sup>30</sup>Hapo wakamwambia, "Utafanya ishara gani ili tuione tupate kukuamini? Utafanya kitu gani?
<scripture passage="John 6:31" parsed="|John|6|31|0|0" osisRef="Bible:John.6.31" />
<sup>31</sup>Wazee wetu walikula mana kule jangwani, kama yasemavyo Maandiko: `Aliwalisha mkate kutoka mbinguni."`
<scripture passage="John 6:32" parsed="|John|6|32|0|0" osisRef="Bible:John.6.32" />
<sup>32</sup>Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, Mose hakuwapeni mkate kutoka mbinguni; Baba yangu ndiye awapaye ninyi mkate halisi kutoka mbinguni.
<scripture passage="John 6:33" parsed="|John|6|33|0|0" osisRef="Bible:John.6.33" />
<sup>33</sup>Maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uzima."
<scripture passage="John 6:34" parsed="|John|6|34|0|0" osisRef="Bible:John.6.34" />
<sup>34</sup>Basi, wakamwambia, "Mheshimiwa, tupe daima mkate huo."
<scripture passage="John 6:35" parsed="|John|6|35|0|0" osisRef="Bible:John.6.35" />
<sup>35</sup>Yesu akawaambia, "Mimi ndimi mkate wa uzima. Anayekuja kwangu hataona njaa; anayeniamini hataona kiu kamwe.
<scripture passage="John 6:36" parsed="|John|6|36|0|0" osisRef="Bible:John.6.36" />
<sup>36</sup>Lakini niliwaambieni kwamba ingawa mmeniona hamniamini.
<scripture passage="John 6:37" parsed="|John|6|37|0|0" osisRef="Bible:John.6.37" />
<sup>37</sup>Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
<scripture passage="John 6:38" parsed="|John|6|38|0|0" osisRef="Bible:John.6.38" />
<sup>38</sup>kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule aliyenituma.
<scripture passage="John 6:39" parsed="|John|6|39|0|0" osisRef="Bible:John.6.39" />
<sup>39</sup>Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho.
<scripture passage="John 6:40" parsed="|John|6|40|0|0" osisRef="Bible:John.6.40" />
<sup>40</sup>Maana anachotaka Baba yangu ndicho hiki: kila amwonaye Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele; nami nitamfufua Siku ya mwisho."
<scripture passage="John 6:41" parsed="|John|6|41|0|0" osisRef="Bible:John.6.41" />
<sup>41</sup>Basi, Wayahudi wakaanza kunung`unika kwa kuwa alisema: "Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni."
<scripture passage="John 6:42" parsed="|John|6|42|0|0" osisRef="Bible:John.6.42" />
<sup>42</sup>Wakasema, "Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunawajua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?"
<scripture passage="John 6:43" parsed="|John|6|43|0|0" osisRef="Bible:John.6.43" />
<sup>43</sup>Yesu akawaambia, "Acheni kunung`unika ninyi kwa ninyi.
<scripture passage="John 6:44" parsed="|John|6|44|0|0" osisRef="Bible:John.6.44" />
<sup>44</sup>Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtu huyo Siku ya mwisho.
<scripture passage="John 6:45" parsed="|John|6|45|0|0" osisRef="Bible:John.6.45" />
<sup>45</sup>Manabii wameandika: `Watu wote watafundishwa na Mungu.` Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu.
<scripture passage="John 6:46" parsed="|John|6|46|0|0" osisRef="Bible:John.6.46" />
<sup>46</sup>Hii haina maana kwamba yupo mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.
<scripture passage="John 6:47" parsed="|John|6|47|0|0" osisRef="Bible:John.6.47" />
<sup>47</sup>Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uzima wa milele.
<scripture passage="John 6:48" parsed="|John|6|48|0|0" osisRef="Bible:John.6.48" />
<sup>48</sup>Mimi ni mkate wa uzima.
<scripture passage="John 6:49" parsed="|John|6|49|0|0" osisRef="Bible:John.6.49" />
<sup>49</sup>Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa.
<scripture passage="John 6:50" parsed="|John|6|50|0|0" osisRef="Bible:John.6.50" />
<sup>50</sup>Huu ndio mkate kutoka mbinguni; mkate ambao anayekula hatakufa.
<scripture passage="John 6:51" parsed="|John|6|51|0|0" osisRef="Bible:John.6.51" />
<sup>51</sup>Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu."
<scripture passage="John 6:52" parsed="|John|6|52|0|0" osisRef="Bible:John.6.52" />
<sup>52</sup>Ndipo Wayahudi wakaanza kubishana kati yao:
<scripture passage="John 6:53" parsed="|John|6|53|0|0" osisRef="Bible:John.6.53" />
<sup>53</sup>Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, msipokula mwili wa Mwana wa Mtu na kunywa damu yake, hamtakuwa na uzima ndani yenu.
<scripture passage="John 6:54" parsed="|John|6|54|0|0" osisRef="Bible:John.6.54" />
<sup>54</sup>Anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele nami nitamfufua siku ya mwisho.
<scripture passage="John 6:55" parsed="|John|6|55|0|0" osisRef="Bible:John.6.55" />
<sup>55</sup>Maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
<scripture passage="John 6:56" parsed="|John|6|56|0|0" osisRef="Bible:John.6.56" />
<sup>56</sup>Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake.
<scripture passage="John 6:57" parsed="|John|6|57|0|0" osisRef="Bible:John.6.57" />
<sup>57</sup>Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.
<scripture passage="John 6:58" parsed="|John|6|58|0|0" osisRef="Bible:John.6.58" />
<sup>58</sup>Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zetu, wakafa. Aulaye mkate huu ataishi milele."
<scripture passage="John 6:59" parsed="|John|6|59|0|0" osisRef="Bible:John.6.59" />
<sup>59</sup>Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu.
<scripture passage="John 6:60" parsed="|John|6|60|0|0" osisRef="Bible:John.6.60" />
<sup>60</sup>Basi, wengi wa wafuasi wake waliposikia hayo, wakasema, "Haya ni mambo magumu! Nani awezaye kuyasikiliza?"
<scripture passage="John 6:61" parsed="|John|6|61|0|0" osisRef="Bible:John.6.61" />
<sup>61</sup>Yesu alijua bila kuambiwa na mtu kwamba wanafunzi wake walikuwa wananung`unika juu ya jambo hilo, akawauliza, "Je, jambo hili linawafanya muwe na mashaka?
<scripture passage="John 6:62" parsed="|John|6|62|0|0" osisRef="Bible:John.6.62" />
<sup>62</sup>Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?
<scripture passage="John 6:63" parsed="|John|6|63|0|0" osisRef="Bible:John.6.63" />
<sup>63</sup>Roho ndiye atiaye uzima; binadamu peke yake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho, ni uzima.
<scripture passage="John 6:64" parsed="|John|6|64|0|0" osisRef="Bible:John.6.64" />
<sup>64</sup>Hata hivyo, wako baadhi yenu wasioamini." (Yesu alisema hivyo kwani alijua tangu mwanzo ni kina nani wasioamini, na pia ni nani atakayemsaliti.)
<scripture passage="John 6:65" parsed="|John|6|65|0|0" osisRef="Bible:John.6.65" />
<sup>65</sup>Kisha akasema, "Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakuna awezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba yangu."
<scripture passage="John 6:66" parsed="|John|6|66|0|0" osisRef="Bible:John.6.66" />
<sup>66</sup>Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma wasiandamane naye tena.
<scripture passage="John 6:67" parsed="|John|6|67|0|0" osisRef="Bible:John.6.67" />
<sup>67</sup>Basi, Yesu akawauliza wale kumi na wawili, "Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?"
<scripture passage="John 6:68" parsed="|John|6|68|0|0" osisRef="Bible:John.6.68" />
<sup>68</sup>Simoni Petro akamjibu, "Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele.
<scripture passage="John 6:69" parsed="|John|6|69|0|0" osisRef="Bible:John.6.69" />
<sup>69</sup>Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu."
<scripture passage="John 6:70" parsed="|John|6|70|0|0" osisRef="Bible:John.6.70" />
<sup>70</sup>Yesu akawaambia, "Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!"
<scripture passage="John 6:71" parsed="|John|6|71|0|0" osisRef="Bible:John.6.71" />
<sup>71</sup>Yesu alisema hayo juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyu alikuwa ndiye atakayemsaliti, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili.
</p>
</div3>

<div3 title="John 7" progress="37.04%" prev="John.6" next="John.8" id="John.7">
<h3 id="John.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="John.7-p1">
<scripture passage="John 7:1" parsed="|John|7|1|0|0" osisRef="Bible:John.7.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumwua.
<scripture passage="John 7:2" parsed="|John|7|2|0|0" osisRef="Bible:John.7.2" />
<sup>2</sup>Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
<scripture passage="John 7:3" parsed="|John|7|3|0|0" osisRef="Bible:John.7.3" />
<sup>3</sup>Basi ndugu zake wakamwambia, "Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.
<scripture passage="John 7:4" parsed="|John|7|4|0|0" osisRef="Bible:John.7.4" />
<sup>4</sup>Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kujulikana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya, basi, jidhihirishe kwa ulimwengu."
<scripture passage="John 7:5" parsed="|John|7|5|0|0" osisRef="Bible:John.7.5" />
<sup>5</sup>Hata ndugu zake hawakumwamini!)
<scripture passage="John 7:6" parsed="|John|7|6|0|0" osisRef="Bible:John.7.6" />
<sup>6</sup>Basi, Yesu akawaambia, "Wakati wangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa.
<scripture passage="John 7:7" parsed="|John|7|7|0|0" osisRef="Bible:John.7.7" />
<sup>7</sup>Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazi kwamba matendo yake ni maovu.
<scripture passage="John 7:8" parsed="|John|7|8|0|0" osisRef="Bible:John.7.8" />
<sup>8</sup>Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika."
<scripture passage="John 7:9" parsed="|John|7|9|0|0" osisRef="Bible:John.7.9" />
<sup>9</sup>Alisema hayo kisha akabaki huko Galilaya.
<scripture passage="John 7:10" parsed="|John|7|10|0|0" osisRef="Bible:John.7.10" />
<sup>10</sup>Baada ya ndugu zake kwenda kwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuenda kwa hadhara bali kwa siri.
<scripture passage="John 7:11" parsed="|John|7|11|0|0" osisRef="Bible:John.7.11" />
<sup>11</sup>Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: "Yuko wapi?"
<scripture passage="John 7:12" parsed="|John|7|12|0|0" osisRef="Bible:John.7.12" />
<sup>12</sup>Kulikuwa na minong`ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, "Ni mtu mwema." Wengine walisema, "La! Anawapotosha watu."
<scripture passage="John 7:13" parsed="|John|7|13|0|0" osisRef="Bible:John.7.13" />
<sup>13</sup>Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema, habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi.
<scripture passage="John 7:14" parsed="|John|7|14|0|0" osisRef="Bible:John.7.14" />
<sup>14</sup>Sikukuu hiyo ilipofikia katikati, Yesu naye alikwenda Hekaluni, akaanza kufundisha.
<scripture passage="John 7:15" parsed="|John|7|15|0|0" osisRef="Bible:John.7.15" />
<sup>15</sup>Basi, Wayahudi wakashangaa na kusema "Mtu huyu amepataje elimu naye hakusoma shuleni?"
<scripture passage="John 7:16" parsed="|John|7|16|0|0" osisRef="Bible:John.7.16" />
<sup>16</sup>Hapo Yesu akawajibu, "Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
<scripture passage="John 7:17" parsed="|John|7|17|0|0" osisRef="Bible:John.7.17" />
<sup>17</sup>Mtu anayependa kufanya yale anayotaka Mungu, atajua kama mafundisho yangu yametoka kwa Mungu, au mimi najisemea tu mwenyewe.
<scripture passage="John 7:18" parsed="|John|7|18|0|0" osisRef="Bible:John.7.18" />
<sup>18</sup>Yeye anayejisemea tu mwenyewe anatafuta sifa yake mwenyewe; lakini anayetafuta sifa ya yule aliyemtuma, huyo ni mwaminifu, na ndani yake hamna uovu wowote.
<scripture passage="John 7:19" parsed="|John|7|19|0|0" osisRef="Bible:John.7.19" />
<sup>19</sup>Je, Mose hakuwapeni Sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika Sheria. Kwa nini mnataka kuniua?"
<scripture passage="John 7:20" parsed="|John|7|20|0|0" osisRef="Bible:John.7.20" />
<sup>20</sup>Hapo watu wakamjibu, "Una wazimu wewe! Nani anataka kukuua?"
<scripture passage="John 7:21" parsed="|John|7|21|0|0" osisRef="Bible:John.7.21" />
<sup>21</sup>Yesu akawajibu, "Kuna jambo moja nililofanya, nanyi mnalistaajabia.
<scripture passage="John 7:22" parsed="|John|7|22|0|0" osisRef="Bible:John.7.22" />
<sup>22</sup>Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato.
<scripture passage="John 7:23" parsed="|John|7|23|0|0" osisRef="Bible:John.7.23" />
<sup>23</sup>Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi Sheria ya Mose isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?
<scripture passage="John 7:24" parsed="|John|7|24|0|0" osisRef="Bible:John.7.24" />
<sup>24</sup>Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki."
<scripture passage="John 7:25" parsed="|John|7|25|0|0" osisRef="Bible:John.7.25" />
<sup>25</sup>Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, "Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
<scripture passage="John 7:26" parsed="|John|7|26|0|0" osisRef="Bible:John.7.26" />
<sup>26</sup>Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?
<scripture passage="John 7:27" parsed="|John|7|27|0|0" osisRef="Bible:John.7.27" />
<sup>27</sup>Kristo atakapokuja hakuna mtu atakayejua mahali alikotoka, lakini sisi tunajua alikotoka mtu huyu!"
<scripture passage="John 7:28" parsed="|John|7|28|0|0" osisRef="Bible:John.7.28" />
<sup>28</sup>Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, "Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui.
<scripture passage="John 7:29" parsed="|John|7|29|0|0" osisRef="Bible:John.7.29" />
<sup>29</sup>Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma."
<scripture passage="John 7:30" parsed="|John|7|30|0|0" osisRef="Bible:John.7.30" />
<sup>30</sup>Basi, watu wakataka kumtia nguvuni, lakini hakuna mtu aliyethubutu kumkamata kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
<scripture passage="John 7:31" parsed="|John|7|31|0|0" osisRef="Bible:John.7.31" />
<sup>31</sup>Wengi katika ule umati wa watu walimwamini, wakasema, "Je, Kristo akija atafanya ishara kubwa zaidi kuliko alizozifanya huyu?"
<scripture passage="John 7:32" parsed="|John|7|32|0|0" osisRef="Bible:John.7.32" />
<sup>32</sup>Mafarisayo waliwasikia watu wakinong`ona maneno hayo juu ya Yesu. Basi, wao pamoja na makuhani wakuu wakawatuma walinzi wamtie nguvuni.
<scripture passage="John 7:33" parsed="|John|7|33|0|0" osisRef="Bible:John.7.33" />
<sup>33</sup>Yesu akasema, "Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.
<scripture passage="John 7:34" parsed="|John|7|34|0|0" osisRef="Bible:John.7.34" />
<sup>34</sup>Mtanitafuta lakini hamtaniona, maana pale nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika."
<scripture passage="John 7:35" parsed="|John|7|35|0|0" osisRef="Bible:John.7.35" />
<sup>35</sup>Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, "Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?
<scripture passage="John 7:36" parsed="|John|7|36|0|0" osisRef="Bible:John.7.36" />
<sup>36</sup>Ana maana gani anaposema: `Mtanitafuta lakini hamtanipata, na mahali nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika?"`
<scripture passage="John 7:37" parsed="|John|7|37|0|0" osisRef="Bible:John.7.37" />
<sup>37</sup>Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalum. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, "Aliye na kiu na aje kwangu anywe.
<scripture passage="John 7:38" parsed="|John|7|38|0|0" osisRef="Bible:John.7.38" />
<sup>38</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: `Anayeniamini mimi, mito ya maji yenye uzima itatiririka kutoka moyoni mwake!"`
<scripture passage="John 7:39" parsed="|John|7|39|0|0" osisRef="Bible:John.7.39" />
<sup>39</sup>Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.)
<scripture passage="John 7:40" parsed="|John|7|40|0|0" osisRef="Bible:John.7.40" />
<sup>40</sup>Baadhi ya watu katika ule umati walisikia maneno hayo, wakasema, "Kweli mtu huyu ndiye yule nabii!"
<scripture passage="John 7:41" parsed="|John|7|41|0|0" osisRef="Bible:John.7.41" />
<sup>41</sup>Wengine wakasema, "Huyu ndiye Kristo!" Lakini wengine walisema, "Je, yawezekana Kristo akatoka Galilaya?
<scripture passage="John 7:42" parsed="|John|7|42|0|0" osisRef="Bible:John.7.42" />
<sup>42</sup>Maandiko Matakatifu yasemaje? Yanasema: `Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi, na atazaliwa Bethlehemu, mji wa Daudi!"`
<scripture passage="John 7:43" parsed="|John|7|43|0|0" osisRef="Bible:John.7.43" />
<sup>43</sup>Basi, kukatokea mafarakano juu yake katika ule umati wa watu.
<scripture passage="John 7:44" parsed="|John|7|44|0|0" osisRef="Bible:John.7.44" />
<sup>44</sup>Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata.
<scripture passage="John 7:45" parsed="|John|7|45|0|0" osisRef="Bible:John.7.45" />
<sup>45</sup>Kisha wale walinzi wakarudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo; nao wakawauliza, "Kwa nini hamkumleta?"
<scripture passage="John 7:46" parsed="|John|7|46|0|0" osisRef="Bible:John.7.46" />
<sup>46</sup>Walinzi wakawajibu, "Hakuna mtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyo mtu huyu!"
<scripture passage="John 7:47" parsed="|John|7|47|0|0" osisRef="Bible:John.7.47" />
<sup>47</sup>Mafarisayo wakawauliza, "Je, nanyi pia mmedanganyika?
<scripture passage="John 7:48" parsed="|John|7|48|0|0" osisRef="Bible:John.7.48" />
<sup>48</sup>Je, mmekwisha mwona hata mmoja wa viongozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini?
<scripture passage="John 7:49" parsed="|John|7|49|0|0" osisRef="Bible:John.7.49" />
<sup>49</sup>Lakini umati huu haujui Sheria ya Mose; umelaaniwa!"
<scripture passage="John 7:50" parsed="|John|7|50|0|0" osisRef="Bible:John.7.50" />
<sup>50</sup>Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia,
<scripture passage="John 7:51" parsed="|John|7|51|0|0" osisRef="Bible:John.7.51" />
<sup>51</sup>"Je, Sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?"
<scripture passage="John 7:52" parsed="|John|7|52|0|0" osisRef="Bible:John.7.52" />
<sup>52</sup>Nao wakamjibu, "Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachunguze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilaya hakutoki kamwe nabii!" [[[
<scripture passage="John 7:53" parsed="|John|7|53|0|0" osisRef="Bible:John.7.53" />
<sup>53</sup>Basi, wote wakaondoka, kila mtu akaenda zake;
</p>
</div3>

<div3 title="John 8" progress="37.62%" prev="John.7" next="John.9" id="John.8">
<h3 id="John.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="John.8-p1">
<scripture passage="John 8:1" parsed="|John|8|1|0|0" osisRef="Bible:John.8.1" />
<sup>1</sup>lakini Yesu akaenda kwenye mlima wa Mizeituni.
<scripture passage="John 8:2" parsed="|John|8|2|0|0" osisRef="Bible:John.8.2" />
<sup>2</sup>Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena Hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
<scripture passage="John 8:3" parsed="|John|8|3|0|0" osisRef="Bible:John.8.3" />
<sup>3</sup>Basi, walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamletea mwanamke mmoja aliyefumaniwa katika uzinzi. Wakamsimamisha katikati yao.
<scripture passage="John 8:4" parsed="|John|8|4|0|0" osisRef="Bible:John.8.4" />
<sup>4</sup>Kisha wakamwuliza Yesu, "Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi.
<scripture passage="John 8:5" parsed="|John|8|5|0|0" osisRef="Bible:John.8.5" />
<sup>5</sup>Katika Sheria yetu Mose alituamuru mwanamke kama huyu apigwe mawe. Basi, wewe wasemaje?"
<scripture passage="John 8:6" parsed="|John|8|6|0|0" osisRef="Bible:John.8.6" />
<sup>6</sup>Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
<scripture passage="John 8:7" parsed="|John|8|7|0|0" osisRef="Bible:John.8.7" />
<sup>7</sup>Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, "Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe."
<scripture passage="John 8:8" parsed="|John|8|8|0|0" osisRef="Bible:John.8.8" />
<sup>8</sup>Kisha akainama tena, akawa anaandika ardhini.
<scripture passage="John 8:9" parsed="|John|8|9|0|0" osisRef="Bible:John.8.9" />
<sup>9</sup>Waliposikia hivyo, wakaanza kutoweka mmojammoja, wakitanguliwa na wazee. Yesu akabaki peke yake, na yule mwanamke amesimama palepale.
<scripture passage="John 8:10" parsed="|John|8|10|0|0" osisRef="Bible:John.8.10" />
<sup>10</sup>Yesu alipoinuka akamwuliza huyo mwanamke, "Wako wapi wale watu? Je, hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?"
<scripture passage="John 8:11" parsed="|John|8|11|0|0" osisRef="Bible:John.8.11" />
<sup>11</sup>Huyo mwanamke akamjibu, "Mheshimiwa, hakuna hata mmoja!" Naye Yesu akamwambia, "Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; na tangu sasa usitende dhambi tena."]<i>fb</i> mahali pengine.
<scripture passage="John 8:12" parsed="|John|8|12|0|0" osisRef="Bible:John.8.12" />
<sup>12</sup>Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, "Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uzima."
<scripture passage="John 8:13" parsed="|John|8|13|0|0" osisRef="Bible:John.8.13" />
<sup>13</sup>Basi, Mafarisayo wakamwambia, "Wewe unajishuhudia mwenyewe; kwa hiyo ushahidi wako si halali."
<scripture passage="John 8:14" parsed="|John|8|14|0|0" osisRef="Bible:John.8.14" />
<sup>14</sup>Yesu akawajibu, "Hata kama ninajishuhudia mwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli kwa sababu mimi najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda.
<scripture passage="John 8:15" parsed="|John|8|15|0|0" osisRef="Bible:John.8.15" />
<sup>15</sup>Ninyi mnahukumu kwa fikira za kibinadamu, lakini mimi simhukumu mtu.
<scripture passage="John 8:16" parsed="|John|8|16|0|0" osisRef="Bible:John.8.16" />
<sup>16</sup>Hata nikihukumu, hukumu yangu ni ya haki kwa sababu mimi siko peke yangu; Baba aliyenituma yuko pamoja nami.
<scripture passage="John 8:17" parsed="|John|8|17|0|0" osisRef="Bible:John.8.17" />
<sup>17</sup>Imeandikwa katika Sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali.
<scripture passage="John 8:18" parsed="|John|8|18|0|0" osisRef="Bible:John.8.18" />
<sup>18</sup>Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma, ananishuhudia pia."
<scripture passage="John 8:19" parsed="|John|8|19|0|0" osisRef="Bible:John.8.19" />
<sup>19</sup>Hapo wakamwuliza, "Baba yako yuko wapi?" Yesu akawajibu "Ninyi hamnijui mimi wala hamumjui Baba. Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia."
<scripture passage="John 8:20" parsed="|John|8|20|0|0" osisRef="Bible:John.8.20" />
<sup>20</sup>Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
<scripture passage="John 8:21" parsed="|John|8|21|0|0" osisRef="Bible:John.8.21" />
<sup>21</sup>Yesu akawaambia tena, "Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi,ninyi hamwezi kufika."
<scripture passage="John 8:22" parsed="|John|8|22|0|0" osisRef="Bible:John.8.22" />
<sup>22</sup>Basi, viongozi wa Wayahudi wakasema, "Je, atajiua? Mbona anasema: `Niendako ninyi hamwezi kufika?"`
<scripture passage="John 8:23" parsed="|John|8|23|0|0" osisRef="Bible:John.8.23" />
<sup>23</sup>Yesu akawaambia, "Ninyi mmetoka papa hapa chini, mimi nimetoka juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.
<scripture passage="John 8:24" parsed="|John|8|24|0|0" osisRef="Bible:John.8.24" />
<sup>24</sup>Ndiyo maana niliwaambieni mtakufa katika dhambi zenu. Kama msipoamini kwamba `Mimi ndimi`, mtakufa katika dhambi zenu."
<scripture passage="John 8:25" parsed="|John|8|25|0|0" osisRef="Bible:John.8.25" />
<sup>25</sup>Nao wakamwuliza, "Wewe ni nani?" Yesu akawajibu, "Nimewaambieni tangu mwanzo!
<scripture passage="John 8:26" parsed="|John|8|26|0|0" osisRef="Bible:John.8.26" />
<sup>26</sup>Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake."
<scripture passage="John 8:27" parsed="|John|8|27|0|0" osisRef="Bible:John.8.27" />
<sup>27</sup>Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba.
<scripture passage="John 8:28" parsed="|John|8|28|0|0" osisRef="Bible:John.8.28" />
<sup>28</sup>Basi, Yesu akawaambia, "Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu hapo ndipo mtakapojua kwamba `Mimi ndimi`, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha.
<scripture passage="John 8:29" parsed="|John|8|29|0|0" osisRef="Bible:John.8.29" />
<sup>29</sup>Yule aliyenituma yuko pamoja nami; yeye hakuniacha peke yangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza."
<scripture passage="John 8:30" parsed="|John|8|30|0|0" osisRef="Bible:John.8.30" />
<sup>30</sup>Baada ya kusema hayo watu wengi walimwamini.
<scripture passage="John 8:31" parsed="|John|8|31|0|0" osisRef="Bible:John.8.31" />
<sup>31</sup>Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, "Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.
<scripture passage="John 8:32" parsed="|John|8|32|0|0" osisRef="Bible:John.8.32" />
<sup>32</sup>Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru."
<scripture passage="John 8:33" parsed="|John|8|33|0|0" osisRef="Bible:John.8.33" />
<sup>33</sup>Nao wakamjibu, "Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: `mtakuwa huru?"`
<scripture passage="John 8:34" parsed="|John|8|34|0|0" osisRef="Bible:John.8.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, kila mtu anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi.
<scripture passage="John 8:35" parsed="|John|8|35|0|0" osisRef="Bible:John.8.35" />
<sup>35</sup>Mtumwa hana makao ya kudumu nyumbani, lakini mwana anayo makao ya kudumu.
<scripture passage="John 8:36" parsed="|John|8|36|0|0" osisRef="Bible:John.8.36" />
<sup>36</sup>Kama mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli.
<scripture passage="John 8:37" parsed="|John|8|37|0|0" osisRef="Bible:John.8.37" />
<sup>37</sup>Najua kwamba ninyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamuyakubali mafundisho yangu.
<scripture passage="John 8:38" parsed="|John|8|38|0|0" osisRef="Bible:John.8.38" />
<sup>38</sup>Mimi nasema yale aliyonionyesha Baba, lakini ninyi mwafanya yale aliyowaambieni baba yenu."
<scripture passage="John 8:39" parsed="|John|8|39|0|0" osisRef="Bible:John.8.39" />
<sup>39</sup>Wao wakamjibu, "Baba yetu ni Abrahamu!" Yesu akawaambia, "Kama ninyi mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngefanya kama alivyofanya Abrahamu,
<scripture passage="John 8:40" parsed="|John|8|40|0|0" osisRef="Bible:John.8.40" />
<sup>40</sup>Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
<scripture passage="John 8:41" parsed="|John|8|41|0|0" osisRef="Bible:John.8.41" />
<sup>41</sup>Ninyi mnafanya mambo yaleyale aliyofanya babu yenu." Wao wakamwambia, "Sisi si watoto haramu! Tunaye baba mmoja tu, yaani Mungu."
<scripture passage="John 8:42" parsed="|John|8|42|0|0" osisRef="Bible:John.8.42" />
<sup>42</sup>Yesu akawaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.
<scripture passage="John 8:43" parsed="|John|8|43|0|0" osisRef="Bible:John.8.43" />
<sup>43</sup>Kwa nini hamwelewi hayo ninayosema? Ni kwa kuwa hamwezi kuusikiliza ujumbe wangu.
<scripture passage="John 8:44" parsed="|John|8|44|0|0" osisRef="Bible:John.8.44" />
<sup>44</sup>Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na hali yake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wa uongo.
<scripture passage="John 8:45" parsed="|John|8|45|0|0" osisRef="Bible:John.8.45" />
<sup>45</sup>Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana ninyi hamniamini.
<scripture passage="John 8:46" parsed="|John|8|46|0|0" osisRef="Bible:John.8.46" />
<sup>46</sup>Nani kati yenu awezaye kuthibitisha kuwa mimi nina dhambi? Ikiwa basi nasema ukweli, kwa nini hamniamini?
<scripture passage="John 8:47" parsed="|John|8|47|0|0" osisRef="Bible:John.8.47" />
<sup>47</sup>Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini ninyi hamsikilizi kwa sababu ninyi si (watu wa) Mungu."
<scripture passage="John 8:48" parsed="|John|8|48|0|0" osisRef="Bible:John.8.48" />
<sup>48</sup>Wayahudi wakamwambia, "Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena una pepo?"
<scripture passage="John 8:49" parsed="|John|8|49|0|0" osisRef="Bible:John.8.49" />
<sup>49</sup>Yesu akajibu, "Mimi sina pepo; mimi namheshimu Baba yangu, lakini ninyi hamniheshimu.
<scripture passage="John 8:50" parsed="|John|8|50|0|0" osisRef="Bible:John.8.50" />
<sup>50</sup>Mimi sijitafutii utukufu wangu mwenyewe; yuko mmoja mwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu.
<scripture passage="John 8:51" parsed="|John|8|51|0|0" osisRef="Bible:John.8.51" />
<sup>51</sup>Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele."
<scripture passage="John 8:52" parsed="|John|8|52|0|0" osisRef="Bible:John.8.52" />
<sup>52</sup>Basi, Wayahudi wakasema, "Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, `Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!`
<scripture passage="John 8:53" parsed="|John|8|53|0|0" osisRef="Bible:John.8.53" />
<sup>53</sup>Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?"
<scripture passage="John 8:54" parsed="|John|8|54|0|0" osisRef="Bible:John.8.54" />
<sup>54</sup>Yesu akawajibu, "Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiye anayenitukuza.
<scripture passage="John 8:55" parsed="|John|8|55|0|0" osisRef="Bible:John.8.55" />
<sup>55</sup>Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
<scripture passage="John 8:56" parsed="|John|8|56|0|0" osisRef="Bible:John.8.56" />
<sup>56</sup>Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi."
<scripture passage="John 8:57" parsed="|John|8|57|0|0" osisRef="Bible:John.8.57" />
<sup>57</sup>Basi, Wayahudi wakamwambia, "Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?"
<scripture passage="John 8:58" parsed="|John|8|58|0|0" osisRef="Bible:John.8.58" />
<sup>58</sup>Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko."
<scripture passage="John 8:59" parsed="|John|8|59|0|0" osisRef="Bible:John.8.59" />
<sup>59</sup>Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni.
</p>
</div3>

<div3 title="John 9" progress="38.30%" prev="John.8" next="John.10" id="John.9">
<h3 id="John.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="John.9-p1">
<scripture passage="John 9:1" parsed="|John|9|1|0|0" osisRef="Bible:John.9.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu mmoja, kipofu tangu kuzaliwa.
<scripture passage="John 9:2" parsed="|John|9|2|0|0" osisRef="Bible:John.9.2" />
<sup>2</sup>Basi, wanafunzi wakamwuliza, "Mwalimu! Ni nani aliyetenda dhambi: mtu huyu, ama wazazi wake, hata akazaliwa kipofu?"
<scripture passage="John 9:3" parsed="|John|9|3|0|0" osisRef="Bible:John.9.3" />
<sup>3</sup>Yesu akajibu, "Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake.
<scripture passage="John 9:4" parsed="|John|9|4|0|0" osisRef="Bible:John.9.4" />
<sup>4</sup>Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
<scripture passage="John 9:5" parsed="|John|9|5|0|0" osisRef="Bible:John.9.5" />
<sup>5</sup>Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu."
<scripture passage="John 9:6" parsed="|John|9|6|0|0" osisRef="Bible:John.9.6" />
<sup>6</sup>Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
<scripture passage="John 9:7" parsed="|John|9|7|0|0" osisRef="Bible:John.9.7" />
<sup>7</sup>akamwambia, "Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu." (maana ya jina hili ni "aliyetumwa"). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
<scripture passage="John 9:8" parsed="|John|9|8|0|0" osisRef="Bible:John.9.8" />
<sup>8</sup>Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, "Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?"
<scripture passage="John 9:9" parsed="|John|9|9|0|0" osisRef="Bible:John.9.9" />
<sup>9</sup>Baadhi yao wakasema, "Ndiye." Wengine wakasema, "La! Ila anafanana naye." Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, "Ni mimi!"
<scripture passage="John 9:10" parsed="|John|9|10|0|0" osisRef="Bible:John.9.10" />
<sup>10</sup>Basi, wakamwuliza, "Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?"
<scripture passage="John 9:11" parsed="|John|9|11|0|0" osisRef="Bible:John.9.11" />
<sup>11</sup>Naye akawajibu, "Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: `Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.` Basi, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona."
<scripture passage="John 9:12" parsed="|John|9|12|0|0" osisRef="Bible:John.9.12" />
<sup>12</sup>Wakamwuliza, "Yeye yuko wapi?" Naye akawajibu, "Mimi sijui!"
<scripture passage="John 9:13" parsed="|John|9|13|0|0" osisRef="Bible:John.9.13" />
<sup>13</sup>Kisha wakampeleka huyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo.
<scripture passage="John 9:14" parsed="|John|9|14|0|0" osisRef="Bible:John.9.14" />
<sup>14</sup>Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato.
<scripture passage="John 9:15" parsed="|John|9|15|0|0" osisRef="Bible:John.9.15" />
<sup>15</sup>Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtu huyo, "Umepataje kuona?" Naye akawaambia, "Alinipaka tope machoni, nami nikanawa na sasa naona."
<scripture passage="John 9:16" parsed="|John|9|16|0|0" osisRef="Bible:John.9.16" />
<sup>16</sup>Baadhi ya Mafarisayo wakasema, "Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato." Lakini wengine wakasema, "Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?" Kukawa na mafarakano kati yao.
<scripture passage="John 9:17" parsed="|John|9|17|0|0" osisRef="Bible:John.9.17" />
<sup>17</sup>Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, "Maadam yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?" Naye akawaambia, "Yeye ni nabii!"
<scripture passage="John 9:18" parsed="|John|9|18|0|0" osisRef="Bible:John.9.18" />
<sup>18</sup>Viongozi wa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwa kipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaita wazazi wake.
<scripture passage="John 9:19" parsed="|John|9|19|0|0" osisRef="Bible:John.9.19" />
<sup>19</sup>Basi, wakawauliza hao wazazi, "Je, huyu ndiye mtoto wenu ambaye ninyi mwasema alizaliwa kipofu? Sasa amepataje kuona?"
<scripture passage="John 9:20" parsed="|John|9|20|0|0" osisRef="Bible:John.9.20" />
<sup>20</sup>Wazazi wake wakajibu, "Tunajua kwamba huyu ni mtoto wetu, na kwamba alizaliwa kipofu.
<scripture passage="John 9:21" parsed="|John|9|21|0|0" osisRef="Bible:John.9.21" />
<sup>21</sup>Lakini amepataje kuona, hatujui; na wala hatumjui yule aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima, anaweza kujitetea mwenyewe."
<scripture passage="John 9:22" parsed="|John|9|22|0|0" osisRef="Bible:John.9.22" />
<sup>22</sup>Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
<scripture passage="John 9:23" parsed="|John|9|23|0|0" osisRef="Bible:John.9.23" />
<sup>23</sup>Ndiyo maana wazazi wake walisema: "Yeye ni mtu mzima, mwulizeni."
<scripture passage="John 9:24" parsed="|John|9|24|0|0" osisRef="Bible:John.9.24" />
<sup>24</sup>Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu, wakamwambia, "Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi."
<scripture passage="John 9:25" parsed="|John|9|25|0|0" osisRef="Bible:John.9.25" />
<sup>25</sup>Yeye akajibu, "Kama ni mwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu, na sasa naona."
<scripture passage="John 9:26" parsed="|John|9|26|0|0" osisRef="Bible:John.9.26" />
<sup>26</sup>Basi, wakamwuliza, "Alikufanyia nini? Alikufumbuaje macho yako?"
<scripture passage="John 9:27" parsed="|John|9|27|0|0" osisRef="Bible:John.9.27" />
<sup>27</sup>Huyo mtu akawajibu, "Nimekwisha waambieni, nanyi hamkusikiliza; kwa nini mwataka kusikia tena? Je, ninyi pia mnataka kuwa wafuasi wake?"
<scripture passage="John 9:28" parsed="|John|9|28|0|0" osisRef="Bible:John.9.28" />
<sup>28</sup>Lakini wao wakamtukana wakisema, "Wewe ni mfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose.
<scripture passage="John 9:29" parsed="|John|9|29|0|0" osisRef="Bible:John.9.29" />
<sup>29</sup>Sisi tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini mtu huyu hatujui ametoka wapi!"
<scripture passage="John 9:30" parsed="|John|9|30|0|0" osisRef="Bible:John.9.30" />
<sup>30</sup>Naye akawajibu, "Hili ni jambo la kushangaza! Ninyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!
<scripture passage="John 9:31" parsed="|John|9|31|0|0" osisRef="Bible:John.9.31" />
<sup>31</sup>Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.
<scripture passage="John 9:32" parsed="|John|9|32|0|0" osisRef="Bible:John.9.32" />
<sup>32</sup>Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
<scripture passage="John 9:33" parsed="|John|9|33|0|0" osisRef="Bible:John.9.33" />
<sup>33</sup>Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!"
<scripture passage="John 9:34" parsed="|John|9|34|0|0" osisRef="Bible:John.9.34" />
<sup>34</sup>Wao wakamjibu, "Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?" Basi, wakamfukuzia mbali.
<scripture passage="John 9:35" parsed="|John|9|35|0|0" osisRef="Bible:John.9.35" />
<sup>35</sup>Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, "Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?"
<scripture passage="John 9:36" parsed="|John|9|36|0|0" osisRef="Bible:John.9.36" />
<sup>36</sup>Huyo mtu akajibu, "Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini."
<scripture passage="John 9:37" parsed="|John|9|37|0|0" osisRef="Bible:John.9.37" />
<sup>37</sup>Yesu akamwambia, "Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa."
<scripture passage="John 9:38" parsed="|John|9|38|0|0" osisRef="Bible:John.9.38" />
<sup>38</sup>Basi, huyo mtu akasema, "Ninaamini Bwana!" Akamsujudia.
<scripture passage="John 9:39" parsed="|John|9|39|0|0" osisRef="Bible:John.9.39" />
<sup>39</sup>Yesu akasema, "Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu."
<scripture passage="John 9:40" parsed="|John|9|40|0|0" osisRef="Bible:John.9.40" />
<sup>40</sup>Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye walisikia maneno hayo, wakamwuliza, "Je, sisi pia ni vipofu?"
<scripture passage="John 9:41" parsed="|John|9|41|0|0" osisRef="Bible:John.9.41" />
<sup>41</sup>Yesu akawajibu, "Kama mngekuwa vipofu, hamngekuwa na hatia; lakini sasa ninyi mwasema: `Sisi tunaona`, na hiyo yaonyesha kwamba mna hatia bado.
</p>
</div3>

<div3 title="John 10" progress="38.77%" prev="John.9" next="John.11" id="John.10">
<h3 id="John.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="John.10-p1">
<scripture passage="John 10:1" parsed="|John|10|1|0|0" osisRef="Bible:John.10.1" />
<sup>1</sup>Yesu alisema "Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang`anyi.
<scripture passage="John 10:2" parsed="|John|10|2|0|0" osisRef="Bible:John.10.2" />
<sup>2</sup>Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.
<scripture passage="John 10:3" parsed="|John|10|3|0|0" osisRef="Bible:John.10.3" />
<sup>3</sup>Mngoja mlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake na kuwaongoza nje.
<scripture passage="John 10:4" parsed="|John|10|4|0|0" osisRef="Bible:John.10.4" />
<sup>4</sup>Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
<scripture passage="John 10:5" parsed="|John|10|5|0|0" osisRef="Bible:John.10.5" />
<sup>5</sup>Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake."
<scripture passage="John 10:6" parsed="|John|10|6|0|0" osisRef="Bible:John.10.6" />
<sup>6</sup>Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
<scripture passage="John 10:7" parsed="|John|10|7|0|0" osisRef="Bible:John.10.7" />
<sup>7</sup>Basi, akasema tena, "Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.
<scripture passage="John 10:8" parsed="|John|10|8|0|0" osisRef="Bible:John.10.8" />
<sup>8</sup>Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang`anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.
<scripture passage="John 10:9" parsed="|John|10|9|0|0" osisRef="Bible:John.10.9" />
<sup>9</sup>Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.
<scripture passage="John 10:10" parsed="|John|10|10|0|0" osisRef="Bible:John.10.10" />
<sup>10</sup>Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima--uzima kamili.
<scripture passage="John 10:11" parsed="|John|10|11|0|0" osisRef="Bible:John.10.11" />
<sup>11</sup>"Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
<scripture passage="John 10:12" parsed="|John|10|12|0|0" osisRef="Bible:John.10.12" />
<sup>12</sup>Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
<scripture passage="John 10:13" parsed="|John|10|13|0|0" osisRef="Bible:John.10.13" />
<sup>13</sup>Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.
<scripture passage="John 10:14" parsed="|John|10|14|0|0" osisRef="Bible:John.10.14" />
<sup>14</sup>Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
<scripture passage="John 10:15" parsed="|John|10|15|0|0" osisRef="Bible:John.10.15" />
<sup>15</sup>kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
<scripture passage="John 10:16" parsed="|John|10|16|0|0" osisRef="Bible:John.10.16" />
<sup>16</sup>Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
<scripture passage="John 10:17" parsed="|John|10|17|0|0" osisRef="Bible:John.10.17" />
<sup>17</sup>"Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.
<scripture passage="John 10:18" parsed="|John|10|18|0|0" osisRef="Bible:John.10.18" />
<sup>18</sup>Hakuna mtu anayeninyang`anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye."
<scripture passage="John 10:19" parsed="|John|10|19|0|0" osisRef="Bible:John.10.19" />
<sup>19</sup>Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
<scripture passage="John 10:20" parsed="|John|10|20|0|0" osisRef="Bible:John.10.20" />
<sup>20</sup>Wengi wao wakasema, "Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?"
<scripture passage="John 10:21" parsed="|John|10|21|0|0" osisRef="Bible:John.10.21" />
<sup>21</sup>Wengine wakasema, "Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?"
<scripture passage="John 10:22" parsed="|John|10|22|0|0" osisRef="Bible:John.10.22" />
<sup>22</sup>Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.
<scripture passage="John 10:23" parsed="|John|10|23|0|0" osisRef="Bible:John.10.23" />
<sup>23</sup>Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.
<scripture passage="John 10:24" parsed="|John|10|24|0|0" osisRef="Bible:John.10.24" />
<sup>24</sup>Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, "Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi."
<scripture passage="John 10:25" parsed="|John|10|25|0|0" osisRef="Bible:John.10.25" />
<sup>25</sup>Yesu akawajibu, "Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.
<scripture passage="John 10:26" parsed="|John|10|26|0|0" osisRef="Bible:John.10.26" />
<sup>26</sup>Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
<scripture passage="John 10:27" parsed="|John|10|27|0|0" osisRef="Bible:John.10.27" />
<sup>27</sup>Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.
<scripture passage="John 10:28" parsed="|John|10|28|0|0" osisRef="Bible:John.10.28" />
<sup>28</sup>Mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.
<scripture passage="John 10:29" parsed="|John|10|29|0|0" osisRef="Bible:John.10.29" />
<sup>29</sup>Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wale hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.
<scripture passage="John 10:30" parsed="|John|10|30|0|0" osisRef="Bible:John.10.30" />
<sup>30</sup>Mimi na Baba, tu mmoja."
<scripture passage="John 10:31" parsed="|John|10|31|0|0" osisRef="Bible:John.10.31" />
<sup>31</sup>Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie.
<scripture passage="John 10:32" parsed="|John|10|32|0|0" osisRef="Bible:John.10.32" />
<sup>32</sup>Yesu akawaambia, "Nimewaonyesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?"
<scripture passage="John 10:33" parsed="|John|10|33|0|0" osisRef="Bible:John.10.33" />
<sup>33</sup>Wayahudi wakamjibu, "Hatukupigi mawe kwa ajili ya tendo jema, ila kwa sababu ya kukufuru! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu."
<scripture passage="John 10:34" parsed="|John|10|34|0|0" osisRef="Bible:John.10.34" />
<sup>34</sup>Yesu akawajibu, "Je, haikuandikwa katika Sheria yenu: `Mimi nimesema, ninyi ni miungu?`
<scripture passage="John 10:35" parsed="|John|10|35|0|0" osisRef="Bible:John.10.35" />
<sup>35</sup>Mungu aliwaita miungu wale waliopewa neno lake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima.
<scripture passage="John 10:36" parsed="|John|10|36|0|0" osisRef="Bible:John.10.36" />
<sup>36</sup>Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: `Unakufuru`, eti kwa sababu nilisema: `Mimi ni Mwana wa Mungu?`
<scripture passage="John 10:37" parsed="|John|10|37|0|0" osisRef="Bible:John.10.37" />
<sup>37</sup>Kama sifanyi kazi za Baba yangu msiniamini.
<scripture passage="John 10:38" parsed="|John|10|38|0|0" osisRef="Bible:John.10.38" />
<sup>38</sup>Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake."
<scripture passage="John 10:39" parsed="|John|10|39|0|0" osisRef="Bible:John.10.39" />
<sup>39</sup>Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao.
<scripture passage="John 10:40" parsed="|John|10|40|0|0" osisRef="Bible:John.10.40" />
<sup>40</sup>Yesu akaenda tena ng`ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
<scripture passage="John 10:41" parsed="|John|10|41|0|0" osisRef="Bible:John.10.41" />
<sup>41</sup>Watu wengi walimwendea wakasema, "Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa."
<scripture passage="John 10:42" parsed="|John|10|42|0|0" osisRef="Bible:John.10.42" />
<sup>42</sup>Watu wengi mahali hapo wakamwamini.
</p>
</div3>

<div3 title="John 11" progress="39.20%" prev="John.10" next="John.12" id="John.11">
<h3 id="John.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="John.11-p1">
<scripture passage="John 11:1" parsed="|John|11|1|0|0" osisRef="Bible:John.11.1" />
<sup>1</sup>Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.
<scripture passage="John 11:2" parsed="|John|11|2|0|0" osisRef="Bible:John.11.2" />
<sup>2</sup>Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa.)
<scripture passage="John 11:3" parsed="|John|11|3|0|0" osisRef="Bible:John.11.3" />
<sup>3</sup>Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: "Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!"
<scripture passage="John 11:4" parsed="|John|11|4|0|0" osisRef="Bible:John.11.4" />
<sup>4</sup>Yesu aliposikia hivyo akasema, "Ugonjwa huo hautaleta kifo, ila ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu; ameugua ili kwa njia hiyo Mwana wa Mungu atukuzwe."
<scripture passage="John 11:5" parsed="|John|11|5|0|0" osisRef="Bible:John.11.5" />
<sup>5</sup>Yesu aliwapenda Martha, dada yake na Lazaro.
<scripture passage="John 11:6" parsed="|John|11|6|0|0" osisRef="Bible:John.11.6" />
<sup>6</sup>Alipopata habari kwamba Lazaro ni mgonjwa, Yesu aliendelea kukaa mahali hapo alipokuwa kwa siku mbili zaidi.
<scripture passage="John 11:7" parsed="|John|11|7|0|0" osisRef="Bible:John.11.7" />
<sup>7</sup>Kisha akawaambia wanafunzi wake, "Twendeni tena Yudea!"
<scripture passage="John 11:8" parsed="|John|11|8|0|0" osisRef="Bible:John.11.8" />
<sup>8</sup>Wanafunzi wakamwambia, "Mwalimu! Muda mfupi tu umepita tangu Wayahudi walipotaka kukuua kwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?"
<scripture passage="John 11:9" parsed="|John|11|9|0|0" osisRef="Bible:John.11.9" />
<sup>9</sup>Yesu akajibu, "Je, saa za mchana si kumi na mbili? Basi, mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa kuwa anauona mwanga wa ulimwengu huu.
<scripture passage="John 11:10" parsed="|John|11|10|0|0" osisRef="Bible:John.11.10" />
<sup>10</sup>Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake."
<scripture passage="John 11:11" parsed="|John|11|11|0|0" osisRef="Bible:John.11.11" />
<sup>11</sup>Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini mimi nitakwenda kumwamsha."
<scripture passage="John 11:12" parsed="|John|11|12|0|0" osisRef="Bible:John.11.12" />
<sup>12</sup>Wanafunzi wake wakamwambia, "Bwana, ikiwa amelala, basi atapona."
<scripture passage="John 11:13" parsed="|John|11|13|0|0" osisRef="Bible:John.11.13" />
<sup>13</sup>Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.
<scripture passage="John 11:14" parsed="|John|11|14|0|0" osisRef="Bible:John.11.14" />
<sup>14</sup>Basi, Yesu akawaambia waziwazi, "Lazaro amekufa;
<scripture passage="John 11:15" parsed="|John|11|15|0|0" osisRef="Bible:John.11.15" />
<sup>15</sup>Lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake."
<scripture passage="John 11:16" parsed="|John|11|16|0|0" osisRef="Bible:John.11.16" />
<sup>16</sup>Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, "Twendeni nasi tukafe pamoja naye!"
<scripture passage="John 11:17" parsed="|John|11|17|0|0" osisRef="Bible:John.11.17" />
<sup>17</sup>Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.
<scripture passage="John 11:18" parsed="|John|11|18|0|0" osisRef="Bible:John.11.18" />
<sup>18</sup>Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu umbali upatao kilomita tatu.
<scripture passage="John 11:19" parsed="|John|11|19|0|0" osisRef="Bible:John.11.19" />
<sup>19</sup>Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.
<scripture passage="John 11:20" parsed="|John|11|20|0|0" osisRef="Bible:John.11.20" />
<sup>20</sup>Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.
<scripture passage="John 11:21" parsed="|John|11|21|0|0" osisRef="Bible:John.11.21" />
<sup>21</sup>Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!
<scripture passage="John 11:22" parsed="|John|11|22|0|0" osisRef="Bible:John.11.22" />
<sup>22</sup>Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."
<scripture passage="John 11:23" parsed="|John|11|23|0|0" osisRef="Bible:John.11.23" />
<sup>23</sup>Yesu akamwambia, "Kaka yako atafufuka."
<scripture passage="John 11:24" parsed="|John|11|24|0|0" osisRef="Bible:John.11.24" />
<sup>24</sup>Martha akamjibu, "Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho."
<scripture passage="John 11:25" parsed="|John|11|25|0|0" osisRef="Bible:John.11.25" />
<sup>25</sup>Yesu akamwambia, "Mimi ndimi ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi:
<scripture passage="John 11:26" parsed="|John|11|26|0|0" osisRef="Bible:John.11.26" />
<sup>26</sup>na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?"
<scripture passage="John 11:27" parsed="|John|11|27|0|0" osisRef="Bible:John.11.27" />
<sup>27</sup>Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana! Naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni."
<scripture passage="John 11:28" parsed="|John|11|28|0|0" osisRef="Bible:John.11.28" />
<sup>28</sup>Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwabia faraghani, "Mwalimu yuko hapa, anakuita."
<scripture passage="John 11:29" parsed="|John|11|29|0|0" osisRef="Bible:John.11.29" />
<sup>29</sup>Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.
<scripture passage="John 11:30" parsed="|John|11|30|0|0" osisRef="Bible:John.11.30" />
<sup>30</sup>Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahali palepale Martha alipomlaki.
<scripture passage="John 11:31" parsed="|John|11|31|0|0" osisRef="Bible:John.11.31" />
<sup>31</sup>Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
<scripture passage="John 11:32" parsed="|John|11|32|0|0" osisRef="Bible:John.11.32" />
<sup>32</sup>Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwabia, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!"
<scripture passage="John 11:33" parsed="|John|11|33|0|0" osisRef="Bible:John.11.33" />
<sup>33</sup>Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.
<scripture passage="John 11:34" parsed="|John|11|34|0|0" osisRef="Bible:John.11.34" />
<sup>34</sup>Kisha akawauliza, "Mlimweka wapi?" Wakamwambia, "Bwana, njoo uone."
<scripture passage="John 11:35" parsed="|John|11|35|0|0" osisRef="Bible:John.11.35" />
<sup>35</sup>Yesu akalia machozi.
<scripture passage="John 11:36" parsed="|John|11|36|0|0" osisRef="Bible:John.11.36" />
<sup>36</sup>Basi, Wayahudi wakasema, "Tazameni jinsi alivyompenda!"
<scripture passage="John 11:37" parsed="|John|11|37|0|0" osisRef="Bible:John.11.37" />
<sup>37</sup>Lakini baadhi yao wakasema, "Je, huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?"
<scripture passage="John 11:38" parsed="|John|11|38|0|0" osisRef="Bible:John.11.38" />
<sup>38</sup>Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.
<scripture passage="John 11:39" parsed="|John|11|39|0|0" osisRef="Bible:John.11.39" />
<sup>39</sup>Yesu akasema, "Ondoeni hilo jiwe!" Martha, dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, "Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!"
<scripture passage="John 11:40" parsed="|John|11|40|0|0" osisRef="Bible:John.11.40" />
<sup>40</sup>Yesu akamwambia, "Je, sikukwambia kwamba ukiamini utaona utukufu wa Mungu?"
<scripture passage="John 11:41" parsed="|John|11|41|0|0" osisRef="Bible:John.11.41" />
<sup>41</sup>Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema, "Nakushukuru Baba kwa kuwa wewe wanisikiliza.
<scripture passage="John 11:42" parsed="|John|11|42|0|0" osisRef="Bible:John.11.42" />
<sup>42</sup>Najua kwamba unanisikiliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watu hawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma."
<scripture passage="John 11:43" parsed="|John|11|43|0|0" osisRef="Bible:John.11.43" />
<sup>43</sup>Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: "Lazaro! Toka nje!"
<scripture passage="John 11:44" parsed="|John|11|44|0|0" osisRef="Bible:John.11.44" />
<sup>44</sup>Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, "Mfungueni, mkamwache aende zake."
<scripture passage="John 11:45" parsed="|John|11|45|0|0" osisRef="Bible:John.11.45" />
<sup>45</sup>Basi, Wayahudi wengi waliokuwa wamefika kwa Maria walipoona kitendo hicho alichokifanya Yesu wakamwamini.
<scripture passage="John 11:46" parsed="|John|11|46|0|0" osisRef="Bible:John.11.46" />
<sup>46</sup>Lakini baadhi yao walikwenda kwa Mafarisayo wakatoa taarifa ya jambo hilo alilofanya Yesu.
<scripture passage="John 11:47" parsed="|John|11|47|0|0" osisRef="Bible:John.11.47" />
<sup>47</sup>kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema, "Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.
<scripture passage="John 11:48" parsed="|John|11|48|0|0" osisRef="Bible:John.11.48" />
<sup>48</sup>Tukimwacha tu watu wote watamwamini, nao Waroma watakuja kuliharibu Hekalu letu na taifa letu!"
<scripture passage="John 11:49" parsed="|John|11|49|0|0" osisRef="Bible:John.11.49" />
<sup>49</sup>Hapo, mmoja wao aitwaye Kayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, "Ninyi hamjui kitu!
<scripture passage="John 11:50" parsed="|John|11|50|0|0" osisRef="Bible:John.11.50" />
<sup>50</sup>Je, hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zima liangamizwe?"
<scripture passage="John 11:51" parsed="|John|11|51|0|0" osisRef="Bible:John.11.51" />
<sup>51</sup>Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;
<scripture passage="John 11:52" parsed="|John|11|52|0|0" osisRef="Bible:John.11.52" />
<sup>52</sup>na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.
<scripture passage="John 11:53" parsed="|John|11|53|0|0" osisRef="Bible:John.11.53" />
<sup>53</sup>Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu.
<scripture passage="John 11:54" parsed="|John|11|54|0|0" osisRef="Bible:John.11.54" />
<sup>54</sup>Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
<scripture passage="John 11:55" parsed="|John|11|55|0|0" osisRef="Bible:John.11.55" />
<sup>55</sup>Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa karibu, na watu wengi walikwenda Yerusalemu ili wajitakase kabla ya sikukuu hiyo.
<scripture passage="John 11:56" parsed="|John|11|56|0|0" osisRef="Bible:John.11.56" />
<sup>56</sup>Basi, wakawa wanamtafuta Yesu; nao walipokusanyika pamoja Hekaluni wakaulizana, "Mwaonaje? Yaonekana kwamba haji kabisa kwenye sikukuu, au sivyo?"
<scripture passage="John 11:57" parsed="|John|11|57|0|0" osisRef="Bible:John.11.57" />
<sup>57</sup>Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba mtu akijua mahali aliko Yesu awaarifu kusudi wamtie nguvuni.
</p>
</div3>

<div3 title="John 12" progress="39.80%" prev="John.11" next="John.13" id="John.12">
<h3 id="John.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="John.12-p1">
<scripture passage="John 12:1" parsed="|John|12|1|0|0" osisRef="Bible:John.12.1" />
<sup>1</sup>Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua kutoka wafu.
<scripture passage="John 12:2" parsed="|John|12|2|0|0" osisRef="Bible:John.12.2" />
<sup>2</sup>Huko walimwandalia chakula cha jioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu.
<scripture passage="John 12:3" parsed="|John|12|3|0|0" osisRef="Bible:John.12.3" />
<sup>3</sup>Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi.
<scripture passage="John 12:4" parsed="|John|12|4|0|0" osisRef="Bible:John.12.4" />
<sup>4</sup>Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
<scripture passage="John 12:5" parsed="|John|12|5|0|0" osisRef="Bible:John.12.5" />
<sup>5</sup>"Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini?"
<scripture passage="John 12:6" parsed="|John|12|6|0|0" osisRef="Bible:John.12.6" />
<sup>6</sup>Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
<scripture passage="John 12:7" parsed="|John|12|7|0|0" osisRef="Bible:John.12.7" />
<sup>7</sup>Lakini Yesu akasema, "Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.
<scripture passage="John 12:8" parsed="|John|12|8|0|0" osisRef="Bible:John.12.8" />
<sup>8</sup>Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote." ic
<scripture passage="John 12:9" parsed="|John|12|9|0|0" osisRef="Bible:John.12.9" />
<sup>9</sup>Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu.
<scripture passage="John 12:10" parsed="|John|12|10|0|0" osisRef="Bible:John.12.10" />
<sup>10</sup>Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro,
<scripture passage="John 12:11" parsed="|John|12|11|0|0" osisRef="Bible:John.12.11" />
<sup>11</sup>Maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.
<scripture passage="John 12:12" parsed="|John|12|12|0|0" osisRef="Bible:John.12.12" />
<sup>12</sup>Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu.
<scripture passage="John 12:13" parsed="|John|12|13|0|0" osisRef="Bible:John.12.13" />
<sup>13</sup>Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti wakisema: "Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli."
<scripture passage="John 12:14" parsed="|John|12|14|0|0" osisRef="Bible:John.12.14" />
<sup>14</sup>Yesu akampata mwana punda mmoja akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko:
<scripture passage="John 12:15" parsed="|John|12|15|0|0" osisRef="Bible:John.12.15" />
<sup>15</sup>"Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalme wako anakuja, Amepanda mwana punda."
<scripture passage="John 12:16" parsed="|John|12|16|0|0" osisRef="Bible:John.12.16" />
<sup>16</sup>Wakati huo wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwamba hayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watu walikuwa wamemtendea hivyo.
<scripture passage="John 12:17" parsed="|John|12|17|0|0" osisRef="Bible:John.12.17" />
<sup>17</sup>Kundi la watu wale waliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.
<scripture passage="John 12:18" parsed="|John|12|18|0|0" osisRef="Bible:John.12.18" />
<sup>18</sup>Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wote walisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo.
<scripture passage="John 12:19" parsed="|John|12|19|0|0" osisRef="Bible:John.12.19" />
<sup>19</sup>Basi, Mafarisayo wakaambiana, "Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unamfuata."
<scripture passage="John 12:20" parsed="|John|12|20|0|0" osisRef="Bible:John.12.20" />
<sup>20</sup>Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
<scripture passage="John 12:21" parsed="|John|12|21|0|0" osisRef="Bible:John.12.21" />
<sup>21</sup>Hao walimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, "Mheshimiwa, tunataka kumwona Yesu."
<scripture passage="John 12:22" parsed="|John|12|22|0|0" osisRef="Bible:John.12.22" />
<sup>22</sup>Filipo akaenda akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu.
<scripture passage="John 12:23" parsed="|John|12|23|0|0" osisRef="Bible:John.12.23" />
<sup>23</sup>Yesu akawaambia, "Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika!
<scripture passage="John 12:24" parsed="|John|12|24|0|0" osisRef="Bible:John.12.24" />
<sup>24</sup>Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi.
<scripture passage="John 12:25" parsed="|John|12|25|0|0" osisRef="Bible:John.12.25" />
<sup>25</sup>Anayependa maisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uzima wa milele.
<scripture passage="John 12:26" parsed="|John|12|26|0|0" osisRef="Bible:John.12.26" />
<sup>26</sup>Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.
<scripture passage="John 12:27" parsed="|John|12|27|0|0" osisRef="Bible:John.12.27" />
<sup>27</sup>"Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: `Baba, usiruhusu saa hii inifikie`? Lakini ndiyo maana nimekuja--ili nipite katika saa hii.
<scripture passage="John 12:28" parsed="|John|12|28|0|0" osisRef="Bible:John.12.28" />
<sup>28</sup>Baba, ulitukuze jina lako." Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, "Nimelitukuza, na nitalitukuza tena."
<scripture passage="John 12:29" parsed="|John|12|29|0|0" osisRef="Bible:John.12.29" />
<sup>29</sup>Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikia sauti hiyo, na baadhi yao walisema, "Malaika ameongea naye!"
<scripture passage="John 12:30" parsed="|John|12|30|0|0" osisRef="Bible:John.12.30" />
<sup>30</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu.
<scripture passage="John 12:31" parsed="|John|12|31|0|0" osisRef="Bible:John.12.31" />
<sup>31</sup>Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa.
<scripture passage="John 12:32" parsed="|John|12|32|0|0" osisRef="Bible:John.12.32" />
<sup>32</sup>Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu."
<scripture passage="John 12:33" parsed="|John|12|33|0|0" osisRef="Bible:John.12.33" />
<sup>33</sup>Kwa kusema hivyo alionyesha atakufa kifo gani).
<scripture passage="John 12:34" parsed="|John|12|34|0|0" osisRef="Bible:John.12.34" />
<sup>34</sup>Basi, umati huo ukamjibu, "Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?"
<scripture passage="John 12:35" parsed="|John|12|35|0|0" osisRef="Bible:John.12.35" />
<sup>35</sup>Yesu akawaambia, "Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.
<scripture passage="John 12:36" parsed="|John|12|36|0|0" osisRef="Bible:John.12.36" />
<sup>36</sup>Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga." Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
<scripture passage="John 12:37" parsed="|John|12|37|0|0" osisRef="Bible:John.12.37" />
<sup>37</sup>Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.
<scripture passage="John 12:38" parsed="|John|12|38|0|0" osisRef="Bible:John.12.38" />
<sup>38</sup>Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: "Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?"
<scripture passage="John 12:39" parsed="|John|12|39|0|0" osisRef="Bible:John.12.39" />
<sup>39</sup>Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:
<scripture passage="John 12:40" parsed="|John|12|40|0|0" osisRef="Bible:John.12.40" />
<sup>40</sup>"Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya."
<scripture passage="John 12:41" parsed="|John|12|41|0|0" osisRef="Bible:John.12.41" />
<sup>41</sup>Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
<scripture passage="John 12:42" parsed="|John|12|42|0|0" osisRef="Bible:John.12.42" />
<sup>42</sup>Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.
<scripture passage="John 12:43" parsed="|John|12|43|0|0" osisRef="Bible:John.12.43" />
<sup>43</sup>Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu
<scripture passage="John 12:44" parsed="|John|12|44|0|0" osisRef="Bible:John.12.44" />
<sup>44</sup>Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, "Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.
<scripture passage="John 12:45" parsed="|John|12|45|0|0" osisRef="Bible:John.12.45" />
<sup>45</sup>Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.
<scripture passage="John 12:46" parsed="|John|12|46|0|0" osisRef="Bible:John.12.46" />
<sup>46</sup>Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.
<scripture passage="John 12:47" parsed="|John|12|47|0|0" osisRef="Bible:John.12.47" />
<sup>47</sup>Anayeyasikia maneno yangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu; maana sikuja kuhukumu ulimwengu bali kuuokoa.
<scripture passage="John 12:48" parsed="|John|12|48|0|0" osisRef="Bible:John.12.48" />
<sup>48</sup>Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
<scripture passage="John 12:49" parsed="|John|12|49|0|0" osisRef="Bible:John.12.49" />
<sup>49</sup>Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.
<scripture passage="John 12:50" parsed="|John|12|50|0|0" osisRef="Bible:John.12.50" />
<sup>50</sup>Nami najua kuwa amri yake huleta uzima wa milele. Basi, mimi nasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme."
</p>
</div3>

<div3 title="John 13" progress="40.38%" prev="John.12" next="John.14" id="John.13">
<h3 id="John.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="John.13-p1">
<scripture passage="John 13:1" parsed="|John|13|1|0|0" osisRef="Bible:John.13.1" />
<sup>1</sup>Ilikuwa kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
<scripture passage="John 13:2" parsed="|John|13|2|0|0" osisRef="Bible:John.13.2" />
<sup>2</sup>Basi, Yesu na wanafunzi wake walikuwa mezani kwa chakula cha jioni. Ibilisi alikwisha mtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, nia ya kumsaliti Yesu.
<scripture passage="John 13:3" parsed="|John|13|3|0|0" osisRef="Bible:John.13.3" />
<sup>3</sup>Yesu alijua kwamba Baba alikuwa amemkabidhi kila kitu, na kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwa Mungu.
<scripture passage="John 13:4" parsed="|John|13|4|0|0" osisRef="Bible:John.13.4" />
<sup>4</sup>Basi, Yesu aliondoka mezani, akaweka kando vazi lake, akachukua kitambaa na kujifunga kiunoni.
<scripture passage="John 13:5" parsed="|John|13|5|0|0" osisRef="Bible:John.13.5" />
<sup>5</sup>Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuipangusa kwa kile kitambaa alichojifungia.
<scripture passage="John 13:6" parsed="|John|13|6|0|0" osisRef="Bible:John.13.6" />
<sup>6</sup>Basi, akamfikia Simoni Petro; naye Petro akasema, "Bwana, wewe utaniosha miguu mimi?"
<scripture passage="John 13:7" parsed="|John|13|7|0|0" osisRef="Bible:John.13.7" />
<sup>7</sup>Yesu akamjibu, "Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye."
<scripture passage="John 13:8" parsed="|John|13|8|0|0" osisRef="Bible:John.13.8" />
<sup>8</sup>Petro akamwambia, "Wewe hutaniosha miguu kamwe!" Yesu akamjibu, "Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena."
<scripture passage="John 13:9" parsed="|John|13|9|0|0" osisRef="Bible:John.13.9" />
<sup>9</sup>Simoni Petro akamwambia, "Bwana, nioshe, si miguu tu, bali na mikono yangu na kichwa pia."
<scripture passage="John 13:10" parsed="|John|13|10|0|0" osisRef="Bible:John.13.10" />
<sup>10</sup>Yesu akamwambia, "Aliyekwisha oga hana lazima ya kunawa isipokuwa miguu, maana amekwisha takata mwili wote. Ninyi mmetakata, lakini si nyote."
<scripture passage="John 13:11" parsed="|John|13|11|0|0" osisRef="Bible:John.13.11" />
<sup>11</sup>Yesu alimjua yule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema: "Ninyi mmetakata, lakini si nyote.")
<scripture passage="John 13:12" parsed="|John|13|12|0|0" osisRef="Bible:John.13.12" />
<sup>12</sup>Alipokwisha waosha miguu na kuvaa tena vazi lake, aliketi mezani, akawaambia, "Je, mmeelewa hayo niliyowatendeeni?
<scripture passage="John 13:13" parsed="|John|13|13|0|0" osisRef="Bible:John.13.13" />
<sup>13</sup>Ninyi mwaniita Mwalimu na Bwana, nanyi mwasema vyema, kwa kuwa ndimi.
<scripture passage="John 13:14" parsed="|John|13|14|0|0" osisRef="Bible:John.13.14" />
<sup>14</sup>Basi, ikiwa mimi niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha ninyi miguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.
<scripture passage="John 13:15" parsed="|John|13|15|0|0" osisRef="Bible:John.13.15" />
<sup>15</sup>Nimewapeni mfano, ili nanyi pia mfanye kama nilivyowafanyieni.
<scripture passage="John 13:16" parsed="|John|13|16|0|0" osisRef="Bible:John.13.16" />
<sup>16</sup>Kweli nawaambieni, mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu zaidi kuliko yule aliyemtuma.
<scripture passage="John 13:17" parsed="|John|13|17|0|0" osisRef="Bible:John.13.17" />
<sup>17</sup>Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza.
<scripture passage="John 13:18" parsed="|John|13|18|0|0" osisRef="Bible:John.13.18" />
<sup>18</sup>"Haya nisemayo hayawahusu ninyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: `Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.`
<scripture passage="John 13:19" parsed="|John|13|19|0|0" osisRef="Bible:John.13.19" />
<sup>19</sup>Mimi nimewaambieni mambo haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini kuwa mimi ndimi.
<scripture passage="John 13:20" parsed="|John|13|20|0|0" osisRef="Bible:John.13.20" />
<sup>20</sup>Kweli nawaambieni anayempokea yule ninayemtuma anaponipokea mimi; na anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma."
<scripture passage="John 13:21" parsed="|John|13|21|0|0" osisRef="Bible:John.13.21" />
<sup>21</sup>Alipokwisha sema hayo, Yesu alifadhaika sana rohoni, akasema wazi, "Kweli nawaambieni, mmoja wenu atanisaliti!"
<scripture passage="John 13:22" parsed="|John|13|22|0|0" osisRef="Bible:John.13.22" />
<sup>22</sup>Wanafunzi wakatazama wasiweze kabisa kujua anasema nani.
<scripture passage="John 13:23" parsed="|John|13|23|0|0" osisRef="Bible:John.13.23" />
<sup>23</sup>Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibu na Yesu.
<scripture passage="John 13:24" parsed="|John|13|24|0|0" osisRef="Bible:John.13.24" />
<sup>24</sup>Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: "Mwulize anasema juu ya nani."
<scripture passage="John 13:25" parsed="|John|13|25|0|0" osisRef="Bible:John.13.25" />
<sup>25</sup>Mwanafunzi huyo akasogea karibu zaidi na Yesu, akamwuliza, "Bwana, ni nani?"
<scripture passage="John 13:26" parsed="|John|13|26|0|0" osisRef="Bible:John.13.26" />
<sup>26</sup>Yesu akajibu, "Yule nitakayempa kipande cha mkate nilichochovya katika sahani, ndiye." Basi, akatwaa kipande cha mkate, akakichovya katika sahani, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti.
<scripture passage="John 13:27" parsed="|John|13|27|0|0" osisRef="Bible:John.13.27" />
<sup>27</sup>Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia. Basi Yesu akamwambia, "Unachotaka kufanya, kifanye haraka!"
<scripture passage="John 13:28" parsed="|John|13|28|0|0" osisRef="Bible:John.13.28" />
<sup>28</sup>Lakini hakuna hata mmoja wa wale waliokaa pale mezani aliyefahamu kwa nini alikuwa amemwambia hivyo.
<scripture passage="John 13:29" parsed="|John|13|29|0|0" osisRef="Bible:John.13.29" />
<sup>29</sup>Kwa kuwa Yuda alikuwa na wajibu wa kuutunza mfuko wa fedha, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
<scripture passage="John 13:30" parsed="|John|13|30|0|0" osisRef="Bible:John.13.30" />
<sup>30</sup>Basi, Yuda alipokwisha twaa kile kipande cha mkate, akatoka nje mara. Na ilikuwa usiku.
<scripture passage="John 13:31" parsed="|John|13|31|0|0" osisRef="Bible:John.13.31" />
<sup>31</sup>Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema, "Sasa Mwana wa Mtu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake.
<scripture passage="John 13:32" parsed="|John|13|32|0|0" osisRef="Bible:John.13.32" />
<sup>32</sup>Na kama utukufu wa Mungu umefunuliwa ndani ya Mwana, basi, naye Mungu ataudhihirisha utukufu wa Mwana ndani yake mwenyewe, na atafanya hivyo mara.
<scripture passage="John 13:33" parsed="|John|13|33|0|0" osisRef="Bible:John.13.33" />
<sup>33</sup>"Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: `Niendako ninyi hamwezi kwenda!`
<scripture passage="John 13:34" parsed="|John|13|34|0|0" osisRef="Bible:John.13.34" />
<sup>34</sup>Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.
<scripture passage="John 13:35" parsed="|John|13|35|0|0" osisRef="Bible:John.13.35" />
<sup>35</sup>Mkipendana, watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu."
<scripture passage="John 13:36" parsed="|John|13|36|0|0" osisRef="Bible:John.13.36" />
<sup>36</sup>Simoni Petro akamwuliza, "Bwana, unakwenda wapi?" Yesu akajibu, "Niendako huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye."
<scripture passage="John 13:37" parsed="|John|13|37|0|0" osisRef="Bible:John.13.37" />
<sup>37</sup>Petro akamwambia "Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajili yako!"
<scripture passage="John 13:38" parsed="|John|13|38|0|0" osisRef="Bible:John.13.38" />
<sup>38</sup>Yesu akajibu, "Je, uko tayari kweli kufa kwa ajili yangu? Kweli nakwambia, kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu!"
</p>
</div3>

<div3 title="John 14" progress="40.83%" prev="John.13" next="John.15" id="John.14">
<h3 id="John.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="John.14-p1">
<scripture passage="John 14:1" parsed="|John|14|1|0|0" osisRef="Bible:John.14.1" />
<sup>1</sup>Yesu aliwaambia, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.
<scripture passage="John 14:2" parsed="|John|14|2|0|0" osisRef="Bible:John.14.2" />
<sup>2</sup>Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; la sivyo ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi.
<scripture passage="John 14:3" parsed="|John|14|3|0|0" osisRef="Bible:John.14.3" />
<sup>3</sup>Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi.
<scripture passage="John 14:4" parsed="|John|14|4|0|0" osisRef="Bible:John.14.4" />
<sup>4</sup>Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda."
<scripture passage="John 14:5" parsed="|John|14|5|0|0" osisRef="Bible:John.14.5" />
<sup>5</sup>Thoma akamwuliza, "Bwana, hatujui unakokwenda, tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?"
<scripture passage="John 14:6" parsed="|John|14|6|0|0" osisRef="Bible:John.14.6" />
<sup>6</sup>Yesu akamjibu, "Mimi ni njia, na ukweli na uzima. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.
<scripture passage="John 14:7" parsed="|John|14|7|0|0" osisRef="Bible:John.14.7" />
<sup>7</sup>Ikiwa mnanijua mimi mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua, tena mmekwisha mwona."
<scripture passage="John 14:8" parsed="|John|14|8|0|0" osisRef="Bible:John.14.8" />
<sup>8</sup>Filipo akamwambia, "Bwana, tuonyeshe Baba, nasi tutatosheka."
<scripture passage="John 14:9" parsed="|John|14|9|0|0" osisRef="Bible:John.14.9" />
<sup>9</sup>Yesu akamwambia, "Filipo, nimekaa nanyi muda wote huu, nawe hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: `Tuonyeshe Baba?`
<scripture passage="John 14:10" parsed="|John|14|10|0|0" osisRef="Bible:John.14.10" />
<sup>10</sup>Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambieni nyote siyasemi kwa mamlaka yangu; Baba aliye ndani yangu anafanya kazi yake.
<scripture passage="John 14:11" parsed="|John|14|11|0|0" osisRef="Bible:John.14.11" />
<sup>11</sup>Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya.
<scripture passage="John 14:12" parsed="|John|14|12|0|0" osisRef="Bible:John.14.12" />
<sup>12</sup>Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi, maana nakwenda kwa Baba.
<scripture passage="John 14:13" parsed="|John|14|13|0|0" osisRef="Bible:John.14.13" />
<sup>13</sup>Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
<scripture passage="John 14:14" parsed="|John|14|14|0|0" osisRef="Bible:John.14.14" />
<sup>14</sup>Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.
<scripture passage="John 14:15" parsed="|John|14|15|0|0" osisRef="Bible:John.14.15" />
<sup>15</sup>"Mkinipenda mtazishika amri zangu.
<scripture passage="John 14:16" parsed="|John|14|16|0|0" osisRef="Bible:John.14.16" />
<sup>16</sup>Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele.
<scripture passage="John 14:17" parsed="|John|14|17|0|0" osisRef="Bible:John.14.17" />
<sup>17</sup>Yeye ni Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini ninyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.
<scripture passage="John 14:18" parsed="|John|14|18|0|0" osisRef="Bible:John.14.18" />
<sup>18</sup>"Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja tena kwenu.
<scripture passage="John 14:19" parsed="|John|14|19|0|0" osisRef="Bible:John.14.19" />
<sup>19</sup>Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai.
<scripture passage="John 14:20" parsed="|John|14|20|0|0" osisRef="Bible:John.14.20" />
<sup>20</sup>Siku ile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu.
<scripture passage="John 14:21" parsed="|John|14|21|0|0" osisRef="Bible:John.14.21" />
<sup>21</sup>Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."
<scripture passage="John 14:22" parsed="|John|14|22|0|0" osisRef="Bible:John.14.22" />
<sup>22</sup>Yuda (si yule Iskarioti) akamwambia, "Bwana, itawezekanaje wewe kujidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?"
<scripture passage="John 14:23" parsed="|John|14|23|0|0" osisRef="Bible:John.14.23" />
<sup>23</sup>Yesu akamjibu, "Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye.
<scripture passage="John 14:24" parsed="|John|14|24|0|0" osisRef="Bible:John.14.24" />
<sup>24</sup>Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
<scripture passage="John 14:25" parsed="|John|14|25|0|0" osisRef="Bible:John.14.25" />
<sup>25</sup>"Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi
<scripture passage="John 14:26" parsed="|John|14|26|0|0" osisRef="Bible:John.14.26" />
<sup>26</sup>lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni.
<scripture passage="John 14:27" parsed="|John|14|27|0|0" osisRef="Bible:John.14.27" />
<sup>27</sup>"Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi ninyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.
<scripture passage="John 14:28" parsed="|John|14|28|0|0" osisRef="Bible:John.14.28" />
<sup>28</sup>Mlikwisha sikia nikiwaambieni: `Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.` Kama mngalinipenda mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi.
<scripture passage="John 14:29" parsed="|John|14|29|0|0" osisRef="Bible:John.14.29" />
<sup>29</sup>Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini.
<scripture passage="John 14:30" parsed="|John|14|30|0|0" osisRef="Bible:John.14.30" />
<sup>30</sup>Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana mtawala wa ulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu;
<scripture passage="John 14:31" parsed="|John|14|31|0|0" osisRef="Bible:John.14.31" />
<sup>31</sup>lakini ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampenda Baba, na ndiyo maana nafanya kila kitu kama Baba alivyoniamuru. Simameni, tutoke hapa!"
</p>
</div3>

<div3 title="John 15" progress="41.17%" prev="John.14" next="John.16" id="John.15">
<h3 id="John.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="John.15-p1">
<scripture passage="John 15:1" parsed="|John|15|1|0|0" osisRef="Bible:John.15.1" />
<sup>1</sup>"Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
<scripture passage="John 15:2" parsed="|John|15|2|0|0" osisRef="Bible:John.15.2" />
<sup>2</sup>Yeye huliondoa ndani yangu kila tawi lisilozaa matunda, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
<scripture passage="John 15:3" parsed="|John|15|3|0|0" osisRef="Bible:John.15.3" />
<sup>3</sup>Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni.
<scripture passage="John 15:4" parsed="|John|15|4|0|0" osisRef="Bible:John.15.4" />
<sup>4</sup>Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipokaa katika mzabibu hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu. ic
<scripture passage="John 15:5" parsed="|John|15|5|0|0" osisRef="Bible:John.15.5" />
<sup>5</sup>"Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.
<scripture passage="John 15:6" parsed="|John|15|6|0|0" osisRef="Bible:John.15.6" />
<sup>6</sup>Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue.
<scripture passage="John 15:7" parsed="|John|15|7|0|0" osisRef="Bible:John.15.7" />
<sup>7</sup>Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.
<scripture passage="John 15:8" parsed="|John|15|8|0|0" osisRef="Bible:John.15.8" />
<sup>8</sup>Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
<scripture passage="John 15:9" parsed="|John|15|9|0|0" osisRef="Bible:John.15.9" />
<sup>9</sup>Mimi nimewapenda ninyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.
<scripture passage="John 15:10" parsed="|John|15|10|0|0" osisRef="Bible:John.15.10" />
<sup>10</sup>Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
<scripture passage="John 15:11" parsed="|John|15|11|0|0" osisRef="Bible:John.15.11" />
<sup>11</sup>Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.
<scripture passage="John 15:12" parsed="|John|15|12|0|0" osisRef="Bible:John.15.12" />
<sup>12</sup>Hii ndiyo amri yangu: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.
<scripture passage="John 15:13" parsed="|John|15|13|0|0" osisRef="Bible:John.15.13" />
<sup>13</sup>Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
<scripture passage="John 15:14" parsed="|John|15|14|0|0" osisRef="Bible:John.15.14" />
<sup>14</sup>Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.
<scripture passage="John 15:15" parsed="|John|15|15|0|0" osisRef="Bible:John.15.15" />
<sup>15</sup>Ninyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita ninyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.
<scripture passage="John 15:16" parsed="|John|15|16|0|0" osisRef="Bible:John.15.16" />
<sup>16</sup>Ninyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.
<scripture passage="John 15:17" parsed="|John|15|17|0|0" osisRef="Bible:John.15.17" />
<sup>17</sup>Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii: pendaneni.
<scripture passage="John 15:18" parsed="|John|15|18|0|0" osisRef="Bible:John.15.18" />
<sup>18</sup>"Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
<scripture passage="John 15:19" parsed="|John|15|19|0|0" osisRef="Bible:John.15.19" />
<sup>19</sup>Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda ninyi kama watu wake. Lakini kwa vile ninyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni.
<scripture passage="John 15:20" parsed="|John|15|20|0|0" osisRef="Bible:John.15.20" />
<sup>20</sup>Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.
<scripture passage="John 15:21" parsed="|John|15|21|0|0" osisRef="Bible:John.15.21" />
<sup>21</sup>Lakini hayo yote watawatendeeni ninyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma.
<scripture passage="John 15:22" parsed="|John|15|22|0|0" osisRef="Bible:John.15.22" />
<sup>22</sup>Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
<scripture passage="John 15:23" parsed="|John|15|23|0|0" osisRef="Bible:John.15.23" />
<sup>23</sup>Anayenichukia mimi, anamchukia na Baba yangu pia.
<scripture passage="John 15:24" parsed="|John|15|24|0|0" osisRef="Bible:John.15.24" />
<sup>24</sup>Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakinichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.
<scripture passage="John 15:25" parsed="|John|15|25|0|0" osisRef="Bible:John.15.25" />
<sup>25</sup>Na hivi ni lazima yatimie yale yaliyoandikwa katika Sheria yao: `Wamenichukia bure!`
<scripture passage="John 15:26" parsed="|John|15|26|0|0" osisRef="Bible:John.15.26" />
<sup>26</sup>"Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.
<scripture passage="John 15:27" parsed="|John|15|27|0|0" osisRef="Bible:John.15.27" />
<sup>27</sup>Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo.
</p>
</div3>

<div3 title="John 16" progress="41.48%" prev="John.15" next="John.17" id="John.16">
<h3 id="John.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="John.16-p1">
<scripture passage="John 16:1" parsed="|John|16|1|0|0" osisRef="Bible:John.16.1" />
<sup>1</sup>"Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu.
<scripture passage="John 16:2" parsed="|John|16|2|0|0" osisRef="Bible:John.16.2" />
<sup>2</sup>Watu watawatenga ninyi na masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua ninyi atadhani anamhudumia Mungu.
<scripture passage="John 16:3" parsed="|John|16|3|0|0" osisRef="Bible:John.16.3" />
<sup>3</sup>Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi.
<scripture passage="John 16:4" parsed="|John|16|4|0|0" osisRef="Bible:John.16.4" />
<sup>4</sup>Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. "Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
<scripture passage="John 16:5" parsed="|John|16|5|0|0" osisRef="Bible:John.16.5" />
<sup>5</sup>Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: `Unakwenda wapi?`
<scripture passage="John 16:6" parsed="|John|16|6|0|0" osisRef="Bible:John.16.6" />
<sup>6</sup>Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaa huzuni mioyoni mwenu.
<scripture passage="John 16:7" parsed="|John|16|7|0|0" osisRef="Bible:John.16.7" />
<sup>7</sup>Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.
<scripture passage="John 16:8" parsed="|John|16|8|0|0" osisRef="Bible:John.16.8" />
<sup>8</sup>Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.
<scripture passage="John 16:9" parsed="|John|16|9|0|0" osisRef="Bible:John.16.9" />
<sup>9</sup>Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini;
<scripture passage="John 16:10" parsed="|John|16|10|0|0" osisRef="Bible:John.16.10" />
<sup>10</sup>kuhusu uadilifu, kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena;
<scripture passage="John 16:11" parsed="|John|16|11|0|0" osisRef="Bible:John.16.11" />
<sup>11</sup>kuhusu hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.
<scripture passage="John 16:12" parsed="|John|16|12|0|0" osisRef="Bible:John.16.12" />
<sup>12</sup>"Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili.
<scripture passage="John 16:13" parsed="|John|16|13|0|0" osisRef="Bible:John.16.13" />
<sup>13</sup>Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja.
<scripture passage="John 16:14" parsed="|John|16|14|0|0" osisRef="Bible:John.16.14" />
<sup>14</sup>Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.
<scripture passage="John 16:15" parsed="|John|16|15|0|0" osisRef="Bible:John.16.15" />
<sup>15</sup>Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.
<scripture passage="John 16:16" parsed="|John|16|16|0|0" osisRef="Bible:John.16.16" />
<sup>16</sup>"Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!"
<scripture passage="John 16:17" parsed="|John|16|17|0|0" osisRef="Bible:John.16.17" />
<sup>17</sup>Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, "Ana maana gani anapotwambia: `Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?` Tena anasema: `Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!"`
<scripture passage="John 16:18" parsed="|John|16|18|0|0" osisRef="Bible:John.16.18" />
<sup>18</sup>Basi, wakawa wanaulizana, "Ana maana gani anaposema: `Bado kitambo kidogo?` Hatuelewi anaongelea nini."
<scripture passage="John 16:19" parsed="|John|16|19|0|0" osisRef="Bible:John.16.19" />
<sup>19</sup>Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, "Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: `Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?`
<scripture passage="John 16:20" parsed="|John|16|20|0|0" osisRef="Bible:John.16.20" />
<sup>20</sup>Nawaambieni kweli, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi: mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
<scripture passage="John 16:21" parsed="|John|16|21|0|0" osisRef="Bible:John.16.21" />
<sup>21</sup>Wakati mama anapojifungua huona huzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akisha jifungua hayakumbuki tena maumivu hayo kwa sababu ya furaha kwamba mtu amezaliwa duniani.
<scripture passage="John 16:22" parsed="|John|16|22|0|0" osisRef="Bible:John.16.22" />
<sup>22</sup>Ninyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
<scripture passage="John 16:23" parsed="|John|16|23|0|0" osisRef="Bible:John.16.23" />
<sup>23</sup>Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
<scripture passage="John 16:24" parsed="|John|16|24|0|0" osisRef="Bible:John.16.24" />
<sup>24</sup>Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
<scripture passage="John 16:25" parsed="|John|16|25|0|0" osisRef="Bible:John.16.25" />
<sup>25</sup>"Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tena nanyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu ya Baba.
<scripture passage="John 16:26" parsed="|John|16|26|0|0" osisRef="Bible:John.16.26" />
<sup>26</sup>Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;
<scripture passage="John 16:27" parsed="|John|16|27|0|0" osisRef="Bible:John.16.27" />
<sup>27</sup>maana yeye mwenyewe anawapenda ninyi, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu.
<scripture passage="John 16:28" parsed="|John|16|28|0|0" osisRef="Bible:John.16.28" />
<sup>28</sup>Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni; na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba."
<scripture passage="John 16:29" parsed="|John|16|29|0|0" osisRef="Bible:John.16.29" />
<sup>29</sup>Basi, wanafunzi wake wakamwambia, "Ahaa! Sasa unasema waziwazi kabisa bila kutumia mafumbo.
<scripture passage="John 16:30" parsed="|John|16|30|0|0" osisRef="Bible:John.16.30" />
<sup>30</sup>Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu."
<scripture passage="John 16:31" parsed="|John|16|31|0|0" osisRef="Bible:John.16.31" />
<sup>31</sup>Yesu akawajibu, "Je, mnaamini sasa?
<scripture passage="John 16:32" parsed="|John|16|32|0|0" osisRef="Bible:John.16.32" />
<sup>32</sup>Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
<scripture passage="John 16:33" parsed="|John|16|33|0|0" osisRef="Bible:John.16.33" />
<sup>33</sup>Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!"
</p>
</div3>

<div3 title="John 17" progress="41.88%" prev="John.16" next="John.18" id="John.17">
<h3 id="John.17-p0.1">Chapter 17</h3>
<p id="John.17-p1">
<scripture passage="John 17:1" parsed="|John|17|1|0|0" osisRef="Bible:John.17.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juu mbinguni, akasema, "Baba, saa imefika! Mtukuze Mwanao ili naye Mwana apate kukutukuza.
<scripture passage="John 17:2" parsed="|John|17|2|0|0" osisRef="Bible:John.17.2" />
<sup>2</sup>Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wote hao uliompa.
<scripture passage="John 17:3" parsed="|John|17|3|0|0" osisRef="Bible:John.17.3" />
<sup>3</sup>Na uzima wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.
<scripture passage="John 17:4" parsed="|John|17|4|0|0" osisRef="Bible:John.17.4" />
<sup>4</sup>Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa nifanye.
<scripture passage="John 17:5" parsed="|John|17|5|0|0" osisRef="Bible:John.17.5" />
<sup>5</sup>Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu.
<scripture passage="John 17:6" parsed="|John|17|6|0|0" osisRef="Bible:John.17.6" />
<sup>6</sup>"Nimekufanya ujulikane kwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika neno lako.
<scripture passage="John 17:7" parsed="|John|17|7|0|0" osisRef="Bible:John.17.7" />
<sup>7</sup>Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako.
<scripture passage="John 17:8" parsed="|John|17|8|0|0" osisRef="Bible:John.17.8" />
<sup>8</sup>Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma.
<scripture passage="John 17:9" parsed="|John|17|9|0|0" osisRef="Bible:John.17.9" />
<sup>9</sup>"Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea hao ulionipa, maana ni wako.
<scripture passage="John 17:10" parsed="|John|17|10|0|0" osisRef="Bible:John.17.10" />
<sup>10</sup>Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao.
<scripture passage="John 17:11" parsed="|John|17|11|0|0" osisRef="Bible:John.17.11" />
<sup>11</sup>Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
<scripture passage="John 17:12" parsed="|John|17|12|0|0" osisRef="Bible:John.17.12" />
<sup>12</sup>Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimika kupotea ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
<scripture passage="John 17:13" parsed="|John|17|13|0|0" osisRef="Bible:John.17.13" />
<sup>13</sup>Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.
<scripture passage="John 17:14" parsed="|John|17|14|0|0" osisRef="Bible:John.17.14" />
<sup>14</sup>Mimi nimewapa neno lako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
<scripture passage="John 17:15" parsed="|John|17|15|0|0" osisRef="Bible:John.17.15" />
<sup>15</sup>Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.
<scripture passage="John 17:16" parsed="|John|17|16|0|0" osisRef="Bible:John.17.16" />
<sup>16</sup>Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
<scripture passage="John 17:17" parsed="|John|17|17|0|0" osisRef="Bible:John.17.17" />
<sup>17</sup>Waweke wakfu kwa ukweli; neno lako ni ukweli.
<scripture passage="John 17:18" parsed="|John|17|18|0|0" osisRef="Bible:John.17.18" />
<sup>18</sup>Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
<scripture passage="John 17:19" parsed="|John|17|19|0|0" osisRef="Bible:John.17.19" />
<sup>19</sup>na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli.
<scripture passage="John 17:20" parsed="|John|17|20|0|0" osisRef="Bible:John.17.20" />
<sup>20</sup>"Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao.
<scripture passage="John 17:21" parsed="|John|17|21|0|0" osisRef="Bible:John.17.21" />
<sup>21</sup>Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
<scripture passage="John 17:22" parsed="|John|17|22|0|0" osisRef="Bible:John.17.22" />
<sup>22</sup>Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;
<scripture passage="John 17:23" parsed="|John|17|23|0|0" osisRef="Bible:John.17.23" />
<sup>23</sup>mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
<scripture passage="John 17:24" parsed="|John|17|24|0|0" osisRef="Bible:John.17.24" />
<sup>24</sup>"Baba! Nataka wao ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu.
<scripture passage="John 17:25" parsed="|John|17|25|0|0" osisRef="Bible:John.17.25" />
<sup>25</sup>Baba Mwema! Ulimwengu haukujui, lakini mimi nakujua. Hawa nao wanajua kwamba wewe ulinituma.
<scripture passage="John 17:26" parsed="|John|17|26|0|0" osisRef="Bible:John.17.26" />
<sup>26</sup>Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao."
</p>
</div3>

<div3 title="John 18" progress="42.18%" prev="John.17" next="John.19" id="John.18">
<h3 id="John.18-p0.1">Chapter 18</h3>
<p id="John.18-p1">
<scripture passage="John 18:1" parsed="|John|18|1|0|0" osisRef="Bible:John.18.1" />
<sup>1</sup>Yesu alipokwisha sema hayo, alikwenda ng`ambo ya kijito Kedroni, pamoja na wanafunzi wake. Mahali hapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingia humo pamoja na wanafunzi wake.
<scripture passage="John 18:2" parsed="|John|18|2|0|0" osisRef="Bible:John.18.2" />
<sup>2</sup>Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
<scripture passage="John 18:3" parsed="|John|18|3|0|0" osisRef="Bible:John.18.3" />
<sup>3</sup>Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
<scripture passage="John 18:4" parsed="|John|18|4|0|0" osisRef="Bible:John.18.4" />
<sup>4</sup>Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, "Mnamtafuta nani?"
<scripture passage="John 18:5" parsed="|John|18|5|0|0" osisRef="Bible:John.18.5" />
<sup>5</sup>Nao wakamjibu, "Yesu wa Nazareti!" Yesu akawaambia, "Mimi ndiye." Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
<scripture passage="John 18:6" parsed="|John|18|6|0|0" osisRef="Bible:John.18.6" />
<sup>6</sup>Basi, Yesu alipowaambia: "Mimi ndiye", wakarudi nyuma, wakaanguka chini.
<scripture passage="John 18:7" parsed="|John|18|7|0|0" osisRef="Bible:John.18.7" />
<sup>7</sup>Yesu akawauliza tena, "Mnamtafuta nani?" Wakamjibu, "Yesu wa Nazareti!"
<scripture passage="John 18:8" parsed="|John|18|8|0|0" osisRef="Bible:John.18.8" />
<sup>8</sup>Yesu akawaambia, "Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao."
<scripture passage="John 18:9" parsed="|John|18|9|0|0" osisRef="Bible:John.18.9" />
<sup>9</sup>Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: "Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.")
<scripture passage="John 18:10" parsed="|John|18|10|0|0" osisRef="Bible:John.18.10" />
<sup>10</sup>Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
<scripture passage="John 18:11" parsed="|John|18|11|0|0" osisRef="Bible:John.18.11" />
<sup>11</sup>Basi, Yesu akamwambia Petro, "Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipa Baba?"
<scripture passage="John 18:12" parsed="|John|18|12|0|0" osisRef="Bible:John.18.12" />
<sup>12</sup>Kile kikosi cha askari, mkuu wake na walinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga
<scripture passage="John 18:13" parsed="|John|18|13|0|0" osisRef="Bible:John.18.13" />
<sup>13</sup>na kumpeleka kwanza kwa Anasi; Anasi alikuwa baba mkwe wa Kayafa ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo.
<scripture passage="John 18:14" parsed="|John|18|14|0|0" osisRef="Bible:John.18.14" />
<sup>14</sup>Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudi kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa.
<scripture passage="John 18:15" parsed="|John|18|15|0|0" osisRef="Bible:John.18.15" />
<sup>15</sup>Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu.
<scripture passage="John 18:16" parsed="|John|18|16|0|0" osisRef="Bible:John.18.16" />
<sup>16</sup>Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngoja mlango, akamwingiza Petro ndani.
<scripture passage="John 18:17" parsed="|John|18|17|0|0" osisRef="Bible:John.18.17" />
<sup>17</sup>Huyo msichana mngoja mlango akamwuliza Petro, "Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?" Petro akamwambia, "Si mimi!"
<scripture passage="John 18:18" parsed="|John|18|18|0|0" osisRef="Bible:John.18.18" />
<sup>18</sup>Watumishi na walinzi walikuwa wamewasha moto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawa wanaota moto. Naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
<scripture passage="John 18:19" parsed="|John|18|19|0|0" osisRef="Bible:John.18.19" />
<sup>19</sup>Basi, Kuhani akamwuliza Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
<scripture passage="John 18:20" parsed="|John|18|20|0|0" osisRef="Bible:John.18.20" />
<sup>20</sup>Yesu akamjibu, "Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na Hekaluni, mahali wakutanikiapo Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
<scripture passage="John 18:21" parsed="|John|18|21|0|0" osisRef="Bible:John.18.21" />
<sup>21</sup>Kwa nini waniuliza mimi? Waulize wale waliosikia nini niliwaambia. Wao wanajua nilivyosema."
<scripture passage="John 18:22" parsed="|John|18|22|0|0" osisRef="Bible:John.18.22" />
<sup>22</sup>Alipokwisha sema hayo mlinzi mmoja aliyekuwa amesimama hapo akampiga kofi akisema, "Je, ndivyo unavyomjibu Kuhani Mkuu?"
<scripture passage="John 18:23" parsed="|John|18|23|0|0" osisRef="Bible:John.18.23" />
<sup>23</sup>Yesu akamjibu, "Kama nimesema vibaya, onyesha huo ubaya; lakini ikiwa nimesema vema, mbona wanipiga?"
<scripture passage="John 18:24" parsed="|John|18|24|0|0" osisRef="Bible:John.18.24" />
<sup>24</sup>Basi, Anasi akampeleka Yesu akiwa amefungwa, kwa Kuhani Mkuu Kayafa.
<scripture passage="John 18:25" parsed="|John|18|25|0|0" osisRef="Bible:John.18.25" />
<sup>25</sup>Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, "Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?" Yeye akakana na kusema, "Si mimi!"
<scripture passage="John 18:26" parsed="|John|18|26|0|0" osisRef="Bible:John.18.26" />
<sup>26</sup>Mmoja wa watumishi wa Kuhani Mkuu, jamaa wa yule aliyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, "Je, mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?"
<scripture passage="John 18:27" parsed="|John|18|27|0|0" osisRef="Bible:John.18.27" />
<sup>27</sup>Petro akakana tena; mara jogoo akawika.
<scripture passage="John 18:28" parsed="|John|18|28|0|0" osisRef="Bible:John.18.28" />
<sup>28</sup>Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa najisi.
<scripture passage="John 18:29" parsed="|John|18|29|0|0" osisRef="Bible:John.18.29" />
<sup>29</sup>Kwa hiyo, Pilato aliwaendea nje, akasema, "Mna mashtaka gani juu ya mtu huyu?"
<scripture passage="John 18:30" parsed="|John|18|30|0|0" osisRef="Bible:John.18.30" />
<sup>30</sup>Wakamjibu, "Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako."
<scripture passage="John 18:31" parsed="|John|18|31|0|0" osisRef="Bible:John.18.31" />
<sup>31</sup>Pilato akawaambia, "Haya, mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kufuatana na Sheria yenu." Wayahudi wakamjibu, "Sisi hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote."
<scripture passage="John 18:32" parsed="|John|18|32|0|0" osisRef="Bible:John.18.32" />
<sup>32</sup>Ilifanyika hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonyesha atakufa kifo gani.)
<scripture passage="John 18:33" parsed="|John|18|33|0|0" osisRef="Bible:John.18.33" />
<sup>33</sup>Pilato akaingia tena ndani ya ikulu, akamwita Yesu na kumwuliza: "Ati wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?"
<scripture passage="John 18:34" parsed="|John|18|34|0|0" osisRef="Bible:John.18.34" />
<sup>34</sup>Yesu akamjibu, "Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekwambia habari zangu?"
<scripture passage="John 18:35" parsed="|John|18|35|0|0" osisRef="Bible:John.18.35" />
<sup>35</sup>Pilato akamjibu, "Je, ni Myahudi mimi? Taifa lako na makuhani wamekuleta kwangu. Umefanya nini?"
<scripture passage="John 18:36" parsed="|John|18|36|0|0" osisRef="Bible:John.18.36" />
<sup>36</sup>Yesu akamjibu, "Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu watumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa."
<scripture passage="John 18:37" parsed="|John|18|37|0|0" osisRef="Bible:John.18.37" />
<sup>37</sup>Hapo Pilato akamwambia, "Basi, wewe ni Mfalme?" Yesu akajibu, "Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza."
<scripture passage="John 18:38" parsed="|John|18|38|0|0" osisRef="Bible:John.18.38" />
<sup>38</sup>Pilato akamwambia, "Ukweli ni kitu gani?" Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, "Mimi sioni hatia yoyote kwake.
<scripture passage="John 18:39" parsed="|John|18|39|0|0" osisRef="Bible:John.18.39" />
<sup>39</sup>Lakini, mnayo desturi kwamba mimi niwafungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Basi, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?"
<scripture passage="John 18:40" parsed="|John|18|40|0|0" osisRef="Bible:John.18.40" />
<sup>40</sup>Hapo wakapiga kelele: "La! Si huyu ila Baraba!" Naye Baraba alikuwa mnyang`anyi.
</p>
</div3>

<div3 title="John 19" progress="42.67%" prev="John.18" next="John.20" id="John.19">
<h3 id="John.19-p0.1">Chapter 19</h3>
<p id="John.19-p1">
<scripture passage="John 19:1" parsed="|John|19|1|0|0" osisRef="Bible:John.19.1" />
<sup>1</sup>Basi, Pilato akaamuru Yesu achukuliwe, apigwe viboko.
<scripture passage="John 19:2" parsed="|John|19|2|0|0" osisRef="Bible:John.19.2" />
<sup>2</sup>Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika na joho la rangi ya zambarau.
<scripture passage="John 19:3" parsed="|John|19|3|0|0" osisRef="Bible:John.19.3" />
<sup>3</sup>Wakawa wanakuja mbele yake na kusema: "Shikamoo, Mfalme wa Wayahudi!" Wakampiga makofi.
<scripture passage="John 19:4" parsed="|John|19|4|0|0" osisRef="Bible:John.19.4" />
<sup>4</sup>Pilato akatoka tena nje, akawaambia, "Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake."
<scripture passage="John 19:5" parsed="|John|19|5|0|0" osisRef="Bible:John.19.5" />
<sup>5</sup>Basi, Yesu akatoka nje amevaa taji ya miiba na joho la rangi ya zambarau. Pilato akawaambia, "Tazameni! Mtu mwenyewe ni huyo."
<scripture passage="John 19:6" parsed="|John|19|6|0|0" osisRef="Bible:John.19.6" />
<sup>6</sup>Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaaza sauti: "Msulubishe! Msulubishe!" Pilato akawaambia, "Mchukueni basi, ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake."
<scripture passage="John 19:7" parsed="|John|19|7|0|0" osisRef="Bible:John.19.7" />
<sup>7</sup>Wayahudi wakamjibu, "Sisi tunayo Sheria, na kufuatana na Sheria hiyo, ni lazima afe, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu."
<scripture passage="John 19:8" parsed="|John|19|8|0|0" osisRef="Bible:John.19.8" />
<sup>8</sup>Pilato aliposikia maneno hayo akazidi kuogopa.
<scripture passage="John 19:9" parsed="|John|19|9|0|0" osisRef="Bible:John.19.9" />
<sup>9</sup>Basi, akaingia tena ndani ya ikulu, akamwuliza Yesu, "Umetoka wapi wewe?" Lakini Yesu hakumjibu neno.
<scripture passage="John 19:10" parsed="|John|19|10|0|0" osisRef="Bible:John.19.10" />
<sup>10</sup>Hivyo Pilato akamwambia, "Husemi nami? Je, hujui kwamba ninayo mamlaka ya kukufungua na mamlaka ya kukusulubisha?"
<scripture passage="John 19:11" parsed="|John|19|11|0|0" osisRef="Bible:John.19.11" />
<sup>11</sup>Yesu akamjibu, "Hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa na Mungu. Kwa sababu hiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambi kubwa zaidi."
<scripture passage="John 19:12" parsed="|John|19|12|0|0" osisRef="Bible:John.19.12" />
<sup>12</sup>Tangu hapo, Pilato akawa anatafuta njia ya kumwachilia, lakini Wayahudi wakapiga kelele: "Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu anayejifanya kuwa Mfalme humpinga Kaisari!"
<scripture passage="John 19:13" parsed="|John|19|13|0|0" osisRef="Bible:John.19.13" />
<sup>13</sup>Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo: "Sakafu ya Mawe" (kwa Kiebrania, Gabatha).
<scripture passage="John 19:14" parsed="|John|19|14|0|0" osisRef="Bible:John.19.14" />
<sup>14</sup>Ilikuwa yapata saa sita mchana, siku ya maandalio ya Pasaka. Pilato akawaambia Wayahudi, "Tazameni, Mfalme wenu!"
<scripture passage="John 19:15" parsed="|John|19|15|0|0" osisRef="Bible:John.19.15" />
<sup>15</sup>Wao wakapaaza sauti: "Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!" Makuhani wakuu wakajibu, "Sisi hatuna Mfalme isipokuwa Kaisari!"
<scripture passage="John 19:16" parsed="|John|19|16|0|0" osisRef="Bible:John.19.16" />
<sup>16</sup>Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
<scripture passage="John 19:17" parsed="|John|19|17|0|0" osisRef="Bible:John.19.17" />
<sup>17</sup>Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo "Fuvu la Kichwa", (kwa Kiebrania Golgotha).
<scripture passage="John 19:18" parsed="|John|19|18|0|0" osisRef="Bible:John.19.18" />
<sup>18</sup>Hapo ndipo walipomsulubisha, na pamoja naye waliwasulubisha watu wengine wawili; mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto, naye Yesu katikati.
<scripture passage="John 19:19" parsed="|John|19|19|0|0" osisRef="Bible:John.19.19" />
<sup>19</sup>Pilato aliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi: "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi."
<scripture passage="John 19:20" parsed="|John|19|20|0|0" osisRef="Bible:John.19.20" />
<sup>20</sup>Wayahudi wengi waliisoma ilani hiyo, maana mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji. Tena ilani hiyo ilikuwa imeandikwa kwa Kiebrania, Kilatini, na Kigiriki.
<scripture passage="John 19:21" parsed="|John|19|21|0|0" osisRef="Bible:John.19.21" />
<sup>21</sup>Basi, makuhani wakuu wakamwambia Pilato, "Usiandike: `Mfalme wa Wayahudi`, ila `Yeye alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi."`
<scripture passage="John 19:22" parsed="|John|19|22|0|0" osisRef="Bible:John.19.22" />
<sup>22</sup>Pilato akajibu, "Niliyoandika, nimeandika!"
<scripture passage="John 19:23" parsed="|John|19|23|0|0" osisRef="Bible:John.19.23" />
<sup>23</sup>Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
<scripture passage="John 19:24" parsed="|John|19|24|0|0" osisRef="Bible:John.19.24" />
<sup>24</sup>Basi, hao askari wakashauriana: "Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani." Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: "Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura." Basi, ndivyo walivyofanya hao askari. ic
<scripture passage="John 19:25" parsed="|John|19|25|0|0" osisRef="Bible:John.19.25" />
<sup>25</sup>Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
<scripture passage="John 19:26" parsed="|John|19|26|0|0" osisRef="Bible:John.19.26" />
<sup>26</sup>Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: "Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao."
<scripture passage="John 19:27" parsed="|John|19|27|0|0" osisRef="Bible:John.19.27" />
<sup>27</sup>Halafu akamwambia yule mwanafunzi: "Tazama, huyo ndiye mama yako." Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
<scripture passage="John 19:28" parsed="|John|19|28|0|0" osisRef="Bible:John.19.28" />
<sup>28</sup>Yesu alijua kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, "Naona kiu."
<scripture passage="John 19:29" parsed="|John|19|29|0|0" osisRef="Bible:John.19.29" />
<sup>29</sup>Hapo palikuwa na bakuli limejaa siki. Basi, wakachovya sifongo katika hiyo siki, wakaitia juu ya ufito wa husopo, wakamwekea mdomoni.
<scripture passage="John 19:30" parsed="|John|19|30|0|0" osisRef="Bible:John.19.30" />
<sup>30</sup>Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, "Yametimia!" Kisha akainama kichwa, akatoa roho.
<scripture passage="John 19:31" parsed="|John|19|31|0|0" osisRef="Bible:John.19.31" />
<sup>31</sup>Ilikuwa Ijumaa, siku ya Maandalio. Kwa hiyo, kusudi miili isikae msalabani siku ya Sabato, maana siku hiyo ya Sabato ilikuwa siku kubwa, Wayahudi walimwomba Pilato miguu ya hao waliosulubiwa ivunjwe na miili yao iondolewe.
<scripture passage="John 19:32" parsed="|John|19|32|0|0" osisRef="Bible:John.19.32" />
<sup>32</sup>Basi, askari walikwenda, wakaivunja miguu ya yule mtu wa kwanza na yule wa pili ambao walikuwa wamesulubiwa pamoja na Yesu.
<scripture passage="John 19:33" parsed="|John|19|33|0|0" osisRef="Bible:John.19.33" />
<sup>33</sup>Lakini walipomfikia Yesu waliona kwamba alikwisha kufa, na hivyo hawakumvunja miguu.
<scripture passage="John 19:34" parsed="|John|19|34|0|0" osisRef="Bible:John.19.34" />
<sup>34</sup>Lakini askari mmoja alimtoboa ubavuni kwa mkuki, na mara ikatoka damu na maji.
<scripture passage="John 19:35" parsed="|John|19|35|0|0" osisRef="Bible:John.19.35" />
<sup>35</sup>Naye aliyeona tukio hilo ametoa habari zake ili nanyi mpate kuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasema ukweli.)
<scripture passage="John 19:36" parsed="|John|19|36|0|0" osisRef="Bible:John.19.36" />
<sup>36</sup>Jambo hilo lilitendwa ili Maandiko Matakatifu yatimie: "Hapana hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa."
<scripture passage="John 19:37" parsed="|John|19|37|0|0" osisRef="Bible:John.19.37" />
<sup>37</sup>Tena Maandiko mengine yanasema: "Watamtazama yule waliyemtoboa."
<scripture passage="John 19:38" parsed="|John|19|38|0|0" osisRef="Bible:John.19.38" />
<sup>38</sup>Baada ya hayo, Yosefu, mwenyeji wa Armathaya, alimwomba Pilato ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. (Yosefu alikuwa mfuasi wa Yesu, lakini kwa siri, maana aliwaogopa viongozi wa Wayahudi). Basi, Pilato akamruhusu. Hivyo Yosefu alikwenda, akauondoa mwili wa Yesu.
<scripture passage="John 19:39" parsed="|John|19|39|0|0" osisRef="Bible:John.19.39" />
<sup>39</sup>Naye Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku, akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane na ubani kiasi cha kilo thelathini.
<scripture passage="John 19:40" parsed="|John|19|40|0|0" osisRef="Bible:John.19.40" />
<sup>40</sup>Basi, waliutwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatana na desturi ya Wayahudi katika kuzika.
<scripture passage="John 19:41" parsed="|John|19|41|0|0" osisRef="Bible:John.19.41" />
<sup>41</sup>Mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani, na katika bustani hiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtu yeyote ndani yake.
<scripture passage="John 19:42" parsed="|John|19|42|0|0" osisRef="Bible:John.19.42" />
<sup>42</sup>Basi, kwa sababu ya shughuli za Wayahudi za maandalio ya Sabato, na kwa vile kaburi hilo lilikuwa karibu, wakamweka Yesu humo.
</p>
</div3>

<div3 title="John 20" progress="43.25%" prev="John.19" next="John.21" id="John.20">
<h3 id="John.20-p0.1">Chapter 20</h3>
<p id="John.20-p1">
<scripture passage="John 20:1" parsed="|John|20|1|0|0" osisRef="Bible:John.20.1" />
<sup>1</sup>Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
<scripture passage="John 20:2" parsed="|John|20|2|0|0" osisRef="Bible:John.20.2" />
<sup>2</sup>Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, "Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka."
<scripture passage="John 20:3" parsed="|John|20|3|0|0" osisRef="Bible:John.20.3" />
<sup>3</sup>Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini.
<scripture passage="John 20:4" parsed="|John|20|4|0|0" osisRef="Bible:John.20.4" />
<sup>4</sup>Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.
<scripture passage="John 20:5" parsed="|John|20|5|0|0" osisRef="Bible:John.20.5" />
<sup>5</sup>Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.
<scripture passage="John 20:6" parsed="|John|20|6|0|0" osisRef="Bible:John.20.6" />
<sup>6</sup>Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,
<scripture passage="John 20:7" parsed="|John|20|7|0|0" osisRef="Bible:John.20.7" />
<sup>7</sup>na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.
<scripture passage="John 20:8" parsed="|John|20|8|0|0" osisRef="Bible:John.20.8" />
<sup>8</sup>Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyemtangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaaamini.
<scripture passage="John 20:9" parsed="|John|20|9|0|0" osisRef="Bible:John.20.9" />
<sup>9</sup>Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu).
<scripture passage="John 20:10" parsed="|John|20|10|0|0" osisRef="Bible:John.20.10" />
<sup>10</sup>Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani.
<scripture passage="John 20:11" parsed="|John|20|11|0|0" osisRef="Bible:John.20.11" />
<sup>11</sup>Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, akilia. Huku akiwa bado analia, aliinama na kuchungulia kaburini,
<scripture passage="John 20:12" parsed="|John|20|12|0|0" osisRef="Bible:John.20.12" />
<sup>12</sup>akawaona malaika wawili waliovaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja kichwani na wa pili miguuni.
<scripture passage="John 20:13" parsed="|John|20|13|0|0" osisRef="Bible:John.20.13" />
<sup>13</sup>Hao malaika wakamwuliza, "Mama, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Wamemwondoa Bwana wangu, na wala sijui walikomweka!"
<scripture passage="John 20:14" parsed="|John|20|14|0|0" osisRef="Bible:John.20.14" />
<sup>14</sup>Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu.
<scripture passage="John 20:15" parsed="|John|20|15|0|0" osisRef="Bible:John.20.15" />
<sup>15</sup>Yesu akamwuliza, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, "Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."
<scripture passage="John 20:16" parsed="|John|20|16|0|0" osisRef="Bible:John.20.16" />
<sup>16</sup>Yesu akamwambia, "Maria!" Naye Maria akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, "Raboni" (yaani "Mwalimu").
<scripture passage="John 20:17" parsed="|John|20|17|0|0" osisRef="Bible:John.20.17" />
<sup>17</sup>Yesu akamwambia, "Usinishike; sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."
<scripture passage="John 20:18" parsed="|John|20|18|0|0" osisRef="Bible:John.20.18" />
<sup>18</sup>Hivyo Maria Magdalene akaenda akawapa habari wale wanafunzi kuwa amemwona Bwana, na kwamba alikuwa amemwambia hivyo.
<scripture passage="John 20:19" parsed="|John|20|19|0|0" osisRef="Bible:John.20.19" />
<sup>19</sup>Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, "Amani kwenu!"
<scripture passage="John 20:20" parsed="|John|20|20|0|0" osisRef="Bible:John.20.20" />
<sup>20</sup>Alipokwisha sema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana.
<scripture passage="John 20:21" parsed="|John|20|21|0|0" osisRef="Bible:John.20.21" />
<sup>21</sup>Yesu akawaambia tena, "Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi."
<scripture passage="John 20:22" parsed="|John|20|22|0|0" osisRef="Bible:John.20.22" />
<sup>22</sup>Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, "Pokeeni Roho Mtakatifu.
<scripture passage="John 20:23" parsed="|John|20|23|0|0" osisRef="Bible:John.20.23" />
<sup>23</sup>Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowaondolea, hawasamehewi."
<scripture passage="John 20:24" parsed="|John|20|24|0|0" osisRef="Bible:John.20.24" />
<sup>24</sup>Thoma mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja.
<scripture passage="John 20:25" parsed="|John|20|25|0|0" osisRef="Bible:John.20.25" />
<sup>25</sup>Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, "Tumemwona Bwana." Thoma akawaambia, "Nisipoona mikononi mwake alama za misumari, na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki."
<scripture passage="John 20:26" parsed="|John|20|26|0|0" osisRef="Bible:John.20.26" />
<sup>26</sup>Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, "Amani kwenu!"
<scripture passage="John 20:27" parsed="|John|20|27|0|0" osisRef="Bible:John.20.27" />
<sup>27</sup>Kisha akamwambia Thoma, "Lete kidole chako hapa uitazame mikono yangu; lete mkono wako ukautie ubavuni mwangu. Usiwe na mashaka, ila amini!"
<scripture passage="John 20:28" parsed="|John|20|28|0|0" osisRef="Bible:John.20.28" />
<sup>28</sup>Thoma akamjibu, "Bwana wangu na Mungu wangu!"
<scripture passage="John 20:29" parsed="|John|20|29|0|0" osisRef="Bible:John.20.29" />
<sup>29</sup>Yesu akamwambia, "Je, unaamini kwa kuwa umeniona? Heri yao wale ambao hawajaona, lakini wameamini."
<scripture passage="John 20:30" parsed="|John|20|30|0|0" osisRef="Bible:John.20.30" />
<sup>30</sup>Yesu alifanya mbele ya wanafunzi wake ishara nyingine nyingi ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki.
<scripture passage="John 20:31" parsed="|John|20|31|0|0" osisRef="Bible:John.20.31" />
<sup>31</sup>Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa nguvu ya jina lake.
</p>
</div3>

<div3 title="John 21" progress="43.64%" prev="John.20" next="Acts" id="John.21">
<h3 id="John.21-p0.1">Chapter 21</h3>
<p id="John.21-p1">
<scripture passage="John 21:1" parsed="|John|21|1|0|0" osisRef="Bible:John.21.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo Yesu aliwatokea tena wanafunzi wake kando ya ziwa Tiberia. Aliwatokea hivi:
<scripture passage="John 21:2" parsed="|John|21|2|0|0" osisRef="Bible:John.21.2" />
<sup>2</sup>Simoni Petro, Thoma (aitwaye Pacha), na Nathanieli mwenyeji wa Kana Galilaya, wana wawili wa Zebedayo na wanafunzi wake wengine wawili, walikuwa wote pamoja.
<scripture passage="John 21:3" parsed="|John|21|3|0|0" osisRef="Bible:John.21.3" />
<sup>3</sup>Simoni Petro aliwaambia, "Nakwenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Nasi tutafuatana nawe." Basi, wakaenda, wakapanda mashua, lakini usiku huo hawakupata chochote.
<scripture passage="John 21:4" parsed="|John|21|4|0|0" osisRef="Bible:John.21.4" />
<sup>4</sup>Kulipoanza kupambazuka, Yesu alisimama kando ya ziwa, lakini wanafunzi hawakujua kwamba alikuwa yeye.
<scripture passage="John 21:5" parsed="|John|21|5|0|0" osisRef="Bible:John.21.5" />
<sup>5</sup>Basi, Yesu akawauliza, "Vijana, hamjapata samaki wowote sio?" Wao wakamjibu, "La! Hatujapata kitu."
<scripture passage="John 21:6" parsed="|John|21|6|0|0" osisRef="Bible:John.21.6" />
<sup>6</sup>Yesu akawaambia, "Tupeni wavu upande wa kulia wa mashua nanyi mtapata samaki." Basi, wakatupa wavu lakini sasa hawakuweza kuuvuta tena kwa wingi wa samaki.
<scripture passage="John 21:7" parsed="|John|21|7|0|0" osisRef="Bible:John.21.7" />
<sup>7</sup>Hapo yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, "Ni Bwana!" Simoni Petro aliposikia ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa), akarukia majini.
<scripture passage="John 21:8" parsed="|John|21|8|0|0" osisRef="Bible:John.21.8" />
<sup>8</sup>Lakini wale wanafunzi wengine walikuja pwani kwa mashua huku wanauvuta wavu uliojaa samaki; hawakuwa mbali na nchi kavu, ila walikuwa yapata mita mia moja kutoka ukingoni.
<scripture passage="John 21:9" parsed="|John|21|9|0|0" osisRef="Bible:John.21.9" />
<sup>9</sup>Walipofika nchi kavu waliona moto wa makaa umewashwa na juu yake pamewekwa samaki na mkate.
<scripture passage="John 21:10" parsed="|John|21|10|0|0" osisRef="Bible:John.21.10" />
<sup>10</sup>Yesu akawaambia, "Leteni hapa baadhi ya samaki mliovua."
<scripture passage="John 21:11" parsed="|John|21|11|0|0" osisRef="Bible:John.21.11" />
<sup>11</sup>Basi, Simoni Petro akapanda mashuani, akavuta hadi nchi kavu ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa mia moja na hamsini na watatu. Na ingawa walikuwa wengi hivyo wavu haukukatika.
<scripture passage="John 21:12" parsed="|John|21|12|0|0" osisRef="Bible:John.21.12" />
<sup>12</sup>Yesu akawaambia, "Njoni mkafungue kinywa." Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza: "Wewe ni nani?" Maana walijua alikuwa Bwana.
<scripture passage="John 21:13" parsed="|John|21|13|0|0" osisRef="Bible:John.21.13" />
<sup>13</sup>Yesu akaja, akatwaa mkate akawapa; akafanya vivyo hivyo na wale samaki.
<scripture passage="John 21:14" parsed="|John|21|14|0|0" osisRef="Bible:John.21.14" />
<sup>14</sup>Hii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake baada ya kufufuka kutoka wafu.
<scripture passage="John 21:15" parsed="|John|21|15|0|0" osisRef="Bible:John.21.15" />
<sup>15</sup>Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, "Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi zaidi kuliko hawa?" Naye akajibu, "Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda." Yesu akamwambia, "Tunza wana kondoo wangu."
<scripture passage="John 21:16" parsed="|John|21|16|0|0" osisRef="Bible:John.21.16" />
<sup>16</sup>Kisha akamwambia mara ya pili, "Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?" Petro akamjibu, "Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda." Yesu akamwambia, "Tunza kondoo wangu."
<scripture passage="John 21:17" parsed="|John|21|17|0|0" osisRef="Bible:John.21.17" />
<sup>17</sup>Akamwuliza mara ya tatu, "Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?" Hapo Petro akahuzunika kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: "Wanipenda?" akamwambia, "Bwana, wewe wajua yote; wewe wajua kwamba mimi nakupenda." Yesu akamwambia, "Tunza kondoo wangu!
<scripture passage="John 21:18" parsed="|John|21|18|0|0" osisRef="Bible:John.21.18" />
<sup>18</sup>Kweli nakwambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda."
<scripture passage="John 21:19" parsed="|John|21|19|0|0" osisRef="Bible:John.21.19" />
<sup>19</sup>(Kwa kusema hivyo, alionyesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu.) Kisha akamwambia, "Nifuate."
<scripture passage="John 21:20" parsed="|John|21|20|0|0" osisRef="Bible:John.21.20" />
<sup>20</sup>Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda, anafuata (Huyu mwanafunzi ndiye yule ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibu sana na Yesu na kumwuliza: "Bwana ni nani atakayekusaliti?")
<scripture passage="John 21:21" parsed="|John|21|21|0|0" osisRef="Bible:John.21.21" />
<sup>21</sup>Basi, Petro alipomwona huyo akamwuliza Yesu, "Bwana, na huyu je?"
<scripture passage="John 21:22" parsed="|John|21|22|0|0" osisRef="Bible:John.21.22" />
<sup>22</sup>Yesu akamjibu, "Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi."
<scripture passage="John 21:23" parsed="|John|21|23|0|0" osisRef="Bible:John.21.23" />
<sup>23</sup>Basi, habari hiyo ikaenea miongoni mwa wale ndugu kwamba mwanafunzi huyo hafi. Lakini Yesu hakumwambia kwamba mwanafunzi huyo hafi, ila, "Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini?"
<scripture passage="John 21:24" parsed="|John|21|24|0|0" osisRef="Bible:John.21.24" />
<sup>24</sup>Huyo ndiye yule aliyeshuhudia mambo haya na kuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasema ni kweli.
<scripture passage="John 21:25" parsed="|John|21|25|0|0" osisRef="Bible:John.21.25" />
<sup>25</sup>Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Acts" progress="44.01%" prev="John.21" next="Acts.1" id="Acts">
<h2 id="Acts-p0.1">Acts</h2>

<div3 title="Acts 1" progress="44.01%" prev="Acts" next="Acts.2" id="Acts.1">
<h3 id="Acts.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Acts.1-p1">
<scripture passage="Acts 1:1" parsed="|Acts|1|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.1" />
<sup>1</sup>Ndugu Theofilo, Katika kitabu cha kwanza niliandika juu ya mambo yote Yesu aliyotenda na kufundisha tangu mwanzo wa kazi yake
<scripture passage="Acts 1:2" parsed="|Acts|1|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.2" />
<sup>2</sup>mpaka siku ile alipochukuliwa mbinguni. Kabla ya kuchukuliwa mbinguni aliwapa maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua.
<scripture passage="Acts 1:3" parsed="|Acts|1|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.3" />
<sup>3</sup>Kwa muda wa siku arobaini baada ya kifo chake aliwatokea mara nyingi kwa namna ambazo zilithibitisha kabisa kwamba alikuwa hai. Walimwona, naye aliongea nao juu ya ufalme wa Mungu.
<scripture passage="Acts 1:4" parsed="|Acts|1|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.4" />
<sup>4</sup>Wakati walipokutana pamoja aliwaamuru hivi: "Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeeni ile zawadi aliyoahidi Baba, zawadi ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
<scripture passage="Acts 1:5" parsed="|Acts|1|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.5" />
<sup>5</sup>Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu."
<scripture passage="Acts 1:6" parsed="|Acts|1|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.6" />
<sup>6</sup>Basi, mitume walipokutana pamoja na Yesu, walimwuliza, "Je Bwana, wakati huu ndipo utakaporudisha ule ufalme kwa Israeli?"
<scripture passage="Acts 1:7" parsed="|Acts|1|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.7" />
<sup>7</sup>Lakini Yesu akawaambia, "Nyakati na majira ya mambo hayo viko chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.
<scripture passage="Acts 1:8" parsed="|Acts|1|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.8" />
<sup>8</sup>Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia."
<scripture passage="Acts 1:9" parsed="|Acts|1|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.9" />
<sup>9</sup>Baada ya kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwa mbinguni; wingu likamficha wasimwone tena.
<scripture passage="Acts 1:10" parsed="|Acts|1|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.10" />
<sup>10</sup>Walipokuwa bado wanatazama juu angani, akiwa anakwenda zake, mara watu wawili waliokuwa wamevaa nguo nyeupe walisimama karibu nao,
<scripture passage="Acts 1:11" parsed="|Acts|1|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.11" />
<sup>11</sup>wakasema, "Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mliivyomwona akienda mbinguni."
<scripture passage="Acts 1:12" parsed="|Acts|1|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.12" />
<sup>12</sup>Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
<scripture passage="Acts 1:13" parsed="|Acts|1|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.13" />
<sup>13</sup>Walipofika mjini waliingia katika chumba ghorofani ambamo walikuwa wanakaa; nao walikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipo na Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.
<scripture passage="Acts 1:14" parsed="|Acts|1|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.14" />
<sup>14</sup>Hawa wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria mama yake Yesu, na ndugu zake.
<scripture passage="Acts 1:15" parsed="|Acts|1|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.15" />
<sup>15</sup>Siku chache baadaye, kulikuwa na mkutano wa waumini, karibu watu mia moja na ishirini. Petro alisimama mbele yao,
<scripture passage="Acts 1:16" parsed="|Acts|1|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.16" />
<sup>16</sup>akasema, "Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu nguvuni.
<scripture passage="Acts 1:17" parsed="|Acts|1|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.17" />
<sup>17</sup>Yuda alikuwa mmoja wa kikundi chetu maana alichaguliwa ashiriki huduma yetu.
<scripture passage="Acts 1:18" parsed="|Acts|1|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.18" />
<sup>18</sup>"Mnajua kwamba yeye alinunua shamba kwa zile fedha alizopata kutokana na kitendo chake kiovu. Akaanguka chini, akapasuka na matumbo yake yakamwagika nje.
<scripture passage="Acts 1:19" parsed="|Acts|1|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.19" />
<sup>19</sup>Kila mtu katika Yerusalemu alisikia habari za tukio hilo na hivyo, kwa lugha yao, wakaliita lile shamba `Hekeli Dama`, maana yake, `Shamba la Damu.`)
<scripture passage="Acts 1:20" parsed="|Acts|1|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.20" />
<sup>20</sup>Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: `Nyumba yake ibaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake.` Tena imeandikwa: `Mtu mwingine achukue nafasi yake katika huduma hiyo.`
<scripture passage="Acts 1:21" parsed="|Acts|1|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.21" />
<sup>21</sup>Kwa hiyo, ni lazima mtu mwingine ajiunge nasi kama shahidi wa ufufuo wake Bwana Yesu. Anapaswa kuwa mmoja wa wale waliokuwa katika kundi letu wakati wote Bwana alipokuwa anasafiri pamoja nasi, tangu wakati Yohane alipokuwa anabatiza mpaka siku ile Yesu alipochukuliwa kutoka kwetu kwenda mbinguni."
<scripture passage="Acts 1:22" parsed="|Acts|1|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.22" />
<sup>22</sup>[]
<scripture passage="Acts 1:23" parsed="|Acts|1|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.23" />
<sup>23</sup>Basi, wakataja majina ya watu wawili; wa kwanza Yosefu aliyeitwa Barsaba (au pia Yusto), na wa pili Mathia.
<scripture passage="Acts 1:24" parsed="|Acts|1|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.24" />
<sup>24</sup>Kisha wakasali: "Bwana, wewe unajua mioyo ya watu wote. Hivyo, utuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua
<scripture passage="Acts 1:25" parsed="|Acts|1|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.25" />
<sup>25</sup>ili achukue nafasi hii ya huduma ya kitume aliyoacha Yuda akaenda mahali pake mwenyewe."
<scripture passage="Acts 1:26" parsed="|Acts|1|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.1.26" />
<sup>26</sup>Hapo, wakapiga kura; kura ikampata Mathia, naye akaongezwa katika idadi ya wale mitume wengine kumi na mmoja.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 2" progress="44.39%" prev="Acts.1" next="Acts.3" id="Acts.2">
<h3 id="Acts.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Acts.2-p1">
<scripture passage="Acts 2:1" parsed="|Acts|2|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.1" />
<sup>1</sup>Siku ya Pentekoste ilipofika, waumini wote walikuwa wamekusanyika pamoja.
<scripture passage="Acts 2:2" parsed="|Acts|2|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.2" />
<sup>2</sup>Ghafla, sauti ikasikika kutoka angani; sauti iliyokuwa kama ya upepo mkali, ikajaza ile nyumba yote walimokuwa wamekaa.
<scripture passage="Acts 2:3" parsed="|Acts|2|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.3" />
<sup>3</sup>Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kama ndimi za moto, vikagawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao.
<scripture passage="Acts 2:4" parsed="|Acts|2|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.4" />
<sup>4</sup>Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha.
<scripture passage="Acts 2:5" parsed="|Acts|2|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.5" />
<sup>5</sup>Na huko Yerusalemu walikuwako Wayahudi, watu wamchao Mungu, waliotoka katika kila nchi duniani.
<scripture passage="Acts 2:6" parsed="|Acts|2|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.6" />
<sup>6</sup>Waliposikia sauti hiyo, kundi kubwa la watu lilikusanyika. Wote walishtuka sana kwani kila mmoja wao aliwasikia hao waumini wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
<scripture passage="Acts 2:7" parsed="|Acts|2|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.7" />
<sup>7</sup>Walistaajabu na kushangaa, wakisema, "Je, hawa wote tunaowasikia wakisema hivi, si wenyeji wa Galilaya?
<scripture passage="Acts 2:8" parsed="|Acts|2|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.8" />
<sup>8</sup>Imekuwaje, basi, kwamba kila mmoja wetu anawasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe?
<scripture passage="Acts 2:9" parsed="|Acts|2|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.9" />
<sup>9</sup>Baadhi yetu ni Waparthi, Wamedi na Waelami; wengine ni wenyeji wa Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto na Asia,
<scripture passage="Acts 2:10" parsed="|Acts|2|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.10" />
<sup>10</sup>Frugia na Pamfulia, Misri na sehemu za Libya karibu na Kurene; wengine wetu ni wageni kutoka Roma,
<scripture passage="Acts 2:11" parsed="|Acts|2|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.11" />
<sup>11</sup>Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu."
<scripture passage="Acts 2:12" parsed="|Acts|2|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.12" />
<sup>12</sup>Wote walishangaa na kufadhaika huku wakiulizana, "Hii ina maana gani?"
<scripture passage="Acts 2:13" parsed="|Acts|2|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.13" />
<sup>13</sup>Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, "Watu hawa wamelewa divai mpya!"
<scripture passage="Acts 2:14" parsed="|Acts|2|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.14" />
<sup>14</sup>Lakini Petro alisimama pamoja na wale kumi na mmoja akaanza kuwahutubia watu kwa sauti kubwa: "Ndugu Wayahudi nanyi nyote mnaokaa hapa Yerusalemu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
<scripture passage="Acts 2:15" parsed="|Acts|2|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.15" />
<sup>15</sup>Watu hawa hawakulewa kama mnavyodhani; mbona ni saa tatu tu asubuhi?
<scripture passage="Acts 2:16" parsed="|Acts|2|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.16" />
<sup>16</sup>Ukweli ni kwamba jambo hili ni lile alilosema nabii Yoeli:
<scripture passage="Acts 2:17" parsed="|Acts|2|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.17" />
<sup>17</sup>`Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
<scripture passage="Acts 2:18" parsed="|Acts|2|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.18" />
<sup>18</sup>Naam, hata watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, nitawamiminia Roho wangu, siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu.
<scripture passage="Acts 2:19" parsed="|Acts|2|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.19" />
<sup>19</sup>Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito;
<scripture passage="Acts 2:20" parsed="|Acts|2|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.20" />
<sup>20</sup>jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana.
<scripture passage="Acts 2:21" parsed="|Acts|2|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.21" />
<sup>21</sup>Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.`
<scripture passage="Acts 2:22" parsed="|Acts|2|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.22" />
<sup>22</sup>"Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.
<scripture passage="Acts 2:23" parsed="|Acts|2|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.23" />
<sup>23</sup>Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe.
<scripture passage="Acts 2:24" parsed="|Acts|2|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.24" />
<sup>24</sup>Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu akamwokoa katika maumivu ya kifo kwa maana haingewezekana kabisa kifo kimfunge.
<scripture passage="Acts 2:25" parsed="|Acts|2|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.25" />
<sup>25</sup>Maana Daudi alisema juu yake hivi: `Nilimwona Bwana mbele yangu daima; yuko nami upande wangu wa kulia, na hivyo sitatikisika.
<scripture passage="Acts 2:26" parsed="|Acts|2|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.26" />
<sup>26</sup>Kwa hiyo, moyo wangu ulifurahi; tena nilipiga vigelegele vya furaha. Mwili wangu utakaa katika tumaini;
<scripture passage="Acts 2:27" parsed="|Acts|2|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.27" />
<sup>27</sup>kwa kuwa hutaiacha roho yangu katika kuzimu, wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.
<scripture passage="Acts 2:28" parsed="|Acts|2|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.28" />
<sup>28</sup>Umenionyesha njia za kuufikia uzima, kuwako kwako kwanijaza furaha!`
<scripture passage="Acts 2:29" parsed="|Acts|2|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.29" />
<sup>29</sup>"Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake liko papa hapa petu mpaka leo.
<scripture passage="Acts 2:30" parsed="|Acts|2|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.30" />
<sup>30</sup>Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.
<scripture passage="Acts 2:31" parsed="|Acts|2|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.31" />
<sup>31</sup>Daudi aliona kabla mambo yatakayofanywa na Mungu na hivyo akasema juu ya ufufuo wa Kristo wakati aliposema: `Hakuachwa kuzimu, mwili wake haukuoza.`
<scripture passage="Acts 2:32" parsed="|Acts|2|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.32" />
<sup>32</sup>Basi, Mungu alimfufua huyo Yesu na sisi sote ni mashahidi wa tukio hilo.
<scripture passage="Acts 2:33" parsed="|Acts|2|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.33" />
<sup>33</sup>Yesu aliinuliwa juu mpaka upande wa kulia wa Mungu, akapokea kutoka kwa Baba ile zawadi aliyoahidi yaani Roho Mtakatifu; na mnachoona sasa na kusikia ni mmiminiko wa huyo Roho.
<scripture passage="Acts 2:34" parsed="|Acts|2|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.34" />
<sup>34</sup>Maana Daudi mwenyewe, hakupanda mpaka mbinguni; ila yeye alisema: `Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia,
<scripture passage="Acts 2:35" parsed="|Acts|2|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.35" />
<sup>35</sup>hadi nitakapowafanya adui zako kibao cha kukanyagia miguu yako.`
<scripture passage="Acts 2:36" parsed="|Acts|2|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.36" />
<sup>36</sup>"Watu wote wa Israeli wanapaswa kufahamu kwa hakika kwamba huyo Yesu mliyemsulubisha ninyi, ndiye huyo ambaye Mungu amemfanya kuwa Bwana na Kristo."
<scripture passage="Acts 2:37" parsed="|Acts|2|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.37" />
<sup>37</sup>Basi, watu waliposikia hayo, walichomwa moyo, wakawauliza Petro na wale mitume wenzake: "Ndugu zetu, tufanye nini?"
<scripture passage="Acts 2:38" parsed="|Acts|2|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.38" />
<sup>38</sup>Petro akajibu, "Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile zawadi ya Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Acts 2:39" parsed="|Acts|2|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.39" />
<sup>39</sup>Maana, ahadi ile ilikuwa kwa ajili yenu, kwa ajili ya watoto wenu, kwa ajili ya wote wanaokaa mbali; na kwa ajili ya kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita kwake."
<scripture passage="Acts 2:40" parsed="|Acts|2|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.40" />
<sup>40</sup>Kwa maneno mengine mengi, Petro alisisitiza na kuwahimiza watu akisema, "Jiokoeni katika kizazi hiki kiovu."
<scripture passage="Acts 2:41" parsed="|Acts|2|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.41" />
<sup>41</sup>Wengi waliyakubali maneno yake, wakabatizwa. Watu wapatao elfu tatu wakaongezeka katika kile kikundi siku hiyo.
<scripture passage="Acts 2:42" parsed="|Acts|2|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.42" />
<sup>42</sup>Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kidugu, kumega mkate na kusali.
<scripture passage="Acts 2:43" parsed="|Acts|2|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.43" />
<sup>43</sup>Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu.
<scripture passage="Acts 2:44" parsed="|Acts|2|44|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.44" />
<sup>44</sup>Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawana pamoja.
<scripture passage="Acts 2:45" parsed="|Acts|2|45|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.45" />
<sup>45</sup>Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja.
<scripture passage="Acts 2:46" parsed="|Acts|2|46|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.46" />
<sup>46</sup>Waliendelea kukutana pamoja kila siku Hekaluni. Lakini wakati wa kumega mkate, walikutana katika nyumba zao na wakakishiriki chakula hicho kwa furaha na moyo mkunjufu.
<scripture passage="Acts 2:47" parsed="|Acts|2|47|0|0" osisRef="Bible:Acts.2.47" />
<sup>47</sup>Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 3" progress="44.96%" prev="Acts.2" next="Acts.4" id="Acts.3">
<h3 id="Acts.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Acts.3-p1">
<scripture passage="Acts 3:1" parsed="|Acts|3|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.1" />
<sup>1</sup>Siku moja, saa tisa alasiri, Petro na Yohane walikuwa wanakwenda Hekaluni, wakati wa sala.
<scripture passage="Acts 3:2" parsed="|Acts|3|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.2" />
<sup>2</sup>Na pale karibu na mlango wa Hekalu uitwao "Mlango Mzuri", palikuwa na mtu mmoja, kiwete tangu kuzaliwa. Watu walimbeba huyo mtu kila siku na kumweka hapo ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia Hekaluni.
<scripture passage="Acts 3:3" parsed="|Acts|3|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.3" />
<sup>3</sup>Alipowaona Petro na Yohane wakiingia Hekaluni, aliwaomba wampe chochote.
<scripture passage="Acts 3:4" parsed="|Acts|3|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.4" />
<sup>4</sup>Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, "Tutazame!"
<scripture passage="Acts 3:5" parsed="|Acts|3|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.5" />
<sup>5</sup>Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
<scripture passage="Acts 3:6" parsed="|Acts|3|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.6" />
<sup>6</sup>Kisha Petro akamwambia, "Sina fedha wala dhahabu lakini kile nilicho nacho nitakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!"
<scripture passage="Acts 3:7" parsed="|Acts|3|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.7" />
<sup>7</sup>Halafu, akamshika mkono wa kulia, akamwinua. Papo hapo miguu na magoti yake yakapata nguvu.
<scripture passage="Acts 3:8" parsed="|Acts|3|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.8" />
<sup>8</sup>Akaruka, akasimama na kuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja nao Hekaluni, akitembea na kurukaruka huku akimtukuza Mungu.
<scripture passage="Acts 3:9" parsed="|Acts|3|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.9" />
<sup>9</sup>Watu wote waliokuwa hapo walimwona akitembea na kumsifu Mungu.
<scripture passage="Acts 3:10" parsed="|Acts|3|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.10" />
<sup>10</sup>Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule "Mlango Mzuri" wa Hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
<scripture passage="Acts 3:11" parsed="|Acts|3|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.11" />
<sup>11</sup>Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa "Ukumbi wa Solomoni," ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
<scripture passage="Acts 3:12" parsed="|Acts|3|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.12" />
<sup>12</sup>Basi, Petro alipowaona watu hao akawaambia, "Wananchi wa Israeli, kwa nini mnashangazwa na jambo hili? Mbona mnatukodolea macho kana kwamba ni kwa nguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewe tumemfanya mtu huyu aweze kutembea?
<scripture passage="Acts 3:13" parsed="|Acts|3|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.13" />
<sup>13</sup>Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Yesu mtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.
<scripture passage="Acts 3:14" parsed="|Acts|3|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.14" />
<sup>14</sup>Alikuwa mtakatifu na mwema; lakini ninyi mlimkataa, mkataka mtu mwingine aliyekuwa muuaji afunguliwe.
<scripture passage="Acts 3:15" parsed="|Acts|3|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.15" />
<sup>15</sup>Basi, mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uzima. Lakini Mungu alimfufua, na sisi ni mashahidi wa tukio hilo.
<scripture passage="Acts 3:16" parsed="|Acts|3|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.16" />
<sup>16</sup>Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
<scripture passage="Acts 3:17" parsed="|Acts|3|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.17" />
<sup>17</sup>"Sasa ndugu zangu, nafahamu kwamba ninyi na wakuu wenu mlitenda hayo kwa sababu ya kutojua kwenu.
<scripture passage="Acts 3:18" parsed="|Acts|3|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.18" />
<sup>18</sup>Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yale aliyotangaza zamani kwa njia ya manabii wote, kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke.
<scripture passage="Acts 3:19" parsed="|Acts|3|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.19" />
<sup>19</sup>Basi, tubuni mkamrudie Mungu ili afute dhambi zenu.
<scripture passage="Acts 3:20" parsed="|Acts|3|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.20" />
<sup>20</sup>Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu.
<scripture passage="Acts 3:21" parsed="|Acts|3|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.21" />
<sup>21</sup>Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake watakatifu wa tangu zamani.
<scripture passage="Acts 3:22" parsed="|Acts|3|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.22" />
<sup>22</sup>Kwa maana Mose alisema, `Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu ninyi wenyewe.
<scripture passage="Acts 3:23" parsed="|Acts|3|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.23" />
<sup>23</sup>Yeyote yule ambaye hatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na watu wa Mungu na kuangamizwa.`
<scripture passage="Acts 3:24" parsed="|Acts|3|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.24" />
<sup>24</sup>Manabii wote, kuanzia Samweli na wale waliomfuata, walitangaza habari za mambo haya ambayo yamekuwa yakitendeka siku hizi.
<scripture passage="Acts 3:25" parsed="|Acts|3|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.25" />
<sup>25</sup>Ahadi zile Mungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajili yenu; na mnashiriki lile agano Mungu alilofanya na babu zenu, kama alivyomwambia Abrahamu: `Kwa njia ya wazawa wako, jamaa zote za dunia zitabarikiwa.`
<scripture passage="Acts 3:26" parsed="|Acts|3|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.3.26" />
<sup>26</sup>Basi, ilikuwa kwa ajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufua mtumishi wake, alimtuma awabariki kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake."
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 4" progress="45.31%" prev="Acts.3" next="Acts.5" id="Acts.4">
<h3 id="Acts.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Acts.4-p1">
<scripture passage="Acts 4:1" parsed="|Acts|4|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.1" />
<sup>1</sup>Petro na Yohane walipokuwa bado wanawahutubia watu, makuhani na mkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na Masadukayo *walifika.
<scripture passage="Acts 4:2" parsed="|Acts|4|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.2" />
<sup>2</sup>Walikasirika sana, maana hao mitume walikuwa wanawahubiria watu kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba wafu watafufuka.
<scripture passage="Acts 4:3" parsed="|Acts|4|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.3" />
<sup>3</sup>Basi, waliwatia nguvuni na kwa kuwa usiku ulikuwa umekaribia, wakawaweka chini ya ulinzi mpaka kesho yake.
<scripture passage="Acts 4:4" parsed="|Acts|4|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.4" />
<sup>4</sup>Lakini wengi kati ya wale waliosikia ujumbe wao waliamini, na idadi ya waumini ikawa imefika karibu elfu tano.
<scripture passage="Acts 4:5" parsed="|Acts|4|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.5" />
<sup>5</sup>Kesho yake, viongozi wa Wayahudi, wazee na walimu wa Sheria, walikusanyika pamoja huko Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 4:6" parsed="|Acts|4|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.6" />
<sup>6</sup>Walikutana pamoja na Anasi, Kayafa, Yohane, Aleksanda na wengine waliokuwa wa ukoo wa Kuhani Mkuu.
<scripture passage="Acts 4:7" parsed="|Acts|4|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.7" />
<sup>7</sup>Waliwasimamisha mitume mbele yao, wakawauliza, "Ninyi mmefanya jambo hili kwa nguvu gani na kwa jina la nani?"
<scripture passage="Acts 4:8" parsed="|Acts|4|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.8" />
<sup>8</sup>Hapo, Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akawaambia, "Viongozi na wazee wa watu!
<scripture passage="Acts 4:9" parsed="|Acts|4|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.9" />
<sup>9</sup>Ikiwa mnatuuliza leo juu ya kile kitendo chema alichofanyiwa yule mtu aliyekuwa kiwete na jinsi alivyopata kuwa mzima,
<scripture passage="Acts 4:10" parsed="|Acts|4|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.10" />
<sup>10</sup>basi, ninyi na watu wote wa Israeli mnapaswa kujua kwamba mtu huyu anasimama mbele yenu leo, mzima kabisa, kwa nguvu ya jina lake Yesu wa Nazareti ambaye ninyi mlimsulubisha, lakini Mungu akamfufua kutoka wafu.
<scripture passage="Acts 4:11" parsed="|Acts|4|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.11" />
<sup>11</sup>Huyu ndiye ambaye Maandiko Matakatifu yanasema: `Jiwe mlilokataa ninyi waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.`
<scripture passage="Acts 4:12" parsed="|Acts|4|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.12" />
<sup>12</sup>Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza kuokolewa naye."
<scripture passage="Acts 4:13" parsed="|Acts|4|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.13" />
<sup>13</sup>Hao wazee wa baraza, wakiwa wanajua kwamba Petro na Yohane walikuwa watu wasio na kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juu ya jinsi walivyosema kwa uhodari. Wakatambua kwamba walikuwa wamejiunga na Yesu.
<scripture passage="Acts 4:14" parsed="|Acts|4|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.14" />
<sup>14</sup>Lakini walipomwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao, hawakuweza kusema kitu.
<scripture passage="Acts 4:15" parsed="|Acts|4|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.15" />
<sup>15</sup>Hivyo, waliwaamuru watoke nje ya baraza, nao wakabaki ndani wakizungumza kwa faragha.
<scripture passage="Acts 4:16" parsed="|Acts|4|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.16" />
<sup>16</sup>Wakaulizana, "Tufanye nini na watu hawa? Kila mtu anayeishi Yerusalemu anajua kwamba mwujiza huu wa ajabu umefanyika, nasi hatuwezi kukana jambo hilo.
<scripture passage="Acts 4:17" parsed="|Acts|4|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.17" />
<sup>17</sup>Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu."
<scripture passage="Acts 4:18" parsed="|Acts|4|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.18" />
<sup>18</sup>Kwa hiyo wakawaita tena ndani, wakawaonya wasiongee tena hadharani, wala kufundisha kwa jina la Yesu.
<scripture passage="Acts 4:19" parsed="|Acts|4|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.19" />
<sup>19</sup>Lakini Petro na Yohane wakawajibu, "Amueni ninyi wenyewe kama ni haki mbele ya Mungu kuwatii ninyi kuliko kumtii yeye.
<scripture passage="Acts 4:20" parsed="|Acts|4|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.20" />
<sup>20</sup>Kwa maana hatuwezi kuacha kusema juu ya mambo yale tuliyoyaona na kuyasikia."
<scripture passage="Acts 4:21" parsed="|Acts|4|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.21" />
<sup>21</sup>Basi, hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukali zaidi, halafu wakawaacha huru. Hawakuweza kuwapa adhabu kwa sababu watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa sababu ya tukio hilo.
<scripture passage="Acts 4:22" parsed="|Acts|4|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.22" />
<sup>22</sup>Huyo mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya arobaini.
<scripture passage="Acts 4:23" parsed="|Acts|4|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.23" />
<sup>23</sup>Mara tu walipoachwa huru, Petro na Yohane walirudi kwa wenzao, wakawaeleza yale waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee.
<scripture passage="Acts 4:24" parsed="|Acts|4|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.24" />
<sup>24</sup>Waliposikia habari hiyo waliungana pamoja katika kumwomba Mungu wakisema, "Bwana, wewe ni Muumba wa mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo!
<scripture passage="Acts 4:25" parsed="|Acts|4|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.25" />
<sup>25</sup>Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, babu yetu Daudi, aseme kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: `Kwa nini mataifa yameghadhibika? Mbona watu wamefanya mipango ya bure?
<scripture passage="Acts 4:26" parsed="|Acts|4|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.26" />
<sup>26</sup>Wafalme wa dunia walijiweka tayari, na watawala walikutana pamoja, ili kumwasi Bwana na Kristo wake.`
<scripture passage="Acts 4:27" parsed="|Acts|4|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.27" />
<sup>27</sup>"Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye umemtia mafuta.
<scripture passage="Acts 4:28" parsed="|Acts|4|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.28" />
<sup>28</sup>Naam, walikutana ili wafanye yale ambayo ulikusudia na kupanga tangu mwanzo kwa uwezo wako na mapenzi yako.
<scripture passage="Acts 4:29" parsed="|Acts|4|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.29" />
<sup>29</sup>Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitisho vyao. Utuwezeshe sisi watumishi wako kuhubiri neno lako kwa uhodari.
<scripture passage="Acts 4:30" parsed="|Acts|4|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.30" />
<sup>30</sup>Nyosha mkono wako uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu."
<scripture passage="Acts 4:31" parsed="|Acts|4|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.31" />
<sup>31</sup>Walipomaliza kusali, pale mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa Roho Mtakatifu. Wote wakaanza kuhubiri neno la Mungu bila uoga.
<scripture passage="Acts 4:32" parsed="|Acts|4|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.32" />
<sup>32</sup>Jumuiya yote ya waumini ilikuwa moyo mmoja na roho moja. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwa mali yake binafsi, ila waligawana vyote walivyokuwa navyo.
<scripture passage="Acts 4:33" parsed="|Acts|4|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.33" />
<sup>33</sup>Mitume walishuhudia kwa nguvu nyingi kufufuka kwa Bwana Yesu, naye Mungu akawapa baraka nyingi.
<scripture passage="Acts 4:34" parsed="|Acts|4|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.34" />
<sup>34</sup>Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maana waliokuwa na mashamba au nyumba walikuwa wanaviuza
<scripture passage="Acts 4:35" parsed="|Acts|4|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.35" />
<sup>35</sup>na kuwakabidhi mitume fedha hizo, zikagawiwa kila mmoja kadiri ya mahitaji yake.
<scripture passage="Acts 4:36" parsed="|Acts|4|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.36" />
<sup>36</sup>Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwa wa Kupro, jina lake Yosefu, ambaye mitume walimwita jina Barnaba (maana yake, "Mtu mwenye kutia moyo").
<scripture passage="Acts 4:37" parsed="|Acts|4|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.4.37" />
<sup>37</sup>Yeye pia alikuwa na shamba lake, akaliuza; akazichukua zile fedha, akawakabidhi mitume.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 5" progress="45.79%" prev="Acts.4" next="Acts.6" id="Acts.5">
<h3 id="Acts.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Acts.5-p1">
<scripture passage="Acts 5:1" parsed="|Acts|5|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.1" />
<sup>1</sup>Mtu mmoja aitwaye Anania na mkewe Safira waliuza shamba lao vilevile.
<scripture passage="Acts 5:2" parsed="|Acts|5|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.2" />
<sup>2</sup>Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
<scripture passage="Acts 5:3" parsed="|Acts|5|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.3" />
<sup>3</sup>Basi, Petro akamwuliza, "Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
<scripture passage="Acts 5:4" parsed="|Acts|5|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.4" />
<sup>4</sup>Kabla ya kuliuza lilikuwa mali yako, na baada ya kuliuza, bado hizo fedha zilikuwa zako uzitumie utakavyo. Kwa nini basi, uliamua moyoni mwako kufanya jambo la namna hii? Hukumdanganya mtu; umemdanganya Mungu!"
<scripture passage="Acts 5:5" parsed="|Acts|5|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.5" />
<sup>5</sup>Anania aliposikia hayo, akaanguka chini, akafa. Watu wote waliosikia habari ya tukio hilo waliogopa sana.
<scripture passage="Acts 5:6" parsed="|Acts|5|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.6" />
<sup>6</sup>Vijana wakafika wakaufunika mwili wake, wakamtoa nje, wakamzika.
<scripture passage="Acts 5:7" parsed="|Acts|5|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.7" />
<sup>7</sup>Baada ya muda wa saa tatu hivi, mke wake, bila kufahamu mambo yaliyotukia, akaingia mle ndani.
<scripture passage="Acts 5:8" parsed="|Acts|5|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.8" />
<sup>8</sup>Petro akamwambia, "Niambie! Je, kiasi hiki cha fedha ndicho mlichopata kwa kuuza lile shamba?" Yeye akamjibu, "Naam, ni kiasi hicho."
<scripture passage="Acts 5:9" parsed="|Acts|5|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.9" />
<sup>9</sup>Naye Petro akamwambia, "Mbona mmekula njama kumjaribu Roho wa Bwana? Sikiliza! Wale watu waliokwenda kumzika mume wako, sasa wako mlangoni na watakuchukua wewe pia."
<scripture passage="Acts 5:10" parsed="|Acts|5|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.10" />
<sup>10</sup>Mara Safira akaanguka mbele ya miguu ya Petro, akafa. Wale vijana walipoingia, walimkuta amekwisha kufa; hivyo wakamtoa nje, wakamzika karibu na mume wake.
<scripture passage="Acts 5:11" parsed="|Acts|5|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.11" />
<sup>11</sup>Kanisa lote pamoja na wote waliosikia habari ya tukio hilo, waliogopa sana.
<scripture passage="Acts 5:12" parsed="|Acts|5|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.12" />
<sup>12</sup>Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
<scripture passage="Acts 5:13" parsed="|Acts|5|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.13" />
<sup>13</sup>Mtu yeyote mwingine ambaye hakuwa mwamini hakuthubutu kujiunga nao. Hata hivyo, watu wengine wasiokuwa wa imani hiyo waliwasifu.
<scripture passage="Acts 5:14" parsed="|Acts|5|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.14" />
<sup>14</sup>Idadi ya watu waliomwamini Bwana, wanaume kwa wanawake, iliongezeka zaidi na zaidi.
<scripture passage="Acts 5:15" parsed="|Acts|5|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.15" />
<sup>15</sup>Kwa sababu hiyo, watu walikuwa wakipeleka wagonjwa barabarani na kuwalaza juu ya vitanda na mikeka ili Petro akipita, walau kivuli chake kiwaguse baadhi yao.
<scripture passage="Acts 5:16" parsed="|Acts|5|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.16" />
<sup>16</sup>Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kando kando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
<scripture passage="Acts 5:17" parsed="|Acts|5|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.17" />
<sup>17</sup>Kisha, Kuhani Mkuu na wenzake waliokuwa wa kikundi cha Masadukayo wa mahali hapo, wakawaonea mitume wivu.
<scripture passage="Acts 5:18" parsed="|Acts|5|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.18" />
<sup>18</sup>Basi, wakawatia nguvuni, wakawafunga ndani ya gereza kuu.
<scripture passage="Acts 5:19" parsed="|Acts|5|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.19" />
<sup>19</sup>Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia,
<scripture passage="Acts 5:20" parsed="|Acts|5|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.20" />
<sup>20</sup>"Nendeni mkasimame Hekaluni na kuwaambia watu kila kitu kuhusu maisha haya mapya."
<scripture passage="Acts 5:21" parsed="|Acts|5|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.21" />
<sup>21</sup>Mitume walitii, wakaingia Hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani Mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu, yaani halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
<scripture passage="Acts 5:22" parsed="|Acts|5|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.22" />
<sup>22</sup>Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni,
<scripture passage="Acts 5:23" parsed="|Acts|5|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.23" />
<sup>23</sup>wakisema, "Tulikuta gereza limefungwa kila upande na walinzi wakilinda milango. Lakini tulipofungua hatukumkuta mtu yeyote ndani."
<scripture passage="Acts 5:24" parsed="|Acts|5|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.24" />
<sup>24</sup>Mkuu wa walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
<scripture passage="Acts 5:25" parsed="|Acts|5|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.25" />
<sup>25</sup>Akafika mtu mmoja, akawaambia, "Wale watu mliowafunga gerezani, hivi sasa wamo Hekaluni, wanawafundisha watu."
<scripture passage="Acts 5:26" parsed="|Acts|5|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.26" />
<sup>26</sup>Hapo mkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na watu wake walikwenda Hekaluni, akawaleta. Lakini hawakuwakamata kwa kutumia nguvu, maana waliogopa kwamba watu wangewapiga mawe.
<scripture passage="Acts 5:27" parsed="|Acts|5|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.27" />
<sup>27</sup>Basi, wakawapeleka, wakawasimamisha mbele ya Baraza. Kuhani Mkuu akawaambia,
<scripture passage="Acts 5:28" parsed="|Acts|5|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.28" />
<sup>28</sup>"Tuliwakatazeni waziwazi kufundisha kwa jina la mtu huyu; sasa mmeyaeneza mafundisho yenu pote katika Yerusalemu na mnakusudia kutuwekea lawama ya kifo cha mtu huyo."
<scripture passage="Acts 5:29" parsed="|Acts|5|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.29" />
<sup>29</sup>Hapo Petro, akiwa pamoja na wale mitume wengine, akajibu, "Lazima tumtii Mungu, na siyo binadamu.
<scripture passage="Acts 5:30" parsed="|Acts|5|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.30" />
<sup>30</sup>Mungu wa babu zetu alimfufua Yesu baada ya ninyi kumwua kwa kumtundika msalabani.
<scripture passage="Acts 5:31" parsed="|Acts|5|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.31" />
<sup>31</sup>Huyu ndiye yule aliyekwezwa na Mungu mpaka upande wake wa kulia, akawa kiongozi na Mwokozi, ili awawezeshe watu wa Israeli watubu, wapate kusamehewa dhambi zao.
<scripture passage="Acts 5:32" parsed="|Acts|5|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.32" />
<sup>32</sup>Sisi ni mashahidi wa tukio hilo, naye Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii, anashuhudia pia tukio hilo."
<scripture passage="Acts 5:33" parsed="|Acts|5|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.33" />
<sup>33</sup>Wajumbe wote wa lile Baraza waliposikia hayo, wakawaka hasira, hata wakaamua kuwaua.
<scripture passage="Acts 5:34" parsed="|Acts|5|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.34" />
<sup>34</sup>Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa Sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.
<scripture passage="Acts 5:35" parsed="|Acts|5|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.35" />
<sup>35</sup>Kisha akawaambia wale wajumbe wa Baraza, "Wananchi wa Israeli, tahadhari kabla ya kutekeleza hicho mnachotaka kuwatenda watu hawa!
<scripture passage="Acts 5:36" parsed="|Acts|5|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.36" />
<sup>36</sup>Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu mia nne wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
<scripture passage="Acts 5:37" parsed="|Acts|5|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.37" />
<sup>37</sup>Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye, aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
<scripture passage="Acts 5:38" parsed="|Acts|5|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.38" />
<sup>38</sup>Na sasa pia mimi nawaambieni, msiwachukulie watu hawa hatua yoyote; waacheni! Kwa maana, ikiwa mpango huu au shughuli hii yao imeanzishwa na binadamu, itatoweka yenyewe.
<scripture passage="Acts 5:39" parsed="|Acts|5|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.39" />
<sup>39</sup>Lakini kama imeanzishwa na Mungu, siyo tu kwamba hamtaweza kuwashinda, bali mtajikuta mnapigana na Mungu." Basi, wakakubaliana naye.
<scripture passage="Acts 5:40" parsed="|Acts|5|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.40" />
<sup>40</sup>Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.
<scripture passage="Acts 5:41" parsed="|Acts|5|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.41" />
<sup>41</sup>Basi, mitume wakatoka nje ya ule mkutano wa halmashauri wakiwa wamejaa furaha, kwani walistahili kuaibishwa kwa ajili ya jina la Yesu.
<scripture passage="Acts 5:42" parsed="|Acts|5|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.5.42" />
<sup>42</sup>Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo, Hekaluni na nyumbani mwa watu.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 6" progress="46.36%" prev="Acts.5" next="Acts.7" id="Acts.6">
<h3 id="Acts.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Acts.6-p1">
<scripture passage="Acts 6:1" parsed="|Acts|6|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.1" />
<sup>1</sup>Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manung`uniko kati ya wanafunzi waliosema Kigiriki na wale waliosema Kiebrania. Wale waliosema Kigiriki walinung`unika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
<scripture passage="Acts 6:2" parsed="|Acts|6|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.2" />
<sup>2</sup>Kwa hiyo, mitume kumi na wawili waliita jumuiya yote ya wanafunzi, wakasema, "Si vizuri sisi tuache kulihubiri neno la Mungu ili tushughulikie ugawaji wa mahitaji.
<scripture passage="Acts 6:3" parsed="|Acts|6|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.3" />
<sup>3</sup>Hivyo, ndugu zetu, chagueni miongoni mwenu watu saba wenye sifa njema, waliojawa na Roho na wenye hekima; nasi tutawakabidhi jukumu hilo.
<scripture passage="Acts 6:4" parsed="|Acts|6|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.4" />
<sup>4</sup>Sisi, lakini, tutashughulika na sala na kazi ya kuhubiri neno la Mungu."
<scripture passage="Acts 6:5" parsed="|Acts|6|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.5" />
<sup>5</sup>Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujawa na Roho Mtakatifu, Filipo, Prokoro, Nikanora, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye hapo awali alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.
<scripture passage="Acts 6:6" parsed="|Acts|6|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.6" />
<sup>6</sup>Wakawaweka mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono.
<scripture passage="Acts 6:7" parsed="|Acts|6|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.7" />
<sup>7</sup>Neno la Mungu likazidi kuenea na idadi ya waumini huko Yerusalemu ikaongezeka zaidi, na kundi kubwa la makuhani wakaipokea imani.
<scripture passage="Acts 6:8" parsed="|Acts|6|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.8" />
<sup>8</sup>Mungu alimjalia Stefano neema tele, akampa nguvu nyingi hata akawa anatenda miujiza na maajabu kati ya watu.
<scripture passage="Acts 6:9" parsed="|Acts|6|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.9" />
<sup>9</sup>Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa "Sunagogi la Watu Huru", nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
<scripture passage="Acts 6:10" parsed="|Acts|6|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.10" />
<sup>10</sup>Lakini hawakuweza kumshinda kwa sababu ya hekima yake na kwa sababu ya yule Roho aliyeongoza maneno yake.
<scripture passage="Acts 6:11" parsed="|Acts|6|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.11" />
<sup>11</sup>Kwa hiyo waliwahonga watu kadhaa waseme: "Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kumkashifu Mose na kumkashifu Mungu."
<scripture passage="Acts 6:12" parsed="|Acts|6|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.12" />
<sup>12</sup>Kwa namna hiyo, waliwachochea watu, wazee na walimu wa Sheria. Basi, wakamjia Stefano, wakamkamata na kumleta mbele ya Baraza kuu.
<scripture passage="Acts 6:13" parsed="|Acts|6|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.13" />
<sup>13</sup>Walileta Barazani mashahidi wa uongo ambao walisema, "Mtu huyu haachi kamwe kusema maneno ya kupakashifu mahali hapa patakatifu na Sheria ya Mose.
<scripture passage="Acts 6:14" parsed="|Acts|6|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.14" />
<sup>14</sup>Kwa maana tulikwisha msikia akisema eti huyo Yesu wa Nazareti atapaharibu kabisa mahali hapa na kufutilia mbali desturi zile tulizopokea kutoka kwa Mose."
<scripture passage="Acts 6:15" parsed="|Acts|6|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.6.15" />
<sup>15</sup>Wote waliokuwa katika kile kikao cha Baraza walimkodolea macho Stefano, wakauona uso wake umekuwa kama wa malaika.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 7" progress="46.59%" prev="Acts.6" next="Acts.8" id="Acts.7">
<h3 id="Acts.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Acts.7-p1">
<scripture passage="Acts 7:1" parsed="|Acts|7|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.1" />
<sup>1</sup>Basi, Kuhani Mkuu akamwuliza, "Je, mambo haya ni kweli?"
<scripture passage="Acts 7:2" parsed="|Acts|7|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.2" />
<sup>2</sup>Naye Stefano akasema, "Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni! Mungu alimtokea baba yetu Abrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kabla hajaenda kukaa kule Harani.
<scripture passage="Acts 7:3" parsed="|Acts|7|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.3" />
<sup>3</sup>Mungu alimwambia: `Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonyesha!`
<scripture passage="Acts 7:4" parsed="|Acts|7|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.4" />
<sup>4</sup>Kwa hivyo, Abrahamu alihama nchi ya Kaldayo, akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu alimtoa tena Harani akaja kukaa katika nchi hii mnayokaa sasa.
<scripture passage="Acts 7:5" parsed="|Acts|7|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.5" />
<sup>5</sup>Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata hivyo, alimwahidia kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwa na mtoto.
<scripture passage="Acts 7:6" parsed="|Acts|7|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.6" />
<sup>6</sup>Mungu alimwambia hivi: `Wazao wako watapelekwa katika nchi inayotawaliwa na watu wengine, na huko watafanywa watumwa na kutendewa vibaya kwa muda wa miaka mia nne.
<scripture passage="Acts 7:7" parsed="|Acts|7|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.7" />
<sup>7</sup>Lakini mimi nitalihukumu taifa hilo litakalowafanya watumwa. Kisha nitawatoa katika nchi hiyo ili waje kuniabudu mahali hapa.`
<scripture passage="Acts 7:8" parsed="|Acts|7|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.8" />
<sup>8</sup>Halafu Mungu aliifanya tohara iwe ishara ya agano. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka, siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
<scripture passage="Acts 7:9" parsed="|Acts|7|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.9" />
<sup>9</sup>"Wale mababu walimwonea wivu Yosefu, wakamuuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,
<scripture passage="Acts 7:10" parsed="|Acts|7|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.10" />
<sup>10</sup>akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa ile nchi na nyumba ya kifalme.
<scripture passage="Acts 7:11" parsed="|Acts|7|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.11" />
<sup>11</sup>Kisha, kulizuka njaa kubwa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, ikasababisha dhiki kubwa. Babu zetu hawakuweza kupata chakula chochote.
<scripture passage="Acts 7:12" parsed="|Acts|7|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.12" />
<sup>12</sup>Basi, Yakobo alipopata habari kwamba huko Misri kulikuwa na nafaka, aliwatuma watoto wake, yaani babu zetu, waende huko Misri mara ya kwanza.
<scripture passage="Acts 7:13" parsed="|Acts|7|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.13" />
<sup>13</sup>Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
<scripture passage="Acts 7:14" parsed="|Acts|7|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.14" />
<sup>14</sup>Yosefu alituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote, jumla watu sabini na tano, waje Misri.
<scripture passage="Acts 7:15" parsed="|Acts|7|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.15" />
<sup>15</sup>Hivyo, Yakobo alikwenda Misri ambako yeye na babu zetu wengine walikufa.
<scripture passage="Acts 7:16" parsed="|Acts|7|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.16" />
<sup>16</sup>Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi Abrahamu alilonunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
<scripture passage="Acts 7:17" parsed="|Acts|7|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.17" />
<sup>17</sup>"Wakati ulipotimia Mungu aitimize ahadi aliyompa Abrahamu, idadi ya wale watu kule Misri ilikwisha ongezeka na kuwa kubwa zaidi.
<scripture passage="Acts 7:18" parsed="|Acts|7|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.18" />
<sup>18</sup>Mwishowe, mfalme mmoja ambaye hakumtambua Yosefu alianza kutawala huko Misri.
<scripture passage="Acts 7:19" parsed="|Acts|7|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.19" />
<sup>19</sup>Alilifanyia taifa letu ukatili, akawatendea vibaya babu zetu kwa kuwalazimisha waweke nje watoto wao wachanga ili wafe.
<scripture passage="Acts 7:20" parsed="|Acts|7|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.20" />
<sup>20</sup>Mose alizaliwa wakati huo. Alikuwa mtoto mzuri sana. Alilelewa nyumbani kwa muda wa miezi mitatu,
<scripture passage="Acts 7:21" parsed="|Acts|7|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.21" />
<sup>21</sup>na alipotolewa nje, binti wa Farao alimchukua, akamlea kama mtoto wake.
<scripture passage="Acts 7:22" parsed="|Acts|7|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.22" />
<sup>22</sup>Mose alifundishwa mambo yote ya hekima ya Wamisri akawa mashuhuri kwa maneno na matendo.
<scripture passage="Acts 7:23" parsed="|Acts|7|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.23" />
<sup>23</sup>"Alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kwenda kuwaona ndugu zake Waisraeli.
<scripture passage="Acts 7:24" parsed="|Acts|7|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.24" />
<sup>24</sup>Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri.
<scripture passage="Acts 7:25" parsed="|Acts|7|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.25" />
<sup>25</sup>Alidhani kwamba Waisraeli wenzake wangeelewa kwamba Mungu angemtumia yeye kuwakomboa, lakini hawakuelewa hivyo.)
<scripture passage="Acts 7:26" parsed="|Acts|7|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.26" />
<sup>26</sup>Kesho yake, aliwaona Waisraeli wawili wakipigana, akajaribu kuwapatanisha, akisema: `Ninyi ni ndugu; kwa nini basi, kutendeana vibaya ninyi kwa ninyi?`
<scripture passage="Acts 7:27" parsed="|Acts|7|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.27" />
<sup>27</sup>Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: `Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wa watu?
<scripture passage="Acts 7:28" parsed="|Acts|7|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.28" />
<sup>28</sup>Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?`
<scripture passage="Acts 7:29" parsed="|Acts|7|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.29" />
<sup>29</sup>Baada ya kusikia hayo Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata watoto wawili.
<scripture passage="Acts 7:30" parsed="|Acts|7|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.30" />
<sup>30</sup>"Miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana alimtokea Mose katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto kule jangwani karibu na mlima Sinai.
<scripture passage="Acts 7:31" parsed="|Acts|7|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.31" />
<sup>31</sup>Mose alistaajabu sana kuona jambo hilo hata akasogea karibu ili achungulie; lakini alisikia sauti ya Bwana:
<scripture passage="Acts 7:32" parsed="|Acts|7|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.32" />
<sup>32</sup>`Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo!` Mose akatetemeka kwa hofu na wala hakuthubutu kutazama zaidi.
<scripture passage="Acts 7:33" parsed="|Acts|7|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.33" />
<sup>33</sup>Bwana akamwambia: `Vua viatu vyako maana hapa unaposimama ni mahali patakatifu.
<scripture passage="Acts 7:34" parsed="|Acts|7|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.34" />
<sup>34</sup>Nimeyaona mabaya wanayotendewa watu wangu kule Misri. Nimesikia kilio chao, nami nimekuja kuwaokoa. Basi sasa, nitakutuma Misri.`
<scripture passage="Acts 7:35" parsed="|Acts|7|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.35" />
<sup>35</sup>"Huyu Mose ndiye yule watu wa Israeli waliyemkataa waliposema: `Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?` Kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto, Mungu alimtuma Mose huyo awe kiongozi na mkombozi.
<scripture passage="Acts 7:36" parsed="|Acts|7|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.36" />
<sup>36</sup>Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa muda wa miaka arobaini.
<scripture passage="Acts 7:37" parsed="|Acts|7|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.37" />
<sup>37</sup>Mose ndiye aliyewaambia watu wa Israeli: `Mungu atawateulieni nabii kama mimi kutoka katika ndugu zenu ninyi wenyewe.`
<scripture passage="Acts 7:38" parsed="|Acts|7|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.38" />
<sup>38</sup>Wakati watu wa Israeli walipokutana pamoja kule jangwani, Mose ndiye aliyekuwako huko pamoja nao. Alikuwa huko pamoja na babu zetu na yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai; ndiye aliyekabidhiwa yale maneno yaletayo uzima atupe sisi.
<scripture passage="Acts 7:39" parsed="|Acts|7|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.39" />
<sup>39</sup>"Lakini yeye ndiye babu zetu waliyemkataa kumsikiliza; walimsukuma kando, wakatamani kurudi Misri.
<scripture passage="Acts 7:40" parsed="|Acts|7|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.40" />
<sup>40</sup>Walimwambia Aroni: `Tutengenezee miungu itakayotuongoza njiani, maana hatujui yaliyompata Mose huyu aliyetuongoza kutoka Misri!`
<scripture passage="Acts 7:41" parsed="|Acts|7|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.41" />
<sup>41</sup>Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
<scripture passage="Acts 7:42" parsed="|Acts|7|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.42" />
<sup>42</sup>Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: `Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea dhabihu na sadaka kwa muda wa miaka arobaini kule jangwani!
<scripture passage="Acts 7:43" parsed="|Acts|7|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.43" />
<sup>43</sup>Ninyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwa sababu hiyo nitakupeleka mateka mbali kupita Babuloni!`
<scripture passage="Acts 7:44" parsed="|Acts|7|44|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.44" />
<sup>44</sup>Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema lililoshuhudia kuweko kwa Mungu. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichoonyeshwa.
<scripture passage="Acts 7:45" parsed="|Acts|7|45|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.45" />
<sup>45</sup>Kisha babu zetu walilipokezana wao kwa wao mpaka wakati wa Yoshua, walipoinyakua ile nchi kutoka kwa mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao. Hapo lilikaa mpaka nyakati za Daudi.
<scripture passage="Acts 7:46" parsed="|Acts|7|46|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.46" />
<sup>46</sup>Daudi alipata upendeleo kwa Mungu, akamwomba Mungu ruhusa ya kumjengea makao yeye aliye Mungu wa Yakobo.
<scripture passage="Acts 7:47" parsed="|Acts|7|47|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.47" />
<sup>47</sup>Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba.
<scripture passage="Acts 7:48" parsed="|Acts|7|48|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.48" />
<sup>48</sup>"Hata hivyo, Mungu Mkuu haishi katika nyumba zilizojengwa na binadamu; kama nabii asemavyo:
<scripture passage="Acts 7:49" parsed="|Acts|7|49|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.49" />
<sup>49</sup>`Bwana asema: Mbingu ni kiti changu cha enzi na dunia ni kiti changu cha kuwekea miguu.
<scripture passage="Acts 7:50" parsed="|Acts|7|50|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.50" />
<sup>50</sup>Ni nyumba ya namna gani basi mnayoweza kunijengea, na ni mahali gani nitakapopumzika? Vitu hivi vyote ni mimi nimevifanya, au sivyo?`
<scripture passage="Acts 7:51" parsed="|Acts|7|51|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.51" />
<sup>51</sup>"Enyi wakaidi wakuu! Mioyo na masikio yenu ni kama ya watu wa mataifa. Ninyi ni kama baba zenu. Siku zote mnampinga Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Acts 7:52" parsed="|Acts|7|52|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.52" />
<sup>52</sup>Je, yuko nabii yeyote ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua hao Mungu aliowatuma watangaze kuja kwake yule Mwenye Haki. Na sasa, ninyi mmemsaliti, mkamuua.
<scripture passage="Acts 7:53" parsed="|Acts|7|53|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.53" />
<sup>53</sup>Ninyi mliipokea ile Sheria iliyoletwa kwenu na Malaika, lakini hamkuitii."
<scripture passage="Acts 7:54" parsed="|Acts|7|54|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.54" />
<sup>54</sup>Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana, wakamsagia meno kwa hasira.
<scripture passage="Acts 7:55" parsed="|Acts|7|55|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.55" />
<sup>55</sup>Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.
<scripture passage="Acts 7:56" parsed="|Acts|7|56|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.56" />
<sup>56</sup>Akasema, "Tazameni! Ninaona mbingu zimefunuliwa na Mwana wa Mtu amesimama upande wa kulia wa Mungu."
<scripture passage="Acts 7:57" parsed="|Acts|7|57|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.57" />
<sup>57</sup>Hapo, watu wote katika kile kikao cha Baraza, wakapiga kelele na kuziba masikio yao kwa mikono yao. Kisha wakamrukia wote kwa pamoja,
<scripture passage="Acts 7:58" parsed="|Acts|7|58|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.58" />
<sup>58</sup>wakamtoa nje ya mji, wakampiga mawe. Wale mashahidi wakayaweka makoti yao chini ya ulinzi wa kijana mmoja jina lake Saulo.
<scripture passage="Acts 7:59" parsed="|Acts|7|59|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.59" />
<sup>59</sup>Waliendelea kumpiga mawe Stefano, huku akiwa anasali: "Bwana Yesu, ipokee roho yangu!"
<scripture passage="Acts 7:60" parsed="|Acts|7|60|0|0" osisRef="Bible:Acts.7.60" />
<sup>60</sup>Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: "Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii." Baada ya kusema hivyo, akafa.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 8" progress="47.38%" prev="Acts.7" next="Acts.9" id="Acts.8">
<h3 id="Acts.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Acts.8-p1">
<scripture passage="Acts 8:1" parsed="|Acts|8|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.1" />
<sup>1</sup>Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa sawa. Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote, isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za mashambani za Yudea na Samaria.
<scripture passage="Acts 8:2" parsed="|Acts|8|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.2" />
<sup>2</sup>Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia maombolezo makubwa.
<scripture passage="Acts 8:3" parsed="|Acts|8|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.3" />
<sup>3</sup>Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia gerezani.
<scripture passage="Acts 8:4" parsed="|Acts|8|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.4" />
<sup>4</sup>Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe.
<scripture passage="Acts 8:5" parsed="|Acts|8|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.5" />
<sup>5</sup>Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa wenyeji wa hapo.
<scripture passage="Acts 8:6" parsed="|Acts|8|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.6" />
<sup>6</sup>Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
<scripture passage="Acts 8:7" parsed="|Acts|8|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.7" />
<sup>7</sup>Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na waliolemaa waliponywa.
<scripture passage="Acts 8:8" parsed="|Acts|8|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.8" />
<sup>8</sup>Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
<scripture passage="Acts 8:9" parsed="|Acts|8|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.9" />
<sup>9</sup>Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
<scripture passage="Acts 8:10" parsed="|Acts|8|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.10" />
<sup>10</sup>Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema, "Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa `Nguvu Kubwa."`
<scripture passage="Acts 8:11" parsed="|Acts|8|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.11" />
<sup>11</sup>Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake kwa muda mrefu.
<scripture passage="Acts 8:12" parsed="|Acts|8|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.12" />
<sup>12</sup>Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
<scripture passage="Acts 8:13" parsed="|Acts|8|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.13" />
<sup>13</sup>Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa akiandamana na Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.
<scripture passage="Acts 8:14" parsed="|Acts|8|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.14" />
<sup>14</sup>Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari kwamba wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro na Yohane.
<scripture passage="Acts 8:15" parsed="|Acts|8|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.15" />
<sup>15</sup>Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu;
<scripture passage="Acts 8:16" parsed="|Acts|8|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.16" />
<sup>16</sup>maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote kati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
<scripture passage="Acts 8:17" parsed="|Acts|8|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.17" />
<sup>17</sup>Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Acts 8:18" parsed="|Acts|8|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.18" />
<sup>18</sup>Hapo Simoni aling`amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
<scripture passage="Acts 8:19" parsed="|Acts|8|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.19" />
<sup>19</sup>"Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu."
<scripture passage="Acts 8:20" parsed="|Acts|8|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.20" />
<sup>20</sup>Lakini Petro akamjibu, "Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
<scripture passage="Acts 8:21" parsed="|Acts|8|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.21" />
<sup>21</sup>Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
<scripture passage="Acts 8:22" parsed="|Acts|8|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.22" />
<sup>22</sup>Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
<scripture passage="Acts 8:23" parsed="|Acts|8|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.23" />
<sup>23</sup>Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa dhambi!"
<scripture passage="Acts 8:24" parsed="|Acts|8|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.24" />
<sup>24</sup>Simoni akajibu, "Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema."
<scripture passage="Acts 8:25" parsed="|Acts|8|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.25" />
<sup>25</sup>Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
<scripture passage="Acts 8:26" parsed="|Acts|8|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.26" />
<sup>26</sup>Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, "Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza." (Njia hiyo hupita jangwani.)
<scripture passage="Acts 8:27" parsed="|Acts|8|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.27" />
<sup>27</sup>Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
<scripture passage="Acts 8:28" parsed="|Acts|8|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.28" />
<sup>28</sup>Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya.
<scripture passage="Acts 8:29" parsed="|Acts|8|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.29" />
<sup>29</sup>Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, "Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo."
<scripture passage="Acts 8:30" parsed="|Acts|8|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.30" />
<sup>30</sup>Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, "Je, unaelewa hayo unayosoma?"
<scripture passage="Acts 8:31" parsed="|Acts|8|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.31" />
<sup>31</sup>Huyo mtu akamjibu, "Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?" Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
<scripture passage="Acts 8:32" parsed="|Acts|8|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.32" />
<sup>32</sup>Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: "Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
<scripture passage="Acts 8:33" parsed="|Acts|8|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.33" />
<sup>33</sup>Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani."
<scripture passage="Acts 8:34" parsed="|Acts|8|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.34" />
<sup>34</sup>Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, "Niambie, huyu nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?"
<scripture passage="Acts 8:35" parsed="|Acts|8|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.35" />
<sup>35</sup>Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
<scripture passage="Acts 8:36" parsed="|Acts|8|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.36" />
<sup>36</sup>Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji na huyo ofisa akasema, "Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe?"<i>fa</i>
<scripture passage="Acts 8:37" parsed="|Acts|8|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.37" />
<sup>37</sup>missing
<scripture passage="Acts 8:38" parsed="|Acts|8|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.38" />
<sup>38</sup>Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
<scripture passage="Acts 8:39" parsed="|Acts|8|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.39" />
<sup>39</sup>Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.
<scripture passage="Acts 8:40" parsed="|Acts|8|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.8.40" />
<sup>40</sup>Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea. kubatizwa." Naye akajibu, "Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu."
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 9" progress="47.90%" prev="Acts.8" next="Acts.10" id="Acts.9">
<h3 id="Acts.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Acts.9-p1">
<scripture passage="Acts 9:1" parsed="|Acts|9|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.1" />
<sup>1</sup>Wakati huo Saulo alikuwa akizidisha vitisho vikali vya kuwaua wafuasi wa Bwana. Alikwenda kwa Kuhani Mkuu,
<scripture passage="Acts 9:2" parsed="|Acts|9|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.2" />
<sup>2</sup>akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia ya Bwana, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 9:3" parsed="|Acts|9|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.3" />
<sup>3</sup>Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote.
<scripture passage="Acts 9:4" parsed="|Acts|9|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.4" />
<sup>4</sup>Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: "Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?"
<scripture passage="Acts 9:5" parsed="|Acts|9|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.5" />
<sup>5</sup>Naye Saulo akauliza, "Ni nani wewe Bwana?" Na ile sauti ikajibu, "Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
<scripture passage="Acts 9:6" parsed="|Acts|9|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.6" />
<sup>6</sup>Lakini simama sasa, uingie mjini na huko utaambiwa unachopaswa kufanya."
<scripture passage="Acts 9:7" parsed="|Acts|9|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.7" />
<sup>7</sup>Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja na Saulo walisimama pale, wakiwa hawana la kusema; walisikia ile sauti lakini hawakumwona mtu.
<scripture passage="Acts 9:8" parsed="|Acts|9|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.8" />
<sup>8</sup>Saulo aliinuka, na alipofumbua macho yake hakuweza kuona chochote; hivyo wale watu wakamwongoza kwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko.
<scripture passage="Acts 9:9" parsed="|Acts|9|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.9" />
<sup>9</sup>Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakati huo hakula au kunywa chochote.
<scripture passage="Acts 9:10" parsed="|Acts|9|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.10" />
<sup>10</sup>Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, "Anania!" Anania akaitika, "Niko hapa, Bwana."
<scripture passage="Acts 9:11" parsed="|Acts|9|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.11" />
<sup>11</sup>Naye Bwana akamwambia, "Jitayarishe uende kwenye barabara inayoitwa Barabara ya Moja kwa Moja, na katika nyumba ya Yuda umtake mtu mmoja kutoka Tarso aitwaye Saulo. Sasa anasali;
<scripture passage="Acts 9:12" parsed="|Acts|9|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.12" />
<sup>12</sup>na katika maono ameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani na kumwekea mikono ili apate kuona tena."
<scripture passage="Acts 9:13" parsed="|Acts|9|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.13" />
<sup>13</sup>Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kutoka kwa watu wengi; nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watu wako huko Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 9:14" parsed="|Acts|9|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.14" />
<sup>14</sup>Na amekuja hapa akiwa na mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwa jina lako."
<scripture passage="Acts 9:15" parsed="|Acts|9|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.15" />
<sup>15</sup>Lakini Bwana akamwambia, "Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.
<scripture passage="Acts 9:16" parsed="|Acts|9|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.16" />
<sup>16</sup>Mimi mwenyewe nitamwonyesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu."
<scripture passage="Acts 9:17" parsed="|Acts|9|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.17" />
<sup>17</sup>Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikono yake juu ya Saulo, akasema, "Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu."
<scripture passage="Acts 9:18" parsed="|Acts|9|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.18" />
<sup>18</sup>Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka macho ya Saulo, akaweza kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
<scripture passage="Acts 9:19" parsed="|Acts|9|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.19" />
<sup>19</sup>Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia. Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko.
<scripture passage="Acts 9:20" parsed="|Acts|9|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.20" />
<sup>20</sup>Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
<scripture passage="Acts 9:21" parsed="|Acts|9|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.21" />
<sup>21</sup>Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, "Je, mtu huyu si yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu hao na kuwapeleka kwa makuhani!"
<scripture passage="Acts 9:22" parsed="|Acts|9|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.22" />
<sup>22</sup>Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa.
<scripture passage="Acts 9:23" parsed="|Acts|9|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.23" />
<sup>23</sup>Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi walikusanyika na kufanya mpango wa kumwua Saulo.
<scripture passage="Acts 9:24" parsed="|Acts|9|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.24" />
<sup>24</sup>Lakini Saulo alipata habari ya mpango huo. Usiku na mchana walilinda milango ya kuingia mjini ili wapate kumwua.
<scripture passage="Acts 9:25" parsed="|Acts|9|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.25" />
<sup>25</sup>Lakini wakati wa usiku wanafunzi wake walimchukua, wakamteremsha chini ndani ya kapu kubwa kwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani. ic
<scripture passage="Acts 9:26" parsed="|Acts|9|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.26" />
<sup>26</sup>Saulo alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na wale wanafunzi. Lakini wote walimwogopa, na hawakuweza kuamini kwamba yeye amekuwa mfuasi.
<scripture passage="Acts 9:27" parsed="|Acts|9|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.27" />
<sup>27</sup>Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila uoga kule Damasko.
<scripture passage="Acts 9:28" parsed="|Acts|9|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.28" />
<sup>28</sup>Basi, Saulo alikaa pamoja nao, akatembelea Yerusalemu yote akihubiri neno la Bwana bila hofu.
<scripture passage="Acts 9:29" parsed="|Acts|9|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.29" />
<sup>29</sup>Pia aliongea na kubishana na Wayahudi wasemao Kigiriki, lakini wao walijaribu kumwua.
<scripture passage="Acts 9:30" parsed="|Acts|9|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.30" />
<sup>30</sup>Wale ndugu walipogundua jambo hilo walimchukua Saulo, wakampeleka Kaisarea, wakamwacha aende zake Tarso.
<scripture passage="Acts 9:31" parsed="|Acts|9|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.31" />
<sup>31</sup>Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Acts 9:32" parsed="|Acts|9|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.32" />
<sup>32</sup>Petro alipokuwa anasafirisafiri kila mahali alifika pia kwa watu wa Mungu waliokuwa wanaishi Luda.
<scripture passage="Acts 9:33" parsed="|Acts|9|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.33" />
<sup>33</sup>Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Enea ambaye kwa muda wa miaka minane alikuwa amelala kitandani kwa sababu alikuwa amepooza.
<scripture passage="Acts 9:34" parsed="|Acts|9|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.34" />
<sup>34</sup>Basi, Petro akamwambia, "Enea, Yesu Kristo anakuponya. Amka utandike kitanda chako." Enea akaamka mara.
<scripture passage="Acts 9:35" parsed="|Acts|9|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.35" />
<sup>35</sup>Wakazi wote wa Luda na Saroni walimwona Enea, na wote wakamgeukia Bwana.
<scripture passage="Acts 9:36" parsed="|Acts|9|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.36" />
<sup>36</sup>Kulikuwa na mfuasi mmoja mwanamke mjini Yopa aitwaye Tabitha (kwa Kigiriki ni Dorka, maana yake, Paa). Huyo mwanamke alikuwa akitenda mema na kuwasaidia maskini daima.
<scripture passage="Acts 9:37" parsed="|Acts|9|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.37" />
<sup>37</sup>Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakauzika katika chumba ghorofani.
<scripture passage="Acts 9:38" parsed="|Acts|9|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.38" />
<sup>38</sup>Yopa si mbali sana na Luda; kwa hiyo wafuasi waliposikia kwamba Petro alikuwa Luda, wakawatuma watu wawili kwake na ujumbe: "Njoo kwetu haraka iwezekanavyo."
<scripture passage="Acts 9:39" parsed="|Acts|9|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.39" />
<sup>39</sup>Basi, Petro akaenda pamoja nao. Alipofika alipelekwa ghorofani katika kile chumba. Huko wajane wengi walimzunguka Petro wakilia na kumwonyesha makoti na nguo ambazo Dorka alikuwa akitengeneza wakati alipokuwa hai.
<scripture passage="Acts 9:40" parsed="|Acts|9|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.40" />
<sup>40</sup>Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akamgeukia yule maiti, akasema, "Tabitha, amka" Naye akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.
<scripture passage="Acts 9:41" parsed="|Acts|9|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.41" />
<sup>41</sup>Petro akamsaidia kusimama, halafu akawaita wale watu wa Mungu na wale wajane, akamkabidhi kwao akiwa mzima.
<scripture passage="Acts 9:42" parsed="|Acts|9|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.42" />
<sup>42</sup>Habari ya tukio hili ilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi wakamwamini Bwana.
<scripture passage="Acts 9:43" parsed="|Acts|9|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.9.43" />
<sup>43</sup>Petro alikaa siku kadhaa huko Yopa, akiishi kwa mtu mmoja mtengenezaji wa ngozi aitwaye Simoni.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 10" progress="48.48%" prev="Acts.9" next="Acts.11" id="Acts.10">
<h3 id="Acts.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Acts.10-p1">
<scripture passage="Acts 10:1" parsed="|Acts|10|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.1" />
<sup>1</sup>Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, Jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho "Kikosi cha Italia."
<scripture passage="Acts 10:2" parsed="|Acts|10|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.2" />
<sup>2</sup>Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
<scripture passage="Acts 10:3" parsed="|Acts|10|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.3" />
<sup>3</sup>Yapata saa tisa mchana, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, "Kornelio!"
<scripture passage="Acts 10:4" parsed="|Acts|10|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.4" />
<sup>4</sup>Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, "Kuna nini Mheshimiwa?" Huyo malaika akamwambia, "Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini.
<scripture passage="Acts 10:5" parsed="|Acts|10|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.5" />
<sup>5</sup>Sasa, watume watu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.
<scripture passage="Acts 10:6" parsed="|Acts|10|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.6" />
<sup>6</sup>Yeye yumo nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi ambaye nyumba yake iko karibu na bahari."
<scripture passage="Acts 10:7" parsed="|Acts|10|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.7" />
<sup>7</sup>Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
<scripture passage="Acts 10:8" parsed="|Acts|10|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.8" />
<sup>8</sup>akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.
<scripture passage="Acts 10:9" parsed="|Acts|10|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.9" />
<sup>9</sup>Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana ili kusali.
<scripture passage="Acts 10:10" parsed="|Acts|10|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.10" />
<sup>10</sup>Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, alipatwa na usingizi mzito akaona maono.
<scripture passage="Acts 10:11" parsed="|Acts|10|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.11" />
<sup>11</sup>Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.
<scripture passage="Acts 10:12" parsed="|Acts|10|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.12" />
<sup>12</sup>Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: wanyama wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani.
<scripture passage="Acts 10:13" parsed="|Acts|10|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.13" />
<sup>13</sup>Akasikia sauti ikimwambia: "Petro, amka uchinje, ule!"
<scripture passage="Acts 10:14" parsed="|Acts|10|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.14" />
<sup>14</sup>Petro akajibu, "La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu."
<scripture passage="Acts 10:15" parsed="|Acts|10|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.15" />
<sup>15</sup>Ile sauti ikasikika tena ikimwambia: "Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa!"
<scripture passage="Acts 10:16" parsed="|Acts|10|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.16" />
<sup>16</sup>Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni.
<scripture passage="Acts 10:17" parsed="|Acts|10|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.17" />
<sup>17</sup>Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hilo maono alilokuwa ameliona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
<scripture passage="Acts 10:18" parsed="|Acts|10|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.18" />
<sup>18</sup>Wakaita kwa sauti: "Je, kuna mgeni humu aitwaye Simoni Petro?"
<scripture passage="Acts 10:19" parsed="|Acts|10|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.19" />
<sup>19</sup>Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa lile maono, na hapo Roho akamwambia, "Sikiliza! kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.
<scripture passage="Acts 10:20" parsed="|Acts|10|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.20" />
<sup>20</sup>Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma."
<scripture passage="Acts 10:21" parsed="|Acts|10|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.21" />
<sup>21</sup>Basi, Petro akateremka chini, akawaambia hao watu, "Mimi ndiye mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?"
<scripture passage="Acts 10:22" parsed="|Acts|10|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.22" />
<sup>22</sup>Wao wakamjibu, "Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema."
<scripture passage="Acts 10:23" parsed="|Acts|10|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.23" />
<sup>23</sup>Petro akawaalika ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.
<scripture passage="Acts 10:24" parsed="|Acts|10|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.24" />
<sup>24</sup>Siku ya pili yake, walifika Kaisarea na huko Kornelio alikuwa anawangojea pamoja na jamaa na marafiki aliokuwa amewaalika.
<scripture passage="Acts 10:25" parsed="|Acts|10|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.25" />
<sup>25</sup>Petro alipokuwa anaingia, Kornelio alitoka nje kumlaki, akapiga magoti mbele yake na kuinama chini kabisa.
<scripture passage="Acts 10:26" parsed="|Acts|10|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.26" />
<sup>26</sup>Lakini Petro alimwinua, akamwambia, "Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu."
<scripture passage="Acts 10:27" parsed="|Acts|10|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.27" />
<sup>27</sup>Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika.
<scripture passage="Acts 10:28" parsed="|Acts|10|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.28" />
<sup>28</sup>Petro akawaambia, "Ninyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na Sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu.
<scripture passage="Acts 10:29" parsed="|Acts|10|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.29" />
<sup>29</sup>Kwa sababu hiyo, mliponiita nimekuja bila kusita. Basi, nawaulizeni: kwa nini mmeniita?"
<scripture passage="Acts 10:30" parsed="|Acts|10|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.30" />
<sup>30</sup>Kornelio akasema, "Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kun`gaa alisimama mbele yangu,
<scripture passage="Acts 10:31" parsed="|Acts|10|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.31" />
<sup>31</sup>akasema: `Kornelio! Sala yako na sadaka zako kwa maskini vimekubaliwa na Mungu.
<scripture passage="Acts 10:32" parsed="|Acts|10|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.32" />
<sup>32</sup>Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petroi; yuko nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi karibu na bahari.`
<scripture passage="Acts 10:33" parsed="|Acts|10|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.33" />
<sup>33</sup>Kwa hiyo nilikutumia ujumbe bila kuchelewa, nawe umefanya vyema kuja. Sasa, sisi tuko mbele ya Mungu, kusikiliza chochote ambacho bwana amekuamuru kusema."
<scripture passage="Acts 10:34" parsed="|Acts|10|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.34" />
<sup>34</sup>Hapo Petro akaanza kusema: "Sasa nimetambua kwamba hakika Mungu hana ubaguzi.
<scripture passage="Acts 10:35" parsed="|Acts|10|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.35" />
<sup>35</sup>Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda haki anapokelewa naye.
<scripture passage="Acts 10:36" parsed="|Acts|10|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.36" />
<sup>36</sup>Huu ndio ule ujumbe Mungu alioupeleka kwa watu wa Israeli, akitangaza Habari Njema iletayo amani kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote.
<scripture passage="Acts 10:37" parsed="|Acts|10|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.37" />
<sup>37</sup>Ninyi mnajua jambo lililotukia katika nchi yote ya Wayahudi kuanzia Galilaya baada ya ule ubatizo aliohubiri Yohane.
<scripture passage="Acts 10:38" parsed="|Acts|10|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.38" />
<sup>38</sup>Mnajua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi.
<scripture passage="Acts 10:39" parsed="|Acts|10|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.39" />
<sup>39</sup>Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
<scripture passage="Acts 10:40" parsed="|Acts|10|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.40" />
<sup>40</sup>lakini Mungu alimfufua siku ya tatu, akamfanya aonekane
<scripture passage="Acts 10:41" parsed="|Acts|10|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.41" />
<sup>41</sup>si kwa watu wote ila kwa wale Mungu aliokwisha wachagua wawe mashahidi wake, yaani sisi tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka wafu.
<scripture passage="Acts 10:42" parsed="|Acts|10|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.42" />
<sup>42</sup>Alituamuru kuihubiri Habari Njema kwa watu wote na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa na Mungu awe Mwamuzi wa wazima na wafu.
<scripture passage="Acts 10:43" parsed="|Acts|10|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.43" />
<sup>43</sup>Manabii wote waliongea juu yake kwamba kila mtu atakayemwamini atasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake."
<scripture passage="Acts 10:44" parsed="|Acts|10|44|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.44" />
<sup>44</sup>Wakati Petro alipokuwa bado anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wanasikiliza ujumbe huo.
<scripture passage="Acts 10:45" parsed="|Acts|10|45|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.45" />
<sup>45</sup>Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia zawadi ya Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
<scripture passage="Acts 10:46" parsed="|Acts|10|46|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.46" />
<sup>46</sup>maana waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali wakimtukuza Mungu. Hapo Petro akasema,
<scripture passage="Acts 10:47" parsed="|Acts|10|47|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.47" />
<sup>47</sup>"Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi wenyewe tulivyompokea. Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuia wasibatizwe kwa maji?"
<scripture passage="Acts 10:48" parsed="|Acts|10|48|0|0" osisRef="Bible:Acts.10.48" />
<sup>48</sup>Basi, akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Kisha wakamwomba akae nao kwa siku chache.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 11" progress="49.08%" prev="Acts.10" next="Acts.12" id="Acts.11">
<h3 id="Acts.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Acts.11-p1">
<scripture passage="Acts 11:1" parsed="|Acts|11|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.1" />
<sup>1</sup>Mitume na ndugu kule Yudea walisikia kwamba watu wa mataifa mengine pia walikuwa wamelipokea neno la Mungu.
<scripture passage="Acts 11:2" parsed="|Acts|11|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.2" />
<sup>2</sup>Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:
<scripture passage="Acts 11:3" parsed="|Acts|11|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.3" />
<sup>3</sup>"Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao!
<scripture passage="Acts 11:4" parsed="|Acts|11|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.4" />
<sup>4</sup>Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu mwanzo:
<scripture passage="Acts 11:5" parsed="|Acts|11|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.5" />
<sup>5</sup>"Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa likishushwa chini kutoka mbinguni likiwa limeshikwa pembe zake nne, likawekwa kando yangu.
<scripture passage="Acts 11:6" parsed="|Acts|11|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.6" />
<sup>6</sup>Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
<scripture passage="Acts 11:7" parsed="|Acts|11|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.7" />
<sup>7</sup>Kisha nikasikia sauti ikiniambia: `Petro amka, chinja, ule.`
<scripture passage="Acts 11:8" parsed="|Acts|11|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.8" />
<sup>8</sup>Lakini mimi nikasema: `La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.`
<scripture passage="Acts 11:9" parsed="|Acts|11|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.9" />
<sup>9</sup>Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: `Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.`
<scripture passage="Acts 11:10" parsed="|Acts|11|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.10" />
<sup>10</sup>Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni.
<scripture passage="Acts 11:11" parsed="|Acts|11|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.11" />
<sup>11</sup>Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea waliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.
<scripture passage="Acts 11:12" parsed="|Acts|11|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.12" />
<sup>12</sup>Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.
<scripture passage="Acts 11:13" parsed="|Acts|11|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.13" />
<sup>13</sup>Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama nyumbani mwake na kumwambia: `Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.
<scripture passage="Acts 11:14" parsed="|Acts|11|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.14" />
<sup>14</sup>Yeye atakuambia maneno ambayo kwayo wewe na jamaa yako yote mtaokolewa.`
<scripture passage="Acts 11:15" parsed="|Acts|11|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.15" />
<sup>15</sup>Na nilipoanza tu kuongea, Roho Mtakatifu aliwashukia kama alivyotushukia sisi pale awali.
<scripture passage="Acts 11:16" parsed="|Acts|11|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.16" />
<sup>16</sup>Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: `Yohane alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.`
<scripture passage="Acts 11:17" parsed="|Acts|11|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.17" />
<sup>17</sup>Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine zawadi ileile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?"
<scripture passage="Acts 11:18" parsed="|Acts|11|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.18" />
<sup>18</sup>Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, "Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na uzima!"
<scripture passage="Acts 11:19" parsed="|Acts|11|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.19" />
<sup>19</sup>Kutokana na mateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa, waumini walitawanyika. Wengine walikwenda mpaka Foinike, Kupro na Antiokia wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu.
<scripture passage="Acts 11:20" parsed="|Acts|11|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.20" />
<sup>20</sup>Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria ile Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
<scripture passage="Acts 11:21" parsed="|Acts|11|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.21" />
<sup>21</sup>Bwana aliwasaidia na idadi kubwa ya watu iliamini na kumgeukia Bwana.
<scripture passage="Acts 11:22" parsed="|Acts|11|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.22" />
<sup>22</sup>Habari ya jambo hilo ikasikika kwa lile kanisa la Yerusalemu. Hivyo wakamtuma Barnaba aende Antiokia.
<scripture passage="Acts 11:23" parsed="|Acts|11|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.23" />
<sup>23</sup>Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
<scripture passage="Acts 11:24" parsed="|Acts|11|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.24" />
<sup>24</sup>Barnaba alikuwa mtu mwema na mwenye kujaa Roho Mtakatifu na imani. Kundi kubwa la watu lilivutwa kwa Bwana.
<scripture passage="Acts 11:25" parsed="|Acts|11|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.25" />
<sup>25</sup>Kisha, Barnaba alikwenda Tarso kumtafuta Saulo
<scripture passage="Acts 11:26" parsed="|Acts|11|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.26" />
<sup>26</sup>Alipompata, alimleta Antiokia. Nao wote wawili walikaa na lile kanisa kwa mwaka wote mzima wakifundisha kundi kubwa la watu. Huko Antiokia, ndiko, kwa mara ya kwanza, wafuasi waliitwa Wakristo. ic
<scripture passage="Acts 11:27" parsed="|Acts|11|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.27" />
<sup>27</sup>Wakati huohuo, manabii kadhaa walikuja Antiokia kutoka Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 11:28" parsed="|Acts|11|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.28" />
<sup>28</sup>Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).
<scripture passage="Acts 11:29" parsed="|Acts|11|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.29" />
<sup>29</sup>Wale wanafunzi waliamua kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake apeleke chochote ili kuwasaidia wale ndugu waliokuwa wanaishi Yudea.
<scripture passage="Acts 11:30" parsed="|Acts|11|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.11.30" />
<sup>30</sup>Basi, wakafanya hivyo na kupeleka mchango wao kwa wazee wa kanisa kwa mikono ya Barnaba na Saulo.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 12" progress="49.45%" prev="Acts.11" next="Acts.13" id="Acts.12">
<h3 id="Acts.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Acts.12-p1">
<scripture passage="Acts 12:1" parsed="|Acts|12|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.1" />
<sup>1</sup>Karibu wakati huohuo, mfalme Herode alianza kuwatesa baadhi ya Wakristo.
<scripture passage="Acts 12:2" parsed="|Acts|12|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.2" />
<sup>2</sup>Alimwua kwa upanga Yakobo ndugu yake Yohane.
<scripture passage="Acts 12:3" parsed="|Acts|12|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.3" />
<sup>3</sup>Alipoona kuwa kitendo hiki kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu.)
<scripture passage="Acts 12:4" parsed="|Acts|12|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.4" />
<sup>4</sup>Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
<scripture passage="Acts 12:5" parsed="|Acts|12|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.5" />
<sup>5</sup>Basi, Petro alipokuwa gerezani, kanisa lilikuwa linamwombea kwa Mungu kwa moyo.
<scripture passage="Acts 12:6" parsed="|Acts|12|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.6" />
<sup>6</sup>Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
<scripture passage="Acts 12:7" parsed="|Acts|12|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.7" />
<sup>7</sup>Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa akisema, "Amka upesi!" Mara ile minyororo ikaanguka kutoka katika mikono yake.
<scripture passage="Acts 12:8" parsed="|Acts|12|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.8" />
<sup>8</sup>Malaika akamwambia, "Jifunge mshipi wako, vaa viatu vyako." Akafanya hivyo. Kisha huyo malaika akamwambia, "Vaa koti lako, unifuate."
<scripture passage="Acts 12:9" parsed="|Acts|12|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.9" />
<sup>9</sup>Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
<scripture passage="Acts 12:10" parsed="|Acts|12|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.10" />
<sup>10</sup>Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
<scripture passage="Acts 12:11" parsed="|Acts|12|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.11" />
<sup>11</sup>Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, "Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa kutoka katika mkono wa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia."
<scripture passage="Acts 12:12" parsed="|Acts|12|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.12" />
<sup>12</sup>Alipotambua hivyo alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Maria mama yake Yohane aitwaye Marko. Humo watu wengi walikuwa wamekusanyika wakisali.
<scripture passage="Acts 12:13" parsed="|Acts|12|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.13" />
<sup>13</sup>Petro alibisha mlango wa nje na mtumishi mmoja msichana aitwaye Roda, akaenda mlangoni kuitikia.
<scripture passage="Acts 12:14" parsed="|Acts|12|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.14" />
<sup>14</sup>Huyo msichana aliitambua sauti ya Petro akafurahi mno, hata badala ya kuufungua ule mlango, akakimbilia ndani na kuwaambia kwamba Petro alikuwa amesimama nje mlangoni.
<scripture passage="Acts 12:15" parsed="|Acts|12|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.15" />
<sup>15</sup>Wakamwambia yule msichana, "Una wazimu!" Lakini yeye akasisitiza kwamba ilikuwa kweli. Nao wakamwambia, "Huyo ni malaika wake."
<scripture passage="Acts 12:16" parsed="|Acts|12|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.16" />
<sup>16</sup>Wakati huo Petro alikuwa anaendelea kupiga hodi. Mwishowe walifungua mlango, wakamwona, wakashangaa.
<scripture passage="Acts 12:17" parsed="|Acts|12|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.17" />
<sup>17</sup>Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
<scripture passage="Acts 12:18" parsed="|Acts|12|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.18" />
<sup>18</sup>Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
<scripture passage="Acts 12:19" parsed="|Acts|12|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.19" />
<sup>19</sup>Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea akaenda Kaisarea ambako alikaa.
<scripture passage="Acts 12:20" parsed="|Acts|12|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.20" />
<sup>20</sup>Herode alikasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Lakini wao walimpelekea wajumbe. Nao wakafaulu kwanza kumpata Blasto awe upande wao. Blasto alikuwa msimamizi mkuu wa ikulu ya mfalme. Kisha, wakamwendea Herode wakamwomba kuwe na amani, kwa maana nchi yao ilitegemea nchi ya mfalme kwa chakula.
<scripture passage="Acts 12:21" parsed="|Acts|12|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.21" />
<sup>21</sup>Siku moja iliyochaguliwa, Herode akiwa amevaa mavazi rasmi na kuketi katika kiti cha kifalme aliwahutubia watu.
<scripture passage="Acts 12:22" parsed="|Acts|12|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.22" />
<sup>22</sup>Wale watu walimpigia kelele za shangwe wakisema, "Hii ni sauti ya mungu, si ya mtu."
<scripture passage="Acts 12:23" parsed="|Acts|12|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.23" />
<sup>23</sup>Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
<scripture passage="Acts 12:24" parsed="|Acts|12|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.24" />
<sup>24</sup>Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua.
<scripture passage="Acts 12:25" parsed="|Acts|12|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.12.25" />
<sup>25</sup>Baada ya Barnaba na Saulo kutekeleza shughuli zao, walitoka tena Yerusalemu wakamchukua Yohane aitwaye pia Marko.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 13" progress="49.82%" prev="Acts.12" next="Acts.14" id="Acts.13">
<h3 id="Acts.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Acts.13-p1">
<scripture passage="Acts 13:1" parsed="|Acts|13|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.1" />
<sup>1</sup>Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.
<scripture passage="Acts 13:2" parsed="|Acts|13|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.2" />
<sup>2</sup>Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: "Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia."
<scripture passage="Acts 13:3" parsed="|Acts|13|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.3" />
<sup>3</sup>Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.
<scripture passage="Acts 13:4" parsed="|Acts|13|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.4" />
<sup>4</sup>Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
<scripture passage="Acts 13:5" parsed="|Acts|13|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.5" />
<sup>5</sup>Walipofika Salami walihubiri neno la Mungu katika masunagogi ya Kiyahudi. Yohane (Marko) alikuwa msaidizi wao.
<scripture passage="Acts 13:6" parsed="|Acts|13|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.6" />
<sup>6</sup>Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo upande wa pili, na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambaye alijisingizia kuwa nabii.
<scripture passage="Acts 13:7" parsed="|Acts|13|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.7" />
<sup>7</sup>Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili asikie neno la Mungu.
<scripture passage="Acts 13:8" parsed="|Acts|13|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.8" />
<sup>8</sup>Lakini huyo mchawi Elima (kama alivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki), alijaribu kuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwa asije akaigeukia imani ya Kikristo.
<scripture passage="Acts 13:9" parsed="|Acts|13|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.9" />
<sup>9</sup>Basi, Saulo ambaye aliitwa pia Paulo, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alimkodolea macho huyo mchawi,
<scripture passage="Acts 13:10" parsed="|Acts|13|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.10" />
<sup>10</sup>akasema, "Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.
<scripture passage="Acts 13:11" parsed="|Acts|13|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.11" />
<sup>11</sup>Sasa, mkono wa Bwana utakuadhibu: utakuwa kipofu na hutaweza kuuona mwanga wa jua kwa kitambo." Mara kila kitu kikawa kama ukungu na giza kwake, akaanza kwenda huku na huku akitafuta mtu wa kumshika mkono amwongoze.
<scripture passage="Acts 13:12" parsed="|Acts|13|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.12" />
<sup>12</sup>Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa muumini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
<scripture passage="Acts 13:13" parsed="|Acts|13|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.13" />
<sup>13</sup>Kutoka Pafo, Paulo na wenzake walipanda meli wakaenda hadi Perga katika Pamfulia; lakini Yohane (Marko) aliwaacha, akarudi Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 13:14" parsed="|Acts|13|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.14" />
<sup>14</sup>Lakini wao waliendelea na safari toka Pisga hadi mjini Antiokia Pisidia. Siku ya Sabato waliingia ndani ya Sunagogi, wakakaa.
<scripture passage="Acts 13:15" parsed="|Acts|13|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.15" />
<sup>15</sup>Baada ya masomo katika kitabu cha Sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: "Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni."
<scripture passage="Acts 13:16" parsed="|Acts|13|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.16" />
<sup>16</sup>Basi, Paulo alisimama, akatoa ishara kwa mkono, akaanza kuongea: "Wananchi wa Israeli na wengine wote mnaomcha Mungu, sikilizeni!
<scripture passage="Acts 13:17" parsed="|Acts|13|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.17" />
<sup>17</sup>Mungu wa taifa hili la Israeli aliwateua babu zetu na kuwafanya wawe taifa kubwa walipokuwa ugenini kule Misri. Mungu aliwatoa huko kwa uwezo wake mkuu.
<scripture passage="Acts 13:18" parsed="|Acts|13|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.18" />
<sup>18</sup>Aliwavumilia kwa muda wa miaka arobaini kule jangwani.
<scripture passage="Acts 13:19" parsed="|Acts|13|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.19" />
<sup>19</sup>Aliyaangamiza mataifa ya nchi ya Kanaani akawapa hao watu wake ile nchi kuwa mali yao.
<scripture passage="Acts 13:20" parsed="|Acts|13|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.20" />
<sup>20</sup>Miaka mia nne na hamsini ilipita, halafu akawapatia waamuzi wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samweli.
<scripture passage="Acts 13:21" parsed="|Acts|13|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.21" />
<sup>21</sup>Hapo wakapendelea kuwa na mfalme, na Mungu akawapa Saulo, mtoto wa Kishi wa kabila la Benyamini, awe mfalme wao kwa muda wa miaka arobaini.
<scripture passage="Acts 13:22" parsed="|Acts|13|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.22" />
<sup>22</sup>Baada ya kumwondoa Saulo, Mungu alimteua Daudi kuwa mfalme wao. Mungu alionyesha kibali chake kwake akisema: `Nimemwona Daudi mtoto wa Yese; ni mtu anayepatana na moyo wangu; mtu ambaye atatimiza yale yote ninayotaka kuyatenda.`
<scripture passage="Acts 13:23" parsed="|Acts|13|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.23" />
<sup>23</sup>Kutokana na ukoo wake mtu huyu, Mungu, kama alivyoahidi, amewapelekea watu wa Israeli Mwokozi, ndiye Yesu.
<scripture passage="Acts 13:24" parsed="|Acts|13|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.24" />
<sup>24</sup>Kabla ya kuja kwake Yesu, Yohane alimtangulia akiwahubiria watu wote wa Israeli kwamba ni lazima watubu na kubatizwa.
<scripture passage="Acts 13:25" parsed="|Acts|13|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.25" />
<sup>25</sup>Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: `Mnadhani mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.`
<scripture passage="Acts 13:26" parsed="|Acts|13|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.26" />
<sup>26</sup>"Ndugu, ninyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
<scripture passage="Acts 13:27" parsed="|Acts|13|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.27" />
<sup>27</sup>Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye kuwa Mwokozi. Wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu Yesu adhabu ya kifo.
<scripture passage="Acts 13:28" parsed="|Acts|13|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.28" />
<sup>28</sup>Ingawa hawakumpata na hatia inayostahili auawe, walimwomba Pilato amhukumu auawe.
<scripture passage="Acts 13:29" parsed="|Acts|13|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.29" />
<sup>29</sup>Na baada ya kutekeleza yote yaliyokuwa yameandikwa kumhusu yeye, walimshusha kutoka msalabani, wakamweka kaburini.
<scripture passage="Acts 13:30" parsed="|Acts|13|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.30" />
<sup>30</sup>Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu.
<scripture passage="Acts 13:31" parsed="|Acts|13|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.31" />
<sup>31</sup>Naye, kwa siku nyingi aliwatokea wale waliofuatana naye kutoka Galilaya mpaka Yerusalemu. Hao ndio walio sasa mashahidi wake kwa watu wa Israeli.
<scripture passage="Acts 13:32" parsed="|Acts|13|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.32" />
<sup>32</sup>Sisi tumekuja hapa kuwaleteeni Habari Njema: jambo lile Mungu alilowaahidia babu zetu amelitimiza sasa kwa ajili yetu sisi tulio wajukuu wao kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Kama ilivyoandikwa katika zaburi ya pili: `Wewe ni Mwanangu, mimi leo nimekuwa baba yako.`
<scripture passage="Acts 13:33" parsed="|Acts|13|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.33" />
<sup>33</sup>[]
<scripture passage="Acts 13:34" parsed="|Acts|13|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.34" />
<sup>34</sup>Na juu ya kumfufua kutoka wafu, asipate tena kurudi huko na kuoza, Mungu alisema hivi: `Nitakupa baraka takatifu na za kweli nilizomwahidia Daudi.`
<scripture passage="Acts 13:35" parsed="|Acts|13|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.35" />
<sup>35</sup>Naam, na katika sehemu nyingine za zaburi asema: `Hutamwacha Mtakatifu wako aoze.`
<scripture passage="Acts 13:36" parsed="|Acts|13|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.36" />
<sup>36</sup>Sasa, Daudi mwenyewe alitimiza mapenzi ya Mungu wakati wake; kisha akafa na kuzikwa karibu na wazee wake, na mwili wake ukaoza.
<scripture passage="Acts 13:37" parsed="|Acts|13|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.37" />
<sup>37</sup>Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka wafu hakupata kuoza.
<scripture passage="Acts 13:38" parsed="|Acts|13|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.38" />
<sup>38</sup>Jueni wazi, ndugu zangu, kwamba ujumbe kuhusu kusamehewa dhambi unahubiriwa kwenu kwa njia ya Yesu Kristo; na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo halingewezekana kwa njia ya Sheria ya Mose.
<scripture passage="Acts 13:39" parsed="|Acts|13|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.39" />
<sup>39</sup>[]
<scripture passage="Acts 13:40" parsed="|Acts|13|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.40" />
<sup>40</sup>Jihadharini basi, msije mkapatwa na yale yaliyosemwa na manabii:
<scripture passage="Acts 13:41" parsed="|Acts|13|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.41" />
<sup>41</sup>`Sikilizeni enyi wenye madharau, shangaeni mpotee! Kwa maana kitu ninachofanya sasa, nyakati zenu, ni kitu ambacho hamtakiamini hata kama mtu akiwaelezeni."`
<scripture passage="Acts 13:42" parsed="|Acts|13|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.42" />
<sup>42</sup>Paulo na Barnaba walipokuwa wanatoka katika ile sunagogi, wale watu waliwaalika waje tena siku ya Sabato iliyofuata, waongee zaidi juu ya mambo hayo.
<scripture passage="Acts 13:43" parsed="|Acts|13|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.43" />
<sup>43</sup>Mkutano huo ulipomalizika, Wayahudi wengi na watu wa mataifa mengine waliokuwa wameongokea dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Barnaba. Hao mitume waliongea nao, wakawatia moyo waendelee kuishi wakitegemea neema ya Mungu.
<scripture passage="Acts 13:44" parsed="|Acts|13|44|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.44" />
<sup>44</sup>Siku ya Sabato iliyofuata, karibu kila mtu katika ule mji alikuja kusikiliza neno la Bwana.
<scripture passage="Acts 13:45" parsed="|Acts|13|45|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.45" />
<sup>45</sup>Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
<scripture passage="Acts 13:46" parsed="|Acts|13|46|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.46" />
<sup>46</sup>Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, "Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni ninyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uzima wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Acts 13:47" parsed="|Acts|13|47|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.47" />
<sup>47</sup>Maana Bwana alituagiza hivi: `Nimekuteua wewe uwe mwanga kwa mataifa, uwe njia ya wokovu kwa ulimwengu wote."`
<scripture passage="Acts 13:48" parsed="|Acts|13|48|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.48" />
<sup>48</sup>Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uzima wa milele, wakawa waumini.
<scripture passage="Acts 13:49" parsed="|Acts|13|49|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.49" />
<sup>49</sup>Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile.
<scripture passage="Acts 13:50" parsed="|Acts|13|50|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.50" />
<sup>50</sup>Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo lao.
<scripture passage="Acts 13:51" parsed="|Acts|13|51|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.51" />
<sup>51</sup>Basi, mitume wakayakung`uta mavumbi yaliyokuwa katika miguu yao kama onyo, kisha wakaenda Ikonio.
<scripture passage="Acts 13:52" parsed="|Acts|13|52|0|0" osisRef="Bible:Acts.13.52" />
<sup>52</sup>Lakini hao wafuasi walikuwa wamejaa furaha na Roho Mtakatifu.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 14" progress="50.55%" prev="Acts.13" next="Acts.15" id="Acts.14">
<h3 id="Acts.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Acts.14-p1">
<scripture passage="Acts 14:1" parsed="|Acts|14|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.1" />
<sup>1</sup>Kule Ikonio, mambo yalikuwa kama yalivyokuwa kule Antiokia; Paulo na Barnaba walikwenda katika sunagogi la Wayahudi wakaongea kwa uhodari hata Wayahudi wengi na Wagiriki wakawa waumini.
<scripture passage="Acts 14:2" parsed="|Acts|14|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.2" />
<sup>2</sup>Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwa waumini walichochea na kutia chuki katika mioyo ya watu wa mataifa mengine ili wawapinge hao ndugu.
<scripture passage="Acts 14:3" parsed="|Acts|14|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.3" />
<sup>3</sup>Paulo na Barnaba waliendelea kukaa huko kwa muda mrefu. Waliongea kwa uhodari juu ya Bwana, naye Bwana akathibitisha ukweli wa ujumbe walioutoa juu ya neema yake, kwa kuwawezesha kutenda miujiza na maajabu.
<scripture passage="Acts 14:4" parsed="|Acts|14|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.4" />
<sup>4</sup>Watu wa mji huo waligawanyika: wengine waliwaunga mkono Wayahudi, na wengine walikuwa upande wa mitume.
<scripture passage="Acts 14:5" parsed="|Acts|14|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.5" />
<sup>5</sup>Mwishowe, baadhi ya watu wa mataifa mengine na Wayahudi, wakishirikiana na wakuu wao, waliazimu kuwatendea vibaya hao mitume na kuwapiga mawe.
<scripture passage="Acts 14:6" parsed="|Acts|14|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.6" />
<sup>6</sup>Mitume walipogundua jambo hilo, walikimbilia Lustra na Derbe, miji ya Lukaonia, na katika sehemu za jirani,
<scripture passage="Acts 14:7" parsed="|Acts|14|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.7" />
<sup>7</sup>wakawa wanahubiri Habari Njema huko.
<scripture passage="Acts 14:8" parsed="|Acts|14|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.8" />
<sup>8</sup>Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa amelemaa miguu tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
<scripture passage="Acts 14:9" parsed="|Acts|14|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.9" />
<sup>9</sup>Mtu huyo alikuwa anamsikiliza Paulo alipokuwa anahubiri. Paulo alimtazama kwa makini, na alipoona kuwa alikuwa na imani ya kuweza kuponywa,
<scripture passage="Acts 14:10" parsed="|Acts|14|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.10" />
<sup>10</sup>akasema kwa sauti kubwa, "Simama wima kwa miguu yako!" Huyo mtu aliyelemaa akainuka ghafla, akaanza kutembea.
<scripture passage="Acts 14:11" parsed="|Acts|14|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.11" />
<sup>11</sup>Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: "Miungu imetujia katika sura za binadamu!"
<scripture passage="Acts 14:12" parsed="|Acts|14|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.12" />
<sup>12</sup>Barnaba akaitwa Zeu, na Paulo, kwa vile yeye ndiye aliyekuwa anaongea, akaitwa Herme.
<scripture passage="Acts 14:13" parsed="|Acts|14|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.13" />
<sup>13</sup>Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume.
<scripture passage="Acts 14:14" parsed="|Acts|14|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.14" />
<sup>14</sup>Barnaba na Paulo walipopata habari hiyo waliyararua mavazi yao na kukimbilia katika lile kundi la watu wakisema kwa sauti kubwa:
<scripture passage="Acts 14:15" parsed="|Acts|14|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.15" />
<sup>15</sup>"Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama ninyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo.
<scripture passage="Acts 14:16" parsed="|Acts|14|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.16" />
<sup>16</sup>Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda.
<scripture passage="Acts 14:17" parsed="|Acts|14|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.17" />
<sup>17</sup>Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha."
<scripture passage="Acts 14:18" parsed="|Acts|14|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.18" />
<sup>18</sup>Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu wasiwatambikie.
<scripture passage="Acts 14:19" parsed="|Acts|14|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.19" />
<sup>19</sup>Lakini Wayahudi kadhaa walikuja kutoka Antiokia na Ikonio, wakawafanya watu wajiunge nao, wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji wakidhani amekwisha kufa.
<scripture passage="Acts 14:20" parsed="|Acts|14|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.20" />
<sup>20</sup>Lakini waumini walipokusanyika na kumzunguka, aliamka akarudi mjini. Kesho yake, yeye pamoja na Barnaba walikwenda Derbe.
<scripture passage="Acts 14:21" parsed="|Acts|14|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.21" />
<sup>21</sup>Baada ya Paulo na Barnabas kuhubiri Habari Njema huko Derbe na kupata wafuasi wengi, walifunga safari kwenda Antiokia kwa kupitia Lustra na Ikonio.
<scripture passage="Acts 14:22" parsed="|Acts|14|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.22" />
<sup>22</sup>Waliwaimarisha waumini wa miji hiyo na kuwatia moyo wabaki imara katika imani. Wakawaambia, "Ni lazima sisi sote tupitie katika taabu nyingi ili tuingie katika ufalme wa Mungu."
<scripture passage="Acts 14:23" parsed="|Acts|14|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.23" />
<sup>23</sup>Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
<scripture passage="Acts 14:24" parsed="|Acts|14|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.24" />
<sup>24</sup>Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia, walifika Pamfulia.
<scripture passage="Acts 14:25" parsed="|Acts|14|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.25" />
<sup>25</sup>Baada ya kuhubiri ule ujumbe huko Perga, walikwenda Atalia.
<scripture passage="Acts 14:26" parsed="|Acts|14|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.26" />
<sup>26</sup>Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.
<scripture passage="Acts 14:27" parsed="|Acts|14|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.27" />
<sup>27</sup>Walipofika huko Antiokia walifanya mkutano wa kanisa la mahali hapo, wakawapa taarifa juu ya mambo Mungu aliyofanya pamoja nao, na jinsi alivyowafungulia mlango watu wa mataifa mengine mlango wa kuingia katika imani.
<scripture passage="Acts 14:28" parsed="|Acts|14|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.14.28" />
<sup>28</sup>Wakakaa pamoja na wale waumini kwa muda mrefu.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 15" progress="50.94%" prev="Acts.14" next="Acts.16" id="Acts.15">
<h3 id="Acts.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Acts.15-p1">
<scripture passage="Acts 15:1" parsed="|Acts|15|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.1" />
<sup>1</sup>Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, "Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo ya Sheria ya Mose, hamtaweza kuokolewa."
<scripture passage="Acts 15:2" parsed="|Acts|15|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.2" />
<sup>2</sup>Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
<scripture passage="Acts 15:3" parsed="|Acts|15|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.3" />
<sup>3</sup>Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
<scripture passage="Acts 15:4" parsed="|Acts|15|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.4" />
<sup>4</sup>Walipofika Yerusalemu walikaribishwa na kanisa, mitume na wazee; nao wakawapa taarifa juu ya yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
<scripture passage="Acts 15:5" parsed="|Acts|15|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.5" />
<sup>5</sup>Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, "Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata Sheria ya Mose."
<scripture passage="Acts 15:6" parsed="|Acts|15|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.6" />
<sup>6</sup>Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalum wa kuchunguza jambo hilo.
<scripture passage="Acts 15:7" parsed="|Acts|15|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.7" />
<sup>7</sup>Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama, akasema, "Ndugu zangu, ninyi mnafahamu kwamba hapo awali Mungu alipenda kunichagua mimi miongoni mwenu niihubiri Habari Njema, ili watu wa mataifa wapate kusikia na kuamini.
<scripture passage="Acts 15:8" parsed="|Acts|15|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.8" />
<sup>8</sup>Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
<scripture passage="Acts 15:9" parsed="|Acts|15|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.9" />
<sup>9</sup>Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani.
<scripture passage="Acts 15:10" parsed="|Acts|15|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.10" />
<sup>10</sup>Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
<scripture passage="Acts 15:11" parsed="|Acts|15|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.11" />
<sup>11</sup>Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao, tunaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu."
<scripture passage="Acts 15:12" parsed="|Acts|15|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.12" />
<sup>12</sup>Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Acts 15:13" parsed="|Acts|15|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.13" />
<sup>13</sup>Walipomaliza kuongea, Yakobo alianza kusema: "Ndugu zangu, nisikilizeni!
<scripture passage="Acts 15:14" parsed="|Acts|15|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.14" />
<sup>14</sup>Simoni ameeleza jinsi Mungu hapo awali alivyojishughulisha na watu wa mataifa mengine, akachagua baadhi yao wawe watu wake.
<scripture passage="Acts 15:15" parsed="|Acts|15|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.15" />
<sup>15</sup>Jambo hili ni sawa kabisa na maneno ya manabii, kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:
<scripture passage="Acts 15:16" parsed="|Acts|15|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.16" />
<sup>16</sup>`Baada ya mambo haya nitarudi. Nitaijenga tena ile nyumba ya Daudi iliyoanguka; nitayatengeneza magofu yake na kuijenga tena.
<scripture passage="Acts 15:17" parsed="|Acts|15|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.17" />
<sup>17</sup>Hapo watu wengine wote, watu wa mataifa yote niliowaita wawe wangu, watamtafuta Bwana.
<scripture passage="Acts 15:18" parsed="|Acts|15|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.18" />
<sup>18</sup>Ndivyo asemavyo Bwana, aliyefanya jambo hili lijulikane tangu kale.`
<scripture passage="Acts 15:19" parsed="|Acts|15|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.19" />
<sup>19</sup>"Kwa hiyo, uamuzi wangu ni huu: tusiwataabishe watu wa mataifa wanomgeukia Mungu.
<scripture passage="Acts 15:20" parsed="|Acts|15|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.20" />
<sup>20</sup>Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa najisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu; wajiepushe na uasherati; wasile mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu.
<scripture passage="Acts 15:21" parsed="|Acts|15|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.21" />
<sup>21</sup>Kwa maana kwa muda mrefu maneno ya Mose yamekuwa yakihubiriwa katika kila mji na kusomwa katika masunagogi yote kila siku ya Sabato." ic
<scripture passage="Acts 15:22" parsed="|Acts|15|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.22" />
<sup>22</sup>Mitume, wazee na kanisa lote waliamua kuwachagua watu fulani miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Basi, wakamchagua Yuda aitwaye pia Barsaba, na Sila ambao wote walikuwa wanajulikana zaidi kati ya ndugu.
<scripture passage="Acts 15:23" parsed="|Acts|15|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.23" />
<sup>23</sup>Wakawapa barua hii: mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
<scripture passage="Acts 15:24" parsed="|Acts|15|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.24" />
<sup>24</sup>Tumesikia kwamba watu wengine kutoka huku kwetu waliwavurugeni kwa maneno yao, wakaitia mioyo yenu katika wasiwasi. Lakini wamefanya hivyo bila ya idhini yoyote kutoka kwetu.
<scripture passage="Acts 15:25" parsed="|Acts|15|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.25" />
<sup>25</sup>Hivyo, tumeamua kwa pamoja kuwachagua watu kadhaa na kuwatuma kwenu pamoja na wapenzi wetu Barnaba na Paulo,
<scripture passage="Acts 15:26" parsed="|Acts|15|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.26" />
<sup>26</sup>ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Acts 15:27" parsed="|Acts|15|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.27" />
<sup>27</sup>Kwa hiyo, tunawatuma Yuda na Sila kwenu; hawa watawaambieni wao wenyewe haya tuliyoandika.
<scripture passage="Acts 15:28" parsed="|Acts|15|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.28" />
<sup>28</sup>Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:
<scripture passage="Acts 15:29" parsed="|Acts|15|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.29" />
<sup>29</sup>Msile vyakula vilivyotambikiwa sanamu; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!"
<scripture passage="Acts 15:30" parsed="|Acts|15|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.30" />
<sup>30</sup>Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
<scripture passage="Acts 15:31" parsed="|Acts|15|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.31" />
<sup>31</sup>Walipoisoma hiyo barua, maneno yake yaliwatia moyo, wakafurahi sana.
<scripture passage="Acts 15:32" parsed="|Acts|15|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.32" />
<sup>32</sup>Yuda na Sila, ambao nao walikuwa manabii, walizungumza na hao ndugu kwa muda mrefu wakiwatia moyo na kuwaimarisha.
<scripture passage="Acts 15:33" parsed="|Acts|15|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.33" />
<sup>33</sup>Baada ya kukaa huko kwa muda fulani, ndugu wa Antiokia waliwaaga wakiwatakia amani, kisha wakarudi kwa wale waliokuwa wamewatuma.<i>fb</i>
<scripture passage="Acts 15:34" parsed="|Acts|15|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.34" />
<sup>34</sup>missing
<scripture passage="Acts 15:35" parsed="|Acts|15|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.35" />
<sup>35</sup>Paulo na Barnaba walibaki huko Antiokia kwa muda; wakafundisha na kuhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
<scripture passage="Acts 15:36" parsed="|Acts|15|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.36" />
<sup>36</sup>Baada ya siku kadhaa, Paulo alimwambia Barnaba, "Turudi tukawatembelee wale ndugu katika kila mji tulikolihubiri neno la Bwana tukajionee jinsi wanavyoendelea."
<scripture passage="Acts 15:37" parsed="|Acts|15|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.37" />
<sup>37</sup>Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko.
<scripture passage="Acts 15:38" parsed="|Acts|15|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.38" />
<sup>38</sup>Lakini Paulo hakupendelea kumchukua Marko, ambaye awali aliwaacha kule Pamfulia na kukataa kushiriki katika kazi yao.
<scripture passage="Acts 15:39" parsed="|Acts|15|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.39" />
<sup>39</sup>Basi kukatokea ubishi mkali kati yao, na wakaachana. Barnaba akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro.
<scripture passage="Acts 15:40" parsed="|Acts|15|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.40" />
<sup>40</sup>Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.
<scripture passage="Acts 15:41" parsed="|Acts|15|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.15.41" />
<sup>41</sup>Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia akiyaimarisha makanisa.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 16" progress="51.47%" prev="Acts.15" next="Acts.17" id="Acts.16">
<h3 id="Acts.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Acts.16-p1">
<scripture passage="Acts 16:1" parsed="|Acts|16|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.1" />
<sup>1</sup>Paulo alifika Derbe na Lustra, ambako aliishi mfuasi mmoja aitwaye Timotheo. Mama yake ambaye pia alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini baba yake alikuwa Mgiriki.
<scripture passage="Acts 16:2" parsed="|Acts|16|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.2" />
<sup>2</sup>Timotheo alikuwa na sifa kubwa kati ya wale ndugu wa Lustra na Ikonio.
<scripture passage="Acts 16:3" parsed="|Acts|16|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.3" />
<sup>3</sup>Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
<scripture passage="Acts 16:4" parsed="|Acts|16|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.4" />
<sup>4</sup>Walipokuwa wanapita katika ile miji waliwapa watu yale maagizo yaliyotolewa na mitume na wazee kule Yerusalemu, wakawaambia wayazingatie.
<scripture passage="Acts 16:5" parsed="|Acts|16|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.5" />
<sup>5</sup>Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya waumini ikaongezeka kila siku.
<scripture passage="Acts 16:6" parsed="|Acts|16|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.6" />
<sup>6</sup>Walipitia sehemu za Frugia na Galatia kwani Roho Mtakatifu hakuwaruhusu kuhubiri huo ujumbe mkoani Asia.
<scripture passage="Acts 16:7" parsed="|Acts|16|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.7" />
<sup>7</sup>Walipofika kwenye mipaka ya Musia, walijaribu kuingia mkoani Bithunia, lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.
<scripture passage="Acts 16:8" parsed="|Acts|16|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.8" />
<sup>8</sup>Basi, walipitia Musia, wakaenda moja kwa moja mpaka Troa.
<scripture passage="Acts 16:9" parsed="|Acts|16|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.9" />
<sup>9</sup>Usiku huo, Paulo aliona ono ambalo alimwona mtu mmoja wa Makedonia amesimama pale na kumwomba: "Vuka, uje Makedonia ukatusaidie."
<scripture passage="Acts 16:10" parsed="|Acts|16|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.10" />
<sup>10</sup>Mara baada ya Paulo kuona ono hilo, tulijitayarisha kwenda Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita tuwapelekee Habari Njema.
<scripture passage="Acts 16:11" parsed="|Acts|16|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.11" />
<sup>11</sup>Kutoka Troa, tulisafiri kwa meli moja kwa moja mpaka Samothrake, na kesho yake tukatia nanga Neapoli.
<scripture passage="Acts 16:12" parsed="|Acts|16|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.12" />
<sup>12</sup>Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.
<scripture passage="Acts 16:13" parsed="|Acts|16|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.13" />
<sup>13</sup>Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.
<scripture passage="Acts 16:14" parsed="|Acts|16|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.14" />
<sup>14</sup>Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
<scripture passage="Acts 16:15" parsed="|Acts|16|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.15" />
<sup>15</sup>Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika akisema, "Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni nyumbani kwangu mkakae." Akatuhimiza twende.
<scripture passage="Acts 16:16" parsed="|Acts|16|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.16" />
<sup>16</sup>Siku moja, tulipokuwa tunakwenda mahali pa kusali, msichana mmoja aliyekuwa na pepo mwenye uwezo wa kuagua alikutana nasi. Msichana huyo alikuwa anawapatia matajiri wake fedha nyingi kwa uaguzi wake.
<scripture passage="Acts 16:17" parsed="|Acts|16|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.17" />
<sup>17</sup>Basi, huyo msichana alimfuata Paulo na sisi, akipiga kelele na kusema, "Hawa watu ni watumishi wa Mungu Mkuu. Wanawatangazieni njia ya wokovu."
<scripture passage="Acts 16:18" parsed="|Acts|16|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.18" />
<sup>18</sup>Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, "Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu!" Mara huyo pepo akamtoka.
<scripture passage="Acts 16:19" parsed="|Acts|16|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.19" />
<sup>19</sup>Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu.
<scripture passage="Acts 16:20" parsed="|Acts|16|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.20" />
<sup>20</sup>Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, "Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.
<scripture passage="Acts 16:21" parsed="|Acts|16|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.21" />
<sup>21</sup>Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Roma haturuhusiwi kuzikubali wala kuzifuata."
<scripture passage="Acts 16:22" parsed="|Acts|16|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.22" />
<sup>22</sup>Kundi la watu likajiunga nao, likawashambulia. Wale mahakimu wakawatatulia Paulo na Sila mavazi yao, wakaamuru wapigwe viboko.
<scripture passage="Acts 16:23" parsed="|Acts|16|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.23" />
<sup>23</sup>Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
<scripture passage="Acts 16:24" parsed="|Acts|16|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.24" />
<sup>24</sup>Kutokana na maagizo hayo, huyo askari aliwaweka katika chumba cha ndani kabisa cha gereza na kuifunga miguu yao kwenye nguzo.
<scripture passage="Acts 16:25" parsed="|Acts|16|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.25" />
<sup>25</sup>Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza.
<scripture passage="Acts 16:26" parsed="|Acts|16|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.26" />
<sup>26</sup>Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo iliyowafunga hao wafungwa ikaachana.
<scripture passage="Acts 16:27" parsed="|Acts|16|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.27" />
<sup>27</sup>Askari wa gereza alipoamka na kuiona milango ya gereza imefunguliwa, alidhani kwamba wafungwa wote walikuwa wametoroka na hivyo akauchomoa upanga wake, akataka kujiua.
<scripture passage="Acts 16:28" parsed="|Acts|16|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.28" />
<sup>28</sup>Lakini Paulo akaita kwa sauti kubwa: "Usijidhuru mwenyewe kwa maana sisi sote tuko hapa."
<scripture passage="Acts 16:29" parsed="|Acts|16|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.29" />
<sup>29</sup>Baada ya kumwita mtu alete taa, huyo askari wa gereza alikimbilia ndani, akajitupa mbele ya miguu ya Paulo na Sila huku akitetemeka kwa hofu.
<scripture passage="Acts 16:30" parsed="|Acts|16|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.30" />
<sup>30</sup>Halafu aliwaongoza nje, akawauliza, "Waheshimiwa, nifanye nini nipate kuokoka?"
<scripture passage="Acts 16:31" parsed="|Acts|16|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.31" />
<sup>31</sup>Wao wakamjibu, "Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa pamoja na jamaa yako yote."
<scripture passage="Acts 16:32" parsed="|Acts|16|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.32" />
<sup>32</sup>Basi, wakamhubiria neno la Bwana yeye pamoja na jamaa yake.
<scripture passage="Acts 16:33" parsed="|Acts|16|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.33" />
<sup>33</sup>Yule askari aliwachukua saa ileile ya usiku akawasafisha majeraha yao, kisha yeye na jamaa yake wakabatizwa papo hapo.
<scripture passage="Acts 16:34" parsed="|Acts|16|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.34" />
<sup>34</sup>Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa wanamwamini Mungu.
<scripture passage="Acts 16:35" parsed="|Acts|16|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.35" />
<sup>35</sup>Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema, "Wafungueni wale watu."
<scripture passage="Acts 16:36" parsed="|Acts|16|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.36" />
<sup>36</sup>Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: "Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani."
<scripture passage="Acts 16:37" parsed="|Acts|16|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.37" />
<sup>37</sup>Lakini Paulo alimjibu, "Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie."
<scripture passage="Acts 16:38" parsed="|Acts|16|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.38" />
<sup>38</sup>Hao maofisa waliwapasha habari mahakimu juu ya jambo hilo, nao waliposikia kwamba Paulo na Sila walikuwa raia wa Roma, waliogopa.
<scripture passage="Acts 16:39" parsed="|Acts|16|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.39" />
<sup>39</sup>Hivyo, walikwenda kuwataka radhi na baada ya kuwatoa ndani waliwaomba watoke katika mji ule.
<scripture passage="Acts 16:40" parsed="|Acts|16|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.16.40" />
<sup>40</sup>Paulo na Sila walitoka gerezani, wakaenda nyumbani kwa Ludia. Huko walionana na ndugu waumini na baada ya kuwatia moyo wakaondoka.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 17" progress="52.02%" prev="Acts.16" next="Acts.18" id="Acts.17">
<h3 id="Acts.17-p0.1">Chapter 17</h3>
<p id="Acts.17-p1">
<scripture passage="Acts 17:1" parsed="|Acts|17|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.1" />
<sup>1</sup>Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonika ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi.
<scripture passage="Acts 17:2" parsed="|Acts|17|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.2" />
<sup>2</sup>Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akatumia Maandiko Matakatifu.
<scripture passage="Acts 17:3" parsed="|Acts|17|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.3" />
<sup>3</sup>Aliyaeleza na kuonyesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka wafu. Akawaambia, "Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo."
<scripture passage="Acts 17:4" parsed="|Acts|17|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.4" />
<sup>4</sup>Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika, idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa tabaka la juu, walijiunga nao.
<scripture passage="Acts 17:5" parsed="|Acts|17|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.5" />
<sup>5</sup>Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni, wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
<scripture passage="Acts 17:6" parsed="|Acts|17|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.6" />
<sup>6</sup>Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: "Watu hawa wamekuwa wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini.
<scripture passage="Acts 17:7" parsed="|Acts|17|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.7" />
<sup>7</sup>Yasoni amewakaribisha nyumbani kwake. Wote wanafanya kinyume cha amri ya Kaisari wakisema eti `Kuna mfalme mwingine aitwaye Yesu."`
<scripture passage="Acts 17:8" parsed="|Acts|17|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.8" />
<sup>8</sup>Kwa maneno hayo waliwatia wasiwasi wakuu wa mji na kundi la watu.
<scripture passage="Acts 17:9" parsed="|Acts|17|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.9" />
<sup>9</sup>Wakawafanya Yasoni na wenzake watoe dhamana, kisha wakawaacha waende zao.
<scripture passage="Acts 17:10" parsed="|Acts|17|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.10" />
<sup>10</sup>Usiku, wale ndugu waliwahimiza Paulo na Sila waende Berea. Mara tu walipofika huko, walikwenda katika sunagogi la Wayahudi.
<scripture passage="Acts 17:11" parsed="|Acts|17|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.11" />
<sup>11</sup>Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonika. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli.
<scripture passage="Acts 17:12" parsed="|Acts|17|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.12" />
<sup>12</sup>Wengi wao waliamini na pia wanawake wa Kigiriki wa tabaka la juu na wanaume pia.
<scripture passage="Acts 17:13" parsed="|Acts|17|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.13" />
<sup>13</sup>Lakini, Wayahudi wa Thesalonika walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.
<scripture passage="Acts 17:14" parsed="|Acts|17|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.14" />
<sup>14</sup>Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na Timotheo walibaki Berea.
<scripture passage="Acts 17:15" parsed="|Acts|17|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.15" />
<sup>15</sup>Wale ndugu waliomsindikiza Paulo walikwenda pamoja naye mpaka Athene. Kisha, wakarudi pamoja na maagizo kutoka kwa Paulo kwamba Sila na Timotheo wamfuate upesi iwezekanavyo.
<scripture passage="Acts 17:16" parsed="|Acts|17|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.16" />
<sup>16</sup>Paulo alipokuwa anawasubiri Sila na Timotheo huko Athene, moyo wake ulighadhibika sana alipoona jinsi mji huo ulivyokuwa umejaa sanamu za miungu.
<scripture passage="Acts 17:17" parsed="|Acts|17|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.17" />
<sup>17</sup>Alijadiliana na Wayahudi na watu wengine waliomcha Mungu katika sunagogi; na kila siku alikuwa na majadiliano sokoni pamoja na wowote wale waliojitokeza.
<scripture passage="Acts 17:18" parsed="|Acts|17|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.18" />
<sup>18</sup>Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, "Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?" Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, "Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni."
<scripture passage="Acts 17:19" parsed="|Acts|17|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.19" />
<sup>19</sup>Hivyo walimchukua Paulo, wakampeleka Areopago, wakasema, "Tunataka kujua jambo hili jipya ulilokuwa unazungumzia.
<scripture passage="Acts 17:20" parsed="|Acts|17|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.20" />
<sup>20</sup>Vitu vingine tulivyosikia kwa masikio yetu vinaonekana kuwa viroja kwetu. Tungependa kujua mambo haya yana maana gani."
<scripture passage="Acts 17:21" parsed="|Acts|17|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.21" />
<sup>21</sup>Wananchi wa Athene na wakazi wengine wa huko walikuwa wanatumia wakati wao wote kuhadithiana na kusikiliza habari mpyampya. ic
<scripture passage="Acts 17:22" parsed="|Acts|17|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.22" />
<sup>22</sup>Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, "Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba ninyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana.
<scripture passage="Acts 17:23" parsed="|Acts|17|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.23" />
<sup>23</sup>Sababu yenyewe ni kwamba katika pitapita yangu niliangalia sanamu zenu za ibada nikakuta madhabahu moja ambayo imeandikwa: `Kwa ajili ya Mungu yule Asiyejulikana.` Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye ninayemhubiri kwenu.
<scripture passage="Acts 17:24" parsed="|Acts|17|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.24" />
<sup>24</sup>Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
<scripture passage="Acts 17:25" parsed="|Acts|17|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.25" />
<sup>25</sup>Wala hatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na anawapa kila kitu.
<scripture passage="Acts 17:26" parsed="|Acts|17|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.26" />
<sup>26</sup>Kutokana na mtu mmoja aliumba mataifa yote na kuyawezesha kuishi duniani kote. Aliamua na kupanga kabla kabisa lini na wapi mataifa hayo yangeishi.
<scripture passage="Acts 17:27" parsed="|Acts|17|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.27" />
<sup>27</sup>Alifanya hivyo, ili mataifa hayo yapate kumfuata, na kama vile kwa kupapasapapasa, yapate kumfikia. Hata hivyo lakini, Mungu hayuko mbali na kila mmoja wetu.
<scripture passage="Acts 17:28" parsed="|Acts|17|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.28" />
<sup>28</sup>Kama alivyosema mtu mmoja: `Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, na tuko!` Ni kama washairi wenu wengine walivyosema: `Sisi ni watoto wake.`
<scripture passage="Acts 17:29" parsed="|Acts|17|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.29" />
<sup>29</sup>Ikiwa basi, sisi ni watoto wa Mungu, haifai kumfikiria Mungu kuwa kama dhahabu, fedha au hata jiwe lililochongwa na kutiwa nakshi na binadamu.
<scripture passage="Acts 17:30" parsed="|Acts|17|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.30" />
<sup>30</sup>Mungu alifanya kama kwamba haoni nyakati zile watu walipokuwa wajinga. Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahali watubu.
<scripture passage="Acts 17:31" parsed="|Acts|17|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.31" />
<sup>31</sup>Kwa maana amekwisha weka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki kwa njia ya mtu mmoja aliyemteua. Mungu amewathibitishia wote jambo hili kwa kumfufua mtu huyo kutoka wafu!"
<scripture passage="Acts 17:32" parsed="|Acts|17|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.32" />
<sup>32</sup>Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu, wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, "Tunataka kukusikia tena juu ya jambo hili!"
<scripture passage="Acts 17:33" parsed="|Acts|17|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.33" />
<sup>33</sup>Hivyo, Paulo aliwaacha, akatoka barazani.
<scripture passage="Acts 17:34" parsed="|Acts|17|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.17.34" />
<sup>34</sup>Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, mwanamke mmoja aitwaye Damari na wengineo.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 18" progress="52.53%" prev="Acts.17" next="Acts.19" id="Acts.18">
<h3 id="Acts.18-p0.1">Chapter 18</h3>
<p id="Acts.18-p1">
<scripture passage="Acts 18:1" parsed="|Acts|18|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, Paulo aliondoka Athene, akaenda Korintho.
<scripture passage="Acts 18:2" parsed="|Acts|18|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.2" />
<sup>2</sup>Huko Korintho, alimkuta Myahudi mmoja aitwaye Akula, mzaliwa wa Ponto. Akula pamoja na mkewe aitwaye Priskila, walikuwa wamerudi kutoka Italia siku hizohizo kwa sababu Kaisari Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Roma. Paulo alikwenda kuwaona,
<scripture passage="Acts 18:3" parsed="|Acts|18|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.3" />
<sup>3</sup>na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama alivyokuwa yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
<scripture passage="Acts 18:4" parsed="|Acts|18|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.4" />
<sup>4</sup>Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.
<scripture passage="Acts 18:5" parsed="|Acts|18|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.5" />
<sup>5</sup>Baada ya Sila na Timotheo kuwasili kutoka Makedonia, Paulo alianza kutumia wakati wake wote kwa ajili ya kuhubiri, akawathibitishia Wayahudi kwamba Yesu ndiye Kristo.
<scripture passage="Acts 18:6" parsed="|Acts|18|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.6" />
<sup>6</sup>Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung`uta mavazi yake mbele yao akisema, "Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine."
<scripture passage="Acts 18:7" parsed="|Acts|18|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.7" />
<sup>7</sup>Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi.
<scripture passage="Acts 18:8" parsed="|Acts|18|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.8" />
<sup>8</sup>Lakini Krispo, mkuu wa sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
<scripture passage="Acts 18:9" parsed="|Acts|18|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.9" />
<sup>9</sup>Siku moja usiku, Bwana alimwambia Paulo katika maono: "Usiogope, endelea kuhubiri tu bila kufa moyo,
<scripture passage="Acts 18:10" parsed="|Acts|18|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.10" />
<sup>10</sup>maana mimi niko pamoja nawe. Hakuna mtu atakayejaribu kukudhuru maana hapa mjini pana watu wengi walio upande wangu."
<scripture passage="Acts 18:11" parsed="|Acts|18|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.11" />
<sup>11</sup>Basi, Paulo alikaa huko akifundisha neno la Mungu kati yao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.
<scripture passage="Acts 18:12" parsed="|Acts|18|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.12" />
<sup>12</sup>Lakini wakati Galio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Akaya, Wayahudi walimvamia Paulo kwa pamoja na kumpeleka mahakamani.
<scripture passage="Acts 18:13" parsed="|Acts|18|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.13" />
<sup>13</sup>Wakasema, "Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na Sheria."
<scripture passage="Acts 18:14" parsed="|Acts|18|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.14" />
<sup>14</sup>Kabla tu Paulo hajaanza kusema, Galio aliwaambia Wayahudi, "Sikilizeni enyi Wayahudi! Kama kweli jambo hili lingekuwa juu ya uhalifu au uovu ningekuwa tayari kuwasikilizeni.
<scripture passage="Acts 18:15" parsed="|Acts|18|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.15" />
<sup>15</sup>Lakini kama ni shauri la ubishi kuhusu maneno na majina ya Sheria yenu, amueni ninyi wenyewe. Mimi sitaki kuwa hakimu wa mambo haya!"
<scripture passage="Acts 18:16" parsed="|Acts|18|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.16" />
<sup>16</sup>Basi, akawafukuza kutoka mahakamani.
<scripture passage="Acts 18:17" parsed="|Acts|18|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.17" />
<sup>17</sup>Nao wote wakamkamata Sosthene ambaye alikuwa kiongozi wa sunagogi, wakampiga palepale mbele ya mahakama. Lakini Galio hakujali kitendo hicho hata kidogo.
<scripture passage="Acts 18:18" parsed="|Acts|18|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.18" />
<sup>18</sup>Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula. Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameweka.
<scripture passage="Acts 18:19" parsed="|Acts|18|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.19" />
<sup>19</sup>Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.
<scripture passage="Acts 18:20" parsed="|Acts|18|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.20" />
<sup>20</sup>Walimwomba akae nao muda mrefu zaidi, lakini hakupenda.
<scripture passage="Acts 18:21" parsed="|Acts|18|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.21" />
<sup>21</sup>Bali alipokuwa anaondoka, alisema, "Mungu akipenda nitakuja kwenu tena." Akaondoka Efeso kwa meli.
<scripture passage="Acts 18:22" parsed="|Acts|18|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.22" />
<sup>22</sup>Meli ilitia nanga Kaisarea, naye Paulo akaenda Yerusalemu kulisalimia lile kanisa, kisha akaenda Antiokia.
<scripture passage="Acts 18:23" parsed="|Acts|18|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.23" />
<sup>23</sup>Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
<scripture passage="Acts 18:24" parsed="|Acts|18|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.24" />
<sup>24</sup>Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
<scripture passage="Acts 18:25" parsed="|Acts|18|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.25" />
<sup>25</sup>Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu. Akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
<scripture passage="Acts 18:26" parsed="|Acts|18|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.26" />
<sup>26</sup>Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo Njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
<scripture passage="Acts 18:27" parsed="|Acts|18|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.27" />
<sup>27</sup>Apolo alipoamua kwenda Akaya, wale ndugu walimtia moyo kwa kuwaandikia wafuasi kule Akaya wampokee. Alipofika huko, aliweza kwa msaada wa neema ya Mungu, kuwasaidia sana wale ndugu waliopata kuwa waumini;
<scripture passage="Acts 18:28" parsed="|Acts|18|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.18.28" />
<sup>28</sup>kwa maana aliendelea kwa uhodari kuwashinda Wayahudi hadharani akithibitisha kwa Maandiko Matakatifu kuwa Yesu ni Kristo.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 19" progress="52.93%" prev="Acts.18" next="Acts.20" id="Acts.19">
<h3 id="Acts.19-p0.1">Chapter 19</h3>
<p id="Acts.19-p1">
<scripture passage="Acts 19:1" parsed="|Acts|19|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.1" />
<sup>1</sup>Wakati Apolo alipokuwa Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso ambako aliwakuta wanafunzi kadhaa.
<scripture passage="Acts 19:2" parsed="|Acts|19|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.2" />
<sup>2</sup>Akauliza, "Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?" Nao wakamjibu, "La! Hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatujasikia."
<scripture passage="Acts 19:3" parsed="|Acts|19|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.3" />
<sup>3</sup>Naye akasema, "Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?" Wakamjibu, "Ubatizo wa Yohane."
<scripture passage="Acts 19:4" parsed="|Acts|19|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.4" />
<sup>4</sup>Naye Paulo akasema, "Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu."
<scripture passage="Acts 19:5" parsed="|Acts|19|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.5" />
<sup>5</sup>Baada ya kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
<scripture passage="Acts 19:6" parsed="|Acts|19|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.6" />
<sup>6</sup>Basi, Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia, wakaanza kusema lugha mbalimbali na kutangaza ujumbe wa Mungu.
<scripture passage="Acts 19:7" parsed="|Acts|19|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.7" />
<sup>7</sup>Wote jumla, walikuwa watu wapatao kumi na wawili.
<scripture passage="Acts 19:8" parsed="|Acts|19|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.8" />
<sup>8</sup>Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya Ufalme wa Mungu.
<scripture passage="Acts 19:9" parsed="|Acts|19|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.9" />
<sup>9</sup>Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya hadharani juu ya Njia ya Bwana. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.
<scripture passage="Acts 19:10" parsed="|Acts|19|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.10" />
<sup>10</sup>Aliendelea kufanya hivyo kwa muda wa miaka miwili hata wakazi wote wa Asia, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, wakaweza kusikia neno la Bwana.
<scripture passage="Acts 19:11" parsed="|Acts|19|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.11" />
<sup>11</sup>Mungu alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo.
<scripture passage="Acts 19:12" parsed="|Acts|19|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.12" />
<sup>12</sup>Watu walikuwa wakichukua leso na nguo nyingine za kazi ambazo Paulo alikuwa amezitumia, wakazipeleka kwa wagonjwa, nao wakaponywa magonjwa yao; na wale waliokuwa na pepo wabaya wakatokwa na pepo hao.
<scripture passage="Acts 19:13" parsed="|Acts|19|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.13" />
<sup>13</sup>Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya, walisafiri huko na huko, wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: "Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri."
<scripture passage="Acts 19:14" parsed="|Acts|19|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.14" />
<sup>14</sup>Watoto saba wa Skewa, Kuhani Mkuu wa Kiyahudi, walikuwa miongoni mwa hao waliokuwa wanafanya hivyo.
<scripture passage="Acts 19:15" parsed="|Acts|19|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.15" />
<sup>15</sup>Lakini pepo mbaya aliwajibu, "Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia Paulo, lakini ninyi ni nani?"
<scripture passage="Acts 19:16" parsed="|Acts|19|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.16" />
<sup>16</sup>Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
<scripture passage="Acts 19:17" parsed="|Acts|19|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.17" />
<sup>17</sup>Kila mtu huko Efeso, Myahudi na asiye Myahudi, alisikia juu ya tukio hilo. Wote waliingiwa na hofu, wakalitukuza jina la Bwana Yesu.
<scripture passage="Acts 19:18" parsed="|Acts|19|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.18" />
<sup>18</sup>Waumini wengi walijitokeza wakakiri hadharani mambo waliyokuwa wametenda.
<scripture passage="Acts 19:19" parsed="|Acts|19|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.19" />
<sup>19</sup>Wengine waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikia vipande vya fedha elfu hamsini.
<scripture passage="Acts 19:20" parsed="|Acts|19|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.20" />
<sup>20</sup>Kwa namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu zaidi.
<scripture passage="Acts 19:21" parsed="|Acts|19|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.21" />
<sup>21</sup>Baada ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya. Alisema, "Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona Roma pia."
<scripture passage="Acts 19:22" parsed="|Acts|19|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.22" />
<sup>22</sup>Hivyo, aliwatuma wawili wa wasaidizi wake, Timotheo na Erasto, wamtangulie kwenda Makedonia, naye akabaki kwa muda huko Asia.
<scripture passage="Acts 19:23" parsed="|Acts|19|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.23" />
<sup>23</sup>Wakati huo ndipo kulipotokea ghasia kubwa huko Efeso kwa sababu ya hiyo Njia ya Bwana.
<scripture passage="Acts 19:24" parsed="|Acts|19|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.24" />
<sup>24</sup>Kulikuwa na mfua fedha mmoja aitwaye Demetrio, ambaye alikuwa na kazi ya kutengeneza sanamu za nyumba ya mungu wa kike aitwaye Artemi. Shughuli hiyo iliwapatia mafundi faida kubwa.
<scripture passage="Acts 19:25" parsed="|Acts|19|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.25" />
<sup>25</sup>Demetrio aliwakusanya hao wafanyakazi pamoja na wengine waliokuwa na kazi kama hiyo, akawaambia, "Wananchi, mnafahamu kwamba kipato chetu kinatokana na biashara hii.
<scripture passage="Acts 19:26" parsed="|Acts|19|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.26" />
<sup>26</sup>Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya, si tu hapa Efeso, ila pia kote katika Asia. Yeye amewashawishi na kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu ile iliyotengenezwa na watu si miungu hata kidogo.
<scripture passage="Acts 19:27" parsed="|Acts|19|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.27" />
<sup>27</sup>Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha." ic
<scripture passage="Acts 19:28" parsed="|Acts|19|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.28" />
<sup>28</sup>Waliposikia hayo, waliwaka hasira, wakaanza kupiga kelele: "Mkuu ni Artemi, wa Efeso!"
<scripture passage="Acts 19:29" parsed="|Acts|19|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.29" />
<sup>29</sup>Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
<scripture passage="Acts 19:30" parsed="|Acts|19|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.30" />
<sup>30</sup>Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia.
<scripture passage="Acts 19:31" parsed="|Acts|19|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.31" />
<sup>31</sup>Maofisa wengine wa huo mkoa wa Asia, waliokuwa rafiki zake, walimtumia Paulo ujumbe wakimsihi asijihatarishe kwa kwenda kwenye ukumbi wa michezo.
<scripture passage="Acts 19:32" parsed="|Acts|19|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.32" />
<sup>32</sup>Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
<scripture passage="Acts 19:33" parsed="|Acts|19|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.33" />
<sup>33</sup>Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
<scripture passage="Acts 19:34" parsed="|Acts|19|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.34" />
<sup>34</sup>Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele: "Mkuu ni Artemi wa Efeso!" Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda wa saa mbili.
<scripture passage="Acts 19:35" parsed="|Acts|19|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.35" />
<sup>35</sup>Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, "Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.
<scripture passage="Acts 19:36" parsed="|Acts|19|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.36" />
<sup>36</sup>Hakuna anayeweza kukana mambo haya. Hivyo basi, tulieni; msifanye chochote bila hadhari.
<scripture passage="Acts 19:37" parsed="|Acts|19|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.37" />
<sup>37</sup>Mmewaita watu hawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumba ya mungu wala kumtukana mungu wetu wa kike.
<scripture passage="Acts 19:38" parsed="|Acts|19|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.38" />
<sup>38</sup>Kama, basi Demetrio na wafanyakazi wake wana mashtaka yao kuhusu watu hawa, yapo mahakama na wakuu wa mikoa; wanaweza kushtakiana huko.
<scripture passage="Acts 19:39" parsed="|Acts|19|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.39" />
<sup>39</sup>Kama mna matatizo mengine, yapelekeni katika kikao halali.
<scripture passage="Acts 19:40" parsed="|Acts|19|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.40" />
<sup>40</sup>Kwa maana tungaliweza kushtakiwa kwa kusababisha ghasia kutokana na vituko vya leo. Ghasia hii haina msingi halali na hatungeweza kutoa sababu za kuridhisha za ghasia hiyo."
<scripture passage="Acts 19:41" parsed="|Acts|19|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.19.41" />
<sup>41</sup>Baada ya kusema hayo aliuvunja mkutano.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 20" progress="53.51%" prev="Acts.19" next="Acts.21" id="Acts.20">
<h3 id="Acts.20-p0.1">Chapter 20</h3>
<p id="Acts.20-p1">
<scripture passage="Acts 20:1" parsed="|Acts|20|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.1" />
<sup>1</sup>Ile ghasia ya Efeso ilipokwisha tulia Paulo aliwaita pamoja wale waumini, akawatia moyo. Kisha akawaaga, akasafiri kwenda Makedonia.
<scripture passage="Acts 20:2" parsed="|Acts|20|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.2" />
<sup>2</sup>Alipitia sehemu za nchi zile akiwatia watu moyo kwa maneno mengi. Halafu akafika Ugiriki.
<scripture passage="Acts 20:3" parsed="|Acts|20|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.3" />
<sup>3</sup>ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
<scripture passage="Acts 20:4" parsed="|Acts|20|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.4" />
<sup>4</sup>Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea, aliandamana naye; pia Aristarko na Sekundo kutoka Thesalonika, Gayo kutoka Derbe, Timotheo, Tukiko na Trofimo wa mkoa wa Asia.
<scripture passage="Acts 20:5" parsed="|Acts|20|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.5" />
<sup>5</sup>Hao walitutangulia na kutungojea kule Troa.
<scripture passage="Acts 20:6" parsed="|Acts|20|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.6" />
<sup>6</sup>Sisi, baada ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.
<scripture passage="Acts 20:7" parsed="|Acts|20|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.7" />
<sup>7</sup>Jumamosi jioni, tulikutana ili kumega mkate. Kwa vile Paulo alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliwahutubia watu na kuendelea kuongea nao hadi usiku wa manane.
<scripture passage="Acts 20:8" parsed="|Acts|20|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.8" />
<sup>8</sup>Katika chumba tulimokuwa, ghorofani, kulikuwa na taa nyingi zinawaka.
<scripture passage="Acts 20:9" parsed="|Acts|20|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.9" />
<sup>9</sup>Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu. Wakamwokota amekwisha kufa.
<scripture passage="Acts 20:10" parsed="|Acts|20|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.10" />
<sup>10</sup>Lakini Paulo alishuka chini, akainama, akamkumbatia na kusema, "Msiwe na wasiwasi maana kuna uhai bado ndani yake."
<scripture passage="Acts 20:11" parsed="|Acts|20|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.11" />
<sup>11</sup>Kisha akapanda tena ghorofani, akamega mkate, akala. Aliendelea kuhubiri kwa muda mrefu hadi alfajiri, halafu akaondoka.
<scripture passage="Acts 20:12" parsed="|Acts|20|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.12" />
<sup>12</sup>Wale watu walimchukua yule kijana nyumbani akiwa mzima kabisa, wakapata kitulizo kikubwa.
<scripture passage="Acts 20:13" parsed="|Acts|20|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.13" />
<sup>13</sup>Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu.
<scripture passage="Acts 20:14" parsed="|Acts|20|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.14" />
<sup>14</sup>Basi, alitukuta kule Aso, tukampandisha melini, tukaenda Mitulene.
<scripture passage="Acts 20:15" parsed="|Acts|20|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.15" />
<sup>15</sup>Kutoka huko tulisafiri tukafika Kio kesho yake. Siku ya pili, tulitia nanga Samo na kesho yake tukafika Mileto.
<scripture passage="Acts 20:16" parsed="|Acts|20|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.16" />
<sup>16</sup>Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.
<scripture passage="Acts 20:17" parsed="|Acts|20|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.17" />
<sup>17</sup>Kutoka Mileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee wa Efeso wakutane naye.
<scripture passage="Acts 20:18" parsed="|Acts|20|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.18" />
<sup>18</sup>Walipofika kwake aliwaambia, "Mnajua jinsi nilivyotumia wakati wote pamoja nanyi tangu siku ile ya kwanza nilipofika Asia.
<scripture passage="Acts 20:19" parsed="|Acts|20|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.19" />
<sup>19</sup>Mnajua jinsi nilivyomtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, kwa machozi na matatizo yaliyonipata kutokana na mipango ya hila ya Wayahudi.
<scripture passage="Acts 20:20" parsed="|Acts|20|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.20" />
<sup>20</sup>Mnajua kwamba sikusita hata kidogo kuwahubiria hadharani na nyumbani mwenu na kuwafundisha chochote ambacho kingewasaidieni.
<scripture passage="Acts 20:21" parsed="|Acts|20|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.21" />
<sup>21</sup>Niliwaonya wote--Wayahudi kadhalika na watu wa mataifa, wamgeukie Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu.
<scripture passage="Acts 20:22" parsed="|Acts|20|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.22" />
<sup>22</sup>Sasa, sikilizeni! Mimi, nikiwa ninamtii Roho, nakwenda Yerusalemu bila kufahamu yatakayonipata huko.
<scripture passage="Acts 20:23" parsed="|Acts|20|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.23" />
<sup>23</sup>Ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu ananithibitishia katika kila mji kwamba vifungo na mateso ndivyo vinavyoningojea.
<scripture passage="Acts 20:24" parsed="|Acts|20|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.24" />
<sup>24</sup>Lakini, siuthamini uhai wangu kuwa ni kitu sana kwangu. Nataka tu nikamilishe ule utume wangu na kumaliza ile kazi aliyonipa Bwana Yesu niifanye, yaani nitangaze Habari Njema ya neema ya Mungu.
<scripture passage="Acts 20:25" parsed="|Acts|20|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.25" />
<sup>25</sup>"Nimekuwa nikienda huko na huko kati yenu nikiuhubiri Ufalme wa Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.
<scripture passage="Acts 20:26" parsed="|Acts|20|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.26" />
<sup>26</sup>Hivyo, leo hii ninawathibitishieni rasmi kwamba ikijatokea akapotea mmoja wenu, mimi sina lawama yoyote.
<scripture passage="Acts 20:27" parsed="|Acts|20|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.27" />
<sup>27</sup>Kwa maana sikusita hata kidogo kuwatangazieni azimio lote la Mungu.
<scripture passage="Acts 20:28" parsed="|Acts|20|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.28" />
<sup>28</sup>Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo amejipatia kwa damu ya Mwanae.
<scripture passage="Acts 20:29" parsed="|Acts|20|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.29" />
<sup>29</sup>Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
<scripture passage="Acts 20:30" parsed="|Acts|20|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.30" />
<sup>30</sup>Hata kutoka miongoni mwenu watatokea watu ambao watasema mambo ya uongo ili kuwapotosha watu na kuwafanya wawafuate wao tu.
<scripture passage="Acts 20:31" parsed="|Acts|20|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.31" />
<sup>31</sup>Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi.
<scripture passage="Acts 20:32" parsed="|Acts|20|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.32" />
<sup>32</sup>"Na sasa basi, ninawaweka ninyi chini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga ninyi na kuwawezesha mzipate zile baraka alizowawekea watu wake.
<scripture passage="Acts 20:33" parsed="|Acts|20|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.33" />
<sup>33</sup>Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote.
<scripture passage="Acts 20:34" parsed="|Acts|20|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.34" />
<sup>34</sup>Mnajua ninyi wenyewe kwamba nimefanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na ya wenzangu.
<scripture passage="Acts 20:35" parsed="|Acts|20|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.35" />
<sup>35</sup>Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: `Heri zaidi kutoa kuliko kupokea."`
<scripture passage="Acts 20:36" parsed="|Acts|20|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.36" />
<sup>36</sup>Baada ya kusema hayo, Paulo alipiga magoti pamoja nao wote, akasali.
<scripture passage="Acts 20:37" parsed="|Acts|20|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.37" />
<sup>37</sup>Wote walikuwa wanalia; wakamwaga kwa kumkumbatia na kumbusu.
<scripture passage="Acts 20:38" parsed="|Acts|20|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.20.38" />
<sup>38</sup>Jambo lililowahuzunisha zaidi lilikuwa neno alilosema kwamba hawangemwona tena. Basi, wakamsindikiza hadi melini.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 21" progress="54.01%" prev="Acts.20" next="Acts.22" id="Acts.21">
<h3 id="Acts.21-p0.1">Chapter 21</h3>
<p id="Acts.21-p1">
<scripture passage="Acts 21:1" parsed="|Acts|21|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.1" />
<sup>1</sup>Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake tulifika Rodo, na kutoka huko tulikwenda Patara.
<scripture passage="Acts 21:2" parsed="|Acts|21|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.2" />
<sup>2</sup>Huko, tulikuta meli iliyokuwa inakwenda Foinike, hivyo tulipanda, tukasafiri.
<scripture passage="Acts 21:3" parsed="|Acts|21|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.3" />
<sup>3</sup>Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
<scripture passage="Acts 21:4" parsed="|Acts|21|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.4" />
<sup>4</sup>Tulikuta waumini huko, tukakaa pamoja nao kwa muda wa juma moja. Waumini hao wakawa waongea kwa nguvu ya Roho, wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 21:5" parsed="|Acts|21|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.5" />
<sup>5</sup>Lakini muda wetu ulipokwisha tuliondoka. Wote pamoja na wanawake na watoto wao walitusindikiza mpaka nje ya mji. Tulipofika pwani, sote tulipiga magoti tukasali.
<scripture passage="Acts 21:6" parsed="|Acts|21|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.6" />
<sup>6</sup>Kisha tuliagana; sisi tukapanda meli nao wakarudi makwao.
<scripture passage="Acts 21:7" parsed="|Acts|21|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.7" />
<sup>7</sup>Sisi tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai ambapo tuliwasalimu ndugu zetu, tukakaa nao siku moja.
<scripture passage="Acts 21:8" parsed="|Acts|21|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.8" />
<sup>8</sup>Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisarea tulikwenda nyumbani kwa mhubiri Filipo. Yeye alikuwa mmoja wa wale saba waliochaguliwa kule Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 21:9" parsed="|Acts|21|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.9" />
<sup>9</sup>Alikuwa na binti watatu ambao walikuwa na kipaji cha unabii.
<scripture passage="Acts 21:10" parsed="|Acts|21|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.10" />
<sup>10</sup>Baada ya kukaa huko siku kadhaa, nabii mmoja aitwaye Agabo alifika kutoka Yudea.
<scripture passage="Acts 21:11" parsed="|Acts|21|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.11" />
<sup>11</sup>Alitujia, akachukua mkanda wa Paulo, akajifunga mikono na miguu, akasema "Roho Mtakatifu asema hivi: `Wayahudi kule Yerusalemu watamfunga namna hii mtu mwenye ukanda na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa."`
<scripture passage="Acts 21:12" parsed="|Acts|21|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.12" />
<sup>12</sup>Tuliposikia hayo, sisi na wale watu wengine waliokuwa hapo tulimsihi Paulo asiende Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 21:13" parsed="|Acts|21|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.13" />
<sup>13</sup>Lakini yeye alijibu, "Mnataka kufanya nini? Mnataka kuvunja moyo wangu kwa machozi? Niko tayari siyo tu kutiwa ndani kule Yerusalemu, ila hata kufa kwa ajili ya Bwana Yesu."
<scripture passage="Acts 21:14" parsed="|Acts|21|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.14" />
<sup>14</sup>Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: "Mapenzi ya Bwana yafanyike"
<scripture passage="Acts 21:15" parsed="|Acts|21|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.15" />
<sup>15</sup>Baada ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safari kwenda Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 21:16" parsed="|Acts|21|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.16" />
<sup>16</sup>Wengine kati ya wale wafuasi wa Kaisarea walienda pamoja nasi, wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda. Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa muumini kwa siku nyingi.
<scripture passage="Acts 21:17" parsed="|Acts|21|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.17" />
<sup>17</sup>Tulipofika Yerusalemu, ndugu waumini walitupokea vizuri sana.
<scripture passage="Acts 21:18" parsed="|Acts|21|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.18" />
<sup>18</sup>Kesho yake Paulo alikwenda pamoja nasi kumwamkia Yakobo, na wazee wote wa kanisa walikuwako pia.
<scripture passage="Acts 21:19" parsed="|Acts|21|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.19" />
<sup>19</sup>Baada ya kuwasalimu, Paulo aliwapa taarifa kamili kuhusu yote Mungu aliyokuwa ametenda kati ya mataifa kwa njia ya utumishi wake.
<scripture passage="Acts 21:20" parsed="|Acts|21|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.20" />
<sup>20</sup>Waliposikia hayo, walimtukuza Mungu. Kisha wakamwambia Paulo, "Ndugu, unaweza kuona kwamba kuna maelfu ya Wayahudi ambao sasa wamekuwa waumini na wote hao wanashika kwa makini Sheria ya Mose.
<scripture passage="Acts 21:21" parsed="|Acts|21|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.21" />
<sup>21</sup>Wamepata habari zako kwamba umekuwa ukiwafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya mataifa mengine kuwa wasiijali Sheria ya Mose, wasiwatahiri watoto wao na kwamba wasizifuate mila za Wayahudi.
<scripture passage="Acts 21:22" parsed="|Acts|21|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.22" />
<sup>22</sup>Sasa, mambo yatakuwaje? Ni dhahiri kuwa watapata habari kwamba umekwisha wasili hapa.
<scripture passage="Acts 21:23" parsed="|Acts|21|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.23" />
<sup>23</sup>Basi, fanya kama tunavyokushauri. Tunao hapa watu wanne ambao wameweka nadhiri.
<scripture passage="Acts 21:24" parsed="|Acts|21|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.24" />
<sup>24</sup>Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya Sheria za Mose.
<scripture passage="Acts 21:25" parsed="|Acts|21|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.25" />
<sup>25</sup>Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: wasile chochote kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati."
<scripture passage="Acts 21:26" parsed="|Acts|21|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.26" />
<sup>26</sup>Basi, kesho yake Paulo aliwachukua wale watu akafanya ibada ya kujitakasa pamoja nao. Kisha akaingia Hekaluni kutoa taarifa kuhusu mwisho wa siku za kujitakasa na kuhusu dhabihu itakayotolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.
<scripture passage="Acts 21:27" parsed="|Acts|21|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.27" />
<sup>27</sup>Wakati siku hizo saba zilipokaribia kuisha, Wayahudi waliokuwa wametoka katika mkoa wa Asia walimwona Paulo Hekaluni. Wakachochea hasira kati ya kundi lote la watu, wakamtia nguvuni
<scripture passage="Acts 21:28" parsed="|Acts|21|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.28" />
<sup>28</sup>wakipiga kelele: "Wananchi wa Israeli, msaada, msaada! Huyu ndiye yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo yanayopinga watu wa Israeli, yanayopinga Sheria ya Mose na mahali hapa patakatifu. Hata sasa amewaingiza watu wa mataifa mengine Hekaluni na kupatia najisi mahali hapa patakatifu."
<scripture passage="Acts 21:29" parsed="|Acts|21|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.29" />
<sup>29</sup>Sababu ya kusema hivyo ni kwamba walikuwa wamemwona Trofimo mwenyeji, wa Efeso, akiwa pamoja na Paulo mjini, wakadhani kwamba Paulo alikuwa amemwingiza Hekaluni.
<scripture passage="Acts 21:30" parsed="|Acts|21|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.30" />
<sup>30</sup>Mji wote ulienea ghasia; watu wakaja kutoka pande zote, wakamkamata Paulo, wakamburuta, wakamtoa nje ya Hekalu na papo hapo milango ya Hekalu ikafungwa.
<scripture passage="Acts 21:31" parsed="|Acts|21|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.31" />
<sup>31</sup>Walikuwa tayari kumuua, lakini habari zilimfikia mkuu wa jeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.
<scripture passage="Acts 21:32" parsed="|Acts|21|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.32" />
<sup>32</sup>Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.
<scripture passage="Acts 21:33" parsed="|Acts|21|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.33" />
<sup>33</sup>Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na kuamuru afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, "Ni mtu gani huyu, na amefanya nini?"
<scripture passage="Acts 21:34" parsed="|Acts|21|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.34" />
<sup>34</sup>Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.
<scripture passage="Acts 21:35" parsed="|Acts|21|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.35" />
<sup>35</sup>Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
<scripture passage="Acts 21:36" parsed="|Acts|21|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.36" />
<sup>36</sup>Kwa maana kundi kubwa la watu walimfuata wakipiga kelele, "Muulie mbali!" ic
<scripture passage="Acts 21:37" parsed="|Acts|21|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.37" />
<sup>37</sup>Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa jeshi akisema, "Naweza kukwambia kitu?" Yule mkuu wa jeshi akamjibu, "Je unajua Kigiriki?
<scripture passage="Acts 21:38" parsed="|Acts|21|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.38" />
<sup>38</sup>Kwani wewe si yule Mmisri ambaye hivi majuzi alianzisha uasi na kuwaongoza majahili elfu nne hadi jangwani?"
<scripture passage="Acts 21:39" parsed="|Acts|21|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.39" />
<sup>39</sup>Paulo akajibu, "Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia; mimi ni raia wa mji maarufu. Tafadhali, niruhusu niongee na watu.
<scripture passage="Acts 21:40" parsed="|Acts|21|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.21.40" />
<sup>40</sup>Yule mkuu wa jeshi akamruhusu. Hivyo Paulo alisimama juu ya ngazi, akawapungia mkono wale watu na walipokaa kimya, akaanza kuongea nao kwa Kiebrania.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 22" progress="54.62%" prev="Acts.21" next="Acts.23" id="Acts.22">
<h3 id="Acts.22-p0.1">Chapter 22</h3>
<p id="Acts.22-p1">
<scripture passage="Acts 22:1" parsed="|Acts|22|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.1" />
<sup>1</sup>"Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni sasa nikijitetea mbele yenu!"
<scripture passage="Acts 22:2" parsed="|Acts|22|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.2" />
<sup>2</sup>Waliposikia akiongea nao kwa Kiebrania wakazidi kukaa kimya zaidi kuliko hapo awali. Naye Paulo akaendelea kusema,
<scripture passage="Acts 22:3" parsed="|Acts|22|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.3" />
<sup>3</sup>"Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti Sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama ninyi wenyewe mlivyo hivi leo.
<scripture passage="Acts 22:4" parsed="|Acts|22|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.4" />
<sup>4</sup>Niliwatesa hata kuwaua wale watu waliofuata Njia hii. Niliwatia nguvuni wanaume kwa wanawake na kuwafunga gerezani.
<scripture passage="Acts 22:5" parsed="|Acts|22|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.5" />
<sup>5</sup>Kuhani Mkuu na baraza lote la wazee wanaweza kushuhudia jambo hilo. Kutoka kwao nilipokea barua walioandikiwa wale ndugu Wayahudi waliokuwa huko Damasko. Nilikwenda Damasko ili niwatie nguvuni watu hao na kuwaleta wamefungwa mpaka Yerusalemu ili waadhibiwe.
<scripture passage="Acts 22:6" parsed="|Acts|22|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.6" />
<sup>6</sup>"Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote.
<scripture passage="Acts 22:7" parsed="|Acts|22|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.7" />
<sup>7</sup>Hapo nilianguka chini, nikasikia sauti ikiniambia: `Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?`
<scripture passage="Acts 22:8" parsed="|Acts|22|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.8" />
<sup>8</sup>Nami nikauliza: `Nani wewe, Bwana?` Naye akaniambia: `Mimi ni Yesu wa Nazareti ambaye wewe unamtesa.`
<scripture passage="Acts 22:9" parsed="|Acts|22|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.9" />
<sup>9</sup>Wale wenzangu waliuona ule mwanga lakini hawakusikia sauti ya yule aliyeongea nami.
<scripture passage="Acts 22:10" parsed="|Acts|22|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.10" />
<sup>10</sup>Basi, mimi nikauliza: `Nifanye nini Bwana?` Naye Bwana akaniambia: `Simama, nenda Damasko na huko utaambiwa yote ambayo umepangiwa kufanya.`
<scripture passage="Acts 22:11" parsed="|Acts|22|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.11" />
<sup>11</sup>Kutokana na ule mwanga mkali sikuweza kuona na hivyo iliwabidi wale wenzangu kuniongoza kwa kunishika mkono mpaka nikafika Damasko.
<scripture passage="Acts 22:12" parsed="|Acts|22|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.12" />
<sup>12</sup>"Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii Sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.
<scripture passage="Acts 22:13" parsed="|Acts|22|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.13" />
<sup>13</sup>Yeye alikuja kuniona, akasimama karibu nami, akasema: `Ndugu Saulo! Ona tena.` Papo hapo nikaona tena, nikamwangalia.
<scripture passage="Acts 22:14" parsed="|Acts|22|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.14" />
<sup>14</sup>Halafu Anania akasema: `Mungu wa babu zetu amekuchagua upate kujua matakwa yake na kumwona yule mtumishi wake mwadilifu na kumsikia yeye mwenyewe akiongea.
<scripture passage="Acts 22:15" parsed="|Acts|22|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.15" />
<sup>15</sup>Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona na kuyasikia.
<scripture passage="Acts 22:16" parsed="|Acts|22|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.16" />
<sup>16</sup>Sasa basi, ya nini kukawia zaidi? Simama ubatizwe na uondolewe dhambi zako kwa kuliungama jina lake.`
<scripture passage="Acts 22:17" parsed="|Acts|22|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.17" />
<sup>17</sup>"Basi, nilirudi Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali Hekaluni, niliona maono.
<scripture passage="Acts 22:18" parsed="|Acts|22|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.18" />
<sup>18</sup>Nilimwona Bwana akiniambia: `Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa maana watu wa hapa binadamu hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.`
<scripture passage="Acts 22:19" parsed="|Acts|22|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.19" />
<sup>19</sup>Nami nikamjibu: `Bwana, wao wanajua wazi kwamba mimi ni yule aliyekuwa anapitapita katika masunagogi na kuwatia nguvuni na kuwapiga wale waliokuwa wanakuamini.
<scripture passage="Acts 22:20" parsed="|Acts|22|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.20" />
<sup>20</sup>Na kwamba wakati shahidi wako Stefano alipouawa, mimi binafsi nilikuwako pale nikakubaliana na kitendo hicho na kuyalinda makoti ya wale waliokuwa wanamuua.`
<scripture passage="Acts 22:21" parsed="|Acts|22|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.21" />
<sup>21</sup>Naye Bwana akaniambia: `Nenda; ninakutuma mbali kwa mataifa mengine."`
<scripture passage="Acts 22:22" parsed="|Acts|22|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.22" />
<sup>22</sup>Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiza, lakini aliposema maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, "Mwondoe duniani! Mtu wa namna hiyo hastahili kuishi."
<scripture passage="Acts 22:23" parsed="|Acts|22|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.23" />
<sup>23</sup>Waliendelea kupayukapayuka huku wakitikisa makoti yao na kurusha vumbi angani.
<scripture passage="Acts 22:24" parsed="|Acts|22|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.24" />
<sup>24</sup>Mkuu wa jeshi aliwaamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome, akawaambia wamchape viboko ili wapate kujua kisa cha Wayahudi kumpigia kelele.
<scripture passage="Acts 22:25" parsed="|Acts|22|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.25" />
<sup>25</sup>Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza jemadari mmoja aliyesimama hapo, "Je, ni halali kwenu kumpiga viboko raia wa Roma kabla hajahukumiwa?"
<scripture passage="Acts 22:26" parsed="|Acts|22|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.26" />
<sup>26</sup>Yule jemadari aliposikia hayo, alimpasha habari mkuu wa jeshi akisema, "Unataka kufanya nini? Mtu huyu ni raia wa Roma!"
<scripture passage="Acts 22:27" parsed="|Acts|22|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.27" />
<sup>27</sup>Basi, mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamwambia, "Niambie; je, wewe ni raia wa Roma?" Paulo akamjibu, "Naam."
<scripture passage="Acts 22:28" parsed="|Acts|22|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.28" />
<sup>28</sup>Mkuu wa jeshi akasema, "Mimi nami nimekuwa raia wa Roma kwa kulipa gharama kubwa." Paulo akasema, "Lakini mimi ni raia wa Roma kwa kuzaliwa."
<scripture passage="Acts 22:29" parsed="|Acts|22|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.29" />
<sup>29</sup>Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.
<scripture passage="Acts 22:30" parsed="|Acts|22|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.22.30" />
<sup>30</sup>Kesho yake, mkuu wa jeshi alitaka kujua mashtaka kamili ambayo Wayahudi walikuwa wamemwekea Paulo. Hivyo, alimfungua Paulo minyororo, akaamuru makuhani wakuu na Baraza lote wafanye kikao. Kisha alimleta Paulo, akamsimamisha mbele ya Baraza.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 23" progress="55.05%" prev="Acts.22" next="Acts.24" id="Acts.23">
<h3 id="Acts.23-p0.1">Chapter 23</h3>
<p id="Acts.23-p1">
<scripture passage="Acts 23:1" parsed="|Acts|23|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.1" />
<sup>1</sup>Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema, "Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele ya Mungu."
<scripture passage="Acts 23:2" parsed="|Acts|23|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.2" />
<sup>2</sup>Hapo Kuhani Mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wampige kofi mdomoni.
<scripture passage="Acts 23:3" parsed="|Acts|23|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.3" />
<sup>3</sup>Basi, Paulo akamwambia, "Mungu mwenyewe atakupiga kofi wewe uliye kama ukuta uliopakwa chokaa! Unawezaje kukaa hapo ili unihukumu kisheria na huku wewe mwenyewe unaivunja Sheria kwa kuamuru nipigwe?"
<scripture passage="Acts 23:4" parsed="|Acts|23|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.4" />
<sup>4</sup>Watu waliokuwa wamesimama pale wakamwambia Paulo, "Unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu!"
<scripture passage="Acts 23:5" parsed="|Acts|23|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.5" />
<sup>5</sup>Paulo akajibu, "Ndugu zangu, sikujua kama yeye ni Kuhani Mkuu. Maana Maandiko yasema hivi: `Usiseme vibaya juu ya mtawala wa watu wako."`
<scripture passage="Acts 23:6" parsed="|Acts|23|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.6" />
<sup>6</sup>Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaaza sauti yake mbele ya Baraza: "Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu watafufuka."
<scripture passage="Acts 23:7" parsed="|Acts|23|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.7" />
<sup>7</sup>Baada ya kusema hivyo, mzozo mkali ulitokea kati ya Mafarisayo na Masadukayo na mkutano ukagawanyika sehemu mbili.
<scripture passage="Acts 23:8" parsed="|Acts|23|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.8" />
<sup>8</sup>Kisa chenyewe kilikuwa hiki: Masadukayo hushikilia kwamba wafu hawafufuki, hakuna malaika, na roho nazo hazipo. Lakini Mafarisayo husadiki hayo yote matatu.
<scripture passage="Acts 23:9" parsed="|Acts|23|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.9" />
<sup>9</sup>Kelele ziliongezeka na baadhi ya walimu wa Sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: "Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye."
<scripture passage="Acts 23:10" parsed="|Acts|23|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.10" />
<sup>10</sup>Mzozo ulizidi kuwa mwingi hata mkuu wa jeshi akaogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipandevipande. Kwa hiyo, aliwaamuru askari wake kuingia kati ya lile kundi, wamtoe Paulo na kumrudisha ndani ya ngome.
<scripture passage="Acts 23:11" parsed="|Acts|23|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.11" />
<sup>11</sup>Usiku uliofuata, Bwana alisimama karibu na Paulo, akamwambia, "Jipe moyo! Umenishuhudia katika Yerusalemu, utafanya vivyo hivyo mjini Roma."
<scripture passage="Acts 23:12" parsed="|Acts|23|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.12" />
<sup>12</sup>Kulipokucha, Wayahudi walifanya kikao cha faragha. Wakala kiapo: "Hatutakula wala kunywa mpaka tutakapokuwa tumekwisha muua Paulo."
<scripture passage="Acts 23:13" parsed="|Acts|23|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.13" />
<sup>13</sup>Watu zaidi ya arobaini ndio waliokula njama kufanya hivyo.
<scripture passage="Acts 23:14" parsed="|Acts|23|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.14" />
<sup>14</sup>Basi, walikwenda kwa makuhani wakuu na wazee, wakasema, "Sisi tumeapa kwamba hatutaonja chochote kwa vinywa vyetu mpaka hapo tutakapokuwa tumemuua Paulo.
<scripture passage="Acts 23:15" parsed="|Acts|23|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.15" />
<sup>15</sup>Sasa basi, ninyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumuua hata kabla hajafika karibu."
<scripture passage="Acts 23:16" parsed="|Acts|23|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.16" />
<sup>16</sup>Lakini mtoto wa kiume wa dada yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
<scripture passage="Acts 23:17" parsed="|Acts|23|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.17" />
<sup>17</sup>Hapo Paulo akamwita mmoja wa askari, akamwambia, "Mchukue kijana huyu kwa mkuu wa jeshi; ana kitu cha kumwambia."
<scripture passage="Acts 23:18" parsed="|Acts|23|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.18" />
<sup>18</sup>Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, "Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukwambia."
<scripture passage="Acts 23:19" parsed="|Acts|23|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.19" />
<sup>19</sup>Mkuu wa jeshi alimshika huyo kijana mkono, akampeleka mahali pa faragha, akamwuliza, "Una nini cha kuniambia?"
<scripture passage="Acts 23:20" parsed="|Acts|23|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.20" />
<sup>20</sup>Yeye akasema, "Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
<scripture passage="Acts 23:21" parsed="|Acts|23|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.21" />
<sup>21</sup>Lakini wewe usikubali kwa maana kuna watu zaidi ya arobaini walio tayari kumvamia. Wameapa kutokula wala kunywa mpaka watakapokuwa wamemuua. Sasa wako tayari, wanangojea tu uamuzi wako."
<scripture passage="Acts 23:22" parsed="|Acts|23|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.22" />
<sup>22</sup>Mkuu wa jeshi alimwacha aende zake akimwonya asimwambie mtu yeyote kwamba amemletea habari hizo.
<scripture passage="Acts 23:23" parsed="|Acts|23|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.23" />
<sup>23</sup>Basi, mkuu wa jeshi aliwaita askari wawili akawaambia, "Wekeni tayari askari mia mbili, wapanda farasi sabini na askari mia mbili wa mikuki, waende Kaisarea; muwe tayari kuondoka kabla ya saa tatu leo usiku.
<scripture passage="Acts 23:24" parsed="|Acts|23|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.24" />
<sup>24</sup>Wekeni farasi kadhaa kwa ajili ya Paulo; mfikisheni salama kwa Felisi, mkuu wa mkoa."
<scripture passage="Acts 23:25" parsed="|Acts|23|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.25" />
<sup>25</sup>Halafu mkuu huyo wa jeshi akaandika barua hivi:
<scripture passage="Acts 23:26" parsed="|Acts|23|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.26" />
<sup>26</sup>"Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu wa mkoa. Salamu!
<scripture passage="Acts 23:27" parsed="|Acts|23|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.27" />
<sup>27</sup>"Wayahudi walimkamata mtu huyu na karibu wangemuua kama nisingalifahamishwa kwamba yeye ni raia wa Roma na hivyo nikaenda pamoja na askari nikamwokoa.
<scripture passage="Acts 23:28" parsed="|Acts|23|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.28" />
<sup>28</sup>Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao.
<scripture passage="Acts 23:29" parsed="|Acts|23|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.29" />
<sup>29</sup>Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za Sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
<scripture passage="Acts 23:30" parsed="|Acts|23|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.30" />
<sup>30</sup>Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumuua, niliamua kumleta kwako. Nikamwambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako."
<scripture passage="Acts 23:31" parsed="|Acts|23|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.31" />
<sup>31</sup>Basi, hao askari walimchukua Paulo kama walivyoamriwa; wakampeleka usiku uleule mpaka Antipatri.
<scripture passage="Acts 23:32" parsed="|Acts|23|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.32" />
<sup>32</sup>Kesho yake askari wa miguu walirudi ngomeni, wakawaacha wale askari wapanda farasi waendelee na safari pamoja na Paulo.
<scripture passage="Acts 23:33" parsed="|Acts|23|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.33" />
<sup>33</sup>Walipofika Kaisarea walimpa mkuu wa mkoa ile barua na kumweka Paulo chini ya mamlaka yake.
<scripture passage="Acts 23:34" parsed="|Acts|23|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.34" />
<sup>34</sup>Felisi alipoisoma hiyo barua aliwauliza Paulo ametoka mkoa gani. Alipofahamishwa kwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia,
<scripture passage="Acts 23:35" parsed="|Acts|23|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.23.35" />
<sup>35</sup>akasema, "Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika." Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 24" progress="55.56%" prev="Acts.23" next="Acts.25" id="Acts.24">
<h3 id="Acts.24-p0.1">Chapter 24</h3>
<p id="Acts.24-p1">
<scripture passage="Acts 24:1" parsed="|Acts|24|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.1" />
<sup>1</sup>Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
<scripture passage="Acts 24:2" parsed="|Acts|24|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.2" />
<sup>2</sup>Paulo aliitwa na Tertulo akafungua mashtaka hivi: "Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
<scripture passage="Acts 24:3" parsed="|Acts|24|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.3" />
<sup>3</sup>Tunalipokea jambo hili kwa furaha daima na kutoa shukrani nyingi kwako kila mahali.
<scripture passage="Acts 24:4" parsed="|Acts|24|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.4" />
<sup>4</sup>Lakini, bila kupoteza wakati wako zaidi, tunakusihi kwa wema wako, usikilize taarifa yetu fupi.
<scripture passage="Acts 24:5" parsed="|Acts|24|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.5" />
<sup>5</sup>Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama cha Wanazareti.
<scripture passage="Acts 24:6" parsed="|Acts|24|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.6" />
<sup>6</sup>Tena alijaribu kulikufuru Hekalu nasi tukamtia nguvuni. Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo."<i>fc</i>
<scripture passage="Acts 24:7" parsed="|Acts|24|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.7" />
<sup>7</sup>missing
<scripture passage="Acts 24:8" parsed="|Acts|24|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.8" />
<sup>8</sup>missing
<scripture passage="Acts 24:9" parsed="|Acts|24|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.9" />
<sup>9</sup>Nao Wayahudi waliunga mkono mashtaka hayo wakisema kwamba hayo yote yalikuwa kweli. jeshi, aliingilia kati, akamchukua kwa nguvu kutoka mikononi mwetu. 8 Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.
<scripture passage="Acts 24:10" parsed="|Acts|24|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.10" />
<sup>10</sup>Basi, mkuu wa mkoa alimwashiria Paulo aseme. Naye Paulo akasema, "Nafurahi kujitetea mbele yako nikijua kwamba umekuwa hakimu wa taifa hili kwa miaka mingi.
<scripture passage="Acts 24:11" parsed="|Acts|24|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.11" />
<sup>11</sup>Unaweza kujihakikishia kwamba si zaidi ya siku kumi na mbili tu zimepita tangu nilipokwenda kuabudu Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 24:12" parsed="|Acts|24|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.12" />
<sup>12</sup>Wayahudi hawakunikuta nikijadiliana na mtu yeyote. Hawakunikuta nikichochea watu Hekaluni wala katika masunagogi yao, wala mahali pengine popote katika mji huo.
<scripture passage="Acts 24:13" parsed="|Acts|24|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.13" />
<sup>13</sup>Wala hawawezi kuthibitisha mashtaka waliyotoa juu yangu.
<scripture passage="Acts 24:14" parsed="|Acts|24|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.14" />
<sup>14</sup>Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu na wazee wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na manabii.
<scripture passage="Acts 24:15" parsed="|Acts|24|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.15" />
<sup>15</sup>Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo, kwamba watu, wema na wabaya, watafufuka.
<scripture passage="Acts 24:16" parsed="|Acts|24|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.16" />
<sup>16</sup>Kwa hiyo ninajitahidi daima kuwa na dhamiri njema mbele ya Mungu na mbele ya watu.
<scripture passage="Acts 24:17" parsed="|Acts|24|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.17" />
<sup>17</sup>"Baada ya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudi Yerusalemu ili kuwapelekea wananchi wenzangu msaada na kutoa dhabihu.
<scripture passage="Acts 24:18" parsed="|Acts|24|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.18" />
<sup>18</sup>Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta Hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
<scripture passage="Acts 24:19" parsed="|Acts|24|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.19" />
<sup>19</sup>Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
<scripture passage="Acts 24:20" parsed="|Acts|24|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.20" />
<sup>20</sup>Au, waache hawa walio hapa waseme kosa waliloliona kwangu wakati niliposimama mbele ya Baraza lao kuu,
<scripture passage="Acts 24:21" parsed="|Acts|24|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.21" />
<sup>21</sup>isipokuwa tu maneno haya niliyosema niliposimama mbele yao: `Mnanihukumu leo hii kwa sababu ya kushikilia kwamba wafu watafufuliwa!"`
<scripture passage="Acts 24:22" parsed="|Acts|24|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.22" />
<sup>22</sup>Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo Njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, "Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Luisa, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa."
<scripture passage="Acts 24:23" parsed="|Acts|24|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.23" />
<sup>23</sup>Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
<scripture passage="Acts 24:24" parsed="|Acts|24|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.24" />
<sup>24</sup>Baada ya siku chache, Felisi alifika pamoja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Aliamuru Paulo aletwe, akamsikiliza akiongea juu ya kumwamini Yesu Kristo.
<scripture passage="Acts 24:25" parsed="|Acts|24|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.25" />
<sup>25</sup>Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu ya kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa, akasema, "Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata nafasi."
<scripture passage="Acts 24:26" parsed="|Acts|24|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.26" />
<sup>26</sup>Wakati huohuo alikuwa anatumaini kwamba Paulo angempa fedha. Kwa sababu hii alimwita Paulo mara kwa mara na kuzungumza naye.
<scripture passage="Acts 24:27" parsed="|Acts|24|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.24.27" />
<sup>27</sup>Baada ya miaka miwili, Porkio Festo alichukua nafasi ya Felisi, akawa mkuu wa Mkoa. Kwa kuwa alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, Felisi alimwacha Paulo kizuizini.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 25" progress="55.94%" prev="Acts.24" next="Acts.26" id="Acts.25">
<h3 id="Acts.25-p0.1">Chapter 25</h3>
<p id="Acts.25-p1">
<scripture passage="Acts 25:1" parsed="|Acts|25|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.1" />
<sup>1</sup>Siku tatu baada ya kufika mkoani, Festo alitoka Kaisarea, akaenda Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 25:2" parsed="|Acts|25|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.2" />
<sup>2</sup>Makuhani wakuu pamoja na viongozi wa Wayahudi walimpa habari kuhusu mashtaka yaliyokuwa yanamkabili Paulo. Walimsihi Festo
<scripture passage="Acts 25:3" parsed="|Acts|25|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.3" />
<sup>3</sup>awafanyie fadhili kwa kumleta Paulo Yerusalemu; walikuwa wamekula njama wamuue akiwa njiani.
<scripture passage="Acts 25:4" parsed="|Acts|25|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.4" />
<sup>4</sup>Lakini Festo alijibu, "Paulo atabaki kizuizini kule Kaisarea na mimi nitakwenda huko karibuni.
<scripture passage="Acts 25:5" parsed="|Acts|25|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.5" />
<sup>5</sup>Waacheni viongozi wenu waende huko pamoja nami wakatoe mashtaka yao juu yake kama amefanya chochote kiovu."
<scripture passage="Acts 25:6" parsed="|Acts|25|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.6" />
<sup>6</sup>Festo alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi hivi, kisha akarudi Kaisarea. Kesho yake alikwenda barazani, akaamuru Paulo aletwe ndani.
<scripture passage="Acts 25:7" parsed="|Acts|25|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.7" />
<sup>7</sup>Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
<scripture passage="Acts 25:8" parsed="|Acts|25|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.8" />
<sup>8</sup>Kwa kujitetea, Paulo alisema, "Mimi sikufanya kosa lolote kuhusu Sheria ya Wayahudi, wala kuhusu Hekalu, wala kumhusu Kaisari."
<scripture passage="Acts 25:9" parsed="|Acts|25|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.9" />
<sup>9</sup>Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi na hivyo akamwuliza Paulo, "Je, ungependa kwenda Yerusalemu na huko ukahukumiwe mbele yangu kuhusu mashtaka haya?"
<scripture passage="Acts 25:10" parsed="|Acts|25|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.10" />
<sup>10</sup>Paulo akajibu, "Nasimama mbele ya mahakama ya Kaisari na papa hapa ndipo ninapopaswa kupewa hukumu. Kama unavyojua vizuri, sikuwatendea Wayahudi ubaya wowote.
<scripture passage="Acts 25:11" parsed="|Acts|25|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.11" />
<sup>11</sup>Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!"
<scripture passage="Acts 25:12" parsed="|Acts|25|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.12" />
<sup>12</sup>Basi, baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia Paulo, "Umekata rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari."
<scripture passage="Acts 25:13" parsed="|Acts|25|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.13" />
<sup>13</sup>Siku chache baadaye, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisarea ili kutoa heshima zao kwa Festo.
<scripture passage="Acts 25:14" parsed="|Acts|25|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.14" />
<sup>14</sup>Walikuwa huko siku kadhaa naye Festo akamweleza mfalme kesi ya Paulo: "Kuna mtu mmoja hapa ambaye Felisi alimwacha kizuizini.
<scripture passage="Acts 25:15" parsed="|Acts|25|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.15" />
<sup>15</sup>Nilipokwenda Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walimshtaki na kuniomba nimhukumu.
<scripture passage="Acts 25:16" parsed="|Acts|25|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.16" />
<sup>16</sup>Lakini mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu aadhibiwe kabla mshtakiwa hajakutana na washtaki wake ana kwa ana na kupewa fursa ya kujitetea kuhusu hayo mashtaka.
<scripture passage="Acts 25:17" parsed="|Acts|25|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.17" />
<sup>17</sup>Basi, walipofika hapa sikukawia, ila nilifanya kikao mahakamani kesho yake, nikaamuru mtu huyo aletwe.
<scripture passage="Acts 25:18" parsed="|Acts|25|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.18" />
<sup>18</sup>Washtaki wake walisimama lakini hawakutoa mashtaka maovu kama nilivyokuwa ninatazamia.
<scripture passage="Acts 25:19" parsed="|Acts|25|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.19" />
<sup>19</sup>Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
<scripture passage="Acts 25:20" parsed="|Acts|25|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.20" />
<sup>20</sup>Sikujua la kufanya kuhusu shauri hilo. Basi, nilimwuliza Paulo kama angependa kwenda mahakamani kule Yerusalemu kwa ajili ya mashtaka hayo.
<scripture passage="Acts 25:21" parsed="|Acts|25|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.21" />
<sup>21</sup>Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari."
<scripture passage="Acts 25:22" parsed="|Acts|25|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.22" />
<sup>22</sup>Basi Agripa akamwambia Festo, "Ningependa kumsikia mtu huyu mimi mwenyewe." Festo akamwambia, "Utamsikia kesho."
<scripture passage="Acts 25:23" parsed="|Acts|25|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.23" />
<sup>23</sup>Hivyo, kesho yake, Agripa na Bernike walifika kwa shangwe katika ukumbi wa mkutano wakiwa wameandamana na wakuu wa majeshi na viongozi wa mji. Festo aliamuru Paulo aletwe ndani,
<scripture passage="Acts 25:24" parsed="|Acts|25|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.24" />
<sup>24</sup>Kisha akasema, "Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
<scripture passage="Acts 25:25" parsed="|Acts|25|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.25" />
<sup>25</sup>Lakini mimi sikuona kuwa alikuwa ametenda chochote kibaya hata astahili kupewa adhabu ya kifo. Lakini, kwa vile Paulo mwenyewe alikata rufani kwa Kaisari, niliamua kumpeleka.
<scripture passage="Acts 25:26" parsed="|Acts|25|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.26" />
<sup>26</sup>Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
<scripture passage="Acts 25:27" parsed="|Acts|25|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.25.27" />
<sup>27</sup>Kwa maana nadhani itakuwa kichekesho kumpeleka mfungwa bila kutaja wazi mashtaka yanayomkabili."
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 26" progress="56.33%" prev="Acts.25" next="Acts.27" id="Acts.26">
<h3 id="Acts.26-p0.1">Chapter 26</h3>
<p id="Acts.26-p1">
<scripture passage="Acts 26:1" parsed="|Acts|26|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.1" />
<sup>1</sup>Basi, Agripa akamwambia Paulo, "Unaruhusiwa kujitetea." Hapo Paulo alinyosha mkono wake akajitetea hivi:
<scripture passage="Acts 26:2" parsed="|Acts|26|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.2" />
<sup>2</sup>"Mfalme Agripa, ninajiona mwenye bahati leo kujitetea mbele yako kuhusu yale mashtaka yote ambayo Wayahudi walikuwa wamesema juu yangu.
<scripture passage="Acts 26:3" parsed="|Acts|26|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.3" />
<sup>3</sup>Hasa kwa vile wewe mwenyewe ni mtaalamu wa desturi za Wayahudi na migogoro yao, ninakuomba basi unisikilize kwa uvumilivu.
<scripture passage="Acts 26:4" parsed="|Acts|26|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.4" />
<sup>4</sup>"Wayahudi wanajua habari za maisha yangu tangu utoto, jinsi nilivyoishi tangu mwanzo kati ya taifa langu huko Yerusalemu.
<scripture passage="Acts 26:5" parsed="|Acts|26|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.5" />
<sup>5</sup>Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali zaidi katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
<scripture passage="Acts 26:6" parsed="|Acts|26|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.6" />
<sup>6</sup>Na sasa niko hapa nihukumiwe kwa sababu ninaitumainia ile ahadi ambayo Mungu aliwaahidia babu zetu.
<scripture passage="Acts 26:7" parsed="|Acts|26|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.7" />
<sup>7</sup>Ahadi hiyo ndiyo ileile inayotumainiwa na makabila kumi na mawili ya taifa letu, wakimtumikia Mungu kwa dhati mchana na usiku. Mheshimiwa mfalme, Wayahudi wananishtaki kwa sababu ya tumaini hilo!
<scripture passage="Acts 26:8" parsed="|Acts|26|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.8" />
<sup>8</sup>Kwa nini ninyi mnaona shida sana kuamini kwamba Mungu huwafufua wafu?
<scripture passage="Acts 26:9" parsed="|Acts|26|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.9" />
<sup>9</sup>Kwa kweli mimi mwenyewe niliamini kwamba ni wajibu wangu kufanya mambo mengi kulipinga jina la Yesu wa Nazareti.
<scripture passage="Acts 26:10" parsed="|Acts|26|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.10" />
<sup>10</sup>Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
<scripture passage="Acts 26:11" parsed="|Acts|26|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.11" />
<sup>11</sup>Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasaka mpaka miji ya mbali.
<scripture passage="Acts 26:12" parsed="|Acts|26|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.12" />
<sup>12</sup>"Kwa mujibu huohuo, nilikwenda Damasko wakati mmoja, nikiwa na mamlaka na maagizo kutoka kwa makuhani wakuu.
<scripture passage="Acts 26:13" parsed="|Acts|26|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.13" />
<sup>13</sup>Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
<scripture passage="Acts 26:14" parsed="|Acts|26|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.14" />
<sup>14</sup>Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: `Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda anayepiga teke fimbo ya bwana wake.`
<scripture passage="Acts 26:15" parsed="|Acts|26|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.15" />
<sup>15</sup>Mimi nikauliza: `Ni nani wewe Bwana?` Naye Bwana akajibu: `Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
<scripture passage="Acts 26:16" parsed="|Acts|26|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.16" />
<sup>16</sup>Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonyesha.
<scripture passage="Acts 26:17" parsed="|Acts|26|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.17" />
<sup>17</sup>Nitakuokoa na watu wa Israeli na watu wa mataifa mengine ambao mimi ninakutuma kwao.
<scripture passage="Acts 26:18" parsed="|Acts|26|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.18" />
<sup>18</sup>Utayafumbua macho yao na kuwawezesha watoke gizani na kuingia katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukie Mungu; ili kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu.`
<scripture passage="Acts 26:19" parsed="|Acts|26|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.19" />
<sup>19</sup>"Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuwa mkaidi kwa maono hilo la mbinguni.
<scripture passage="Acts 26:20" parsed="|Acts|26|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.20" />
<sup>20</sup>Ila nilianza kuhubiri kwanza kwa watu wa Damasko, halafu kwa wale wa Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine. Niliwahimiza wamgeukie Mungu na kuonyesha kwa vitendo kwamba wamebadilisha mioyo yao.
<scripture passage="Acts 26:21" parsed="|Acts|26|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.21" />
<sup>21</sup>Kwa sababu hiyo, Wayahudi walinikamata nikiwa Hekaluni, wakajaribu kuniua.
<scripture passage="Acts 26:22" parsed="|Acts|26|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.22" />
<sup>22</sup>Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;
<scripture passage="Acts 26:23" parsed="|Acts|26|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.23" />
<sup>23</sup>yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine."
<scripture passage="Acts 26:24" parsed="|Acts|26|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.24" />
<sup>24</sup>Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa sauti kubwa, "Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!"
<scripture passage="Acts 26:25" parsed="|Acts|26|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.25" />
<sup>25</sup>Lakini Paulo akasema, "Sina wazimu mheshimiwa Festo: Ninachosema ni ukweli mtupu.
<scripture passage="Acts 26:26" parsed="|Acts|26|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.26" />
<sup>26</sup>Wewe Mfalme unayafahamu mambo haya, kwa hiyo ninaweza kuongea bila uoga mbele yako. Sina mashaka kwamba matukio hayo yanajulikana kwako maana jambo hili halikutendeka mafichoni.
<scripture passage="Acts 26:27" parsed="|Acts|26|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.27" />
<sup>27</sup>Mfalme Agripa, je, una imani na manabii? Najua kwamba unaamini."
<scripture passage="Acts 26:28" parsed="|Acts|26|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.28" />
<sup>28</sup>Agripa akamjibu Paulo, "Kidogo tu utanifanya Mkristo!"
<scripture passage="Acts 26:29" parsed="|Acts|26|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.29" />
<sup>29</sup>Paulo akamjibu, "Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo."
<scripture passage="Acts 26:30" parsed="|Acts|26|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.30" />
<sup>30</sup>Hapo mfalme Agripa, mkuu wa mkoa, Bernike na wale wote waliokuwa pamoja nao, walisimama.
<scripture passage="Acts 26:31" parsed="|Acts|26|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.31" />
<sup>31</sup>Walipokwisha ondoka, waliambiana, "Mtu huyu hakufanya chochote kinachostahili adhabu ya kifo au kifungo."
<scripture passage="Acts 26:32" parsed="|Acts|26|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.26.32" />
<sup>32</sup>Naye Agripa akamwambia Festo, "Mtu huyu angeweza kufunguliwa kama asingalikuwa amekata rufani kwa Kaisari."
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 27" progress="56.79%" prev="Acts.26" next="Acts.28" id="Acts.27">
<h3 id="Acts.27-p0.1">Chapter 27</h3>
<p id="Acts.27-p1">
<scripture passage="Acts 27:1" parsed="|Acts|27|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.1" />
<sup>1</sup>Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho "Kikosi cha Augusto."
<scripture passage="Acts 27:2" parsed="|Acts|27|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.2" />
<sup>2</sup>Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa Makedonia kutoka Thesalonika, alikuwa pamoja nasi.
<scripture passage="Acts 27:3" parsed="|Acts|27|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.3" />
<sup>3</sup>Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
<scripture passage="Acts 27:4" parsed="|Acts|27|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.4" />
<sup>4</sup>Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepo haukuwa mwingi.
<scripture passage="Acts 27:5" parsed="|Acts|27|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.5" />
<sup>5</sup>Halafu tulivuka bahari ya Kilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura, mji wa Lukia.
<scripture passage="Acts 27:6" parsed="|Acts|27|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.6" />
<sup>6</sup>Hapo yule ofisa alikuta meli moja ya Aleksandria iliyokuwa inakwenda Italia, na hivyo akatupandisha ndani.
<scripture passage="Acts 27:7" parsed="|Acts|27|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.7" />
<sup>7</sup>Kwa muda wa siku nyingi tulisafiri polepole, na kwa shida tulifika karibu na Nido. Kwa sababu upepo ulikuwa bado unatupinga, tuliendelea mbele moja kwa moja tukapitia upande wa Krete karibu na rasi Salmone ambapo upepo haukuwa mwingi.
<scripture passage="Acts 27:8" parsed="|Acts|27|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.8" />
<sup>8</sup>Tulipita kando yake polepole tukafika mahali paitwapo "Bandari Nzuri", karibu na mji wa Lasea.
<scripture passage="Acts 27:9" parsed="|Acts|27|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.9" />
<sup>9</sup>Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
<scripture passage="Acts 27:10" parsed="|Acts|27|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.10" />
<sup>10</sup>"Waheshimiwa, nahisi kwamba safari hii itakuwa ya shida na hasara nyingi si kwa shehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu."
<scripture passage="Acts 27:11" parsed="|Acts|27|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.11" />
<sup>11</sup>Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni ya nahodha na ya mwenye meli kuliko yale aliyosema Paulo.
<scripture passage="Acts 27:12" parsed="|Acts|27|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.12" />
<sup>12</sup>Kwa kuwa bandari hiyo haikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wa baridi, wengi walipendelea kuendelea na safari, ikiwezekana mpaka Foinike. Foinike ni bandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibi na kaskazini-magharibi; na huko wangeweza kukaa wakati wa baridi.
<scripture passage="Acts 27:13" parsed="|Acts|27|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.13" />
<sup>13</sup>Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang`oa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
<scripture passage="Acts 27:14" parsed="|Acts|27|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.14" />
<sup>14</sup>Lakini haukupita muda, upepo mkali uitwao "Upepo wa Kaskazi" ulianza kuvuma kutoka kisiwani.
<scripture passage="Acts 27:15" parsed="|Acts|27|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.15" />
<sup>15</sup>Upepo uliipiga ile meli, na kwa kuwa hatukuweza kuukabili, tukaiacha ikokotwe na huo upepo.
<scripture passage="Acts 27:16" parsed="|Acts|27|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.16" />
<sup>16</sup>Kisiwa kimoja kiitwacho Kanda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
<scripture passage="Acts 27:17" parsed="|Acts|27|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.17" />
<sup>17</sup>Wale wanamaji waliuvuta mtumbwi ndani, kisha wakaizungushia meli kamba na kuifunga kwa nguvu. Waliogopa kwamba wangeweza kukwama kwenye ufuko wa bahari, pwani ya Libya. Kwa hiyo walishusha matanga na kuiacha meli ikokotwe na upepo.
<scripture passage="Acts 27:18" parsed="|Acts|27|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.18" />
<sup>18</sup>Dhoruba iliendelea kuvuma na kesho yake wakaanza kutupa nje shehena ya meli.
<scripture passage="Acts 27:19" parsed="|Acts|27|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.19" />
<sup>19</sup>Siku ya tatu, wakaanza pia kutupa majini vifaa vya meli kwa mikono yao wenyewe.
<scripture passage="Acts 27:20" parsed="|Acts|27|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.20" />
<sup>20</sup>Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
<scripture passage="Acts 27:21" parsed="|Acts|27|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.21" />
<sup>21</sup>Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati yao, akasema, "Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka shida hii na hasara hizi zote.
<scripture passage="Acts 27:22" parsed="|Acts|27|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.22" />
<sup>22</sup>Lakini sasa ninawaombeni muwe na moyo; hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake; meli tu ndiyo itakayopotea.
<scripture passage="Acts 27:23" parsed="|Acts|27|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.23" />
<sup>23</sup>Kwa maana jana usiku malaika wa yule Mungu ambaye mimi ni wake na ambaye mimi ninamwabudu alinitokea,
<scripture passage="Acts 27:24" parsed="|Acts|27|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.24" />
<sup>24</sup>akaniambia: `Paulo usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote wanaosafiri nawe wasiangamie.`
<scripture passage="Acts 27:25" parsed="|Acts|27|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.25" />
<sup>25</sup>Hivyo, waheshimiwa, jipeni moyo! Maana ninamwamini Mungu kwamba itakuwa sawa kama nilivyoambiwa.
<scripture passage="Acts 27:26" parsed="|Acts|27|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.26" />
<sup>26</sup>Lakini ni lazima tutatupwa ufukoni mwa kisiwa fulani."
<scripture passage="Acts 27:27" parsed="|Acts|27|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.27" />
<sup>27</sup>Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huku katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi kuwa karibu na nchi kavu.
<scripture passage="Acts 27:28" parsed="|Acts|27|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.28" />
<sup>28</sup>Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arobaini. Baadaye wakapima tena wakapata mita thelathini.
<scripture passage="Acts 27:29" parsed="|Acts|27|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.29" />
<sup>29</sup>Kwa sababu ya kuogopa kukwama kwenye miamba, waliteremsha nanga nne nyuma ya meli; wakaomba kuche upesi.
<scripture passage="Acts 27:30" parsed="|Acts|27|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.30" />
<sup>30</sup>Wanamaji walitaka kutoroka, na walikwisha kuteremsha ule mtumbwi majini, wakijisingizia kwamba wanakwenda kuteremsha nanga upande wa mbele wa meli.
<scripture passage="Acts 27:31" parsed="|Acts|27|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.31" />
<sup>31</sup>Lakini Paulo alimwambia yule ofisa wa jeshi na askari wake, "Kama wanamaji hawa hawabaki ndani ya meli, hamtaokoka."
<scripture passage="Acts 27:32" parsed="|Acts|27|32|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.32" />
<sup>32</sup>Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji.
<scripture passage="Acts 27:33" parsed="|Acts|27|33|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.33" />
<sup>33</sup>Karibu na alfajiri, Paulo aliwahimiza wote wale chakula: "Kwa siku kumi na nne sasa mmekuwa katika mashaka na bila kula; hamjala kitu chochote.
<scripture passage="Acts 27:34" parsed="|Acts|27|34|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.34" />
<sup>34</sup>Basi, ninawasihi mle chakula kwa maana mnakihitaji ili mweze kuendelea kuishi. Maana hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea."
<scripture passage="Acts 27:35" parsed="|Acts|27|35|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.35" />
<sup>35</sup>Baada ya kusema hivyo, Paulo alichukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.
<scripture passage="Acts 27:36" parsed="|Acts|27|36|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.36" />
<sup>36</sup>Hapo wote wakapata moyo, nao pia wakala chakula.
<scripture passage="Acts 27:37" parsed="|Acts|27|37|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.37" />
<sup>37</sup>Jumla tulikuwa watu mia mbili na sabini na sita katika meli.
<scripture passage="Acts 27:38" parsed="|Acts|27|38|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.38" />
<sup>38</sup>Baada ya kila mmoja kula chakula cha kutosha, walipunguza uzito wa meli kwa kutupa nafaka baharini.
<scripture passage="Acts 27:39" parsed="|Acts|27|39|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.39" />
<sup>39</sup>Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
<scripture passage="Acts 27:40" parsed="|Acts|27|40|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.40" />
<sup>40</sup>Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
<scripture passage="Acts 27:41" parsed="|Acts|27|41|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.41" />
<sup>41</sup>Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi.
<scripture passage="Acts 27:42" parsed="|Acts|27|42|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.42" />
<sup>42</sup>Askari walitaka kuwaua wafungwa wote kwa kuogopa kwamba wangeogelea hadi pwani na kutoroka.
<scripture passage="Acts 27:43" parsed="|Acts|27|43|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.43" />
<sup>43</sup>Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,
<scripture passage="Acts 27:44" parsed="|Acts|27|44|0|0" osisRef="Bible:Acts.27.44" />
<sup>44</sup>na wengine wafuate wakijishikilia kwenye mbao au kwenye vipande vya meli iliyovunjika. Ndivyo sisi sote tulivyofika salama pwani.
</p>
</div3>

<div3 title="Acts 28" progress="57.41%" prev="Acts.27" next="Rom" id="Acts.28">
<h3 id="Acts.28-p0.1">Chapter 28</h3>
<p id="Acts.28-p1">
<scripture passage="Acts 28:1" parsed="|Acts|28|1|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.1" />
<sup>1</sup>Tulipokwisha fika salama kwenye nchi kavu, tuligundua kwamba kile kisiwa kinaitwa Malta.
<scripture passage="Acts 28:2" parsed="|Acts|28|2|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.2" />
<sup>2</sup>Wenyeji wa hapo walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwa inaanza kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyo waliwasha moto, wakatukaribisha.
<scripture passage="Acts 28:3" parsed="|Acts|28|3|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.3" />
<sup>3</sup>Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
<scripture passage="Acts 28:4" parsed="|Acts|28|4|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.4" />
<sup>4</sup>Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaning`inia kwenye mkono wake waliambiana, "Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa ameokoka kuangamia baharini, `Haki` haitamwacha aendelee kuishi!"
<scripture passage="Acts 28:5" parsed="|Acts|28|5|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.5" />
<sup>5</sup>Lakini Paulo alikikung`utia kile kiumbe motoni na hakuumizwa hata kidogo.
<scripture passage="Acts 28:6" parsed="|Acts|28|6|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.6" />
<sup>6</sup>Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au hapohapo angeanguka chini na kufa. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa ni mungu.
<scripture passage="Acts 28:7" parsed="|Acts|28|7|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.7" />
<sup>7</sup>Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku tatu.
<scripture passage="Acts 28:8" parsed="|Acts|28|8|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.8" />
<sup>8</sup>Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani, mgonjwa, ana homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali, akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.
<scripture passage="Acts 28:9" parsed="|Acts|28|9|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.9" />
<sup>9</sup>Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja wakaponywa.
<scripture passage="Acts 28:10" parsed="|Acts|28|10|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.10" />
<sup>10</sup>Watu walitupatia zawadi mbalimbali na wakati tulipoanza tena safari, walitia ndani ya meli masurufu tuliyohitaji.
<scripture passage="Acts 28:11" parsed="|Acts|28|11|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.11" />
<sup>11</sup>Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo "Miungu Pacha". Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
<scripture passage="Acts 28:12" parsed="|Acts|28|12|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.12" />
<sup>12</sup>Tulifika katika mji wa Sirakusa, tukakaa hapo kwa siku tatu.
<scripture passage="Acts 28:13" parsed="|Acts|28|13|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.13" />
<sup>13</sup>Toka huko tuling`oa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
<scripture passage="Acts 28:14" parsed="|Acts|28|14|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.14" />
<sup>14</sup>Huko tuliwakuta ndugu kadhaa ambao walituomba tukae nao kwa juma moja. Hivi ndivyo tulivyopata kufika Roma.
<scripture passage="Acts 28:15" parsed="|Acts|28|15|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.15" />
<sup>15</sup>Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akapata moyo.
<scripture passage="Acts 28:16" parsed="|Acts|28|16|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.16" />
<sup>16</sup>Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari mmoja wa kumlinda. ic
<scripture passage="Acts 28:17" parsed="|Acts|28|17|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.17" />
<sup>17</sup>Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiyahudi wa mahali hapo. Walipokusanyika, Paulo aliwaambia, "Wananchi wenzangu, mimi, ingawa sikufanya chochote kibaya wala kupinga desturi za wazee wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemu na kutiwa mikononi mwa Waroma.
<scripture passage="Acts 28:18" parsed="|Acts|28|18|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.18" />
<sup>18</sup>Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yeyote, walitaka kuniacha.
<scripture passage="Acts 28:19" parsed="|Acts|28|19|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.19" />
<sup>19</sup>Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
<scripture passage="Acts 28:20" parsed="|Acts|28|20|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.20" />
<sup>20</sup>Ni kwa sababu hiyo nimeomba kuonana na kuongea nanyi, maana nimefungwa minyororo hii kwa sababu ya tumaini lile la Israeli."
<scripture passage="Acts 28:21" parsed="|Acts|28|21|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.21" />
<sup>21</sup>Wao wakamwambia, "Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.
<scripture passage="Acts 28:22" parsed="|Acts|28|22|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.22" />
<sup>22</sup>Lakini tunafikiri inafaa tusikie kutoka kwako mwenyewe mambo yaliyo kichwani mwako. Kwa maana tujualo sisi kuhusu hicho kikundi ni kwamba kinapingwa kila mahali."
<scripture passage="Acts 28:23" parsed="|Acts|28|23|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.23" />
<sup>23</sup>Basi, walipanga naye siku kamili ya kukutana, na wengi wakafika huko alikokuwa anakaa. Tangu asubuhi mpaka jioni Paulo aliwaeleza na kuwafafanulia juu ya Ufalme wa Mungu akijaribu kuwafanya wakubali habari juu ya Yesu kwa kutumia Sheria ya Mose na maandiko ya manabii.
<scripture passage="Acts 28:24" parsed="|Acts|28|24|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.24" />
<sup>24</sup>Baadhi yao walikubali maneno yake, lakini wengine hawakuamini.
<scripture passage="Acts 28:25" parsed="|Acts|28|25|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.25" />
<sup>25</sup>Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili, "Kweli ni sawa yale aliyoyanena Roho Mtakatifu kwa wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
<scripture passage="Acts 28:26" parsed="|Acts|28|26|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.26" />
<sup>26</sup>akisema: `Nenda kwa watu hawa ukawaambie: kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
<scripture passage="Acts 28:27" parsed="|Acts|28|27|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.27" />
<sup>27</sup>Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameziba masikio yao, wamefumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya."`
<scripture passage="Acts 28:28" parsed="|Acts|28|28|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.28" />
<sup>28</sup>Halafu Paulo akamaliza na kusema, "Jueni basi, kwamba ujumbe wa Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watu wa mataifa. Wao watasikiliza!"<i>fd</i> walijiondokea huku wakiwa wanabishana vikali wao kwa wao.
<scripture passage="Acts 28:29" parsed="|Acts|28|29|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.29" />
<sup>29</sup>missing
<scripture passage="Acts 28:30" parsed="|Acts|28|30|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.30" />
<sup>30</sup>Kwa muda wa miaka miwili mizima Paulo aliishi katika nyumba aliyoipanga yeye mwenyewe; akawa anawakaribisha wote waliofika kumsalimu.
<scripture passage="Acts 28:31" parsed="|Acts|28|31|0|0" osisRef="Bible:Acts.28.31" />
<sup>31</sup>Alikuwa akihubiri Ufalme wa Mungu na kufundisha juu ya Bwana Yesu Kristo kwa uhodari, bila kizuizi.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Romans" progress="57.88%" prev="Acts.28" next="Rom.1" id="Rom">
<h2 id="Rom-p0.1">Romans</h2>

<div3 title="Romans 1" progress="57.88%" prev="Rom" next="Rom.2" id="Rom.1">
<h3 id="Rom.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Rom.1-p1">
<scripture passage="Rom 1:1" parsed="|Rom|1|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.1" />
<sup>1</sup>Kutoka kwangu mimi Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, na mtume niliyeteuliwa na kuitwa kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema ya Mungu.
<scripture passage="Rom 1:2" parsed="|Rom|1|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.2" />
<sup>2</sup>Hapo kale, Mungu aliwaahidia watu hii Habari Njema kwa njia ya manabii wake katika Maandiko Matakatifu.
<scripture passage="Rom 1:3" parsed="|Rom|1|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.3" />
<sup>3</sup>Hii Habari Njema inamhusu Mwana wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye mintarafu ubinadamu wake, alikuwa mzawa wa Daudi;
<scripture passage="Rom 1:4" parsed="|Rom|1|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.4" />
<sup>4</sup>mintarafu utakatifu wake wa kimungu, alithibitishwa kwa uwezo mkuu kwamba ni Mwana wa Mungu kwa kufufuliwa kutoka wafu.
<scripture passage="Rom 1:5" parsed="|Rom|1|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.5" />
<sup>5</sup>Kwa njia yake, mimi nimepewa neema ya kuwa mtume, ili kwa ajili yake niwaongoze watu wa mataifa yote wapate kuamini na kutii.
<scripture passage="Rom 1:6" parsed="|Rom|1|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.6" />
<sup>6</sup>Ninyi ni miongoni mwa watu hao; mmeitwa muwe watu wake Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 1:7" parsed="|Rom|1|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.7" />
<sup>7</sup>Basi, ninawaandikia ninyi nyote mlioko Roma ambao Mungu anawapenda, akawateua muwe watu wake. Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 1:8" parsed="|Rom|1|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.8" />
<sup>8</sup>Awali ya yote, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inasikika duniani kote.
<scripture passage="Rom 1:9" parsed="|Rom|1|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.9" />
<sup>9</sup>Mungu, ambaye ninamtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri Habari Njema ya Mwanae, ni shahidi wangu kwamba ninawakumbukeni
<scripture passage="Rom 1:10" parsed="|Rom|1|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.10" />
<sup>10</sup>daima katika sala zangu. Namwomba Mungu akipenda, anipatie nafasi nzuri ya kuja kwenu sasa.
<scripture passage="Rom 1:11" parsed="|Rom|1|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.11" />
<sup>11</sup>Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi ya kiroho na kuwaimarisha.
<scripture passage="Rom 1:12" parsed="|Rom|1|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.12" />
<sup>12</sup>Ndiyo kusema, tutaimarishana: imani yenu itaniimarisha mimi, na yangu itawaimarisha ninyi.
<scripture passage="Rom 1:13" parsed="|Rom|1|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.13" />
<sup>13</sup>Ndugu zangu, nataka mjue kwamba mara nyingi nilikusudia kuwatembeleeni, lakini mpaka sasa nimezuiwa. Ningependa kupata mafanikio mema kati yenu kama nilivyopata kati ya watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Rom 1:14" parsed="|Rom|1|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.14" />
<sup>14</sup>Ninalo jukumu kwa watu wote, waliostaarabika na wasiostaarabika, wenye elimu na wasio na elimu.
<scripture passage="Rom 1:15" parsed="|Rom|1|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.15" />
<sup>15</sup>Ndiyo maana ninatamani pia kuihubiri Habari Njema kwenu ninyi mlioko huko Roma.
<scripture passage="Rom 1:16" parsed="|Rom|1|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.16" />
<sup>16</sup>Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na wasio Wayahudi pia.
<scripture passage="Rom 1:17" parsed="|Rom|1|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.17" />
<sup>17</sup>Kwa maana Habari Njema inaonyesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka mwisho. Kama ilivyoandikwa: "Mwadilifu<i>fa</i> kwa imani ataishi."
<scripture passage="Rom 1:18" parsed="|Rom|1|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.18" />
<sup>18</sup>Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane.
<scripture passage="Rom 1:19" parsed="|Rom|1|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.19" />
<sup>19</sup>Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maana Mungu mwenyewe ameyadhirisha.
<scripture passage="Rom 1:20" parsed="|Rom|1|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.20" />
<sup>20</sup>Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!
<scripture passage="Rom 1:21" parsed="|Rom|1|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.21" />
<sup>21</sup>Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili, wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao tupu zimejaa giza.
<scripture passage="Rom 1:22" parsed="|Rom|1|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.22" />
<sup>22</sup>Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.
<scripture passage="Rom 1:23" parsed="|Rom|1|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.23" />
<sup>23</sup>Wanaacha kumwabudu Mungu aishiye milele, na badala yake, wanaabudu sanamu zilizo mfano wa binadamu ambaye hufa, mfano wa wanyama, ndege, au wanyama watambaao.
<scripture passage="Rom 1:24" parsed="|Rom|1|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.24" />
<sup>24</sup>Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao.
<scripture passage="Rom 1:25" parsed="|Rom|1|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.25" />
<sup>25</sup>Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina.
<scripture passage="Rom 1:26" parsed="|Rom|1|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.26" />
<sup>26</sup>Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile.
<scripture passage="Rom 1:27" parsed="|Rom|1|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.27" />
<sup>27</sup>Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu.
<scripture passage="Rom 1:28" parsed="|Rom|1|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.28" />
<sup>28</sup>Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
<scripture passage="Rom 1:29" parsed="|Rom|1|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.29" />
<sup>29</sup>Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya,
<scripture passage="Rom 1:30" parsed="|Rom|1|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.30" />
<sup>30</sup>na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii wazazi wao;
<scripture passage="Rom 1:31" parsed="|Rom|1|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.31" />
<sup>31</sup>hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine.
<scripture passage="Rom 1:32" parsed="|Rom|1|32|0|0" osisRef="Bible:Rom.1.32" />
<sup>32</sup>Wanajua kwamba Sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 2" progress="58.32%" prev="Rom.1" next="Rom.3" id="Rom.2">
<h3 id="Rom.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Rom.2-p1">
<scripture passage="Rom 2:1" parsed="|Rom|2|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.1" />
<sup>1</sup>Basi, rafiki, kama unawahukumu wengine, huwezi kamwe kujitetea haidhuru wewe ni nani. Kwa maana, kwa kuwahukumu wengine, unajilaani wewe mwenyewe kwa vile nawe unayafanya mambo yaleyale unayohukumu.
<scripture passage="Rom 2:2" parsed="|Rom|2|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.2" />
<sup>2</sup>Tunajua kwamba hukumu ya Mungu kwa wale wanaofanya mambo kama hayo ni hukumu ya haki.
<scripture passage="Rom 2:3" parsed="|Rom|2|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.3" />
<sup>3</sup>Lakini wewe, rafiki, unayewahukumu wale wanaofanya mambo kama hayo bali wewe pia unayafanya, je unadhani utaiepa hukumu ya Mungu?
<scripture passage="Rom 2:4" parsed="|Rom|2|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.4" />
<sup>4</sup>Au labda unaudharau wema wake mkuu, uvumilivu wake na saburi yake, bila kutambua kwamba wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate kutubu?
<scripture passage="Rom 2:5" parsed="|Rom|2|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.5" />
<sup>5</sup>Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajilundikia adhabu kwa Siku ile ambayo ghadhabu ya Mungu na hukumu zake za haki vitadhihirishwa.
<scripture passage="Rom 2:6" parsed="|Rom|2|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.6" />
<sup>6</sup>Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake.
<scripture passage="Rom 2:7" parsed="|Rom|2|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.7" />
<sup>7</sup>Wale wanaozingatia kutenda mema, kutafuta utukufu na heshima ya Mungu na kutokufa, watapata uzima wa milele.
<scripture passage="Rom 2:8" parsed="|Rom|2|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.8" />
<sup>8</sup>Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.
<scripture passage="Rom 2:9" parsed="|Rom|2|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.9" />
<sup>9</sup>Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.
<scripture passage="Rom 2:10" parsed="|Rom|2|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.10" />
<sup>10</sup>Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wale wanaotenda mema; Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.
<scripture passage="Rom 2:11" parsed="|Rom|2|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.11" />
<sup>11</sup>Maana Mungu hambagui mtu yeyote.
<scripture passage="Rom 2:12" parsed="|Rom|2|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.12" />
<sup>12</sup>Wale wanaotenda dhambi bila kuijua Sheria ya Mose wataangamia ingawaje hawajui Sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua Sheria watahukumiwa kisheria.
<scripture passage="Rom 2:13" parsed="|Rom|2|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.13" />
<sup>13</sup>Mtu hafanywi kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kuisikia Sheria, bali kwa kuitii Sheria.
<scripture passage="Rom 2:14" parsed="|Rom|2|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.14" />
<sup>14</sup>Mathalan: watu wa mataifa mengine hawana Sheria ya Mose; lakini kila wanapotimiza matakwa ya Sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha Sheria ingawa hawaijui Sheria.
<scripture passage="Rom 2:15" parsed="|Rom|2|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.15" />
<sup>15</sup>Mwenendo wao unaonyesha kwamba matakwa ya Sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
<scripture passage="Rom 2:16" parsed="|Rom|2|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.16" />
<sup>16</sup>Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 2:17" parsed="|Rom|2|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.17" />
<sup>17</sup>Na wewe, je? Wewe mwenyewe unajiita Myahudi; unaitumainia Sheria na kujivunia kuwa wa Mungu;
<scripture passage="Rom 2:18" parsed="|Rom|2|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.18" />
<sup>18</sup>kwa njia ya Sheria unajua matakwa ya Mungu na unaweza kuchagua jambo jema;
<scripture passage="Rom 2:19" parsed="|Rom|2|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.19" />
<sup>19</sup>wewe unajiona kuwa kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walio gizani;
<scripture passage="Rom 2:20" parsed="|Rom|2|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.20" />
<sup>20</sup>unajiona kuwa mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa wale wasiokomaa bado. Unayo katika Sheria picha kamili ya elimu na ukweli.
<scripture passage="Rom 2:21" parsed="|Rom|2|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.21" />
<sup>21</sup>Basi, wewe unawafundisha wengine; kwa nini hujifundishi wewe mwenyewe? Unawahubiria wengine wasiibe, lakini kumbe wewe mwenyewe unaiba.
<scripture passage="Rom 2:22" parsed="|Rom|2|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.22" />
<sup>22</sup>Unasema: "Msizini," na huku wewe unazini; unachukia sanamu za miungu hali wewe unajitajirisha kwa kuiba katika nyumba za miungu.
<scripture passage="Rom 2:23" parsed="|Rom|2|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.23" />
<sup>23</sup>Kwa kujigamba ati unayo Sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa kuivunja Sheria unamdharau Mungu?
<scripture passage="Rom 2:24" parsed="|Rom|2|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.24" />
<sup>24</sup>Kama vile Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Watu wa mataifa mengine wamelikufuru jina la Mungu kwa sababu yenu ninyi Wayahudi!"
<scripture passage="Rom 2:25" parsed="|Rom|2|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.25" />
<sup>25</sup>Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii Sheria. Lakini kama unaivunja Sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
<scripture passage="Rom 2:26" parsed="|Rom|2|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.26" />
<sup>26</sup>Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa ya Sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.
<scripture passage="Rom 2:27" parsed="|Rom|2|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.27" />
<sup>27</sup>Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja Sheria, ingawaje unayo maandishi ya Sheria na umetahiriwa, hali wao wanaitii Sheria ingawa hawakutahiriwa.
<scripture passage="Rom 2:28" parsed="|Rom|2|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.28" />
<sup>28</sup>Ndiyo kusema, si kila anayeonekana kwa nje kuwa Myahudi ni Myahudi wa kweli, wala mtu hawi Myahudi wa kweli ati kwa kuwa ametahiriwa kimwili.
<scripture passage="Rom 2:29" parsed="|Rom|2|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.2.29" />
<sup>29</sup>Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya Sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 3" progress="58.71%" prev="Rom.2" next="Rom.4" id="Rom.3">
<h3 id="Rom.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Rom.3-p1">
<scripture passage="Rom 3:1" parsed="|Rom|3|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.1" />
<sup>1</sup>Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa kuna faida gani?
<scripture passage="Rom 3:2" parsed="|Rom|3|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.2" />
<sup>2</sup>Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake.
<scripture passage="Rom 3:3" parsed="|Rom|3|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.3" />
<sup>3</sup>Lakini itakuwaje iwapo baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je, jambo hilo litaondoa uaminifu wa Mungu?
<scripture passage="Rom 3:4" parsed="|Rom|3|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.4" />
<sup>4</sup>Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Kila usemapo, maneno yako ni ya haki; na katika hukumu, wewe hushinda."
<scripture passage="Rom 3:5" parsed="|Rom|3|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.5" />
<sup>5</sup>Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa naongea kibinadamu).
<scripture passage="Rom 3:6" parsed="|Rom|3|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.6" />
<sup>6</sup>Hata kidogo! Ingekuwa hivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu?
<scripture passage="Rom 3:7" parsed="|Rom|3|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.7" />
<sup>7</sup>Labda utasema: "Ikiwa ukosefu wa uaminifu kwa upande wangu unamdhihirisha Mungu kuwa mwaminifu zaidi na hivyo kumpatia utukufu, basi singepaswa kuhukumiwa kuwa mwenye dhambi!"
<scripture passage="Rom 3:8" parsed="|Rom|3|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.8" />
<sup>8</sup>Ni sawa na kusema: tufanye maovu ili tupate mema! Ndivyo wengine walivyotukashifu kwa kutushtaki kwamba tumefundisha hivyo. Watahukumiwa wanavyostahili!
<scripture passage="Rom 3:9" parsed="|Rom|3|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.9" />
<sup>9</sup>Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora zaidi kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.
<scripture passage="Rom 3:10" parsed="|Rom|3|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.10" />
<sup>10</sup>Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu!
<scripture passage="Rom 3:11" parsed="|Rom|3|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.11" />
<sup>11</sup>Hakuna mtu anayeelewa, wala anayemtafuta Mungu.
<scripture passage="Rom 3:12" parsed="|Rom|3|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.12" />
<sup>12</sup>Wote wamepotoka wote wamekosa; hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja.
<scripture passage="Rom 3:13" parsed="|Rom|3|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.13" />
<sup>13</sup>Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.
<scripture passage="Rom 3:14" parsed="|Rom|3|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.14" />
<sup>14</sup>Vinywa vyao vimejaa laana chungu.
<scripture passage="Rom 3:15" parsed="|Rom|3|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.15" />
<sup>15</sup>Miguu yao iko mbioni kumwaga damu,
<scripture passage="Rom 3:16" parsed="|Rom|3|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.16" />
<sup>16</sup>popote waendapo husababisha maafa na mateso;
<scripture passage="Rom 3:17" parsed="|Rom|3|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.17" />
<sup>17</sup>njia ya amani hawaijui.
<scripture passage="Rom 3:18" parsed="|Rom|3|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.18" />
<sup>18</sup>Hawajali kabisa kumcha Mungu."
<scripture passage="Rom 3:19" parsed="|Rom|3|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.19" />
<sup>19</sup>Tunajua kwamba Sheria huwahusu walio chini ya Sheria hiyo, hata hawawezi kuwa na kisingizio chochote, na ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu.
<scripture passage="Rom 3:20" parsed="|Rom|3|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.20" />
<sup>20</sup>Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kuishika Sheria; kazi ya Sheria ni kumwonyesha tu mtu kwamba ametenda dhambi.
<scripture passage="Rom 3:21" parsed="|Rom|3|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.21" />
<sup>21</sup>Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwakubali watu kuwa waadilifu imekwisha dhihirishwa, tena bila kutegemea Sheria. Sheria na manabii hushuhudia jambo hili.
<scripture passage="Rom 3:22" parsed="|Rom|3|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.22" />
<sup>22</sup>Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.
<scripture passage="Rom 3:23" parsed="|Rom|3|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.23" />
<sup>23</sup>Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.
<scripture passage="Rom 3:24" parsed="|Rom|3|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.24" />
<sup>24</sup>Lakini kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo anayewakomboa.
<scripture passage="Rom 3:25" parsed="|Rom|3|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.25" />
<sup>25</sup>Mungu alimtoa Yesu kusudi, kwa damu yake, awe njia ya kuwaondolea watu dhambi zao kwa imani yao kwake. Alifanya hivyo ili apate kuonyesha kwamba yeye ni mwadilifu. Hapo zamani Mungu alikuwa mvumilivu bila kuzijali dhambi za watu;
<scripture passage="Rom 3:26" parsed="|Rom|3|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.26" />
<sup>26</sup>lakini sasa, wakati huu, anazikabili dhambi za watu apate kuonyesha uadilifu wake. Kwa namna hiyo Mungu mwenyewe huonyesha kwamba yeye ni mwadilifu na kwamba humkubali kuwa mwadilifu mtu yeyote anayemwamini Yesu.
<scripture passage="Rom 3:27" parsed="|Rom|3|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.27" />
<sup>27</sup>Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza Sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
<scripture passage="Rom 3:28" parsed="|Rom|3|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.28" />
<sup>28</sup>Maana mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimiza matakwa ya Sheria.
<scripture passage="Rom 3:29" parsed="|Rom|3|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.29" />
<sup>29</sup>Au je, Mungu nu Mungu wa Wayahudi tu, ama pia wa watu wa mataifa mengine? Naam, wa mataifa mengine pia.
<scripture passage="Rom 3:30" parsed="|Rom|3|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.30" />
<sup>30</sup>Mungu ni mmoja, naye atawakubali Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
<scripture passage="Rom 3:31" parsed="|Rom|3|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.3.31" />
<sup>31</sup>Je, tunaitumia imani kuibatilisha Sheria? Hata kidogo; bali tunaipa Sheria thamani yake kamili.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 4" progress="59.08%" prev="Rom.3" next="Rom.5" id="Rom.4">
<h3 id="Rom.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Rom.4-p1">
<scripture passage="Rom 4:1" parsed="|Rom|4|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.1" />
<sup>1</sup>Tuseme nini basi, juu ya Abrahamu baba yetu?
<scripture passage="Rom 4:2" parsed="|Rom|4|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.2" />
<sup>2</sup>Kama Abrahamu alikubaliwa kuwa mwadilifu kutokana na matendo yake, basi, anacho kitu cha kujivunia mbele ya Mungu.
<scripture passage="Rom 4:3" parsed="|Rom|4|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.3" />
<sup>3</sup>Kwa maana, Maandiko Matakatifu yasema: "Abrahamu alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu."
<scripture passage="Rom 4:4" parsed="|Rom|4|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.4" />
<sup>4</sup>Mfanyakazi hulipwa mshahara; mshahara wake si zawadi bali ni haki yake.
<scripture passage="Rom 4:5" parsed="|Rom|4|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.5" />
<sup>5</sup>Lakini mtu asiyetegemea matendo yake mwenyewe, bali anamwamini Mungu ambaye huwasamehe waovu, basi, Mungu huijali imani ya mtu huyo, na hivi humkubali kuwa mwadilifu.
<scripture passage="Rom 4:6" parsed="|Rom|4|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.6" />
<sup>6</sup>Naye Daudi asema hivi juu ya furaha ya mtu ambaye Mungu amemkubali kuwa mwadilifu bila kuyajali matendo yake:
<scripture passage="Rom 4:7" parsed="|Rom|4|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.7" />
<sup>7</sup>"Heri wale waliosamehewa makosa yao ambao makosa yao yamefutwa.
<scripture passage="Rom 4:8" parsed="|Rom|4|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.8" />
<sup>8</sup>Heri mtu yule ambaye Bwana hataziweka dhambi zake katika kumbukumbu."
<scripture passage="Rom 4:9" parsed="|Rom|4|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.9" />
<sup>9</sup>Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: "Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu."
<scripture passage="Rom 4:10" parsed="|Rom|4|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.10" />
<sup>10</sup>Je, Abrahamu alikubaliwa kabla ya kutahiriwa ama baada ya kutahiriwa? Kabla ya kutahiriwa, na si baada ya kutahiriwa.
<scripture passage="Rom 4:11" parsed="|Rom|4|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.11" />
<sup>11</sup>Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini Mungu, wakafanywa waadilifu.
<scripture passage="Rom 4:12" parsed="|Rom|4|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.12" />
<sup>12</sup>Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.
<scripture passage="Rom 4:13" parsed="|Rom|4|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.13" />
<sup>13</sup>Mungu alimwahidi Abrahamu na wazawa wake kwamba ulimwengu ungekuwa mali yao. Ahadi hiyo haikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitii Sheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwa kuwa mwadilifu.
<scripture passage="Rom 4:14" parsed="|Rom|4|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.14" />
<sup>14</sup>Maana kama watakaopewa hayo aliyoahidi Mungu ni wale tu wanaoitii Sheria, basi, imani haina maana yoyote, nayo ahadi ya Mungu si kitu.
<scripture passage="Rom 4:15" parsed="|Rom|4|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.15" />
<sup>15</sup>Sheria husababisha ghadhabu; lakini kama hakuna Sheria, haiwezekani kuivunja.
<scripture passage="Rom 4:16" parsed="|Rom|4|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.16" />
<sup>16</sup>Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote: si kwa wale tu wanaoishika Sheria, bali pia kwa wale waishio kwa imani kama Abrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote.
<scripture passage="Rom 4:17" parsed="|Rom|4|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.17" />
<sup>17</sup>Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi." Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu alimwamini--Mungu ambaye huwapa wafu uzima, na kwa amri yake, vitu ambavyo havikuwapo huwa.
<scripture passage="Rom 4:18" parsed="|Rom|4|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.18" />
<sup>18</sup>Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Wazao wako watakuwa wengi kama nyota!"
<scripture passage="Rom 4:19" parsed="|Rom|4|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.19" />
<sup>19</sup>Alikuwa mzee wa karibu miaka mia moja, lakini imani yake haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia mkewe, Sara, alikuwa tasa.
<scripture passage="Rom 4:20" parsed="|Rom|4|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.20" />
<sup>20</sup>Abrahamu hakuionea mashaka ile ahadi ya Mungu; alipata nguvu kutokana na imani, akamtukuza Mungu.
<scripture passage="Rom 4:21" parsed="|Rom|4|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.21" />
<sup>21</sup>Alijua kwamba Mungu anaweza kuyatekeleza yale aliyoahidi.
<scripture passage="Rom 4:22" parsed="|Rom|4|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.22" />
<sup>22</sup>Ndiyo maana Mungu alimkubali kuwa mwadilifu.
<scripture passage="Rom 4:23" parsed="|Rom|4|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.23" />
<sup>23</sup>Inaposemwa, "Alimkubali," haisemwi kwa ajili yake mwenyewe tu.
<scripture passage="Rom 4:24" parsed="|Rom|4|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.24" />
<sup>24</sup>Jambo hili linatuhusu sisi pia ambao tunamwamini Mungu aliyemfufua Yesu, Bwana wetu, kutoka wafu.
<scripture passage="Rom 4:25" parsed="|Rom|4|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.4.25" />
<sup>25</sup>Yeye alitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka ili tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 5" progress="59.42%" prev="Rom.4" next="Rom.6" id="Rom.5">
<h3 id="Rom.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Rom.5-p1">
<scripture passage="Rom 5:1" parsed="|Rom|5|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.1" />
<sup>1</sup>Sasa, kwa vile tumekubaliwa kuwa wadilifu kwa imani, basi, tunayo amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 5:2" parsed="|Rom|5|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.2" />
<sup>2</sup>Kwa imani yetu, yeye ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu ambamo sasa tunaishi. Basi, tunajivunia tumaini tulilo nalo la kushiriki utukufu wa Mungu.
<scripture passage="Rom 5:3" parsed="|Rom|5|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.3" />
<sup>3</sup>Naam, si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi,
<scripture passage="Rom 5:4" parsed="|Rom|5|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.4" />
<sup>4</sup>nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini.
<scripture passage="Rom 5:5" parsed="|Rom|5|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.5" />
<sup>5</sup>Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.
<scripture passage="Rom 5:6" parsed="|Rom|5|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.6" />
<sup>6</sup>Tulipokuwa bado wanyonge, Kristo, wakati ulipotimia, alikufa kwa ajili yetu sisi waovu.
<scripture passage="Rom 5:7" parsed="|Rom|5|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.7" />
<sup>7</sup>Si rahisi mtu kufa kwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anaweza kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
<scripture passage="Rom 5:8" parsed="|Rom|5|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.8" />
<sup>8</sup>Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
<scripture passage="Rom 5:9" parsed="|Rom|5|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.9" />
<sup>9</sup>Kwa kuwa sasa tumekubaliwa kuwa waadilifu kwa damu ya Kristo, ni dhahiri zaidi kwamba atatuokoa katika ghadhabu ya Mungu.
<scripture passage="Rom 5:10" parsed="|Rom|5|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.10" />
<sup>10</sup>Maana, tulipokuwa bado adui zake, Mungu alitupatanisha naye kwa kifo cha Mwanae. Na kwa vile sasa tumepatanishwa naye, ni dhahiri zaidi kwamba tutaokolewa kwa uzima wa Kristo.
<scripture passage="Rom 5:11" parsed="|Rom|5|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.11" />
<sup>11</sup>Wala si hayo tu, ila tunafurahi pia katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametupatanisha na Mungu.
<scripture passage="Rom 5:12" parsed="|Rom|5|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.12" />
<sup>12</sup>Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo ikasababisha kifo. Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi.
<scripture passage="Rom 5:13" parsed="|Rom|5|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.13" />
<sup>13</sup>Kabla ya Sheria kuwako, dhambi ilikuwako ulimwenguni; lakini dhambi haiwekwi katika kumbukumbu bila sheria.
<scripture passage="Rom 5:14" parsed="|Rom|5|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.14" />
<sup>14</sup>Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha yule ambaye atakuja baadaye.
<scripture passage="Rom 5:15" parsed="|Rom|5|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.15" />
<sup>15</sup>Lakini ipo tofauti: neema ya Mungu si kama dhambi ya Adamu. Maana, ingawa dhambi ya mtu mmoja ilisababisha kifo kwa wote, kwa fadhili ya mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, Mungu amewazidishia wote neema na zawadi zake.
<scripture passage="Rom 5:16" parsed="|Rom|5|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.16" />
<sup>16</sup>Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu, na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.
<scripture passage="Rom 5:17" parsed="|Rom|5|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.17" />
<sup>17</sup>Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja kifo kilianza kutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kukubaliwa kuwa waadilifu, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 5:18" parsed="|Rom|5|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.18" />
<sup>18</sup>Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kimoja kiadilifu kinawapa uhuru na uzima.
<scripture passage="Rom 5:19" parsed="|Rom|5|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.19" />
<sup>19</sup>Na kama kwa kutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi wakubaliwe kuwa waadilifu.
<scripture passage="Rom 5:20" parsed="|Rom|5|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.20" />
<sup>20</sup>Sheria ilitokea, ikasababisha kuongezeka kwa uhalifu; lakini pale dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi.
<scripture passage="Rom 5:21" parsed="|Rom|5|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.5.21" />
<sup>21</sup>Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala kwa njia ya uadilifu, na kuleta uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 6" progress="59.74%" prev="Rom.5" next="Rom.7" id="Rom.6">
<h3 id="Rom.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Rom.6-p1">
<scripture passage="Rom 6:1" parsed="|Rom|6|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.1" />
<sup>1</sup>Tuseme nini basi? Je, twendelee kubaki katika dhambi ili neema ya Mungu iongezeke?
<scripture passage="Rom 6:2" parsed="|Rom|6|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.2" />
<sup>2</sup>Hata kidogo! Kuhusu dhambi sisi tumekufa--tutaendeleaje kuishi tena katika dhambi?
<scripture passage="Rom 6:3" parsed="|Rom|6|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.3" />
<sup>3</sup>Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.
<scripture passage="Rom 6:4" parsed="|Rom|6|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.4" />
<sup>4</sup>Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.
<scripture passage="Rom 6:5" parsed="|Rom|6|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.5" />
<sup>5</sup>Maana, kama sisi tumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyo hivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutoka wafu kama yeye.
<scripture passage="Rom 6:6" parsed="|Rom|6|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.6" />
<sup>6</sup>Tunajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili hali ya dhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wa dhambi.
<scripture passage="Rom 6:7" parsed="|Rom|6|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.7" />
<sup>7</sup>Kwa maana, mtu aliyekufa, amenasuliwa kutoka katika nguvu ya dhambi.
<scripture passage="Rom 6:8" parsed="|Rom|6|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.8" />
<sup>8</sup>Basi, ikiwa tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pia pamoja naye.
<scripture passage="Rom 6:9" parsed="|Rom|6|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.9" />
<sup>9</sup>Maana, tunajua kwamba Kristo amekwisha fufuliwa kutoka wafu na hafi tena; kifo hakimtawali tena.
<scripture passage="Rom 6:10" parsed="|Rom|6|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.10" />
<sup>10</sup>Hivyo, kwa kuwa alikufa--mara moja tu--dhambi haina nguvu tena juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
<scripture passage="Rom 6:11" parsed="|Rom|6|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.11" />
<sup>11</sup>Hali kadhalika nanyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusu dhambi, lakini kama mnaoishi katika umoja na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
<scripture passage="Rom 6:12" parsed="|Rom|6|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.12" />
<sup>12</sup>Kwa hiyo, dhambi isiitawale tena miili yenu ambayo hufa, na hivyo kuzitii tamaa zake.
<scripture passage="Rom 6:13" parsed="|Rom|6|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.13" />
<sup>13</sup>Wala msitoe hata sehemu moja ya miili yenu iwe chombo cha kutenda uovu na dhambi. Badala yake, jitoleeni ninyi wenyewe kwa Mungu kama watu waliofufuliwa kutoka wafu; toeni nafsi zenu zote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu.
<scripture passage="Rom 6:14" parsed="|Rom|6|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.14" />
<sup>14</sup>Maana, dhambi haitawatawala ninyi tena, kwani hamko chini ya Sheria, bali chini ya neema.
<scripture passage="Rom 6:15" parsed="|Rom|6|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.15" />
<sup>15</sup>Basi, tuseme nini? Je, tutende dhambi ati kwa sababu hatuko chini ya Sheria bali chini ya neema? Hata kidogo!
<scripture passage="Rom 6:16" parsed="|Rom|6|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.16" />
<sup>16</sup>Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo--au watumwa wa dhambi, na matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa waadilifu.
<scripture passage="Rom 6:17" parsed="|Rom|6|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.17" />
<sup>17</sup>Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini--namshukuru Mungu--mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
<scripture passage="Rom 6:18" parsed="|Rom|6|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.18" />
<sup>18</sup>Mlikombolewa kutoka utumwa wa dhambi, mkawa watumwa wa uadilifu.
<scripture passage="Rom 6:19" parsed="|Rom|6|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.19" />
<sup>19</sup>(Hapa natumia lugha ya kawaida ya watu kwa sababu ya udhaifu wenu wenyewe.) Kama vile wakati fulani mlivyojitolea ninyi wenyewe kutumikia uchafu na uhalifu kwa ajili ya uovu, vivyo hivyo sasa jitoleeni nafsi zenu wenyewe kutumikia uadilifu kwa ajili ya utakatifu.
<scripture passage="Rom 6:20" parsed="|Rom|6|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.20" />
<sup>20</sup>Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na uadilifu.
<scripture passage="Rom 6:21" parsed="|Rom|6|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.21" />
<sup>21</sup>Sasa, mlipata faida gani siku zile kutokana na mambo yale ambayo mnayaonea aibu sasa? Maana, matokeo ya mambo haya ni kifo!
<scripture passage="Rom 6:22" parsed="|Rom|6|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.22" />
<sup>22</sup>Lakini sasa, mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na matokeo yake ni uzima wa milele.
<scripture passage="Rom 6:23" parsed="|Rom|6|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.6.23" />
<sup>23</sup>Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uzima wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 7" progress="60.04%" prev="Rom.6" next="Rom.8" id="Rom.7">
<h3 id="Rom.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Rom.7-p1">
<scripture passage="Rom 7:1" parsed="|Rom|7|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.1" />
<sup>1</sup>Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia watu wanaojua Sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
<scripture passage="Rom 7:2" parsed="|Rom|7|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.2" />
<sup>2</sup>Mathalan: mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe anapokuw hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo mwanamke.
<scripture passage="Rom 7:3" parsed="|Rom|7|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.3" />
<sup>3</sup>Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
<scripture passage="Rom 7:4" parsed="|Rom|7|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.4" />
<sup>4</sup>Hali kadhalika ninyi ndugu zangu: ninyi pia mmekufa kuhusu Sheria kwa kuwa ninyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.
<scripture passage="Rom 7:5" parsed="|Rom|7|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.5" />
<sup>5</sup>Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na Sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.
<scripture passage="Rom 7:6" parsed="|Rom|7|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.6" />
<sup>6</sup>Lakini sasa tumekuwa huru kutoka vifungo vya Sheria, kwa sababu tumekufa kuhusu lile jambo lililotufanya sisi watumwa. Sasa tunatumikia kufuatana na maisha mapya ya Roho, na si kufuatana na hali ile ya kale ya Sheria iliyoandikwa.
<scripture passage="Rom 7:7" parsed="|Rom|7|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.7" />
<sup>7</sup>Je, tuseme basi, kwamba Sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila Sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama Sheria isingalikuwa imesema: "Usitamani."
<scripture passage="Rom 7:8" parsed="|Rom|7|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.8" />
<sup>8</sup>Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila Sheria dhambi ni kitu kilichokufa.
<scripture passage="Rom 7:9" parsed="|Rom|7|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.9" />
<sup>9</sup>Wakati mmoja mimi nilikuwa hai mbali na Sheria; lakini amri ilipokuja, dhambi ilifufuka,
<scripture passage="Rom 7:10" parsed="|Rom|7|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.10" />
<sup>10</sup>nami nikafa. Hiyo amri ambayo shabaha yake ilikuwa kuleta uhai, kwangu imeleta kifo.
<scripture passage="Rom 7:11" parsed="|Rom|7|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.11" />
<sup>11</sup>Maana, dhambi ilichukua fursa iliyopatiwa na amri hiyo, ikanidanganya na kuniua.
<scripture passage="Rom 7:12" parsed="|Rom|7|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.12" />
<sup>12</sup>Basi, Sheria yenyewe ni takatifu, na amri yenyewe ni takatifu, ni ya haki na nzuri.
<scripture passage="Rom 7:13" parsed="|Rom|7|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.13" />
<sup>13</sup>Je, hii inamaanisha kwamba kile kilicho kizuri kimesababisha kifo changu? Hata kidogo! Iliyo ni kwamba, dhambi, ili ionekane dhahiri kuwa ni dhambi, imekitumia kile kilicho kizuri na kusababisha kifo changu. Hivyo dhambi, kwa njia ya ile amri, ilijionyesha kikamilifu jinsi ilivyo mbaya mno.
<scripture passage="Rom 7:14" parsed="|Rom|7|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.14" />
<sup>14</sup>Tunajua kwamba Sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia, mimi nimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi.
<scripture passage="Rom 7:15" parsed="|Rom|7|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.15" />
<sup>15</sup>Sielewi nifanyacho, maana kile ninachotaka sikifanyi, bali kile ninachochukia ndicho nikifanyacho.
<scripture passage="Rom 7:16" parsed="|Rom|7|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.16" />
<sup>16</sup>Ikiwa basi, ninatenda kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba nakubali kuwa ile Sheria ni nzuri.
<scripture passage="Rom 7:17" parsed="|Rom|7|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.17" />
<sup>17</sup>Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, bali ile dhambi iliyo ndani yangu.
<scripture passage="Rom 7:18" parsed="|Rom|7|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.18" />
<sup>18</sup>Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.
<scripture passage="Rom 7:19" parsed="|Rom|7|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.19" />
<sup>19</sup>Yaani, badala ya kufanya lile jambo jema ninalotaka, nafanya lile baya nisilotaka.
<scripture passage="Rom 7:20" parsed="|Rom|7|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.20" />
<sup>20</sup>Basi, kama ninafanya kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba si mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambi iliyo ndani yangu.
<scripture passage="Rom 7:21" parsed="|Rom|7|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.21" />
<sup>21</sup>Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
<scripture passage="Rom 7:22" parsed="|Rom|7|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.22" />
<sup>22</sup>Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahia sheria ya Mungu.
<scripture passage="Rom 7:23" parsed="|Rom|7|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.23" />
<sup>23</sup>Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini mwangu.
<scripture passage="Rom 7:24" parsed="|Rom|7|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.24" />
<sup>24</sup>Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka katika mwili huu unaonipeleka kifoni?
<scripture passage="Rom 7:25" parsed="|Rom|7|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.7.25" />
<sup>25</sup>Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya dhambi.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 8" progress="60.40%" prev="Rom.7" next="Rom.9" id="Rom.8">
<h3 id="Rom.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Rom.8-p1">
<scripture passage="Rom 8:1" parsed="|Rom|8|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.1" />
<sup>1</sup>Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao wameungana na Kristo.
<scripture passage="Rom 8:2" parsed="|Rom|8|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.2" />
<sup>2</sup>Maana, sheria ya Roho iletayo uzima kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo.
<scripture passage="Rom 8:3" parsed="|Rom|8|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.3" />
<sup>3</sup>Mungu ametekeleza jambo lile ambalo Sheria haikuweza kutekeleza kwa sababu ya udhaifu w binadamu. Mungu alimtuma Mwanae akiwa mwenye mwili sawa na miili yetu sisi wenye dhambi, ili aikabili dhambi, na kwa mwili huo akaiangamiza dhambi.
<scripture passage="Rom 8:4" parsed="|Rom|8|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.4" />
<sup>4</sup>Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya Sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho.
<scripture passage="Rom 8:5" parsed="|Rom|8|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.5" />
<sup>5</sup>Maana, wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya mwili, hutawaliwa na fikira za mwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya Roho Mtakatifu, hutawaliwa na fikira za Roho.
<scripture passage="Rom 8:6" parsed="|Rom|8|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.6" />
<sup>6</sup>Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uzima na amani.
<scripture passage="Rom 8:7" parsed="|Rom|8|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.7" />
<sup>7</sup>Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii.
<scripture passage="Rom 8:8" parsed="|Rom|8|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.8" />
<sup>8</sup>Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
<scripture passage="Rom 8:9" parsed="|Rom|8|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.9" />
<sup>9</sup>Lakini ninyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
<scripture passage="Rom 8:10" parsed="|Rom|8|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.10" />
<sup>10</sup>Lakini kama Kristo yumo ndani yenu, ingawa miili yenu itakufa kwa sababu ya dhambi, kwenu Roho ndiye uhai kwa sababu mmekubaliwa kuwa waadilifu.
<scripture passage="Rom 8:11" parsed="|Rom|8|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.11" />
<sup>11</sup>Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
<scripture passage="Rom 8:12" parsed="|Rom|8|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.12" />
<sup>12</sup>Hivyo basi, ndugu zangu, tunalo jukumu, lakini si la kuishi kufuatana na maumbile ya kibinadamu.
<scripture passage="Rom 8:13" parsed="|Rom|8|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.13" />
<sup>13</sup>Kwa maana, kama mkiishi kufuatana na matakwa ya maumbile ya kibinadamu, hakika mtakufa. Lakini, kama kwa njia ya Roho mnayaua matendo yenu maovu, basi, mtaishi.
<scripture passage="Rom 8:14" parsed="|Rom|8|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.14" />
<sup>14</sup>Wote wanaoongozwa na Roho wa MUngu ni watoto wa Mungu.
<scripture passage="Rom 8:15" parsed="|Rom|8|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.15" />
<sup>15</sup>Kwa maana, Roho mliyempokea si Roho mwenye kuwafanya ninyi watumwa na kuwatia tena hofu; sivyo, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya ninyi watoto wa Mungu, na kwa nguvu ya huyo Roho, sisi tunaweza kumwita Mungu, "Aba," yaani "Baba!"
<scripture passage="Rom 8:16" parsed="|Rom|8|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.16" />
<sup>16</sup>Naye Roho mwenyewe anajiunga na roho zetu na kuthibitisha kwamba sisi ni watoto wa Mungu.
<scripture passage="Rom 8:17" parsed="|Rom|8|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.17" />
<sup>17</sup>Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
<scripture passage="Rom 8:18" parsed="|Rom|8|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.18" />
<sup>18</sup>Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyafananisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu.
<scripture passage="Rom 8:19" parsed="|Rom|8|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.19" />
<sup>19</sup>Viumbe vyote vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.
<scripture passage="Rom 8:20" parsed="|Rom|8|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.20" />
<sup>20</sup>Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, si kwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenzi ya Mungu. Hata hivyo yapo matumaini,
<scripture passage="Rom 8:21" parsed="|Rom|8|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.21" />
<sup>21</sup>maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu, vishiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu.
<scripture passage="Rom 8:22" parsed="|Rom|8|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.22" />
<sup>22</sup>Kwa maana tunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbe vyote vinalia kwa maumivu kama ya kujifungua mtoto.
<scripture passage="Rom 8:23" parsed="|Rom|8|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.23" />
<sup>23</sup>Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukitazamia kufanywa watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
<scripture passage="Rom 8:24" parsed="|Rom|8|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.24" />
<sup>24</sup>Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa; lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
<scripture passage="Rom 8:25" parsed="|Rom|8|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.25" />
<sup>25</sup>Kama tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado, basi, tunakingojea kwa uvumilivu.
<scripture passage="Rom 8:26" parsed="|Rom|8|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.26" />
<sup>26</sup>Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.
<scripture passage="Rom 8:27" parsed="|Rom|8|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.27" />
<sup>27</sup>Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.
<scripture passage="Rom 8:28" parsed="|Rom|8|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.28" />
<sup>28</sup>Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake.
<scripture passage="Rom 8:29" parsed="|Rom|8|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.29" />
<sup>29</sup>Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
<scripture passage="Rom 8:30" parsed="|Rom|8|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.30" />
<sup>30</sup>Basi, Mungu aliwaita wale aliokuwa amewateua; na hao aliowaita aliwakubali kuwa waadilifu; na hao aliowakubali kuwa waadilifu aliwashirikisha pia utukufu wake.
<scripture passage="Rom 8:31" parsed="|Rom|8|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.31" />
<sup>31</sup>Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
<scripture passage="Rom 8:32" parsed="|Rom|8|32|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.32" />
<sup>32</sup>Mungu hakumhurumia hata mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
<scripture passage="Rom 8:33" parsed="|Rom|8|33|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.33" />
<sup>33</sup>Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu mwenyewe huwaondolea hatia!
<scripture passage="Rom 8:34" parsed="|Rom|8|34|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.34" />
<sup>34</sup>Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea!
<scripture passage="Rom 8:35" parsed="|Rom|8|35|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.35" />
<sup>35</sup>Ni nani awezaye kututenga na mapendo ya Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kuuawa?
<scripture passage="Rom 8:36" parsed="|Rom|8|36|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.36" />
<sup>36</sup>Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Kwa ajili yako, twakikabili kifo kutwa kucha: tunatendewa kama kondoo wa kuchinjwa."
<scripture passage="Rom 8:37" parsed="|Rom|8|37|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.37" />
<sup>37</sup>Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda.
<scripture passage="Rom 8:38" parsed="|Rom|8|38|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.38" />
<sup>38</sup>Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: wala kifo, wala uhai; wala malaika, au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka;
<scripture passage="Rom 8:39" parsed="|Rom|8|39|0|0" osisRef="Bible:Rom.8.39" />
<sup>39</sup>Wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu kwetu kwa njia ya Kristo Yesu Bwana wetu.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 9" progress="60.96%" prev="Rom.8" next="Rom.10" id="Rom.9">
<h3 id="Rom.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Rom.9-p1">
<scripture passage="Rom 9:1" parsed="|Rom|9|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.1" />
<sup>1</sup>Nasema ukweli mtupu; nimeungana na Kristo nami sisemi uongo. Dhamiri yangu ikiongozwa na Roho Mtakatifu inanithibitishia jambo hili pia.
<scripture passage="Rom 9:2" parsed="|Rom|9|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.2" />
<sup>2</sup>Nataka kusema hivi: nina huzuni kubwa na maumivu yasiyopimika moyoni mwangu
<scripture passage="Rom 9:3" parsed="|Rom|9|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.3" />
<sup>3</sup>kwa ajili ya watu wangu, walio damu moja nami! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.
<scripture passage="Rom 9:4" parsed="|Rom|9|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.4" />
<sup>4</sup>Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; aliagana nao, akawapa Sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.
<scripture passage="Rom 9:5" parsed="|Rom|9|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.5" />
<sup>5</sup>Wao ni wajukuu wa mababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamu wake, ametoka katika ukoo wao. Mungu atawalaye juu ya yote, na atukuzwe milele! Amina.
<scripture passage="Rom 9:6" parsed="|Rom|9|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.6" />
<sup>6</sup>Sisemi kwamba ahadi ya Mungu imebatilika; maana si watu wote wa Israeli ni wateule wa Mungu.
<scripture passage="Rom 9:7" parsed="|Rom|9|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.7" />
<sup>7</sup>Wala, si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Wazao wake watatokana na Isaka."
<scripture passage="Rom 9:8" parsed="|Rom|9|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.8" />
<sup>8</sup>Nido kusema, wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.
<scripture passage="Rom 9:9" parsed="|Rom|9|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.9" />
<sup>9</sup>Maana ahadi yenyewe ni hii: "Nitakujia wakati maalum, naye Sara atapata mtoto."
<scripture passage="Rom 9:10" parsed="|Rom|9|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.10" />
<sup>10</sup>Tena si hayo tu ila pia Rebeka naye alipata mapacha kwa baba mmoja, yaani Isaka, babu yetu.
<scripture passage="Rom 9:11" parsed="|Rom|9|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.11" />
<sup>11</sup>Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,
<scripture passage="Rom 9:12" parsed="|Rom|9|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.12" />
<sup>12</sup>Rebeka aliambiwa kwamba yule mtoto wa kwanza atamtumikia yule wa nyuma. Hivyo uchaguzi wa Mungu unategemea jinsi anavyoita mwenyewe, na si matendo ya binadamu.
<scripture passage="Rom 9:13" parsed="|Rom|9|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.13" />
<sup>13</sup>Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia."
<scripture passage="Rom 9:14" parsed="|Rom|9|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.14" />
<sup>14</sup>Basi, tuseme nini? Je, Mungu amekosa haki? Hata kidogo!
<scripture passage="Rom 9:15" parsed="|Rom|9|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.15" />
<sup>15</sup>Maana alimwambia Mose: "Nitamhurumia mtu yeyote ninayetaka kumhurumia; nitamwonea huruma mtu yeyote ninayetaka."
<scripture passage="Rom 9:16" parsed="|Rom|9|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.16" />
<sup>16</sup>Kwa hiyo, yote hutegemea huruma ya Mungu, na si bidii au mapenzi ya mtu.
<scripture passage="Rom 9:17" parsed="|Rom|9|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.17" />
<sup>17</sup>Maana Maandiko Matakatifu yasema hivi kwa Farao: "Nilikufanya mfalme ili kwa njia yako, uwezo wangu ujulikane, na jina langu litangazwe popote duniani."
<scripture passage="Rom 9:18" parsed="|Rom|9|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.18" />
<sup>18</sup>Ni wazi,basi, kwamba Mungu humhurumia yeyote anayetaka kumhurumia, na akipenda kumfanya mtu awe mkaidi, hufanya hivyo.
<scripture passage="Rom 9:19" parsed="|Rom|9|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.19" />
<sup>19</sup>Labda utaniuliza: "Ikiwa mambo yako hivyo, Mungu anawezaje kumlaumu mtu? Nani awezaye kuyapinga mapenzi yake?"
<scripture passage="Rom 9:20" parsed="|Rom|9|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.20" />
<sup>20</sup>Lakini, ewe binadamu, u nani hata uthubutu kumhoji Mungu? Je, chungu chaweza kumwuliza mfinyanzi wake: "Kwa nini umenitengeneza namna hii?"
<scripture passage="Rom 9:21" parsed="|Rom|9|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.21" />
<sup>21</sup>Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
<scripture passage="Rom 9:22" parsed="|Rom|9|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.22" />
<sup>22</sup>Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu. Alitaka kuonyesha ghadhabu yake na kujulisha uwezo wake, Basi, alikuwa na saburi sana, akiwavumilia wale ambao walikuwa lengo la ghadhabu yake, ambao walistahili kuangamizwa.
<scripture passage="Rom 9:23" parsed="|Rom|9|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.23" />
<sup>23</sup>Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.
<scripture passage="Rom 9:24" parsed="|Rom|9|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.24" />
<sup>24</sup>Maana sisi ndio hao aliowaita, si tu kutoka miongoni mwa Wayahudi bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Rom 9:25" parsed="|Rom|9|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.25" />
<sup>25</sup>Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea: "Wale waliokuwa `Si watu wangu` nitawaita: `Watu wangu!` Naye `Sikupendi` ataitwa: `Mpenzi wangu!`
<scripture passage="Rom 9:26" parsed="|Rom|9|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.26" />
<sup>26</sup>Na pale walipoambiwa: `Ninyi si wangu` hapo wataitwa: `Watoto wa Mungu hai."`
<scripture passage="Rom 9:27" parsed="|Rom|9|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.27" />
<sup>27</sup>Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaaza sauti: "Hata kama watoto wa Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaookolewa;
<scripture passage="Rom 9:28" parsed="|Rom|9|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.28" />
<sup>28</sup>maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya ulimwengu wote."
<scripture passage="Rom 9:29" parsed="|Rom|9|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.29" />
<sup>29</sup>Ni kama Isaya alivyosema hapo awali: "Kama Bwana Mwenye Nguvu asingalituachia baadhi ya watoto wa Israeli, tungalikwisha kuwa kama Sodoma, tungalikwisha kuwa ma Gomora."
<scripture passage="Rom 9:30" parsed="|Rom|9|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.30" />
<sup>30</sup>Basi, tuseme nini? Ni hivi: watu wa mataifa ambao hawakutafuta kukubaliwa kuwa waadilifu, wamekubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani,
<scripture passage="Rom 9:31" parsed="|Rom|9|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.31" />
<sup>31</sup>hali watu wa Israeli waliokuwa wakitafuta Sheria iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu, hawakuipata.
<scripture passage="Rom 9:32" parsed="|Rom|9|32|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.32" />
<sup>32</sup>Kwa nini? Kwa sababu walitegemea matendo yao badala ya kutegemea imani. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa
<scripture passage="Rom 9:33" parsed="|Rom|9|33|0|0" osisRef="Bible:Rom.9.33" />
<sup>33</sup>kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: "Tazama! Naweka huko Sioni jiwe likwazalo, mwamba utakaowafanya watu waanguke. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa!"
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 10" progress="61.40%" prev="Rom.9" next="Rom.11" id="Rom.10">
<h3 id="Rom.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Rom.10-p1">
<scripture passage="Rom 10:1" parsed="|Rom|10|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.1" />
<sup>1</sup>Ndugu zangu, ninataka na kutazamia kwa moyo wangu wote hao wananchi wenzangu wakombolewe. Tena nawaombea kwa Mungu daima.
<scripture passage="Rom 10:2" parsed="|Rom|10|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.2" />
<sup>2</sup>Maana naweza kuthibitisha kwa niaba yao kwamba wanayo bidii ya kumtafuta Mungu; lakini bidii hiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli.
<scripture passage="Rom 10:3" parsed="|Rom|10|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.3" />
<sup>3</sup>Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu, na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe, na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu.
<scripture passage="Rom 10:4" parsed="|Rom|10|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.4" />
<sup>4</sup>Maana kwa kuja kwake Kristo, Sheria imefikia kikomo chake, ili kila mtu anayeamini akubaliwe kuwa mwadilifu.
<scripture passage="Rom 10:5" parsed="|Rom|10|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.5" />
<sup>5</sup>Kuhusu kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa kuitii Sheria, Mose aliandika hivi: "Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya Sheria ataishi."
<scripture passage="Rom 10:6" parsed="|Rom|10|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.6" />
<sup>6</sup>Lakini, kuhusu kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa njia ya imani, yasemwa hivi: "Usiseme moyoni mwako: `Nani atapanda mpaka mbinguni?` (yaani, kumleta Kristo chini);
<scripture passage="Rom 10:7" parsed="|Rom|10|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.7" />
<sup>7</sup>wala usiseme: `Nani atashuka mpaka Kuzimu` (yaani, kumleta Kristo kutoka kwa wafu)."
<scripture passage="Rom 10:8" parsed="|Rom|10|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.8" />
<sup>8</sup>Maandiko Matakatifu yesema hivi, "Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako" nao ndio ile imani tunayoihubiri.
<scripture passage="Rom 10:9" parsed="|Rom|10|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.9" />
<sup>9</sup>Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka.
<scripture passage="Rom 10:10" parsed="|Rom|10|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.10" />
<sup>10</sup>Maana tunaamini kwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; na tunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa.
<scripture passage="Rom 10:11" parsed="|Rom|10|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.11" />
<sup>11</sup>Maandiko Matakatifu yasema: "Kila amwaminiye hatakuwa na sababu ya kuaibika."
<scripture passage="Rom 10:12" parsed="|Rom|10|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.12" />
<sup>12</sup>Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
<scripture passage="Rom 10:13" parsed="|Rom|10|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.13" />
<sup>13</sup>Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa."
<scripture passage="Rom 10:14" parsed="|Rom|10|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.14" />
<sup>14</sup>Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama hakuna mhubiri?
<scripture passage="Rom 10:15" parsed="|Rom|10|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.15" />
<sup>15</sup>Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!"
<scripture passage="Rom 10:16" parsed="|Rom|10|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.16" />
<sup>16</sup>Lakini wote hawakuipokea hiyo Habari Njema. Maana Isaya alisema: "Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?"
<scripture passage="Rom 10:17" parsed="|Rom|10|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.17" />
<sup>17</sup>Hivyo basi, imani inatokana na kuusikiliza ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
<scripture passage="Rom 10:18" parsed="|Rom|10|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.18" />
<sup>18</sup>Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu."
<scripture passage="Rom 10:19" parsed="|Rom|10|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.19" />
<sup>19</sup>Tena nauliza: je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni kwa kwanza kujibu: "Nitawafanyeni mwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu."
<scripture passage="Rom 10:20" parsed="|Rom|10|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.20" />
<sup>20</sup>Tena Isaya anathubutu hata kusema: "Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionyesha kwao wasiouliza habari zangu."
<scripture passage="Rom 10:21" parsed="|Rom|10|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.10.21" />
<sup>21</sup>Lakini kuhusu Israeli anasema: "Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii."
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 11" progress="61.68%" prev="Rom.10" next="Rom.12" id="Rom.11">
<h3 id="Rom.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Rom.11-p1">
<scripture passage="Rom 11:1" parsed="|Rom|11|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.1" />
<sup>1</sup>Basi, nauliza: je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mini binafsi ni Mwisraeli mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.
<scripture passage="Rom 11:2" parsed="|Rom|11|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.2" />
<sup>2</sup>Mungu hakuwakataa watu wake aliowateua tangu mwanzo. Mnakumbuka yasemavyo Maandiko Matakatifu juu ya Eliya wakati alipomnung`unikia Mungu kuhusu Israeli:
<scripture passage="Rom 11:3" parsed="|Rom|11|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.3" />
<sup>3</sup>"Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua?"
<scripture passage="Rom 11:4" parsed="|Rom|11|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.4" />
<sup>4</sup>Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: "Nimejiwekea elfu saba ambao hawakumwabudu Baali."
<scripture passage="Rom 11:5" parsed="|Rom|11|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.5" />
<sup>5</sup>Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake.
<scripture passage="Rom 11:6" parsed="|Rom|11|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.6" />
<sup>6</sup>Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.
<scripture passage="Rom 11:7" parsed="|Rom|11|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.7" />
<sup>7</sup>Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,
<scripture passage="Rom 11:8" parsed="|Rom|11|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.8" />
<sup>8</sup>kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito, na mpaka leo hii hawawezi kuona kwa macho yao wala kusikia kwa masikio yao."
<scripture passage="Rom 11:9" parsed="|Rom|11|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.9" />
<sup>9</sup>Naye Daudi anasema: "Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa, waanguke na kuadhibiwa.
<scripture passage="Rom 11:10" parsed="|Rom|11|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.10" />
<sup>10</sup>Macho yao yatiwe giza wasiweze kuona. Migongo yao ipindike kwa taabu daima!"
<scripture passage="Rom 11:11" parsed="|Rom|11|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.11" />
<sup>11</sup>Basi, nauliza: je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu.
<scripture passage="Rom 11:12" parsed="|Rom|11|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.12" />
<sup>12</sup>Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha baraka nyingi zaidi.
<scripture passage="Rom 11:13" parsed="|Rom|11|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.13" />
<sup>13</sup>Basi, sasa nawaambieni ninyi watu wa mataifa mengine: Maadamu mimi nimekuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine, ninajivunia huduma yangu,
<scripture passage="Rom 11:14" parsed="|Rom|11|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.14" />
<sup>14</sup>nipate kuwafanya wananchi wenzangu wawaonee ninyi wivu, na hivyo nipate kuwaokoa baadhi yao.
<scripture passage="Rom 11:15" parsed="|Rom|11|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.15" />
<sup>15</sup>Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
<scripture passage="Rom 11:16" parsed="|Rom|11|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.16" />
<sup>16</sup>Ikiwa kipande cha kwanza cha mkate kimewekwa wakfu, mkate wote umewekwa wakfu; mizizi ya mti ikiwa mizuri, na matawi yake huwa mazuri pia.
<scripture passage="Rom 11:17" parsed="|Rom|11|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.17" />
<sup>17</sup>Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Ninyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
<scripture passage="Rom 11:18" parsed="|Rom|11|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.18" />
<sup>18</sup>Basi, msiwadharau wale waliokatwa kama matawi! Na, hata kama kuna la kujivunia, kumbukeni kwamba si ninyi mnaoitegemeza mizizi, bali mizizi ndiyo inayowategemeza ninyi.
<scripture passage="Rom 11:19" parsed="|Rom|11|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.19" />
<sup>19</sup>Lakini utasema: "Matawi yalikatwa kusudi mimi nipandikizwe mahali pake."
<scripture passage="Rom 11:20" parsed="|Rom|11|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.20" />
<sup>20</sup>Sawa! Yalikatwa kwa sababu ya kukosa imani, bali wewe unasimama kwa imani yako. Lakini usijivune; ila uwe na tahadhari.
<scripture passage="Rom 11:21" parsed="|Rom|11|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.21" />
<sup>21</sup>Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwahurumia Wayahudi ambao ni kama matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe?
<scripture passage="Rom 11:22" parsed="|Rom|11|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.22" />
<sup>22</sup>Kumbuka, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.
<scripture passage="Rom 11:23" parsed="|Rom|11|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.23" />
<sup>23</sup>Nao Wayahudi, hali kadhalika; wakiacha utovu wao wa imani, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
<scripture passage="Rom 11:24" parsed="|Rom|11|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.24" />
<sup>24</sup>Ninyi watu wa mataifa mengine, kwa asili ni kama tawi la mzeituni mwitu, lakini mmeondolewa huko, mkapandikizwa katika mzeituni bustanini mahali ambapo kwa asili si penu. Lakini, Wayahudi kwa asili ni kama mzeituni bustanini, na itakuwa jambo rahisi zaidi kwao kupandikizwa tena katika mti huohuo wao.
<scripture passage="Rom 11:25" parsed="|Rom|11|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.25" />
<sup>25</sup>Ndugu zangu, napenda mjue ukweli huu uliofichika msije mkajiona wenye akili sana. Ukaidi wa Wayahudi ulikuwa ni wa muda tu, mpaka watu wa mataifa mengine watakapokuwa wamemfikia Mungu.
<scripture passage="Rom 11:26" parsed="|Rom|11|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.26" />
<sup>26</sup>Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: "Mkombozi atakuja kutoka Sioni, atauondoa uovu wa Yakobo.
<scripture passage="Rom 11:27" parsed="|Rom|11|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.27" />
<sup>27</sup>Hili ndilo agano nitakalofanya nao wakati nitakapoziondoa dhambi zao."
<scripture passage="Rom 11:28" parsed="|Rom|11|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.28" />
<sup>28</sup>Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa adui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni rafiki wa Mungu kwa sababu ya baba zao.
<scripture passage="Rom 11:29" parsed="|Rom|11|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.29" />
<sup>29</sup>Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo.
<scripture passage="Rom 11:30" parsed="|Rom|11|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.30" />
<sup>30</sup>Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata huruma yake kutokana na kuasi kwao.
<scripture passage="Rom 11:31" parsed="|Rom|11|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.31" />
<sup>31</sup>Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu.
<scripture passage="Rom 11:32" parsed="|Rom|11|32|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.32" />
<sup>32</sup>Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili wapate kuwahurumia wote.
<scripture passage="Rom 11:33" parsed="|Rom|11|33|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.33" />
<sup>33</sup>Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
<scripture passage="Rom 11:34" parsed="|Rom|11|34|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.34" />
<sup>34</sup>"Nani aliyepata kuyajua mawazo ya Bwana? Nani awezaye kuwa mshauri wake?
<scripture passage="Rom 11:35" parsed="|Rom|11|35|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.35" />
<sup>35</sup>Au, nani aliyempa yeye kitu kwanza hata aweze kulipwa tena kitu hicho?"
<scripture passage="Rom 11:36" parsed="|Rom|11|36|0|0" osisRef="Bible:Rom.11.36" />
<sup>36</sup>Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 12" progress="62.19%" prev="Rom.11" next="Rom.13" id="Rom.12">
<h3 id="Rom.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Rom.12-p1">
<scripture passage="Rom 12:1" parsed="|Rom|12|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.1" />
<sup>1</sup>Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
<scripture passage="Rom 12:2" parsed="|Rom|12|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.2" />
<sup>2</sup>Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
<scripture passage="Rom 12:3" parsed="|Rom|12|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.3" />
<sup>3</sup>Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
<scripture passage="Rom 12:4" parsed="|Rom|12|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.4" />
<sup>4</sup>Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
<scripture passage="Rom 12:5" parsed="|Rom|12|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.5" />
<sup>5</sup>Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
<scripture passage="Rom 12:6" parsed="|Rom|12|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.6" />
<sup>6</sup>Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
<scripture passage="Rom 12:7" parsed="|Rom|12|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.7" />
<sup>7</sup>Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
<scripture passage="Rom 12:8" parsed="|Rom|12|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.8" />
<sup>8</sup>Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
<scripture passage="Rom 12:9" parsed="|Rom|12|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.9" />
<sup>9</sup>Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
<scripture passage="Rom 12:10" parsed="|Rom|12|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.10" />
<sup>10</sup>Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
<scripture passage="Rom 12:11" parsed="|Rom|12|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.11" />
<sup>11</sup>Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
<scripture passage="Rom 12:12" parsed="|Rom|12|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.12" />
<sup>12</sup>Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
<scripture passage="Rom 12:13" parsed="|Rom|12|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.13" />
<sup>13</sup>Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
<scripture passage="Rom 12:14" parsed="|Rom|12|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.14" />
<sup>14</sup>Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.
<scripture passage="Rom 12:15" parsed="|Rom|12|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.15" />
<sup>15</sup>Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
<scripture passage="Rom 12:16" parsed="|Rom|12|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.16" />
<sup>16</sup>Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.
<scripture passage="Rom 12:17" parsed="|Rom|12|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.17" />
<sup>17</sup>Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.
<scripture passage="Rom 12:18" parsed="|Rom|12|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.18" />
<sup>18</sup>Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.
<scripture passage="Rom 12:19" parsed="|Rom|12|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.19" />
<sup>19</sup>Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana."
<scripture passage="Rom 12:20" parsed="|Rom|12|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.20" />
<sup>20</sup>Tena, Maandiko yasema: "Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake."
<scripture passage="Rom 12:21" parsed="|Rom|12|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.12.21" />
<sup>21</sup>Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 13" progress="62.44%" prev="Rom.12" next="Rom.14" id="Rom.13">
<h3 id="Rom.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Rom.13-p1">
<scripture passage="Rom 13:1" parsed="|Rom|13|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.1" />
<sup>1</sup>Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu.
<scripture passage="Rom 13:2" parsed="|Rom|13|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.2" />
<sup>2</sup>Anayepinga mamlaka ya viongozi anapinga agizo la Mungu; nao wafanyao hivyo wanajiletea hukumu wenyewe,
<scripture passage="Rom 13:3" parsed="|Rom|13|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.3" />
<sup>3</sup>Maana, watawala hawasababishi hofu kwa watu wema, ila kwa watu wabaya. Basi, wataka usimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanya mema naye atakusifu;
<scripture passage="Rom 13:4" parsed="|Rom|13|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.4" />
<sup>4</sup>maana yeye ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwa faida yako. Lakini ukifanya mabaya, basi, huna budi kumwogopa, maana anao kweli uwezo wa kutoa adhabu. Yeye ni mtumishi wa Mungu na huitekeleza ghadhabu ya Mungu kwao watendao maovu.
<scripture passage="Rom 13:5" parsed="|Rom|13|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.5" />
<sup>5</sup>Kwa hiyo ni lazima kuwatii wenye mamlaka, si tu kwa sababu ya kuogopa ghadhabu ya Mungu, bali pia kwa sababu dhamiri inadai hivyo.
<scripture passage="Rom 13:6" parsed="|Rom|13|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.6" />
<sup>6</sup>Kwa sababu hiyohiyo ninyi hulipa kodi; maana viongozi hao humtumikia Mungu ikiwa wanatimiza wajibu wao.
<scripture passage="Rom 13:7" parsed="|Rom|13|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.7" />
<sup>7</sup>Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima.
<scripture passage="Rom 13:8" parsed="|Rom|13|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.8" />
<sup>8</sup>Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza Sheria.
<scripture passage="Rom 13:9" parsed="|Rom|13|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.9" />
<sup>9</sup>Maana, amri hizi: "Usizini; Usiue; Usitamani;" na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
<scripture passage="Rom 13:10" parsed="|Rom|13|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.10" />
<sup>10</sup>Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, kwa mapendo Sheria yote hutimizwa.
<scripture passage="Rom 13:11" parsed="|Rom|13|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.11" />
<sup>11</sup>Zaidi ya hayo, ninyi mnajua tumo katika wakati gani: sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu u karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.
<scripture passage="Rom 13:12" parsed="|Rom|13|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.12" />
<sup>12</sup>Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga.
<scripture passage="Rom 13:13" parsed="|Rom|13|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.13" />
<sup>13</sup>Mwenendo wetu uwe wa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana; tusiwe na ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu.
<scripture passage="Rom 13:14" parsed="|Rom|13|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.13.14" />
<sup>14</sup>Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 14" progress="62.63%" prev="Rom.13" next="Rom.15" id="Rom.14">
<h3 id="Rom.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Rom.14-p1">
<scripture passage="Rom 14:1" parsed="|Rom|14|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.1" />
<sup>1</sup>Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.
<scripture passage="Rom 14:2" parsed="|Rom|14|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.2" />
<sup>2</sup>Watu huhitilafiana: mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.
<scripture passage="Rom 14:3" parsed="|Rom|14|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.3" />
<sup>3</sup>Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali.
<scripture passage="Rom 14:4" parsed="|Rom|14|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.4" />
<sup>4</sup>Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
<scripture passage="Rom 14:5" parsed="|Rom|14|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.5" />
<sup>5</sup>Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake.
<scripture passage="Rom 14:6" parsed="|Rom|14|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.6" />
<sup>6</sup>Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.
<scripture passage="Rom 14:7" parsed="|Rom|14|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.7" />
<sup>7</sup>Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe
<scripture passage="Rom 14:8" parsed="|Rom|14|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.8" />
<sup>8</sup>maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.
<scripture passage="Rom 14:9" parsed="|Rom|14|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.9" />
<sup>9</sup>Maana Kristo alikufa, akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazima na wafu.
<scripture passage="Rom 14:10" parsed="|Rom|14|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.10" />
<sup>10</sup>Kwa nini, basi wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
<scripture passage="Rom 14:11" parsed="|Rom|14|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.11" />
<sup>11</sup>Maana Maandiko yanasema: "Kama niishivyo, asema Bwana kila mtu atanipigia magoti, na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu."
<scripture passage="Rom 14:12" parsed="|Rom|14|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.12" />
<sup>12</sup>Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja yake mbele ya Mungu.
<scripture passage="Rom 14:13" parsed="|Rom|14|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.13" />
<sup>13</sup>Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
<scripture passage="Rom 14:14" parsed="|Rom|14|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.14" />
<sup>14</sup>Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi.
<scripture passage="Rom 14:15" parsed="|Rom|14|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.15" />
<sup>15</sup>Kama ukimhuzunisha ndugu yako kwa sababu ya chakula unachokula, basi mwenendo wako hauongozwi na mapendo. Usikubali hata kidogo chakula chako kiwe sababu ya kupotea kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake!
<scripture passage="Rom 14:16" parsed="|Rom|14|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.16" />
<sup>16</sup>Basi, msikubalie kitu mnachokiona kuwa kwenu ni kitu chema kidharauliwe.
<scripture passage="Rom 14:17" parsed="|Rom|14|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.17" />
<sup>17</sup>Maana Utawala wa Mungu si shauri la kula na kunywa, bali unahusika na kuwa na uadilifu, amani na furaha iletwayo na Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Rom 14:18" parsed="|Rom|14|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.18" />
<sup>18</sup>Anayemtumikia Kristo namna hiyo humpendeza Mungu, na kukubaliwa na watu.
<scripture passage="Rom 14:19" parsed="|Rom|14|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.19" />
<sup>19</sup>Kwa hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani, na yanayotusaidia kujengana.
<scripture passage="Rom 14:20" parsed="|Rom|14|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.20" />
<sup>20</sup>Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya ubishi juu ya chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.
<scripture passage="Rom 14:21" parsed="|Rom|14|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.21" />
<sup>21</sup>Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.
<scripture passage="Rom 14:22" parsed="|Rom|14|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.22" />
<sup>22</sup>Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
<scripture passage="Rom 14:23" parsed="|Rom|14|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.14.23" />
<sup>23</sup>Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 15" progress="62.96%" prev="Rom.14" next="Rom.16" id="Rom.15">
<h3 id="Rom.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Rom.15-p1">
<scripture passage="Rom 15:1" parsed="|Rom|15|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.1" />
<sup>1</sup>Sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale walio dhaifu wayakabili matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu.
<scripture passage="Rom 15:2" parsed="|Rom|15|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.2" />
<sup>2</sup>Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwa wema ili huyo apate kujijenga katika imani.
<scripture passage="Rom 15:3" parsed="|Rom|15|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.3" />
<sup>3</sup>Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo Maandiko: "Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi."
<scripture passage="Rom 15:4" parsed="|Rom|15|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.4" />
<sup>4</sup>Maana yote yalioandikwa yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na Maandiko hayo Matakatifu tupate kuwa na matumaini.
<scripture passage="Rom 15:5" parsed="|Rom|15|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.5" />
<sup>5</sup>Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni ninyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
<scripture passage="Rom 15:6" parsed="|Rom|15|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.6" />
<sup>6</sup>ili ninyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Rom 15:7" parsed="|Rom|15|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.7" />
<sup>7</sup>Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.
<scripture passage="Rom 15:8" parsed="|Rom|15|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.8" />
<sup>8</sup>Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
<scripture passage="Rom 15:9" parsed="|Rom|15|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.9" />
<sup>9</sup>ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa sababu hiyo, nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako."
<scripture passage="Rom 15:10" parsed="|Rom|15|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.10" />
<sup>10</sup>Tena Maandiko yasema: "Furahini, enyi watu wa mataifa; furahini pamoja na watu wake."
<scripture passage="Rom 15:11" parsed="|Rom|15|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.11" />
<sup>11</sup>Na tena: "Enyi mataifa yote, msifuni Bwana; enyi watu wote, msifuni."
<scripture passage="Rom 15:12" parsed="|Rom|15|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.12" />
<sup>12</sup>Tena Isaya asema: "Atatokea mtu katika ukoo wa Yese, naye atawatawala watu wa mataifa; nao watamtumainia."
<scripture passage="Rom 15:13" parsed="|Rom|15|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.13" />
<sup>13</sup>Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Rom 15:14" parsed="|Rom|15|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.14" />
<sup>14</sup>Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba ninyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana ninyi kwa ninyi.
<scripture passage="Rom 15:15" parsed="|Rom|15|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.15" />
<sup>15</sup>Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga, nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwa sababu ya neema aliyonijalia Mungu
<scripture passage="Rom 15:16" parsed="|Rom|15|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.16" />
<sup>16</sup>ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, dhabihu iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Rom 15:17" parsed="|Rom|15|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.17" />
<sup>17</sup>Kwa hiyo, nikiwa nimeungana na Kristo Yesu, naweza kujivunia huduma yangu kwa ajili ya Mungu.
<scripture passage="Rom 15:18" parsed="|Rom|15|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.18" />
<sup>18</sup>Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,
<scripture passage="Rom 15:19" parsed="|Rom|15|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.19" />
<sup>19</sup>kwa nguvu ya miujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho wa Mungu. Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko, nimeihubiri kikamilifu Habari Njema ya Kristo.
<scripture passage="Rom 15:20" parsed="|Rom|15|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.20" />
<sup>20</sup>Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.
<scripture passage="Rom 15:21" parsed="|Rom|15|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.21" />
<sup>21</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Watu wote ambao hawakuambiwa habari zote wataona; nao wale ambao hawajapata kusikia, wataelewa."
<scripture passage="Rom 15:22" parsed="|Rom|15|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.22" />
<sup>22</sup>Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi kuja kwenu.
<scripture passage="Rom 15:23" parsed="|Rom|15|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.23" />
<sup>23</sup>Lakini maadam sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu,
<scripture passage="Rom 15:24" parsed="|Rom|15|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.24" />
<sup>24</sup>natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
<scripture passage="Rom 15:25" parsed="|Rom|15|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.25" />
<sup>25</sup>Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumia watu wa Mungu kule Yerusalem.
<scripture passage="Rom 15:26" parsed="|Rom|15|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.26" />
<sup>26</sup>Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yemeamua kutoka mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu walio maskini huko Yerusalem.
<scripture passage="Rom 15:27" parsed="|Rom|15|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.27" />
<sup>27</sup>Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi katika mahitaji yao ya kidunia.
<scripture passage="Rom 15:28" parsed="|Rom|15|28|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.28" />
<sup>28</sup>Nitakapokwisha tekeleza kazi hiyo na kuwakabidhi mchango huo uliokusanywa kwa ajili yao, nitawatembeleeni ninyi nikiwa safarini kwenda Spania.
<scripture passage="Rom 15:29" parsed="|Rom|15|29|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.29" />
<sup>29</sup>Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.
<scripture passage="Rom 15:30" parsed="|Rom|15|30|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.30" />
<sup>30</sup>Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa kuniombea kwa Mungu.
<scripture passage="Rom 15:31" parsed="|Rom|15|31|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.31" />
<sup>31</sup>Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko Uyahudi, nayo huduma yangu huko Yerusalem ipate kukubaliwa na watu wa Mungu walioko huko.
<scripture passage="Rom 15:32" parsed="|Rom|15|32|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.32" />
<sup>32</sup>Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha, nikapumzike pamoja nanyi.
<scripture passage="Rom 15:33" parsed="|Rom|15|33|0|0" osisRef="Bible:Rom.15.33" />
<sup>33</sup>Mungu aliye chanzo cha amani na awe nanyi nyote! Amina!
</p>
</div3>

<div3 title="Romans 16" progress="63.41%" prev="Rom.15" next="iCor" id="Rom.16">
<h3 id="Rom.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Rom.16-p1">
<scripture passage="Rom 16:1" parsed="|Rom|16|1|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.1" />
<sup>1</sup>Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
<scripture passage="Rom 16:2" parsed="|Rom|16|2|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.2" />
<sup>2</sup>Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia.
<scripture passage="Rom 16:3" parsed="|Rom|16|3|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.3" />
<sup>3</sup>Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu.
<scripture passage="Rom 16:4" parsed="|Rom|16|4|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.4" />
<sup>4</sup>Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Rom 16:5" parsed="|Rom|16|5|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.5" />
<sup>5</sup>Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
<scripture passage="Rom 16:6" parsed="|Rom|16|6|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.6" />
<sup>6</sup>Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
<scripture passage="Rom 16:7" parsed="|Rom|16|7|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.7" />
<sup>7</sup>Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu waliofungwa gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena walikuwa Wakristo kabla yangu mimi.
<scripture passage="Rom 16:8" parsed="|Rom|16|8|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.8" />
<sup>8</sup>Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana na Bwana.
<scripture passage="Rom 16:9" parsed="|Rom|16|9|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.9" />
<sup>9</sup>Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika utumishi wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku.
<scripture passage="Rom 16:10" parsed="|Rom|16|10|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.10" />
<sup>10</sup>Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo umethibitishwa. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
<scripture passage="Rom 16:11" parsed="|Rom|16|11|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.11" />
<sup>11</sup>Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa jamaa yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana.
<scripture passage="Rom 16:12" parsed="|Rom|16|12|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.12" />
<sup>12</sup>Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi wa Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Bwana.
<scripture passage="Rom 16:13" parsed="|Rom|16|13|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.13" />
<sup>13</sup>Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana, na mama yake ambaye ni mama yangu pia.
<scripture passage="Rom 16:14" parsed="|Rom|16|14|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.14" />
<sup>14</sup>Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.
<scripture passage="Rom 16:15" parsed="|Rom|16|15|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.15" />
<sup>15</sup>Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olumpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.
<scripture passage="Rom 16:16" parsed="|Rom|16|16|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.16" />
<sup>16</sup>Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara ya upendo. Salamu kwenu kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.
<scripture passage="Rom 16:17" parsed="|Rom|16|17|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.17" />
<sup>17</sup>Ndugu zangu, nawasihi muwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,
<scripture passage="Rom 16:18" parsed="|Rom|16|18|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.18" />
<sup>18</sup>maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.
<scripture passage="Rom 16:19" parsed="|Rom|16|19|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.19" />
<sup>19</sup>Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya furaha yangu. Nawatakeni muwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya.
<scripture passage="Rom 16:20" parsed="|Rom|16|20|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.20" />
<sup>20</sup>Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
<scripture passage="Rom 16:21" parsed="|Rom|16|21|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.21" />
<sup>21</sup>Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali kadhalika Lukio, Yasoni, na Sosipatro, wananchi wenzangu, wanawasalimu.
<scripture passage="Rom 16:22" parsed="|Rom|16|22|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.22" />
<sup>22</sup>Nami Tertio, ninayeandika barua hii nawasalimuni katika Bwana.
<scripture passage="Rom 16:23" parsed="|Rom|16|23|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.23" />
<sup>23</sup>Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana kwake, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto, wanawasalimu.<i>fb</i>
<scripture passage="Rom 16:24" parsed="|Rom|16|24|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.24" />
<sup>24</sup>missing
<scripture passage="Rom 16:25" parsed="|Rom|16|25|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.25" />
<sup>25</sup>Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya ujumbe wa Yesu Kristo, na katika ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi zilizopita.
<scripture passage="Rom 16:26" parsed="|Rom|16|26|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.26" />
<sup>26</sup>Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirisha kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii.
<scripture passage="Rom 16:27" parsed="|Rom|16|27|0|0" osisRef="Bible:Rom.16.27" />
<sup>27</sup>Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu kwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="1 Corinthians" progress="63.76%" prev="Rom.16" next="iCor.1" id="iCor">
<h2 id="iCor-p0.1">1 Corinthians</h2>

<div3 title="1 Corinthians 1" progress="63.76%" prev="iCor" next="iCor.2" id="iCor.1">
<h3 id="iCor.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iCor.1-p1">
<scripture passage="iCor 1:1" parsed="|1Cor|1|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,
<scripture passage="iCor 1:2" parsed="|1Cor|1|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.2" />
<sup>2</sup>tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia.
<scripture passage="iCor 1:3" parsed="|1Cor|1|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.3" />
<sup>3</sup>Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iCor 1:4" parsed="|1Cor|1|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.4" />
<sup>4</sup>Ninamshukuru Mungu wangu daima kwa ajili yenu kwa sababu amewatunukia ninyi neema yake kwa njia ya Kristo Yesu.
<scripture passage="iCor 1:5" parsed="|1Cor|1|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.5" />
<sup>5</sup>Maana, kwa kuungana na Kristo mmetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwa elimu yote na uwezo wote wa kuhubiri,
<scripture passage="iCor 1:6" parsed="|1Cor|1|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.6" />
<sup>6</sup>kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwa ndani yenu,
<scripture passage="iCor 1:7" parsed="|1Cor|1|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.7" />
<sup>7</sup>hata hampungukiwi kipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iCor 1:8" parsed="|1Cor|1|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.8" />
<sup>8</sup>Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia Siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iCor 1:9" parsed="|1Cor|1|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.9" />
<sup>9</sup>Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae Yesu Kristo Bwana wetu.
<scripture passage="iCor 1:10" parsed="|1Cor|1|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.10" />
<sup>10</sup>Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na fikira moja na nia moja.
<scripture passage="iCor 1:11" parsed="|1Cor|1|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.11" />
<sup>11</sup>Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
<scripture passage="iCor 1:12" parsed="|1Cor|1|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.12" />
<sup>12</sup>Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, "Mimi ni wa Paulo," mwingine: "Mimi ni wa Apolo," mwingine: "Mimi ni wa Kefa," na mwingine: "Mimi ni wa Kristo,".
<scripture passage="iCor 1:13" parsed="|1Cor|1|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.13" />
<sup>13</sup>Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?
<scripture passage="iCor 1:14" parsed="|1Cor|1|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.14" />
<sup>14</sup>Namshukuru Mungu kwamba sikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa tu Krispo na Gayo.
<scripture passage="iCor 1:15" parsed="|1Cor|1|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.15" />
<sup>15</sup>Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jina langu.
<scripture passage="iCor 1:16" parsed="|1Cor|1|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.16" />
<sup>16</sup>Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
<scripture passage="iCor 1:17" parsed="|1Cor|1|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.17" />
<sup>17</sup>Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
<scripture passage="iCor 1:18" parsed="|1Cor|1|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.18" />
<sup>18</sup>Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.
<scripture passage="iCor 1:19" parsed="|1Cor|1|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.19" />
<sup>19</sup>Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na elimu ya wataalamu nitaitupilia mbali."
<scripture passage="iCor 1:20" parsed="|1Cor|1|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.20" />
<sup>20</sup>Yu wapi basi, mwenye hekima? Yu wapi basi, mwalimu wa Sheria? Naye bingwa wa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanya hekima ya ulimwengu kuwa upumbavu.
<scripture passage="iCor 1:21" parsed="|1Cor|1|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.21" />
<sup>21</sup>Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.
<scripture passage="iCor 1:22" parsed="|1Cor|1|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.22" />
<sup>22</sup>Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima;
<scripture passage="iCor 1:23" parsed="|1Cor|1|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.23" />
<sup>23</sup>lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;
<scripture passage="iCor 1:24" parsed="|1Cor|1|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.24" />
<sup>24</sup>lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu.
<scripture passage="iCor 1:25" parsed="|1Cor|1|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.25" />
<sup>25</sup>Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.
<scripture passage="iCor 1:26" parsed="|1Cor|1|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.26" />
<sup>26</sup>Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu wa tabaka ya juu.
<scripture passage="iCor 1:27" parsed="|1Cor|1|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.27" />
<sup>27</sup>Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
<scripture passage="iCor 1:28" parsed="|1Cor|1|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.28" />
<sup>28</sup>Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.
<scripture passage="iCor 1:29" parsed="|1Cor|1|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.29" />
<sup>29</sup>Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu.
<scripture passage="iCor 1:30" parsed="|1Cor|1|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.30" />
<sup>30</sup>Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
<scripture passage="iCor 1:31" parsed="|1Cor|1|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.1.31" />
<sup>31</sup>Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mwenye kutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana."
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 2" progress="64.19%" prev="iCor.1" next="iCor.3" id="iCor.2">
<h3 id="iCor.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iCor.2-p1">
<scripture passage="iCor 2:1" parsed="|1Cor|2|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu.
<scripture passage="iCor 2:2" parsed="|1Cor|2|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.2" />
<sup>2</sup>Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa.
<scripture passage="iCor 2:3" parsed="|1Cor|2|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.3" />
<sup>3</sup>Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi.
<scripture passage="iCor 2:4" parsed="|1Cor|2|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.4" />
<sup>4</sup>Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.
<scripture passage="iCor 2:5" parsed="|1Cor|2|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.5" />
<sup>5</sup>Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.
<scripture passage="iCor 2:6" parsed="|1Cor|2|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.6" />
<sup>6</sup>Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
<scripture passage="iCor 2:7" parsed="|1Cor|2|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.7" />
<sup>7</sup>Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
<scripture passage="iCor 2:8" parsed="|1Cor|2|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.8" />
<sup>8</sup>Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangalielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
<scripture passage="iCor 2:9" parsed="|1Cor|2|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.9" />
<sup>9</sup>Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao."
<scripture passage="iCor 2:10" parsed="|1Cor|2|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.10" />
<sup>10</sup>Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu.
<scripture passage="iCor 2:11" parsed="|1Cor|2|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.11" />
<sup>11</sup>Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
<scripture passage="iCor 2:12" parsed="|1Cor|2|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.12" />
<sup>12</sup>Sasa sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu.
<scripture passage="iCor 2:13" parsed="|1Cor|2|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.13" />
<sup>13</sup>Basi sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho.
<scripture passage="iCor 2:14" parsed="|1Cor|2|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.14" />
<sup>14</sup>Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho.
<scripture passage="iCor 2:15" parsed="|1Cor|2|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.15" />
<sup>15</sup>Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine.
<scripture passage="iCor 2:16" parsed="|1Cor|2|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.2.16" />
<sup>16</sup>Maandiko yasema: "Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?" Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 3" progress="64.41%" prev="iCor.2" next="iCor.4" id="iCor.3">
<h3 id="iCor.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iCor.3-p1">
<scripture passage="iCor 3:1" parsed="|1Cor|3|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu mlio na huyo Roho. Nilipaswa kusema nanyi kama watu wa kidunia, kama watoto wachanga katika maisha ya Kikristo.
<scripture passage="iCor 3:2" parsed="|1Cor|3|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.2" />
<sup>2</sup>Ilinibidi kuwalisheni kwa maziwa, na si kwa chakula kigumu, kwani hamkuwa tayari kukipokea. Hata sasa hamko tayari.
<scripture passage="iCor 3:3" parsed="|1Cor|3|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.3" />
<sup>3</sup>Maana bado mu watu wa kidunia. Je, si kweli kwamba bado uko wivu na magombano kati yenu? Mambo hayo yanaonyesha wazi kwamba ninyi bado ni watu wa kidunia, mnaishi mtindo wa kidunia.
<scripture passage="iCor 3:4" parsed="|1Cor|3|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.4" />
<sup>4</sup>Mmoja wenu anaposema, "Mimi ni wa Paulo", na mwingine, "Mimi ni wa Apolo", je, hiyo haionyeshi kwamba mnaishi bado kama watu wa dunia hii tu?
<scripture passage="iCor 3:5" parsed="|1Cor|3|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.5" />
<sup>5</sup>Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Sisi ni watumishi tu ambao tuliwaleteeni ninyi imani. Kila mmoja wetu anafanya kazi aliyopewa na Bwana.
<scripture passage="iCor 3:6" parsed="|1Cor|3|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.6" />
<sup>6</sup>Mimi nilipanda mbegu, Apolo akamwagilia maji; lakini aliyeiotesha mbegu ni Mungu.
<scripture passage="iCor 3:7" parsed="|1Cor|3|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.7" />
<sup>7</sup>Wa maana si yule aliyepanda mbegu, au yule aliyemwagilia maji; wa maana ni Mungu aliyeiwezesha mbegu kuota.
<scripture passage="iCor 3:8" parsed="|1Cor|3|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.8" />
<sup>8</sup>Yule aliyepanda na yule aliyemwagilia maji wote ni sawa, ingawa kila mmoja atapokea tuzo lake kufuatana na jitihada yake mwenyewe.
<scripture passage="iCor 3:9" parsed="|1Cor|3|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.9" />
<sup>9</sup>Maana sisi ni ndugu, wafanyakazi pamoja na Mungu; na ninyi ni shamba lake; ninyi ni jengo lake.
<scripture passage="iCor 3:10" parsed="|1Cor|3|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.10" />
<sup>10</sup>Kwa msaada wa neema aliyonipa Mungu, nimefaulu, kama mwashi stadi mwenye busara, kuweka msingi ambao juu yake mtu mwingine anajenga. Basi, kila mmoja awe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake.
<scripture passage="iCor 3:11" parsed="|1Cor|3|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.11" />
<sup>11</sup>Hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine badala ya ule uliokwisha wekwa, yaani Yesu Kristo.
<scripture passage="iCor 3:12" parsed="|1Cor|3|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.12" />
<sup>12</sup>Juu ya msingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha au mawe ya thamani; anaweza kutumia miti, majani au nyasi.
<scripture passage="iCor 3:13" parsed="|1Cor|3|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.13" />
<sup>13</sup>Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati Siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonyesha ubora wake.
<scripture passage="iCor 3:14" parsed="|1Cor|3|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.14" />
<sup>14</sup>Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo;
<scripture passage="iCor 3:15" parsed="|1Cor|3|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.15" />
<sup>15</sup>lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni.
<scripture passage="iCor 3:16" parsed="|1Cor|3|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.16" />
<sup>16</sup>Je, hamjui kwamba ninyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
<scripture passage="iCor 3:17" parsed="|1Cor|3|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.17" />
<sup>17</sup>Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni ninyi wenyewe.
<scripture passage="iCor 3:18" parsed="|1Cor|3|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.18" />
<sup>18</sup>Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
<scripture passage="iCor 3:19" parsed="|1Cor|3|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.19" />
<sup>19</sup>Maana, hekima ya kidunia ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwani Maandiko Matakatifu yasema: "Mungu huwanasa wenye hekima katika ujanja wao."
<scripture passage="iCor 3:20" parsed="|1Cor|3|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.20" />
<sup>20</sup>Na tena: "Bwana ajua kwamba mawazo ya wenye hekima hayafai."
<scripture passage="iCor 3:21" parsed="|1Cor|3|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.21" />
<sup>21</sup>Basi, mtu asijivunie watu. Maana kila kitu ni chenu.
<scripture passage="iCor 3:22" parsed="|1Cor|3|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.22" />
<sup>22</sup>Paulo, Apolo na Kefa, ulimwengu, maisha na kifo; mambo ya sasa na ya baadaye, yote ni yenu.
<scripture passage="iCor 3:23" parsed="|1Cor|3|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.3.23" />
<sup>23</sup>Lakini ninyi ni wa Kristo naye Kristo ni wa Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 4" progress="64.70%" prev="iCor.3" next="iCor.5" id="iCor.4">
<h3 id="iCor.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iCor.4-p1">
<scripture passage="iCor 4:1" parsed="|1Cor|4|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.1" />
<sup>1</sup>Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu.
<scripture passage="iCor 4:2" parsed="|1Cor|4|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.2" />
<sup>2</sup>Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu.
<scripture passage="iCor 4:3" parsed="|1Cor|4|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.3" />
<sup>3</sup>Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, au na mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu.
<scripture passage="iCor 4:4" parsed="|1Cor|4|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.4" />
<sup>4</sup>Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwamba sina lawama. Bwana ndiye anayenihukumu.
<scripture passage="iCor 4:5" parsed="|1Cor|4|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.5" />
<sup>5</sup>Basi, msihukumu kabla ya wakati wake acheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichua mambo ya giza yaliyofichika, na kuonyesha wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
<scripture passage="iCor 4:6" parsed="|1Cor|4|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.6" />
<sup>6</sup>Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: "Zingatieni yaliyoandikwa." Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
<scripture passage="iCor 4:7" parsed="|1Cor|4|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.7" />
<sup>7</sup>Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
<scripture passage="iCor 4:8" parsed="|1Cor|4|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.8" />
<sup>8</sup>Haya, mmekwisha shiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalme bila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweli watawala, ili nasi pia tuweze kutawala pamoja nanyi.
<scripture passage="iCor 4:9" parsed="|1Cor|4|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.9" />
<sup>9</sup>Nafikiri Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kama watu waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu.
<scripture passage="iCor 4:10" parsed="|1Cor|4|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.10" />
<sup>10</sup>Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, ninyi ni wenye nguvu. Ninyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.
<scripture passage="iCor 4:11" parsed="|1Cor|4|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.11" />
<sup>11</sup>Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi.
<scripture passage="iCor 4:12" parsed="|1Cor|4|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.12" />
<sup>12</sup>Tena twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia;
<scripture passage="iCor 4:13" parsed="|1Cor|4|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.13" />
<sup>13</sup>tukisingiziwa, tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kama uchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi ni takataka!
<scripture passage="iCor 4:14" parsed="|1Cor|4|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.14" />
<sup>14</sup>Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi.
<scripture passage="iCor 4:15" parsed="|1Cor|4|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.15" />
<sup>15</sup>Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
<scripture passage="iCor 4:16" parsed="|1Cor|4|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.16" />
<sup>16</sup>Kwa hiyo, nawasihi: fuateni mfano wangu.
<scripture passage="iCor 4:17" parsed="|1Cor|4|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.17" />
<sup>17</sup>Ndiyo maana nimemtuma Timetheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuishi maisha ya Kikristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
<scripture passage="iCor 4:18" parsed="|1Cor|4|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.18" />
<sup>18</sup>Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu.
<scripture passage="iCor 4:19" parsed="|1Cor|4|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.19" />
<sup>19</sup>Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kila wanachoweza kufanya.
<scripture passage="iCor 4:20" parsed="|1Cor|4|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.20" />
<sup>20</sup>Maana Utawala wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu.
<scripture passage="iCor 4:21" parsed="|1Cor|4|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.4.21" />
<sup>21</sup>Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 5" progress="64.98%" prev="iCor.4" next="iCor.6" id="iCor.5">
<h3 id="iCor.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iCor.5-p1">
<scripture passage="iCor 5:1" parsed="|1Cor|5|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.1" />
<sup>1</sup>Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!
<scripture passage="iCor 5:2" parsed="|1Cor|5|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.2" />
<sup>2</sup>Mnawezaje kujivuna? Ingekuwa afadhali kwenu kuomboleza, na huyo aliyefanya kitu hicho aondolewe miongoni mwenu.
<scripture passage="iCor 5:3" parsed="|1Cor|5|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.3" />
<sup>3</sup>Nami, kwa upande wangu, ingawa kwa mwili niko mbali nanyi, hata hivyo kwa roho niko hapo pamoja nanyi: na hivyo, kama vile nipo hapo, nimekwisha mhukumu huyo aliyefanya jambo hilo la aibu.
<scripture passage="iCor 5:4" parsed="|1Cor|5|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.4" />
<sup>4</sup>Wakati mnapokusanyika pamoja kwa jina la Bwana Yesu, nami nikiwa pamoja nanyi kwa roho, basi, kwa uwezo wa Bwana wetu Yesu,
<scripture passage="iCor 5:5" parsed="|1Cor|5|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.5" />
<sup>5</sup>mkabidhini mtu huyo kwa Shetani ili mwili wake uharibiwe na roho yake iweze kuokolewa Siku ile ya Bwana.
<scripture passage="iCor 5:6" parsed="|1Cor|5|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.6" />
<sup>6</sup>Majivuno yenu hayafai! Je, hamjui kwamba chachu kidogo huchachusha donge lote la unga?
<scripture passage="iCor 5:7" parsed="|1Cor|5|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.7" />
<sup>7</sup>Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo, Pasaka yetu, amekwisha tolewa tambiko.
<scripture passage="iCor 5:8" parsed="|1Cor|5|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.8" />
<sup>8</sup>Basi, tufanye karamu hiyo si kwa chachu ile ya kale, chachu ya ubaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, mkate wa usafi na kweli.
<scripture passage="iCor 5:9" parsed="|1Cor|5|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.9" />
<sup>9</sup>Niliwaandikia katika barua yangu msishirikiane na wazinzi.
<scripture passage="iCor 5:10" parsed="|1Cor|5|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.10" />
<sup>10</sup>Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu ninyi kuihama dunia hii kabisa!
<scripture passage="iCor 5:11" parsed="|1Cor|5|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.11" />
<sup>11</sup>Nilichoandika ni hiki: msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.
<scripture passage="iCor 5:12" parsed="|1Cor|5|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.12" />
<sup>12</sup>Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, ninyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu ninyi wenyewe?
<scripture passage="iCor 5:13" parsed="|1Cor|5|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.5.13" />
<sup>13</sup>Mfukuzeni mbali nanyi huyo mwovu!
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 6" progress="65.16%" prev="iCor.5" next="iCor.7" id="iCor.6">
<h3 id="iCor.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="iCor.6-p1">
<scripture passage="iCor 6:1" parsed="|1Cor|6|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.1" />
<sup>1</sup>Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu muumini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
<scripture passage="iCor 6:2" parsed="|1Cor|6|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.2" />
<sup>2</sup>Je, hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi, ulimwengu utahukumiwa nanyi, kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika mambo madogo?
<scripture passage="iCor 6:3" parsed="|1Cor|6|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.3" />
<sup>3</sup>Je, hamjui kwamba, licha ya kuhukumu mambo ya kawaida ya kila siku, tutawahukumu hata malaika?
<scripture passage="iCor 6:4" parsed="|1Cor|6|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.4" />
<sup>4</sup>Mnapokuwa na mizozo juu ya mambo ya kawaida, je, mnawaita wawe mahakimu watu ambao hata hawalijali kanisa?
<scripture passage="iCor 6:5" parsed="|1Cor|6|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.5" />
<sup>5</sup>Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
<scripture passage="iCor 6:6" parsed="|1Cor|6|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.6" />
<sup>6</sup>Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu yake mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini.
<scripture passage="iCor 6:7" parsed="|1Cor|6|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.7" />
<sup>7</sup>Kwa kweli huko kushtakiana tu wenyewe kwa wenyewe kwabainisha kwamba mmeshindwa kabisa! Je, haingekuwa jambo bora zaidi kwenu kudhulumiwa! Haingekuwa bora zaidi kwenu kunyang`anywa mali yenu?
<scripture passage="iCor 6:8" parsed="|1Cor|6|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.8" />
<sup>8</sup>Lakini, badala yake, ninyi ndio mnaodhulumu na kunyang`anya; tena, hayo mnawafanyia ndugu zenu!
<scripture passage="iCor 6:9" parsed="|1Cor|6|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.9" />
<sup>9</sup>Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,
<scripture passage="iCor 6:10" parsed="|1Cor|6|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.10" />
<sup>10</sup>wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang`anyi, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu.
<scripture passage="iCor 6:11" parsed="|1Cor|6|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.11" />
<sup>11</sup>Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa watakatifu, na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.
<scripture passage="iCor 6:12" parsed="|1Cor|6|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.12" />
<sup>12</sup>Mtu anaweza kusema: "Kwangu mimi kila kitu ni halali." Sawa; lakini si kila kitu kinafaa. Nakubali kwamba kila kitu ni halali kwangu lakini sitaki kutawaliwa na kitu chochote.
<scripture passage="iCor 6:13" parsed="|1Cor|6|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.13" />
<sup>13</sup>Unaweza kusema: "Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula." Sawa; lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mtu si kwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili ya kumtumikia Bwana, naye Bwana ni kwa ajili ya mwili.
<scripture passage="iCor 6:14" parsed="|1Cor|6|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.14" />
<sup>14</sup>Basi, Mungu aliyemfufua Bwana kutoka wafu atatufufua nasi pia kwa nguvu yake.
<scripture passage="iCor 6:15" parsed="|1Cor|6|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.15" />
<sup>15</sup>Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo!
<scripture passage="iCor 6:16" parsed="|1Cor|6|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.16" />
<sup>16</sup>Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye--kama ilivyoandikwa: "Nao wawili watakuwa mwili mmoja."
<scripture passage="iCor 6:17" parsed="|1Cor|6|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.17" />
<sup>17</sup>Lakini aliyejiunga na Bwana huwa roho moja naye.
<scripture passage="iCor 6:18" parsed="|1Cor|6|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.18" />
<sup>18</sup>Jiepusheni kabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zote hutendwa nje ya mwili lakini mzinzi hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
<scripture passage="iCor 6:19" parsed="|1Cor|6|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.19" />
<sup>19</sup>Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Ninyi basi, si mali yenu wenyewe.
<scripture passage="iCor 6:20" parsed="|1Cor|6|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.6.20" />
<sup>20</sup>Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 7" progress="65.44%" prev="iCor.6" next="iCor.8" id="iCor.7">
<h3 id="iCor.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="iCor.7-p1">
<scripture passage="iCor 7:1" parsed="|1Cor|7|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.1" />
<sup>1</sup>Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi;
<scripture passage="iCor 7:2" parsed="|1Cor|7|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.2" />
<sup>2</sup>lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
<scripture passage="iCor 7:3" parsed="|1Cor|7|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.3" />
<sup>3</sup>Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.
<scripture passage="iCor 7:4" parsed="|1Cor|7|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.4" />
<sup>4</sup>Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.
<scripture passage="iCor 7:5" parsed="|1Cor|7|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.5" />
<sup>5</sup>Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu.
<scripture passage="iCor 7:6" parsed="|1Cor|7|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.6" />
<sup>6</sup>Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri.
<scripture passage="iCor 7:7" parsed="|1Cor|7|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.7" />
<sup>7</sup>Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine kile.
<scripture passage="iCor 7:8" parsed="|1Cor|7|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.8" />
<sup>8</sup>Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
<scripture passage="iCor 7:9" parsed="|1Cor|7|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.9" />
<sup>9</sup>Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.
<scripture passage="iCor 7:10" parsed="|1Cor|7|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.10" />
<sup>10</sup>Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke asiachane na mumewe;
<scripture passage="iCor 7:11" parsed="|1Cor|7|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.11" />
<sup>11</sup>lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
<scripture passage="iCor 7:12" parsed="|1Cor|7|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.12" />
<sup>12</sup>Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
<scripture passage="iCor 7:13" parsed="|1Cor|7|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.13" />
<sup>13</sup>Na, kama mwanamke Mkristo anaye mume asiyeamini, na huyo mwanamume akakubali kuendelea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe.
<scripture passage="iCor 7:14" parsed="|1Cor|7|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.14" />
<sup>14</sup>Kwa maana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mkewe; na huyo mke asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwa si wa Mungu; kumbe sasa ni watoto wake Mungu.
<scripture passage="iCor 7:15" parsed="|1Cor|7|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.15" />
<sup>15</sup>Hata hivyo, ikiwa yule asiyeamini anataka kumwacha mwenzake aliye Mkristo, basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo, mume au mke, atakuwa huru. Maana Mungu amewaiteni ninyi muishi kwa amani.
<scripture passage="iCor 7:16" parsed="|1Cor|7|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.16" />
<sup>16</sup>Wewe mama Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mume wako? Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza kumwokoa mkeo?
<scripture passage="iCor 7:17" parsed="|1Cor|7|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.17" />
<sup>17</sup>Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa makanisa yote.
<scripture passage="iCor 7:18" parsed="|1Cor|7|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.18" />
<sup>18</sup>Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
<scripture passage="iCor 7:19" parsed="|1Cor|7|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.19" />
<sup>19</sup>Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilicho muhimu ni kuzishika amri za Mungu.
<scripture passage="iCor 7:20" parsed="|1Cor|7|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.20" />
<sup>20</sup>Basi, kila mmoja na abaki kama alivyokuwa wakati alipoitwa.
<scripture passage="iCor 7:21" parsed="|1Cor|7|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.21" />
<sup>21</sup>Je, wewe ulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakini ukipata fursa ya kuwa huru, itumie.
<scripture passage="iCor 7:22" parsed="|1Cor|7|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.22" />
<sup>22</sup>Maana yeye aliyeitwa na Bwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwa mtu huru, huwa mtumwa wa Kristo.
<scripture passage="iCor 7:23" parsed="|1Cor|7|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.23" />
<sup>23</sup>Nyote mmenunuliwa kwa bei; kwa hiyo msiwe tena watumwa wa watu.
<scripture passage="iCor 7:24" parsed="|1Cor|7|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.24" />
<sup>24</sup>Ndugu zangu, kila mmoja wenu basi, na abaki na Mungu kama alivyokuwa wakati alipoitwa.
<scripture passage="iCor 7:25" parsed="|1Cor|7|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.25" />
<sup>25</sup>Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
<scripture passage="iCor 7:26" parsed="|1Cor|7|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.26" />
<sup>26</sup>Basi, kutokana na shida iliyopo sasa nadhani ingefaa mtu abaki kama alivyo.
<scripture passage="iCor 7:27" parsed="|1Cor|7|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.27" />
<sup>27</sup>Je, umeoa? Basi, usitake kuachana na mkeo. Wewe hukuoa? Basi, usitake kuoa.
<scripture passage="iCor 7:28" parsed="|1Cor|7|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.28" />
<sup>28</sup>Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate ninyi.
<scripture passage="iCor 7:29" parsed="|1Cor|7|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.29" />
<sup>29</sup>Ndugu, nataka kusema hivi: muda uliobaki ni mfupi. Na tangu sasa wale waliooa na waishi kama vile hawakuoa;
<scripture passage="iCor 7:30" parsed="|1Cor|7|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.30" />
<sup>30</sup>wenye kulia wawe kama hawalii, na wenye kufurahi wawe kama hawafurahi; wanaonunua wawe kama hawana kitu;
<scripture passage="iCor 7:31" parsed="|1Cor|7|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.31" />
<sup>31</sup>nao wenye shughuli na dunia hii wawe kama vile hawana shughuli sana nayo. Maana ulimwengu huu, kama tuujuavyo, unapita.
<scripture passage="iCor 7:32" parsed="|1Cor|7|32|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.32" />
<sup>32</sup>Ningependa ninyi msiwe na wasiwasi. Mtu asiye na mke hujishughulisha na kazi ya Bwana jinsi atakavyompendeza Bwana.
<scripture passage="iCor 7:33" parsed="|1Cor|7|33|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.33" />
<sup>33</sup>Mtu aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia jinsi atakavyompendeza mkewe,
<scripture passage="iCor 7:34" parsed="|1Cor|7|34|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.34" />
<sup>34</sup>naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
<scripture passage="iCor 7:35" parsed="|1Cor|7|35|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.35" />
<sup>35</sup>Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuio. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
<scripture passage="iCor 7:36" parsed="|1Cor|7|36|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.36" />
<sup>36</sup>Kama mtu anaona kwamba hamtendei vyema mchumba wake asipomwoa, na kama tamaa zake zinamshinda, na afanye atakavyo; waoane tu; hatakuwa ametenda dhambi.
<scripture passage="iCor 7:37" parsed="|1Cor|7|37|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.37" />
<sup>37</sup>Lakini kama huyo mwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooa na kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamua namna ya kufanya, basi, anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyo mwenzake bikira.
<scripture passage="iCor 7:38" parsed="|1Cor|7|38|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.38" />
<sup>38</sup>Kwa maneno mengine: yule anayeamua kumwoa huyo mchumba wake anafanya vema; naye anayeamua kutomwoa anafanya vema zaidi.
<scripture passage="iCor 7:39" parsed="|1Cor|7|39|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.39" />
<sup>39</sup>Mwanamke huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
<scripture passage="iCor 7:40" parsed="|1Cor|7|40|0|0" osisRef="Bible:1Cor.7.40" />
<sup>40</sup>Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 8" progress="65.97%" prev="iCor.7" next="iCor.9" id="iCor.8">
<h3 id="iCor.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="iCor.8-p1">
<scripture passage="iCor 8:1" parsed="|1Cor|8|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.1" />
<sup>1</sup>Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga.
<scripture passage="iCor 8:2" parsed="|1Cor|8|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.2" />
<sup>2</sup>Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
<scripture passage="iCor 8:3" parsed="|1Cor|8|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.3" />
<sup>3</sup>Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye.
<scripture passage="iCor 8:4" parsed="|1Cor|8|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.4" />
<sup>4</sup>Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.
<scripture passage="iCor 8:5" parsed="|1Cor|8|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.5" />
<sup>5</sup>Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata kama wako miungu na mabwana wengi,
<scripture passage="iCor 8:6" parsed="|1Cor|8|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.6" />
<sup>6</sup>hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake.
<scripture passage="iCor 8:7" parsed="|1Cor|8|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.7" />
<sup>7</sup>Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
<scripture passage="iCor 8:8" parsed="|1Cor|8|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.8" />
<sup>8</sup>Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.
<scripture passage="iCor 8:9" parsed="|1Cor|8|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.9" />
<sup>9</sup>Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
<scripture passage="iCor 8:10" parsed="|1Cor|8|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.10" />
<sup>10</sup>Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
<scripture passage="iCor 8:11" parsed="|1Cor|8|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.11" />
<sup>11</sup>Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
<scripture passage="iCor 8:12" parsed="|1Cor|8|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.12" />
<sup>12</sup>Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
<scripture passage="iCor 8:13" parsed="|1Cor|8|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.8.13" />
<sup>13</sup>Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 9" progress="66.15%" prev="iCor.8" next="iCor.10" id="iCor.9">
<h3 id="iCor.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="iCor.9-p1">
<scripture passage="iCor 9:1" parsed="|1Cor|9|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.1" />
<sup>1</sup>Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?
<scripture passage="iCor 9:2" parsed="|1Cor|9|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.2" />
<sup>2</sup>Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
<scripture passage="iCor 9:3" parsed="|1Cor|9|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.3" />
<sup>3</sup>Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii:
<scripture passage="iCor 9:4" parsed="|1Cor|9|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.4" />
<sup>4</sup>Je, hatuna haki ya kula na kunywa?
<scripture passage="iCor 9:5" parsed="|1Cor|9|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.5" />
<sup>5</sup>Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara zetu, kama vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa?
<scripture passage="iCor 9:6" parsed="|1Cor|9|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.6" />
<sup>6</sup>Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi?
<scripture passage="iCor 9:7" parsed="|1Cor|9|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.7" />
<sup>7</sup>Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
<scripture passage="iCor 9:8" parsed="|1Cor|9|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.8" />
<sup>8</sup>Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemi hivyo?
<scripture passage="iCor 9:9" parsed="|1Cor|9|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.9" />
<sup>9</sup>Imeandikwa katika Sheria ya Mose: "Usimfunge kinywa ng`ombe anapoliwata nafaka." Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng`ombe?
<scripture passage="iCor 9:10" parsed="|1Cor|9|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.10" />
<sup>10</sup>Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili yetu; kwani yule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wana haki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno.
<scripture passage="iCor 9:11" parsed="|1Cor|9|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.11" />
<sup>11</sup>Ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia?
<scripture passage="iCor 9:12" parsed="|1Cor|9|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.12" />
<sup>12</sup>Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.
<scripture passage="iCor 9:13" parsed="|1Cor|9|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.13" />
<sup>13</sup>Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
<scripture passage="iCor 9:14" parsed="|1Cor|9|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.14" />
<sup>14</sup>Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo.
<scripture passage="iCor 9:15" parsed="|1Cor|9|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.15" />
<sup>15</sup>Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure.
<scripture passage="iCor 9:16" parsed="|1Cor|9|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.16" />
<sup>16</sup>Ikiwa ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!
<scripture passage="iCor 9:17" parsed="|1Cor|9|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.17" />
<sup>17</sup>Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadam naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze.
<scripture passage="iCor 9:18" parsed="|1Cor|9|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.18" />
<sup>18</sup>Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.
<scripture passage="iCor 9:19" parsed="|1Cor|9|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.19" />
<sup>19</sup>Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
<scripture passage="iCor 9:20" parsed="|1Cor|9|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.20" />
<sup>20</sup>Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini ya Sheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili niwapate hao walio chini ya Sheria.
<scripture passage="iCor 9:21" parsed="|1Cor|9|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.21" />
<sup>21</sup>Na kwa wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
<scripture passage="iCor 9:22" parsed="|1Cor|9|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.22" />
<sup>22</sup>Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
<scripture passage="iCor 9:23" parsed="|1Cor|9|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.23" />
<sup>23</sup>Nafanya haya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki baraka zake.
<scripture passage="iCor 9:24" parsed="|1Cor|9|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.24" />
<sup>24</sup>Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
<scripture passage="iCor 9:25" parsed="|1Cor|9|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.25" />
<sup>25</sup>Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima.
<scripture passage="iCor 9:26" parsed="|1Cor|9|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.26" />
<sup>26</sup>Ndivyo basi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyo ninavyopigana, na si kama bondia anayetupa ngumi zake hewani.
<scripture passage="iCor 9:27" parsed="|1Cor|9|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.9.27" />
<sup>27</sup>Naupa mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine. ic
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 10" progress="66.52%" prev="iCor.9" next="iCor.11" id="iCor.10">
<h3 id="iCor.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="iCor.10-p1">
<scripture passage="iCor 10:1" parsed="|1Cor|10|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.
<scripture passage="iCor 10:2" parsed="|1Cor|10|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.2" />
<sup>2</sup>Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari.
<scripture passage="iCor 10:3" parsed="|1Cor|10|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.3" />
<sup>3</sup>Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,
<scripture passage="iCor 10:4" parsed="|1Cor|10|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.4" />
<sup>4</sup>wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
<scripture passage="iCor 10:5" parsed="|1Cor|10|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.5" />
<sup>5</sup>Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
<scripture passage="iCor 10:6" parsed="|1Cor|10|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.6" />
<sup>6</sup>Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
<scripture passage="iCor 10:7" parsed="|1Cor|10|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.7" />
<sup>7</sup>Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: "Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza."
<scripture passage="iCor 10:8" parsed="|1Cor|10|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.8" />
<sup>8</sup>Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini na tatu elfu.
<scripture passage="iCor 10:9" parsed="|1Cor|10|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.9" />
<sup>9</sup>Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
<scripture passage="iCor 10:10" parsed="|1Cor|10|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.10" />
<sup>10</sup>Wala msinung`unike kama baadhi yao walivyonung`unika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
<scripture passage="iCor 10:11" parsed="|1Cor|10|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.11" />
<sup>11</sup>Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili.
<scripture passage="iCor 10:12" parsed="|1Cor|10|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.12" />
<sup>12</sup>Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
<scripture passage="iCor 10:13" parsed="|1Cor|10|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.13" />
<sup>13</sup>Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
<scripture passage="iCor 10:14" parsed="|1Cor|10|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.14" />
<sup>14</sup>Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.
<scripture passage="iCor 10:15" parsed="|1Cor|10|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.15" />
<sup>15</sup>Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
<scripture passage="iCor 10:16" parsed="|1Cor|10|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.16" />
<sup>16</sup>Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
<scripture passage="iCor 10:17" parsed="|1Cor|10|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.17" />
<sup>17</sup>Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
<scripture passage="iCor 10:18" parsed="|1Cor|10|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.18" />
<sup>18</sup>Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.
<scripture passage="iCor 10:19" parsed="|1Cor|10|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.19" />
<sup>19</sup>Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu?
<scripture passage="iCor 10:20" parsed="|1Cor|10|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.20" />
<sup>20</sup>Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.
<scripture passage="iCor 10:21" parsed="|1Cor|10|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.21" />
<sup>21</sup>Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.
<scripture passage="iCor 10:22" parsed="|1Cor|10|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.22" />
<sup>22</sup>Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
<scripture passage="iCor 10:23" parsed="|1Cor|10|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.23" />
<sup>23</sup>Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.
<scripture passage="iCor 10:24" parsed="|1Cor|10|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.24" />
<sup>24</sup>Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
<scripture passage="iCor 10:25" parsed="|1Cor|10|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.25" />
<sup>25</sup>Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;
<scripture passage="iCor 10:26" parsed="|1Cor|10|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.26" />
<sup>26</sup>maana Maandiko yasema: "Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana."
<scripture passage="iCor 10:27" parsed="|1Cor|10|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.27" />
<sup>27</sup>Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
<scripture passage="iCor 10:28" parsed="|1Cor|10|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.28" />
<sup>28</sup>Lakini mtu akiwaambieni: "Chakula hiki kimetambikiwa sanamu," basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
<scripture passage="iCor 10:29" parsed="|1Cor|10|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.29" />
<sup>29</sup>Nasema, "kwa ajili ya dhamiri," si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: "Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
<scripture passage="iCor 10:30" parsed="|1Cor|10|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.30" />
<sup>30</sup>Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?"
<scripture passage="iCor 10:31" parsed="|1Cor|10|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.31" />
<sup>31</sup>Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
<scripture passage="iCor 10:32" parsed="|1Cor|10|32|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.32" />
<sup>32</sup>Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu.
<scripture passage="iCor 10:33" parsed="|1Cor|10|33|0|0" osisRef="Bible:1Cor.10.33" />
<sup>33</sup>Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 11" progress="66.89%" prev="iCor.10" next="iCor.12" id="iCor.11">
<h3 id="iCor.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="iCor.11-p1">
<scripture passage="iCor 11:1" parsed="|1Cor|11|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.1" />
<sup>1</sup>Niigeni mimi kama ninavyomwiga Kristo.
<scripture passage="iCor 11:2" parsed="|1Cor|11|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.2" />
<sup>2</sup>Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
<scripture passage="iCor 11:3" parsed="|1Cor|11|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.3" />
<sup>3</sup>Lakini napenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, na mwanamume ni kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo.
<scripture passage="iCor 11:4" parsed="|1Cor|11|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.4" />
<sup>4</sup>Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
<scripture passage="iCor 11:5" parsed="|1Cor|11|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.5" />
<sup>5</sup>Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe wa Mungu bila kufunika kichwa chake, anamdharau mumewe; anayefanya hivyo ni sawa tu na mwanamke aliyenyoa kichwa chake.
<scripture passage="iCor 11:6" parsed="|1Cor|11|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.6" />
<sup>6</sup>Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
<scripture passage="iCor 11:7" parsed="|1Cor|11|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.7" />
<sup>7</sup>Haifai mwanamume kufunika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na kioo cha utukufu wake Mungu; lakini mwanamke ni kioo cha utukufu wa mwanamume.
<scripture passage="iCor 11:8" parsed="|1Cor|11|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.8" />
<sup>8</sup>Mwanamume hakutoka kwa mwanamke, ila mwanamke alitoka kwa mwanamume.
<scripture passage="iCor 11:9" parsed="|1Cor|11|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.9" />
<sup>9</sup>Mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, ila mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
<scripture passage="iCor 11:10" parsed="|1Cor|11|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.10" />
<sup>10</sup>Ndiyo maana mwanamke hufunika kichwa chake, iwe ishara ya mamlaka yaliyo juu yake, na pia kwa sababu ya malaika.
<scripture passage="iCor 11:11" parsed="|1Cor|11|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.11" />
<sup>11</sup>Hata hivyo, mbele ya Bwana mwanamke si kitu bila mwanamume, naye mwanamume si kitu bila mwanamke.
<scripture passage="iCor 11:12" parsed="|1Cor|11|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.12" />
<sup>12</sup>Kama vile mwanamke alivyotokana na mwanamume, vivyo hivyo mwanamume huzaliwa na mwanamke; kila kitu hutoka kwa Mungu.
<scripture passage="iCor 11:13" parsed="|1Cor|11|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.13" />
<sup>13</sup>Amueni wenyewe: Je, inafaa mwanamke kumwomba Mungu bila kuvaa kitu kichwani?
<scripture passage="iCor 11:14" parsed="|1Cor|11|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.14" />
<sup>14</sup>Hata maumbile yenyewe huonyesha wazi kwamba kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu ni aibu kwake mwenyewe;
<scripture passage="iCor 11:15" parsed="|1Cor|11|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.15" />
<sup>15</sup>lakini kwa mwanamke kuwa na nywele ni heshima kwake; nywele zake ndefu amepewa ili zimfunike.
<scripture passage="iCor 11:16" parsed="|1Cor|11|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.16" />
<sup>16</sup>Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
<scripture passage="iCor 11:17" parsed="|1Cor|11|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.17" />
<sup>17</sup>Nikiwa bado nawapeni maagizo haya, siwezi hata kidogo kuwapa ninyi hongera kuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyi waumini yaleta hasara zaidi kuliko faida.
<scripture passage="iCor 11:18" parsed="|1Cor|11|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.18" />
<sup>18</sup>Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
<scripture passage="iCor 11:19" parsed="|1Cor|11|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.19" />
<sup>19</sup>maana ni lazima fikira tofauti ziweko miongoni mwenu, ili wale walio thabiti wapate kutambulikana.
<scripture passage="iCor 11:20" parsed="|1Cor|11|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.20" />
<sup>20</sup>Kweli mnakutana, lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana!
<scripture passage="iCor 11:21" parsed="|1Cor|11|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.21" />
<sup>21</sup>Maana mnapokula kila mmoja hukikalia chakula chake mwenyewe, hata hutokea kwamba baadhi yenu wana njaa, na wengine wamelewa!
<scripture passage="iCor 11:22" parsed="|1Cor|11|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.22" />
<sup>22</sup>Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
<scripture passage="iCor 11:23" parsed="|1Cor|11|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.23" />
<sup>23</sup>Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: kwamba, usiku ule Bwana Yesu aliotolewa, alitwaa mkate,
<scripture passage="iCor 11:24" parsed="|1Cor|11|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.24" />
<sup>24</sup>akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: "Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka."
<scripture passage="iCor 11:25" parsed="|1Cor|11|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.25" />
<sup>25</sup>Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: "Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka."
<scripture passage="iCor 11:26" parsed="|1Cor|11|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.26" />
<sup>26</sup>Maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.
<scripture passage="iCor 11:27" parsed="|1Cor|11|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.27" />
<sup>27</sup>Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.
<scripture passage="iCor 11:28" parsed="|1Cor|11|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.28" />
<sup>28</sup>Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho;
<scripture passage="iCor 11:29" parsed="|1Cor|11|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.29" />
<sup>29</sup>maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe.
<scripture passage="iCor 11:30" parsed="|1Cor|11|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.30" />
<sup>30</sup>Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa.
<scripture passage="iCor 11:31" parsed="|1Cor|11|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.31" />
<sup>31</sup>Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo.
<scripture passage="iCor 11:32" parsed="|1Cor|11|32|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.32" />
<sup>32</sup>Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
<scripture passage="iCor 11:33" parsed="|1Cor|11|33|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.33" />
<sup>33</sup>Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana kula chakula cha Bwana, kila mmoja amngoje mwenzake.
<scripture passage="iCor 11:34" parsed="|1Cor|11|34|0|0" osisRef="Bible:1Cor.11.34" />
<sup>34</sup>Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kukutana kwenu kusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine, nitawapeni maelezo nitakapokuja.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 12" progress="67.30%" prev="iCor.11" next="iCor.13" id="iCor.12">
<h3 id="iCor.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="iCor.12-p1">
<scripture passage="iCor 12:1" parsed="|1Cor|12|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya:
<scripture passage="iCor 12:2" parsed="|1Cor|12|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.2" />
<sup>2</sup>Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu.
<scripture passage="iCor 12:3" parsed="|1Cor|12|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.3" />
<sup>3</sup>Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: "Yesu alaaniwe!" Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: "Yesu ni Bwana," asipoongozwa na Roho Mtakatifu.
<scripture passage="iCor 12:4" parsed="|1Cor|12|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.4" />
<sup>4</sup>Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.
<scripture passage="iCor 12:5" parsed="|1Cor|12|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.5" />
<sup>5</sup>Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.
<scripture passage="iCor 12:6" parsed="|1Cor|12|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.6" />
<sup>6</sup>Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote.
<scripture passage="iCor 12:7" parsed="|1Cor|12|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.7" />
<sup>7</sup>Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote.
<scripture passage="iCor 12:8" parsed="|1Cor|12|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.8" />
<sup>8</sup>Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huyohuyo.
<scripture passage="iCor 12:9" parsed="|1Cor|12|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.9" />
<sup>9</sup>Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya;
<scripture passage="iCor 12:10" parsed="|1Cor|12|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.10" />
<sup>10</sup>humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua.
<scripture passage="iCor 12:11" parsed="|1Cor|12|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.11" />
<sup>11</sup>Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.
<scripture passage="iCor 12:12" parsed="|1Cor|12|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.12" />
<sup>12</sup>Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote--ingawaje ni vingi--hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.
<scripture passage="iCor 12:13" parsed="|1Cor|12|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.13" />
<sup>13</sup>Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.
<scripture passage="iCor 12:14" parsed="|1Cor|12|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.14" />
<sup>14</sup>Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.
<scripture passage="iCor 12:15" parsed="|1Cor|12|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.15" />
<sup>15</sup>Kama mguu ungejisemea: "Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili", je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!
<scripture passage="iCor 12:16" parsed="|1Cor|12|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.16" />
<sup>16</sup>Kama sikio lingejisemea: "Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili", je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
<scripture passage="iCor 12:17" parsed="|1Cor|12|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.17" />
<sup>17</sup>Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?
<scripture passage="iCor 12:18" parsed="|1Cor|12|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.18" />
<sup>18</sup>Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.
<scripture passage="iCor 12:19" parsed="|1Cor|12|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.19" />
<sup>19</sup>Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
<scripture passage="iCor 12:20" parsed="|1Cor|12|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.20" />
<sup>20</sup>Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.
<scripture passage="iCor 12:21" parsed="|1Cor|12|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.21" />
<sup>21</sup>Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: "Sikuhitaji wewe", wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: "Siwahitaji ninyi."
<scripture passage="iCor 12:22" parsed="|1Cor|12|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.22" />
<sup>22</sup>Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.
<scripture passage="iCor 12:23" parsed="|1Cor|12|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.23" />
<sup>23</sup>Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
<scripture passage="iCor 12:24" parsed="|1Cor|12|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.24" />
<sup>24</sup>ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima,
<scripture passage="iCor 12:25" parsed="|1Cor|12|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.25" />
<sup>25</sup>ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote vishughulikiane.
<scripture passage="iCor 12:26" parsed="|1Cor|12|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.26" />
<sup>26</sup>Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
<scripture passage="iCor 12:27" parsed="|1Cor|12|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.27" />
<sup>27</sup>Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo.
<scripture passage="iCor 12:28" parsed="|1Cor|12|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.28" />
<sup>28</sup>Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
<scripture passage="iCor 12:29" parsed="|1Cor|12|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.29" />
<sup>29</sup>Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza?
<scripture passage="iCor 12:30" parsed="|1Cor|12|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.30" />
<sup>30</sup>Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?
<scripture passage="iCor 12:31" parsed="|1Cor|12|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.12.31" />
<sup>31</sup>Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 13" progress="67.66%" prev="iCor.12" next="iCor.14" id="iCor.13">
<h3 id="iCor.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="iCor.13-p1">
<scripture passage="iCor 13:1" parsed="|1Cor|13|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.1" />
<sup>1</sup>Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
<scripture passage="iCor 13:2" parsed="|1Cor|13|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.2" />
<sup>2</sup>Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.
<scripture passage="iCor 13:3" parsed="|1Cor|13|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.3" />
<sup>3</sup>Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
<scripture passage="iCor 13:4" parsed="|1Cor|13|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.4" />
<sup>4</sup>Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
<scripture passage="iCor 13:5" parsed="|1Cor|13|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.5" />
<sup>5</sup>Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,
<scripture passage="iCor 13:6" parsed="|1Cor|13|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.6" />
<sup>6</sup>hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
<scripture passage="iCor 13:7" parsed="|1Cor|13|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.7" />
<sup>7</sup>Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
<scripture passage="iCor 13:8" parsed="|1Cor|13|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.8" />
<sup>8</sup>Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.
<scripture passage="iCor 13:9" parsed="|1Cor|13|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.9" />
<sup>9</sup>Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili.
<scripture passage="iCor 13:10" parsed="|1Cor|13|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.10" />
<sup>10</sup>Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika, vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.
<scripture passage="iCor 13:11" parsed="|1Cor|13|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.11" />
<sup>11</sup>Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu mzima, mambo ya kitoto nimeyaacha.
<scripture passage="iCor 13:12" parsed="|1Cor|13|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.12" />
<sup>12</sup>Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi.
<scripture passage="iCor 13:13" parsed="|1Cor|13|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.13.13" />
<sup>13</sup>Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 14" progress="67.83%" prev="iCor.13" next="iCor.15" id="iCor.14">
<h3 id="iCor.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="iCor.14-p1">
<scripture passage="iCor 14:1" parsed="|1Cor|14|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.1" />
<sup>1</sup>Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
<scripture passage="iCor 14:2" parsed="|1Cor|14|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.2" />
<sup>2</sup>Mwenye kunena lugha ngeni hasemi na watu bali anasema na Mungu. Yeye hunena kwa nguvu ya Roho mambo yaliyofichika.
<scripture passage="iCor 14:3" parsed="|1Cor|14|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.3" />
<sup>3</sup>Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, husema na watu kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji na kuwatia moyo.
<scripture passage="iCor 14:4" parsed="|1Cor|14|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.4" />
<sup>4</sup>Mwenye kunena lugha ngeni anajijenga mwenyewe. Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, analijenga kanisa.
<scripture passage="iCor 14:5" parsed="|1Cor|14|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.5" />
<sup>5</sup>Basi, ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni lakini ningependelea hasa muwe na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, maana mtu mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, ni wa maana zaidi kuliko yule mwenye kusema lugha ngeni, isipokuwa tu kama yupo hapo mtu awezaye kuyafafanua hayo mambo asemayo, ili kanisa lipate kujengwa.
<scripture passage="iCor 14:6" parsed="|1Cor|14|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.6" />
<sup>6</sup>Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.
<scripture passage="iCor 14:7" parsed="|1Cor|14|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.7" />
<sup>7</sup>Ndivyo ilivyo kwa vyombo visivyo na uhai vyenye kutoa sauti kama vile filimbi au kinanda. Je, mtu anawezaje kuutambua wimbo unaochezwa kama vyombo hivyo havitoi sauti waziwazi vinapopigwa?
<scripture passage="iCor 14:8" parsed="|1Cor|14|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.8" />
<sup>8</sup>La mgambo likilia bila kufuata taratibu zake, nani atajiweka tayari kwa vita?
<scripture passage="iCor 14:9" parsed="|1Cor|14|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.9" />
<sup>9</sup>Hali kadhalika na ninyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.
<scripture passage="iCor 14:10" parsed="|1Cor|14|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.10" />
<sup>10</sup>Zipo lugha mbalimbali ulimwenguni, na hakuna hata mojawapo isiyo na maana.
<scripture passage="iCor 14:11" parsed="|1Cor|14|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.11" />
<sup>11</sup>Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
<scripture passage="iCor 14:12" parsed="|1Cor|14|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.12" />
<sup>12</sup>Hali kadhalika na ninyi, maadam mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.
<scripture passage="iCor 14:13" parsed="|1Cor|14|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.13" />
<sup>13</sup>Kwa hiyo, mwenye kunena lugha ngeni na aombe apate uwezo wa kuzifafanua.
<scripture passage="iCor 14:14" parsed="|1Cor|14|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.14" />
<sup>14</sup>Maana, nikisali kwa lugha ngeni roho yangu ndiyo inayosali, lakini akili yangu hubaki bure.
<scripture passage="iCor 14:15" parsed="|1Cor|14|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.15" />
<sup>15</sup>Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu, nitasali pia kwa akili yangu; nitaimba kwa roho yangu, nitaimba pia kwa akili yangu.
<scripture passage="iCor 14:16" parsed="|1Cor|14|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.16" />
<sup>16</sup>Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: "Amina," kama haelewi unachosema?
<scripture passage="iCor 14:17" parsed="|1Cor|14|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.17" />
<sup>17</sup>Sala yako ya shukrani yaweza kweli kuwa bora, lakini huyo mwingine haitamfaidia.
<scripture passage="iCor 14:18" parsed="|1Cor|14|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.18" />
<sup>18</sup>Namshukuru Mungu kwamba mimi nasema kwa lugha ngeni zaidi kuliko ninyi nyote.
<scripture passage="iCor 14:19" parsed="|1Cor|14|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.19" />
<sup>19</sup>Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.
<scripture passage="iCor 14:20" parsed="|1Cor|14|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.20" />
<sup>20</sup>Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu waliokomaa.
<scripture passage="iCor 14:21" parsed="|1Cor|14|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.21" />
<sup>21</sup>Imeandikwa katika Sheria: "Bwana asema hivi: `Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza."`
<scripture passage="iCor 14:22" parsed="|1Cor|14|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.22" />
<sup>22</sup>Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.
<scripture passage="iCor 14:23" parsed="|1Cor|14|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.23" />
<sup>23</sup>Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba ninyi mna wazimu?
<scripture passage="iCor 14:24" parsed="|1Cor|14|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.24" />
<sup>24</sup>Lakini, wote wakiwa wanautangaza ujumbe wa Mungu, akija mtu wa kawaida au asiyeamini, yote atakayosikia yatamhakikishia ubaya wake mwenyewe; yote atakayosikia yatamhukumu.
<scripture passage="iCor 14:25" parsed="|1Cor|14|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.25" />
<sup>25</sup>Siri za moyo wake zitafichuliwa, naye atapiga magoti na kumwabudu Mungu akisema: "Kweli Mungu yupo pamoja nanyi."
<scripture passage="iCor 14:26" parsed="|1Cor|14|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.26" />
<sup>26</sup>Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
<scripture passage="iCor 14:27" parsed="|1Cor|14|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.27" />
<sup>27</sup>Wakiwepo watu wenye vipaji vya kusema kwa lugha ngeni, waseme wawili au watatu, si zaidi, tena mmojammoja; na aweko mtu wa kufafanua yanayosemwa.
<scripture passage="iCor 14:28" parsed="|1Cor|14|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.28" />
<sup>28</sup>Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusema lugha ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe na Mungu.
<scripture passage="iCor 14:29" parsed="|1Cor|14|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.29" />
<sup>29</sup>Kuhusu wale wenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, waseme wawili au watatu, na wengine wayapime maneno yao.
<scripture passage="iCor 14:30" parsed="|1Cor|14|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.30" />
<sup>30</sup>Ikiwa mmoja anaposema mwingine wa wasikilizaji amepata ufunuo kutoka kwa Mungu, basi, yule anayesema anyamaze.
<scripture passage="iCor 14:31" parsed="|1Cor|14|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.31" />
<sup>31</sup>Maana nyote mwaweza kutangaza ujumbe wa Mungu, mmoja baada ya mwingine, ili nyote mpate kujifunza na kutiwa moyo.
<scripture passage="iCor 14:32" parsed="|1Cor|14|32|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.32" />
<sup>32</sup>Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni lazima kitawaliwe na huyo mwenye hicho kipaji.
<scripture passage="iCor 14:33" parsed="|1Cor|14|33|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.33" />
<sup>33</sup>Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani.
<scripture passage="iCor 14:34" parsed="|1Cor|14|34|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.34" />
<sup>34</sup>Kama ilivyo desturi katika makanisa yote ya watu wa Mungu, wanawake wakae kimya katika mikutano ya waumini. Hawana ruhusa kusema; ila wawe watii kama isemavyo Sheria.
<scripture passage="iCor 14:35" parsed="|1Cor|14|35|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.35" />
<sup>35</sup>Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.
<scripture passage="iCor 14:36" parsed="|1Cor|14|36|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.36" />
<sup>36</sup>Je, mnadhani neno la Mungu limetoka kwenu ninyi au kwamba limewajieni ninyi peke yenu?
<scripture passage="iCor 14:37" parsed="|1Cor|14|37|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.37" />
<sup>37</sup>Kama mtu yeyote anadhani kwamba yeye ni mjumbe wa Mungu au kwamba anacho kipaji cha Roho, na ajue kwamba haya ninayowaandikia ninyi ni amri ya Bwana.
<scripture passage="iCor 14:38" parsed="|1Cor|14|38|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.38" />
<sup>38</sup>Lakini mtu asiyetambua hayo, basi, mtu asimjali mtu huyo.
<scripture passage="iCor 14:39" parsed="|1Cor|14|39|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.39" />
<sup>39</sup>Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswa kuwa na hamu ya kutangaza ujumbe wa Mungu; lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni.
<scripture passage="iCor 14:40" parsed="|1Cor|14|40|0|0" osisRef="Bible:1Cor.14.40" />
<sup>40</sup>Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 15" progress="68.39%" prev="iCor.14" next="iCor.16" id="iCor.15">
<h3 id="iCor.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="iCor.15-p1">
<scripture passage="iCor 15:1" parsed="|1Cor|15|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.1" />
<sup>1</sup>Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake.
<scripture passage="iCor 15:2" parsed="|1Cor|15|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.2" />
<sup>2</sup>Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.
<scripture passage="iCor 15:3" parsed="|1Cor|15|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.3" />
<sup>3</sup>Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;
<scripture passage="iCor 15:4" parsed="|1Cor|15|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.4" />
<sup>4</sup>kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa;
<scripture passage="iCor 15:5" parsed="|1Cor|15|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.5" />
<sup>5</sup>kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.
<scripture passage="iCor 15:6" parsed="|1Cor|15|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.6" />
<sup>6</sup>Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
<scripture passage="iCor 15:7" parsed="|1Cor|15|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.7" />
<sup>7</sup>Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote.
<scripture passage="iCor 15:8" parsed="|1Cor|15|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.8" />
<sup>8</sup>Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati.
<scripture passage="iCor 15:9" parsed="|1Cor|15|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.9" />
<sup>9</sup>Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume na wala sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu.
<scripture passage="iCor 15:10" parsed="|1Cor|15|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.10" />
<sup>10</sup>Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.
<scripture passage="iCor 15:11" parsed="|1Cor|15|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.11" />
<sup>11</sup>Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndicho tunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini.
<scripture passage="iCor 15:12" parsed="|1Cor|15|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.12" />
<sup>12</sup>Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
<scripture passage="iCor 15:13" parsed="|1Cor|15|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.13" />
<sup>13</sup>Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka;
<scripture passage="iCor 15:14" parsed="|1Cor|15|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.14" />
<sup>14</sup>na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana.
<scripture passage="iCor 15:15" parsed="|1Cor|15|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.15" />
<sup>15</sup>Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua--kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.
<scripture passage="iCor 15:16" parsed="|1Cor|15|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.16" />
<sup>16</sup>Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo hakufufuka.
<scripture passage="iCor 15:17" parsed="|1Cor|15|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.17" />
<sup>17</sup>Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu.
<scripture passage="iCor 15:18" parsed="|1Cor|15|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.18" />
<sup>18</sup>Zaidi ya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana na Kristo wamepotea kabisa.
<scripture passage="iCor 15:19" parsed="|1Cor|15|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.19" />
<sup>19</sup>Kama matumaini yetu katika Kristo yanahusu tu maisha haya ya sasa, basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote duniani.
<scripture passage="iCor 15:20" parsed="|1Cor|15|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.20" />
<sup>20</sup>Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, limbuko lao wale waliolala katika kifo.
<scripture passage="iCor 15:21" parsed="|1Cor|15|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.21" />
<sup>21</sup>Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa na mtu mmoja.
<scripture passage="iCor 15:22" parsed="|1Cor|15|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.22" />
<sup>22</sup>Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo.
<scripture passage="iCor 15:23" parsed="|1Cor|15|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.23" />
<sup>23</sup>Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza, halafu wale walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja.
<scripture passage="iCor 15:24" parsed="|1Cor|15|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.24" />
<sup>24</sup>Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
<scripture passage="iCor 15:25" parsed="|1Cor|15|25|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.25" />
<sup>25</sup>Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda adui zake na kuwaweka chini ya miguu yake.
<scripture passage="iCor 15:26" parsed="|1Cor|15|26|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.26" />
<sup>26</sup>Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.
<scripture passage="iCor 15:27" parsed="|1Cor|15|27|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.27" />
<sup>27</sup>Maana, Maandiko yasema: "Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake." Lakini, Maandiko yanaposema: "Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale" ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
<scripture passage="iCor 15:28" parsed="|1Cor|15|28|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.28" />
<sup>28</sup>Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
<scripture passage="iCor 15:29" parsed="|1Cor|15|29|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.29" />
<sup>29</sup>Kama hakuna ufufuo, je watu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainia kupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwa kwa ajili yao?
<scripture passage="iCor 15:30" parsed="|1Cor|15|30|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.30" />
<sup>30</sup>Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa?
<scripture passage="iCor 15:31" parsed="|1Cor|15|31|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.31" />
<sup>31</sup>Ndugu, mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juu yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu inanifanya nitangaze jambo hili.
<scripture passage="iCor 15:32" parsed="|1Cor|15|32|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.32" />
<sup>32</sup>Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, "Tule na tunywe, maana kesho tutakufa."
<scripture passage="iCor 15:33" parsed="|1Cor|15|33|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.33" />
<sup>33</sup>Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.
<scripture passage="iCor 15:34" parsed="|1Cor|15|34|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.34" />
<sup>34</sup>Amkeni! Anzeni kuishi vema, na acheni kutenda dhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa. Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu!
<scripture passage="iCor 15:35" parsed="|1Cor|15|35|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.35" />
<sup>35</sup>Lakini mtu anaweza kuuliza: "Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?"
<scripture passage="iCor 15:36" parsed="|1Cor|15|36|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.36" />
<sup>36</sup>Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza haitaota.
<scripture passage="iCor 15:37" parsed="|1Cor|15|37|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.37" />
<sup>37</sup>Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokea baadaye.
<scripture passage="iCor 15:38" parsed="|1Cor|15|38|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.38" />
<sup>38</sup>Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee.
<scripture passage="iCor 15:39" parsed="|1Cor|15|39|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.39" />
<sup>39</sup>Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia ni ya namna nyingine.
<scripture passage="iCor 15:40" parsed="|1Cor|15|40|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.40" />
<sup>40</sup>Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine.
<scripture passage="iCor 15:41" parsed="|1Cor|15|41|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.41" />
<sup>41</sup>Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwa uzuri.
<scripture passage="iCor 15:42" parsed="|1Cor|15|42|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.42" />
<sup>42</sup>Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kama vile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwa katika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwa katika hali ya kutoharibika.
<scripture passage="iCor 15:43" parsed="|1Cor|15|43|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.43" />
<sup>43</sup>Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu; huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenye nguvu.
<scripture passage="iCor 15:44" parsed="|1Cor|15|44|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.44" />
<sup>44</sup>Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho. Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwili wa kiroho.
<scripture passage="iCor 15:45" parsed="|1Cor|15|45|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.45" />
<sup>45</sup>Maana Maandiko yasema: "Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenye uhai;" lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima.
<scripture passage="iCor 15:46" parsed="|1Cor|15|46|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.46" />
<sup>46</sup>Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili wa kawaida kisha ule mwili wa kiroho.
<scripture passage="iCor 15:47" parsed="|1Cor|15|47|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.47" />
<sup>47</sup>Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni.
<scripture passage="iCor 15:48" parsed="|1Cor|15|48|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.48" />
<sup>48</sup>Wote walio wa dunia wako kama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo; wale walio wa mbinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni.
<scripture passage="iCor 15:49" parsed="|1Cor|15|49|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.49" />
<sup>49</sup>Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo, vivyo hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni.
<scripture passage="iCor 15:50" parsed="|1Cor|15|50|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.50" />
<sup>50</sup>Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
<scripture passage="iCor 15:51" parsed="|1Cor|15|51|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.51" />
<sup>51</sup>Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa
<scripture passage="iCor 15:52" parsed="|1Cor|15|52|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.52" />
<sup>52</sup>wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa.
<scripture passage="iCor 15:53" parsed="|1Cor|15|53|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.53" />
<sup>53</sup>Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.
<scripture passage="iCor 15:54" parsed="|1Cor|15|54|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.54" />
<sup>54</sup>Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: "Kifo kimeangamizwa ushindi umekamilika!"
<scripture passage="iCor 15:55" parsed="|1Cor|15|55|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.55" />
<sup>55</sup>"Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?"
<scripture passage="iCor 15:56" parsed="|1Cor|15|56|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.56" />
<sup>56</sup>Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika Sheria.
<scripture passage="iCor 15:57" parsed="|1Cor|15|57|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.57" />
<sup>57</sup>Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iCor 15:58" parsed="|1Cor|15|58|0|0" osisRef="Bible:1Cor.15.58" />
<sup>58</sup>Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Corinthians 16" progress="69.10%" prev="iCor.15" next="iiCor" id="iCor.16">
<h3 id="iCor.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="iCor.16-p1">
<scripture passage="iCor 16:1" parsed="|1Cor|16|1|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.1" />
<sup>1</sup>Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.
<scripture passage="iCor 16:2" parsed="|1Cor|16|2|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.2" />
<sup>2</sup>Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja.
<scripture passage="iCor 16:3" parsed="|1Cor|16|3|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.3" />
<sup>3</sup>Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
<scripture passage="iCor 16:4" parsed="|1Cor|16|4|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.4" />
<sup>4</sup>Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.
<scripture passage="iCor 16:5" parsed="|1Cor|16|5|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.5" />
<sup>5</sup>Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia--maana nataraji kupitia Makedonia.
<scripture passage="iCor 16:6" parsed="|1Cor|16|6|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.6" />
<sup>6</sup>Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
<scripture passage="iCor 16:7" parsed="|1Cor|16|7|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.7" />
<sup>7</sup>Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
<scripture passage="iCor 16:8" parsed="|1Cor|16|8|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.8" />
<sup>8</sup>Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.
<scripture passage="iCor 16:9" parsed="|1Cor|16|9|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.9" />
<sup>9</sup>Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi.
<scripture passage="iCor 16:10" parsed="|1Cor|16|10|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.10" />
<sup>10</sup>Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.
<scripture passage="iCor 16:11" parsed="|1Cor|16|11|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.11" />
<sup>11</sup>Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu.
<scripture passage="iCor 16:12" parsed="|1Cor|16|12|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.12" />
<sup>12</sup>Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
<scripture passage="iCor 16:13" parsed="|1Cor|16|13|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.13" />
<sup>13</sup>Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.
<scripture passage="iCor 16:14" parsed="|1Cor|16|14|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.14" />
<sup>14</sup>Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.
<scripture passage="iCor 16:15" parsed="|1Cor|16|15|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.15" />
<sup>15</sup>Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu,
<scripture passage="iCor 16:16" parsed="|1Cor|16|16|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.16" />
<sup>16</sup>muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao.
<scripture passage="iCor 16:17" parsed="|1Cor|16|17|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.17" />
<sup>17</sup>Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu.
<scripture passage="iCor 16:18" parsed="|1Cor|16|18|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.18" />
<sup>18</sup>Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii.
<scripture passage="iCor 16:19" parsed="|1Cor|16|19|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.19" />
<sup>19</sup>Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana.
<scripture passage="iCor 16:20" parsed="|1Cor|16|20|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.20" />
<sup>20</sup>Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu.
<scripture passage="iCor 16:21" parsed="|1Cor|16|21|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.21" />
<sup>21</sup>Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe.
<scripture passage="iCor 16:22" parsed="|1Cor|16|22|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.22" />
<sup>22</sup>Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA--BWANA, njoo!
<scripture passage="iCor 16:23" parsed="|1Cor|16|23|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.23" />
<sup>23</sup>Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
<scripture passage="iCor 16:24" parsed="|1Cor|16|24|0|0" osisRef="Bible:1Cor.16.24" />
<sup>24</sup>Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="2 Corinthians" progress="69.35%" prev="iCor.16" next="iiCor.1" id="iiCor">
<h2 id="iiCor-p0.1">2 Corinthians</h2>

<div3 title="2 Corinthians 1" progress="69.35%" prev="iiCor" next="iiCor.2" id="iiCor.1">
<h3 id="iiCor.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiCor.1-p1">
<scripture passage="iiCor 1:1" parsed="|2Cor|1|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo, tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho, na watu wote wa Mungu kila mahali katika Akaya.
<scripture passage="iiCor 1:2" parsed="|2Cor|1|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.2" />
<sup>2</sup>Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="iiCor 1:3" parsed="|2Cor|1|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.3" />
<sup>3</sup>Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote.
<scripture passage="iiCor 1:4" parsed="|2Cor|1|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.4" />
<sup>4</sup>Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu.
<scripture passage="iiCor 1:5" parsed="|2Cor|1|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.5" />
<sup>5</sup>Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye.
<scripture passage="iiCor 1:6" parsed="|2Cor|1|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.6" />
<sup>6</sup>Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
<scripture passage="iiCor 1:7" parsed="|2Cor|1|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.7" />
<sup>7</sup>Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
<scripture passage="iiCor 1:8" parsed="|2Cor|1|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.8" />
<sup>8</sup>Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.
<scripture passage="iiCor 1:9" parsed="|2Cor|1|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.9" />
<sup>9</sup>Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe.
<scripture passage="iiCor 1:10" parsed="|2Cor|1|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.10" />
<sup>10</sup>Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena,
<scripture passage="iiCor 1:11" parsed="|2Cor|1|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.11" />
<sup>11</sup>ninyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.
<scripture passage="iiCor 1:12" parsed="|2Cor|1|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.12" />
<sup>12</sup>Sisi tunajivunia kitu kimoja: dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali neema ya Mungu.
<scripture passage="iiCor 1:13" parsed="|2Cor|1|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.13" />
<sup>13</sup>Tunawaandikia ninyi mambo mnayoweza kuyasoma na kuyaelewa. Ninatumaini kwamba mtaelewa vizuri kabisa,
<scripture passage="iiCor 1:14" parsed="|2Cor|1|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.14" />
<sup>14</sup>maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile Siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea ninyi fahari.
<scripture passage="iiCor 1:15" parsed="|2Cor|1|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.15" />
<sup>15</sup>Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu.
<scripture passage="iiCor 1:16" parsed="|2Cor|1|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.16" />
<sup>16</sup>Nilikusudia kupita kwenu nikiwa safarini kwenda Makedonia, na wakati wa kurudi pia, ili nipate msaada wenu kwa safari yangu kwenda Yudea.
<scripture passage="iiCor 1:17" parsed="|2Cor|1|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.17" />
<sup>17</sup>Je, mnadhani nilipopanga hivyo nimekuwa kama mtu asiye na msimamo? Je, mnadhani kwamba ninafanya uamuzi wangu kwa fikira za kibinadamu na kwamba nasema "Ndiyo" na "Siyo" papo hapo?
<scripture passage="iiCor 1:18" parsed="|2Cor|1|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.18" />
<sup>18</sup>Mungu ni ukweli mtupu; basi, kile tulichowaambia ninyi si jambo la "Ndiyo" na "Siyo".
<scripture passage="iiCor 1:19" parsed="|2Cor|1|19|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.19" />
<sup>19</sup>Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa "Ndiyo" na "Siyo"; bali yeye daima ni "Ndiyo" ya Mungu.
<scripture passage="iiCor 1:20" parsed="|2Cor|1|20|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.20" />
<sup>20</sup>Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa "Ndiyo". Kwa sababu hiyo, "Amina" yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.
<scripture passage="iiCor 1:21" parsed="|2Cor|1|21|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.21" />
<sup>21</sup>Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na ninyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;
<scripture passage="iiCor 1:22" parsed="|2Cor|1|22|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.22" />
<sup>22</sup>ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa mali yake yeye na kutujalia Roho mioyoni mwetu kama dhamana ya mambo yote ambayo ametuwekea.
<scripture passage="iiCor 1:23" parsed="|2Cor|1|23|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.23" />
<sup>23</sup>Mungu ndiye shahidi wangu--yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
<scripture passage="iiCor 1:24" parsed="|2Cor|1|24|0|0" osisRef="Bible:2Cor.1.24" />
<sup>24</sup>Hatutaki kutumia mabavu juu ya imani yenu; ninyi mko imara katika imani yenu. Wajibu wetu ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya furaha yenu.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 2" progress="69.69%" prev="iiCor.1" next="iiCor.3" id="iiCor.2">
<h3 id="iiCor.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iiCor.2-p1">
<scripture passage="iiCor 2:1" parsed="|2Cor|2|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.1" />
<sup>1</sup>Basi nimeamua nisiwatembelee tena kuwatia huzuni.
<scripture passage="iiCor 2:2" parsed="|2Cor|2|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.2" />
<sup>2</sup>Maana nikiwahuzunisha ninyi, basi, ni nani atakayenifariji? Ni walewale niliowahuzunisha!
<scripture passage="iiCor 2:3" parsed="|2Cor|2|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.3" />
<sup>3</sup>Ndiyo maana niliwaandikia--sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na ninyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba, mimi nikifurahi, ninyi nyote pia mnafurahi.
<scripture passage="iiCor 2:4" parsed="|2Cor|2|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.4" />
<sup>4</sup>Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwaonyesheni kwamba nawapenda mno.
<scripture passage="iiCor 2:5" parsed="|2Cor|2|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.5" />
<sup>5</sup>Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi--ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
<scripture passage="iiCor 2:6" parsed="|2Cor|2|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.6" />
<sup>6</sup>Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.
<scripture passage="iiCor 2:7" parsed="|2Cor|2|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.7" />
<sup>7</sup>Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.
<scripture passage="iiCor 2:8" parsed="|2Cor|2|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.8" />
<sup>8</sup>Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda.
<scripture passage="iiCor 2:9" parsed="|2Cor|2|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.9" />
<sup>9</sup>Madhumuni yangu kuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kama mko tayari kutii katika kila jambo.
<scripture passage="iiCor 2:10" parsed="|2Cor|2|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.10" />
<sup>10</sup>Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe--kama kweli ninacho cha kusamehe--nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
<scripture passage="iiCor 2:11" parsed="|2Cor|2|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.11" />
<sup>11</sup>ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo.
<scripture passage="iiCor 2:12" parsed="|2Cor|2|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.12" />
<sup>12</sup>Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nilikuta mlango u wazi kwa ajili ya kazi ya Bwana.
<scripture passage="iiCor 2:13" parsed="|2Cor|2|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.13" />
<sup>13</sup>Lakini nilifadhaika sana kwa kutomkuta ndugu yetu Tito. Ndiyo maana niliwaaga wote pale nikaenda Makedonia.
<scripture passage="iiCor 2:14" parsed="|2Cor|2|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.14" />
<sup>14</sup>Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
<scripture passage="iiCor 2:15" parsed="|2Cor|2|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.15" />
<sup>15</sup>Maana sisi ni kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristo anamtolea Mungu, harufu nzuri inayofikia wote wanaookolewa na wanaopotea.
<scripture passage="iiCor 2:16" parsed="|2Cor|2|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.16" />
<sup>16</sup>Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi ya namna hiyo?
<scripture passage="iiCor 2:17" parsed="|2Cor|2|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.2.17" />
<sup>17</sup>Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 3" progress="69.90%" prev="iiCor.2" next="iiCor.4" id="iiCor.3">
<h3 id="iiCor.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iiCor.3-p1">
<scripture passage="iiCor 3:1" parsed="|2Cor|3|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.1" />
<sup>1</sup>Je, tunaanza tena kujipendekeza? Je, tunahitaji barua ya utambulisho kwenu, au kutoka kwenu, kama watu wengine?
<scripture passage="iiCor 3:2" parsed="|2Cor|3|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.2" />
<sup>2</sup>Ninyi wenyewe ni barua yetu; barua iliyoandikwa mioyoni mwetu kila mtu aione na kuisoma.
<scripture passage="iiCor 3:3" parsed="|2Cor|3|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.3" />
<sup>3</sup>Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu hai; imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu.
<scripture passage="iiCor 3:4" parsed="|2Cor|3|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.4" />
<sup>4</sup>Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo.
<scripture passage="iiCor 3:5" parsed="|2Cor|3|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.5" />
<sup>5</sup>Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
<scripture passage="iiCor 3:6" parsed="|2Cor|3|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.6" />
<sup>6</sup>maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali Agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uzima.
<scripture passage="iiCor 3:7" parsed="|2Cor|3|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.7" />
<sup>7</sup>Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mng`ao wake. Tena mng`ao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
<scripture passage="iiCor 3:8" parsed="|2Cor|3|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.8" />
<sup>8</sup>basi, huduma ya Roho ina utukufu mkuu zaidi.
<scripture passage="iiCor 3:9" parsed="|2Cor|3|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.9" />
<sup>9</sup>Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma ile iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
<scripture passage="iiCor 3:10" parsed="|2Cor|3|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.10" />
<sup>10</sup>Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
<scripture passage="iiCor 3:11" parsed="|2Cor|3|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.11" />
<sup>11</sup>Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.
<scripture passage="iiCor 3:12" parsed="|2Cor|3|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.12" />
<sup>12</sup>Kwa vile hili ndilo tumaini letu, sisi twasema kwa uhodari mkuu.
<scripture passage="iiCor 3:13" parsed="|2Cor|3|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.13" />
<sup>13</sup>Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mng`ao uliokuwa unafifia.
<scripture passage="iiCor 3:14" parsed="|2Cor|3|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.14" />
<sup>14</sup>Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.
<scripture passage="iiCor 3:15" parsed="|2Cor|3|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.15" />
<sup>15</sup>Naam, mpaka hivi leo kila isomwapo Sheria ya Mose akili zao huwa zimefunikwa.
<scripture passage="iiCor 3:16" parsed="|2Cor|3|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.16" />
<sup>16</sup>Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa.
<scripture passage="iiCor 3:17" parsed="|2Cor|3|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.17" />
<sup>17</sup>Hapa "Bwana" ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru.
<scripture passage="iiCor 3:18" parsed="|2Cor|3|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.3.18" />
<sup>18</sup>Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, twaonyesha kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 4" progress="70.15%" prev="iiCor.3" next="iiCor.5" id="iiCor.4">
<h3 id="iiCor.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iiCor.4-p1">
<scripture passage="iiCor 4:1" parsed="|2Cor|4|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.1" />
<sup>1</sup>Basi, Mungu, kwa huruma yake, ametukabidhi kazi hii na hivyo hatufi moyo.
<scripture passage="iiCor 4:2" parsed="|2Cor|4|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.2" />
<sup>2</sup>Tumeyaacha kabisa mambo yote ya aibu na ya kisirisiri. Hatuishi tena kwa udanganyifu, wala kwa kulipotosha neno la Mungu; bali tunaudhihirisha ukweli kwa kuufanya ukweli, na hivyo kujiweka chini ya uamuzi wa dhamiri za watu mbele ya Mungu.
<scripture passage="iiCor 4:3" parsed="|2Cor|4|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.3" />
<sup>3</sup>Maana, kama Habari Njema tunayohubiri imefichika, imefichika tu kwa wale wanaopotea.
<scripture passage="iiCor 4:4" parsed="|2Cor|4|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.4" />
<sup>4</sup>Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu.
<scripture passage="iiCor 4:5" parsed="|2Cor|4|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.5" />
<sup>5</sup>Maana hatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiri Yesu Kristo aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwa watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
<scripture passage="iiCor 4:6" parsed="|2Cor|4|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.6" />
<sup>6</sup>Mungu ambaye alisema, "Mwanga na uangaze kutoka gizani," ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo.
<scripture passage="iiCor 4:7" parsed="|2Cor|4|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.7" />
<sup>7</sup>Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe.
<scripture passage="iiCor 4:8" parsed="|2Cor|4|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.8" />
<sup>8</sup>Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa;
<scripture passage="iiCor 4:9" parsed="|2Cor|4|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.9" />
<sup>9</sup>twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa chini, hatukuangamizwa.
<scripture passage="iiCor 4:10" parsed="|2Cor|4|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.10" />
<sup>10</sup>Kila wakati tumekuwa tukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo, ili uhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu.
<scripture passage="iiCor 4:11" parsed="|2Cor|4|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.11" />
<sup>11</sup>Naam, katika maisha yetu yote tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uzima wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
<scripture passage="iiCor 4:12" parsed="|2Cor|4|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.12" />
<sup>12</sup>Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanya kazi.
<scripture passage="iiCor 4:13" parsed="|2Cor|4|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.13" />
<sup>13</sup>Maandiko Matakatifu yasema: "Niliamini, ndiyo maana nilinena." Nasi pia, tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini, na kwa sababu hiyo twanena.
<scripture passage="iiCor 4:14" parsed="|2Cor|4|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.14" />
<sup>14</sup>Tunajua kwamba yule aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka mbele yake pamoja nanyi.
<scripture passage="iiCor 4:15" parsed="|2Cor|4|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.15" />
<sup>15</sup>Yote haya ni kwa faida yenu; ili kama vile neema ya Mungu inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi vivyo hivyo watu wengi zaidi watoe shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
<scripture passage="iiCor 4:16" parsed="|2Cor|4|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.16" />
<sup>16</sup>Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku.
<scripture passage="iiCor 4:17" parsed="|2Cor|4|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.17" />
<sup>17</sup>Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu: lakini itatupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho.
<scripture passage="iiCor 4:18" parsed="|2Cor|4|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.4.18" />
<sup>18</sup>Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vile visivyoonekana ni vya milele.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 5" progress="70.40%" prev="iiCor.4" next="iiCor.6" id="iiCor.5">
<h3 id="iiCor.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iiCor.5-p1">
<scripture passage="iiCor 5:1" parsed="|2Cor|5|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.1" />
<sup>1</sup>Maana tunajua kwamba hema hii ambayo ndani yake tunaishi sasa hapa duniani, yaani mwili wetu, itakapong`olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
<scripture passage="iiCor 5:2" parsed="|2Cor|5|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.2" />
<sup>2</sup>Na sasa, katika hali hii, tunaugua, tukitazamia kwa hamu kubwa kuvikwa makao yetu yaliyo mbinguni.
<scripture passage="iiCor 5:3" parsed="|2Cor|5|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.3" />
<sup>3</sup>Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya Mungu bila vazi.
<scripture passage="iiCor 5:4" parsed="|2Cor|5|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.4" />
<sup>4</sup>Tukiwa bado katika hema hii ya duniani, tunalia kwa kukandamizwa; si kwamba tunataka kuuvua mwili huu wa kufa, ila tuna hamu ya kuvalishwa ule usiokufa, ili kile chenye kufa kimezwe kabisa na uhai.
<scripture passage="iiCor 5:5" parsed="|2Cor|5|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.5" />
<sup>5</sup>Mungu mwenyewe alitutayarishia mabadiliko hayo, naye ametupa Roho wake awe dhamana ya yote aliyotuwekea.
<scripture passage="iiCor 5:6" parsed="|2Cor|5|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.6" />
<sup>6</sup>Tuko imara daima. Tunajua kwamba kuishi katika mwili huu tu ni kukaa mbali na Bwana.
<scripture passage="iiCor 5:7" parsed="|2Cor|5|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.7" />
<sup>7</sup>Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona.
<scripture passage="iiCor 5:8" parsed="|2Cor|5|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.8" />
<sup>8</sup>Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana.
<scripture passage="iiCor 5:9" parsed="|2Cor|5|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.9" />
<sup>9</sup>Lakini jambo la maana zaidi, tunataka kumpendeza, iwe tunaishi hapa duniani au huko.
<scripture passage="iiCor 5:10" parsed="|2Cor|5|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.10" />
<sup>10</sup>Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.
<scripture passage="iiCor 5:11" parsed="|2Cor|5|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.11" />
<sup>11</sup>Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia mnatujua kinaganaga.
<scripture passage="iiCor 5:12" parsed="|2Cor|5|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.12" />
<sup>12</sup>Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa ninyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.
<scripture passage="iiCor 5:13" parsed="|2Cor|5|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.13" />
<sup>13</sup>Ikiwa tumeonekana kuwa wendawazimu, hiyo ni kwa ajili ya Mungu; na ikiwa tunazo akili zetu timamu, hiyo ni kwa faida yenu.
<scripture passage="iiCor 5:14" parsed="|2Cor|5|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.14" />
<sup>14</sup>Maana mapendo ya Kristo yanatumiliki sisi ambao tunatambua ya kwamba mtu mmoja tu amekufa kwa ajili ya wote, na hiyo ina maana kwamba wote wanashiriki kifo chake.
<scripture passage="iiCor 5:15" parsed="|2Cor|5|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.15" />
<sup>15</sup>Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili yao.
<scripture passage="iiCor 5:16" parsed="|2Cor|5|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.16" />
<sup>16</sup>Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
<scripture passage="iiCor 5:17" parsed="|2Cor|5|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.17" />
<sup>17</sup>Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.
<scripture passage="iiCor 5:18" parsed="|2Cor|5|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.18" />
<sup>18</sup>Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, akatupa nasi jukumu la kuwapatanisha watu naye.
<scripture passage="iiCor 5:19" parsed="|2Cor|5|19|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.19" />
<sup>19</sup>Ndiyo kusema: Mungu, amekuwa akiupatanisha ulimwengu naye kwa njia ya Kristo, bila kutia maanani dhambi zao binadamu. Yeye ametupa ujumbe kuhusu kuwapatanisha watu naye.
<scripture passage="iiCor 5:20" parsed="|2Cor|5|20|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.20" />
<sup>20</sup>Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi ninyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
<scripture passage="iiCor 5:21" parsed="|2Cor|5|21|0|0" osisRef="Bible:2Cor.5.21" />
<sup>21</sup>Kristo hakuwa na dhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 6" progress="70.69%" prev="iiCor.5" next="iiCor.7" id="iiCor.6">
<h3 id="iiCor.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="iiCor.6-p1">
<scripture passage="iiCor 6:1" parsed="|2Cor|6|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.1" />
<sup>1</sup>Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.
<scripture passage="iiCor 6:2" parsed="|2Cor|6|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.2" />
<sup>2</sup>Mungu asema hivi: "Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia." Basi, sasa ndio wakati wa kufaa, sasa ndiyo siku ya wokovu!
<scripture passage="iiCor 6:3" parsed="|2Cor|6|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.3" />
<sup>3</sup>Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuio chochote.
<scripture passage="iiCor 6:4" parsed="|2Cor|6|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.4" />
<sup>4</sup>Badala yake, tunajionyesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu.
<scripture passage="iiCor 6:5" parsed="|2Cor|6|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.5" />
<sup>5</sup>Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula.
<scripture passage="iiCor 6:6" parsed="|2Cor|6|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.6" />
<sup>6</sup>Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki,
<scripture passage="iiCor 6:7" parsed="|2Cor|6|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.7" />
<sup>7</sup>kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia na upande wa kushoto.
<scripture passage="iiCor 6:8" parsed="|2Cor|6|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.8" />
<sup>8</sup>Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli;
<scripture passage="iiCor 6:9" parsed="|2Cor|6|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.9" />
<sup>9</sup>kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote, kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni wazima kabisa.
<scripture passage="iiCor 6:10" parsed="|2Cor|6|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.10" />
<sup>10</sup>Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
<scripture passage="iiCor 6:11" parsed="|2Cor|6|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.11" />
<sup>11</sup>Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko wazi kabisa.
<scripture passage="iiCor 6:12" parsed="|2Cor|6|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.12" />
<sup>12</sup>Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu ninyi wenyewe, na si kwa upande wetu.
<scripture passage="iiCor 6:13" parsed="|2Cor|6|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.13" />
<sup>13</sup>Sasa nasema nanyi kama watoto wangu, wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.
<scripture passage="iiCor 6:14" parsed="|2Cor|6|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.14" />
<sup>14</sup>Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
<scripture passage="iiCor 6:15" parsed="|2Cor|6|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.15" />
<sup>15</sup>Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Muumini ana uhusiano gani na asiyeamini?
<scripture passage="iiCor 6:16" parsed="|2Cor|6|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.16" />
<sup>16</sup>Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: "Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao; Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu."
<scripture passage="iiCor 6:17" parsed="|2Cor|6|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.17" />
<sup>17</sup>Kwa hiyo Bwana asema pia: "Ondokeni kati yao, mkajitenge nao, msiguse kitu najisi, nami nitawapokea.
<scripture passage="iiCor 6:18" parsed="|2Cor|6|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.6.18" />
<sup>18</sup>Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa watoto wangu, waume kwa wake, asema Bwana Mwenye Uwezo."
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 7" progress="70.92%" prev="iiCor.6" next="iiCor.8" id="iiCor.7">
<h3 id="iiCor.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="iiCor.7-p1">
<scripture passage="iiCor 7:1" parsed="|2Cor|7|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.1" />
<sup>1</sup>Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewa ahadi hizi zote, na tujitakase na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu, tuwe watakatifu kabisa, na tuishi kwa kumcha Mungu.
<scripture passage="iiCor 7:2" parsed="|2Cor|7|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.2" />
<sup>2</sup>Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.
<scripture passage="iiCor 7:3" parsed="|2Cor|7|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.3" />
<sup>3</sup>Sisemi mambo haya kwa ajili ya kumhukumu mtu; maana, kama nilivyokwisha sema, ninyi mko mioyoni mwetu, tufe pamoja, tuishi pamoja.
<scripture passage="iiCor 7:4" parsed="|2Cor|7|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.4" />
<sup>4</sup>Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.
<scripture passage="iiCor 7:5" parsed="|2Cor|7|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.5" />
<sup>5</sup>Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi; ndani hofu.
<scripture passage="iiCor 7:6" parsed="|2Cor|7|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.6" />
<sup>6</sup>Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito.
<scripture passage="iiCor 7:7" parsed="|2Cor|7|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.7" />
<sup>7</sup>Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompa ninyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.
<scripture passage="iiCor 7:8" parsed="|2Cor|7|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.8" />
<sup>8</sup>Maana, hata kama kwa barua ile yangu nimewahuzunisha, sioni sababu ya kujuta. Naam, naona kwamba barua hiyo iliwatia huzuni lakini kwa muda.
<scripture passage="iiCor 7:9" parsed="|2Cor|7|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.9" />
<sup>9</sup>Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru ninyi kwa vyovyote.
<scripture passage="iiCor 7:10" parsed="|2Cor|7|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.10" />
<sup>10</sup>Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu, husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
<scripture passage="iiCor 7:11" parsed="|2Cor|7|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.11" />
<sup>11</sup>Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: ninyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Ninyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
<scripture passage="iiCor 7:12" parsed="|2Cor|7|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.12" />
<sup>12</sup>Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
<scripture passage="iiCor 7:13" parsed="|2Cor|7|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.13" />
<sup>13</sup>Ndiyo maana sisi tulifarijika sana. Siyo kwamba tulifarijika tu, ila pia Tito alitufurahisha kwa furaha aliyokuwa nayo kutokana na jinsi mlivyomchangamsha moyo.
<scripture passage="iiCor 7:14" parsed="|2Cor|7|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.14" />
<sup>14</sup>Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia ninyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli mtupu.
<scripture passage="iiCor 7:15" parsed="|2Cor|7|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.15" />
<sup>15</sup>Hivyo upendo wake wa moyo kwenu unaongezeka zaidi akikumbuka jinsi ninyi nyote mlivyo tayari kutii, na jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu nyingi na kutetemeka.
<scripture passage="iiCor 7:16" parsed="|2Cor|7|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.7.16" />
<sup>16</sup>Nafurahi sana kwamba naweza kuwategemea ninyi kabisa katika kila jambo.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 8" progress="71.18%" prev="iiCor.7" next="iiCor.9" id="iiCor.8">
<h3 id="iiCor.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="iiCor.8-p1">
<scripture passage="iiCor 8:1" parsed="|2Cor|8|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, tunapenda kuwapa habari juu ya neema ambazo Mungu ameyajalia makanisa ya Makedonia.
<scripture passage="iiCor 8:2" parsed="|2Cor|8|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.2" />
<sup>2</sup>Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana.
<scripture passage="iiCor 8:3" parsed="|2Cor|8|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.3" />
<sup>3</sup>Naweza kushuhudia kwamba walikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao na hata zaidi. Kwa hiari yao wenyewe,
<scripture passage="iiCor 8:4" parsed="|2Cor|8|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.4" />
<sup>4</sup>walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu.
<scripture passage="iiCor 8:5" parsed="|2Cor|8|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.5" />
<sup>5</sup>Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia, kufuatana na mapenzi ya Mungu.
<scripture passage="iiCor 8:6" parsed="|2Cor|8|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.6" />
<sup>6</sup>Kwa sababu hiyo, tulimsihi Tito aliyeianza kazi hiyo awasaidieni pia muitekeleze huduma hii ya upendo miongoni mwenu.
<scripture passage="iiCor 8:7" parsed="|2Cor|8|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.7" />
<sup>7</sup>Ninyi mna kila kitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katika huduma hii ya upendo.
<scripture passage="iiCor 8:8" parsed="|2Cor|8|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.8" />
<sup>8</sup>Siwapi ninyi amri, lakini nataka tu kuonyesha jinsi wengine walivyo na bidii ya kusaidia ili nipate kujua jinsi upendo wenu ulivyo wa kweli.
<scripture passage="iiCor 8:9" parsed="|2Cor|8|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.9" />
<sup>9</sup>Maana, ninyi mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo: yeye, ingawa alikuwa na kila kitu, alijifanya maskini kwa ajili yenu, ili kutokana na umaskini wake, awatajirishe.
<scripture passage="iiCor 8:10" parsed="|2Cor|8|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.10" />
<sup>10</sup>Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Ninyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
<scripture passage="iiCor 8:11" parsed="|2Cor|8|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.11" />
<sup>11</sup>Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu, kuikamilisha.
<scripture passage="iiCor 8:12" parsed="|2Cor|8|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.12" />
<sup>12</sup>Maana ikiwa mtu ana moyo wa kusaidia, Mungu hupokea kila anachoweza kutoa: hadai zaidi.
<scripture passage="iiCor 8:13" parsed="|2Cor|8|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.13" />
<sup>13</sup>Ninyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
<scripture passage="iiCor 8:14" parsed="|2Cor|8|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.14" />
<sup>14</sup>Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie ninyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe na usawa.
<scripture passage="iiCor 8:15" parsed="|2Cor|8|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.15" />
<sup>15</sup>Kama Maandiko yasemavyo: "Aliyekusanya kwa wingi hakuwa na ziada, na yule aliyekusanya kidogo hakupungukiwa."
<scripture passage="iiCor 8:16" parsed="|2Cor|8|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.16" />
<sup>16</sup>Namshukuru Mungu aliyeweka ndani ya moyo wa Tito hamu hiyo niliyo nayo mimi ya kuwasaidia.
<scripture passage="iiCor 8:17" parsed="|2Cor|8|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.17" />
<sup>17</sup>Si tu kwamba alikubali ombi letu, ila pia alikuwa na hamu kubwa ya kusaidia, hata akaamua kwa hiari yake mwenyewe kuja kwenu.
<scripture passage="iiCor 8:18" parsed="|2Cor|8|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.18" />
<sup>18</sup>Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika kueneza Habari Njema zimeenea katika makanisa yote.
<scripture passage="iiCor 8:19" parsed="|2Cor|8|19|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.19" />
<sup>19</sup>Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.
<scripture passage="iiCor 8:20" parsed="|2Cor|8|20|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.20" />
<sup>20</sup>Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadi hii karimu.
<scripture passage="iiCor 8:21" parsed="|2Cor|8|21|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.21" />
<sup>21</sup>Nia yetu ni kufanya vema, si tu mbele ya Bwana, lakini pia mbele ya watu.
<scripture passage="iiCor 8:22" parsed="|2Cor|8|22|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.22" />
<sup>22</sup>Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani sana nanyi.
<scripture passage="iiCor 8:23" parsed="|2Cor|8|23|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.23" />
<sup>23</sup>Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini kuhusu hawa ndugu zetu wengine, wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, na utukufu kwa Kristo.
<scripture passage="iiCor 8:24" parsed="|2Cor|8|24|0|0" osisRef="Bible:2Cor.8.24" />
<sup>24</sup>Basi, waonyesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 9" progress="71.51%" prev="iiCor.8" next="iiCor.10" id="iiCor.9">
<h3 id="iiCor.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="iiCor.9-p1">
<scripture passage="iiCor 9:1" parsed="|2Cor|9|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.1" />
<sup>1</sup>Si lazima kuandika zaidi kuhusu huduma hiyo yenu kwa ajili ya watu wa Mungu.
<scripture passage="iiCor 9:2" parsed="|2Cor|9|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.2" />
<sup>2</sup>Ninajua jinsi mlivyo na moyo wa kusaidia, na nilijivuna juu yenu kuhusu jambo hilo mbele ya watu wa Makedonia. Niliwaambia: "Ndugu zetu wa Akaya wako tayari tangu mwaka jana." Hivyo, moto wenu umekwisha wahimiza watu wengi zaidi.
<scripture passage="iiCor 9:3" parsed="|2Cor|9|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.3" />
<sup>3</sup>Basi, nimewatuma ndugu zetu hao, ili fahari yetu juu yenu ionekane kwamba si maneno matupu, na kwamba mko tayari kabisa na msaada wenu kama nilivyosema.
<scripture passage="iiCor 9:4" parsed="|2Cor|9|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.4" />
<sup>4</sup>Isije ikawa kwamba watu wa Makedonia watakapokuja pamoja nami tukawakuta hamko tayari, hapo sisi tutaaibika--bila kutaja aibu mtakayopata ninyi wenyewe--kwa sababu tutakuwa tumewatumainia kupita kiasi.
<scripture passage="iiCor 9:5" parsed="|2Cor|9|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.5" />
<sup>5</sup>Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ionyeshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
<scripture passage="iiCor 9:6" parsed="|2Cor|9|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.6" />
<sup>6</sup>Kumbukeni: "Apandaye kidogo huvuna kidogo; apandaye kwa wingi huvuna kwa wingi."
<scripture passage="iiCor 9:7" parsed="|2Cor|9|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.7" />
<sup>7</sup>Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha.
<scripture passage="iiCor 9:8" parsed="|2Cor|9|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.8" />
<sup>8</sup>Mungu anaweza kuwapeni ninyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
<scripture passage="iiCor 9:9" parsed="|2Cor|9|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.9" />
<sup>9</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Yeye hutoa kwa ukarimu, huwapa maskini, wema wahudumu milele."
<scripture passage="iiCor 9:10" parsed="|2Cor|9|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.10" />
<sup>10</sup>Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa ninyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, ziwe na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
<scripture passage="iiCor 9:11" parsed="|2Cor|9|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.11" />
<sup>11</sup>Yeye atawatajirisha ninyi daima kwa kila kitu, ili watu wapate kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi zenu wanazozipokea kwa mikono yetu.
<scripture passage="iiCor 9:12" parsed="|2Cor|9|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.12" />
<sup>12</sup>Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si tu kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
<scripture passage="iiCor 9:13" parsed="|2Cor|9|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.13" />
<sup>13</sup>Kutokana na uthibitisho unaoonyeshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
<scripture passage="iiCor 9:14" parsed="|2Cor|9|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.14" />
<sup>14</sup>Kwa hiyo watawaombea ninyi kwa moyo kwa sababu ya neema ya pekee aliyowajalieni Mungu.
<scripture passage="iiCor 9:15" parsed="|2Cor|9|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.9.15" />
<sup>15</sup>Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 10" progress="71.74%" prev="iiCor.9" next="iiCor.11" id="iiCor.10">
<h3 id="iiCor.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="iiCor.10-p1">
<scripture passage="iiCor 10:1" parsed="|2Cor|10|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo mwenyewe ambaye naonekana kuwa mpole nikiwa pamoja nanyi, lakini mkali wakati nikiwa mbali nanyi, nawasihini kwa huruma na wema wake Kristo.
<scripture passage="iiCor 10:2" parsed="|2Cor|10|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.2" />
<sup>2</sup>Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
<scripture passage="iiCor 10:3" parsed="|2Cor|10|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.3" />
<sup>3</sup>Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.
<scripture passage="iiCor 10:4" parsed="|2Cor|10|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.4" />
<sup>4</sup>Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo,
<scripture passage="iiCor 10:5" parsed="|2Cor|10|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.5" />
<sup>5</sup>na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu; tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo.
<scripture passage="iiCor 10:6" parsed="|2Cor|10|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.6" />
<sup>6</sup>Mkisha kuwa wakamilifu katika kutii, sisi tuko tayari kuadhibu kila namna ya kutotii.
<scripture passage="iiCor 10:7" parsed="|2Cor|10|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.7" />
<sup>7</sup>Ninyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
<scripture passage="iiCor 10:8" parsed="|2Cor|10|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.8" />
<sup>8</sup>Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa--uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa--hata hivyo sijutii hata kidogo.
<scripture passage="iiCor 10:9" parsed="|2Cor|10|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.9" />
<sup>9</sup>Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha ninyi kwa barua zangu.
<scripture passage="iiCor 10:10" parsed="|2Cor|10|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.10" />
<sup>10</sup>Mtu anaweza kusema: "Barua za Paulo ni kali na zenye maneno mazito, lakini yeye mwenyewe anapokuwa pamoja nasi ni mtu dhaifu, na hata anapoongea maneno yake ni kama si kitu."
<scripture passage="iiCor 10:11" parsed="|2Cor|10|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.11" />
<sup>11</sup>Mtu asemaye hivyo heri akumbuke kwamba hakuna tofauti ya yale tunayoandika katika barua wakati tuko mbali, na yale tutakayofanya wakati tutakapokuwa nanyi.
<scripture passage="iiCor 10:12" parsed="|2Cor|10|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.12" />
<sup>12</sup>Kwa vyovyote hatungethubutu kujiweka au kujilinganisha na wale watu wanaojisifia wenyewe. Watu wenye kujifanya wao kuwa kipimo cha kujipimia, na watu wanaojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, ni wapumbavu.
<scripture passage="iiCor 10:13" parsed="|2Cor|10|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.13" />
<sup>13</sup>Lakini sisi hatutajivuna kupita kiasi; kujivuna huko kutabaki katika kile kipimo cha kazi aliyotukabidhi Mungu, kazi ambayo tunaifanya pia kwenu.
<scripture passage="iiCor 10:14" parsed="|2Cor|10|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.14" />
<sup>14</sup>Na kwa vile ninyi mu katika mipaka hiyo, hatukuipita tulipokuja kwenu, tukiwaleteeni Habari Njema juu ya Kristo.
<scripture passage="iiCor 10:15" parsed="|2Cor|10|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.15" />
<sup>15</sup>Basi, hatujivunii kazi waliyofanya wengine zaidi ya kipimo tulichopewa; ila tunatumaini kwamba imani yenu itazidi miongoni mwenu kufuatana na kipimo alichotuwekea Mungu.
<scripture passage="iiCor 10:16" parsed="|2Cor|10|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.16" />
<sup>16</sup>Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
<scripture passage="iiCor 10:17" parsed="|2Cor|10|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.17" />
<sup>17</sup>Lakini kama yasemavyo Maandiko: "Mwenye kuona fahari na aone fahari juu ya alichofanya Bwana."
<scripture passage="iiCor 10:18" parsed="|2Cor|10|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.10.18" />
<sup>18</sup>Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 11" progress="71.99%" prev="iiCor.10" next="iiCor.12" id="iiCor.11">
<h3 id="iiCor.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="iiCor.11-p1">
<scripture passage="iiCor 11:1" parsed="|2Cor|11|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.1" />
<sup>1</sup>Laiti mngenivumilia kidogo, hata kama mimi ni mjinga kiasi fulani! Naam, nivumilieni kidogo.
<scripture passage="iiCor 11:2" parsed="|2Cor|11|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.2" />
<sup>2</sup>Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana ninyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
<scripture passage="iiCor 11:3" parsed="|2Cor|11|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.3" />
<sup>3</sup>Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
<scripture passage="iiCor 11:4" parsed="|2Cor|11|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.4" />
<sup>4</sup>Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, ninyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au habari njema tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
<scripture passage="iiCor 11:5" parsed="|2Cor|11|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.5" />
<sup>5</sup>Sidhani kwamba mimi ni mdogo kuliko hao "mitume wakuu."
<scripture passage="iiCor 11:6" parsed="|2Cor|11|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.6" />
<sup>6</sup>Labda sina ufasaha wa lugha, lakini elimu ninayo; jambo hili tumelionyesha wazi kwenu, kila mahali na kila wakati.
<scripture passage="iiCor 11:7" parsed="|2Cor|11|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.7" />
<sup>7</sup>Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi. Je, nilifanya vibaya?
<scripture passage="iiCor 11:8" parsed="|2Cor|11|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.8" />
<sup>8</sup>Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia ninyi.
<scripture passage="iiCor 11:9" parsed="|2Cor|11|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.9" />
<sup>9</sup>Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
<scripture passage="iiCor 11:10" parsed="|2Cor|11|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.10" />
<sup>10</sup>Naahidi kwa ule ukweli wa Kristo ulio ndani yangu, kwamba hakuna kitakachoweza kunizuia kujivunia jambo hilo popote katika Akaya.
<scripture passage="iiCor 11:11" parsed="|2Cor|11|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.11" />
<sup>11</sup>Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu eti siwapendi ninyi? Mungu anajua kwamba nawapenda!
<scripture passage="iiCor 11:12" parsed="|2Cor|11|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.12" />
<sup>12</sup>Nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa, ili nisiwape nafasi wale wanaotafuta nafasi, nafasi ya kujivuna kwamba eti wanafanya kazi kama sisi.
<scripture passage="iiCor 11:13" parsed="|2Cor|11|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.13" />
<sup>13</sup>Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu wanojisingizia kuwa mitume wa Kristo.
<scripture passage="iiCor 11:14" parsed="|2Cor|11|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.14" />
<sup>14</sup>Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga!
<scripture passage="iiCor 11:15" parsed="|2Cor|11|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.15" />
<sup>15</sup>Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
<scripture passage="iiCor 11:16" parsed="|2Cor|11|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.16" />
<sup>16</sup>Tena nasema: Mtu asinifikirie kuwa mpumbavu. Lakini kama mkifikiri hivyo, basi, nichukueni kama mpumbavu ili nami nipate kuwa na cha kujivunia angaa kidogo.
<scripture passage="iiCor 11:17" parsed="|2Cor|11|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.17" />
<sup>17</sup>Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
<scripture passage="iiCor 11:18" parsed="|2Cor|11|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.18" />
<sup>18</sup>Maadam wengi hujivuna kwa sababu za kidunia, nami pia nitajivuna.
<scripture passage="iiCor 11:19" parsed="|2Cor|11|19|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.19" />
<sup>19</sup>Ninyi ni wenye busara, ndiyo maana hata mnawavumilia wapumbavu!
<scripture passage="iiCor 11:20" parsed="|2Cor|11|20|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.20" />
<sup>20</sup>Mnamvumilia hata mtu anayewafanya ninyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
<scripture passage="iiCor 11:21" parsed="|2Cor|11|21|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.21" />
<sup>21</sup>Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu--nasema kama mtu mpumbavu--mimi nathubutu pia.
<scripture passage="iiCor 11:22" parsed="|2Cor|11|22|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.22" />
<sup>22</sup>Je, wao ni Waebrania? Hata mimi. Je, wao ni Waisraeli? Hata mimi. Wao ni wazawa wa Abrahamu? Hata mimi.
<scripture passage="iiCor 11:23" parsed="|2Cor|11|23|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.23" />
<sup>23</sup>Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi--nanena hayo kiwazimu--ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
<scripture passage="iiCor 11:24" parsed="|2Cor|11|24|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.24" />
<sup>24</sup>Mara tano nilichapwa vile viboko thelathini na tisa vya Wayahudi.
<scripture passage="iiCor 11:25" parsed="|2Cor|11|25|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.25" />
<sup>25</sup>Nilipigwa viboko mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
<scripture passage="iiCor 11:26" parsed="|2Cor|11|26|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.26" />
<sup>26</sup>Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo
<scripture passage="iiCor 11:27" parsed="|2Cor|11|27|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.27" />
<sup>27</sup>Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
<scripture passage="iiCor 11:28" parsed="|2Cor|11|28|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.28" />
<sup>28</sup>Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.
<scripture passage="iiCor 11:29" parsed="|2Cor|11|29|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.29" />
<sup>29</sup>Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi. ic
<scripture passage="iiCor 11:30" parsed="|2Cor|11|30|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.30" />
<sup>30</sup>Ikinilazimu kujivuna, basi, nitajivunia udhaifu wangu.
<scripture passage="iiCor 11:31" parsed="|2Cor|11|31|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.31" />
<sup>31</sup>Mungu na Baba wa Bwana Yesu--jina lake litukuzwe milele--yeye anajua kwamba sisemi uongo.
<scripture passage="iiCor 11:32" parsed="|2Cor|11|32|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.32" />
<sup>32</sup>Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa, aliyekuwa chini ya mfalme Areta, alikuwa akiulinda mji wa Damasko ili apate kunikamata.
<scripture passage="iiCor 11:33" parsed="|2Cor|11|33|0|0" osisRef="Bible:2Cor.11.33" />
<sup>33</sup>Lakini, ndani ya kapu kubwa, niliteremshwa nje kupitia katika nafasi ukutani, nikachopoka mikononi mwake.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 12" progress="72.43%" prev="iiCor.11" next="iiCor.13" id="iiCor.12">
<h3 id="iiCor.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="iiCor.12-p1">
<scripture passage="iiCor 12:1" parsed="|2Cor|12|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.1" />
<sup>1</sup>Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana.
<scripture passage="iiCor 12:2" parsed="|2Cor|12|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.2" />
<sup>2</sup>Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua.)
<scripture passage="iiCor 12:3" parsed="|2Cor|12|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.3" />
<sup>3</sup>Narudia: najua kwamba mtu huyo alinyakuliwa mpaka peponi. (Lakini sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua.)
<scripture passage="iiCor 12:4" parsed="|2Cor|12|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.4" />
<sup>4</sup>Huko akasikia mambo ya siri ambayo binadamu hastahili kuyatamka.
<scripture passage="iiCor 12:5" parsed="|2Cor|12|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.5" />
<sup>5</sup>Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
<scripture passage="iiCor 12:6" parsed="|2Cor|12|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.6" />
<sup>6</sup>Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana ningekuwa nasema ukweli mtupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.
<scripture passage="iiCor 12:7" parsed="|2Cor|12|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.7" />
<sup>7</sup>Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga nisijivune kupita kiasi.
<scripture passage="iiCor 12:8" parsed="|2Cor|12|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.8" />
<sup>8</sup>Nilimsihi Bwana mara tatu kuhusu jambo hili ili linitoke.
<scripture passage="iiCor 12:9" parsed="|2Cor|12|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.9" />
<sup>9</sup>Lakini akaniambia: "Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu." Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.
<scripture passage="iiCor 12:10" parsed="|2Cor|12|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.10" />
<sup>10</sup>Kwa hiyo nakubali kwa radhi udhaifu, madharau, taabu, udhalimu na mateso, kwa ajili ya Kristo; maana ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa na nguvu.
<scripture passage="iiCor 12:11" parsed="|2Cor|12|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.11" />
<sup>11</sup>Nimekuwa kama mpumbavu, lakini, ninyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Ninyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo zaidi kuliko hao "mitume wakuu."
<scripture passage="iiCor 12:12" parsed="|2Cor|12|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.12" />
<sup>12</sup>Miujiza na maajabu yaonyeshayo wazi kwamba mimi ni mtume yalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivu wote.
<scripture passage="iiCor 12:13" parsed="|2Cor|12|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.13" />
<sup>13</sup>Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani kwa kuwakoseeni haki hiyo!
<scripture passage="iiCor 12:14" parsed="|2Cor|12|14|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.14" />
<sup>14</sup>Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni ninyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
<scripture passage="iiCor 12:15" parsed="|2Cor|12|15|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.15" />
<sup>15</sup>Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda ninyi mno?
<scripture passage="iiCor 12:16" parsed="|2Cor|12|16|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.16" />
<sup>16</sup>Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: "Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai."
<scripture passage="iiCor 12:17" parsed="|2Cor|12|17|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.17" />
<sup>17</sup>Je, mimi niliwanyonyeni kwa njia ya mjumbe yeyote niliyemtuma kwenu?
<scripture passage="iiCor 12:18" parsed="|2Cor|12|18|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.18" />
<sup>18</sup>Mimi nilimwita Tito, nikamtuma kwenu na ndugu yetu mwingine. Je, Tito aliwanyonyeni? Je, hamjui kwamba sisi tumekuwa tukiongozwa na roho yuleyule, na mwenendo wetu ni mmoja?
<scripture passage="iiCor 12:19" parsed="|2Cor|12|19|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.19" />
<sup>19</sup>Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambo hayo, yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
<scripture passage="iiCor 12:20" parsed="|2Cor|12|20|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.20" />
<sup>20</sup>Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyano, kunong`ona, majivuno na fujo kati yenu.
<scripture passage="iiCor 12:21" parsed="|2Cor|12|21|0|0" osisRef="Bible:2Cor.12.21" />
<sup>21</sup>Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujutia huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Corinthians 13" progress="72.77%" prev="iiCor.12" next="Gal" id="iiCor.13">
<h3 id="iiCor.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="iiCor.13-p1">
<scripture passage="iiCor 13:1" parsed="|2Cor|13|1|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.1" />
<sup>1</sup>Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. "Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu," yasema Maandiko.
<scripture passage="iiCor 13:2" parsed="|2Cor|13|2|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.2" />
<sup>2</sup>Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, watakiona cha mtema kuni.
<scripture passage="iiCor 13:3" parsed="|2Cor|13|3|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.3" />
<sup>3</sup>Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
<scripture passage="iiCor 13:4" parsed="|2Cor|13|4|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.4" />
<sup>4</sup>Maana hata kama alisulubiwa kwa sababu ya udhaifu, lakini sasa anaishi kwa uwezo wa Mungu. Sisi pia tu dhaifu kwa kuungana naye lakini tutaishi naye kwa uwezo wa Mungu kwa ajili yenu.
<scripture passage="iiCor 13:5" parsed="|2Cor|13|5|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.5" />
<sup>5</sup>Jichunguzeni ninyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni ninyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi ninyi mmeshindwa.
<scripture passage="iiCor 13:6" parsed="|2Cor|13|6|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.6" />
<sup>6</sup>Lakini natumaini kwamba ninyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa.
<scripture passage="iiCor 13:7" parsed="|2Cor|13|7|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.7" />
<sup>7</sup>Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
<scripture passage="iiCor 13:8" parsed="|2Cor|13|8|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.8" />
<sup>8</sup>Maana hatuwezi kuupinga ukweli; uwezo tulio nao ni wa kuuendeleza ukweli.
<scripture passage="iiCor 13:9" parsed="|2Cor|13|9|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.9" />
<sup>9</sup>Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.
<scripture passage="iiCor 13:10" parsed="|2Cor|13|10|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.10" />
<sup>10</sup>Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
<scripture passage="iiCor 13:11" parsed="|2Cor|13|11|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.11" />
<sup>11</sup>Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa mapendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
<scripture passage="iiCor 13:12" parsed="|2Cor|13|12|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.12" />
<sup>12</sup>Salimianeni kwa ishara ya upendo. Watu wote wa Mungu huku wanawasalimuni.
<scripture passage="iiCor 13:13" parsed="|2Cor|13|13|0|0" osisRef="Bible:2Cor.13.13" />
<sup>13</sup>Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na umoja wa Roho Mtakatifu, viwe nanyi nyote.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Galatians" progress="72.95%" prev="iiCor.13" next="Gal.1" id="Gal">
<h2 id="Gal-p0.1">Galatians</h2>

<div3 title="Galatians 1" progress="72.95%" prev="Gal" next="Gal.2" id="Gal.1">
<h3 id="Gal.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Gal.1-p1">
<scripture passage="Gal 1:1" parsed="|Gal|1|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo mtume,
<scripture passage="Gal 1:2" parsed="|Gal|1|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.2" />
<sup>2</sup>na ndugu wote walio pamoja nami, tunayaandikia makanisa yaliyoko Galatia. Mimi nimepata kuwa mtume si kutokana na mamlaka ya binadamu, wala si kwa nguvu ya mtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na wa Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka wafu.
<scripture passage="Gal 1:3" parsed="|Gal|1|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.3" />
<sup>3</sup>Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="Gal 1:4" parsed="|Gal|1|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.4" />
<sup>4</sup>Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba, ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu mbaya wa sasa.
<scripture passage="Gal 1:5" parsed="|Gal|1|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.5" />
<sup>5</sup>Kwake yeye uwe utukufu milele! Amina.
<scripture passage="Gal 1:6" parsed="|Gal|1|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.6" />
<sup>6</sup>Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi yule aliyewaita kwa neema ya Kristo, mkafuata Habari Njema ya namna nyingine.
<scripture passage="Gal 1:7" parsed="|Gal|1|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.7" />
<sup>7</sup>Lakini hakuna "Habari Njema" nyingine. Ukweli ni kwamba wako watu wanaowavurugeni, watu wanaotaka kuipotosha Habari Njema ya Kristo.
<scripture passage="Gal 1:8" parsed="|Gal|1|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.8" />
<sup>8</sup>Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni Habari Njema tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
<scripture passage="Gal 1:9" parsed="|Gal|1|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.9" />
<sup>9</sup>Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni Habari Njema ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
<scripture passage="Gal 1:10" parsed="|Gal|1|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.10" />
<sup>10</sup>Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
<scripture passage="Gal 1:11" parsed="|Gal|1|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.11" />
<sup>11</sup>Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Habari Njema niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
<scripture passage="Gal 1:12" parsed="|Gal|1|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.12" />
<sup>12</sup>Wala mimi sikuipokea kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia.
<scripture passage="Gal 1:13" parsed="|Gal|1|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.13" />
<sup>13</sup>Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
<scripture passage="Gal 1:14" parsed="|Gal|1|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.14" />
<sup>14</sup>Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
<scripture passage="Gal 1:15" parsed="|Gal|1|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.15" />
<sup>15</sup>Lakini Mungu, kwa neema yake, alikuwa ameniteua hata kabla sijazaliwa, akaniita nimtumikie.
<scripture passage="Gal 1:16" parsed="|Gal|1|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.16" />
<sup>16</sup>Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
<scripture passage="Gal 1:17" parsed="|Gal|1|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.17" />
<sup>17</sup>na bila kwenda kwanza Yerusalemu kwa wale waliopata kuwa mitume kabla yangu, nilikwenda kwanza Arabia, kisha nikarudi tena Damasko.
<scripture passage="Gal 1:18" parsed="|Gal|1|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.18" />
<sup>18</sup>Ilikuwa tu baada ya miaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemu kuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi na tano.
<scripture passage="Gal 1:19" parsed="|Gal|1|19|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.19" />
<sup>19</sup>Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
<scripture passage="Gal 1:20" parsed="|Gal|1|20|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.20" />
<sup>20</sup>Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua; sisemi uongo.
<scripture passage="Gal 1:21" parsed="|Gal|1|21|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.21" />
<sup>21</sup>Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia.
<scripture passage="Gal 1:22" parsed="|Gal|1|22|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.22" />
<sup>22</sup>Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo kule Yudea.
<scripture passage="Gal 1:23" parsed="|Gal|1|23|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.23" />
<sup>23</sup>Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: "Mtu yule aliyekuwa akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu kuiangamiza."
<scripture passage="Gal 1:24" parsed="|Gal|1|24|0|0" osisRef="Bible:Gal.1.24" />
<sup>24</sup>Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
</p>
</div3>

<div3 title="Galatians 2" progress="73.24%" prev="Gal.1" next="Gal.3" id="Gal.2">
<h3 id="Gal.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Gal.2-p1">
<scripture passage="Gal 2:1" parsed="|Gal|2|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.1" />
<sup>1</sup>Baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yerusalemu pamoja na Barnaba; nilimchukua pia Tito pamoja nami.
<scripture passage="Gal 2:2" parsed="|Gal|2|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.2" />
<sup>2</sup>Kwenda kwangu kulitokana na ufunuo alionipa Mungu. Katika kikao cha faragha niliwaeleza hao viongozi ujumbe wa Habari Njema niliohubiri kwa watu wa mataifa. Nilifanya hivyo kusudi kazi yangu niliyokuwa nimefanya, na ile ninayofanya sasa isije ikawa bure.
<scripture passage="Gal 2:3" parsed="|Gal|2|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.3" />
<sup>3</sup>Lakini, hata mwenzangu Tito, ambaye ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa,
<scripture passage="Gal 2:4" parsed="|Gal|2|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.4" />
<sup>4</sup>ingawa kulikuwa na ndugu wengine wa uongo waliotaka atahiriwe. Watu hawa walijiingiza kwa ujanja na kupeleleza uhuru wetu tulio nao katika kuungana na Kristo Yesu, ili wapate kutufanya watumwa.
<scripture passage="Gal 2:5" parsed="|Gal|2|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.5" />
<sup>5</sup>Hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Habari Njema ubaki nanyi daima.
<scripture passage="Gal 2:6" parsed="|Gal|2|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.6" />
<sup>6</sup>Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi--kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje--watu hawa hawakuwa na kitu cha kuongeza katika Habari hii Njema kama niihubirivyo.
<scripture passage="Gal 2:7" parsed="|Gal|2|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.7" />
<sup>7</sup>Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri Habari Njema kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
<scripture passage="Gal 2:8" parsed="|Gal|2|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.8" />
<sup>8</sup>Maana, yule aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi, ndiye aliyeniwezesha nami pia kuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine.
<scripture passage="Gal 2:9" parsed="|Gal|2|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.9" />
<sup>9</sup>Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu, walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono, yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
<scripture passage="Gal 2:10" parsed="|Gal|2|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.10" />
<sup>10</sup>Wakatuomba lakini kitu kimoja: tuwakumbuke maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kutekeleza.
<scripture passage="Gal 2:11" parsed="|Gal|2|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.11" />
<sup>11</sup>Lakini Kefa alipofika Antiokia nilimpinga waziwazi maana alikuwa amekosea.
<scripture passage="Gal 2:12" parsed="|Gal|2|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.12" />
<sup>12</sup>Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
<scripture passage="Gal 2:13" parsed="|Gal|2|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.13" />
<sup>13</sup>Hata ndugu wengine Wayahudi walimuunga mkono Petro katika kitendo hiki cha unafiki, naye Barnaba akakumbwa na huo unafiki wao.
<scripture passage="Gal 2:14" parsed="|Gal|2|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.14" />
<sup>14</sup>Basi, nilipoona kuwa msimamo wao kuhusu ukweli wa Habari Njema haukuwa umenyooka, nikamwambia Kefa mbele ya watu wote: "Ingawa wewe ni Myahudi, unaishi kama watu wa mataifa mengine na si kama Myahudi! Unawezaje, basi kujaribu kuwalazimisha watu wa mataifa mengine kuishi kama Wayahudi?"
<scripture passage="Gal 2:15" parsed="|Gal|2|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.15" />
<sup>15</sup>Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine hao wenye dhambi!
<scripture passage="Gal 2:16" parsed="|Gal|2|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.16" />
<sup>16</sup>Lakini, tunajua kwa hakika kwamba mtu hawezi kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa kuitii Sheria, bali tu kwa kumwamini Yesu Kristo. Na sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani yetu kwa Kristo, na si kwa kuitii Sheria.
<scripture passage="Gal 2:17" parsed="|Gal|2|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.17" />
<sup>17</sup>Sasa, ikiwa katika kutafuta kukubaliwa kuwa waadilifu kwa kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
<scripture passage="Gal 2:18" parsed="|Gal|2|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.18" />
<sup>18</sup>Lakini ikiwa ninajenga tena kile nilichokwisha bomoa, basi nahakikisha kwamba mimi ni mhalifu.
<scripture passage="Gal 2:19" parsed="|Gal|2|19|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.19" />
<sup>19</sup>Maana, kuhusu Sheria hiyo, mimi nimekufa; Sheria yenyewe iliniua, nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. Mimi nimeuawa pamoja na Kristo msalabani,
<scripture passage="Gal 2:20" parsed="|Gal|2|20|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.20" />
<sup>20</sup>na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu.
<scripture passage="Gal 2:21" parsed="|Gal|2|21|0|0" osisRef="Bible:Gal.2.21" />
<sup>21</sup>Sipendi kuikataa neema ya Mungu. Kama mtu huweza kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa njia ya Sheria, basi, Kristo alikufa bure!
</p>
</div3>

<div3 title="Galatians 3" progress="73.60%" prev="Gal.2" next="Gal.4" id="Gal.3">
<h3 id="Gal.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Gal.3-p1">
<scripture passage="Gal 3:1" parsed="|Gal|3|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.1" />
<sup>1</sup>Enyi Wagalatia, mmekuwa wajinga kweli! Ni nani aliyewaloga? Habari juu ya kusulubiwa kwake Yesu Kristo ilielezwa waziwazi mbele ya macho yenu.
<scripture passage="Gal 3:2" parsed="|Gal|3|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.2" />
<sup>2</sup>Napenda kujua tu kitu kimoja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa sababu ya kutimiza matakwa ya Sheria ama kwa sababu ya kuisikia na kuiamini Habari Njema?
<scripture passage="Gal 3:3" parsed="|Gal|3|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.3" />
<sup>3</sup>Je, mu wajinga kiasi hicho? Ninyi mlianza yote kwa msaada wa Roho je, mnataka sasa kumaliza kwa nguvu zenu wenyewe?
<scripture passage="Gal 3:4" parsed="|Gal|3|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.4" />
<sup>4</sup>Je, mambo yale yote yaliyowapata ninyi yamekuwa bure tu? Haiwezekani!
<scripture passage="Gal 3:5" parsed="|Gal|3|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.5" />
<sup>5</sup>Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Habari Njema na kuiamini?
<scripture passage="Gal 3:6" parsed="|Gal|3|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.6" />
<sup>6</sup>Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.
<scripture passage="Gal 3:7" parsed="|Gal|3|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.7" />
<sup>7</sup>Sasa basi jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu.
<scripture passage="Gal 3:8" parsed="|Gal|3|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.8" />
<sup>8</sup>Maandiko Matakatifu yalionyesha kabla kwamba Mungu atawakubali watu wa mataifa kuwa waadilifu kwa njia ya imani. Hivyo Maandiko Matakatifu yalitangulia kumtangazia Abrahamu Habari Njema: "Katika wewe mataifa yote yatabarikiwa."
<scripture passage="Gal 3:9" parsed="|Gal|3|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.9" />
<sup>9</sup>Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini.
<scripture passage="Gal 3:10" parsed="|Gal|3|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.10" />
<sup>10</sup>Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na Sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: "Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria, yuko chini ya laana."
<scripture passage="Gal 3:11" parsed="|Gal|3|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.11" />
<sup>11</sup>Ni dhahiri kwamba Sheria haiwezi kumfanya mtu akubaliwe kuwa mwadilifu; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Mwadilifu kwa imani ataishi."
<scripture passage="Gal 3:12" parsed="|Gal|3|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.12" />
<sup>12</sup>Lakini Sheria haitegemei imani, ila Maandiko yasema: "Mwenye kutimiza yanayotakiwa na Sheria ataishi."
<scripture passage="Gal 3:13" parsed="|Gal|3|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.13" />
<sup>13</sup>Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya Sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: "Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa."
<scripture passage="Gal 3:14" parsed="|Gal|3|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.14" />
<sup>14</sup>Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidia.
<scripture passage="Gal 3:15" parsed="|Gal|3|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.15" />
<sup>15</sup>Ndugu, nitawapeni mfano kutoka maisha yetu ya kila siku. Fikirini juu ya mkataba kati ya watu wawili. Mkataba ukisha fanyika na kutiwa sahihi hapana mtu anayeuweka kando au kuuongezea kitu.
<scripture passage="Gal 3:16" parsed="|Gal|3|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.16" />
<sup>16</sup>Basi, Abrahamu alipewa ahadi, yeye pamoja na mzawa wake. Maandiko hayasemi: "Na wazawa wake," yaani wengi, bali yasema, "Na mzawa wake," yaani mmoja, naye ndiye Kristo.
<scripture passage="Gal 3:17" parsed="|Gal|3|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.17" />
<sup>17</sup>Ninachotaka kusema ni hiki: Mungu alifanya agano lake akalithibitisha; Sheria ambayo ilitokea miaka mia nne na thelathini baadaye, haiwezi kulitangua hilo agano wala kuibatilisha hiyo ahadi.
<scripture passage="Gal 3:18" parsed="|Gal|3|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.18" />
<sup>18</sup>Maana, kama urithi ya Mungu inategemea Sheria, basi, haiwezi kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa sababu aliahidi.
<scripture passage="Gal 3:19" parsed="|Gal|3|19|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.19" />
<sup>19</sup>Ya nini basi, Sheria? Iliongezwa hapo ili kuonyesha uhalifu ni kitu gani, mpaka atakapokuja yule mzawa wa Abrahamu aliyepewa ile ahadi. Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi.
<scripture passage="Gal 3:20" parsed="|Gal|3|20|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.20" />
<sup>20</sup>Ama hakika, mpatanishi hahitajiwi ikiwa jambo lenyewe lamhusu mtu mmoja; na Mungu ni mmoja.
<scripture passage="Gal 3:21" parsed="|Gal|3|21|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.21" />
<sup>21</sup>Je, Sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi, tungeweza kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria.
<scripture passage="Gal 3:22" parsed="|Gal|3|22|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.22" />
<sup>22</sup>Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, kwa kumwamini Yesu Kristo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi.
<scripture passage="Gal 3:23" parsed="|Gal|3|23|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.23" />
<sup>23</sup>Kabla ya kujaliwa imani, Sheria ilitufanya wafungwa mpaka imani hiyo iliyokuwa inakuja ifunuliwe.
<scripture passage="Gal 3:24" parsed="|Gal|3|24|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.24" />
<sup>24</sup>Basi, hiyo Sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani, tukubaliwe kuwa waadilifu.
<scripture passage="Gal 3:25" parsed="|Gal|3|25|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.25" />
<sup>25</sup>Tangu kufika kwa hiyo imani, Sheria si mlezi wetu tena.
<scripture passage="Gal 3:26" parsed="|Gal|3|26|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.26" />
<sup>26</sup>Kwa njia ya imani, ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika kuungana na Kristo.
<scripture passage="Gal 3:27" parsed="|Gal|3|27|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.27" />
<sup>27</sup>Ninyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo.
<scripture passage="Gal 3:28" parsed="|Gal|3|28|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.28" />
<sup>28</sup>Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu.
<scripture passage="Gal 3:29" parsed="|Gal|3|29|0|0" osisRef="Bible:Gal.3.29" />
<sup>29</sup>Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, na mtapokea yale aliyoahidi Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="Galatians 4" progress="74.02%" prev="Gal.3" next="Gal.5" id="Gal.4">
<h3 id="Gal.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Gal.4-p1">
<scripture passage="Gal 4:1" parsed="|Gal|4|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.1" />
<sup>1</sup>Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake.
<scripture passage="Gal 4:2" parsed="|Gal|4|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.2" />
<sup>2</sup>Wakati huo wote yuko chini ya walezi na wadhamini mpaka wakati ule uliowekwa na baba yake.
<scripture passage="Gal 4:3" parsed="|Gal|4|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.3" />
<sup>3</sup>Hali kadhalika na sisi tulipokuwa bado watoto, tulikuwa watumwa wa pepo watawala wa ulimwengu.
<scripture passage="Gal 4:4" parsed="|Gal|4|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.4" />
<sup>4</sup>Lakini wakati ule maalumu ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe aliyezaliwa na mwanamke, akaishi chini ya Sheria
<scripture passage="Gal 4:5" parsed="|Gal|4|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.5" />
<sup>5</sup>apate kuwakomboa wale waliokuwa chini ya Sheria ili sisi tufanywe wana wa Mungu.
<scripture passage="Gal 4:6" parsed="|Gal|4|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.6" />
<sup>6</sup>Kwa vile sasa ninyi ni wana, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwenu, Roho ambaye hulia "Aba," yaani "Baba."
<scripture passage="Gal 4:7" parsed="|Gal|4|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.7" />
<sup>7</sup>Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi, wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.
<scripture passage="Gal 4:8" parsed="|Gal|4|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.8" />
<sup>8</sup>Zamani hamkumjua Mungu na hivyo mkatumikia miungu isiyo miungu kweli.
<scripture passage="Gal 4:9" parsed="|Gal|4|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.9" />
<sup>9</sup>Lakini sasa, kwa vile mnamjua Mungu, au tuseme mnajulikana na Mungu, mnawezaje tena kurudi kwa wale pepo maskini na dhaifu hata kutaka kuwatumikia tena?
<scripture passage="Gal 4:10" parsed="|Gal|4|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.10" />
<sup>10</sup>Bado mnaadhimisha siku, miezi na miaka!
<scripture passage="Gal 4:11" parsed="|Gal|4|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.11" />
<sup>11</sup>Nahofu kwamba labda kazi niliyoifanya kwa ajili yenu imepotea bure!
<scripture passage="Gal 4:12" parsed="|Gal|4|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.12" />
<sup>12</sup>Ndugu, nawasihi muwe kama mimi, kwa vile hata mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wowote.
<scripture passage="Gal 4:13" parsed="|Gal|4|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.13" />
<sup>13</sup>Mnajua kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia fursa ya kuwahubirieni Habari Njema kwa mara ya kwanza.
<scripture passage="Gal 4:14" parsed="|Gal|4|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.14" />
<sup>14</sup>Hata hivyo, wakati ule hamkunidharau wala kunikataa kwa sababu ya udhaifu wangu ingawa mlishawishiwa kufanya hivyo; lakini mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama vile ningekuwa Kristo Yesu mwenyewe.
<scripture passage="Gal 4:15" parsed="|Gal|4|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.15" />
<sup>15</sup>Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyang`oa macho yenu na kunipa mimi.
<scripture passage="Gal 4:16" parsed="|Gal|4|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.16" />
<sup>16</sup>Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu ya kuwaambieni ukweli?
<scripture passage="Gal 4:17" parsed="|Gal|4|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.17" />
<sup>17</sup>Hao watu wengine wanawahangaikia ninyi, lakini nia zao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili ninyi muwahangaikie wao.
<scripture passage="Gal 4:18" parsed="|Gal|4|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.18" />
<sup>18</sup>Kwa kweli ni jambo jema daima kuwahangaikia wengine katika mambo mema, na si tu wakati mimi nipo pamoja nanyi.
<scripture passage="Gal 4:19" parsed="|Gal|4|19|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.19" />
<sup>19</sup>Watoto wangu, kama vile mama mja mzito anavyotaabika wakati wa kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake Kristo itakapoundwa ndani yenu.
<scripture passage="Gal 4:20" parsed="|Gal|4|20|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.20" />
<sup>20</sup>Laiti ningekuwa pamoja nanyi sasa, maana ningalipata msimamo ufaao juu yenu! Nina wasiwasi sana nanyi!
<scripture passage="Gal 4:21" parsed="|Gal|4|21|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.21" />
<sup>21</sup>Niambieni, enyi mnaopenda kutawaliwa na sheria: Je, mnasikia isemavyo Sheria?
<scripture passage="Gal 4:22" parsed="|Gal|4|22|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.22" />
<sup>22</sup>Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
<scripture passage="Gal 4:23" parsed="|Gal|4|23|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.23" />
<sup>23</sup>Yule wa mwanamke mtumwa alizaliwa kama kawaida, lakini yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu.
<scripture passage="Gal 4:24" parsed="|Gal|4|24|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.24" />
<sup>24</sup>Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
<scripture passage="Gal 4:25" parsed="|Gal|4|25|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.25" />
<sup>25</sup>Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
<scripture passage="Gal 4:26" parsed="|Gal|4|26|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.26" />
<sup>26</sup>Lakini Yerusalemu ya juu mbinguni ni mji ulio huru, nao ni mama yetu.
<scripture passage="Gal 4:27" parsed="|Gal|4|27|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.27" />
<sup>27</sup>Maana imeandikwa: "Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa; paaza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto; maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi zaidi kuliko wa yule aliye na mume."
<scripture passage="Gal 4:28" parsed="|Gal|4|28|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.28" />
<sup>28</sup>Sasa, basi, ndugu zangu, ninyi ni watoto wa Mungu kutokana na ahadi yake kama alivyokuwa Isaka.
<scripture passage="Gal 4:29" parsed="|Gal|4|29|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.29" />
<sup>29</sup>Lakini kama vile siku zile yule mtoto aliyezaliwa kwa njia ya kawaida alimdhulumu yule aliyezaliwa kwa uwezo wa Roho wa Mungu, vivyo hivyo na siku hizi.
<scripture passage="Gal 4:30" parsed="|Gal|4|30|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.30" />
<sup>30</sup>Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: "Mfukuze mama mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mama huru."
<scripture passage="Gal 4:31" parsed="|Gal|4|31|0|0" osisRef="Bible:Gal.4.31" />
<sup>31</sup>Kwa hiyo, basi, ndugu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mama huru.
</p>
</div3>

<div3 title="Galatians 5" progress="74.39%" prev="Gal.4" next="Gal.6" id="Gal.5">
<h3 id="Gal.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Gal.5-p1">
<scripture passage="Gal 5:1" parsed="|Gal|5|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.1" />
<sup>1</sup>Kristo alitupa uhuru akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa.
<scripture passage="Gal 5:2" parsed="|Gal|5|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.2" />
<sup>2</sup>Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.
<scripture passage="Gal 5:3" parsed="|Gal|5|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.3" />
<sup>3</sup>Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika Sheria yote.
<scripture passage="Gal 5:4" parsed="|Gal|5|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.4" />
<sup>4</sup>Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
<scripture passage="Gal 5:5" parsed="|Gal|5|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.5" />
<sup>5</sup>Kwa upande wetu, lakini, sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Roho tunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani.
<scripture passage="Gal 5:6" parsed="|Gal|5|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.6" />
<sup>6</sup>Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo. ic
<scripture passage="Gal 5:7" parsed="|Gal|5|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.7" />
<sup>7</sup>Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia ukweli?
<scripture passage="Gal 5:8" parsed="|Gal|5|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.8" />
<sup>8</sup>Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni.
<scripture passage="Gal 5:9" parsed="|Gal|5|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.9" />
<sup>9</sup>"chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!"
<scripture passage="Gal 5:10" parsed="|Gal|5|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.10" />
<sup>10</sup>Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni--awe nani au nani--hakika ataadhibiwa.
<scripture passage="Gal 5:11" parsed="|Gal|5|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.11" />
<sup>11</sup>Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
<scripture passage="Gal 5:12" parsed="|Gal|5|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.12" />
<sup>12</sup>Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!
<scripture passage="Gal 5:13" parsed="|Gal|5|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.13" />
<sup>13</sup>Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.
<scripture passage="Gal 5:14" parsed="|Gal|5|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.14" />
<sup>14</sup>Maana Sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
<scripture passage="Gal 5:15" parsed="|Gal|5|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.15" />
<sup>15</sup>Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!
<scripture passage="Gal 5:16" parsed="|Gal|5|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.16" />
<sup>16</sup>Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.
<scripture passage="Gal 5:17" parsed="|Gal|5|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.17" />
<sup>17</sup>Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.
<scripture passage="Gal 5:18" parsed="|Gal|5|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.18" />
<sup>18</sup>Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.
<scripture passage="Gal 5:19" parsed="|Gal|5|19|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.19" />
<sup>19</sup>Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi;
<scripture passage="Gal 5:20" parsed="|Gal|5|20|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.20" />
<sup>20</sup>kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;
<scripture passage="Gal 5:21" parsed="|Gal|5|21|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.21" />
<sup>21</sup>husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa Mungu.
<scripture passage="Gal 5:22" parsed="|Gal|5|22|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.22" />
<sup>22</sup>Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,
<scripture passage="Gal 5:23" parsed="|Gal|5|23|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.23" />
<sup>23</sup>upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.
<scripture passage="Gal 5:24" parsed="|Gal|5|24|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.24" />
<sup>24</sup>Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
<scripture passage="Gal 5:25" parsed="|Gal|5|25|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.25" />
<sup>25</sup>Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.
<scripture passage="Gal 5:26" parsed="|Gal|5|26|0|0" osisRef="Bible:Gal.5.26" />
<sup>26</sup>Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.
</p>
</div3>

<div3 title="Galatians 6" progress="74.67%" prev="Gal.5" next="Eph" id="Gal.6">
<h3 id="Gal.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Gal.6-p1">
<scripture passage="Gal 6:1" parsed="|Gal|6|1|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, ninyi mnaoongozwa na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa.
<scripture passage="Gal 6:2" parsed="|Gal|6|2|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.2" />
<sup>2</sup>Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.
<scripture passage="Gal 6:3" parsed="|Gal|6|3|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.3" />
<sup>3</sup>Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe.
<scripture passage="Gal 6:4" parsed="|Gal|6|4|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.4" />
<sup>4</sup>Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine.
<scripture passage="Gal 6:5" parsed="|Gal|6|5|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.5" />
<sup>5</sup>Maana kila mmoja anao mzigo wake mwenyewe wa kubeba.
<scripture passage="Gal 6:6" parsed="|Gal|6|6|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.6" />
<sup>6</sup>Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake.
<scripture passage="Gal 6:7" parsed="|Gal|6|7|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.7" />
<sup>7</sup>Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.
<scripture passage="Gal 6:8" parsed="|Gal|6|8|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.8" />
<sup>8</sup>Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele.
<scripture passage="Gal 6:9" parsed="|Gal|6|9|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.9" />
<sup>9</sup>Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.
<scripture passage="Gal 6:10" parsed="|Gal|6|10|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.10" />
<sup>10</sup>Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu.
<scripture passage="Gal 6:11" parsed="|Gal|6|11|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.11" />
<sup>11</sup>Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.
<scripture passage="Gal 6:12" parsed="|Gal|6|12|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.12" />
<sup>12</sup>Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
<scripture passage="Gal 6:13" parsed="|Gal|6|13|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.13" />
<sup>13</sup>Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.
<scripture passage="Gal 6:14" parsed="|Gal|6|14|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.14" />
<sup>14</sup>Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.
<scripture passage="Gal 6:15" parsed="|Gal|6|15|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.15" />
<sup>15</sup>Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya.
<scripture passage="Gal 6:16" parsed="|Gal|6|16|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.16" />
<sup>16</sup>Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli--Wateule wa Mungu.
<scripture passage="Gal 6:17" parsed="|Gal|6|17|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.17" />
<sup>17</sup>Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo mwilini mwangu ni zile za Yesu.
<scripture passage="Gal 6:18" parsed="|Gal|6|18|0|0" osisRef="Bible:Gal.6.18" />
<sup>18</sup>Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Kristo. Amina.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Ephesians" progress="74.88%" prev="Gal.6" next="Eph.1" id="Eph">
<h2 id="Eph-p0.1">Ephesians</h2>

<div3 title="Ephesians 1" progress="74.88%" prev="Eph" next="Eph.2" id="Eph.1">
<h3 id="Eph.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Eph.1-p1">
<scripture passage="Eph 1:1" parsed="|Eph|1|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, nawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Efeso, mlio waaminifu katika kuungana na Kristo Yesu.
<scripture passage="Eph 1:2" parsed="|Eph|1|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.2" />
<sup>2</sup>Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="Eph 1:3" parsed="|Eph|1|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.3" />
<sup>3</sup>Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho mbinguni.
<scripture passage="Eph 1:4" parsed="|Eph|1|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.4" />
<sup>4</sup>Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katika kuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bila hitilafu mbele yake. Kwa sababu ya upendo wake,
<scripture passage="Eph 1:5" parsed="|Eph|1|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.5" />
<sup>5</sup>Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
<scripture passage="Eph 1:6" parsed="|Eph|1|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.6" />
<sup>6</sup>Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu katika Mwanae mpenzi!
<scripture passage="Eph 1:7" parsed="|Eph|1|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.7" />
<sup>7</sup>Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake
<scripture passage="Eph 1:8" parsed="|Eph|1|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.8" />
<sup>8</sup>aliotukirimia bila kipimo! Kwa hekima na ujuzi wake wote
<scripture passage="Eph 1:9" parsed="|Eph|1|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.9" />
<sup>9</sup>Mungu alitekeleza kile alichonuia, akatujulisha mpango wake uliofichika, ambao alikuwa ameazimia kuutekeleza kwa njia ya Kristo.
<scripture passage="Eph 1:10" parsed="|Eph|1|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.10" />
<sup>10</sup>Mpango huo ambao angeutimiza wakati utimiapo ni kukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo.
<scripture passage="Eph 1:11" parsed="|Eph|1|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.11" />
<sup>11</sup>Kila kitu hufanywa kufuatana na mpango na uamuzi wa Mungu; naye Mungu ametuteua sisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katika kuungana na Kristo, kufuatana na azimio alilofanya tangu mwanzo.
<scripture passage="Eph 1:12" parsed="|Eph|1|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.12" />
<sup>12</sup>Basi, sisi tuliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswa kuusifu utukufu wa Mungu!
<scripture passage="Eph 1:13" parsed="|Eph|1|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.13" />
<sup>13</sup>Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia.
<scripture passage="Eph 1:14" parsed="|Eph|1|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.14" />
<sup>14</sup>Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
<scripture passage="Eph 1:15" parsed="|Eph|1|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.15" />
<sup>15</sup>Kwa sababu hiyo, tangu niliposikia juu ya imani yenu kwa Bwana Yesu na mapendo yenu kwa watu wa Mungu,
<scripture passage="Eph 1:16" parsed="|Eph|1|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.16" />
<sup>16</sup>sijaacha kamwe kumshukuru Mungu kwa ajili yenu. Ninawakumbuka katika sala zangu
<scripture passage="Eph 1:17" parsed="|Eph|1|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.17" />
<sup>17</sup>ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Baba mtukufu, awajalieni Roho wake atakayewapa hekima na kuwafunulieni Mungu mpate kumjua.
<scripture passage="Eph 1:18" parsed="|Eph|1|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.18" />
<sup>18</sup>Namwomba Mungu aifunue mioyo yenu iweze kuuona mwanga wake, mpate kutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufu mkuu wa zawadi alizowawekea watu wake,
<scripture passage="Eph 1:19" parsed="|Eph|1|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.19" />
<sup>19</sup>mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na nguvu ile kuu mno
<scripture passage="Eph 1:20" parsed="|Eph|1|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.20" />
<sup>20</sup>aliyomfufua nayo Kristo kutoka wafu, akamketisha kulia kwake mbinguni.
<scripture passage="Eph 1:21" parsed="|Eph|1|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.21" />
<sup>21</sup>Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao.
<scripture passage="Eph 1:22" parsed="|Eph|1|22|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.22" />
<sup>22</sup>Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote.
<scripture passage="Eph 1:23" parsed="|Eph|1|23|0|0" osisRef="Bible:Eph.1.23" />
<sup>23</sup>Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu wake yeye anayekamilisha vitu vyote kila mahali.
</p>
</div3>

<div3 title="Ephesians 2" progress="75.18%" prev="Eph.1" next="Eph.3" id="Eph.2">
<h3 id="Eph.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Eph.2-p1">
<scripture passage="Eph 2:1" parsed="|Eph|2|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.1" />
<sup>1</sup>Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu.
<scripture passage="Eph 2:2" parsed="|Eph|2|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.2" />
<sup>2</sup>Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu.
<scripture passage="Eph 2:3" parsed="|Eph|2|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.3" />
<sup>3</sup>Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
<scripture passage="Eph 2:4" parsed="|Eph|2|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.4" />
<sup>4</sup>Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika,
<scripture passage="Eph 2:5" parsed="|Eph|2|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.5" />
<sup>5</sup>hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu ninyi mmeokolewa.
<scripture passage="Eph 2:6" parsed="|Eph|2|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.6" />
<sup>6</sup>Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni.
<scripture passage="Eph 2:7" parsed="|Eph|2|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.7" />
<sup>7</sup>Ndivyo alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
<scripture passage="Eph 2:8" parsed="|Eph|2|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.8" />
<sup>8</sup>Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu.
<scripture passage="Eph 2:9" parsed="|Eph|2|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.9" />
<sup>9</sup>Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu.
<scripture passage="Eph 2:10" parsed="|Eph|2|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.10" />
<sup>10</sup>Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.
<scripture passage="Eph 2:11" parsed="|Eph|2|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.11" />
<sup>11</sup>Ninyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine--mnaoitwa, "wasiotahiriwa" na Wayahudi ambao hujiita, "Waliotahiriwa," (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao)--kumbukeni mlivyokuwa zamani.
<scripture passage="Eph 2:12" parsed="|Eph|2|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.12" />
<sup>12</sup>Wakati ule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu yoyote katika lile agano la zile ahadi. Mlikuwa bila matumaini Mungu hapa duniani.
<scripture passage="Eph 2:13" parsed="|Eph|2|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.13" />
<sup>13</sup>Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, ninyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.
<scripture passage="Eph 2:14" parsed="|Eph|2|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.14" />
<sup>14</sup>Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui.
<scripture passage="Eph 2:15" parsed="|Eph|2|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.15" />
<sup>15</sup>Aliiondoa ile Sheria ya Wayahudi pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani.
<scripture passage="Eph 2:16" parsed="|Eph|2|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.16" />
<sup>16</sup>Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
<scripture passage="Eph 2:17" parsed="|Eph|2|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.17" />
<sup>17</sup>Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu ninyi watu wa mataifa mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi ambao walikuwa karibu na Mungu.
<scripture passage="Eph 2:18" parsed="|Eph|2|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.18" />
<sup>18</sup>Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, tunaweza kumwendea Baba katika Roho mmoja.
<scripture passage="Eph 2:19" parsed="|Eph|2|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.19" />
<sup>19</sup>Basi, ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
<scripture passage="Eph 2:20" parsed="|Eph|2|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.20" />
<sup>20</sup>Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi.
<scripture passage="Eph 2:21" parsed="|Eph|2|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.21" />
<sup>21</sup>Yeye ndiye mwenye kulitengeneza jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya B wana.
<scripture passage="Eph 2:22" parsed="|Eph|2|22|0|0" osisRef="Bible:Eph.2.22" />
<sup>22</sup>Katika kuungana naye, ninyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.
</p>
</div3>

<div3 title="Ephesians 3" progress="75.49%" prev="Eph.2" next="Eph.4" id="Eph.3">
<h3 id="Eph.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Eph.3-p1">
<scripture passage="Eph 3:1" parsed="|Eph|3|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.1" />
<sup>1</sup>Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu.
<scripture passage="Eph 3:2" parsed="|Eph|3|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.2" />
<sup>2</sup>Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu.
<scripture passage="Eph 3:3" parsed="|Eph|3|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.3" />
<sup>3</sup>Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili,
<scripture passage="Eph 3:4" parsed="|Eph|3|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.4" />
<sup>4</sup>nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo.)
<scripture passage="Eph 3:5" parsed="|Eph|3|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.5" />
<sup>5</sup>Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.
<scripture passage="Eph 3:6" parsed="|Eph|3|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.6" />
<sup>6</sup>Siri yenyewe ni hii: kwa njia ya Habari Njema watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
<scripture passage="Eph 3:7" parsed="|Eph|3|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.7" />
<sup>7</sup>Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Habari Njema kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
<scripture passage="Eph 3:8" parsed="|Eph|3|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.8" />
<sup>8</sup>Mimi ni mdogo kuliko watu wote wa Mungu; lakini amenijalia neema yake, ili niwahubirie watu wa mataifa utajiri wake Kristo usiopimika,
<scripture passage="Eph 3:9" parsed="|Eph|3|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.9" />
<sup>9</sup>tena niwaangazie watu wote waone jinsi mpango wa Mungu uliofichika unavyotekelezwa. Mungu aliye Muumba wa vitu vyote alificha siri hiyo yake tangu milele,
<scripture passage="Eph 3:10" parsed="|Eph|3|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.10" />
<sup>10</sup>kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi.
<scripture passage="Eph 3:11" parsed="|Eph|3|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.11" />
<sup>11</sup>Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
<scripture passage="Eph 3:12" parsed="|Eph|3|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.12" />
<sup>12</sup>Basi, katika kuungana na Kristo, na kwa njia ya imani katika Kristo, sisi tunathubutu kumkaribia Mungu kwa uhodari.
<scripture passage="Eph 3:13" parsed="|Eph|3|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.13" />
<sup>13</sup>Kwa hiyo, nawaombeni msife moyo kwa sababu ya mateso ninayopata kwa ajili yenu, maana hayo ni kwa ajili ya utukufu wenu.
<scripture passage="Eph 3:14" parsed="|Eph|3|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.14" />
<sup>14</sup>Kwa sababu hiyo, nampigia magoti Baba,
<scripture passage="Eph 3:15" parsed="|Eph|3|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.15" />
<sup>15</sup>aliye asili ya jamaa zote duniani na mbinguni.
<scripture passage="Eph 3:16" parsed="|Eph|3|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.16" />
<sup>16</sup>Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalieni kwa uwezo wa Roho wake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu,
<scripture passage="Eph 3:17" parsed="|Eph|3|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.17" />
<sup>17</sup>naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Namwomba mpate kuwa na mzizi na msingi katika mapendo
<scripture passage="Eph 3:18" parsed="|Eph|3|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.18" />
<sup>18</sup>kusudi muweze kufahamu pamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendo wa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu, kwa kimo na kina.
<scripture passage="Eph 3:19" parsed="|Eph|3|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.19" />
<sup>19</sup>Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.
<scripture passage="Eph 3:20" parsed="|Eph|3|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.20" />
<sup>20</sup>Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu, aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria;
<scripture passage="Eph 3:21" parsed="|Eph|3|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.3.21" />
<sup>21</sup>kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina.
</p>
</div3>

<div3 title="Ephesians 4" progress="75.74%" prev="Eph.3" next="Eph.5" id="Eph.4">
<h3 id="Eph.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Eph.4-p1">
<scripture passage="Eph 4:1" parsed="|Eph|4|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.1" />
<sup>1</sup>Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
<scripture passage="Eph 4:2" parsed="|Eph|4|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.2" />
<sup>2</sup>Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni ninyi kwa ninyi kwa mapendo.
<scripture passage="Eph 4:3" parsed="|Eph|4|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.3" />
<sup>3</sup>Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu.
<scripture passage="Eph 4:4" parsed="|Eph|4|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.4" />
<sup>4</sup>Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.
<scripture passage="Eph 4:5" parsed="|Eph|4|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.5" />
<sup>5</sup>Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja;
<scripture passage="Eph 4:6" parsed="|Eph|4|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.6" />
<sup>6</sup>kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote.
<scripture passage="Eph 4:7" parsed="|Eph|4|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.7" />
<sup>7</sup>Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na Kristo.
<scripture passage="Eph 4:8" parsed="|Eph|4|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.8" />
<sup>8</sup>Kama yasemavyo Maandiko: "Alipopaa mbinguni juu kabisa, alichukua mateka; aliwapa watu zawadi."
<scripture passage="Eph 4:9" parsed="|Eph|4|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.9" />
<sup>9</sup>Basi, inaposemwa: "alipaa juu," ina maana gani? Maana yake ni kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani.
<scripture passage="Eph 4:10" parsed="|Eph|4|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.10" />
<sup>10</sup>Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu.
<scripture passage="Eph 4:11" parsed="|Eph|4|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.11" />
<sup>11</sup>Ndiye aliyewapa watu zawadi: wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Habari Njema, wengine wachungaji na walimu.
<scripture passage="Eph 4:12" parsed="|Eph|4|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.12" />
<sup>12</sup>Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo,
<scripture passage="Eph 4:13" parsed="|Eph|4|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.13" />
<sup>13</sup>na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
<scripture passage="Eph 4:14" parsed="|Eph|4|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.14" />
<sup>14</sup>Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu, ili wawapotoshe wengine kwa hila.
<scripture passage="Eph 4:15" parsed="|Eph|4|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.15" />
<sup>15</sup>Ila, sisi tukisema ukweli kwa moyo wa mapendo tutakua zidi katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa;
<scripture passage="Eph 4:16" parsed="|Eph|4|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.16" />
<sup>16</sup>chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo.
<scripture passage="Eph 4:17" parsed="|Eph|4|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.17" />
<sup>17</sup>Basi, kwa jina la Bwana, nawaonyeni: msiishi tena kama watu wasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwa upuuzi mtupu,
<scripture passage="Eph 4:18" parsed="|Eph|4|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.18" />
<sup>18</sup>na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao.
<scripture passage="Eph 4:19" parsed="|Eph|4|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.19" />
<sup>19</sup>Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.
<scripture passage="Eph 4:20" parsed="|Eph|4|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.20" />
<sup>20</sup>Lakini ninyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo.
<scripture passage="Eph 4:21" parsed="|Eph|4|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.21" />
<sup>21</sup>Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu.
<scripture passage="Eph 4:22" parsed="|Eph|4|22|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.22" />
<sup>22</sup>Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu.
<scripture passage="Eph 4:23" parsed="|Eph|4|23|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.23" />
<sup>23</sup>Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu.
<scripture passage="Eph 4:24" parsed="|Eph|4|24|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.24" />
<sup>24</sup>Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.
<scripture passage="Eph 4:25" parsed="|Eph|4|25|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.25" />
<sup>25</sup>Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo.
<scripture passage="Eph 4:26" parsed="|Eph|4|26|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.26" />
<sup>26</sup>Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima.
<scripture passage="Eph 4:27" parsed="|Eph|4|27|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.27" />
<sup>27</sup>Msimpe Ibilisi nafasi.
<scripture passage="Eph 4:28" parsed="|Eph|4|28|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.28" />
<sup>28</sup>Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.
<scripture passage="Eph 4:29" parsed="|Eph|4|29|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.29" />
<sup>29</sup>Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.
<scripture passage="Eph 4:30" parsed="|Eph|4|30|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.30" />
<sup>30</sup>Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba ninyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
<scripture passage="Eph 4:31" parsed="|Eph|4|31|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.31" />
<sup>31</sup>Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele, matusi! Achaneni na kila uovu!
<scripture passage="Eph 4:32" parsed="|Eph|4|32|0|0" osisRef="Bible:Eph.4.32" />
<sup>32</sup>Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.
</p>
</div3>

<div3 title="Ephesians 5" progress="76.11%" prev="Eph.4" next="Eph.6" id="Eph.5">
<h3 id="Eph.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Eph.5-p1">
<scripture passage="Eph 5:1" parsed="|Eph|5|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.1" />
<sup>1</sup>Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi.
<scripture passage="Eph 5:2" parsed="|Eph|5|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.2" />
<sup>2</sup>Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko impendezayo Mungu.
<scripture passage="Eph 5:3" parsed="|Eph|5|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.3" />
<sup>3</sup>Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.
<scripture passage="Eph 5:4" parsed="|Eph|5|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.4" />
<sup>4</sup>Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.
<scripture passage="Eph 5:5" parsed="|Eph|5|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.5" />
<sup>5</sup>Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu.
<scripture passage="Eph 5:6" parsed="|Eph|5|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.6" />
<sup>6</sup>Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.
<scripture passage="Eph 5:7" parsed="|Eph|5|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.7" />
<sup>7</sup>Basi, msishirikiane nao.
<scripture passage="Eph 5:8" parsed="|Eph|5|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.8" />
<sup>8</sup>Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga:
<scripture passage="Eph 5:9" parsed="|Eph|5|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.9" />
<sup>9</sup>maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli.
<scripture passage="Eph 5:10" parsed="|Eph|5|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.10" />
<sup>10</sup>Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.
<scripture passage="Eph 5:11" parsed="|Eph|5|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.11" />
<sup>11</sup>Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni.
<scripture passage="Eph 5:12" parsed="|Eph|5|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.12" />
<sup>12</sup>Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.
<scripture passage="Eph 5:13" parsed="|Eph|5|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.13" />
<sup>13</sup>Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake hudhihirishwa;
<scripture passage="Eph 5:14" parsed="|Eph|5|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.14" />
<sup>14</sup>na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: "Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristo atakuangaza."
<scripture passage="Eph 5:15" parsed="|Eph|5|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.15" />
<sup>15</sup>Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.
<scripture passage="Eph 5:16" parsed="|Eph|5|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.16" />
<sup>16</sup>Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya.
<scripture passage="Eph 5:17" parsed="|Eph|5|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.17" />
<sup>17</sup>Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.
<scripture passage="Eph 5:18" parsed="|Eph|5|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.18" />
<sup>18</sup>Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Eph 5:19" parsed="|Eph|5|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.19" />
<sup>19</sup>Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
<scripture passage="Eph 5:20" parsed="|Eph|5|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.20" />
<sup>20</sup>Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Eph 5:21" parsed="|Eph|5|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.21" />
<sup>21</sup>Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo.
<scripture passage="Eph 5:22" parsed="|Eph|5|22|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.22" />
<sup>22</sup>Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.
<scripture passage="Eph 5:23" parsed="|Eph|5|23|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.23" />
<sup>23</sup>Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake.
<scripture passage="Eph 5:24" parsed="|Eph|5|24|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.24" />
<sup>24</sup>Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
<scripture passage="Eph 5:25" parsed="|Eph|5|25|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.25" />
<sup>25</sup>Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.
<scripture passage="Eph 5:26" parsed="|Eph|5|26|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.26" />
<sup>26</sup>Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji,
<scripture passage="Eph 5:27" parsed="|Eph|5|27|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.27" />
<sup>27</sup>kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
<scripture passage="Eph 5:28" parsed="|Eph|5|28|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.28" />
<sup>28</sup>Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ((
<scripture passage="Eph 5:29" parsed="|Eph|5|29|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.29" />
<sup>29</sup>Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa,
<scripture passage="Eph 5:30" parsed="|Eph|5|30|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.30" />
<sup>30</sup>maana sisi ni viungo vya mwili wake.)
<scripture passage="Eph 5:31" parsed="|Eph|5|31|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.31" />
<sup>31</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja."
<scripture passage="Eph 5:32" parsed="|Eph|5|32|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.32" />
<sup>32</sup>Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake.
<scripture passage="Eph 5:33" parsed="|Eph|5|33|0|0" osisRef="Bible:Eph.5.33" />
<sup>33</sup>Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
</p>
</div3>

<div3 title="Ephesians 6" progress="76.43%" prev="Eph.5" next="Col" id="Eph.6">
<h3 id="Eph.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Eph.6-p1">
<scripture passage="Eph 6:1" parsed="|Eph|6|1|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.1" />
<sup>1</sup>Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
<scripture passage="Eph 6:2" parsed="|Eph|6|2|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.2" />
<sup>2</sup>"Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,
<scripture passage="Eph 6:3" parsed="|Eph|6|3|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.3" />
<sup>3</sup>"Upate fanaka na miaka mingi duniani."
<scripture passage="Eph 6:4" parsed="|Eph|6|4|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.4" />
<sup>4</sup>Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
<scripture passage="Eph 6:5" parsed="|Eph|6|5|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.5" />
<sup>5</sup>Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
<scripture passage="Eph 6:6" parsed="|Eph|6|6|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.6" />
<sup>6</sup>Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo.
<scripture passage="Eph 6:7" parsed="|Eph|6|7|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.7" />
<sup>7</sup>Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
<scripture passage="Eph 6:8" parsed="|Eph|6|8|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.8" />
<sup>8</sup>Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
<scripture passage="Eph 6:9" parsed="|Eph|6|9|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.9" />
<sup>9</sup>Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.
<scripture passage="Eph 6:10" parsed="|Eph|6|10|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.10" />
<sup>10</sup>Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.
<scripture passage="Eph 6:11" parsed="|Eph|6|11|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.11" />
<sup>11</sup>Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
<scripture passage="Eph 6:12" parsed="|Eph|6|12|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.12" />
<sup>12</sup>Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.
<scripture passage="Eph 6:13" parsed="|Eph|6|13|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.13" />
<sup>13</sup>Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.
<scripture passage="Eph 6:14" parsed="|Eph|6|14|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.14" />
<sup>14</sup>Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,
<scripture passage="Eph 6:15" parsed="|Eph|6|15|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.15" />
<sup>15</sup>na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.
<scripture passage="Eph 6:16" parsed="|Eph|6|16|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.16" />
<sup>16</sup>Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.
<scripture passage="Eph 6:17" parsed="|Eph|6|17|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.17" />
<sup>17</sup>Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.
<scripture passage="Eph 6:18" parsed="|Eph|6|18|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.18" />
<sup>18</sup>Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.
<scripture passage="Eph 6:19" parsed="|Eph|6|19|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.19" />
<sup>19</sup>Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.
<scripture passage="Eph 6:20" parsed="|Eph|6|20|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.20" />
<sup>20</sup>Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
<scripture passage="Eph 6:21" parsed="|Eph|6|21|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.21" />
<sup>21</sup>Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
<scripture passage="Eph 6:22" parsed="|Eph|6|22|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.22" />
<sup>22</sup>Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.
<scripture passage="Eph 6:23" parsed="|Eph|6|23|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.23" />
<sup>23</sup>Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="Eph 6:24" parsed="|Eph|6|24|0|0" osisRef="Bible:Eph.6.24" />
<sup>24</sup>Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Colossians" progress="76.71%" prev="Eph.6" next="Col.1" id="Col">
<h2 id="Col-p0.1">Colossians</h2>

<div3 title="Colossians 1" progress="76.71%" prev="Col" next="Col.2" id="Col.1">
<h3 id="Col.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Col.1-p1">
<scripture passage="Col 1:1" parsed="|Col|1|1|0|0" osisRef="Bible:Col.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo,
<scripture passage="Col 1:2" parsed="|Col|1|2|0|0" osisRef="Bible:Col.1.2" />
<sup>2</sup>tunawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
<scripture passage="Col 1:3" parsed="|Col|1|3|0|0" osisRef="Bible:Col.1.3" />
<sup>3</sup>Daima tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, wakati tunapowaombea.
<scripture passage="Col 1:4" parsed="|Col|1|4|0|0" osisRef="Bible:Col.1.4" />
<sup>4</sup>Maana tumesikia juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na juu ya upendo wenu kwa watu wote wa Mungu.
<scripture passage="Col 1:5" parsed="|Col|1|5|0|0" osisRef="Bible:Col.1.5" />
<sup>5</sup>Wakati ujumbe ule wa kweli, yaani Habari Njema, ilipowafikieni kwa mara ya kwanza, mlipata kusikia juu ya lile tumaini linalopatikana kwake. Kwa sababu hiyo imani na upendo wenu vinategemea jambo lile mnalotumainia ambalo mmewekewa salama mbinguni.
<scripture passage="Col 1:6" parsed="|Col|1|6|0|0" osisRef="Bible:Col.1.6" />
<sup>6</sup>Habari Njema inazidi kuzaa matunda na kuenea ulimwenguni kote kama vile ilivyofanya kwenu ninyi tangu siku ile mliposikia juu ya neema ya Mungu na kuitambua ilivyo kweli.
<scripture passage="Col 1:7" parsed="|Col|1|7|0|0" osisRef="Bible:Col.1.7" />
<sup>7</sup>Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
<scripture passage="Col 1:8" parsed="|Col|1|8|0|0" osisRef="Bible:Col.1.8" />
<sup>8</sup>Yeye alitupa habari za upendo wenu mliojaliwa na Roho.
<scripture passage="Col 1:9" parsed="|Col|1|9|0|0" osisRef="Bible:Col.1.9" />
<sup>9</sup>Kwa sababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daima tangu tulipopata habari zenu. Tunamwomba Mungu awajazeni ujuzi kamili wa mapenzi yake, awajazeni hekima yote na elimu iletwayo na Roho wake.
<scripture passage="Col 1:10" parsed="|Col|1|10|0|0" osisRef="Bible:Col.1.10" />
<sup>10</sup>Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.
<scripture passage="Col 1:11" parsed="|Col|1|11|0|0" osisRef="Bible:Col.1.11" />
<sup>11</sup>Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili mweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
<scripture passage="Col 1:12" parsed="|Col|1|12|0|0" osisRef="Bible:Col.1.12" />
<sup>12</sup>Na kwa furaha, mshukuruni Baba aliyewawezesha ninyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale Mungu aliyowawekea watu wake katika utawala wa mwanga.
<scripture passage="Col 1:13" parsed="|Col|1|13|0|0" osisRef="Bible:Col.1.13" />
<sup>13</sup>Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi,
<scripture passage="Col 1:14" parsed="|Col|1|14|0|0" osisRef="Bible:Col.1.14" />
<sup>14</sup>ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.
<scripture passage="Col 1:15" parsed="|Col|1|15|0|0" osisRef="Bible:Col.1.15" />
<sup>15</sup>Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
<scripture passage="Col 1:16" parsed="|Col|1|16|0|0" osisRef="Bible:Col.1.16" />
<sup>16</sup>Maana kwa njia yake vitu vyote viliumbwa duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye mamlaka. Vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.
<scripture passage="Col 1:17" parsed="|Col|1|17|0|0" osisRef="Bible:Col.1.17" />
<sup>17</sup>Kristo alikuwako kabla ya vitu vyote; kwa kuungana naye, vyote vyadumu mahali pake.
<scripture passage="Col 1:18" parsed="|Col|1|18|0|0" osisRef="Bible:Col.1.18" />
<sup>18</sup>Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
<scripture passage="Col 1:19" parsed="|Col|1|19|0|0" osisRef="Bible:Col.1.19" />
<sup>19</sup>Maana Mungu alipenda utimilifu wote uwe ndani yake.
<scripture passage="Col 1:20" parsed="|Col|1|20|0|0" osisRef="Bible:Col.1.20" />
<sup>20</sup>Kwa njia yake Mungu alivipatanisha naye vitu vyote naam, viumbe vyote mbinguni na duniania; alileta amani kwa damu ya Kristo msalabani.
<scripture passage="Col 1:21" parsed="|Col|1|21|0|0" osisRef="Bible:Col.1.21" />
<sup>21</sup>Hapo kwanza ninyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu.
<scripture passage="Col 1:22" parsed="|Col|1|22|0|0" osisRef="Bible:Col.1.22" />
<sup>22</sup>Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awalete mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
<scripture passage="Col 1:23" parsed="|Col|1|23|0|0" osisRef="Bible:Col.1.23" />
<sup>23</sup>Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani hiyo, na msikubali kusukumwa mbali na tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Habari Njema ambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbe duniani.
<scripture passage="Col 1:24" parsed="|Col|1|24|0|0" osisRef="Bible:Col.1.24" />
<sup>24</sup>Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa.
<scripture passage="Col 1:25" parsed="|Col|1|25|0|0" osisRef="Bible:Col.1.25" />
<sup>25</sup>Nami nimefanywa kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na mpango wake Mungu ambao alinikabidhi kwa faida yenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza kwa ukamilifu ujumbe wake,
<scripture passage="Col 1:26" parsed="|Col|1|26|0|0" osisRef="Bible:Col.1.26" />
<sup>26</sup>ambao ni siri aliyowaficha binadamu wote tangu milele, lakini sasa amewajulisha watu wake.
<scripture passage="Col 1:27" parsed="|Col|1|27|0|0" osisRef="Bible:Col.1.27" />
<sup>27</sup>Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa ajili ya watu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo yuko ndani yenu, na jambo hilo lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu.
<scripture passage="Col 1:28" parsed="|Col|1|28|0|0" osisRef="Bible:Col.1.28" />
<sup>28</sup>Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo.
<scripture passage="Col 1:29" parsed="|Col|1|29|0|0" osisRef="Bible:Col.1.29" />
<sup>29</sup>Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu.
</p>
</div3>

<div3 title="Colossians 2" progress="77.13%" prev="Col.1" next="Col.3" id="Col.2">
<h3 id="Col.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Col.2-p1">
<scripture passage="Col 2:1" parsed="|Col|2|1|0|0" osisRef="Bible:Col.2.1" />
<sup>1</sup>Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
<scripture passage="Col 2:2" parsed="|Col|2|2|0|0" osisRef="Bible:Col.2.2" />
<sup>2</sup>Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.
<scripture passage="Col 2:3" parsed="|Col|2|3|0|0" osisRef="Bible:Col.2.3" />
<sup>3</sup>Ndani yake zimefichika hazina zote za hekima na elimu.
<scripture passage="Col 2:4" parsed="|Col|2|4|0|0" osisRef="Bible:Col.2.4" />
<sup>4</sup>Basi, nawaambieni, msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa maneno ya uongo hata kama ni ya kuvutia sana.
<scripture passage="Col 2:5" parsed="|Col|2|5|0|0" osisRef="Bible:Col.2.5" />
<sup>5</sup>Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
<scripture passage="Col 2:6" parsed="|Col|2|6|0|0" osisRef="Bible:Col.2.6" />
<sup>6</sup>Maadamu ninyi mmemkubali Kristo Yesu kuwa Bwana, basi, ishini katika muungano naye.
<scripture passage="Col 2:7" parsed="|Col|2|7|0|0" osisRef="Bible:Col.2.7" />
<sup>7</sup>Mnapaswa kuwa na mizizi ndani yake, kujijenga juu yake na kuwa imara katika imani yenu kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
<scripture passage="Col 2:8" parsed="|Col|2|8|0|0" osisRef="Bible:Col.2.8" />
<sup>8</sup>Angalieni basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu na ya pepo watawala, na wala si Kristo mwenyewe!
<scripture passage="Col 2:9" parsed="|Col|2|9|0|0" osisRef="Bible:Col.2.9" />
<sup>9</sup>Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
<scripture passage="Col 2:10" parsed="|Col|2|10|0|0" osisRef="Bible:Col.2.10" />
<sup>10</sup>nanyi mmepewa uzima kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote.
<scripture passage="Col 2:11" parsed="|Col|2|11|0|0" osisRef="Bible:Col.2.11" />
<sup>11</sup>Katika kuungana na Kristo ninyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
<scripture passage="Col 2:12" parsed="|Col|2|12|0|0" osisRef="Bible:Col.2.12" />
<sup>12</sup>Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa pia pamoja naye kwa imani yenu katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu.
<scripture passage="Col 2:13" parsed="|Col|2|13|0|0" osisRef="Bible:Col.2.13" />
<sup>13</sup>Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu ninyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa ninyi uzima pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote;
<scripture passage="Col 2:14" parsed="|Col|2|14|0|0" osisRef="Bible:Col.2.14" />
<sup>14</sup>alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
<scripture passage="Col 2:15" parsed="|Col|2|15|0|0" osisRef="Bible:Col.2.15" />
<sup>15</sup>Juu ya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
<scripture passage="Col 2:16" parsed="|Col|2|16|0|0" osisRef="Bible:Col.2.16" />
<sup>16</sup>Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya Mwezi mpya au Sabato.
<scripture passage="Col 2:17" parsed="|Col|2|17|0|0" osisRef="Bible:Col.2.17" />
<sup>17</sup>Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye Kristo.
<scripture passage="Col 2:18" parsed="|Col|2|18|0|0" osisRef="Bible:Col.2.18" />
<sup>18</sup>Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganifu za kidunia
<scripture passage="Col 2:19" parsed="|Col|2|19|0|0" osisRef="Bible:Col.2.19" />
<sup>19</sup>na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
<scripture passage="Col 2:20" parsed="|Col|2|20|0|0" osisRef="Bible:Col.2.20" />
<sup>20</sup>Ninyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa kutoka nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
<scripture passage="Col 2:21" parsed="|Col|2|21|0|0" osisRef="Bible:Col.2.21" />
<sup>21</sup>"Msishike hiki," "Msionje kile," "Msiguse kile!"
<scripture passage="Col 2:22" parsed="|Col|2|22|0|0" osisRef="Bible:Col.2.22" />
<sup>22</sup>Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
<scripture passage="Col 2:23" parsed="|Col|2|23|0|0" osisRef="Bible:Col.2.23" />
<sup>23</sup>Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima katika namna ya ibada ya kujitakia wenyewe, unyenyekevu wa uongo na kuutendea mwili kwa ukali; lakini kwa kweli, haifai chochote kuzuia tamaa za mwili.
</p>
</div3>

<div3 title="Colossians 3" progress="77.48%" prev="Col.2" next="Col.4" id="Col.3">
<h3 id="Col.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Col.3-p1">
<scripture passage="Col 3:1" parsed="|Col|3|1|0|0" osisRef="Bible:Col.3.1" />
<sup>1</sup>Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu.
<scripture passage="Col 3:2" parsed="|Col|3|2|0|0" osisRef="Bible:Col.3.2" />
<sup>2</sup>Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.
<scripture passage="Col 3:3" parsed="|Col|3|3|0|0" osisRef="Bible:Col.3.3" />
<sup>3</sup>Maana ninyi mmekufa na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
<scripture passage="Col 3:4" parsed="|Col|3|4|0|0" osisRef="Bible:Col.3.4" />
<sup>4</sup>Uzima wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
<scripture passage="Col 3:5" parsed="|Col|3|5|0|0" osisRef="Bible:Col.3.5" />
<sup>5</sup>Basi, komesheni kabisa kila kitu kilicho ndani yenu ambacho chahusika na mambo ya kidunia: uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).
<scripture passage="Col 3:6" parsed="|Col|3|6|0|0" osisRef="Bible:Col.3.6" />
<sup>6</sup>Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi.
<scripture passage="Col 3:7" parsed="|Col|3|7|0|0" osisRef="Bible:Col.3.7" />
<sup>7</sup>Wakati mmoja ninyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo, mlipotawaliwa nayo.
<scripture passage="Col 3:8" parsed="|Col|3|8|0|0" osisRef="Bible:Col.3.8" />
<sup>8</sup>Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa, uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
<scripture passage="Col 3:9" parsed="|Col|3|9|0|0" osisRef="Bible:Col.3.9" />
<sup>9</sup>Msiambiane uongo, kwani ninyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote,
<scripture passage="Col 3:10" parsed="|Col|3|10|0|0" osisRef="Bible:Col.3.10" />
<sup>10</sup>mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu.
<scripture passage="Col 3:11" parsed="|Col|3|11|0|0" osisRef="Bible:Col.3.11" />
<sup>11</sup>Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.
<scripture passage="Col 3:12" parsed="|Col|3|12|0|0" osisRef="Bible:Col.3.12" />
<sup>12</sup>Ninyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
<scripture passage="Col 3:13" parsed="|Col|3|13|0|0" osisRef="Bible:Col.3.13" />
<sup>13</sup>Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe ninyi.
<scripture passage="Col 3:14" parsed="|Col|3|14|0|0" osisRef="Bible:Col.3.14" />
<sup>14</sup>Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
<scripture passage="Col 3:15" parsed="|Col|3|15|0|0" osisRef="Bible:Col.3.15" />
<sup>15</sup>Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
<scripture passage="Col 3:16" parsed="|Col|3|16|0|0" osisRef="Bible:Col.3.16" />
<sup>16</sup>Ujumbe wa Kristo ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani.
<scripture passage="Col 3:17" parsed="|Col|3|17|0|0" osisRef="Bible:Col.3.17" />
<sup>17</sup>Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.
<scripture passage="Col 3:18" parsed="|Col|3|18|0|0" osisRef="Bible:Col.3.18" />
<sup>18</sup>Enyi akina mama, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana.
<scripture passage="Col 3:19" parsed="|Col|3|19|0|0" osisRef="Bible:Col.3.19" />
<sup>19</sup>Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.
<scripture passage="Col 3:20" parsed="|Col|3|20|0|0" osisRef="Bible:Col.3.20" />
<sup>20</sup>Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.
<scripture passage="Col 3:21" parsed="|Col|3|21|0|0" osisRef="Bible:Col.3.21" />
<sup>21</sup>Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.
<scripture passage="Col 3:22" parsed="|Col|3|22|0|0" osisRef="Bible:Col.3.22" />
<sup>22</sup>Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
<scripture passage="Col 3:23" parsed="|Col|3|23|0|0" osisRef="Bible:Col.3.23" />
<sup>23</sup>Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.
<scripture passage="Col 3:24" parsed="|Col|3|24|0|0" osisRef="Bible:Col.3.24" />
<sup>24</sup>Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!
<scripture passage="Col 3:25" parsed="|Col|3|25|0|0" osisRef="Bible:Col.3.25" />
<sup>25</sup>Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.
</p>
</div3>

<div3 title="Colossians 4" progress="77.77%" prev="Col.3" next="iThess" id="Col.4">
<h3 id="Col.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Col.4-p1">
<scripture passage="Col 4:1" parsed="|Col|4|1|0|0" osisRef="Bible:Col.4.1" />
<sup>1</sup>Nanyi wakuu, watendeeni watumwa wenu kwa uadilifu na haki, mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni.
<scripture passage="Col 4:2" parsed="|Col|4|2|0|0" osisRef="Bible:Col.4.2" />
<sup>2</sup>Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.
<scripture passage="Col 4:3" parsed="|Col|4|3|0|0" osisRef="Bible:Col.4.3" />
<sup>3</sup>Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
<scripture passage="Col 4:4" parsed="|Col|4|4|0|0" osisRef="Bible:Col.4.4" />
<sup>4</sup>Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna itakayodhihirisha siri hiyo.
<scripture passage="Col 4:5" parsed="|Col|4|5|0|0" osisRef="Bible:Col.4.5" />
<sup>5</sup>Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkitumia vizuri kila nafasi mliyo nayo.
<scripture passage="Col 4:6" parsed="|Col|4|6|0|0" osisRef="Bible:Col.4.6" />
<sup>6</sup>Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
<scripture passage="Col 4:7" parsed="|Col|4|7|0|0" osisRef="Bible:Col.4.7" />
<sup>7</sup>Ndugu yetu mpenzi Tukiko, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzetu katika kazi ya Bwana, atawapeni habari zangu zote.
<scripture passage="Col 4:8" parsed="|Col|4|8|0|0" osisRef="Bible:Col.4.8" />
<sup>8</sup>Ndiyo maana namtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwa kuwaambieni habari zetu.
<scripture passage="Col 4:9" parsed="|Col|4|9|0|0" osisRef="Bible:Col.4.9" />
<sup>9</sup>Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika hapa.
<scripture passage="Col 4:10" parsed="|Col|4|10|0|0" osisRef="Bible:Col.4.10" />
<sup>10</sup>Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
<scripture passage="Col 4:11" parsed="|Col|4|11|0|0" osisRef="Bible:Col.4.11" />
<sup>11</sup>Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya Utawala wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
<scripture passage="Col 4:12" parsed="|Col|4|12|0|0" osisRef="Bible:Col.4.12" />
<sup>12</sup>Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu anawasalimuni. Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
<scripture passage="Col 4:13" parsed="|Col|4|13|0|0" osisRef="Bible:Col.4.13" />
<sup>13</sup>Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Laodikea na Hierapoli.
<scripture passage="Col 4:14" parsed="|Col|4|14|0|0" osisRef="Bible:Col.4.14" />
<sup>14</sup>Luka, daktari wetu mpenzi, na Dema, wanawasalimuni.
<scripture passage="Col 4:15" parsed="|Col|4|15|0|0" osisRef="Bible:Col.4.15" />
<sup>15</sup>Salamu zetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
<scripture passage="Col 4:16" parsed="|Col|4|16|0|0" osisRef="Bible:Col.4.16" />
<sup>16</sup>Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na ninyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata kwao.
<scripture passage="Col 4:17" parsed="|Col|4|17|0|0" osisRef="Bible:Col.4.17" />
<sup>17</sup>Mwambieni Arkipo aitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa na Bwana.
<scripture passage="Col 4:18" parsed="|Col|4|18|0|0" osisRef="Bible:Col.4.18" />
<sup>18</sup>Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="1 Thessalonians" progress="77.99%" prev="Col.4" next="iThess.1" id="iThess">
<h2 id="iThess-p0.1">1 Thessalonians</h2>

<div3 title="1 Thessalonians 1" progress="78.00%" prev="iThess" next="iThess.2" id="iThess.1">
<h3 id="iThess.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iThess.1-p1">
<scripture passage="iThess 1:1" parsed="|1Thess|1|1|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="iThess 1:2" parsed="|1Thess|1|2|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.2" />
<sup>2</sup>Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi nyote na kuwakumbukeni daima katika sala zetu.
<scripture passage="iThess 1:3" parsed="|1Thess|1|3|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.3" />
<sup>3</sup>Maana, mbele ya Mungu Baba yetu, twakumbuka jinsi mnavyoonyesha imani yenu kwa matendo, jinsi upendo wenu unavyowawezesha kufanya kazi kwa bidii, na jinsi tumaini lenu katika Bwana wetu Yesu Kristo lilivyo thabiti.
<scripture passage="iThess 1:4" parsed="|1Thess|1|4|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.4" />
<sup>4</sup>Ndugu, twajua kwamba Mungu anawapenda na kwamba amewateua muwe watu wake,
<scripture passage="iThess 1:5" parsed="|1Thess|1|5|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.5" />
<sup>5</sup>maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi; tuliishi kwa manufaa yenu.
<scripture passage="iThess 1:6" parsed="|1Thess|1|6|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.6" />
<sup>6</sup>Ninyi mlifuata mfano wetu, na kumwiga Bwana. Ingawa mliteswa sana, mliupokea ujumbe huo kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.
<scripture passage="iThess 1:7" parsed="|1Thess|1|7|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.7" />
<sup>7</sup>Kwa hiyo ninyi mmekuwa mfano mzuri kwa waumini wote wa Makedonia na Akaya.
<scripture passage="iThess 1:8" parsed="|1Thess|1|8|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.8" />
<sup>8</sup>Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si tu huko Makedonia na Akaya, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi.
<scripture passage="iThess 1:9" parsed="|1Thess|1|9|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.9" />
<sup>9</sup>Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli,
<scripture passage="iThess 1:10" parsed="|1Thess|1|10|0|0" osisRef="Bible:1Thess.1.10" />
<sup>10</sup>na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka wafu, na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Thessalonians 2" progress="78.14%" prev="iThess.1" next="iThess.3" id="iThess.2">
<h3 id="iThess.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iThess.2-p1">
<scripture passage="iThess 2:1" parsed="|1Thess|2|1|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure.
<scripture passage="iThess 2:2" parsed="|1Thess|2|2|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.2" />
<sup>2</sup>Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.
<scripture passage="iThess 2:3" parsed="|1Thess|2|3|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.3" />
<sup>3</sup>Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.
<scripture passage="iThess 2:4" parsed="|1Thess|2|4|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.4" />
<sup>4</sup>Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.
<scripture passage="iThess 2:5" parsed="|1Thess|2|5|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.5" />
<sup>5</sup>Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu na maneno matamu ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
<scripture passage="iThess 2:6" parsed="|1Thess|2|6|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.6" />
<sup>6</sup>Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote,
<scripture passage="iThess 2:7" parsed="|1Thess|2|7|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.7" />
<sup>7</sup>ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa Wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.
<scripture passage="iThess 2:8" parsed="|1Thess|2|8|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.8" />
<sup>8</sup>Tuliwapenda ninyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
<scripture passage="iThess 2:9" parsed="|1Thess|2|9|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.9" />
<sup>9</sup>Ndugu, mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu.
<scripture passage="iThess 2:10" parsed="|1Thess|2|10|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.10" />
<sup>10</sup>Ninyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo wetu kati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri, mwadilifu na usio na lawama.
<scripture passage="iThess 2:11" parsed="|1Thess|2|11|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.11" />
<sup>11</sup>Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe.
<scripture passage="iThess 2:12" parsed="|1Thess|2|12|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.12" />
<sup>12</sup>Tuliwapeni moyo, tuliwafarijini na kuwahimiza ili mpate kuishi maisha yampendezayo Mungu ambaye aliwaiteni mshiriki Utawala na utukufu wake.
<scripture passage="iThess 2:13" parsed="|1Thess|2|13|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.13" />
<sup>13</sup>Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, ninyi mliusikia mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
<scripture passage="iThess 2:14" parsed="|1Thess|2|14|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.14" />
<sup>14</sup>Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Ninyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
<scripture passage="iThess 2:15" parsed="|1Thess|2|15|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.15" />
<sup>15</sup>ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!
<scripture passage="iThess 2:16" parsed="|1Thess|2|16|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.16" />
<sup>16</sup>Hata walijaribu kutuzuia kuwahubiria watu wa mataifa mengine ujumbe utakaowaletea wokovu. Ndivyo walivyokamilisha orodha ya dhambi zote walizotenda siku zote. Lakini sasa hasira ya Mungu imewaangukia.
<scripture passage="iThess 2:17" parsed="|1Thess|2|17|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.17" />
<sup>17</sup>Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
<scripture passage="iThess 2:18" parsed="|1Thess|2|18|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.18" />
<sup>18</sup>Kwa hiyo tuliamua kuwatembeleeni tena. Nami, Paulo, nilijaribu kuja kwenu zaidi ya mara moja, lakini Shetani alituzuia.
<scripture passage="iThess 2:19" parsed="|1Thess|2|19|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.19" />
<sup>19</sup>Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
<scripture passage="iThess 2:20" parsed="|1Thess|2|20|0|0" osisRef="Bible:1Thess.2.20" />
<sup>20</sup>Naam, ninyi ni utukufu wetu na furaha yetu!
</p>
</div3>

<div3 title="1 Thessalonians 3" progress="78.46%" prev="iThess.2" next="iThess.4" id="iThess.3">
<h3 id="iThess.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iThess.3-p1">
<scripture passage="iThess 3:1" parsed="|1Thess|3|1|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.1" />
<sup>1</sup>Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi. Basi, tuliamua kubaki kule Athene peke yetu,
<scripture passage="iThess 3:2" parsed="|1Thess|3|2|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.2" />
<sup>2</sup>na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,
<scripture passage="iThess 3:3" parsed="|1Thess|3|3|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.3" />
<sup>3</sup>kusudi imani ya mtu yeyote miongoni mwenu isije ikafifia kwa sababu ya taabu hizo. Ninyi mnajua kwamba tunapaswa kupata mateso.
<scripture passage="iThess 3:4" parsed="|1Thess|3|4|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.4" />
<sup>4</sup>Maana, tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; na kama mjuavyo ndivyo ilivyotukia.
<scripture passage="iThess 3:5" parsed="|1Thess|3|5|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.5" />
<sup>5</sup>Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!
<scripture passage="iThess 3:6" parsed="|1Thess|3|6|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.6" />
<sup>6</sup>Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
<scripture passage="iThess 3:7" parsed="|1Thess|3|7|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.7" />
<sup>7</sup>Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
<scripture passage="iThess 3:8" parsed="|1Thess|3|8|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.8" />
<sup>8</sup>kwani sasa tunaishi kweli ikiwa ninyi mnasimama imara katika kuungana na Bwana.
<scripture passage="iThess 3:9" parsed="|1Thess|3|9|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.9" />
<sup>9</sup>Sasa twaweza kumshukuru Mungu wetu kwa ajili yenu. Tunamshukuru kwa furaha tuliyo nayo mbele yake kwa sababu yenu.
<scripture passage="iThess 3:10" parsed="|1Thess|3|10|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.10" />
<sup>10</sup>Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.
<scripture passage="iThess 3:11" parsed="|1Thess|3|11|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.11" />
<sup>11</sup>Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu.
<scripture passage="iThess 3:12" parsed="|1Thess|3|12|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.12" />
<sup>12</sup>Bwana awawezeshe ninyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda ninyi.
<scripture passage="iThess 3:13" parsed="|1Thess|3|13|0|0" osisRef="Bible:1Thess.3.13" />
<sup>13</sup>Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Thessalonians 4" progress="78.64%" prev="iThess.3" next="iThess.5" id="iThess.4">
<h3 id="iThess.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iThess.4-p1">
<scripture passage="iThess 4:1" parsed="|1Thess|4|1|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.1" />
<sup>1</sup>Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.
<scripture passage="iThess 4:2" parsed="|1Thess|4|2|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.2" />
<sup>2</sup>Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
<scripture passage="iThess 4:3" parsed="|1Thess|4|3|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.3" />
<sup>3</sup>Mungu anataka ninyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa.
<scripture passage="iThess 4:4" parsed="|1Thess|4|4|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.4" />
<sup>4</sup>Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,
<scripture passage="iThess 4:5" parsed="|1Thess|4|5|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.5" />
<sup>5</sup>na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.
<scripture passage="iThess 4:6" parsed="|1Thess|4|6|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.6" />
<sup>6</sup>Basi, mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili. Tulikwisha waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu wanaofanya mambo hayo.
<scripture passage="iThess 4:7" parsed="|1Thess|4|7|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.7" />
<sup>7</sup>Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu.
<scripture passage="iThess 4:8" parsed="|1Thess|4|8|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.8" />
<sup>8</sup>Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali amdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
<scripture passage="iThess 4:9" parsed="|1Thess|4|9|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.9" />
<sup>9</sup>Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.
<scripture passage="iThess 4:10" parsed="|1Thess|4|10|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.10" />
<sup>10</sup>Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi.
<scripture passage="iThess 4:11" parsed="|1Thess|4|11|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.11" />
<sup>11</sup>Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie mambo yake mwenyewe na afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama tulivyowaagiza pale awali.
<scripture passage="iThess 4:12" parsed="|1Thess|4|12|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.12" />
<sup>12</sup>Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
<scripture passage="iThess 4:13" parsed="|1Thess|4|13|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.13" />
<sup>13</sup>Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini.
<scripture passage="iThess 4:14" parsed="|1Thess|4|14|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.14" />
<sup>14</sup>Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
<scripture passage="iThess 4:15" parsed="|1Thess|4|15|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.15" />
<sup>15</sup>Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana; sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki, wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
<scripture passage="iThess 4:16" parsed="|1Thess|4|16|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.16" />
<sup>16</sup>Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
<scripture passage="iThess 4:17" parsed="|1Thess|4|17|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.17" />
<sup>17</sup>Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.
<scripture passage="iThess 4:18" parsed="|1Thess|4|18|0|0" osisRef="Bible:1Thess.4.18" />
<sup>18</sup>Basi, farijianeni kwa maneno haya.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Thessalonians 5" progress="78.87%" prev="iThess.4" next="iiThess" id="iThess.5">
<h3 id="iThess.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iThess.5-p1">
<scripture passage="iThess 5:1" parsed="|1Thess|5|1|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.1" />
<sup>1</sup>Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya.
<scripture passage="iThess 5:2" parsed="|1Thess|5|2|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.2" />
<sup>2</sup>Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
<scripture passage="iThess 5:3" parsed="|1Thess|5|3|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.3" />
<sup>3</sup>Watu watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama" ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
<scripture passage="iThess 5:4" parsed="|1Thess|5|4|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.4" />
<sup>4</sup>Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.
<scripture passage="iThess 5:5" parsed="|1Thess|5|5|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.5" />
<sup>5</sup>Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza.
<scripture passage="iThess 5:6" parsed="|1Thess|5|6|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.6" />
<sup>6</sup>Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.
<scripture passage="iThess 5:7" parsed="|1Thess|5|7|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.7" />
<sup>7</sup>Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku.
<scripture passage="iThess 5:8" parsed="|1Thess|5|8|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.8" />
<sup>8</sup>Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma.
<scripture passage="iThess 5:9" parsed="|1Thess|5|9|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.9" />
<sup>9</sup>Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
<scripture passage="iThess 5:10" parsed="|1Thess|5|10|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.10" />
<sup>10</sup>ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa.
<scripture passage="iThess 5:11" parsed="|1Thess|5|11|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.11" />
<sup>11</sup>Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama mnavyofanya sasa.
<scripture passage="iThess 5:12" parsed="|1Thess|5|12|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.12" />
<sup>12</sup>Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo.
<scripture passage="iThess 5:13" parsed="|1Thess|5|13|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.13" />
<sup>13</sup>Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.
<scripture passage="iThess 5:14" parsed="|1Thess|5|14|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.14" />
<sup>14</sup>Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.
<scripture passage="iThess 5:15" parsed="|1Thess|5|15|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.15" />
<sup>15</sup>Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
<scripture passage="iThess 5:16" parsed="|1Thess|5|16|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.16" />
<sup>16</sup>Furahini daima,
<scripture passage="iThess 5:17" parsed="|1Thess|5|17|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.17" />
<sup>17</sup>salini kila wakati
<scripture passage="iThess 5:18" parsed="|1Thess|5|18|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.18" />
<sup>18</sup>na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
<scripture passage="iThess 5:19" parsed="|1Thess|5|19|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.19" />
<sup>19</sup>Msimpinge Roho Mtakatifu;
<scripture passage="iThess 5:20" parsed="|1Thess|5|20|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.20" />
<sup>20</sup>msidharau unabii.
<scripture passage="iThess 5:21" parsed="|1Thess|5|21|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.21" />
<sup>21</sup>Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema,
<scripture passage="iThess 5:22" parsed="|1Thess|5|22|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.22" />
<sup>22</sup>na epukeni kila aina ya uovu.
<scripture passage="iThess 5:23" parsed="|1Thess|5|23|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.23" />
<sup>23</sup>Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu--roho, mioyo na miili yenu--mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iThess 5:24" parsed="|1Thess|5|24|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.24" />
<sup>24</sup>Yeye anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.
<scripture passage="iThess 5:25" parsed="|1Thess|5|25|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.25" />
<sup>25</sup>Ndugu, tuombeeni na sisi pia.
<scripture passage="iThess 5:26" parsed="|1Thess|5|26|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.26" />
<sup>26</sup>Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.
<scripture passage="iThess 5:27" parsed="|1Thess|5|27|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.27" />
<sup>27</sup>Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii.
<scripture passage="iThess 5:28" parsed="|1Thess|5|28|0|0" osisRef="Bible:1Thess.5.28" />
<sup>28</sup>Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="2 Thessalonians" progress="79.12%" prev="iThess.5" next="iiThess.1" id="iiThess">
<h2 id="iiThess-p0.1">2 Thessalonians</h2>

<div3 title="2 Thessalonians 1" progress="79.12%" prev="iiThess" next="iiThess.2" id="iiThess.1">
<h3 id="iiThess.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiThess.1-p1">
<scripture passage="iiThess 1:1" parsed="|2Thess|1|1|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="iiThess 1:2" parsed="|2Thess|1|2|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.2" />
<sup>2</sup>Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
<scripture passage="iiThess 1:3" parsed="|2Thess|1|3|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.3" />
<sup>3</sup>Ndugu, tunapaswa kushukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
<scripture passage="iiThess 1:4" parsed="|2Thess|1|4|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.4" />
<sup>4</sup>Ndio maana sisi tunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
<scripture passage="iiThess 1:5" parsed="|2Thess|1|5|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.5" />
<sup>5</sup>Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake ninyi mtastahili Utawala wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
<scripture passage="iiThess 1:6" parsed="|2Thess|1|6|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.6" />
<sup>6</sup>Mungu atafanya jambo la haki: atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi,
<scripture passage="iiThess 1:7" parsed="|2Thess|1|7|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.7" />
<sup>7</sup>na kuwapeni nafuu ninyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake na wakuu
<scripture passage="iiThess 1:8" parsed="|2Thess|1|8|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.8" />
<sup>8</sup>na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu.
<scripture passage="iiThess 1:9" parsed="|2Thess|1|9|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.9" />
<sup>9</sup>Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu,
<scripture passage="iiThess 1:10" parsed="|2Thess|1|10|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.10" />
<sup>10</sup>wakati atakapokuja Siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
<scripture passage="iiThess 1:11" parsed="|2Thess|1|11|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.11" />
<sup>11</sup>Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezeshe muyastahili maisha aliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
<scripture passage="iiThess 1:12" parsed="|2Thess|1|12|0|0" osisRef="Bible:2Thess.1.12" />
<sup>12</sup>Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Thessalonians 2" progress="79.29%" prev="iiThess.1" next="iiThess.3" id="iiThess.2">
<h3 id="iiThess.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iiThess.2-p1">
<scripture passage="iiThess 2:1" parsed="|2Thess|2|1|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.1" />
<sup>1</sup>Sasa yahusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa kwetu pamoja tukae naye. Ndugu, tunawaombeni sana
<scripture passage="iiThess 2:2" parsed="|2Thess|2|2|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.2" />
<sup>2</sup>msifadhaike upesi moyoni, na wala msitiwe wasiwasi kwa sababu ya madai kwamba Siku ya Bwana imekwisha fika. Labda inadhaniwa kwamba jambo hili limetokana na uaguzi fulani, mahubiri au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu.
<scripture passage="iiThess 2:3" parsed="|2Thess|2|3|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.3" />
<sup>3</sup>Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile. Maana Siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule Uasi Mkuu utokee na yule Mwovu aonekane ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.
<scripture passage="iiThess 2:4" parsed="|2Thess|2|4|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.4" />
<sup>4</sup>Yeye atapinga kila kitu wanachokiona watu kuwa ni mungu, au wanachokiabudu. Naam, hata ataingia na kuketi ndani ya Hekalu la Mungu akijidai kuwa Mungu.
<scripture passage="iiThess 2:5" parsed="|2Thess|2|5|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.5" />
<sup>5</sup>Je, hamkumbuki kwamba niliwaambieni haya yote wakati nilipokuwa pamoja nanyi?
<scripture passage="iiThess 2:6" parsed="|2Thess|2|6|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.6" />
<sup>6</sup>Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
<scripture passage="iiThess 2:7" parsed="|2Thess|2|7|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.7" />
<sup>7</sup>Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
<scripture passage="iiThess 2:8" parsed="|2Thess|2|8|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.8" />
<sup>8</sup>Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng`ao wa kuja kwake.
<scripture passage="iiThess 2:9" parsed="|2Thess|2|9|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.9" />
<sup>9</sup>Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
<scripture passage="iiThess 2:10" parsed="|2Thess|2|10|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.10" />
<sup>10</sup>na kutumia udanganyifu wa kila namna kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea. Hao watapotea kwa sababu hawakuupokea na kuupenda ule ukweli ili waokolewe.
<scripture passage="iiThess 2:11" parsed="|2Thess|2|11|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.11" />
<sup>11</sup>Ndiyo maana Mungu amewaweka chini ya nguvu ya upotovu, wauamini uongo.
<scripture passage="iiThess 2:12" parsed="|2Thess|2|12|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.12" />
<sup>12</sup>Matokeo yake ni kwamba wote wasioamini ukweli, ila wafurahia dhambi, watahukumiwa.
<scripture passage="iiThess 2:13" parsed="|2Thess|2|13|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.13" />
<sup>13</sup>Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu, ninyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
<scripture passage="iiThess 2:14" parsed="|2Thess|2|14|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.14" />
<sup>14</sup>Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iiThess 2:15" parsed="|2Thess|2|15|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.15" />
<sup>15</sup>Basi, ndugu, simameni imara na zingatieni yale mafundisho tuliyowafundisheni kwa mahubiri yetu na barua zetu.
<scripture passage="iiThess 2:16" parsed="|2Thess|2|16|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.16" />
<sup>16</sup>Tunamwomba Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu ambaye alitupenda, na kwa neema yake akatujalia faraja ya milele na tumaini jema,
<scripture passage="iiThess 2:17" parsed="|2Thess|2|17|0|0" osisRef="Bible:2Thess.2.17" />
<sup>17</sup>aifariji mioyo yenu na kuwaimarisheni ili mweze daima kutenda na kusema yaliyo mema.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Thessalonians 3" progress="79.52%" prev="iiThess.2" next="iTim" id="iiThess.3">
<h3 id="iiThess.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iiThess.3-p1">
<scripture passage="iiThess 3:1" parsed="|2Thess|3|1|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.1" />
<sup>1</sup>Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
<scripture passage="iiThess 3:2" parsed="|2Thess|3|2|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.2" />
<sup>2</sup>Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanaoamini ujumbe huu.
<scripture passage="iiThess 3:3" parsed="|2Thess|3|3|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.3" />
<sup>3</sup>Lakini Bwana ni mwaminifu. Yeye atawaimarisheni na kuwalinda salama na yule Mwovu.
<scripture passage="iiThess 3:4" parsed="|2Thess|3|4|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.4" />
<sup>4</sup>Naye Bwana anatupatia tumaini kubwa juu yenu, na hatuna shaka kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaambieni.
<scripture passage="iiThess 3:5" parsed="|2Thess|3|5|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.5" />
<sup>5</sup>Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika uvumilivu tunaopewa na Kristo.
<scripture passage="iiThess 3:6" parsed="|2Thess|3|6|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.6" />
<sup>6</sup>Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
<scripture passage="iiThess 3:7" parsed="|2Thess|3|7|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.7" />
<sup>7</sup>Ninyi wenyewe mnajua kwamba mnapaswa kufuata mfano wetu. Sisi tulipokuwa nanyi hatukuwa wavivu;
<scripture passage="iiThess 3:8" parsed="|2Thess|3|8|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.8" />
<sup>8</sup>hatukula chakula kwa mtu yeyote bila ya kumlipa. Tulifanya kazi kwa bidii na taabu mchana na usiku ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote kati yenu.
<scripture passage="iiThess 3:9" parsed="|2Thess|3|9|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.9" />
<sup>9</sup>Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
<scripture passage="iiThess 3:10" parsed="|2Thess|3|10|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.10" />
<sup>10</sup>Tulipokuwa pamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, "Mtu asiyefanya kazi, asile."
<scripture passage="iiThess 3:11" parsed="|2Thess|3|11|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.11" />
<sup>11</sup>Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
<scripture passage="iiThess 3:12" parsed="|2Thess|3|12|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.12" />
<sup>12</sup>Kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo tunawaamuru na kuwaonya watu hao wawe na nidhamu na kufanya kazi ili wajipatie maslahi yao wenyewe.
<scripture passage="iiThess 3:13" parsed="|2Thess|3|13|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.13" />
<sup>13</sup>Lakini ninyi ndugu, msichoke kutenda mema.
<scripture passage="iiThess 3:14" parsed="|2Thess|3|14|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.14" />
<sup>14</sup>Huenda kwamba huko kuna mtu ambaye hatautii huu ujumbe tunaowapelekeeni katika barua hii. Ikiwa hivyo, basi, mfichueni mtu huyo na msiwe na uhusiano wowote naye kusudi aone aibu.
<scripture passage="iiThess 3:15" parsed="|2Thess|3|15|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.15" />
<sup>15</sup>Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu.
<scripture passage="iiThess 3:16" parsed="|2Thess|3|16|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.16" />
<sup>16</sup>Bwana mwenyewe ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote.
<scripture passage="iiThess 3:17" parsed="|2Thess|3|17|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.17" />
<sup>17</sup>Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
<scripture passage="iiThess 3:18" parsed="|2Thess|3|18|0|0" osisRef="Bible:2Thess.3.18" />
<sup>18</sup>Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="1 Timothy" progress="79.73%" prev="iiThess.3" next="iTim.1" id="iTim">
<h2 id="iTim-p0.1">1 Timothy</h2>

<div3 title="1 Timothy 1" progress="79.73%" prev="iTim" next="iTim.2" id="iTim.1">
<h3 id="iTim.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iTim.1-p1">
<scripture passage="iTim 1:1" parsed="|1Tim|1|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mtume wa Yesu Kristo kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Yesu Kristo tumaini letu,
<scripture passage="iTim 1:2" parsed="|1Tim|1|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.2" />
<sup>2</sup>nakuandikia Timotheo mwanangu halisi katika imani. Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Kristo Yesu Bwana wetu.
<scripture passage="iTim 1:3" parsed="|1Tim|1|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.3" />
<sup>3</sup>Napenda ukae huko Efeso, kama nilivyokuomba nilipokuwa ninakwenda Makedonia. Wako watu fulani huko wanaofundisha mafundisho ya uongo. Wakomeshe watu hao.
<scripture passage="iTim 1:4" parsed="|1Tim|1|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.4" />
<sup>4</sup>Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
<scripture passage="iTim 1:5" parsed="|1Tim|1|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.5" />
<sup>5</sup>Shabaha ya amri hii ni kuhimiza mapendo yatokayo katika moyo safi, dhamiri njema, na imani ya kweli.
<scripture passage="iTim 1:6" parsed="|1Tim|1|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.6" />
<sup>6</sup>Watu wengine wamepotoka na kugeukia majadiliano yasiyo na maana.
<scripture passage="iTim 1:7" parsed="|1Tim|1|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.7" />
<sup>7</sup>Wanapenda kuwa walimu wa Sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
<scripture passage="iTim 1:8" parsed="|1Tim|1|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.8" />
<sup>8</sup>Twajua kwamba Sheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo.
<scripture passage="iTim 1:9" parsed="|1Tim|1|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.9" />
<sup>9</sup>Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
<scripture passage="iTim 1:10" parsed="|1Tim|1|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.10" />
<sup>10</sup>sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba watu, waongo, na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho ya kweli.
<scripture passage="iTim 1:11" parsed="|1Tim|1|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.11" />
<sup>11</sup>Mafundisho hayo hupatikana katika Habari Njema ambayo mimi nimekabidhiwa niihubiri, Habari Njema ya Mungu mtukufu na mwenye heri.
<scripture passage="iTim 1:12" parsed="|1Tim|1|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.12" />
<sup>12</sup>Namshukuru Bwana wetu Yesu Kristo aliyenipa nguvu kwa ajili ya kazi yangu. Namshukuru kwa kuniona mimi kuwa ni mwaminifu, akaniteua nimtumikie,
<scripture passage="iTim 1:13" parsed="|1Tim|1|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.13" />
<sup>13</sup>ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
<scripture passage="iTim 1:14" parsed="|1Tim|1|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.14" />
<sup>14</sup>Lakini Bwana wetu alinijalia neema yake kwa wingi, akanipa imani na upendo katika kuungana na Kristo Yesu.
<scripture passage="iTim 1:15" parsed="|1Tim|1|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.15" />
<sup>15</sup>Usemi huu ni wa kuaminika, na tena unafaa kukubaliwa kabisa: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Nami ni mkosefu zaidi kuliko hao wote,
<scripture passage="iTim 1:16" parsed="|1Tim|1|16|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.16" />
<sup>16</sup>lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aonyeshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uzima wa milele.
<scripture passage="iTim 1:17" parsed="|1Tim|1|17|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.17" />
<sup>17</sup>Kwake yeye aliye Mfalme wa milele na asiyekufa, yeye aliye Mungu pekee--kwake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina.
<scripture passage="iTim 1:18" parsed="|1Tim|1|18|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.18" />
<sup>18</sup>Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
<scripture passage="iTim 1:19" parsed="|1Tim|1|19|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.19" />
<sup>19</sup>na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
<scripture passage="iTim 1:20" parsed="|1Tim|1|20|0|0" osisRef="Bible:1Tim.1.20" />
<sup>20</sup>Miongoni mwao ni Humenayo na Aleksanda ambao nimewakabidhi kwa Shetani, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Timothy 2" progress="80.01%" prev="iTim.1" next="iTim.3" id="iTim.2">
<h3 id="iTim.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iTim.2-p1">
<scripture passage="iTim 2:1" parsed="|1Tim|2|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.1" />
<sup>1</sup>Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote,
<scripture passage="iTim 2:2" parsed="|1Tim|2|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.2" />
<sup>2</sup>kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
<scripture passage="iTim 2:3" parsed="|1Tim|2|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.3" />
<sup>3</sup>Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,
<scripture passage="iTim 2:4" parsed="|1Tim|2|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.4" />
<sup>4</sup>ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
<scripture passage="iTim 2:5" parsed="|1Tim|2|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.5" />
<sup>5</sup>Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,
<scripture passage="iTim 2:6" parsed="|1Tim|2|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.6" />
<sup>6</sup>ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia.
<scripture passage="iTim 2:7" parsed="|1Tim|2|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.7" />
<sup>7</sup>Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
<scripture passage="iTim 2:8" parsed="|1Tim|2|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.8" />
<sup>8</sup>Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi.
<scripture passage="iTim 2:9" parsed="|1Tim|2|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.9" />
<sup>9</sup>Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa,
<scripture passage="iTim 2:10" parsed="|1Tim|2|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.10" />
<sup>10</sup>bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
<scripture passage="iTim 2:11" parsed="|1Tim|2|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.11" />
<sup>11</sup>Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza.
<scripture passage="iTim 2:12" parsed="|1Tim|2|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.12" />
<sup>12</sup>Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya.
<scripture passage="iTim 2:13" parsed="|1Tim|2|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.13" />
<sup>13</sup>Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa.
<scripture passage="iTim 2:14" parsed="|1Tim|2|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.14" />
<sup>14</sup>Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu.
<scripture passage="iTim 2:15" parsed="|1Tim|2|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.2.15" />
<sup>15</sup>Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Timothy 3" progress="80.17%" prev="iTim.2" next="iTim.4" id="iTim.3">
<h3 id="iTim.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iTim.3-p1">
<scripture passage="iTim 3:1" parsed="|1Tim|3|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.1" />
<sup>1</sup>Msemo huu ni wa kweli: mtu akitaka kuwa kiongozi katika kanisa, huyo anatamani kazi nzuri.
<scripture passage="iTim 3:2" parsed="|1Tim|3|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.2" />
<sup>2</sup>Basi, kiongozi wa kanisa anapaswa awe mtu asiye na lawama; anapaswa awe na mke mmoja tu, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha;
<scripture passage="iTim 3:3" parsed="|1Tim|3|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.3" />
<sup>3</sup>asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha;
<scripture passage="iTim 3:4" parsed="|1Tim|3|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.4" />
<sup>4</sup>anapaswa awe mtu awezaye kuongoza vema nyumba yake, na kuwafanya watoto wake wawe watii kwa heshima yote.
<scripture passage="iTim 3:5" parsed="|1Tim|3|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.5" />
<sup>5</sup>Maana kama mtu hawezi kuongoza vema nyumba yake, atawezaje kulitunza kanisa la Mungu?
<scripture passage="iTim 3:6" parsed="|1Tim|3|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.6" />
<sup>6</sup>Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.
<scripture passage="iTim 3:7" parsed="|1Tim|3|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.7" />
<sup>7</sup>Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa, ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.
<scripture passage="iTim 3:8" parsed="|1Tim|3|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.8" />
<sup>8</sup>Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
<scripture passage="iTim 3:9" parsed="|1Tim|3|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.9" />
<sup>9</sup>wanapaswa kuzingatia kwa dhamiri njema ukweli wa ndani wa imani.
<scripture passage="iTim 3:10" parsed="|1Tim|3|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.10" />
<sup>10</sup>Ni lazima kwanza wathibitishwe, na wakionekana kuwa wanafaa, basi, watoe huduma yao.
<scripture passage="iTim 3:11" parsed="|1Tim|3|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.11" />
<sup>11</sup>Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
<scripture passage="iTim 3:12" parsed="|1Tim|3|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.12" />
<sup>12</sup>Msaidizi katika kanisa lazima awe na mke moja tu, na awezaye kuongoza vema watoto wake na nyumba yake.
<scripture passage="iTim 3:13" parsed="|1Tim|3|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.13" />
<sup>13</sup>Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
<scripture passage="iTim 3:14" parsed="|1Tim|3|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.14" />
<sup>14</sup>Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi karibuni.
<scripture passage="iTim 3:15" parsed="|1Tim|3|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.15" />
<sup>15</sup>Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
<scripture passage="iTim 3:16" parsed="|1Tim|3|16|0|0" osisRef="Bible:1Tim.3.16" />
<sup>16</sup>Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa popote ulimwenguni, akachukuliwa juu mbinguni katika utukufu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Timothy 4" progress="80.38%" prev="iTim.3" next="iTim.5" id="iTim.4">
<h3 id="iTim.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iTim.4-p1">
<scripture passage="iTim 4:1" parsed="|1Tim|4|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.1" />
<sup>1</sup>Roho asema waziwazi kwamba siku za baadaye watu wengine wataitupilia mbali imani; watazitii roho danganyifu na kufuata mafundisho ya pepo.
<scripture passage="iTim 4:2" parsed="|1Tim|4|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.2" />
<sup>2</sup>Mafundisho ya namna hiyo yanaenezwa na watu waongo wadanganyifu, ambao dhamiri zao ziko kama zimechomwa kwa chuma cha moto.
<scripture passage="iTim 4:3" parsed="|1Tim|4|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.3" />
<sup>3</sup>Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuona na pia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.
<scripture passage="iTim 4:4" parsed="|1Tim|4|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.4" />
<sup>4</sup>Kila kitu alichoumba Mungu ni chema, wala hakuna kinachohitaji kukataliwa, bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani,
<scripture passage="iTim 4:5" parsed="|1Tim|4|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.5" />
<sup>5</sup>kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu.
<scripture passage="iTim 4:6" parsed="|1Tim|4|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.6" />
<sup>6</sup>Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli, ambayo wewe umeyafuata.
<scripture passage="iTim 4:7" parsed="|1Tim|4|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.7" />
<sup>7</sup>Lakini achana na hadithi zile zisizo za kidini na ambazo hazina maana. Jizoeshe kuishi maisha ya uchaji wa Mungu.
<scripture passage="iTim 4:8" parsed="|1Tim|4|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.8" />
<sup>8</sup>Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uzima katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
<scripture passage="iTim 4:9" parsed="|1Tim|4|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.9" />
<sup>9</sup>Usemi huo ni wa kusadikika kabisa na unastahili kukubaliwa.
<scripture passage="iTim 4:10" parsed="|1Tim|4|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.10" />
<sup>10</sup>Sisi tunajitahidi na kufanya kazi kwa bidii kwani tumemwekea tumaini letu Mungu aliye hai ambaye ni Mwokozi wa watu wote, na hasa wale wanaoamini.
<scripture passage="iTim 4:11" parsed="|1Tim|4|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.11" />
<sup>11</sup>Wape maagizo hayo na mafundisho hayo.
<scripture passage="iTim 4:12" parsed="|1Tim|4|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.12" />
<sup>12</sup>Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.
<scripture passage="iTim 4:13" parsed="|1Tim|4|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.13" />
<sup>13</sup>Tumia wakati wako na juhudi yako katika kusoma hadharani Maandiko Matakatifu, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
<scripture passage="iTim 4:14" parsed="|1Tim|4|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.14" />
<sup>14</sup>Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
<scripture passage="iTim 4:15" parsed="|1Tim|4|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.15" />
<sup>15</sup>Fikiri kwa makini juu ya hayo yote na kuyatekeleza kusudi maendeleo yako yaonekane na wote.
<scripture passage="iTim 4:16" parsed="|1Tim|4|16|0|0" osisRef="Bible:1Tim.4.16" />
<sup>16</sup>Angalia sana mambo yako mwenyewe, na mafundisho yako. Endelea kufanya hayo maana ukifanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Timothy 5" progress="80.59%" prev="iTim.4" next="iTim.6" id="iTim.5">
<h3 id="iTim.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iTim.5-p1">
<scripture passage="iTim 5:1" parsed="|1Tim|5|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.1" />
<sup>1</sup>Usimkemee mtu mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana kama ndugu zako,
<scripture passage="iTim 5:2" parsed="|1Tim|5|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.2" />
<sup>2</sup>wanawake wazee kama mama yako, na wasichana kama dada zako, kwa usafi wote.
<scripture passage="iTim 5:3" parsed="|1Tim|5|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.3" />
<sup>3</sup>Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
<scripture passage="iTim 5:4" parsed="|1Tim|5|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.4" />
<sup>4</sup>Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
<scripture passage="iTim 5:5" parsed="|1Tim|5|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.5" />
<sup>5</sup>Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
<scripture passage="iTim 5:6" parsed="|1Tim|5|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.6" />
<sup>6</sup>Lakini mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawa yu hai.
<scripture passage="iTim 5:7" parsed="|1Tim|5|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.7" />
<sup>7</sup>Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama.
<scripture passage="iTim 5:8" parsed="|1Tim|5|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.8" />
<sup>8</sup>Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.
<scripture passage="iTim 5:9" parsed="|1Tim|5|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.9" />
<sup>9</sup>Usimtie katika orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
<scripture passage="iTim 5:10" parsed="|1Tim|5|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.10" />
<sup>10</sup>na awe mwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema.
<scripture passage="iTim 5:11" parsed="|1Tim|5|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.11" />
<sup>11</sup>Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo watataka kuolewa tena,
<scripture passage="iTim 5:12" parsed="|1Tim|5|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.12" />
<sup>12</sup>na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.
<scripture passage="iTim 5:13" parsed="|1Tim|5|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.13" />
<sup>13</sup>Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa kusema.
<scripture passage="iTim 5:14" parsed="|1Tim|5|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.14" />
<sup>14</sup>Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao ili adui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juu yetu.
<scripture passage="iTim 5:15" parsed="|1Tim|5|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.15" />
<sup>15</sup>Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.
<scripture passage="iTim 5:16" parsed="|1Tim|5|16|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.16" />
<sup>16</sup>Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
<scripture passage="iTim 5:17" parsed="|1Tim|5|17|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.17" />
<sup>17</sup>Wazee wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
<scripture passage="iTim 5:18" parsed="|1Tim|5|18|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.18" />
<sup>18</sup>Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Usimfunge ng`ombe kinywa anapopura nafaka." na tena "Mfanyakazi astahili malipo yake."
<scripture passage="iTim 5:19" parsed="|1Tim|5|19|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.19" />
<sup>19</sup>Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu.
<scripture passage="iTim 5:20" parsed="|1Tim|5|20|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.20" />
<sup>20</sup>Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
<scripture passage="iTim 5:21" parsed="|1Tim|5|21|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.21" />
<sup>21</sup>Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya malaika watakatifu uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
<scripture passage="iTim 5:22" parsed="|1Tim|5|22|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.22" />
<sup>22</sup>Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.
<scripture passage="iTim 5:23" parsed="|1Tim|5|23|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.23" />
<sup>23</sup>Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara.
<scripture passage="iTim 5:24" parsed="|1Tim|5|24|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.24" />
<sup>24</sup>Dhambi za watu wengine huonekana waziwazi, nazo zawatangulia kwenye hukumu; lakini dhambi za wengine huonekana tu baadaye.
<scripture passage="iTim 5:25" parsed="|1Tim|5|25|0|0" osisRef="Bible:1Tim.5.25" />
<sup>25</sup>Vivyo hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo si dhahiri hayawezi kufichika.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Timothy 6" progress="80.91%" prev="iTim.5" next="iiTim" id="iTim.6">
<h3 id="iTim.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="iTim.6-p1">
<scripture passage="iTim 6:1" parsed="|1Tim|6|1|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.1" />
<sup>1</sup>Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
<scripture passage="iTim 6:2" parsed="|1Tim|6|2|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.2" />
<sup>2</sup>Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda. Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya.
<scripture passage="iTim 6:3" parsed="|1Tim|6|3|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.3" />
<sup>3</sup>Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho ya dini,
<scripture passage="iTim 6:4" parsed="|1Tim|6|4|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.4" />
<sup>4</sup>huyo amejaa majivuno na wala hajui chochote. Ni mtu wa kupenda ubishi na magombano juu ya maneno matupu, na hiyo husababisha wivu, ugomvi, matusi, shuku mbaya,
<scripture passage="iTim 6:5" parsed="|1Tim|6|5|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.5" />
<sup>5</sup>na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya kujipatia utajiri.
<scripture passage="iTim 6:6" parsed="|1Tim|6|6|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.6" />
<sup>6</sup>Kweli dini humfanya mtu awe tajiri sana, ikiwa anatosheka na vitu alivyo navyo.
<scripture passage="iTim 6:7" parsed="|1Tim|6|7|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.7" />
<sup>7</sup>Maana hatukuleta kitu chochote hapa duniani, wala hatutachukua chochote.
<scripture passage="iTim 6:8" parsed="|1Tim|6|8|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.8" />
<sup>8</sup>Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo.
<scripture passage="iTim 6:9" parsed="|1Tim|6|9|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.9" />
<sup>9</sup>Lakini wale wanaotaka kutajirika huanguka katika majaribu, na kunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbaya za kipumbavu, ambazo huwavuta mpaka kwenye uharibifu na maangamizi.
<scripture passage="iTim 6:10" parsed="|1Tim|6|10|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.10" />
<sup>10</sup>Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.
<scripture passage="iTim 6:11" parsed="|1Tim|6|11|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.11" />
<sup>11</sup>Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, mapendo, subira na unyenyekevu.
<scripture passage="iTim 6:12" parsed="|1Tim|6|12|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.12" />
<sup>12</sup>Piga mbio kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani, ukajipatie tuzo la uzima wa milele, uliloitiwa wakati ulipokiri imani yako mbele ya mashahidi wengi.
<scripture passage="iTim 6:13" parsed="|1Tim|6|13|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.13" />
<sup>13</sup>Mbele ya Mungu anayevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Yesu Kristo aliyetoa ushahidi na kukiri ukweli mbele ya Pontio Pilato,
<scripture passage="iTim 6:14" parsed="|1Tim|6|14|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.14" />
<sup>14</sup>nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka Siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iTim 6:15" parsed="|1Tim|6|15|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.15" />
<sup>15</sup>Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao uliopangwa na Mungu mwenye heri na aliye Mtawala pekee, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.
<scripture passage="iTim 6:16" parsed="|1Tim|6|16|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.16" />
<sup>16</sup>Yeye peke yake anaishi milele, katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe heshima na uwezo wa milele! Amina.
<scripture passage="iTim 6:17" parsed="|1Tim|6|17|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.17" />
<sup>17</sup>Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie.
<scripture passage="iTim 6:18" parsed="|1Tim|6|18|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.18" />
<sup>18</sup>Waamuru watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, na wawe wakarimu na walio tayari kuwashirikisha wengine mali zao.
<scripture passage="iTim 6:19" parsed="|1Tim|6|19|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.19" />
<sup>19</sup>Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uzima ambao ni uzima wa kweli.
<scripture passage="iTim 6:20" parsed="|1Tim|6|20|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.20" />
<sup>20</sup>Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine: "Elimu".
<scripture passage="iTim 6:21" parsed="|1Tim|6|21|0|0" osisRef="Bible:1Tim.6.21" />
<sup>21</sup>Maana wengine wamejidai kuwa na hiyo elimu, na matokeo yake wamepoteza imani. Nawatakieni nyote neema!
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="2 Timothy" progress="81.22%" prev="iTim.6" next="iiTim.1" id="iiTim">
<h2 id="iiTim-p0.1">2 Timothy</h2>

<div3 title="2 Timothy 1" progress="81.22%" prev="iiTim" next="iiTim.2" id="iiTim.1">
<h3 id="iiTim.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiTim.1-p1">
<scripture passage="iiTim 1:1" parsed="|2Tim|1|1|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili niutangaze ule uzima tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,
<scripture passage="iiTim 1:2" parsed="|2Tim|1|2|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.2" />
<sup>2</sup>nakuandikia wewe mwanangu mpenzi Timotheo. Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.
<scripture passage="iiTim 1:3" parsed="|2Tim|1|3|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.3" />
<sup>3</sup>Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka daima katika sala zangu.
<scripture passage="iiTim 1:4" parsed="|2Tim|1|4|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.4" />
<sup>4</sup>Nakumbuka machozi yako na ninatamani usiku na mchana kukuona, ili nijazwe furaha.
<scripture passage="iiTim 1:5" parsed="|2Tim|1|5|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.5" />
<sup>5</sup>Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.
<scripture passage="iiTim 1:6" parsed="|2Tim|1|6|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.6" />
<sup>6</sup>Ndio maana nakukumbusha ukiweke motomoto kile kipaji ulichopewa na Mungu wakati nilipokuwekea mikono yangu.
<scripture passage="iiTim 1:7" parsed="|2Tim|1|7|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.7" />
<sup>7</sup>Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.
<scripture passage="iiTim 1:8" parsed="|2Tim|1|8|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.8" />
<sup>8</sup>Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unazopewa na Mungu.
<scripture passage="iiTim 1:9" parsed="|2Tim|1|9|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.9" />
<sup>9</sup>Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya matendo yetu wenyewe bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo katika Kristo Yesu kabla mwanzo wa nyakati;
<scripture passage="iiTim 1:10" parsed="|2Tim|1|10|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.10" />
<sup>10</sup>lakini sasa imefunuliwa kwetu kwa kuja kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uzima usio kufa.
<scripture passage="iiTim 1:11" parsed="|2Tim|1|11|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.11" />
<sup>11</sup>Mungu amenichagua mimi niwe mtume na mwalimu kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema,
<scripture passage="iiTim 1:12" parsed="|2Tim|1|12|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.12" />
<sup>12</sup>nami nateseka mambo haya kwa sababu hiyo. Lakini niko bado timamu kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina hakika kwamba yeye aweza kukilinda salama kile alichonikabidhi, mpaka Siku ile.
<scripture passage="iiTim 1:13" parsed="|2Tim|1|13|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.13" />
<sup>13</sup>Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha, na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
<scripture passage="iiTim 1:14" parsed="|2Tim|1|14|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.14" />
<sup>14</sup>Jambo lile bora ulilokabidhiwa lilinde kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu.
<scripture passage="iiTim 1:15" parsed="|2Tim|1|15|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.15" />
<sup>15</sup>Kama unavyojua, watu wote mkoani Asia wameniacha, miongoni mwao wakiwa Fugelo na Hermogene.
<scripture passage="iiTim 1:16" parsed="|2Tim|1|16|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.16" />
<sup>16</sup>Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
<scripture passage="iiTim 1:17" parsed="|2Tim|1|17|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.17" />
<sup>17</sup>ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafuta kwa bidii mpaka akanipata.
<scripture passage="iiTim 1:18" parsed="|2Tim|1|18|0|0" osisRef="Bible:2Tim.1.18" />
<sup>18</sup>Bwana amjalie huruma katika Siku ile! Nawe wajua vizuri mengi aliyonifanyia huko Efeso.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Timothy 2" progress="81.46%" prev="iiTim.1" next="iiTim.3" id="iiTim.2">
<h3 id="iiTim.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iiTim.2-p1">
<scripture passage="iiTim 2:1" parsed="|2Tim|2|1|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.1" />
<sup>1</sup>Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika kuungana na Kristo Yesu.
<scripture passage="iiTim 2:2" parsed="|2Tim|2|2|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.2" />
<sup>2</sup>Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.
<scripture passage="iiTim 2:3" parsed="|2Tim|2|3|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.3" />
<sup>3</sup>Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo yesu.
<scripture passage="iiTim 2:4" parsed="|2Tim|2|4|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.4" />
<sup>4</sup>Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi.
<scripture passage="iiTim 2:5" parsed="|2Tim|2|5|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.5" />
<sup>5</sup>Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
<scripture passage="iiTim 2:6" parsed="|2Tim|2|6|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.6" />
<sup>6</sup>Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno.
<scripture passage="iiTim 2:7" parsed="|2Tim|2|7|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.7" />
<sup>7</sup>Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uyaelewe yote.
<scripture passage="iiTim 2:8" parsed="|2Tim|2|8|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.8" />
<sup>8</sup>Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri.
<scripture passage="iiTim 2:9" parsed="|2Tim|2|9|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.9" />
<sup>9</sup>Kwa sababu ya kuihubiri Habari Njema mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo,
<scripture passage="iiTim 2:10" parsed="|2Tim|2|10|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.10" />
<sup>10</sup>na hivyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.
<scripture passage="iiTim 2:11" parsed="|2Tim|2|11|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.11" />
<sup>11</sup>Usemi huu ni wa kweli: "Ikiwa tulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye.
<scripture passage="iiTim 2:12" parsed="|2Tim|2|12|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.12" />
<sup>12</sup>Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.
<scripture passage="iiTim 2:13" parsed="|2Tim|2|13|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.13" />
<sup>13</sup>Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubaki mwaminifu daima, maana yeye hawezi kujikana mwenyewe."
<scripture passage="iiTim 2:14" parsed="|2Tim|2|14|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.14" />
<sup>14</sup>Basi, wakumbushe watu wako mambo haya, na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
<scripture passage="iiTim 2:15" parsed="|2Tim|2|15|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.15" />
<sup>15</sup>Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake, na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.
<scripture passage="iiTim 2:16" parsed="|2Tim|2|16|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.16" />
<sup>16</sup>Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ya kipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu.
<scripture passage="iiTim 2:17" parsed="|2Tim|2|17|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.17" />
<sup>17</sup>Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto.
<scripture passage="iiTim 2:18" parsed="|2Tim|2|18|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.18" />
<sup>18</sup>Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
<scripture passage="iiTim 2:19" parsed="|2Tim|2|19|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.19" />
<sup>19</sup>Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: "Bwana anawafahamu wale walio wake," na "Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu."
<scripture passage="iiTim 2:20" parsed="|2Tim|2|20|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.20" />
<sup>20</sup>Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
<scripture passage="iiTim 2:21" parsed="|2Tim|2|21|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.21" />
<sup>21</sup>Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema.
<scripture passage="iiTim 2:22" parsed="|2Tim|2|22|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.22" />
<sup>22</sup>Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi.
<scripture passage="iiTim 2:23" parsed="|2Tim|2|23|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.23" />
<sup>23</sup>Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
<scripture passage="iiTim 2:24" parsed="|2Tim|2|24|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.24" />
<sup>24</sup>Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
<scripture passage="iiTim 2:25" parsed="|2Tim|2|25|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.25" />
<sup>25</sup>ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli.
<scripture passage="iiTim 2:26" parsed="|2Tim|2|26|0|0" osisRef="Bible:2Tim.2.26" />
<sup>26</sup>Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Timothy 3" progress="81.79%" prev="iiTim.2" next="iiTim.4" id="iiTim.3">
<h3 id="iiTim.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iiTim.3-p1">
<scripture passage="iiTim 3:1" parsed="|2Tim|3|1|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.1" />
<sup>1</sup>Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.
<scripture passage="iiTim 3:2" parsed="|2Tim|3|2|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.2" />
<sup>2</sup>watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu;
<scripture passage="iiTim 3:3" parsed="|2Tim|3|3|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.3" />
<sup>3</sup>watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema;
<scripture passage="iiTim 3:4" parsed="|2Tim|3|4|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.4" />
<sup>4</sup>watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
<scripture passage="iiTim 3:5" parsed="|2Tim|3|5|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.5" />
<sup>5</sup>Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.
<scripture passage="iiTim 3:6" parsed="|2Tim|3|6|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.6" />
<sup>6</sup>Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za kila aina;
<scripture passage="iiTim 3:7" parsed="|2Tim|3|7|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.7" />
<sup>7</sup>wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia ujuzi wa huo ukweli.
<scripture passage="iiTim 3:8" parsed="|2Tim|3|8|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.8" />
<sup>8</sup>Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose.
<scripture passage="iiTim 3:9" parsed="|2Tim|3|9|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.9" />
<sup>9</sup>Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
<scripture passage="iiTim 3:10" parsed="|2Tim|3|10|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.10" />
<sup>10</sup>Wewe lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, subira yangu,
<scripture passage="iiTim 3:11" parsed="|2Tim|3|11|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.11" />
<sup>11</sup>udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
<scripture passage="iiTim 3:12" parsed="|2Tim|3|12|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.12" />
<sup>12</sup>Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana na Kristo Yesu lazima adhulumiwe.
<scripture passage="iiTim 3:13" parsed="|2Tim|3|13|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.13" />
<sup>13</sup>Watu waovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi kwa kuwadanganya wengine na kudanganyika wao wenyewe.
<scripture passage="iiTim 3:14" parsed="|2Tim|3|14|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.14" />
<sup>14</sup>Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa, ukaukubali kabisa. Unawajua wale waliokuwa walimu wako.
<scripture passage="iiTim 3:15" parsed="|2Tim|3|15|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.15" />
<sup>15</sup>Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
<scripture passage="iiTim 3:16" parsed="|2Tim|3|16|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.16" />
<sup>16</sup>Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,
<scripture passage="iiTim 3:17" parsed="|2Tim|3|17|0|0" osisRef="Bible:2Tim.3.17" />
<sup>17</sup>ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendo jema.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Timothy 4" progress="82.00%" prev="iiTim.3" next="Titus" id="iiTim.4">
<h3 id="iiTim.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iiTim.4-p1">
<scripture passage="iiTim 4:1" parsed="|2Tim|4|1|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.1" />
<sup>1</sup>Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:
<scripture passage="iiTim 4:2" parsed="|2Tim|4|2|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.2" />
<sup>2</sup>hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote.
<scripture passage="iiTim 4:3" parsed="|2Tim|4|3|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.3" />
<sup>3</sup>Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.
<scripture passage="iiTim 4:4" parsed="|2Tim|4|4|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.4" />
<sup>4</sup>Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
<scripture passage="iiTim 4:5" parsed="|2Tim|4|5|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.5" />
<sup>5</sup>Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
<scripture passage="iiTim 4:6" parsed="|2Tim|4|6|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.6" />
<sup>6</sup>Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufariki kwangu umefika.
<scripture passage="iiTim 4:7" parsed="|2Tim|4|7|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.7" />
<sup>7</sup>Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
<scripture passage="iiTim 4:8" parsed="|2Tim|4|8|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.8" />
<sup>8</sup>Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
<scripture passage="iiTim 4:9" parsed="|2Tim|4|9|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.9" />
<sup>9</sup>Fanya bidii kuja kwangu karibuni.
<scripture passage="iiTim 4:10" parsed="|2Tim|4|10|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.10" />
<sup>10</sup>Dema ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia.
<scripture passage="iiTim 4:11" parsed="|2Tim|4|11|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.11" />
<sup>11</sup>Luka peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu.
<scripture passage="iiTim 4:12" parsed="|2Tim|4|12|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.12" />
<sup>12</sup>Nilimtuma Tukiko kule Efeso.
<scripture passage="iiTim 4:13" parsed="|2Tim|4|13|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.13" />
<sup>13</sup>Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa; niletee pia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi. ic
<scripture passage="iiTim 4:14" parsed="|2Tim|4|14|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.14" />
<sup>14</sup>Yule sonara aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa kufuatana na hayo matendo yake.
<scripture passage="iiTim 4:15" parsed="|2Tim|4|15|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.15" />
<sup>15</sup>Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.
<scripture passage="iiTim 4:16" parsed="|2Tim|4|16|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.16" />
<sup>16</sup>Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!
<scripture passage="iiTim 4:17" parsed="|2Tim|4|17|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.17" />
<sup>17</sup>Lakini, Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.
<scripture passage="iiTim 4:18" parsed="|2Tim|4|18|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.18" />
<sup>18</sup>Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika Utawala wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina.
<scripture passage="iiTim 4:19" parsed="|2Tim|4|19|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.19" />
<sup>19</sup>Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
<scripture passage="iiTim 4:20" parsed="|2Tim|4|20|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.20" />
<sup>20</sup>Erasto alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa sababu alikuwa mgonjwa.
<scripture passage="iiTim 4:21" parsed="|2Tim|4|21|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.21" />
<sup>21</sup>Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na Klaudia wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.
<scripture passage="iiTim 4:22" parsed="|2Tim|4|22|0|0" osisRef="Bible:2Tim.4.22" />
<sup>22</sup>Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Titus" progress="82.25%" prev="iiTim.4" next="Titus.1" id="Titus">
<h2 id="Titus-p0.1">Titus</h2>

<div3 title="Titus 1" progress="82.26%" prev="Titus" next="Titus.2" id="Titus.1">
<h3 id="Titus.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Titus.1-p1">
<scripture passage="Titus 1:1" parsed="|Titus|1|1|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo naandika. Mimi nimechaguliwa kuijenga imani ya wateule wa Mungu na kuwaongoza waufahamu ukweli wa dini yetu,
<scripture passage="Titus 1:2" parsed="|Titus|1|2|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.2" />
<sup>2</sup>ambayo msingi wake ni tumaini la kupata uzima wa milele. Mungu ambaye hasemi uongo, alituahidia uzima huo kabla ya mwanzo wa nyakati,
<scripture passage="Titus 1:3" parsed="|Titus|1|3|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.3" />
<sup>3</sup>na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo nuutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
<scripture passage="Titus 1:4" parsed="|Titus|1|4|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.4" />
<sup>4</sup>Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
<scripture passage="Titus 1:5" parsed="|Titus|1|5|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.5" />
<sup>5</sup>Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
<scripture passage="Titus 1:6" parsed="|Titus|1|6|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.6" />
<sup>6</sup>mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
<scripture passage="Titus 1:7" parsed="|Titus|1|7|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.7" />
<sup>7</sup>Maana kwa vile kiongozi wa kanisa ni mkurugenzi wa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na hatia. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mkorofi au mchoyo.
<scripture passage="Titus 1:8" parsed="|Titus|1|8|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.8" />
<sup>8</sup>Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
<scripture passage="Titus 1:9" parsed="|Titus|1|9|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.9" />
<sup>9</sup>Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho ya kweli na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
<scripture passage="Titus 1:10" parsed="|Titus|1|10|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.10" />
<sup>10</sup>Maana, wako watu wengi, hasa wale walioongoka kutoka dini ya Kiyahudi, ambao ni wakaidi, wanaowapotosha wengine kwa upumbavu wao.
<scripture passage="Titus 1:11" parsed="|Titus|1|11|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.11" />
<sup>11</sup>Lazima kukomesha maneno yao, kwani wanavuruga jumuiya nzima kwa kufundisha mambo ambayo hawapaswi kufundisha; wanafanya hivyo kwa nia mbaya ya kupata faida ya fedha.
<scripture passage="Titus 1:12" parsed="|Titus|1|12|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.12" />
<sup>12</sup>Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: "Wakrete, husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!"
<scripture passage="Titus 1:13" parsed="|Titus|1|13|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.13" />
<sup>13</sup>Naye alitoboa ukweli kwa sababu hiyo, unapaswa kuwakaripia vikali, ili wawe na imani kamilifu.
<scripture passage="Titus 1:14" parsed="|Titus|1|14|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.14" />
<sup>14</sup>Wasiendelee kushikilia hadithi tupu za Kiyahudi na maagizo ya kibinadamu yanayozuka kwa watu walioukataa ukweli.
<scripture passage="Titus 1:15" parsed="|Titus|1|15|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.15" />
<sup>15</sup>Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
<scripture passage="Titus 1:16" parsed="|Titus|1|16|0|0" osisRef="Bible:Titus.1.16" />
<sup>16</sup>Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
</p>
</div3>

<div3 title="Titus 2" progress="82.50%" prev="Titus.1" next="Titus.3" id="Titus.2">
<h3 id="Titus.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Titus.2-p1">
<scripture passage="Titus 2:1" parsed="|Titus|2|1|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.1" />
<sup>1</sup>Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho safi.
<scripture passage="Titus 2:2" parsed="|Titus|2|2|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.2" />
<sup>2</sup>Waambie wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu.
<scripture passage="Titus 2:3" parsed="|Titus|2|3|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.3" />
<sup>3</sup>Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi, au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema,
<scripture passage="Titus 2:4" parsed="|Titus|2|4|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.4" />
<sup>4</sup>ili wawazoeze kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto,
<scripture passage="Titus 2:5" parsed="|Titus|2|5|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.5" />
<sup>5</sup>wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.
<scripture passage="Titus 2:6" parsed="|Titus|2|6|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.6" />
<sup>6</sup>Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi.
<scripture passage="Titus 2:7" parsed="|Titus|2|7|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.7" />
<sup>7</sup>Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
<scripture passage="Titus 2:8" parsed="|Titus|2|8|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.8" />
<sup>8</sup>Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili adui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
<scripture passage="Titus 2:9" parsed="|Titus|2|9|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.9" />
<sup>9</sup>Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo yote. Wasibishane nao,
<scripture passage="Titus 2:10" parsed="|Titus|2|10|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.10" />
<sup>10</sup>au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonyesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.
<scripture passage="Titus 2:11" parsed="|Titus|2|11|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.11" />
<sup>11</sup>Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
<scripture passage="Titus 2:12" parsed="|Titus|2|12|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.12" />
<sup>12</sup>Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa,
<scripture passage="Titus 2:13" parsed="|Titus|2|13|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.13" />
<sup>13</sup>tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Titus 2:14" parsed="|Titus|2|14|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.14" />
<sup>14</sup>Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
<scripture passage="Titus 2:15" parsed="|Titus|2|15|0|0" osisRef="Bible:Titus.2.15" />
<sup>15</sup>Basi, fundisha mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
</p>
</div3>

<div3 title="Titus 3" progress="82.68%" prev="Titus.2" next="Phlm" id="Titus.3">
<h3 id="Titus.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Titus.3-p1">
<scripture passage="Titus 3:1" parsed="|Titus|3|1|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.1" />
<sup>1</sup>Wakumbushe watu kuwastahi watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila namna kutenda mambo yote mema.
<scripture passage="Titus 3:2" parsed="|Titus|3|2|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.2" />
<sup>2</sup>Waambie wasimtukane mtu yeyote; bali waishi kwa amani na masikizano, wawe daima wapole kwa kila mtu.
<scripture passage="Titus 3:3" parsed="|Titus|3|3|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.3" />
<sup>3</sup>Maana, wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu, wakaidi na wapotovu. Tulikuwa watumwa wa tamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha ya uovu na wivu; watu walituchukia nasi tukawachukia.
<scripture passage="Titus 3:4" parsed="|Titus|3|4|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.4" />
<sup>4</sup>Lakini wakati wema na upendo wa Mungu, Mwokozi wetu, ulipofunuliwa,
<scripture passage="Titus 3:5" parsed="|Titus|3|5|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.5" />
<sup>5</sup>alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
<scripture passage="Titus 3:6" parsed="|Titus|3|6|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.6" />
<sup>6</sup>Mungu alitumiminia Roho Mtakatifu bila kipimo kwa njia ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu,
<scripture passage="Titus 3:7" parsed="|Titus|3|7|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.7" />
<sup>7</sup>ili kwa neema yake tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na kuupokea uzima wa milele tunaoutumainia.
<scripture passage="Titus 3:8" parsed="|Titus|3|8|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.8" />
<sup>8</sup>Jambo hili ni kweli. Ninakutaka uyatilie mkazo mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu, wawe na hamu ya kuutumia wakati wao katika kutenda mema, ambayo ni mambo mazuri na ya manufaa kwa watu.
<scripture passage="Titus 3:9" parsed="|Titus|3|9|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.9" />
<sup>9</sup>Lakini jiepushe na ubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishano juu ya Sheria. Mambo hayo hayana faida yoyote na ni ya bure tu.
<scripture passage="Titus 3:10" parsed="|Titus|3|10|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.10" />
<sup>10</sup>Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye.
<scripture passage="Titus 3:11" parsed="|Titus|3|11|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.11" />
<sup>11</sup>Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake zathibitisha kwamba amekosea.
<scripture passage="Titus 3:12" parsed="|Titus|3|12|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.12" />
<sup>12</sup>Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.
<scripture passage="Titus 3:13" parsed="|Titus|3|13|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.13" />
<sup>13</sup>Jitahidi kumsaidia mwana sheria Zena na Apolo ili waweze kuanza ziara zao na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji.
<scripture passage="Titus 3:14" parsed="|Titus|3|14|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.14" />
<sup>14</sup>Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
<scripture passage="Titus 3:15" parsed="|Titus|3|15|0|0" osisRef="Bible:Titus.3.15" />
<sup>15</sup>Watu wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu katika imani. Nawatakieni nyote neema ya Mungu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Philemon" progress="82.88%" prev="Titus.3" next="Phlm.1" id="Phlm">
<h2 id="Phlm-p0.1">Philemon</h2>

<div3 title="Philemon 1" progress="82.88%" prev="Phlm" next="Heb" id="Phlm.1">
<h3 id="Phlm.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Phlm.1-p1">
<scripture passage="Phlm 1:1" parsed="|Phlm|1|1|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu
<scripture passage="Phlm 1:2" parsed="|Phlm|1|2|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.2" />
<sup>2</sup>na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkupo.
<scripture passage="Phlm 1:3" parsed="|Phlm|1|3|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.3" />
<sup>3</sup>Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo.
<scripture passage="Phlm 1:4" parsed="|Phlm|1|4|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.4" />
<sup>4</sup>Kila wakati ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu
<scripture passage="Phlm 1:5" parsed="|Phlm|1|5|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.5" />
<sup>5</sup>maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu.
<scripture passage="Phlm 1:6" parsed="|Phlm|1|6|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.6" />
<sup>6</sup>Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.
<scripture passage="Phlm 1:7" parsed="|Phlm|1|7|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.7" />
<sup>7</sup>Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.
<scripture passage="Phlm 1:8" parsed="|Phlm|1|8|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.8" />
<sup>8</sup>Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya.
<scripture passage="Phlm 1:9" parsed="|Phlm|1|9|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.9" />
<sup>9</sup>Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake.
<scripture passage="Phlm 1:10" parsed="|Phlm|1|10|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.10" />
<sup>10</sup>Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
<scripture passage="Phlm 1:11" parsed="|Phlm|1|11|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.11" />
<sup>11</sup>Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia.
<scripture passage="Phlm 1:12" parsed="|Phlm|1|12|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.12" />
<sup>12</sup>Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe.
<scripture passage="Phlm 1:13" parsed="|Phlm|1|13|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.13" />
<sup>13</sup>Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Habari Njema.
<scripture passage="Phlm 1:14" parsed="|Phlm|1|14|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.14" />
<sup>14</sup>Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako wewe mwenyewe na si kwa kulazimika.
<scripture passage="Phlm 1:15" parsed="|Phlm|1|15|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.15" />
<sup>15</sup>Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena kuwa naye daima.
<scripture passage="Phlm 1:16" parsed="|Phlm|1|16|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.16" />
<sup>16</sup>Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa: yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana.
<scripture passage="Phlm 1:17" parsed="|Phlm|1|17|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.17" />
<sup>17</sup>Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena kama vile ungenipokea mimi mwenyewe.
<scripture passage="Phlm 1:18" parsed="|Phlm|1|18|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.18" />
<sup>18</sup>Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako, basi, unidai mimi.
<scripture passage="Phlm 1:19" parsed="|Phlm|1|19|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.19" />
<sup>19</sup>Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: yako.)
<scripture passage="Phlm 1:20" parsed="|Phlm|1|20|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.20" />
<sup>20</sup>Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili ya jina la Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo.
<scripture passage="Phlm 1:21" parsed="|Phlm|1|21|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.21" />
<sup>21</sup>Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
<scripture passage="Phlm 1:22" parsed="|Phlm|1|22|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.22" />
<sup>22</sup>Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni.
<scripture passage="Phlm 1:23" parsed="|Phlm|1|23|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.23" />
<sup>23</sup>Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu.
<scripture passage="Phlm 1:24" parsed="|Phlm|1|24|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.24" />
<sup>24</sup>Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu, wanakusalimu.
<scripture passage="Phlm 1:25" parsed="|Phlm|1|25|0|0" osisRef="Bible:Phlm.1.25" />
<sup>25</sup>Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Hebrews" progress="83.15%" prev="Phlm.1" next="Heb.1" id="Heb">
<h2 id="Heb-p0.1">Hebrews</h2>

<div3 title="Hebrews 1" progress="83.15%" prev="Heb" next="Heb.2" id="Heb.1">
<h3 id="Heb.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Heb.1-p1">
<scripture passage="Heb 1:1" parsed="|Heb|1|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.1" />
<sup>1</sup>Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,
<scripture passage="Heb 1:2" parsed="|Heb|1|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.2" />
<sup>2</sup>lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu na akamteua avimiliki vitu vyote.
<scripture passage="Heb 1:3" parsed="|Heb|1|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.3" />
<sup>3</sup>Yeye ni mng`ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
<scripture passage="Heb 1:4" parsed="|Heb|1|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.4" />
<sup>4</sup>Mwana ni mkuu zaidi kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu zaidi kuliko jina lao.
<scripture passage="Heb 1:5" parsed="|Heb|1|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.5" />
<sup>5</sup>Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Wewe ni Mwanangu; Mimi leo nimekuwa Baba yako." Wala hakusema juu ya malaika yeyote: "Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu."
<scripture passage="Heb 1:6" parsed="|Heb|1|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.6" />
<sup>6</sup>Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, alisema: "Malaika wote wa Mungu wanapaswa kumwabudu."
<scripture passage="Heb 1:7" parsed="|Heb|1|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.7" />
<sup>7</sup>Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema: "Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa ndimi za moto."
<scripture passage="Heb 1:8" parsed="|Heb|1|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.8" />
<sup>8</sup>Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema: "Utawala wako ee Mungu, wadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
<scripture passage="Heb 1:9" parsed="|Heb|1|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.9" />
<sup>9</sup>Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa zaidi kuliko wenzako."
<scripture passage="Heb 1:10" parsed="|Heb|1|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.10" />
<sup>10</sup>Pia alisema: "Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako.
<scripture passage="Heb 1:11" parsed="|Heb|1|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.11" />
<sup>11</sup>Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi.
<scripture passage="Heb 1:12" parsed="|Heb|1|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.12" />
<sup>12</sup>Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma."
<scripture passage="Heb 1:13" parsed="|Heb|1|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.13" />
<sup>13</sup>Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako."
<scripture passage="Heb 1:14" parsed="|Heb|1|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.1.14" />
<sup>14</sup>Malaika ni roho tu wanaomtumikia Mungu, na Mungu huwatuma wawasaidie wale watakaopokea wokovu.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 2" progress="83.34%" prev="Heb.1" next="Heb.3" id="Heb.2">
<h3 id="Heb.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Heb.2-p1">
<scripture passage="Heb 2:1" parsed="|Heb|2|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.1" />
<sup>1</sup>Kwa sababu hiyo tunapaswa kuzingatia kwa makini zaidi yote tuliyosikia, ili tusije tukapotoshwa.
<scripture passage="Heb 2:2" parsed="|Heb|2|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.2" />
<sup>2</sup>Ujumbe ule waliopewa wazee wetu na malaika ulionyeshwa kuwa kweli, hata mtu yeyote ambaye hakuufuata au hakuutii aliadhibiwa kama alivyostahili.
<scripture passage="Heb 2:3" parsed="|Heb|2|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.3" />
<sup>3</sup>Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.
<scripture passage="Heb 2:4" parsed="|Heb|2|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.4" />
<sup>4</sup>Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu kadiri ya mapenzi yake.
<scripture passage="Heb 2:5" parsed="|Heb|2|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.5" />
<sup>5</sup>Mungu hakuwaweka malaika wautawale ulimwengu ujao, yaani ulimwengu ule tunaoongea habari zake.
<scripture passage="Heb 2:6" parsed="|Heb|2|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.6" />
<sup>6</sup>Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: "Mtu ni nini ee Mungu, hata umfikirie; mwanaadamu ni nini hata umjali?
<scripture passage="Heb 2:7" parsed="|Heb|2|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.7" />
<sup>7</sup>Ulimfanya kwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kuliko malaika; ukamvika taji ya utukufu na heshima,
<scripture passage="Heb 2:8" parsed="|Heb|2|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.8" />
<sup>8</sup>ukaweka kila kitu chini ya miguu yake, avitawale." Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote yaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.
<scripture passage="Heb 2:9" parsed="|Heb|2|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.9" />
<sup>9</sup>Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.
<scripture passage="Heb 2:10" parsed="|Heb|2|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.10" />
<sup>10</sup>Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye anayewaongoza kwenye wokovu.
<scripture passage="Heb 2:11" parsed="|Heb|2|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.11" />
<sup>11</sup>Yeye anawatakasa watu dhambi zao, naye pamoja na wale waliotakaswa, wote wanaye Baba mmoja. Ndiyo maana Yesu haoni aibu kuwaita hao ndugu zake;
<scripture passage="Heb 2:12" parsed="|Heb|2|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.12" />
<sup>12</sup>kama asemavyo: "Ee Mungu, nitawatangazia ndugu zangu matendo yako. Nitakusifu katika kusanyiko lao."
<scripture passage="Heb 2:13" parsed="|Heb|2|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.13" />
<sup>13</sup>Tena asema: "Nitamwekea Mungu tumaini langu." Na tena: "Mimi niko hapa pamoja na watoto alionipa Mungu."
<scripture passage="Heb 2:14" parsed="|Heb|2|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.14" />
<sup>14</sup>Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili kwa njia ya kifo chake amwangamize Ibilisi, ambaye ana mamlaka juu ya kifo,
<scripture passage="Heb 2:15" parsed="|Heb|2|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.15" />
<sup>15</sup>na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwa maisha yao yote kwa sababu ya hofu yao ya kifo.
<scripture passage="Heb 2:16" parsed="|Heb|2|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.16" />
<sup>16</sup>Maana ni wazi kwamba yeye hakuja kwa ajili ya kuwasaidia malaika, bali kama yasemavyo Maandiko; "Anawasaidia wazawa wa Abrahamu."
<scripture passage="Heb 2:17" parsed="|Heb|2|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.17" />
<sup>17</sup>Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe.
<scripture passage="Heb 2:18" parsed="|Heb|2|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.2.18" />
<sup>18</sup>Na, anaweza sasa kuwasaidia wale wanaojaribiwa na kuteswa.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 3" progress="83.61%" prev="Heb.2" next="Heb.4" id="Heb.3">
<h3 id="Heb.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Heb.3-p1">
<scripture passage="Heb 3:1" parsed="|Heb|3|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.1" />
<sup>1</sup>Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
<scripture passage="Heb 3:2" parsed="|Heb|3|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.2" />
<sup>2</sup>Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
<scripture passage="Heb 3:3" parsed="|Heb|3|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.3" />
<sup>3</sup>Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalika naye Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
<scripture passage="Heb 3:4" parsed="|Heb|3|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.4" />
<sup>4</sup>Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani--na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
<scripture passage="Heb 3:5" parsed="|Heb|3|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.5" />
<sup>5</sup>Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
<scripture passage="Heb 3:6" parsed="|Heb|3|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.6" />
<sup>6</sup>Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile tunachotumainia.
<scripture passage="Heb 3:7" parsed="|Heb|3|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.7" />
<sup>7</sup>Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
<scripture passage="Heb 3:8" parsed="|Heb|3|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.8" />
<sup>8</sup>msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu; kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,
<scripture passage="Heb 3:9" parsed="|Heb|3|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.9" />
<sup>9</sup>Huko wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, asema Bwana, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu kwa miaka arobaini.
<scripture passage="Heb 3:10" parsed="|Heb|3|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.10" />
<sup>10</sup>Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, `Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.`
<scripture passage="Heb 3:11" parsed="|Heb|3|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.11" />
<sup>11</sup>Basi, nilikasirika, nikaapa: `Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko."`
<scripture passage="Heb 3:12" parsed="|Heb|3|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.12" />
<sup>12</sup>Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
<scripture passage="Heb 3:13" parsed="|Heb|3|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.13" />
<sup>13</sup>Maadamu hiyo "Leo" inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
<scripture passage="Heb 3:14" parsed="|Heb|3|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.14" />
<sup>14</sup>Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
<scripture passage="Heb 3:15" parsed="|Heb|3|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.15" />
<sup>15</sup>Maandiko yasema hivi: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu."
<scripture passage="Heb 3:16" parsed="|Heb|3|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.16" />
<sup>16</sup>Ni akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
<scripture passage="Heb 3:17" parsed="|Heb|3|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.17" />
<sup>17</sup>Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
<scripture passage="Heb 3:18" parsed="|Heb|3|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.18" />
<sup>18</sup>Mungu alipoapa: "Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko," alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
<scripture passage="Heb 3:19" parsed="|Heb|3|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.3.19" />
<sup>19</sup>Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 4" progress="83.85%" prev="Heb.3" next="Heb.5" id="Heb.4">
<h3 id="Heb.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Heb.4-p1">
<scripture passage="Heb 4:1" parsed="|Heb|4|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.1" />
<sup>1</sup>Mungu alituahidia kwamba tutaweza kupata pumziko hilo alilosema. Basi, na tuogope ili yeyote kati yenu asije akashindwa kupata pumziko hilo.
<scripture passage="Heb 4:2" parsed="|Heb|4|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.2" />
<sup>2</sup>Maana Habari Njema imehubiriwa kwetu kama vile ilivyohubiriwa kwa hao watu wa kale. Lakini ujumbe huo haukuwafaa chochote, maana waliusikia lakini hawakuupokea kwa imani.
<scripture passage="Heb 4:3" parsed="|Heb|4|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.3" />
<sup>3</sup>Basi, sisi tunaoamini tunapata pumziko hilo aliloahidi Mungu. Kama alivyosema: "Nilikasirika, nikaapa: `Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko."` Mungu alisema hayo ingawa kazi yake ilikuwa imekwisha malizika tangu alipoumba ulimwengu.
<scripture passage="Heb 4:4" parsed="|Heb|4|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.4" />
<sup>4</sup>Maana Maandiko yasema mahali fulani kuhusu siku ya saba: "Mungu alipumzika siku ya saba, akaacha kazi zake zote."
<scripture passage="Heb 4:5" parsed="|Heb|4|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.5" />
<sup>5</sup>Tena jambo hili lasemwa pia: "Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko."
<scripture passage="Heb 4:6" parsed="|Heb|4|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.6" />
<sup>6</sup>Wale waliotangulia kuhubiriwa Habari Njema hawakupata pumziko hilo kwa sababu hawakuamini. Wapo, basi, wengine ambao wangejaliwa kulipata.
<scripture passage="Heb 4:7" parsed="|Heb|4|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.7" />
<sup>7</sup>Jambo hili ni wazi, kwani Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa "Leo". Miaka mingi baadaye Mungu alisema juu ya hiyo siku kwa maneno ya Daudi katika Maandiko yaliyokwisha tajwa: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu."
<scripture passage="Heb 4:8" parsed="|Heb|4|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.8" />
<sup>8</sup>Kama Yoshua angaliwapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
<scripture passage="Heb 4:9" parsed="|Heb|4|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.9" />
<sup>9</sup>Kwa hiyo, basi, bado lipo pumziko kwa watu wa Mungu kama kule kupumzika kwake Mungu siku ya saba.
<scripture passage="Heb 4:10" parsed="|Heb|4|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.10" />
<sup>10</sup>Maana, kila anayepata pumziko aliloahidi Mungu atapumzika baada ya kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika baada ya yake.
<scripture passage="Heb 4:11" parsed="|Heb|4|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.11" />
<sup>11</sup>Basi, tujitahidi kupata pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwenu atakayeshindwa, kama walivyofanya wao kwa sababu ya ukosefu wao wa imani.
<scripture passage="Heb 4:12" parsed="|Heb|4|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.12" />
<sup>12</sup>Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali zaidi kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na mafuta. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.
<scripture passage="Heb 4:13" parsed="|Heb|4|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.13" />
<sup>13</sup>Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake. Kwake, sisi sote tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu.
<scripture passage="Heb 4:14" parsed="|Heb|4|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.14" />
<sup>14</sup>Basi, tunapaswa kuzingatia kwa uthabiti imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka kwa Mungu mwenyewe--Yesu, Mwana wa Mungu.
<scripture passage="Heb 4:15" parsed="|Heb|4|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.15" />
<sup>15</sup>Huyu Kuhani Mkuu wetu si mmoja ambaye hawezi kutuunga mkono katika unyonge wetu, ila ni Kuhani Mkuu ambaye alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi.
<scripture passage="Heb 4:16" parsed="|Heb|4|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.4.16" />
<sup>16</sup>Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu, palipo na neema, ili tukajipatie huruma na neema ya kutusaidia wakati wa lazima.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 5" progress="84.11%" prev="Heb.4" next="Heb.6" id="Heb.5">
<h3 id="Heb.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Heb.5-p1">
<scripture passage="Heb 5:1" parsed="|Heb|5|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.1" />
<sup>1</sup>Kila kuhani mkuu huchaguliwa kutoka miongoni mwa watu kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa niaba yao, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi zao.
<scripture passage="Heb 5:2" parsed="|Heb|5|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.2" />
<sup>2</sup>Maadamu yeye mwenyewe yu dhaifu anaweza kuwaonea huruma wale wasiojua kitu na wanaofanya makosa.
<scripture passage="Heb 5:3" parsed="|Heb|5|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.3" />
<sup>3</sup>Na kwa vile yeye mwenyewe ni dhaifu, anapaswa kutolea dhabihu si tu kwa ajili ya watu, bali pia kwa ajili ya dhambi zake.
<scripture passage="Heb 5:4" parsed="|Heb|5|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.4" />
<sup>4</sup>Hakuna mtu awezaye kujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.
<scripture passage="Heb 5:5" parsed="|Heb|5|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.5" />
<sup>5</sup>Hali kadhalika naye Kristo hakujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani mkuu, bali Mungu alimwambia: "Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa baba yako."
<scripture passage="Heb 5:6" parsed="|Heb|5|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.6" />
<sup>6</sup>Alisema pia mahali pengine: "Wewe ni kuhani milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki."
<scripture passage="Heb 5:7" parsed="|Heb|5|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.7" />
<sup>7</sup>Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kutoka kifo; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu.
<scripture passage="Heb 5:8" parsed="|Heb|5|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.8" />
<sup>8</sup>Lakini, ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwa njia ya mateso.
<scripture passage="Heb 5:9" parsed="|Heb|5|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.9" />
<sup>9</sup>Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wale wote wanaomtii,
<scripture passage="Heb 5:10" parsed="|Heb|5|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.10" />
<sup>10</sup>naye Mungu akamteua kuwa kuhani mkuu kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
<scripture passage="Heb 5:11" parsed="|Heb|5|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.11" />
<sup>11</sup>Tunayo Mengi ya kusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumu kuwaelezeni, kwa sababu ninyi si wepesi wa kuelewa.
<scripture passage="Heb 5:12" parsed="|Heb|5|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.12" />
<sup>12</sup>Sasa mngalipaswa kuwa tayari walimu, lakini mnahitaji bado mtu wa kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo ya ujumbe wa Mungu. Badala ya kula chakula kigumu, mnapaswa bado kunywa maziwa.
<scripture passage="Heb 5:13" parsed="|Heb|5|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.13" />
<sup>13</sup>Kila anayepaswa kunywa maziwa huyo ni mtoto bado, hajui uadilifu ni nini.
<scripture passage="Heb 5:14" parsed="|Heb|5|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.5.14" />
<sup>14</sup>Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, ambao wanaweza kubainisha mema na mabaya.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 6" progress="84.29%" prev="Heb.5" next="Heb.7" id="Heb.6">
<h3 id="Heb.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Heb.6-p1">
<scripture passage="Heb 6:1" parsed="|Heb|6|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.1" />
<sup>1</sup>Basi, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa na kuyaacha nyuma yale mafundisho ya mwanzo ya Kikristo. Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa kurudia yale mafundisho ya mwanzo kama vile kuachana na matendo ya kifo, kumwamini Mungu;
<scripture passage="Heb 6:2" parsed="|Heb|6|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.2" />
<sup>2</sup>mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele.
<scripture passage="Heb 6:3" parsed="|Heb|6|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.3" />
<sup>3</sup>tusonge mbele! Hayo tutayafanya, Mungu akitujalia.
<scripture passage="Heb 6:4" parsed="|Heb|6|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.4" />
<sup>4</sup>Maana watu wanaoiasi imani yao inawezekanaje kuwarudisha watubu tena? Watu hao walikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu, walikwisha onja zawadi ya mbinguni na kushirikishwa Roho Mtakatifu;
<scripture passage="Heb 6:5" parsed="|Heb|6|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.5" />
<sup>5</sup>walikwisha onja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao,
<scripture passage="Heb 6:6" parsed="|Heb|6|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.6" />
<sup>6</sup>kisha wakaiasi imani yao! Haiwezekani kuwarudisha watubu tena, kwa sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu na kumwaibisha hadharani.
<scripture passage="Heb 6:7" parsed="|Heb|6|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.7" />
<sup>7</sup>Mungu huibariki ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima.
<scripture passage="Heb 6:8" parsed="|Heb|6|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.8" />
<sup>8</sup>Lakini kama ardhi hiyo ikiota miti ya miiba na magugu, haina faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto.
<scripture passage="Heb 6:9" parsed="|Heb|6|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.9" />
<sup>9</sup>Lakini, ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tunalo tumaini kubwa juu ya hali yenu. Tunajua kwamba mmepokea baraka zile bora za wokovu wenu.
<scripture passage="Heb 6:10" parsed="|Heb|6|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.10" />
<sup>10</sup>Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mlioonyesha kwa ajili ya jina lake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
<scripture passage="Heb 6:11" parsed="|Heb|6|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.11" />
<sup>11</sup>Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia.
<scripture passage="Heb 6:12" parsed="|Heb|6|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.12" />
<sup>12</sup>Msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu na hivyo wanapokea yake aliyoahidi Mungu.
<scripture passage="Heb 6:13" parsed="|Heb|6|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.13" />
<sup>13</sup>Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
<scripture passage="Heb 6:14" parsed="|Heb|6|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.14" />
<sup>14</sup>Mungu alisema: "Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi."
<scripture passage="Heb 6:15" parsed="|Heb|6|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.15" />
<sup>15</sup>Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo alipokea kile alichoahidiwa na Mungu.
<scripture passage="Heb 6:16" parsed="|Heb|6|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.16" />
<sup>16</sup>Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko wao, na kiapo hicho husuluhisha ubishi wote.
<scripture passage="Heb 6:17" parsed="|Heb|6|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.17" />
<sup>17</sup>Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonyesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake.
<scripture passage="Heb 6:18" parsed="|Heb|6|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.18" />
<sup>18</sup>Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
<scripture passage="Heb 6:19" parsed="|Heb|6|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.19" />
<sup>19</sup>Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo ni imara na thabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu la mbinguni mpaka patakatifu ndani.
<scripture passage="Heb 6:20" parsed="|Heb|6|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.6.20" />
<sup>20</sup>Yesu ametangulia kuingia humo kwa niaba yetu, na amekuwa kuhani mkuu milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 7" progress="84.55%" prev="Heb.6" next="Heb.8" id="Heb.7">
<h3 id="Heb.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Heb.7-p1">
<scripture passage="Heb 7:1" parsed="|Heb|7|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.1" />
<sup>1</sup>Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu. Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedeki alikutana naye akambariki,
<scripture passage="Heb 7:2" parsed="|Heb|7|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.2" />
<sup>2</sup>naye Abrahamu akampa sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina hili Melkisedeki ni "Mfalme wa Uadilifu"; na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya "Mfalme wa Amani.")
<scripture passage="Heb 7:3" parsed="|Heb|7|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.3" />
<sup>3</sup>Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi; haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na anaendelea kuwa kuhani daima.
<scripture passage="Heb 7:4" parsed="|Heb|7|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.4" />
<sup>4</sup>Basi, mwaona jinsi mtu huyu alivyokuwa maarufu. Baba Abrahamu alimpa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyoteka vitani.
<scripture passage="Heb 7:5" parsed="|Heb|7|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.5" />
<sup>5</sup>Tunajua vilevile kwamba kufuatana na Sheria, wana wa Lawi ambao ni makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu ya kumi kutoka kwa watu, yaani ndugu zao, ingawaje nao ni watoto wa Abrahamu.
<scripture passage="Heb 7:6" parsed="|Heb|7|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.6" />
<sup>6</sup>Lakini huyo Melkisedeki hakuwa wa ukoo wa Lawi, hata hivyo alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu; tena akambariki yeye ambaye alikuwa amepewa ahadi ya Mungu.
<scripture passage="Heb 7:7" parsed="|Heb|7|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.7" />
<sup>7</sup>Hakuna mashaka hata kidogo kwamba anayebariki ni mkuu zaidi kuliko yule anayebarikiwa.
<scripture passage="Heb 7:8" parsed="|Heb|7|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.8" />
<sup>8</sup>Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa; lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana kwamba hafi.
<scripture passage="Heb 7:9" parsed="|Heb|7|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.9" />
<sup>9</sup>Twaweza, basi, kusema kwamba Abrahamu alipotoa sehemu moja ya kumi, Lawi (ambaye watoto wake hupokea sehemu moja ya kumi) alitoa sehemu moja ya kumi pia.
<scripture passage="Heb 7:10" parsed="|Heb|7|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.10" />
<sup>10</sup>Maana Lawi hakuwa amezaliwa bado, bali ni kama alikuwa katika mwili wa baba yake, Abrahamu, wakati Melkisedeki alipokutana naye.
<scripture passage="Heb 7:11" parsed="|Heb|7|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.11" />
<sup>11</sup>Kutokana na ukuhani wa Walawi, watu wa Israeli walipewa Sheria. Sasa, kama huduma ya Walawi ingalikuwa kamilifu hapangekuwa tena na haja ya kutokea ukuhani mwingine tofauti, ukuhani ambao umefuata utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki, na si ule wa Aroni.
<scripture passage="Heb 7:12" parsed="|Heb|7|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.12" />
<sup>12</sup>Maana ukuhani ukibadilika ni lazima Sheria nayo ibadilike.
<scripture passage="Heb 7:13" parsed="|Heb|7|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.13" />
<sup>13</sup>Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake, alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
<scripture passage="Heb 7:14" parsed="|Heb|7|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.14" />
<sup>14</sup>Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.
<scripture passage="Heb 7:15" parsed="|Heb|7|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.15" />
<sup>15</sup>Tena jambo hili ni dhahiri zaidi: kuhani mwingine anayefanana na Melkisedeki amekwisha tokea.
<scripture passage="Heb 7:16" parsed="|Heb|7|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.16" />
<sup>16</sup>Yeye hakufanywa kuwa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
<scripture passage="Heb 7:17" parsed="|Heb|7|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.17" />
<sup>17</sup>Maana Maandiko yasema: "Wewe ni kuhani milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki."
<scripture passage="Heb 7:18" parsed="|Heb|7|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.18" />
<sup>18</sup>Basi, ile amri ya zamani ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyofaa kitu.
<scripture passage="Heb 7:19" parsed="|Heb|7|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.19" />
<sup>19</sup>Maana Sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu.
<scripture passage="Heb 7:20" parsed="|Heb|7|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.20" />
<sup>20</sup>Zaidi ya hayo hapa pana kiapo cha Mungu. Wakati wale wengine walipofanywa makuhani hapakuwako kiapo.
<scripture passage="Heb 7:21" parsed="|Heb|7|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.21" />
<sup>21</sup>Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: "Bwana ameapa, wala hataigeuza nia yake: `Wewe ni kuhani milele."`
<scripture passage="Heb 7:22" parsed="|Heb|7|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.22" />
<sup>22</sup>Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
<scripture passage="Heb 7:23" parsed="|Heb|7|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.23" />
<sup>23</sup>Kuna tofauti nyingine pia: hao makuhani wengine walikuwa wengi kwa sababu walikufa na hawakuweza kuendelea na kazi yao.
<scripture passage="Heb 7:24" parsed="|Heb|7|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.24" />
<sup>24</sup>Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake hauondoki kwake.
<scripture passage="Heb 7:25" parsed="|Heb|7|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.25" />
<sup>25</sup>Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.
<scripture passage="Heb 7:26" parsed="|Heb|7|26|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.26" />
<sup>26</sup>Basi, Yesu ndiye Kuhani Mkuu ambaye anatufaa sana katika mahitaji yetu. Yeye ni mtakatifu, hana hatia wala dhambi ndani yake; hayumo katika kundi la wenye dhambi na ameinuliwa mpaka juu mbinguni.
<scripture passage="Heb 7:27" parsed="|Heb|7|27|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.27" />
<sup>27</sup>Yeye si kama wale makuhani wakuu wengine; hana haja ya kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za watu. Yeye alifanya hivyo mara moja tu wakati alipojitoa yeye mwenyewe, na hiyo yatosha kwa nyakati zote.
<scripture passage="Heb 7:28" parsed="|Heb|7|28|0|0" osisRef="Bible:Heb.7.28" />
<sup>28</sup>Sheria ya Mose huwateua watu waliokuwa dhaifu kuwa makuhani wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 8" progress="84.98%" prev="Heb.7" next="Heb.9" id="Heb.8">
<h3 id="Heb.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Heb.8-p1">
<scripture passage="Heb 8:1" parsed="|Heb|8|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.1" />
<sup>1</sup>Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: sisi tunaye Kuhani Mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu mbinguni.
<scripture passage="Heb 8:2" parsed="|Heb|8|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.2" />
<sup>2</sup>Yeye hutoa huduma ya Kuhani Mkuu katika Mahali Patakatifu sana, yaani ndani ya ile hema ya kweli iliyojengwa na Bwana, siyo na binadamu. ic
<scripture passage="Heb 8:3" parsed="|Heb|8|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.3" />
<sup>3</sup>Kila Kuhani Mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu vipawa na dhabihu, na hivyo Kuhani Mkuu wetu lazima pia awe na kitu cha kutolea.
<scripture passage="Heb 8:4" parsed="|Heb|8|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.4" />
<sup>4</sup>Kama yeye angekuwa wa hapa duninani, asingekuwa kamwe kuhani, kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na Sheria.
<scripture passage="Heb 8:5" parsed="|Heb|8|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.5" />
<sup>5</sup>Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Ndivyo pia ilivyokuwa kwa Mose. Wakati alipokuwa karibu kuitengeneza ile hema, Mungu alimwambia: "Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani."
<scripture passage="Heb 8:6" parsed="|Heb|8|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.6" />
<sup>6</sup>Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.
<scripture passage="Heb 8:7" parsed="|Heb|8|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.7" />
<sup>7</sup>Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili.
<scripture passage="Heb 8:8" parsed="|Heb|8|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.8" />
<sup>8</sup>Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema: "Siku zinakuja, asema Bwana, ambapo nitafanya agano jipya na watu wa Israeli na kabila la Yuda.
<scripture passage="Heb 8:9" parsed="|Heb|8|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.9" />
<sup>9</sup>Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao siku ile nilipowaongoza kwa mkono kutoka nchi ya Misri. Hawakuwa waaminifu kwa agano langu; na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
<scripture passage="Heb 8:10" parsed="|Heb|8|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.10" />
<sup>10</sup>Na hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
<scripture passage="Heb 8:11" parsed="|Heb|8|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.11" />
<sup>11</sup>Hakuna mtu atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: `Mjue Bwana.` Maana watu wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
<scripture passage="Heb 8:12" parsed="|Heb|8|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.12" />
<sup>12</sup>Nitawasamehe makosa yao, wala sitakumbuka tena dhambi zao."
<scripture passage="Heb 8:13" parsed="|Heb|8|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.8.13" />
<sup>13</sup>Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 9" progress="85.18%" prev="Heb.8" next="Heb.10" id="Heb.9">
<h3 id="Heb.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Heb.9-p1">
<scripture passage="Heb 9:1" parsed="|Heb|9|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.1" />
<sup>1</sup>Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na pia mahali patakatifu pa ibada palipojengwa na watu.
<scripture passage="Heb 9:2" parsed="|Heb|9|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.2" />
<sup>2</sup>Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyotolewa kwa Mungu.
<scripture passage="Heb 9:3" parsed="|Heb|9|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.3" />
<sup>3</sup>Nyuma ya pazia la pili, kulikuwa na hema iliyoitwa Mahali Patakatifu Kupita Pote.
<scripture passage="Heb 9:4" parsed="|Heb|9|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.4" />
<sup>4</sup>Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani, na Sanduku la Agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana; fimbo ya Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vilivyoandikwa agano.
<scripture passage="Heb 9:5" parsed="|Heb|9|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.5" />
<sup>5</sup>Juu ya hilo Sanduku kulikuwa na viumbe vilivyodhihirisha kuweko kwa Mungu, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa. Lakini sasa, hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.
<scripture passage="Heb 9:6" parsed="|Heb|9|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.6" />
<sup>6</sup>Mipango hiyo ilitekelezwa kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
<scripture passage="Heb 9:7" parsed="|Heb|9|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.7" />
<sup>7</sup>Lakini kuhani Mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka. Anapoingia ndani huwa amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi ambazo watu wamezitenda bila wao wenyewe kujua.
<scripture passage="Heb 9:8" parsed="|Heb|9|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.8" />
<sup>8</sup>Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali Patakatifu haijafunguliwa.
<scripture passage="Heb 9:9" parsed="|Heb|9|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.9" />
<sup>9</sup>Jambo hili ni mfano wa nyakati za sasa. Linaonyesha kwamba zawadi na dhabihu zinazotolewa kwa Mungu haziwezi kuifanya mioyo ya wale wanaoabudu kuwa mikamilifu,
<scripture passage="Heb 9:10" parsed="|Heb|9|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.10" />
<sup>10</sup>kwani haya yote yanahusika na vyakula, vinywaji na taratibu mbalimbali za kutawadha. Yote hayo ni maagizo ya njenje tu; na nguvu yake hukoma wakati Mungu atakaporekebisha vitu vyote.
<scripture passage="Heb 9:11" parsed="|Heb|9|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.11" />
<sup>11</sup>Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa Kuhani Mkuu wa mambo yaliyo mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.
<scripture passage="Heb 9:12" parsed="|Heb|9|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.12" />
<sup>12</sup>Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa amechukua damu ya mbuzi wala ng`ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele.
<scripture passage="Heb 9:13" parsed="|Heb|9|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.13" />
<sup>13</sup>Watu waliokuwa najisi kidini waliweza kutakasika na kuwa safi waliponyunyiziwa damu ya mbuzi na ya ng`ombe pamoja na majivu ya ndama.
<scripture passage="Heb 9:14" parsed="|Heb|9|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.14" />
<sup>14</sup>Lakini, kwa damu ya Kristo, mambo makuu zaidi hufanyika! Kwa nguvu za Roho wa milele, Kristo alijitolea mwenyewe dhabihu kamilifu kwa Mungu. Damu yake itatutakasa dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo kifo, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai.
<scripture passage="Heb 9:15" parsed="|Heb|9|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.15" />
<sup>15</sup>Kwa hiyo, Kristo ndiye aliyeratibisha agano jipya ili wale walioitwa na Mungu wazipokee baraka za milele walizoahidiwa. Watazipata, kwani kifo kimetokea ambacho huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.
<scripture passage="Heb 9:16" parsed="|Heb|9|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.16" />
<sup>16</sup>Kwa kawaida wosia hutambuliwa tu kama kifo cha yule aliyeufanya huo wosia kimethibitishwa.
<scripture passage="Heb 9:17" parsed="|Heb|9|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.17" />
<sup>17</sup>Wosia hauwezi kutekelezwa mpaka kumetokea kifo, kwani wosia hauna maana ikiwa mwenye kuufanya bado anaishi.
<scripture passage="Heb 9:18" parsed="|Heb|9|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.18" />
<sup>18</sup>Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa.
<scripture passage="Heb 9:19" parsed="|Heb|9|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.19" />
<sup>19</sup>Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa katika Sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa kutumia majani ya mti uitwao husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia kile kitabu cha Sheria na hao watu wote.
<scripture passage="Heb 9:20" parsed="|Heb|9|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.20" />
<sup>20</sup>Mose alisema: "Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na Mungu mlitii."
<scripture passage="Heb 9:21" parsed="|Heb|9|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.21" />
<sup>21</sup>Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada.
<scripture passage="Heb 9:22" parsed="|Heb|9|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.22" />
<sup>22</sup>Naam, kadiri ya Sheria karibu kila kitu chaweza kutakaswa kwa damu, na dhambi nazo zaondolewa tu ikiwa damu imemwagwa.
<scripture passage="Heb 9:23" parsed="|Heb|9|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.23" />
<sup>23</sup>Vitu hivi ambavyo ni mfano tu wa mambo halisi ya mbinguni, vililazimika kutakaswa kwa namna hiyo. Lakini vitu vya mbinguni huhitaji dhabihu iliyo bora zaidi.
<scripture passage="Heb 9:24" parsed="|Heb|9|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.24" />
<sup>24</sup>Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.
<scripture passage="Heb 9:25" parsed="|Heb|9|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.25" />
<sup>25</sup>Kuhani Mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka akiwa amechukua damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe mwenyewe mara nyingi,
<scripture passage="Heb 9:26" parsed="|Heb|9|26|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.26" />
<sup>26</sup>maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu, kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe dhabihu.
<scripture passage="Heb 9:27" parsed="|Heb|9|27|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.27" />
<sup>27</sup>Basi, kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu,
<scripture passage="Heb 9:28" parsed="|Heb|9|28|0|0" osisRef="Bible:Heb.9.28" />
<sup>28</sup>vivyo hivyo Kristo naye alijitoa dhabihu mara moja tu kwa ajili ya kuziondoa dhambi za wengi. Atakapotokea mara ya pili si kwa ajili ya kupambana na dhambi, bali ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomngojea.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 10" progress="85.66%" prev="Heb.9" next="Heb.11" id="Heb.10">
<h3 id="Heb.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Heb.10-p1">
<scripture passage="Heb 10:1" parsed="|Heb|10|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.1" />
<sup>1</sup>Sheria ya Wayahudi si picha kamili ya mambo yale halisi: ni kivuli tu cha mema yanayokuja. Dhabihu zilezile hutolewa daima, mwaka baada ya mwaka. Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihu hizo, kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu?
<scripture passage="Heb 10:2" parsed="|Heb|10|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.2" />
<sup>2</sup>Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na dhabihu hizo zote zingekoma.
<scripture passage="Heb 10:3" parsed="|Heb|10|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.3" />
<sup>3</sup>Lakini dhabihu hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao.
<scripture passage="Heb 10:4" parsed="|Heb|10|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.4" />
<sup>4</sup>Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
<scripture passage="Heb 10:5" parsed="|Heb|10|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.5" />
<sup>5</sup>Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu: "Hukutaka dhabihu wala sadaka, lakini umenitayarishia mwili.
<scripture passage="Heb 10:6" parsed="|Heb|10|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.6" />
<sup>6</sup>Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.
<scripture passage="Heb 10:7" parsed="|Heb|10|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.7" />
<sup>7</sup>Hapo nikasema: `Niko hapa ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha Sheria."`
<scripture passage="Heb 10:8" parsed="|Heb|10|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.8" />
<sup>8</sup>Kwanza alisema: "Hutaki, wala hupendezwi na dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi." Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na Sheria.
<scripture passage="Heb 10:9" parsed="|Heb|10|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.9" />
<sup>9</sup>Kisha akasema: "Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako." Hivyo Mungu alibatilisha dhabihu za zamani na mahali pake akaweka dhabihu nyingine moja.
<scripture passage="Heb 10:10" parsed="|Heb|10|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.10" />
<sup>10</sup>Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza mapenzi ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile dhabihu ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha.
<scripture passage="Heb 10:11" parsed="|Heb|10|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.11" />
<sup>11</sup>Kila kuhani Myahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoa dhabibu zilezile mara nyingi, dhabibu ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
<scripture passage="Heb 10:12" parsed="|Heb|10|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.12" />
<sup>12</sup>Lakini Kristo alitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi, dhabihu ifaayo milele, kisha akaketi upande wa kulia wa Mungu.
<scripture passage="Heb 10:13" parsed="|Heb|10|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.13" />
<sup>13</sup>Huko anangoja mpaka adui zake watakapowekwa kama kibao chini ya miguu yake.
<scripture passage="Heb 10:14" parsed="|Heb|10|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.14" />
<sup>14</sup>Basi, kwa dhabihu yake moja tu, amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wanaotakaswa dhambi zao.
<scripture passage="Heb 10:15" parsed="|Heb|10|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.15" />
<sup>15</sup>Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:
<scripture passage="Heb 10:16" parsed="|Heb|10|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.16" />
<sup>16</sup>"Hili ndilo agano nitakalofanya nao, katika siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao."
<scripture passage="Heb 10:17" parsed="|Heb|10|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.17" />
<sup>17</sup>Kisha akaongeza kusema: "Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendo vyao vya uhalifu."
<scripture passage="Heb 10:18" parsed="|Heb|10|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.18" />
<sup>18</sup>Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa dhabihu za kuondoa dhambi.
<scripture passage="Heb 10:19" parsed="|Heb|10|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.19" />
<sup>19</sup>Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu.
<scripture passage="Heb 10:20" parsed="|Heb|10|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.20" />
<sup>20</sup>Yeye ametufungulia njia mpya na yenye uzima kupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wake mwenyewe.
<scripture passage="Heb 10:21" parsed="|Heb|10|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.21" />
<sup>21</sup>Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu.
<scripture passage="Heb 10:22" parsed="|Heb|10|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.22" />
<sup>22</sup>Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.
<scripture passage="Heb 10:23" parsed="|Heb|10|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.23" />
<sup>23</sup>Tushikilie imara tumaini lile tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu.
<scripture passage="Heb 10:24" parsed="|Heb|10|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.24" />
<sup>24</sup>Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema.
<scripture passage="Heb 10:25" parsed="|Heb|10|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.25" />
<sup>25</sup>Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, Siku ile ya Bwana inakaribia.
<scripture passage="Heb 10:26" parsed="|Heb|10|26|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.26" />
<sup>26</sup>Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna dhabihu iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi.
<scripture passage="Heb 10:27" parsed="|Heb|10|27|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.27" />
<sup>27</sup>Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.
<scripture passage="Heb 10:28" parsed="|Heb|10|28|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.28" />
<sup>28</sup>Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawa bila ya huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
<scripture passage="Heb 10:29" parsed="|Heb|10|29|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.29" />
<sup>29</sup>Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?
<scripture passage="Heb 10:30" parsed="|Heb|10|30|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.30" />
<sup>30</sup>Maana tunamfahamu yule aliyesema, "Mimi nitalipiza kisasi, mimi nitalipiza," na ambaye alisema pia, "Bwana atawahukumu watu wake."
<scripture passage="Heb 10:31" parsed="|Heb|10|31|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.31" />
<sup>31</sup>Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!
<scripture passage="Heb 10:32" parsed="|Heb|10|32|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.32" />
<sup>32</sup>Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, ninyi mlistahimili.
<scripture passage="Heb 10:33" parsed="|Heb|10|33|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.33" />
<sup>33</sup>Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo.
<scripture passage="Heb 10:34" parsed="|Heb|10|34|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.34" />
<sup>34</sup>Mlishiriki mateso ya wafungwa, na mliponyang`anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
<scripture passage="Heb 10:35" parsed="|Heb|10|35|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.35" />
<sup>35</sup>Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa.
<scripture passage="Heb 10:36" parsed="|Heb|10|36|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.36" />
<sup>36</sup>Mnahitaji kuwa na uvumilivu, ili mweze kufanya anayotaka Mungu na kupokea kile alichoahidi.
<scripture passage="Heb 10:37" parsed="|Heb|10|37|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.37" />
<sup>37</sup>Maana kama yasemavyo Maandiko: "Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.
<scripture passage="Heb 10:38" parsed="|Heb|10|38|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.38" />
<sup>38</sup>Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi; walakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye."
<scripture passage="Heb 10:39" parsed="|Heb|10|39|0|0" osisRef="Bible:Heb.10.39" />
<sup>39</sup>Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tunaamini na tunaokolewa.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 11" progress="86.12%" prev="Heb.10" next="Heb.12" id="Heb.11">
<h3 id="Heb.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Heb.11-p1">
<scripture passage="Heb 11:1" parsed="|Heb|11|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.1" />
<sup>1</sup>Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.
<scripture passage="Heb 11:2" parsed="|Heb|11|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.2" />
<sup>2</sup>Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya imani yao.
<scripture passage="Heb 11:3" parsed="|Heb|11|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.3" />
<sup>3</sup>Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
<scripture passage="Heb 11:4" parsed="|Heb|11|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.4" />
<sup>4</sup>Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu iliyokuwa bora zaidi kuliko ile ya Kaini. Kwa imani yake alikubaliwa na Mungu kuwa mwadilifu; Mungu mwenyewe alizikubali sadaka zake. Kwa imani yake ingawa amekufa, bado ananena.
<scripture passage="Heb 11:5" parsed="|Heb|11|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.5" />
<sup>5</sup>Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
<scripture passage="Heb 11:6" parsed="|Heb|11|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.6" />
<sup>6</sup>Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.
<scripture passage="Heb 11:7" parsed="|Heb|11|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.7" />
<sup>7</sup>Kwa imani Noa alionywa na Mungu juu ya mambo ya baadaye ambayo hakuweza kuyaona bado. Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamo aliokolewa yeye pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo ulimwengu ulihukumiwa, naye Noa akapokea uadilifu unaotokana na imani.
<scripture passage="Heb 11:8" parsed="|Heb|11|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.8" />
<sup>8</sup>Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
<scripture passage="Heb 11:9" parsed="|Heb|11|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.9" />
<sup>9</sup>Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
<scripture passage="Heb 11:10" parsed="|Heb|11|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.10" />
<sup>10</sup>Maana Abrahamu alikuwa akingojea mji wenye misingi imara, mji ambao Mungu mwenyewe ndiye fundi aliyeubuni na kuujenga.
<scripture passage="Heb 11:11" parsed="|Heb|11|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.11" />
<sup>11</sup>Kwa imani hata Sara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake, kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimba ingawaje alikuwa amepita umri.
<scripture passage="Heb 11:12" parsed="|Heb|11|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.12" />
<sup>12</sup>Kwa hiyo, kutoka katika mtu huyo mmoja, Abrahamu, ambaye alikuwa kama amekufa, walitokea watu wengi wasiohesabika kama vile nyota za mbinguni na mchanga wa pwani.
<scripture passage="Heb 11:13" parsed="|Heb|11|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.13" />
<sup>13</sup>Watu hawa wote walikufa wakiwa na imani. Walikufa kabla ya kupokea mambo ambayo Mungu alikuwa ameahidi, lakini kwa mbali waliyaona, wakashangilia, na kukiri wazi kwamba wao walikuwa wageni na wakimbizi duniani.
<scripture passage="Heb 11:14" parsed="|Heb|11|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.14" />
<sup>14</sup>Watu wanaosema mambo kama hayo, huonyesha wazi kwamba wanaitafuta nchi yao wenyewe.
<scripture passage="Heb 11:15" parsed="|Heb|11|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.15" />
<sup>15</sup>Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko.
<scripture passage="Heb 11:16" parsed="|Heb|11|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.16" />
<sup>16</sup>Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndiyo maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.
<scripture passage="Heb 11:17" parsed="|Heb|11|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.17" />
<sup>17</sup>Kwa imani, Abrahamu alimtoa mwanae Isaka sadaka wakati Mungu alipomjaribu. Huyo Abrahamu ndiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu, lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa dhabihu mwanae wa pekee,
<scripture passage="Heb 11:18" parsed="|Heb|11|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.18" />
<sup>18</sup>ingawa Mungu alikuwa amemwambia: "Wazawa wako watatokana na Isaka."
<scripture passage="Heb 11:19" parsed="|Heb|11|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.19" />
<sup>19</sup>Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu: na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanae kutoka wafu.
<scripture passage="Heb 11:20" parsed="|Heb|11|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.20" />
<sup>20</sup>Kwa imani Isaka aliwabariki Yakobo na Esau, wapate baraka zitakazokuja baadaye.
<scripture passage="Heb 11:21" parsed="|Heb|11|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.21" />
<sup>21</sup>Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ile fimbo yake.
<scripture passage="Heb 11:22" parsed="|Heb|11|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.22" />
<sup>22</sup>Kwa imani Yosefu alipokuwa karibu kufa, alinena juu ya kutoka kwa Waisraeli katika nchi ya Misri, na pia akawaachia maagizo kuhusu mifupa yake.
<scripture passage="Heb 11:23" parsed="|Heb|11|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.23" />
<sup>23</sup>Kwa imani wazazi wa Mose walimficha huyo mtoto kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuzaliwa kwake. Walimwona kuwa ni mtoto mzuri, wala hawakuiogopa amri ya mfalme.
<scripture passage="Heb 11:24" parsed="|Heb|11|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.24" />
<sup>24</sup>Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao.
<scripture passage="Heb 11:25" parsed="|Heb|11|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.25" />
<sup>25</sup>Aliona ni afadhali kuteseka pamoja na watu wa Mungu kuliko kufurahia raha ya dhambi kwa kitambo kidogo.
<scripture passage="Heb 11:26" parsed="|Heb|11|26|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.26" />
<sup>26</sup>Alitambua kwamba kuteseka kwa ajili ya Masiha kuna faida kubwa zaidi kuliko utajiri wote wa nchi ya Misri, maana alikuwa anatazamia tuzo la baadaye.
<scripture passage="Heb 11:27" parsed="|Heb|11|27|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.27" />
<sup>27</sup>Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
<scripture passage="Heb 11:28" parsed="|Heb|11|28|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.28" />
<sup>28</sup>Kwa imani aliadhimisha siku ya Pasaka, akaamuru damu inyunyizwe juu ya milango, ili yule Malaika Mwangamizi asiwaue wazaliwa wa kwanza wa Israeli.
<scripture passage="Heb 11:29" parsed="|Heb|11|29|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.29" />
<sup>29</sup>Kwa imani watu wa Israeli walivuka bahari ya Shamu, kana kwamba ilikuwa nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo walikufa maji.
<scripture passage="Heb 11:30" parsed="|Heb|11|30|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.30" />
<sup>30</sup>Kwa imani kuta za mji wa Yeriko zilianguka watu wa Israeli walipokwisha zunguka kwa muda wa siku saba.
<scripture passage="Heb 11:31" parsed="|Heb|11|31|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.31" />
<sup>31</sup>Kwa imani Rahabu aliyekuwa malaya hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa sababu aliwakaribisha wale wapelelezi.
<scripture passage="Heb 11:32" parsed="|Heb|11|32|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.32" />
<sup>32</sup>Basi, niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kueleza juu ya Gedeoni, Baraki, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii.
<scripture passage="Heb 11:33" parsed="|Heb|11|33|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.33" />
<sup>33</sup>Kwa imani hawa wote walipigana vita na wafalme, wakashinda. Walitenda mambo adili, wakapokea yale aliyoahidi Mungu. Walifunga vinywa vya simba,
<scripture passage="Heb 11:34" parsed="|Heb|11|34|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.34" />
<sup>34</sup>Walizima mioto mikali, waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini walipata nguvu. Walikuwa hodari katika vita wakashinda majeshi ya kigeni.
<scripture passage="Heb 11:35" parsed="|Heb|11|35|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.35" />
<sup>35</sup>Na, wanawake walioamini walirudishiwa wafu wao wakiwa wamefufuliwa. Baadhi yao walikataa kufunguliwa, wakateswa mpaka kufa ili wapate kufufuliwa na kuingia katika maisha bora zaidi.
<scripture passage="Heb 11:36" parsed="|Heb|11|36|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.36" />
<sup>36</sup>Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani.
<scripture passage="Heb 11:37" parsed="|Heb|11|37|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.37" />
<sup>37</sup>Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi, walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
<scripture passage="Heb 11:38" parsed="|Heb|11|38|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.38" />
<sup>38</sup>Ulimwengu haukustahili kuwa na watu hao. Walitangatanga jangwani na mlimani, wakaishi katika mashimo na mapango ya ardhi.
<scripture passage="Heb 11:39" parsed="|Heb|11|39|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.39" />
<sup>39</sup>Watu hawa wote walionekana kuwa mashujaa kwa sababu ya imani yao. Hata hivyo, hawakupokea yale ambayo Mungu aliwaahidia,
<scripture passage="Heb 11:40" parsed="|Heb|11|40|0|0" osisRef="Bible:Heb.11.40" />
<sup>40</sup>maana Mungu alikuwa ameazimia mpango ulio bora zaidi kwa ajili yetu; yaani wao wangeufikia ukamilifu wakiwa pamoja nasi.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 12" progress="86.71%" prev="Heb.11" next="Heb.13" id="Heb.12">
<h3 id="Heb.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Heb.12-p1">
<scripture passage="Heb 12:1" parsed="|Heb|12|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.1" />
<sup>1</sup>Sisi tunalo kundi hili kubwa la mashahidi mbele yetu. Kwa hiyo tuondoe kila kizuizi kinachotuzuia, na dhambi ile inayotung`ang`ania. Tupige mbio kwa uvumilivu katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu.
<scripture passage="Heb 12:2" parsed="|Heb|12|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.2" />
<sup>2</sup>Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kujali juu ya aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
<scripture passage="Heb 12:3" parsed="|Heb|12|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.3" />
<sup>3</sup>Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate tamaa.
<scripture passage="Heb 12:4" parsed="|Heb|12|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.4" />
<sup>4</sup>Maana katika kupambana na dhambi, ninyi hamjapigana mpaka kiasi cha kumwaga damu yenu.
<scripture passage="Heb 12:5" parsed="|Heb|12|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.5" />
<sup>5</sup>Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja ninyi kuwa wanawe? "Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
<scripture passage="Heb 12:6" parsed="|Heb|12|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.6" />
<sup>6</sup>Maana Bwana humwadhibu kila anayempenda, humpinga kila anayekubali kuwa mwanae."
<scripture passage="Heb 12:7" parsed="|Heb|12|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.7" />
<sup>7</sup>Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea ninyi kama wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake?
<scripture passage="Heb 12:8" parsed="|Heb|12|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.8" />
<sup>8</sup>Lakini msipoadhibiwa kama wana wengine, basi, ninyi si wanawe, bali ni wana haramu.
<scripture passage="Heb 12:9" parsed="|Heb|12|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.9" />
<sup>9</sup>Zaidi ya hayo sisi tunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hata wanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidi Baba yetu wa kiroho ili tupate kuishi.
<scripture passage="Heb 12:10" parsed="|Heb|12|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.10" />
<sup>10</sup>Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
<scripture passage="Heb 12:11" parsed="|Heb|12|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.11" />
<sup>11</sup>Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili!
<scripture passage="Heb 12:12" parsed="|Heb|12|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.12" />
<sup>12</sup>Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu.
<scripture passage="Heb 12:13" parsed="|Heb|12|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.13" />
<sup>13</sup>Endeleeni kutembea katika njia iliyonyoka, ili kile kilicholemaa kisiumizwe, bali kiponywe.
<scripture passage="Heb 12:14" parsed="|Heb|12|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.14" />
<sup>14</sup>Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama hayo.
<scripture passage="Heb 12:15" parsed="|Heb|12|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.15" />
<sup>15</sup>Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu yake.
<scripture passage="Heb 12:16" parsed="|Heb|12|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.16" />
<sup>16</sup>Jihadharini ili miongoni mwenu pasiwe na mtu mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, aliyeuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mlo mmoja.
<scripture passage="Heb 12:17" parsed="|Heb|12|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.17" />
<sup>17</sup>Ninyi mnafahamu kwamba hata alipotaka kuipata tena ile baraka iliyokuwa yake, alikataliwa, maana hakupata tena nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.
<scripture passage="Heb 12:18" parsed="|Heb|12|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.18" />
<sup>18</sup>Ninyi hamkuwasili mlimani Sinai, ambao unaweza kushikika kama walivyofanya watu wa Israeli, hamkufika kwenye moto uwakao, penye giza, tufani,
<scripture passage="Heb 12:19" parsed="|Heb|12|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.19" />
<sup>19</sup>mvumo wa tarumbeta na sauti ya maneno. Wale waliosikia sauti hiyo waliomba wasisikie tena neno jingine,
<scripture passage="Heb 12:20" parsed="|Heb|12|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.20" />
<sup>20</sup>kwani hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: "Atakayegusa mlima huu, hata kama ni mnyama, atapigwa mawe."
<scripture passage="Heb 12:21" parsed="|Heb|12|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.21" />
<sup>21</sup>Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema, "Naogopa na kutetemeka."
<scripture passage="Heb 12:22" parsed="|Heb|12|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.22" />
<sup>22</sup>Lakini ninyi mmefika katika mlima wa Sioni, kwenye mji wa Mungu aliye hai. Mmefika Yerusalemu, mji wa mbinguni, ambapo wamekusanyika malaika elfu nyingi wasiohesabika.
<scripture passage="Heb 12:23" parsed="|Heb|12|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.23" />
<sup>23</sup>Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa kuwa wakamilifu.
<scripture passage="Heb 12:24" parsed="|Heb|12|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.24" />
<sup>24</sup>Mmefika kwa Yesu ambaye ameratibisha agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema zaidi kuliko ile ya Abeli.
<scripture passage="Heb 12:25" parsed="|Heb|12|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.25" />
<sup>25</sup>Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza yeye ambaye anasema nanyi. Kama wale walikataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutoka mbinguni?
<scripture passage="Heb 12:26" parsed="|Heb|12|26|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.26" />
<sup>26</sup>Wakati ule sauti ilitetemesha nchi, lakini sasa ameahidi: "Nitatetemesha nchi tena, lakini si nchi tu bali pia mbingu."
<scripture passage="Heb 12:27" parsed="|Heb|12|27|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.27" />
<sup>27</sup>Neno hili: "tena" linatuonyesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa.
<scripture passage="Heb 12:28" parsed="|Heb|12|28|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.28" />
<sup>28</sup>Sisi basi, na tushukuru kwani tunapokea utawala usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;
<scripture passage="Heb 12:29" parsed="|Heb|12|29|0|0" osisRef="Bible:Heb.12.29" />
<sup>29</sup>maana Mungu wetu kweli ni moto mkali unaoteketeza.
</p>
</div3>

<div3 title="Hebrews 13" progress="87.13%" prev="Heb.12" next="Jas" id="Heb.13">
<h3 id="Heb.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Heb.13-p1">
<scripture passage="Heb 13:1" parsed="|Heb|13|1|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.1" />
<sup>1</sup>Endeleeni kupendana kidugu.
<scripture passage="Heb 13:2" parsed="|Heb|13|2|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.2" />
<sup>2</sup>Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
<scripture passage="Heb 13:3" parsed="|Heb|13|3|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.3" />
<sup>3</sup>Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao.
<scripture passage="Heb 13:4" parsed="|Heb|13|4|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.4" />
<sup>4</sup>Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
<scripture passage="Heb 13:5" parsed="|Heb|13|5|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.5" />
<sup>5</sup>Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: "Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa."
<scripture passage="Heb 13:6" parsed="|Heb|13|6|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.6" />
<sup>6</sup>Ndiyo maana tunathubutu kusema: "Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?"
<scripture passage="Heb 13:7" parsed="|Heb|13|7|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.7" />
<sup>7</sup>wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
<scripture passage="Heb 13:8" parsed="|Heb|13|8|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.8" />
<sup>8</sup>Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele.
<scripture passage="Heb 13:9" parsed="|Heb|13|9|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.9" />
<sup>9</sup>Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.
<scripture passage="Heb 13:10" parsed="|Heb|13|10|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.10" />
<sup>10</sup>Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.
<scripture passage="Heb 13:11" parsed="|Heb|13|11|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.11" />
<sup>11</sup>Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
<scripture passage="Heb 13:12" parsed="|Heb|13|12|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.12" />
<sup>12</sup>Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji.
<scripture passage="Heb 13:13" parsed="|Heb|13|13|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.13" />
<sup>13</sup>Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake.
<scripture passage="Heb 13:14" parsed="|Heb|13|14|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.14" />
<sup>14</sup>Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja.
<scripture passage="Heb 13:15" parsed="|Heb|13|15|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.15" />
<sup>15</sup>Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake.
<scripture passage="Heb 13:16" parsed="|Heb|13|16|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.16" />
<sup>16</sup>Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu.
<scripture passage="Heb 13:17" parsed="|Heb|13|17|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.17" />
<sup>17</sup>Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.
<scripture passage="Heb 13:18" parsed="|Heb|13|18|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.18" />
<sup>18</sup>Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima.
<scripture passage="Heb 13:19" parsed="|Heb|13|19|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.19" />
<sup>19</sup>Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo.
<scripture passage="Heb 13:20" parsed="|Heb|13|20|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.20" />
<sup>20</sup>Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.
<scripture passage="Heb 13:21" parsed="|Heb|13|21|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.21" />
<sup>21</sup>Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.
<scripture passage="Heb 13:22" parsed="|Heb|13|22|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.22" />
<sup>22</sup>Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni.
<scripture passage="Heb 13:23" parsed="|Heb|13|23|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.23" />
<sup>23</sup>Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu.
<scripture passage="Heb 13:24" parsed="|Heb|13|24|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.24" />
<sup>24</sup>Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni.
<scripture passage="Heb 13:25" parsed="|Heb|13|25|0|0" osisRef="Bible:Heb.13.25" />
<sup>25</sup>Tunawatakieni nyote neema ya Mungu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="James" progress="87.43%" prev="Heb.13" next="Jas.1" id="Jas">
<h2 id="Jas-p0.1">James</h2>

<div3 title="James 1" progress="87.43%" prev="Jas" next="Jas.2" id="Jas.1">
<h3 id="Jas.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Jas.1-p1">
<scripture passage="Jas 1:1" parsed="|Jas|1|1|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam!
<scripture passage="Jas 1:2" parsed="|Jas|1|2|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.2" />
<sup>2</sup>Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali,
<scripture passage="Jas 1:3" parsed="|Jas|1|3|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.3" />
<sup>3</sup>kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.
<scripture passage="Jas 1:4" parsed="|Jas|1|4|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.4" />
<sup>4</sup>Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
<scripture passage="Jas 1:5" parsed="|Jas|1|5|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.5" />
<sup>5</sup>Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu.
<scripture passage="Jas 1:6" parsed="|Jas|1|6|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.6" />
<sup>6</sup>Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na upepo.
<scripture passage="Jas 1:7" parsed="|Jas|1|7|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.7" />
<sup>7</sup>Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote, asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa Bwana.
<scripture passage="Jas 1:8" parsed="|Jas|1|8|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.8" />
<sup>8</sup>[]
<scripture passage="Jas 1:9" parsed="|Jas|1|9|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.9" />
<sup>9</sup>Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,
<scripture passage="Jas 1:10" parsed="|Jas|1|10|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.10" />
<sup>10</sup>naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini.
<scripture passage="Jas 1:11" parsed="|Jas|1|11|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.11" />
<sup>11</sup>Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake.
<scripture passage="Jas 1:12" parsed="|Jas|1|12|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.12" />
<sup>12</sup>Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda.
<scripture passage="Jas 1:13" parsed="|Jas|1|13|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.13" />
<sup>13</sup>Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.
<scripture passage="Jas 1:14" parsed="|Jas|1|14|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.14" />
<sup>14</sup>Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
<scripture passage="Jas 1:15" parsed="|Jas|1|15|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.15" />
<sup>15</sup>Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.
<scripture passage="Jas 1:16" parsed="|Jas|1|16|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.16" />
<sup>16</sup>Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike!
<scripture passage="Jas 1:17" parsed="|Jas|1|17|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.17" />
<sup>17</sup>Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu.
<scripture passage="Jas 1:18" parsed="|Jas|1|18|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.18" />
<sup>18</sup>Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake.
<scripture passage="Jas 1:19" parsed="|Jas|1|19|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.19" />
<sup>19</sup>Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.
<scripture passage="Jas 1:20" parsed="|Jas|1|20|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.20" />
<sup>20</sup>Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.
<scripture passage="Jas 1:21" parsed="|Jas|1|21|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.21" />
<sup>21</sup>Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambao waweza kuziokoa nafsi zenu.
<scripture passage="Jas 1:22" parsed="|Jas|1|22|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.22" />
<sup>22</sup>Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.
<scripture passage="Jas 1:23" parsed="|Jas|1|23|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.23" />
<sup>23</sup>Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo.
<scripture passage="Jas 1:24" parsed="|Jas|1|24|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.24" />
<sup>24</sup>Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.
<scripture passage="Jas 1:25" parsed="|Jas|1|25|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.25" />
<sup>25</sup>Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.
<scripture passage="Jas 1:26" parsed="|Jas|1|26|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.26" />
<sup>26</sup>Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
<scripture passage="Jas 1:27" parsed="|Jas|1|27|0|0" osisRef="Bible:Jas.1.27" />
<sup>27</sup>Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
</p>
</div3>

<div3 title="James 2" progress="87.75%" prev="Jas.1" next="Jas.3" id="Jas.2">
<h3 id="Jas.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Jas.2-p1">
<scripture passage="Jas 2:1" parsed="|Jas|2|1|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.1" />
<sup>1</sup>Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.
<scripture passage="Jas 2:2" parsed="|Jas|2|2|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.2" />
<sup>2</sup>Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi machafu.
<scripture passage="Jas 2:3" parsed="|Jas|2|3|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.3" />
<sup>3</sup>Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: "Keti hapa mahali pazuri," na kumwambia yule maskini: "Wewe, simama huko," au "Keti hapa sakafuni miguuni pangu,"
<scripture passage="Jas 2:4" parsed="|Jas|2|4|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.4" />
<sup>4</sup>je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya?
<scripture passage="Jas 2:5" parsed="|Jas|2|5|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.5" />
<sup>5</sup>Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea Utawala aliowaahidia wale wanaompenda.
<scripture passage="Jas 2:6" parsed="|Jas|2|6|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.6" />
<sup>6</sup>Lakini ninyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamizeni na kuwapeleka mahakamani?
<scripture passage="Jas 2:7" parsed="|Jas|2|7|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.7" />
<sup>7</sup>Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa?
<scripture passage="Jas 2:8" parsed="|Jas|2|8|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.8" />
<sup>8</sup>Kama mnaitimiza ile sheria ya Utawala kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: "Mpende binadamu mwenzako kama unavyojipenda wewe mwenyewe", mtakuwa mnafanya vema kabisa.
<scripture passage="Jas 2:9" parsed="|Jas|2|9|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.9" />
<sup>9</sup>Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheria inawahukumu ninyi kuwa mna hatia.
<scripture passage="Jas 2:10" parsed="|Jas|2|10|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.10" />
<sup>10</sup>Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja Sheria yote.
<scripture passage="Jas 2:11" parsed="|Jas|2|11|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.11" />
<sup>11</sup>Maana yuleyule aliyesema: "Usizini," alisema pia "Usiue". Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.
<scripture passage="Jas 2:12" parsed="|Jas|2|12|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.12" />
<sup>12</sup>Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.
<scripture passage="Jas 2:13" parsed="|Jas|2|13|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.13" />
<sup>13</sup>Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma. Lakini huruma hushinda hukumu.
<scripture passage="Jas 2:14" parsed="|Jas|2|14|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.14" />
<sup>14</sup>Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa?
<scripture passage="Jas 2:15" parsed="|Jas|2|15|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.15" />
<sup>15</sup>Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula.
<scripture passage="Jas 2:16" parsed="|Jas|2|16|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.16" />
<sup>16</sup>Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
<scripture passage="Jas 2:17" parsed="|Jas|2|17|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.17" />
<sup>17</sup>Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
<scripture passage="Jas 2:18" parsed="|Jas|2|18|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.18" />
<sup>18</sup>Lakini mtu anaweza kusema: "Wewe unayo imani, mimi ninayo matendo!" Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
<scripture passage="Jas 2:19" parsed="|Jas|2|19|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.19" />
<sup>19</sup>Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.
<scripture passage="Jas 2:20" parsed="|Jas|2|20|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.20" />
<sup>20</sup>Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo imekufa?
<scripture passage="Jas 2:21" parsed="|Jas|2|21|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.21" />
<sup>21</sup>Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu.
<scripture passage="Jas 2:22" parsed="|Jas|2|22|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.22" />
<sup>22</sup>Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani yake ilikamilishwa kwa matendo yake.
<scripture passage="Jas 2:23" parsed="|Jas|2|23|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.23" />
<sup>23</sup>Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: "Abrahamu alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu."
<scripture passage="Jas 2:24" parsed="|Jas|2|24|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.24" />
<sup>24</sup>Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake na si kwa imani peke yake.
<scripture passage="Jas 2:25" parsed="|Jas|2|25|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.25" />
<sup>25</sup>Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
<scripture passage="Jas 2:26" parsed="|Jas|2|26|0|0" osisRef="Bible:Jas.2.26" />
<sup>26</sup>Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.
</p>
</div3>

<div3 title="James 3" progress="88.06%" prev="Jas.2" next="Jas.4" id="Jas.3">
<h3 id="Jas.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Jas.3-p1">
<scripture passage="Jas 3:1" parsed="|Jas|3|1|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.1" />
<sup>1</sup>Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu. Kama mjuavyo, sisi walimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.
<scripture passage="Jas 3:2" parsed="|Jas|3|2|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.2" />
<sup>2</sup>Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, na anaweza kutawala nafsi yake yote.
<scripture passage="Jas 3:3" parsed="|Jas|3|3|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.3" />
<sup>3</sup>Sisi huwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii; na kwa njia hiyo twaweza kuwaongoza kokote tunakotaka.
<scripture passage="Jas 3:4" parsed="|Jas|3|4|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.4" />
<sup>4</sup>Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
<scripture passage="Jas 3:5" parsed="|Jas|3|5|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.5" />
<sup>5</sup>Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. ic Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
<scripture passage="Jas 3:6" parsed="|Jas|3|6|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.6" />
<sup>6</sup>Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
<scripture passage="Jas 3:7" parsed="|Jas|3|7|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.7" />
<sup>7</sup>Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote--wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini.
<scripture passage="Jas 3:8" parsed="|Jas|3|8|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.8" />
<sup>8</sup>Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.
<scripture passage="Jas 3:9" parsed="|Jas|3|9|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.9" />
<sup>9</sup>Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
<scripture passage="Jas 3:10" parsed="|Jas|3|10|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.10" />
<sup>10</sup>Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.
<scripture passage="Jas 3:11" parsed="|Jas|3|11|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.11" />
<sup>11</sup>Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?
<scripture passage="Jas 3:12" parsed="|Jas|3|12|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.12" />
<sup>12</sup>Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.
<scripture passage="Jas 3:13" parsed="|Jas|3|13|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.13" />
<sup>13</sup>Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
<scripture passage="Jas 3:14" parsed="|Jas|3|14|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.14" />
<sup>14</sup>Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.
<scripture passage="Jas 3:15" parsed="|Jas|3|15|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.15" />
<sup>15</sup>Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.
<scripture passage="Jas 3:16" parsed="|Jas|3|16|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.16" />
<sup>16</sup>Maana popote palipo na wivu na ubinafsi hapo pana fujo na kila aina ya uovu.
<scripture passage="Jas 3:17" parsed="|Jas|3|17|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.17" />
<sup>17</sup>Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
<scripture passage="Jas 3:18" parsed="|Jas|3|18|0|0" osisRef="Bible:Jas.3.18" />
<sup>18</sup>Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.
</p>
</div3>

<div3 title="James 4" progress="88.29%" prev="Jas.3" next="Jas.5" id="Jas.4">
<h3 id="Jas.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Jas.4-p1">
<scripture passage="Jas 4:1" parsed="|Jas|4|1|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.1" />
<sup>1</sup>Mapigano na magombano yote kati yenu yanatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.
<scripture passage="Jas 4:2" parsed="|Jas|4|2|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.2" />
<sup>2</sup>Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana kupata vitu, lakini hamvipati, hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu.
<scripture passage="Jas 4:3" parsed="|Jas|4|3|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.3" />
<sup>3</sup>Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu.
<scripture passage="Jas 4:4" parsed="|Jas|4|4|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.4" />
<sup>4</sup>Ninyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.
<scripture passage="Jas 4:5" parsed="|Jas|4|5|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.5" />
<sup>5</sup>Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: "Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa."
<scripture passage="Jas 4:6" parsed="|Jas|4|6|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.6" />
<sup>6</sup>Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: "Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu."
<scripture passage="Jas 4:7" parsed="|Jas|4|7|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.7" />
<sup>7</sup>Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni.
<scripture passage="Jas 4:8" parsed="|Jas|4|8|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.8" />
<sup>8</sup>Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!
<scripture passage="Jas 4:9" parsed="|Jas|4|9|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.9" />
<sup>9</sup>Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa.
<scripture passage="Jas 4:10" parsed="|Jas|4|10|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.10" />
<sup>10</sup>Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.
<scripture passage="Jas 4:11" parsed="|Jas|4|11|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.11" />
<sup>11</sup>Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu Sheria. Kama ukiihukumu Sheria, basi, wewe huitii Sheria, bali waihukumu.
<scripture passage="Jas 4:12" parsed="|Jas|4|12|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.12" />
<sup>12</sup>Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka Sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?
<scripture passage="Jas 4:13" parsed="|Jas|4|13|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.13" />
<sup>13</sup>Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: "Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata faida."
<scripture passage="Jas 4:14" parsed="|Jas|4|14|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.14" />
<sup>14</sup>Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
<scripture passage="Jas 4:15" parsed="|Jas|4|15|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.15" />
<sup>15</sup>Mngalipaswa kusema: "Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile."
<scripture passage="Jas 4:16" parsed="|Jas|4|16|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.16" />
<sup>16</sup>Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya.
<scripture passage="Jas 4:17" parsed="|Jas|4|17|0|0" osisRef="Bible:Jas.4.17" />
<sup>17</sup>Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.
</p>
</div3>

<div3 title="James 5" progress="88.50%" prev="Jas.4" next="iPet" id="Jas.5">
<h3 id="Jas.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Jas.5-p1">
<scripture passage="Jas 5:1" parsed="|Jas|5|1|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.1" />
<sup>1</sup>Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni.
<scripture passage="Jas 5:2" parsed="|Jas|5|2|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.2" />
<sup>2</sup>Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo.
<scripture passage="Jas 5:3" parsed="|Jas|5|3|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.3" />
<sup>3</sup>Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia mali katika siku hizi za mwisho!
<scripture passage="Jas 5:4" parsed="|Jas|5|4|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.4" />
<sup>4</sup>Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana, Mwenye Nguvu.
<scripture passage="Jas 5:5" parsed="|Jas|5|5|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.5" />
<sup>5</sup>Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa.
<scripture passage="Jas 5:6" parsed="|Jas|5|6|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.6" />
<sup>6</sup>Mmemhukumu na kumwua mtu asiye na hatia, naye hakuwapigeni.
<scripture passage="Jas 5:7" parsed="|Jas|5|7|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.7" />
<sup>7</sup>Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
<scripture passage="Jas 5:8" parsed="|Jas|5|8|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.8" />
<sup>8</sup>Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia.
<scripture passage="Jas 5:9" parsed="|Jas|5|9|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.9" />
<sup>9</sup>Ndugu zangu, msinung`unikiane ninyi kwa ninyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.
<scripture passage="Jas 5:10" parsed="|Jas|5|10|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.10" />
<sup>10</sup>Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana.
<scripture passage="Jas 5:11" parsed="|Jas|5|11|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.11" />
<sup>11</sup>Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.
<scripture passage="Jas 5:12" parsed="|Jas|5|12|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.12" />
<sup>12</sup>Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni "Ndiyo" kama maana yenu ni ndiyo, na "La" kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.
<scripture passage="Jas 5:13" parsed="|Jas|5|13|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.13" />
<sup>13</sup>Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
<scripture passage="Jas 5:14" parsed="|Jas|5|14|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.14" />
<sup>14</sup>Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
<scripture passage="Jas 5:15" parsed="|Jas|5|15|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.15" />
<sup>15</sup>Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
<scripture passage="Jas 5:16" parsed="|Jas|5|16|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.16" />
<sup>16</sup>Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.
<scripture passage="Jas 5:17" parsed="|Jas|5|17|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.17" />
<sup>17</sup>Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
<scripture passage="Jas 5:18" parsed="|Jas|5|18|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.18" />
<sup>18</sup>Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa mazao yake.
<scripture passage="Jas 5:19" parsed="|Jas|5|19|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.19" />
<sup>19</sup>Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine akamrudisha,
<scripture passage="Jas 5:20" parsed="|Jas|5|20|0|0" osisRef="Bible:Jas.5.20" />
<sup>20</sup>fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi zitaondolewa.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="1 Peter" progress="88.76%" prev="Jas.5" next="iPet.1" id="iPet">
<h2 id="iPet-p0.1">1 Peter</h2>

<div3 title="1 Peter 1" progress="88.76%" prev="iPet" next="iPet.2" id="iPet.1">
<h3 id="iPet.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iPet.1-p1">
<scripture passage="iPet 1:1" parsed="|1Pet|1|1|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo nawaandikia ninyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.
<scripture passage="iPet 1:2" parsed="|1Pet|1|2|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.2" />
<sup>2</sup>Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
<scripture passage="iPet 1:3" parsed="|1Pet|1|3|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.3" />
<sup>3</sup>Asifiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake kuu alitufanya tuzaliwe upya kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujalia tumaini lenye uzima,
<scripture passage="iPet 1:4" parsed="|1Pet|1|4|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.4" />
<sup>4</sup>na hivyo tunatazamia kupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekea watu wake. Mungu amewawekeeni baraka hizo mbinguni ambako haziwezi kuoza au kuharibika au kufifia.
<scripture passage="iPet 1:5" parsed="|1Pet|1|5|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.5" />
<sup>5</sup>Hizo zitakuwa zenu ninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni mwa nyakati.
<scripture passage="iPet 1:6" parsed="|1Pet|1|6|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.6" />
<sup>6</sup>Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.
<scripture passage="iPet 1:7" parsed="|1Pet|1|7|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.7" />
<sup>7</sup>Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
<scripture passage="iPet 1:8" parsed="|1Pet|1|8|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.8" />
<sup>8</sup>Ninyi mnampenda ingawaje hamjamwona, na mnamwamini ingawa hamumwoni sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka,
<scripture passage="iPet 1:9" parsed="|1Pet|1|9|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.9" />
<sup>9</sup>kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu.
<scripture passage="iPet 1:10" parsed="|1Pet|1|10|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.10" />
<sup>10</sup>Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.
<scripture passage="iPet 1:11" parsed="|1Pet|1|11|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.11" />
<sup>11</sup>Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
<scripture passage="iPet 1:12" parsed="|1Pet|1|12|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.12" />
<sup>12</sup>Mungu aliwafunulia kwamba wakati walipokuwa wanasema juu ya hayo mambo ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe waliowatangazieni Habari Njema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.
<scripture passage="iPet 1:13" parsed="|1Pet|1|13|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.13" />
<sup>13</sup>Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha. Wekeni tumaini lenu lote katika baraka ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo atakapoonekana!
<scripture passage="iPet 1:14" parsed="|1Pet|1|14|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.14" />
<sup>14</sup>Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.
<scripture passage="iPet 1:15" parsed="|1Pet|1|15|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.15" />
<sup>15</sup>Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.
<scripture passage="iPet 1:16" parsed="|1Pet|1|16|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.16" />
<sup>16</sup>Maandiko yasema: "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu."
<scripture passage="iPet 1:17" parsed="|1Pet|1|17|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.17" />
<sup>17</sup>Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
<scripture passage="iPet 1:18" parsed="|1Pet|1|18|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.18" />
<sup>18</sup>Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
<scripture passage="iPet 1:19" parsed="|1Pet|1|19|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.19" />
<sup>19</sup>bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
<scripture passage="iPet 1:20" parsed="|1Pet|1|20|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.20" />
<sup>20</sup>Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa, akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.
<scripture passage="iPet 1:21" parsed="|1Pet|1|21|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.21" />
<sup>21</sup>Kwa njia yake, ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.
<scripture passage="iPet 1:22" parsed="|1Pet|1|22|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.22" />
<sup>22</sup>Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
<scripture passage="iPet 1:23" parsed="|1Pet|1|23|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.23" />
<sup>23</sup>Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
<scripture passage="iPet 1:24" parsed="|1Pet|1|24|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.24" />
<sup>24</sup>Kama Maandiko yasemavyo: "Kila binadamu ni kama nyasi, na utukufu wake wote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyauka na maua huanguka.
<scripture passage="iPet 1:25" parsed="|1Pet|1|25|0|0" osisRef="Bible:1Pet.1.25" />
<sup>25</sup>Lakini neno la Bwana hudumu milele." Neno hilo ni hiyo Habari Njema iliyohubiriwa kwenu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Peter 2" progress="89.15%" prev="iPet.1" next="iPet.3" id="iPet.2">
<h3 id="iPet.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iPet.2-p1">
<scripture passage="iPet 2:1" parsed="|1Pet|2|1|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.1" />
<sup>1</sup>Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena.
<scripture passage="iPet 2:2" parsed="|1Pet|2|2|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.2" />
<sup>2</sup>Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa.
<scripture passage="iPet 2:3" parsed="|1Pet|2|3|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.3" />
<sup>3</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mmegundua kwamba Bwana ni mwema."
<scripture passage="iPet 2:4" parsed="|1Pet|2|4|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.4" />
<sup>4</sup>Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamani kubwa.
<scripture passage="iPet 2:5" parsed="|1Pet|2|5|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.5" />
<sup>5</sup>Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho, ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea dhabihu za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
<scripture passage="iPet 2:6" parsed="|1Pet|2|6|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.6" />
<sup>6</sup>Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Tazama! Naweka huko sioni jiwe kuu la msingi, jiwe la thamani kubwa nililoliteua. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa."
<scripture passage="iPet 2:7" parsed="|1Pet|2|7|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.7" />
<sup>7</sup>Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, "Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi."
<scripture passage="iPet 2:8" parsed="|1Pet|2|8|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.8" />
<sup>8</sup>Tena Maandiko yasema: "Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu." Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo.
<scripture passage="iPet 2:9" parsed="|1Pet|2|9|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.9" />
<sup>9</sup>Lakini ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.
<scripture passage="iPet 2:10" parsed="|1Pet|2|10|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.10" />
<sup>10</sup>Wakati mmoja ninyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa ninyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmeipokea.
<scripture passage="iPet 2:11" parsed="|1Pet|2|11|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.11" />
<sup>11</sup>Wapenzi wangu, nawasihi ninyi kama wageni na wakimbizi hapa duniani! Achaneni na tamaa za mwili ambazo hupingana na roho.
<scripture passage="iPet 2:12" parsed="|1Pet|2|12|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.12" />
<sup>12</sup>Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu Siku ya kuja kwake.
<scripture passage="iPet 2:13" parsed="|1Pet|2|13|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.13" />
<sup>13</sup>Basi, jiwekeni chini ya mamlaka yote ya kibinadamu, kwa ajili ya Bwana: utii kwa mfalme aliye mtawala mkuu,
<scripture passage="iPet 2:14" parsed="|1Pet|2|14|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.14" />
<sup>14</sup>utii kwa wakuu wa mikoa ambao wameteuliwa naye kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema.
<scripture passage="iPet 2:15" parsed="|1Pet|2|15|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.15" />
<sup>15</sup>Maana Mungu anataka mweze kuyakomesha maneno ya kijinga ya watu wasio na akili kwa matendo mema mnayofanya.
<scripture passage="iPet 2:16" parsed="|1Pet|2|16|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.16" />
<sup>16</sup>Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu.
<scripture passage="iPet 2:17" parsed="|1Pet|2|17|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.17" />
<sup>17</sup>Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme.
<scripture passage="iPet 2:18" parsed="|1Pet|2|18|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.18" />
<sup>18</sup>Enyi watumishi wa nyumbani, watiini wakuu wenu kwa heshima yote, wawe wema na wapole au wenye kuchukiza.
<scripture passage="iPet 2:19" parsed="|1Pet|2|19|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.19" />
<sup>19</sup>Maana kama mnavumilia maumivu ya mateso msiyostahili kwa sababu mwajua kwamba Mungu anataka hivyo, basi Mungu atawafadhili.
<scripture passage="iPet 2:20" parsed="|1Pet|2|20|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.20" />
<sup>20</sup>Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
<scripture passage="iPet 2:21" parsed="|1Pet|2|21|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.21" />
<sup>21</sup>Hayo ndiyo mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ili muufuate mwenendo wake.
<scripture passage="iPet 2:22" parsed="|1Pet|2|22|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.22" />
<sup>22</sup>Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika mdomoni mwake.
<scripture passage="iPet 2:23" parsed="|1Pet|2|23|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.23" />
<sup>23</sup>Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki.
<scripture passage="iPet 2:24" parsed="|1Pet|2|24|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.24" />
<sup>24</sup>Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.
<scripture passage="iPet 2:25" parsed="|1Pet|2|25|0|0" osisRef="Bible:1Pet.2.25" />
<sup>25</sup>Ninyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Peter 3" progress="89.50%" prev="iPet.2" next="iPet.4" id="iPet.3">
<h3 id="iPet.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iPet.3-p1">
<scripture passage="iPet 3:1" parsed="|1Pet|3|1|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.1" />
<sup>1</sup>Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
<scripture passage="iPet 3:2" parsed="|1Pet|3|2|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.2" />
<sup>2</sup>kwani wataona jinsi mwenendo wenu ulivyo safi na wa kumcha Mungu.
<scripture passage="iPet 3:3" parsed="|1Pet|3|3|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.3" />
<sup>3</sup>Katika kujipamba kwenu msitegemee mambo ya njenje, kama vile mitindo ya kusuka nywele, kujivalia vitu vya dhahabu na nguo maridadi.
<scripture passage="iPet 3:4" parsed="|1Pet|3|4|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.4" />
<sup>4</sup>Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu.
<scripture passage="iPet 3:5" parsed="|1Pet|3|5|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.5" />
<sup>5</sup>Ndivyo walivyojipamba hapo kale wanawake waadilifu waliomtumainia Mungu; walijiweka chini ya mamlaka ya waume zao.
<scripture passage="iPet 3:6" parsed="|1Pet|3|6|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.6" />
<sup>6</sup>Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Ninyi mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.
<scripture passage="iPet 3:7" parsed="|1Pet|3|7|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.7" />
<sup>7</sup>Kadhalika nanyi waume, katika kuishi na wake zenu mnapaswa kutambua kwamba wao ni dhaifu na hivyo muwatendee kwa heshima; maana nao pia watapokea pamoja nanyi zawadi ya uzima anayowapeni Mungu. Hapo ndipo sala zenu hazitakataliwa.
<scripture passage="iPet 3:8" parsed="|1Pet|3|8|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.8" />
<sup>8</sup>Mwisho nasema hivi: mnapaswa kuwa na moyo mmoja, na fikira moja; mnapaswa kupendana kidugu, kuwa wapole na wanyenyekevu ninyi kwa ninyi.
<scripture passage="iPet 3:9" parsed="|1Pet|3|9|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.9" />
<sup>9</sup>Msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni baraka, maana ninyi mliitwa na Mungu mpate kupokea baraka.
<scripture passage="iPet 3:10" parsed="|1Pet|3|10|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.10" />
<sup>10</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Anayetaka kufurahia maisha, na kuona siku za fanaka, anapaswa kuacha kusema mabaya na kuacha kusema uongo.
<scripture passage="iPet 3:11" parsed="|1Pet|3|11|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.11" />
<sup>11</sup>Na ajiepushe na uovu, atende mema, atafute amani na kuizingatia.
<scripture passage="iPet 3:12" parsed="|1Pet|3|12|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.12" />
<sup>12</sup>Maana Bwana huwatazama kwa wema waadilifu na kuzisikiliza sala zao. Lakini huwapa kisogo watu watendao maovu."
<scripture passage="iPet 3:13" parsed="|1Pet|3|13|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.13" />
<sup>13</sup>Ni nani atakayeweza kuwadhuru ninyi kama mkizingatia kutenda mema?
<scripture passage="iPet 3:14" parsed="|1Pet|3|14|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.14" />
<sup>14</sup>Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika wasiwasi.
<scripture passage="iPet 3:15" parsed="|1Pet|3|15|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.15" />
<sup>15</sup>Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,
<scripture passage="iPet 3:16" parsed="|1Pet|3|16|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.16" />
<sup>16</sup>lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.
<scripture passage="iPet 3:17" parsed="|1Pet|3|17|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.17" />
<sup>17</sup>Maana ni afadhali kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, kama Mungu akipenda, kuliko kuteseka kwa sababu ya kutenda uovu.
<scripture passage="iPet 3:18" parsed="|1Pet|3|18|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.18" />
<sup>18</sup>Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke ninyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
<scripture passage="iPet 3:19" parsed="|1Pet|3|19|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.19" />
<sup>19</sup>na kwa maisha yake ya kiroho alikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwa kifungoni.
<scripture passage="iPet 3:20" parsed="|1Pet|3|20|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.20" />
<sup>20</sup>Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa majini,
<scripture passage="iPet 3:21" parsed="|1Pet|3|21|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.21" />
<sup>21</sup>ambayo yalikuwa mfano wa ubatizo unaowaokoa ninyi sasa. Ubatizo si shauri la kuondoa uchafu mwilini, bali ni ahadi kwa Mungu inayofanyika katika dhamiri njema. Huwaokoeni kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo,
<scripture passage="iPet 3:22" parsed="|1Pet|3|22|0|0" osisRef="Bible:1Pet.3.22" />
<sup>22</sup>ambaye alikwenda mbinguni na sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, anatawala juu ya malaika, wakuu na wenye enzi.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Peter 4" progress="89.82%" prev="iPet.3" next="iPet.5" id="iPet.4">
<h3 id="iPet.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iPet.4-p1">
<scripture passage="iPet 4:1" parsed="|1Pet|4|1|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.1" />
<sup>1</sup>Maadamu Kristo aliteseka kimwili, nanyi pia mnapaswa kujiimarisha kwa nia hiyo yake; maana mtu akisha teseka kimwili hahusiki tena na dhambi.
<scripture passage="iPet 4:2" parsed="|1Pet|4|2|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.2" />
<sup>2</sup>Tangu sasa, basi, maisha yaliowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, si na tamaa za kibinadamu.
<scripture passage="iPet 4:3" parsed="|1Pet|4|3|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.3" />
<sup>3</sup>Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu.
<scripture passage="iPet 4:4" parsed="|1Pet|4|4|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.4" />
<sup>4</sup>Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni.
<scripture passage="iPet 4:5" parsed="|1Pet|4|5|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.5" />
<sup>5</sup>Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu aliye tayari kuwahukumu wazima na wafu!
<scripture passage="iPet 4:6" parsed="|1Pet|4|6|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.6" />
<sup>6</sup>Kwa sababu hiyo, hao waliokufa ambao walikuwa wamehukumiwa katika maisha yao ya kimwili kama anavyohukumiwa kila mmoja, walihubiriwa Habari Njema kusudi katika maisha yao ya kiroho waishi kama aishivyo Mungu.
<scripture passage="iPet 4:7" parsed="|1Pet|4|7|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.7" />
<sup>7</sup>Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na nidhamu, ili mweze kusali.
<scripture passage="iPet 4:8" parsed="|1Pet|4|8|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.8" />
<sup>8</sup>Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi.
<scripture passage="iPet 4:9" parsed="|1Pet|4|9|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.9" />
<sup>9</sup>Muwe na ukarimu ninyi kwa ninyi bila kunung`unika.
<scripture passage="iPet 4:10" parsed="|1Pet|4|10|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.10" />
<sup>10</sup>Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile uwakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu.
<scripture passage="iPet 4:11" parsed="|1Pet|4|11|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.11" />
<sup>11</sup>Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumika anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
<scripture passage="iPet 4:12" parsed="|1Pet|4|12|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.12" />
<sup>12</sup>Wapenzi wangu, msishangae kuhusu majaribio makali mnayopata kana kwamba mnapatwa na kitu kisicho cha kawaida.
<scripture passage="iPet 4:13" parsed="|1Pet|4|13|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.13" />
<sup>13</sup>Ila furahini kwamba mnashiriki mateso ya Kristo ili mweze kuwa na furaha tele wakati utukufu wake utakapofunuliwa.
<scripture passage="iPet 4:14" parsed="|1Pet|4|14|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.14" />
<sup>14</sup>Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu yetu.
<scripture passage="iPet 4:15" parsed="|1Pet|4|15|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.15" />
<sup>15</sup>Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni muuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
<scripture passage="iPet 4:16" parsed="|1Pet|4|16|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.16" />
<sup>16</sup>Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo.
<scripture passage="iPet 4:17" parsed="|1Pet|4|17|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.17" />
<sup>17</sup>Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
<scripture passage="iPet 4:18" parsed="|1Pet|4|18|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.18" />
<sup>18</sup>Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Ni vigumu kwa watu waadilifu kuokolewa; itakuwaje basi kwa wasiomcha Mungu na wenye dhambi?"
<scripture passage="iPet 4:19" parsed="|1Pet|4|19|0|0" osisRef="Bible:1Pet.4.19" />
<sup>19</sup>Kwa hiyo, wale wanaoteseka kufuatana na matakwa ya Mungu, wanapaswa, kwa matendo yao mema, kujiweka chini ya Muumba wao ambaye ni wa kuaminika kabisa.
</p>
</div3>

<div3 title="1 Peter 5" progress="90.09%" prev="iPet.4" next="iiPet" id="iPet.5">
<h3 id="iPet.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iPet.5-p1">
<scripture passage="iPet 5:1" parsed="|1Pet|5|1|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.1" />
<sup>1</sup>wazee! Mimi niliye mzee ninalo ombi moja kwenu wazee wenzangu. Mimi mwenyewe nilishuhudia kwa macho yangu mateso ya Kristo na natumaini kuushiriki ule utukufu utakaofunuliwa. Mimi nawaombeni
<scripture passage="iPet 5:2" parsed="|1Pet|5|2|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.2" />
<sup>2</sup>mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
<scripture passage="iPet 5:3" parsed="|1Pet|5|3|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.3" />
<sup>3</sup>Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwe mfano kwa hilo kundi.
<scripture passage="iPet 5:4" parsed="|1Pet|5|4|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.4" />
<sup>4</sup>Na wakati Mchungaji Mkuu atakapotokea, ninyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.
<scripture passage="iPet 5:5" parsed="|1Pet|5|5|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.5" />
<sup>5</sup>Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Ninyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu."
<scripture passage="iPet 5:6" parsed="|1Pet|5|6|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.6" />
<sup>6</sup>Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao.
<scripture passage="iPet 5:7" parsed="|1Pet|5|7|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.7" />
<sup>7</sup>Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.
<scripture passage="iPet 5:8" parsed="|1Pet|5|8|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.8" />
<sup>8</sup>Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.
<scripture passage="iPet 5:9" parsed="|1Pet|5|9|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.9" />
<sup>9</sup>Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.
<scripture passage="iPet 5:10" parsed="|1Pet|5|10|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.10" />
<sup>10</sup>Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni muushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
<scripture passage="iPet 5:11" parsed="|1Pet|5|11|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.11" />
<sup>11</sup>Kwake uwe uwezo milele! Amina.
<scripture passage="iPet 5:12" parsed="|1Pet|5|12|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.12" />
<sup>12</sup>Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
<scripture passage="iPet 5:13" parsed="|1Pet|5|13|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.13" />
<sup>13</sup>Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
<scripture passage="iPet 5:14" parsed="|1Pet|5|14|0|0" osisRef="Bible:1Pet.5.14" />
<sup>14</sup>Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani ninyi mlio wake Kristo.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="2 Peter" progress="90.28%" prev="iPet.5" next="iiPet.1" id="iiPet">
<h2 id="iiPet-p0.1">2 Peter</h2>

<div3 title="2 Peter 1" progress="90.28%" prev="iiPet" next="iiPet.2" id="iiPet.1">
<h3 id="iiPet.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiPet.1-p1">
<scripture passage="iiPet 1:1" parsed="|2Pet|1|1|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia ninyi ambao, kwa wema wake Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo, mmejaliwa imani ileile ya thamani kuu tuliyojaliwa sisi.
<scripture passage="iiPet 1:2" parsed="|2Pet|1|2|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.2" />
<sup>2</sup>Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
<scripture passage="iiPet 1:3" parsed="|2Pet|1|3|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.3" />
<sup>3</sup>Kwa uwezo wake wa kimungu, Mungu ametujalia mambo yote tunayohitaji, ili tuishi maisha ya kumcha Mungu kwa kumjua yeye aliyetuita tuushiriki utukufu na wema wake yeye mwenyewe.
<scripture passage="iiPet 1:4" parsed="|2Pet|1|4|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.4" />
<sup>4</sup>Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na mpate kuishiriki hali yake ya kimungu.
<scripture passage="iiPet 1:5" parsed="|2Pet|1|5|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.5" />
<sup>5</sup>Kwa sababu hiyo, fanyeni bidii ya kuongeza fadhila katika imani yenu: ongezeni elimu katika fadhila yenu,
<scripture passage="iiPet 1:6" parsed="|2Pet|1|6|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.6" />
<sup>6</sup>kuwa na kiasi katika elimu yenu, uvumilivu katika kuwa na kiasi, uchaji wa Mungu katika uvumilivu wenu,
<scripture passage="iiPet 1:7" parsed="|2Pet|1|7|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.7" />
<sup>7</sup>udugu katika uchaji wenu, na mapendo katika udugu wenu.
<scripture passage="iiPet 1:8" parsed="|2Pet|1|8|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.8" />
<sup>8</sup>Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iiPet 1:9" parsed="|2Pet|1|9|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.9" />
<sup>9</sup>Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.
<scripture passage="iiPet 1:10" parsed="|2Pet|1|10|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.10" />
<sup>10</sup>Kwa hiyo basi, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuufanya huo wito wenu mlioitiwa na Mungu uwe jambo la kudumu katika maisha yenu; kama mkiishi namna hiyo hamtaanguka kamwe.
<scripture passage="iiPet 1:11" parsed="|2Pet|1|11|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.11" />
<sup>11</sup>Kwa namna hiyo mtafaulu kupewa haki kamili ya kuingia katika Utawala wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="iiPet 1:12" parsed="|2Pet|1|12|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.12" />
<sup>12</sup>Kwa hiyo nitaendelea kuwakumbusheni daima mambo haya, ingawa mmekwisha yafahamu, na mko imara katika ukweli mlioupokea.
<scripture passage="iiPet 1:13" parsed="|2Pet|1|13|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.13" />
<sup>13</sup>Nadhani ni jambo jema kwangu, muda wote niishio hapa duniani, kuwapeni moyo na kuwakumbusheni juu ya mambo haya.
<scripture passage="iiPet 1:14" parsed="|2Pet|1|14|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.14" />
<sup>14</sup>Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama Bwana alivyoniambia waziwazi.
<scripture passage="iiPet 1:15" parsed="|2Pet|1|15|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.15" />
<sup>15</sup>Basi, nitajitahidi kuwapatieni njia ya kuyakumbuka mambo haya kila wakati, baada ya kufariki kwangu.
<scripture passage="iiPet 1:16" parsed="|2Pet|1|16|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.16" />
<sup>16</sup>Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona utukufu wake kwa macho yetu wenyewe.
<scripture passage="iiPet 1:17" parsed="|2Pet|1|17|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.17" />
<sup>17</sup>Sisi tulikuwapo wakati alipopewa heshima na kutukuzwa na Mungu Baba, wakati sauti ilipomjia kutoka kwake yeye aliye Utukufu Mkuu, ikisema: "Huyu ni Mwanangu mpenzi, nimependezwa naye."
<scripture passage="iiPet 1:18" parsed="|2Pet|1|18|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.18" />
<sup>18</sup>Tena, sisi wenyewe tulisikia sauti hiyo kutoka mbinguni wakati tulipokuwa pamoja naye juu ya ule mlima mtakatifu.
<scripture passage="iiPet 1:19" parsed="|2Pet|1|19|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.19" />
<sup>19</sup>Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka Siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong`ara mioyoni mwenu.
<scripture passage="iiPet 1:20" parsed="|2Pet|1|20|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.20" />
<sup>20</sup>Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
<scripture passage="iiPet 1:21" parsed="|2Pet|1|21|0|0" osisRef="Bible:2Pet.1.21" />
<sup>21</sup>Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe wa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Peter 2" progress="90.57%" prev="iiPet.1" next="iiPet.3" id="iiPet.2">
<h3 id="iiPet.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iiPet.2-p1">
<scripture passage="iiPet 2:1" parsed="|2Pet|2|1|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.1" />
<sup>1</sup>Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo walimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.
<scripture passage="iiPet 2:2" parsed="|2Pet|2|2|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.2" />
<sup>2</sup>Tena watu wengi watazifuata hizo njia zao mbaya, kwa sababu yao, wengine wataipuuza Njia ya ukweli.
<scripture passage="iiPet 2:3" parsed="|2Pet|2|3|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.3" />
<sup>3</sup>Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yu tayari, na Mwangamizi wao yu macho!
<scripture passage="iiPet 2:4" parsed="|2Pet|2|4|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.4" />
<sup>4</sup>Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea Siku ile ya Hukumu.
<scripture passage="iiPet 2:5" parsed="|2Pet|2|5|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.5" />
<sup>5</sup>Mungu hakuihurumia dunia ya hapo kale, bali alileta gharika kuu juu ya nchi ile ya watu wasiomcha Mungu; lakini Noa ambaye alihubiri uadilifu, Mungu alimwokoa pamoja na watu wengine saba.
<scripture passage="iiPet 2:6" parsed="|2Pet|2|6|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.6" />
<sup>6</sup>Mungu aliadhibu miji ya Sodoma na Gomora, akaiteketeza kwa moto, akaifanya iwe mfano wa mambo yatakayowapata watu wasiomcha Mungu.
<scripture passage="iiPet 2:7" parsed="|2Pet|2|7|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.7" />
<sup>7</sup>Alimwokoa Loti, mtu mwema, ambaye alisikitishwa sana na mwenendo mbaya wa watu hao waasi.
<scripture passage="iiPet 2:8" parsed="|2Pet|2|8|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.8" />
<sup>8</sup>Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
<scripture passage="iiPet 2:9" parsed="|2Pet|2|9|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.9" />
<sup>9</sup>Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi Siku ile ya hukumu,
<scripture passage="iiPet 2:10" parsed="|2Pet|2|10|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.10" />
<sup>10</sup>hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni washupavu na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.
<scripture passage="iiPet 2:11" parsed="|2Pet|2|11|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.11" />
<sup>11</sup>Lakini malaika, ambao wana uwezo na nguvu zaidi kuliko hao walimu wa uongo, hawawashtaki na kuwatukana hao mbele ya Bwana.
<scripture passage="iiPet 2:12" parsed="|2Pet|2|12|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.12" />
<sup>12</sup>Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili, ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,
<scripture passage="iiPet 2:13" parsed="|2Pet|2|13|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.13" />
<sup>13</sup>na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, bali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
<scripture passage="iiPet 2:14" parsed="|2Pet|2|14|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.14" />
<sup>14</sup>Macho yao yamejaa uzinzi na uwezo wao wa kutenda dhambi hauna kikomo. Huwaongoza watu walio dhaifu mpaka mitegoni. Mioyo yao imezoea kuwa na tamaa ya mali. Wapo chini ya laana ya Mungu!
<scripture passage="iiPet 2:15" parsed="|2Pet|2|15|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.15" />
<sup>15</sup>Wameiacha njia iliyonyoka, wakapotoka na kuifuata njia aliyofuata Balaamu, mwana wa Beori, ambaye alipendelea kupata faida kwa kufanya udanganyifu,
<scripture passage="iiPet 2:16" parsed="|2Pet|2|16|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.16" />
<sup>16</sup>akakaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena kwa sauti ya binadamu, akaukomesha wazimu wa huyo nabii.
<scripture passage="iiPet 2:17" parsed="|2Pet|2|17|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.17" />
<sup>17</sup>Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.
<scripture passage="iiPet 2:18" parsed="|2Pet|2|18|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.18" />
<sup>18</sup>Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.
<scripture passage="iiPet 2:19" parsed="|2Pet|2|19|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.19" />
<sup>19</sup>Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu--maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.
<scripture passage="iiPet 2:20" parsed="|2Pet|2|20|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.20" />
<sup>20</sup>Watu waliokwisha ponyoka katika upotovu wa ulimwengu kwa kupata kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kisha wakakubali kunaswa na kutawaliwa tena na upotovu huo, hali yao itakuwa mbaya zaidi kuliko awali.
<scripture passage="iiPet 2:21" parsed="|2Pet|2|21|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.21" />
<sup>21</sup>Ingalikuwa afadhali kwao kama wasingalijua kamwe njia hiyo ya uadilifu kuliko kujua na kisha kuiacha na kupoteza amri takatifu waliyopokea.
<scripture passage="iiPet 2:22" parsed="|2Pet|2|22|0|0" osisRef="Bible:2Pet.2.22" />
<sup>22</sup>Ipo mithali isemayo: "Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe," na nyingine isemayo: "Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!" Ndivyo ilivyo kwao sasa.
</p>
</div3>

<div3 title="2 Peter 3" progress="90.94%" prev="iiPet.2" next="iJohn" id="iiPet.3">
<h3 id="iiPet.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iiPet.3-p1">
<scripture passage="iiPet 3:1" parsed="|2Pet|3|1|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.1" />
<sup>1</sup>Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.
<scripture passage="iiPet 3:2" parsed="|2Pet|3|2|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.2" />
<sup>2</sup>Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa na mitume wenu.
<scripture passage="iiPet 3:3" parsed="|2Pet|3|3|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.3" />
<sup>3</sup>Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki ninyi
<scripture passage="iiPet 3:4" parsed="|2Pet|3|4|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.4" />
<sup>4</sup>na kusema: "Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi? Mambo ni yaleyale tangu babu zetu walipokufa; hali ya vitu ni ileile kama ilivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!"
<scripture passage="iiPet 3:5" parsed="|2Pet|3|5|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.5" />
<sup>5</sup>Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na nchi zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji;
<scripture passage="iiPet 3:6" parsed="|2Pet|3|6|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.6" />
<sup>6</sup>na kwa maji hayo, yaani yale maji ya gharika kuu, dunia ya wakati ule iliangamizwa.
<scripture passage="iiPet 3:7" parsed="|2Pet|3|7|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.7" />
<sup>7</sup>Lakini mbingu na nchi za sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya Siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.
<scripture passage="iiPet 3:8" parsed="|2Pet|3|8|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.8" />
<sup>8</sup>Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja.
<scripture passage="iiPet 3:9" parsed="|2Pet|3|9|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.9" />
<sup>9</sup>Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.
<scripture passage="iiPet 3:10" parsed="|2Pet|3|10|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.10" />
<sup>10</sup>Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
<scripture passage="iiPet 3:11" parsed="|2Pet|3|11|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.11" />
<sup>11</sup>Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je, ninyi mnapaswa kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu,
<scripture passage="iiPet 3:12" parsed="|2Pet|3|12|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.12" />
<sup>12</sup>mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi--Siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
<scripture passage="iiPet 3:13" parsed="|2Pet|3|13|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.13" />
<sup>13</sup>Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.
<scripture passage="iiPet 3:14" parsed="|2Pet|3|14|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.14" />
<sup>14</sup>Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnangojea Siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
<scripture passage="iiPet 3:15" parsed="|2Pet|3|15|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.15" />
<sup>15</sup>Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa na Mungu.
<scripture passage="iiPet 3:16" parsed="|2Pet|3|16|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.16" />
<sup>16</sup>Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
<scripture passage="iiPet 3:17" parsed="|2Pet|3|17|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.17" />
<sup>17</sup>Lakini ninyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.
<scripture passage="iiPet 3:18" parsed="|2Pet|3|18|0|0" osisRef="Bible:2Pet.3.18" />
<sup>18</sup>Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="1 John" progress="91.23%" prev="iiPet.3" next="iJohn.1" id="iJohn">
<h2 id="iJohn-p0.1">1 John</h2>

<div3 title="1 John 1" progress="91.23%" prev="iJohn" next="iJohn.2" id="iJohn.1">
<h3 id="iJohn.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iJohn.1-p1">
<scripture passage="iJohn 1:1" parsed="|1John|1|1|0|0" osisRef="Bible:1John.1.1" />
<sup>1</sup>Habari hii ya yahusu Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.
<scripture passage="iJohn 1:2" parsed="|1John|1|2|0|0" osisRef="Bible:1John.1.2" />
<sup>2</sup>Uzima huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uzima huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu.
<scripture passage="iJohn 1:3" parsed="|1John|1|3|0|0" osisRef="Bible:1John.1.3" />
<sup>3</sup>Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi pia ili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
<scripture passage="iJohn 1:4" parsed="|1John|1|4|0|0" osisRef="Bible:1John.1.4" />
<sup>4</sup>Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.
<scripture passage="iJohn 1:5" parsed="|1John|1|5|0|0" osisRef="Bible:1John.1.5" />
<sup>5</sup>Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.
<scripture passage="iJohn 1:6" parsed="|1John|1|6|0|0" osisRef="Bible:1John.1.6" />
<sup>6</sup>Tukisema kwamba tuna umoja naye,na papo hapo twaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo kwa maneno na matendo.
<scripture passage="iJohn 1:7" parsed="|1John|1|7|0|0" osisRef="Bible:1John.1.7" />
<sup>7</sup>Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote.
<scripture passage="iJohn 1:8" parsed="|1John|1|8|0|0" osisRef="Bible:1John.1.8" />
<sup>8</sup>Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe na ukweli haumo ndani yetu.
<scripture passage="iJohn 1:9" parsed="|1John|1|9|0|0" osisRef="Bible:1John.1.9" />
<sup>9</sup>Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
<scripture passage="iJohn 1:10" parsed="|1John|1|10|0|0" osisRef="Bible:1John.1.10" />
<sup>10</sup>Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 John 2" progress="91.36%" prev="iJohn.1" next="iJohn.3" id="iJohn.2">
<h3 id="iJohn.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="iJohn.2-p1">
<scripture passage="iJohn 2:1" parsed="|1John|2|1|0|0" osisRef="Bible:1John.2.1" />
<sup>1</sup>Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa.
<scripture passage="iJohn 2:2" parsed="|1John|2|2|0|0" osisRef="Bible:1John.2.2" />
<sup>2</sup>Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu; wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.
<scripture passage="iJohn 2:3" parsed="|1John|2|3|0|0" osisRef="Bible:1John.2.3" />
<sup>3</sup>Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua.
<scripture passage="iJohn 2:4" parsed="|1John|2|4|0|0" osisRef="Bible:1John.2.4" />
<sup>4</sup>Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake.
<scripture passage="iJohn 2:5" parsed="|1John|2|5|0|0" osisRef="Bible:1John.2.5" />
<sup>5</sup>Lakini mtu yeyote anayeshika neno la Mungu, huyo ndiye aliye na upendo kamili wa Mungu ndani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na hakika kwamba tunaungana naye:
<scripture passage="iJohn 2:6" parsed="|1John|2|6|0|0" osisRef="Bible:1John.2.6" />
<sup>6</sup>mtu yeyote anayesema kwamba ameungana na Mungu, anapaswa kuishi kama alivyoishi Yesu Kristo.
<scripture passage="iJohn 2:7" parsed="|1John|2|7|0|0" osisRef="Bible:1John.2.7" />
<sup>7</sup>Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.
<scripture passage="iJohn 2:8" parsed="|1John|2|8|0|0" osisRef="Bible:1John.2.8" />
<sup>8</sup>Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa ukweli umekwisha anza kuangaza.
<scripture passage="iJohn 2:9" parsed="|1John|2|9|0|0" osisRef="Bible:1John.2.9" />
<sup>9</sup>Yeyote asemaye kwamba yumo katika mwanga, lakini anamchukia ndugu yake, mtu huyo bado yumo gizani.
<scripture passage="iJohn 2:10" parsed="|1John|2|10|0|0" osisRef="Bible:1John.2.10" />
<sup>10</sup>Yeyote ampendaye ndugu yake, yuko katika mwanga, na hamna chochote ndani yake kiwezacho kumkwaza mtu mwingine.
<scripture passage="iJohn 2:11" parsed="|1John|2|11|0|0" osisRef="Bible:1John.2.11" />
<sup>11</sup>Lakini anayemchukia ndugu yake, yumo gizani; anatembea gizani, na hajui anakokwenda, maana giza limempofusha.
<scripture passage="iJohn 2:12" parsed="|1John|2|12|0|0" osisRef="Bible:1John.2.12" />
<sup>12</sup>Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa kuwa dhambi zenu zimeondolewa kwa jina la Kristo.
<scripture passage="iJohn 2:13" parsed="|1John|2|13|0|0" osisRef="Bible:1John.2.13" />
<sup>13</sup>Nawaandikieni ninyi kina baba kwani mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo, Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mmemshinda yule Mwovu.
<scripture passage="iJohn 2:14" parsed="|1John|2|14|0|0" osisRef="Bible:1John.2.14" />
<sup>14</sup>Nawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni ninyi kina baba, kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mmemshinda yule Mwovu.
<scripture passage="iJohn 2:15" parsed="|1John|2|15|0|0" osisRef="Bible:1John.2.15" />
<sup>15</sup>Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.
<scripture passage="iJohn 2:16" parsed="|1John|2|16|0|0" osisRef="Bible:1John.2.16" />
<sup>16</sup>Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.
<scripture passage="iJohn 2:17" parsed="|1John|2|17|0|0" osisRef="Bible:1John.2.17" />
<sup>17</sup>Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.
<scripture passage="iJohn 2:18" parsed="|1John|2|18|0|0" osisRef="Bible:1John.2.18" />
<sup>18</sup>Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba adui wa Kristo anakuja, na sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.
<scripture passage="iJohn 2:19" parsed="|1John|2|19|0|0" osisRef="Bible:1John.2.19" />
<sup>19</sup>Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; Kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu.
<scripture passage="iJohn 2:20" parsed="|1John|2|20|0|0" osisRef="Bible:1John.2.20" />
<sup>20</sup>Ninyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujua ukweli.
<scripture passage="iJohn 2:21" parsed="|1John|2|21|0|0" osisRef="Bible:1John.2.21" />
<sup>21</sup>Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamuujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
<scripture passage="iJohn 2:22" parsed="|1John|2|22|0|0" osisRef="Bible:1John.2.22" />
<sup>22</sup>Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha. Mtu wa namna hiyo ni adui wa Kristo--anamkana Baba na Mwana.
<scripture passage="iJohn 2:23" parsed="|1John|2|23|0|0" osisRef="Bible:1John.2.23" />
<sup>23</sup>Maana yeyote anayemkana Mwana, anamkana pia Baba; na yeyote anayemkubali Mwana, anampata Baba pia.
<scripture passage="iJohn 2:24" parsed="|1John|2|24|0|0" osisRef="Bible:1John.2.24" />
<sup>24</sup>Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae mioyoni mwenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishi daima katika umoja na Mwana na Baba.
<scripture passage="iJohn 2:25" parsed="|1John|2|25|0|0" osisRef="Bible:1John.2.25" />
<sup>25</sup>Na ahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: uzima wa milele.
<scripture passage="iJohn 2:26" parsed="|1John|2|26|0|0" osisRef="Bible:1John.2.26" />
<sup>26</sup>Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha ninyi.
<scripture passage="iJohn 2:27" parsed="|1John|2|27|0|0" osisRef="Bible:1John.2.27" />
<sup>27</sup>Lakini, kwa upande wenu ninyi, Kristo aliwamiminieni Roho wake. Na kama akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana Roho wake anawafundisheni kila kitu na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo.
<scripture passage="iJohn 2:28" parsed="|1John|2|28|0|0" osisRef="Bible:1John.2.28" />
<sup>28</sup>Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu Siku ya kuja kwake.
<scripture passage="iJohn 2:29" parsed="|1John|2|29|0|0" osisRef="Bible:1John.2.29" />
<sup>29</sup>Mnajua kwamba Kristo ni mwadilifu kabisa; basi, mnapaswa kujua pia kwamba kila mtu atendaye mambo adili ni mtoto wa Mungu.
</p>
</div3>

<div3 title="1 John 3" progress="91.78%" prev="iJohn.2" next="iJohn.4" id="iJohn.3">
<h3 id="iJohn.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="iJohn.3-p1">
<scripture passage="iJohn 3:1" parsed="|1John|3|1|0|0" osisRef="Bible:1John.3.1" />
<sup>1</sup>Oneni basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.
<scripture passage="iJohn 3:2" parsed="|1John|3|2|0|0" osisRef="Bible:1John.3.2" />
<sup>2</sup>Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa, lakini bado haijaonekana wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba wakati Kristo atakapotokea, tutafanana naye kwani tutamwona vile alivyo.
<scripture passage="iJohn 3:3" parsed="|1John|3|3|0|0" osisRef="Bible:1John.3.3" />
<sup>3</sup>Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa.
<scripture passage="iJohn 3:4" parsed="|1John|3|4|0|0" osisRef="Bible:1John.3.4" />
<sup>4</sup>Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria.
<scripture passage="iJohn 3:5" parsed="|1John|3|5|0|0" osisRef="Bible:1John.3.5" />
<sup>5</sup>Mnajua kwamba Kristo alikuja kuziondoa dhambi zetu, na kwamba kwake hamna dhambi yoyote.
<scripture passage="iJohn 3:6" parsed="|1John|3|6|0|0" osisRef="Bible:1John.3.6" />
<sup>6</sup>Basi, kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi dhambi; lakini kila mtu atendaye dhambi hakupata kamwe kumwona, wala kumjua Kristo.
<scripture passage="iJohn 3:7" parsed="|1John|3|7|0|0" osisRef="Bible:1John.3.7" />
<sup>7</sup>Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa.
<scripture passage="iJohn 3:8" parsed="|1John|3|8|0|0" osisRef="Bible:1John.3.8" />
<sup>8</sup>Lakini atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maana Ibilisi ametenda dhambi tangu mwanzo. Lakini Mwana wa Mungu alikuja duniani kuiharibu kazi ya Ibilisi.
<scripture passage="iJohn 3:9" parsed="|1John|3|9|0|0" osisRef="Bible:1John.3.9" />
<sup>9</sup>Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.
<scripture passage="iJohn 3:10" parsed="|1John|3|10|0|0" osisRef="Bible:1John.3.10" />
<sup>10</sup>Lakini yeyote asiyetenda mambo maadilifu, au asiyempenda ndugu yake, huyo si mtoto wa Mungu. Hiyo ndiyo tofauti iliyoko kati ya watoto wa Mungu na watoto wa Ibilisi.
<scripture passage="iJohn 3:11" parsed="|1John|3|11|0|0" osisRef="Bible:1John.3.11" />
<sup>11</sup>Na, ujumbe mliousikia tangu mwanzo ndio huu: Tunapaswa kupendana!
<scripture passage="iJohn 3:12" parsed="|1John|3|12|0|0" osisRef="Bible:1John.3.12" />
<sup>12</sup>Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!
<scripture passage="iJohn 3:13" parsed="|1John|3|13|0|0" osisRef="Bible:1John.3.13" />
<sup>13</sup>Basi, ndugu zangu, msishangae kama ulimwengu unawachukia ninyi.
<scripture passage="iJohn 3:14" parsed="|1John|3|14|0|0" osisRef="Bible:1John.3.14" />
<sup>14</sup>Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uzima kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo.
<scripture passage="iJohn 3:15" parsed="|1John|3|15|0|0" osisRef="Bible:1John.3.15" />
<sup>15</sup>Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uzima wa milele ndani yake.
<scripture passage="iJohn 3:16" parsed="|1John|3|16|0|0" osisRef="Bible:1John.3.16" />
<sup>16</sup>Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
<scripture passage="iJohn 3:17" parsed="|1John|3|17|0|0" osisRef="Bible:1John.3.17" />
<sup>17</sup>Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma, anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu?
<scripture passage="iJohn 3:18" parsed="|1John|3|18|0|0" osisRef="Bible:1John.3.18" />
<sup>18</sup>Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.
<scripture passage="iJohn 3:19" parsed="|1John|3|19|0|0" osisRef="Bible:1John.3.19" />
<sup>19</sup>Hivyo ndivyo tuwezavyo kuwa na hakika kwamba sisi ni watu wa ukweli; na hatutakuwa na wasiwasi mbele ya Mungu.
<scripture passage="iJohn 3:20" parsed="|1John|3|20|0|0" osisRef="Bible:1John.3.20" />
<sup>20</sup>Kwa maana, hata kama dhamiri yetu yatuhukumu, twajua kwamba Mungu ni mkuu zaidi kuliko dhamiri, na kwamba yeye ajua kila kitu.
<scripture passage="iJohn 3:21" parsed="|1John|3|21|0|0" osisRef="Bible:1John.3.21" />
<sup>21</sup>Wapenzi wangu, kama dhamiri yetu haina lawama juu yetu, basi, twaweza kuwa na uthabiti mbele ya Mungu,
<scripture passage="iJohn 3:22" parsed="|1John|3|22|0|0" osisRef="Bible:1John.3.22" />
<sup>22</sup>na twaweza kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.
<scripture passage="iJohn 3:23" parsed="|1John|3|23|0|0" osisRef="Bible:1John.3.23" />
<sup>23</sup>Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.
<scripture passage="iJohn 3:24" parsed="|1John|3|24|0|0" osisRef="Bible:1John.3.24" />
<sup>24</sup>Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.
</p>
</div3>

<div3 title="1 John 4" progress="92.10%" prev="iJohn.3" next="iJohn.5" id="iJohn.4">
<h3 id="iJohn.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="iJohn.4-p1">
<scripture passage="iJohn 4:1" parsed="|1John|4|1|0|0" osisRef="Bible:1John.4.1" />
<sup>1</sup>Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni.
<scripture passage="iJohn 4:2" parsed="|1John|4|2|0|0" osisRef="Bible:1John.4.2" />
<sup>2</sup>Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa Mungu.
<scripture passage="iJohn 4:3" parsed="|1John|4|3|0|0" osisRef="Bible:1John.4.3" />
<sup>3</sup>Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni!
<scripture passage="iJohn 4:4" parsed="|1John|4|4|0|0" osisRef="Bible:1John.4.4" />
<sup>4</sup>Lakini ninyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu zaidi kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu.
<scripture passage="iJohn 4:5" parsed="|1John|4|5|0|0" osisRef="Bible:1John.4.5" />
<sup>5</sup>Wao husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani wao ni wa ulimwengu.
<scripture passage="iJohn 4:6" parsed="|1John|4|6|0|0" osisRef="Bible:1John.4.6" />
<sup>6</sup>Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.
<scripture passage="iJohn 4:7" parsed="|1John|4|7|0|0" osisRef="Bible:1John.4.7" />
<sup>7</sup>Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
<scripture passage="iJohn 4:8" parsed="|1John|4|8|0|0" osisRef="Bible:1John.4.8" />
<sup>8</sup>Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo.
<scripture passage="iJohn 4:9" parsed="|1John|4|9|0|0" osisRef="Bible:1John.4.9" />
<sup>9</sup>Na Mungu alionyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake.
<scripture passage="iJohn 4:10" parsed="|1John|4|10|0|0" osisRef="Bible:1John.4.10" />
<sup>10</sup>Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kutuondolea dhambi zetu.
<scripture passage="iJohn 4:11" parsed="|1John|4|11|0|0" osisRef="Bible:1John.4.11" />
<sup>11</sup>Wapenzi wangu, ikiwa Mungu alitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswa kupendana.
<scripture passage="iJohn 4:12" parsed="|1John|4|12|0|0" osisRef="Bible:1John.4.12" />
<sup>12</sup>Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
<scripture passage="iJohn 4:13" parsed="|1John|4|13|0|0" osisRef="Bible:1John.4.13" />
<sup>13</sup>Tunajua kwamba tunaishi katika umoja na Mungu, naye Mungu anaishi katika umoja nasi, kwani yeye ametupa Roho wake.
<scripture passage="iJohn 4:14" parsed="|1John|4|14|0|0" osisRef="Bible:1John.4.14" />
<sup>14</sup>Sisi tumeona na kuwaambia wengine kwamba Baba alimtuma Mwanae awe Mwokozi wa ulimwengu.
<scripture passage="iJohn 4:15" parsed="|1John|4|15|0|0" osisRef="Bible:1John.4.15" />
<sup>15</sup>Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu.
<scripture passage="iJohn 4:16" parsed="|1John|4|16|0|0" osisRef="Bible:1John.4.16" />
<sup>16</sup>Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye.
<scripture passage="iJohn 4:17" parsed="|1John|4|17|0|0" osisRef="Bible:1John.4.17" />
<sup>17</sup>Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri Siku ile ya Hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo.
<scripture passage="iJohn 4:18" parsed="|1John|4|18|0|0" osisRef="Bible:1John.4.18" />
<sup>18</sup>Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza uoga wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga huhusikana na adhabu.
<scripture passage="iJohn 4:19" parsed="|1John|4|19|0|0" osisRef="Bible:1John.4.19" />
<sup>19</sup>Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
<scripture passage="iJohn 4:20" parsed="|1John|4|20|0|0" osisRef="Bible:1John.4.20" />
<sup>20</sup>Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.
<scripture passage="iJohn 4:21" parsed="|1John|4|21|0|0" osisRef="Bible:1John.4.21" />
<sup>21</sup>Basi, hii ndiyo amri aliyotupa Kristo: Anayempenda Mungu anapaswa pia kumpenda ndugu yake.
</p>
</div3>

<div3 title="1 John 5" progress="92.40%" prev="iJohn.4" next="iiJohn" id="iJohn.5">
<h3 id="iJohn.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="iJohn.5-p1">
<scripture passage="iJohn 5:1" parsed="|1John|5|1|0|0" osisRef="Bible:1John.5.1" />
<sup>1</sup>Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu; na, anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
<scripture passage="iJohn 5:2" parsed="|1John|5|2|0|0" osisRef="Bible:1John.5.2" />
<sup>2</sup>Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake;
<scripture passage="iJohn 5:3" parsed="|1John|5|3|0|0" osisRef="Bible:1John.5.3" />
<sup>3</sup>maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu,
<scripture passage="iJohn 5:4" parsed="|1John|5|4|0|0" osisRef="Bible:1John.5.4" />
<sup>4</sup>maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: kwa imani yetu.
<scripture passage="iJohn 5:5" parsed="|1John|5|5|0|0" osisRef="Bible:1John.5.5" />
<sup>5</sup>Nani, basi, awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yule anayeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
<scripture passage="iJohn 5:6" parsed="|1John|5|6|0|0" osisRef="Bible:1John.5.6" />
<sup>6</sup>Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli.
<scripture passage="iJohn 5:7" parsed="|1John|5|7|0|0" osisRef="Bible:1John.5.7" />
<sup>7</sup>Basi, wako mashahidi watatu:
<scripture passage="iJohn 5:8" parsed="|1John|5|8|0|0" osisRef="Bible:1John.5.8" />
<sup>8</sup>Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana.
<scripture passage="iJohn 5:9" parsed="|1John|5|9|0|0" osisRef="Bible:1John.5.9" />
<sup>9</sup>Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae.
<scripture passage="iJohn 5:10" parsed="|1John|5|10|0|0" osisRef="Bible:1John.5.10" />
<sup>10</sup>Anayemwamini mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae.
<scripture passage="iJohn 5:11" parsed="|1John|5|11|0|0" osisRef="Bible:1John.5.11" />
<sup>11</sup>Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uzima wa milele, na uzima huo uko kwa Bwana.
<scripture passage="iJohn 5:12" parsed="|1John|5|12|0|0" osisRef="Bible:1John.5.12" />
<sup>12</sup>Yeyote, aliye na Mwana wa Mungu anao uzima huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uzima.
<scripture passage="iJohn 5:13" parsed="|1John|5|13|0|0" osisRef="Bible:1John.5.13" />
<sup>13</sup>Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uzima wa milele ninyi mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu.
<scripture passage="iJohn 5:14" parsed="|1John|5|14|0|0" osisRef="Bible:1John.5.14" />
<sup>14</sup>Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya mapenzi yake, yeye hutusikiliza.
<scripture passage="iJohn 5:15" parsed="|1John|5|15|0|0" osisRef="Bible:1John.5.15" />
<sup>15</sup>Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba atupatia yote tunayomwomba.
<scripture passage="iJohn 5:16" parsed="|1John|5|16|0|0" osisRef="Bible:1John.5.16" />
<sup>16</sup>Mtu akimwona ndugu yake ametenda dhambi isiyompeleka kwenye kifo anapaswa kumwombea kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Nasema jambo hili kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi yenye kumpeleka mtu kwenye kifo nami sisemi kwamba mnapaswa kumwomba Mungu kwa ajili ya hiyo.
<scripture passage="iJohn 5:17" parsed="|1John|5|17|0|0" osisRef="Bible:1John.5.17" />
<sup>17</sup>Kila tendo lisilo adilifu ni dhambi, lakini kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
<scripture passage="iJohn 5:18" parsed="|1John|5|18|0|0" osisRef="Bible:1John.5.18" />
<sup>18</sup>Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru.
<scripture passage="iJohn 5:19" parsed="|1John|5|19|0|0" osisRef="Bible:1John.5.19" />
<sup>19</sup>Tunajua kwamba sisi ni wake Mungu ingawa ulimwengu wote unatawaliwa na yule Mwovu.
<scripture passage="iJohn 5:20" parsed="|1John|5|20|0|0" osisRef="Bible:1John.5.20" />
<sup>20</sup>Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli--katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uzima wa milele.
<scripture passage="iJohn 5:21" parsed="|1John|5|21|0|0" osisRef="Bible:1John.5.21" />
<sup>21</sup>Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="2 John" progress="92.66%" prev="iJohn.5" next="iiJohn.1" id="iiJohn">
<h2 id="iiJohn-p0.1">2 John</h2>

<div3 title="2 John 1" progress="92.67%" prev="iiJohn" next="iiiJohn" id="iiJohn.1">
<h3 id="iiJohn.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiJohn.1-p1">
<scripture passage="iiJohn 1:1" parsed="|2John|1|1|0|0" osisRef="Bible:2John.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Mzee nakuandikia wewe Bimkubwa mteule, pamoja na watoto wako ninaowapenda kweli. Wala si mimi tu ninayewapenda, bali pia wote wanaoujua ule ukweli wanawapenda ninyi,
<scripture passage="iiJohn 1:2" parsed="|2John|1|2|0|0" osisRef="Bible:2John.1.2" />
<sup>2</sup>kwa sababu ukweli unakaa nasi milele.
<scripture passage="iiJohn 1:3" parsed="|2John|1|3|0|0" osisRef="Bible:2John.1.3" />
<sup>3</sup>Neema na huruma na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika ukweli na upendo.
<scripture passage="iiJohn 1:4" parsed="|2John|1|4|0|0" osisRef="Bible:2John.1.4" />
<sup>4</sup>Nilifurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanaishi katika ukweli kama Baba alivyotuamuru.
<scripture passage="iiJohn 1:5" parsed="|2John|1|5|0|0" osisRef="Bible:2John.1.5" />
<sup>5</sup>Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.
<scripture passage="iiJohn 1:6" parsed="|2John|1|6|0|0" osisRef="Bible:2John.1.6" />
<sup>6</sup>Upendo maana yake ni kuishi kwa kuzitii amri zake Mungu. Amri niliyoisikia tangu mwanzo ndiyo hii: mnapaswa nyote kuishi katika upendo.
<scripture passage="iiJohn 1:7" parsed="|2John|1|7|0|0" osisRef="Bible:2John.1.7" />
<sup>7</sup>Wadanganyifu wengi wamezuka duniani, watu ambao hawakiri kwamba Yesu Kristo amekuja kwetu akawa binadamu. Mtu asemaye hivyo ni mdanganyifu na ni Adui wa Kristo.
<scripture passage="iiJohn 1:8" parsed="|2John|1|8|0|0" osisRef="Bible:2John.1.8" />
<sup>8</sup>Basi, jihadharini ninyi wenyewe ili msije mkapoteza kile mlichokishugulikia, bali mpate tuzo lenu kamili.
<scripture passage="iiJohn 1:9" parsed="|2John|1|9|0|0" osisRef="Bible:2John.1.9" />
<sup>9</sup>Asiyezingatia na kudumu katika mafundisho ya Kristo, bali anayakiuka, hana Mungu. Lakini anayedumu katika mafundisho hayo anaye Baba na Mwana.
<scripture passage="iiJohn 1:10" parsed="|2John|1|10|0|0" osisRef="Bible:2John.1.10" />
<sup>10</sup>Basi, kama mtu akija kwenu bila kuwaleteeni mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu.
<scripture passage="iiJohn 1:11" parsed="|2John|1|11|0|0" osisRef="Bible:2John.1.11" />
<sup>11</sup>Maana anayemsalimu mtu huyo, anashirikiana naye katika matendo yake maovu.
<scripture passage="iiJohn 1:12" parsed="|2John|1|12|0|0" osisRef="Bible:2John.1.12" />
<sup>12</sup>Ninayo mengi ya kuwaambieni lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
<scripture passage="iiJohn 1:13" parsed="|2John|1|13|0|0" osisRef="Bible:2John.1.13" />
<sup>13</sup>Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="3 John" progress="92.83%" prev="iiJohn.1" next="iiiJohn.1" id="iiiJohn">
<h2 id="iiiJohn-p0.1">3 John</h2>

<div3 title="3 John 1" progress="92.83%" prev="iiiJohn" next="Jude" id="iiiJohn.1">
<h3 id="iiiJohn.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="iiiJohn.1-p1">
<scripture passage="iiiJohn 1:1" parsed="|3John|1|1|0|0" osisRef="Bible:3John.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, rafiki yangu, ninayekupenda kweli.
<scripture passage="iiiJohn 1:2" parsed="|3John|1|2|0|0" osisRef="Bible:3John.1.2" />
<sup>2</sup>Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni.
<scripture passage="iiiJohn 1:3" parsed="|3John|1|3|0|0" osisRef="Bible:3John.1.3" />
<sup>3</sup>Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakaiambia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
<scripture passage="iiiJohn 1:4" parsed="|3John|1|4|0|0" osisRef="Bible:3John.1.4" />
<sup>4</sup>Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishi katika ukweli.
<scripture passage="iiiJohn 1:5" parsed="|3John|1|5|0|0" osisRef="Bible:3John.1.5" />
<sup>5</sup>Mpenzi wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu, hata kama ni wageni.
<scripture passage="iiiJohn 1:6" parsed="|3John|1|6|0|0" osisRef="Bible:3John.1.6" />
<sup>6</sup>Ndugu hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali uwasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu,
<scripture passage="iiiJohn 1:7" parsed="|3John|1|7|0|0" osisRef="Bible:3John.1.7" />
<sup>7</sup>Maana wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini.
<scripture passage="iiiJohn 1:8" parsed="|3John|1|8|0|0" osisRef="Bible:3John.1.8" />
<sup>8</sup>Basi, sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushiriki katika kazi yao kwa ajili ya ukweli.
<scripture passage="iiiJohn 1:9" parsed="|3John|1|9|0|0" osisRef="Bible:3John.1.9" />
<sup>9</sup>Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
<scripture passage="iiiJohn 1:10" parsed="|3John|1|10|0|0" osisRef="Bible:3John.1.10" />
<sup>10</sup>Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuzia nje ya kanisa.
<scripture passage="iiiJohn 1:11" parsed="|3John|1|11|0|0" osisRef="Bible:3John.1.11" />
<sup>11</sup>Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
<scripture passage="iiiJohn 1:12" parsed="|3John|1|12|0|0" osisRef="Bible:3John.1.12" />
<sup>12</sup>Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli.
<scripture passage="iiiJohn 1:13" parsed="|3John|1|13|0|0" osisRef="Bible:3John.1.13" />
<sup>13</sup>Ninayo bado mengi ya kukwambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino.
<scripture passage="iiiJohn 1:14" parsed="|3John|1|14|0|0" osisRef="Bible:3John.1.14" />
<sup>14</sup>Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.
<scripture passage="iiiJohn 1:15" parsed="|3John|1|15|0|0" osisRef="Bible:3John.1.15" />
<sup>15</sup>Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kila mmoja binafsi.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Jude" progress="93.01%" prev="iiiJohn.1" next="Jude.1" id="Jude">
<h2 id="Jude-p0.1">Jude</h2>

<div3 title="Jude 1" progress="93.01%" prev="Jude" next="Rev" id="Jude.1">
<h3 id="Jude.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Jude.1-p1">
<scripture passage="Jude 1:1" parsed="|Jude|1|1|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.1" />
<sup>1</sup>Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo.
<scripture passage="Jude 1:2" parsed="|Jude|1|2|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.2" />
<sup>2</sup>Nawatakieni huruma, amani na upendo kwa wingi.
<scripture passage="Jude 1:3" parsed="|Jude|1|3|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.3" />
<sup>3</sup>Ndugu wapenzi, wakati nimo katika jitihada ya kuwaandikieni juu ya ule wokovu tunaoshiriki sote, nimeona lazima ya kuwaandikieni na kuwahimizeni mwendelee kupigana kwa ajili ya imani ambayo Mungu amewajalia watu wake mara moja tu kwa wakati wote.
<scripture passage="Jude 1:4" parsed="|Jude|1|4|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.4" />
<sup>4</sup>Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake kiongozi na Bwana wetu. Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu awali hukumu inayowangojea watu hao.
<scripture passage="Jude 1:5" parsed="|Jude|1|5|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.5" />
<sup>5</sup>Nataka kuwakumbusheni mambo fulani ambayo mmekwisha yajua: kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
<scripture passage="Jude 1:6" parsed="|Jude|1|6|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.6" />
<sup>6</sup>Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe Siku ile kuu.
<scripture passage="Jude 1:7" parsed="|Jude|1|7|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.7" />
<sup>7</sup>Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote.
<scripture passage="Jude 1:8" parsed="|Jude|1|8|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.8" />
<sup>8</sup>Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. ndoto zao huwaongoza katika kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu.
<scripture passage="Jude 1:9" parsed="|Jude|1|9|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.9" />
<sup>9</sup>Hata Mikaeli, malaika mkuu, hakufanya hivyo. Katika ule ubishi kati yake na Ibilisi waliobishana juu ya mwili wa Mose, Mikaeli hakuthubutu kumhukumu Ibilisi kwa matusi; ila alisema: "Bwana mwenyewe na akukaripie."
<scripture passage="Jude 1:10" parsed="|Jude|1|10|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.10" />
<sup>10</sup>Lakini watu hawa hutukana chochote wasichokielewa; mambo yaleyale wanayoyajua kwa silika kama vile wanyama wanayoyajua ndiyo yanayowaangamiza.
<scripture passage="Jude 1:11" parsed="|Jude|1|11|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.11" />
<sup>11</sup>Ole wao! Watu hao wamefuata mwenendo uleule wa Kaini. Kwa ajili ya fedha, wamejiingiza katika mkosi uleule wa Baalamu. Wameasi kama Kora alivyoasi na wameangamizwa kama yeye alivyoangamizwa.
<scripture passage="Jude 1:12" parsed="|Jude|1|12|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.12" />
<sup>12</sup>Kwa makelele yao yasiyo na adabu, watu hao ni kama madoa machafu katika mikutano yenu ya karamu ya Bwana. Hujipendelea wao wenyewe tu, na wako kama mawingu yanayopeperushwa huko na huko na upepo bila ya kuleta mvua. Wao ni kama miti isiyozaa matunda hata wakati wa majira yake, wamekufa kabisa.
<scripture passage="Jude 1:13" parsed="|Jude|1|13|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.13" />
<sup>13</sup>Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu yanaonekana dhahiri kama vile mapovu ya mawimbi. Wao ni kama nyota zinazotangatanga, ambao Mungu amewawekea mahali pao milele katika giza kuu.
<scripture passage="Jude 1:14" parsed="|Jude|1|14|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.14" />
<sup>14</sup>Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hawa: "Sikilizeni! Bwana atakuja pamoja na maelfu ya malaika wake watakatifu
<scripture passage="Jude 1:15" parsed="|Jude|1|15|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.15" />
<sup>15</sup>kutoa hukumu juu ya binadamu wote, kuwahukumu wote kwa ajili ya matendo yao yote maovu waliyotenda na kwa ajili ya maneno yote mabaya ambayo watu waovu walimkashifu nayo."
<scripture passage="Jude 1:16" parsed="|Jude|1|16|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.16" />
<sup>16</sup>Watu hawa wananung`unika daima na kuwalaumu watu wengine. Hufuata tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kusudi wafaulu katika mipango yao.
<scripture passage="Jude 1:17" parsed="|Jude|1|17|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.17" />
<sup>17</sup>Lakini ninyi wapenzi wangu, kumbukeni yale mliyoambiwa hapo awali ni mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo.
<scripture passage="Jude 1:18" parsed="|Jude|1|18|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.18" />
<sup>18</sup>Waliwaambieni: "Siku za mwisho zitakapofika, watatokea watu watakaowadhihaki ninyi, watu wafuatao tamaa zao mbaya."
<scripture passage="Jude 1:19" parsed="|Jude|1|19|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.19" />
<sup>19</sup>Hao ndio watu wanaosababisha mafarakano, watu wanaotawaliwa na tamaa zao za kidunia, watu wasio na Roho wa Mungu.
<scripture passage="Jude 1:20" parsed="|Jude|1|20|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.20" />
<sup>20</sup>Lakini ninyi, wapenzi wangu, endeleeni kujijenga kikamilifu katika imani yenu takatifu. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
<scripture passage="Jude 1:21" parsed="|Jude|1|21|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.21" />
<sup>21</sup>na kubaki katika upendo wa Mungu, mkiwa mnamngojea Bwana wetu Yesu Kristo awapeni uzima wa milele kwa huruma yake.
<scripture passage="Jude 1:22" parsed="|Jude|1|22|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.22" />
<sup>22</sup>Muwe na huruma kwa watu walio na mashaka;
<scripture passage="Jude 1:23" parsed="|Jude|1|23|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.23" />
<sup>23</sup>waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni; na kwa wengine muwe na huruma pamoja na hofu, lakini chukieni hata mavazi yao ambayo yamechafuliwa na tamaa zao mbaya.
<scripture passage="Jude 1:24" parsed="|Jude|1|24|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.24" />
<sup>24</sup>Kwake yeye awezaye kuwalinda msije mkaanguka, na kuwaleta ninyi bila hatia mpaka mbele ya utukufu wake,
<scripture passage="Jude 1:25" parsed="|Jude|1|25|0|0" osisRef="Bible:Jude.1.25" />
<sup>25</sup>kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina.
</p>
</div3>
</div2>

<div2 title="Revelation" progress="93.44%" prev="Jude.1" next="Rev.1" id="Rev">
<h2 id="Rev-p0.1">Revelation</h2>

<div3 title="Revelation 1" progress="93.44%" prev="Rev" next="Rev.2" id="Rev.1">
<h3 id="Rev.1-p0.1">Chapter 1</h3>
<p id="Rev.1-p1">
<scripture passage="Rev 1:1" parsed="|Rev|1|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.1" />
<sup>1</sup>Hizi ni habari za mambo ambayo yalifunuliwa na Yesu Kristo. Mungu alimpa Kristo ufunuo huu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo yanapaswa kutukia karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe Yohane, mtumishi wake, mambo hayo,
<scripture passage="Rev 1:2" parsed="|Rev|1|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.2" />
<sup>2</sup>naye Yohane, ameyasema yote aliyoyaona. Na hii ndio taarifa yake kuhusu ujumbe wa Mungu na ukweli uliofunuliwa na Yesu Kristo.
<scripture passage="Rev 1:3" parsed="|Rev|1|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.3" />
<sup>3</sup>Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki; heri yao wale wanaosikiliza maneno ya ujumbe huu wa kinabii na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia ambapo mambo haya yatatukia.
<scripture passage="Rev 1:4" parsed="|Rev|1|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.4" />
<sup>4</sup>Mimi Yohane nayaandikia makanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
<scripture passage="Rev 1:5" parsed="|Rev|1|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.5" />
<sup>5</sup>na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda, na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vya dhambi zetu,
<scripture passage="Rev 1:6" parsed="|Rev|1|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.6" />
<sup>6</sup>akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina.
<scripture passage="Rev 1:7" parsed="|Rev|1|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.7" />
<sup>7</sup>Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
<scripture passage="Rev 1:8" parsed="|Rev|1|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.8" />
<sup>8</sup>"Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
<scripture passage="Rev 1:9" parsed="|Rev|1|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.9" />
<sup>9</sup>Mimi ni Yohane, ndugu yenu; na kwa kuungana na Kristo nashiriki pamoja nanyi katika kustahimili mateso yanayowapata wale walio wa Utawala wake. Mimi nilikuwa kisiwani Patmo kwa sababu ya kuhubiri ujumbe wa Mungu na ukweli wa Yesu.
<scripture passage="Rev 1:10" parsed="|Rev|1|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.10" />
<sup>10</sup>Basi, wakati mmoja, siku ya Bwana, nilikumbwa na Roho, nikasikia nyuma yangu sauti kubwa kama sauti ya tarumbeta.
<scripture passage="Rev 1:11" parsed="|Rev|1|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.11" />
<sup>11</sup>Nayo ilisema, "Andika katika kitabu yote unayoyaona, ukipeleke kwa makanisa haya saba: Efeso, Smurna, Pergamoni, Thuatira, Sarde, Filadelfia na Laodikea."
<scripture passage="Rev 1:12" parsed="|Rev|1|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.12" />
<sup>12</sup>Basi, nikageuka nimwone huyo aliyesema nami, nikaona vinara vya taa saba vya dhahabu,
<scripture passage="Rev 1:13" parsed="|Rev|1|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.13" />
<sup>13</sup>na katikati yake kulikuwa na kitu kama mtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na ukanda wa dhahabu kifuani.
<scripture passage="Rev 1:14" parsed="|Rev|1|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.14" />
<sup>14</sup>Nywele zake zilikuwa nyeupe kama pamba safi, kama theluji; macho yake yalimetameta kama moto;
<scripture passage="Rev 1:15" parsed="|Rev|1|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.15" />
<sup>15</sup>miguu yake iling`aa kama shaba iliyosafishwa katika tanuru ya moto na kusuguliwa, na sauti yake ilikuwa, kama sauti ya poromoko la maji.
<scripture passage="Rev 1:16" parsed="|Rev|1|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.16" />
<sup>16</sup>Katika mkono wake wa kulia, alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling`aa kama jua kali.
<scripture passage="Rev 1:17" parsed="|Rev|1|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.17" />
<sup>17</sup>Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbele ya miguu yake kama maiti. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akasema, "Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.
<scripture passage="Rev 1:18" parsed="|Rev|1|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.18" />
<sup>18</sup>Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa, lakini, tazama, sasa ni mzima milele na milele. Ninazo funguo za kifo na Kuzimu.
<scripture passage="Rev 1:19" parsed="|Rev|1|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.19" />
<sup>19</sup>Basi, sasa andika mambo haya unayoyaona, mambo yanayotukia sasa na yale yatakayotukia baadaye.
<scripture passage="Rev 1:20" parsed="|Rev|1|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.1.20" />
<sup>20</sup>Siri ya nyota zile saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia, na siri ya vile vinara saba vya taa hii: zile nyota saba ni malaika wa makanisa; na vile vinara saba vya taa ni makanisa saba.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 2" progress="93.75%" prev="Rev.1" next="Rev.3" id="Rev.2">
<h3 id="Rev.2-p0.1">Chapter 2</h3>
<p id="Rev.2-p1">
<scripture passage="Rev 2:1" parsed="|Rev|2|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.1" />
<sup>1</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu.
<scripture passage="Rev 2:2" parsed="|Rev|2|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.2" />
<sup>2</sup>Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.
<scripture passage="Rev 2:3" parsed="|Rev|2|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.3" />
<sup>3</sup>Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo.
<scripture passage="Rev 2:4" parsed="|Rev|2|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.4" />
<sup>4</sup>Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
<scripture passage="Rev 2:5" parsed="|Rev|2|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.5" />
<sup>5</sup>Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako mahali pake.
<scripture passage="Rev 2:6" parsed="|Rev|2|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.6" />
<sup>6</sup>Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
<scripture passage="Rev 2:7" parsed="|Rev|2|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.7" />
<sup>7</sup>"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu.
<scripture passage="Rev 2:8" parsed="|Rev|2|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.8" />
<sup>8</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho, ambaye alikufa na akaishi tena.
<scripture passage="Rev 2:9" parsed="|Rev|2|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.9" />
<sup>9</sup>Najua taabu zako; najua pia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri; najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.
<scripture passage="Rev 2:10" parsed="|Rev|2|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.10" />
<sup>10</sup>Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa, nami nitawapeni taji ya uzima.
<scripture passage="Rev 2:11" parsed="|Rev|2|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.11" />
<sup>11</sup>"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
<scripture passage="Rev 2:12" parsed="|Rev|2|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.12" />
<sup>12</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: "Huu ndio ujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.
<scripture passage="Rev 2:13" parsed="|Rev|2|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.13" />
<sup>13</sup>Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
<scripture passage="Rev 2:14" parsed="|Rev|2|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.14" />
<sup>14</sup>Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi.
<scripture passage="Rev 2:15" parsed="|Rev|2|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.15" />
<sup>15</sup>Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
<scripture passage="Rev 2:16" parsed="|Rev|2|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.16" />
<sup>16</sup>Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
<scripture passage="Rev 2:17" parsed="|Rev|2|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.17" />
<sup>17</sup>"Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
<scripture passage="Rev 2:18" parsed="|Rev|2|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.18" />
<sup>18</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: "Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang`aa kama shaba iliyosuguliwa.
<scripture passage="Rev 2:19" parsed="|Rev|2|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.19" />
<sup>19</sup>Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
<scripture passage="Rev 2:20" parsed="|Rev|2|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.20" />
<sup>20</sup>Lakini nina hoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamke Yezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu.
<scripture passage="Rev 2:21" parsed="|Rev|2|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.21" />
<sup>21</sup>Nimempa muda wa kutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.
<scripture passage="Rev 2:22" parsed="|Rev|2|22|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.22" />
<sup>22</sup>Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeye pamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa na mateso makali. Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubu matendo yao mabaya waliyotenda naye.
<scripture passage="Rev 2:23" parsed="|Rev|2|23|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.23" />
<sup>23</sup>Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
<scripture passage="Rev 2:24" parsed="|Rev|2|24|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.24" />
<sup>24</sup>"Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita `Siri ya Shetani`, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
<scripture passage="Rev 2:25" parsed="|Rev|2|25|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.25" />
<sup>25</sup>Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
<scripture passage="Rev 2:26" parsed="|Rev|2|26|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.26" />
<sup>26</sup>"Wanaoshinda, na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa. Naam, nitawapa uwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani, watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuyavunjavunja kama chombo cha udongo. Tena nitawapa nyota ya asubuhi.
<scripture passage="Rev 2:27" parsed="|Rev|2|27|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.27" />
<sup>27</sup>[]
<scripture passage="Rev 2:28" parsed="|Rev|2|28|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.28" />
<sup>28</sup>[]
<scripture passage="Rev 2:29" parsed="|Rev|2|29|0|0" osisRef="Bible:Rev.2.29" />
<sup>29</sup>"Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 3" progress="94.19%" prev="Rev.2" next="Rev.4" id="Rev.3">
<h3 id="Rev.3-p0.1">Chapter 3</h3>
<p id="Rev.3-p1">
<scripture passage="Rev 3:1" parsed="|Rev|3|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.1" />
<sup>1</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye na roho saba za Mungu na nyota saba. Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
<scripture passage="Rev 3:2" parsed="|Rev|3|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.2" />
<sup>2</sup>Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.
<scripture passage="Rev 3:3" parsed="|Rev|3|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.3" />
<sup>3</sup>Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii na ubadili nia yako mbaya. Usipokesha nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutaijua saa nitakapokujia.
<scripture passage="Rev 3:4" parsed="|Rev|3|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.4" />
<sup>4</sup>Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi meupe.
<scripture passage="Rev 3:5" parsed="|Rev|3|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.5" />
<sup>5</sup>"Wale wanaoshinda, watavikwa mavazi meupe kama hao. Nami sitayafuta majina yao kutoka katika kitabu cha uzima; tena nitawakiri kwamba ni wangu mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika wake.
<scripture passage="Rev 3:6" parsed="|Rev|3|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.6" />
<sup>6</sup>"Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
<scripture passage="Rev 3:7" parsed="|Rev|3|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.7" />
<sup>7</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ule ufunguo wa Daudi, na ambaye hufungua na hakuna mtu awezaye kufungua.
<scripture passage="Rev 3:8" parsed="|Rev|3|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.8" />
<sup>8</sup>Nayajua mambo yako yote! Sasa, nimefungua mbele yako mlango ambao hakuna mtu awezaye kuufunga; najua kwamba ingawa huna nguvu sana, hata hivyo, umezishika amri zangu, umelitii neno langu wala hukulikana jina langu.
<scripture passage="Rev 3:9" parsed="|Rev|3|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.9" />
<sup>9</sup>Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe ni wadanganyifu. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako wapate kujua kwamba kweli nakupenda wewe.
<scripture passage="Rev 3:10" parsed="|Rev|3|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.10" />
<sup>10</sup>Kwa kuwa wewe umezingatia agizo langu la kuwa na uvumilivu, nami pia nitakutegemeza salama wakati ule wa dhiki inayoujia ulimwengu mzima kuwajaribu wote wanaoishi duniani.
<scripture passage="Rev 3:11" parsed="|Rev|3|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.11" />
<sup>11</sup>Naja kwako upesi! Linda, basi, ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang`anywa na mtu yeyote taji yako ya ushindi.
<scripture passage="Rev 3:12" parsed="|Rev|3|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.12" />
<sup>12</sup>"Wale wanaoshinda nitawafanya wawe minara katika Hekalu la Mungu wangu, na hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yao jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yao jina langu jipya.
<scripture passage="Rev 3:13" parsed="|Rev|3|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.13" />
<sup>13</sup>"Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
<scripture passage="Rev 3:14" parsed="|Rev|3|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.14" />
<sup>14</sup>"Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aitwaye `Amina`. Yeye ni shahidi mwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba Mungu.
<scripture passage="Rev 3:15" parsed="|Rev|3|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.15" />
<sup>15</sup>Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridi au moto.
<scripture passage="Rev 3:16" parsed="|Rev|3|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.16" />
<sup>16</sup>Basi, kwa kuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika!
<scripture passage="Rev 3:17" parsed="|Rev|3|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.17" />
<sup>17</sup>Wewe unajisema, `Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote.` Kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tena uko uchi!
<scripture passage="Rev 3:18" parsed="|Rev|3|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.18" />
<sup>18</sup>Nakushauri ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwa tajiri kweli. Tena afadhali ununue pia vazi jeupe, uvae na kufunika aibu ya uchi wako. Nunua pia mafuta ukapake machoni pako upate kuona.
<scripture passage="Rev 3:19" parsed="|Rev|3|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.19" />
<sup>19</sup>Mimi ndiye mwenye kumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyo kaza moyo, achana na dhambi zako.
<scripture passage="Rev 3:20" parsed="|Rev|3|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.20" />
<sup>20</sup>Sikiliza! Mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwake na kula chakula pamoja naye, naye atakula pamoja nami.
<scripture passage="Rev 3:21" parsed="|Rev|3|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.21" />
<sup>21</sup>"Wale wanaoshinda nitawaketisha pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi mwenyewe nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi.
<scripture passage="Rev 3:22" parsed="|Rev|3|22|0|0" osisRef="Bible:Rev.3.22" />
<sup>22</sup>"Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!"
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 4" progress="94.55%" prev="Rev.3" next="Rev.5" id="Rev.4">
<h3 id="Rev.4-p0.1">Chapter 4</h3>
<p id="Rev.4-p1">
<scripture passage="Rev 4:1" parsed="|Rev|4|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, "Njoo hapa juu nami nitakuonyesha mambo yatakayotukia baadaye."
<scripture passage="Rev 4:2" parsed="|Rev|4|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.2" />
<sup>2</sup>Mara nikachukuliwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.
<scripture passage="Rev 4:3" parsed="|Rev|4|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.3" />
<sup>3</sup>Huyo aliyeketi juu yake alikuwa kama almasi na jiwe zuri jekundu. Upinde wa mvua ulikuwa unang`aa kama zumaridi na ulikizunguka kiti cha enzi pande zote.
<scripture passage="Rev 4:4" parsed="|Rev|4|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.4" />
<sup>4</sup>Kulikuwa na duara la viti ishirini na vinne kukizunguka kiti cha enzi, na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wanne walikuwa wameketi wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani.
<scripture passage="Rev 4:5" parsed="|Rev|4|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.5" />
<sup>5</sup>Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
<scripture passage="Rev 4:6" parsed="|Rev|4|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.6" />
<sup>6</sup>Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga`aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo vilikuwa vimejaa macho mbele na nyuma.
<scripture passage="Rev 4:7" parsed="|Rev|4|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.7" />
<sup>7</sup>Kiumbe cha kwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng`ombe, cha tatu kilikuwa na sura kama mtu, na cha nne kilikuwa kama tai anayeruka.
<scripture passage="Rev 4:8" parsed="|Rev|4|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.8" />
<sup>8</sup>Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika huimba: "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!"
<scripture passage="Rev 4:9" parsed="|Rev|4|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.9" />
<sup>9</sup>Kila mara viumbe vinne vilipoimba nyimbo za kumtukuza, kumheshimu na kumshukuru huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, ambaye anaishi milele na milele,
<scripture passage="Rev 4:10" parsed="|Rev|4|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.10" />
<sup>10</sup>wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
<scripture passage="Rev 4:11" parsed="|Rev|4|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.4.11" />
<sup>11</sup>"Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufu na heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako kila kitu kimepewa uhai na uzima."
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 5" progress="94.75%" prev="Rev.4" next="Rev.6" id="Rev.5">
<h3 id="Rev.5-p0.1">Chapter 5</h3>
<p id="Rev.5-p1">
<scripture passage="Rev 5:1" parsed="|Rev|5|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.1" />
<sup>1</sup>Kisha katika mkono wa kulia wa huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, nikaona kitabu; nacho kilikuwa kimeandikwa ndani na nje na kufungwa na mihuri saba.
<scripture passage="Rev 5:2" parsed="|Rev|5|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.2" />
<sup>2</sup>Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kubwa: "Nani anayestahili kuvunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu hicho?"
<scripture passage="Rev 5:3" parsed="|Rev|5|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.3" />
<sup>3</sup>Lakini hakupatikana mtu yeyote mbinguni, wala duniani, wala chini Kuzimu, aliyeweza kukifungua hicho kitabu au kukitazama ndani.
<scripture passage="Rev 5:4" parsed="|Rev|5|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.4" />
<sup>4</sup>Basi, mimi nikalia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kukifungua, au kukitazama ndani.
<scripture passage="Rev 5:5" parsed="|Rev|5|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.5" />
<sup>5</sup>Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, mjukuu maarufu wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu."
<scripture passage="Rev 5:6" parsed="|Rev|5|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.6" />
<sup>6</sup>Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwana kondoo amesimama, akizungukwa kila upande na vile viumbe hai vinne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.
<scripture passage="Rev 5:7" parsed="|Rev|5|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.7" />
<sup>7</sup>Mwanakondoo akaenda, akakitwaa hicho kitabu kutoka mkono wa kulia wa yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi.
<scripture passage="Rev 5:8" parsed="|Rev|5|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.8" />
<sup>8</sup>Mara tu alipokwisha twaa hicho kitabu, vile viumbe hai vinne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka kifudifudi mbele ya Mwanakondoo. Kila mmoja, alikuwa na kinubi na bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, ambao ni sala za watu wa Mungu.
<scripture passage="Rev 5:9" parsed="|Rev|5|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.9" />
<sup>9</sup>Basi, wakaimba wimbo huu mpya: "Wewe unastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
<scripture passage="Rev 5:10" parsed="|Rev|5|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.10" />
<sup>10</sup>Wewe umewafanya wawe ufalme wa makuhani wamtumikie Mungu wetu nao watatawala duniani."
<scripture passage="Rev 5:11" parsed="|Rev|5|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.11" />
<sup>11</sup>Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, vile viumbe hai vinne na wale wazee;
<scripture passage="Rev 5:12" parsed="|Rev|5|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.12" />
<sup>12</sup>wakasema kwa sauti kuu: "Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa."
<scripture passage="Rev 5:13" parsed="|Rev|5|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.13" />
<sup>13</sup>Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini--viumbe vyote ulimwenguni--vikisema: "Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele."
<scripture passage="Rev 5:14" parsed="|Rev|5|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.5.14" />
<sup>14</sup>Na vile viumbe vinne hai vikasema, "Amina!" Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 6" progress="94.99%" prev="Rev.5" next="Rev.7" id="Rev.6">
<h3 id="Rev.6-p0.1">Chapter 6</h3>
<p id="Rev.6-p1">
<scripture passage="Rev 6:1" parsed="|Rev|6|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia kimoja cha vile viumbe hai vinne kikisema kwa sauti kama ya ngurumo, "Njoo!"
<scripture passage="Rev 6:2" parsed="|Rev|6|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.2" />
<sup>2</sup>Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpanda farasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi aendelee kushinda.
<scripture passage="Rev 6:3" parsed="|Rev|6|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.3" />
<sup>3</sup>Kisha, Mwanakondoo akavunja mhuri wa pili. Nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema, "Njoo!"
<scripture passage="Rev 6:4" parsed="|Rev|6|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.4" />
<sup>4</sup>Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpanda farasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, akapewa upanga mkubwa.
<scripture passage="Rev 6:5" parsed="|Rev|6|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.5" />
<sup>5</sup>Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wa tatu. Nikamsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema, "Njoo!" Nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mmoja hapo, mweusi. Mpanda farasi wake alikuwa na vipimo viwili vya kupimia uzito mkononi mwake.
<scripture passage="Rev 6:6" parsed="|Rev|6|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.6" />
<sup>6</sup>Nikasikia kitu kama sauti itokayo kwa vile viumbe hai vinne. Nayo ilisema, "Kibaba kimoja cha unga wa ngano wa kiasi cha fedha dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiharibu mafuta wala divai!"
<scripture passage="Rev 6:7" parsed="|Rev|6|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.7" />
<sup>7</sup>Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wa nne. Nikamsikia yule kiumbe hai wa nne akisema, "Njoo!"
<scripture passage="Rev 6:8" parsed="|Rev|6|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.8" />
<sup>8</sup>Nami nikatazama, na kumbe alikuwapo farasi mmoja hapo, rangi yake kijivu. Na jina la mpanda farasi wake lilikuwa kifo, na Kuzimu alimfuata nyuma. Hao walipewa mamlaka juu ya robo moja ya dunia, wawaue watu kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
<scripture passage="Rev 6:9" parsed="|Rev|6|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.9" />
<sup>9</sup>Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wa tano. Nikaona pale chini ya madhabahu ya kufukizia ubani roho za wale waliouawa kwa sababu ya ujumbe wa Mungu, na kwa sababu ya ushuhuda waliotoa.
<scripture passage="Rev 6:10" parsed="|Rev|6|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.10" />
<sup>10</sup>Basi, wakalia kwa sauti kubwa: "Ee Bwana, uliye mtakatifu na mwaminifu, mpaka lini utakawia kulipiza kisasi kwa wakazi wote wa dunia kwa ajili ya kuuawa kwetu?"
<scripture passage="Rev 6:11" parsed="|Rev|6|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.11" />
<sup>11</sup>Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watawaua kama wao wenyewe walivyouawa.
<scripture passage="Rev 6:12" parsed="|Rev|6|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.12" />
<sup>12</sup>Kisha nikatazama, na wakati Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi; jua likawa jeusi kama gunia; mwezi wote ukawa mwekundu kama damu;
<scripture passage="Rev 6:13" parsed="|Rev|6|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.13" />
<sup>13</sup>nazo nyota za mbingu zikaanguka juu ya ardhi kama matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali.
<scripture passage="Rev 6:14" parsed="|Rev|6|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.14" />
<sup>14</sup>Anga likatoweka kama vile karatasi inavyokunjwakunjwa; milima yote na visima vyote vikaondolewa mahali pake.
<scripture passage="Rev 6:15" parsed="|Rev|6|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.15" />
<sup>15</sup>Kisha wafalme wa duniani, wakuu, majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye majabali milimani.
<scripture passage="Rev 6:16" parsed="|Rev|6|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.16" />
<sup>16</sup>Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali, "Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!
<scripture passage="Rev 6:17" parsed="|Rev|6|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.6.17" />
<sup>17</sup>Maana siku maalum ya ghadhabu yao imefika. Nani awezaye kuikabili?"
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 7" progress="95.28%" prev="Rev.6" next="Rev.8" id="Rev.7">
<h3 id="Rev.7-p0.1">Chapter 7</h3>
<p id="Rev.7-p1">
<scripture passage="Rev 7:1" parsed="|Rev|7|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti.
<scripture passage="Rev 7:2" parsed="|Rev|7|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.2" />
<sup>2</sup>Kisha nikamwona malaika mwingine akipanda juu kutoka mashariki akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai. Akapaaza sauti na kuwaambia hao malaika wanne waliokabidhiwa jukumu la kuiharibu nchi na bahari,
<scripture passage="Rev 7:3" parsed="|Rev|7|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.3" />
<sup>3</sup>"Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso."
<scripture passage="Rev 7:4" parsed="|Rev|7|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.4" />
<sup>4</sup>Kisha nikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu mia moja arobaini na nne elfu wa makabila yote ya watu wa Israeli.
<scripture passage="Rev 7:5" parsed="|Rev|7|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.5" />
<sup>5</sup>Kabila la Yuda walikuwa watu kumi na mbili elfu; kabila la Reubeni, kumi na mbili elfu, kabila la Gadi, kumi na mbili elfu;
<scripture passage="Rev 7:6" parsed="|Rev|7|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.6" />
<sup>6</sup>Kabila la Asheri, kumi na mbili elfu; kabila la Naftali, kumi na mbili elfu; kabila la Manase, kumi na mbili elfu;
<scripture passage="Rev 7:7" parsed="|Rev|7|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.7" />
<sup>7</sup>kabila la Simeoni, kumi na mbili elfu, kabila la Lawi, kumi na mbili elfu, kabila la Isakari, kumi na mbili elfu;
<scripture passage="Rev 7:8" parsed="|Rev|7|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.8" />
<sup>8</sup>kabila la Zabuloni, kumi na mbili elfu; kabila la Yosefu, kumi na mbili elfu, na kabila la Benyamini, kumi na mbili elfu.
<scripture passage="Rev 7:9" parsed="|Rev|7|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.9" />
<sup>9</sup>Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wakiwa wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.
<scripture passage="Rev 7:10" parsed="|Rev|7|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.10" />
<sup>10</sup>Wakapaaza sauti: "Ukombozi wetu watoka kwa Mungu wetu aketiye juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa Mwanakondoo!"
<scripture passage="Rev 7:11" parsed="|Rev|7|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.11" />
<sup>11</sup>Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na vile viumbe hai vinne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
<scripture passage="Rev 7:12" parsed="|Rev|7|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.12" />
<sup>12</sup>wakisema, "Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milele na milele! Amina!"
<scripture passage="Rev 7:13" parsed="|Rev|7|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.13" />
<sup>13</sup>Mmoja wa hao wazee akaniuliza, "Hawa waliovaa mavazi meupe ni watu gani? Na wametoka wapi?"
<scripture passage="Rev 7:14" parsed="|Rev|7|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.14" />
<sup>14</sup>Nami nikamjibu, "Mheshimiwa, wewe wajua!" Naye akaniambia, "Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
<scripture passage="Rev 7:15" parsed="|Rev|7|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.15" />
<sup>15</sup>Ndiyo maana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungu mchana na usiku katika Hekalu lake; naye aketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yao kuwalinda.
<scripture passage="Rev 7:16" parsed="|Rev|7|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.16" />
<sup>16</sup>Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena,
<scripture passage="Rev 7:17" parsed="|Rev|7|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.7.17" />
<sup>17</sup>kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao."
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 8" progress="95.53%" prev="Rev.7" next="Rev.9" id="Rev.8">
<h3 id="Rev.8-p0.1">Chapter 8</h3>
<p id="Rev.8-p1">
<scripture passage="Rev 8:1" parsed="|Rev|8|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.1" />
<sup>1</sup>Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.
<scripture passage="Rev 8:2" parsed="|Rev|8|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.2" />
<sup>2</sup>Kisha nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele ya Mungu wamepewa tarumbeta saba.
<scripture passage="Rev 8:3" parsed="|Rev|8|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.3" />
<sup>3</sup>Malaika mwingine akafika, akiwa anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
<scripture passage="Rev 8:4" parsed="|Rev|8|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.4" />
<sup>4</sup>Moshi wa ubani ukapanda juu, pamoja na sala za watu wa Mungu, kutoka mikononi mwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu.
<scripture passage="Rev 8:5" parsed="|Rev|8|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.5" />
<sup>5</sup>Kisha malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.
<scripture passage="Rev 8:6" parsed="|Rev|8|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.6" />
<sup>6</sup>Kisha wale malaika saba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari kupiga mbiu ya mgambo. ic
<scripture passage="Rev 8:7" parsed="|Rev|8|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.7" />
<sup>7</sup>Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto, pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi moja ya nchi ikaungua, theluthi moja ya miti ikaungua, na majani yote mabichi yakaungua.
<scripture passage="Rev 8:8" parsed="|Rev|8|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.8" />
<sup>8</sup>Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto ukatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawa damu,
<scripture passage="Rev 8:9" parsed="|Rev|8|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.9" />
<sup>9</sup>theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
<scripture passage="Rev 8:10" parsed="|Rev|8|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.10" />
<sup>10</sup>Kisha malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwa ikiwaka kama bonge la moto, ikaanguka kutoka mbinguni, na kutua juu ya theluthi moja ya mito na chemchemi za maji.
<scripture passage="Rev 8:11" parsed="|Rev|8|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.11" />
<sup>11</sup>(Nyota hiyo inaitwa "Uchungu.") Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
<scripture passage="Rev 8:12" parsed="|Rev|8|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.12" />
<sup>12</sup>Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng`ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.
<scripture passage="Rev 8:13" parsed="|Rev|8|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.8.13" />
<sup>13</sup>Kisha nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani anasema kwa sauti kubwa, "Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!"
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 9" progress="95.74%" prev="Rev.8" next="Rev.10" id="Rev.9">
<h3 id="Rev.9-p0.1">Chapter 9</h3>
<p id="Rev.9-p1">
<scripture passage="Rev 9:1" parsed="|Rev|9|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.1" />
<sup>1</sup>Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo la Kuzimu.
<scripture passage="Rev 9:2" parsed="|Rev|9|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.2" />
<sup>2</sup>Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatoka moshi wa tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa Kuzimu.
<scripture passage="Rev 9:3" parsed="|Rev|9|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.3" />
<sup>3</sup>Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani wakapewa nguvu kama ya ng`e.
<scripture passage="Rev 9:4" parsed="|Rev|9|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.4" />
<sup>4</sup>Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.
<scripture passage="Rev 9:5" parsed="|Rev|9|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.5" />
<sup>5</sup>Nzige hao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ila kuwatesa tu kwa muda wa miezi mitano. Maumivu watakayosababisha ni kama maumivu yanayompata mtu wakati anapoumwa na ng`e.
<scripture passage="Rev 9:6" parsed="|Rev|9|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.6" />
<sup>6</sup>Muda huo watu watatafuta kifo lakini hawatakipata; watatamani kufa lakini kifo kitawakimbia.
<scripture passage="Rev 9:7" parsed="|Rev|9|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.7" />
<sup>7</sup>Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
<scripture passage="Rev 9:8" parsed="|Rev|9|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.8" />
<sup>8</sup>Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
<scripture passage="Rev 9:9" parsed="|Rev|9|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.9" />
<sup>9</sup>Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafara wa magari ya farasi wengi wanaokimbilia vitani.
<scripture passage="Rev 9:10" parsed="|Rev|9|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.10" />
<sup>10</sup>Walikuwa na mikia na miiba kama ng`e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
<scripture passage="Rev 9:11" parsed="|Rev|9|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.11" />
<sup>11</sup>Tena wanaye mfalme anayewatawala, naye ndiye malaika wa kuzimu; jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki ni Apolioni, yaani mwangamizi.
<scripture passage="Rev 9:12" parsed="|Rev|9|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.12" />
<sup>12</sup>Maafa ya kwanza yamepita; bado mengine mawili yanafuata.
<scripture passage="Rev 9:13" parsed="|Rev|9|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.13" />
<sup>13</sup>Kisha malaika wa sita akapiga tarumbeta yake. Nami nikasikia sauti moja kutoka katika pembe nne za madhabahu ya dhahabu iliyokuwa mbele ya Mungu.
<scripture passage="Rev 9:14" parsed="|Rev|9|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.14" />
<sup>14</sup>Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, "Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa `Eufrate!"`
<scripture passage="Rev 9:15" parsed="|Rev|9|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.15" />
<sup>15</sup>Naye akawafungulia malaika hao wanne ambao walikuwa wametayarishwa kwa ajili ya saa hiyo ya siku ya mwezi huo, wa mwaka huohuo, kuua theluthi moja ya wanaadamu.
<scripture passage="Rev 9:16" parsed="|Rev|9|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.16" />
<sup>16</sup>Nilisikia idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili.
<scripture passage="Rev 9:17" parsed="|Rev|9|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.17" />
<sup>17</sup>Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao.
<scripture passage="Rev 9:18" parsed="|Rev|9|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.18" />
<sup>18</sup>Theluthi moja ya wanaadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
<scripture passage="Rev 9:19" parsed="|Rev|9|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.19" />
<sup>19</sup>maana nguvu ya farasi hao ilikuwa vinywani mwao na katika mikia yao. Mikia yao ilikuwa na vichwa kama nyoka, na waliitumia hiyo kuwadhuru watu.
<scripture passage="Rev 9:20" parsed="|Rev|9|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.20" />
<sup>20</sup>Wanaadamu wengine waliobaki ambao hawakuuawa na mabaa hayo, hawakugeuka na kuviacha vitu walivyokuwa wametengeneza kwa mikono yao wenyewe; bali wakaendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia wala kutembea.
<scripture passage="Rev 9:21" parsed="|Rev|9|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.9.21" />
<sup>21</sup>Wala hawakutubu na kuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 10" progress="96.05%" prev="Rev.9" next="Rev.11" id="Rev.10">
<h3 id="Rev.10-p0.1">Chapter 10</h3>
<p id="Rev.10-p1">
<scripture passage="Rev 10:1" parsed="|Rev|10|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevikwa wingu, na upinde wa mvua kichwani mwake. Uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake ilikuwa kama moto.
<scripture passage="Rev 10:2" parsed="|Rev|10|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.2" />
<sup>2</sup>Mikononi mwake alishika kitabu kidogo kimefunguliwa. Aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari, na wa kushoto juu ya nchi kavu,
<scripture passage="Rev 10:3" parsed="|Rev|10|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.3" />
<sup>3</sup>na kuita kwa sauti kubwa kama ya mngurumo wa simba. Alipopaaza sauti, ngurumo saba ziliitikia kwa kishindo.
<scripture passage="Rev 10:4" parsed="|Rev|10|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.4" />
<sup>4</sup>Na hizo ngurumo saba ziliposema, mimi nikataka kuandika. Lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni: "Maneno ya ngurumo hizo saba ni siri; usiyaandike!"
<scripture passage="Rev 10:5" parsed="|Rev|10|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.5" />
<sup>5</sup>Kisha yule malaika niliyemwona akisimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu akainua mkono wake wa kulia juu mbinguni,
<scripture passage="Rev 10:6" parsed="|Rev|10|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.6" />
<sup>6</sup>akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, "Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
<scripture passage="Rev 10:7" parsed="|Rev|10|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.7" />
<sup>7</sup>Lakini wakati ule malaika wa saba atakapotoa sauti yake, wakati atakapopiga tarumbeta yake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kama alivyowatangazia watumishi wake manabii."
<scripture passage="Rev 10:8" parsed="|Rev|10|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.8" />
<sup>8</sup>Kisha ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awali ikasema nami tena: "Nenda ukakichukue kile kitabu kilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu."
<scripture passage="Rev 10:9" parsed="|Rev|10|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.9" />
<sup>9</sup>Basi, nikamwendea huyo malaika, nikamwambia anipe hicho kitabu kidogo. Naye akaniambia, "Kichukue, ukile; kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali, lakini tumboni kitakuwa kichungu!"
<scripture passage="Rev 10:10" parsed="|Rev|10|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.10" />
<sup>10</sup>Basi, nikakichukua kitabu hicho kidogo kutoka mkononi mwa huyo malaika, nikakila; nacho kilikuwa kitamu kinywani mwangu kama asali, lakini nilipokimeza kikawa kichungu tumboni mwangu.
<scripture passage="Rev 10:11" parsed="|Rev|10|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.10.11" />
<sup>11</sup>Kisha nikaambiwa, "Inakubidi tena kutangaza ujumbe wa Mungu kuhusu watu wengi, mataifa, watu wa lugha nyingi na wafalme!"
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 11" progress="96.24%" prev="Rev.10" next="Rev.12" id="Rev.11">
<h3 id="Rev.11-p0.1">Chapter 11</h3>
<p id="Rev.11-p1">
<scripture passage="Rev 11:1" parsed="|Rev|11|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, "Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawahesabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu.
<scripture passage="Rev 11:2" parsed="|Rev|11|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.2" />
<sup>2</sup>Lakini uache ukumbi ulio nje ya Hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
<scripture passage="Rev 11:3" parsed="|Rev|11|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.3" />
<sup>3</sup>Nami nitawatuma mashahidi wangu wawili ili watangaze ujumbe wa Mungu kwa muda huo wa siku elfu moja mia mbili na sitini wakiwa wamevaa mavazi ya magunia."
<scripture passage="Rev 11:4" parsed="|Rev|11|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.4" />
<sup>4</sup>Hao mashahidi wawili ni miti miwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimama mbele ya Bwana wa dunia.
<scripture passage="Rev 11:5" parsed="|Rev|11|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.5" />
<sup>5</sup>Kama mtu akijaribu kuwadhuru, moto hutoka kinywani mwao na kuwaangamiza adui zao; na kila mtu atakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.
<scripture passage="Rev 11:6" parsed="|Rev|11|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.6" />
<sup>6</sup>Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga, mvua isinyeshe wakati wanapotangaza ujumbe wa Mungu. Tena wanayo mamlaka ya kuzigeuza chemchemi zote za maji ziwe damu, na ya kusababisha maafa ya kila namna duniani kila mara wapendavyo.
<scripture passage="Rev 11:7" parsed="|Rev|11|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.7" />
<sup>7</sup>Lakini wakisha maliza kutangaza ujumbe huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.
<scripture passage="Rev 11:8" parsed="|Rev|11|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.8" />
<sup>8</sup>Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
<scripture passage="Rev 11:9" parsed="|Rev|11|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.9" />
<sup>9</sup>Watu wa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti hizo kwa muda wa siku tatu na nusu, na hawataruhusu zizikwe.
<scripture passage="Rev 11:10" parsed="|Rev|11|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.10" />
<sup>10</sup>Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
<scripture passage="Rev 11:11" parsed="|Rev|11|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.11" />
<sup>11</sup>Lakini baada ya zile siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
<scripture passage="Rev 11:12" parsed="|Rev|11|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.12" />
<sup>12</sup>Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, "Njoni hapa juu!" Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui wao wakiwa wanawatazama.
<scripture passage="Rev 11:13" parsed="|Rev|11|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.13" />
<sup>13</sup>Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
<scripture passage="Rev 11:14" parsed="|Rev|11|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.14" />
<sup>14</sup>Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.
<scripture passage="Rev 11:15" parsed="|Rev|11|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.15" />
<sup>15</sup>Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, "Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!"
<scripture passage="Rev 11:16" parsed="|Rev|11|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.16" />
<sup>16</sup>Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
<scripture passage="Rev 11:17" parsed="|Rev|11|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.17" />
<sup>17</sup>wakisema: "Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko na uliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yako kuu ukaanza kutawala!
<scripture passage="Rev 11:18" parsed="|Rev|11|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.18" />
<sup>18</sup>Watu wa mataifa waliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watu wako na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia."
<scripture passage="Rev 11:19" parsed="|Rev|11|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.11.19" />
<sup>19</sup>Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 12" progress="96.55%" prev="Rev.11" next="Rev.13" id="Rev.12">
<h3 id="Rev.12-p0.1">Chapter 12</h3>
<p id="Rev.12-p1">
<scripture passage="Rev 12:1" parsed="|Rev|12|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.1" />
<sup>1</sup>Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa hapo mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
<scripture passage="Rev 12:2" parsed="|Rev|12|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.2" />
<sup>2</sup>Alikuwa mja mzito, na akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto.
<scripture passage="Rev 12:3" parsed="|Rev|12|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.3" />
<sup>3</sup>Ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.
<scripture passage="Rev 12:4" parsed="|Rev|12|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.4" />
<sup>4</sup>Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimama mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa.
<scripture passage="Rev 12:5" parsed="|Rev|12|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.5" />
<sup>5</sup>Kisha mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.
<scripture passage="Rev 12:6" parsed="|Rev|12|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.6" />
<sup>6</sup>Huyo mama akakimbilia jangwani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali pa usalama ambapo angehifadhiwa kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
<scripture passage="Rev 12:7" parsed="|Rev|12|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.7" />
<sup>7</sup>Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake.
<scripture passage="Rev 12:8" parsed="|Rev|12|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.8" />
<sup>8</sup>Lakini joka hilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika wake.
<scripture passage="Rev 12:9" parsed="|Rev|12|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.9" />
<sup>9</sup>Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani. Ndiye anayeudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.
<scripture passage="Rev 12:10" parsed="|Rev|12|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.10" />
<sup>10</sup>Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: "Sasa ukombozi utokao kwa Mungu umefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetu umedhihirika. Na Kristo wake ameonyesha mamlaka yake! Maana yule mdhalimu wa ndugu zetu, aliyesimama mbele ya Mungu akiwashtaki usiku na mchana, sasa ametupwa nje.
<scripture passage="Rev 12:11" parsed="|Rev|12|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.11" />
<sup>11</sup>Ndugu zetu wameshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa nguvu ya ukweli walioutangaza; maana hawakuyathamini maisha yao kuwa kitu sana, wakawa tayari kufa.
<scripture passage="Rev 12:12" parsed="|Rev|12|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.12" />
<sup>12</sup>Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba siku zake zilizobakia ni chache."
<scripture passage="Rev 12:13" parsed="|Rev|12|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.13" />
<sup>13</sup>Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
<scripture passage="Rev 12:14" parsed="|Rev|12|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.14" />
<sup>14</sup>Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali, pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
<scripture passage="Rev 12:15" parsed="|Rev|12|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.15" />
<sup>15</sup>Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue.
<scripture passage="Rev 12:16" parsed="|Rev|12|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.16" />
<sup>16</sup>Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
<scripture passage="Rev 12:17" parsed="|Rev|12|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.17" />
<sup>17</sup>Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kuuzingatia ukweli wa Yesu.
<scripture passage="Rev 12:18" parsed="|Rev|12|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.12.18" />
<sup>18</sup>Na likajisimamia ukingoni mwa bahari.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 13" progress="96.83%" prev="Rev.12" next="Rev.14" id="Rev.13">
<h3 id="Rev.13-p0.1">Chapter 13</h3>
<p id="Rev.13-p1">
<scripture passage="Rev 13:1" parsed="|Rev|13|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
<scripture passage="Rev 13:2" parsed="|Rev|13|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.2" />
<sup>2</sup>Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.
<scripture passage="Rev 13:3" parsed="|Rev|13|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.3" />
<sup>3</sup>Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
<scripture passage="Rev 13:4" parsed="|Rev|13|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.4" />
<sup>4</sup>Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, "Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?"
<scripture passage="Rev 13:5" parsed="|Rev|13|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.5" />
<sup>5</sup>Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
<scripture passage="Rev 13:6" parsed="|Rev|13|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.6" />
<sup>6</sup>Basi, akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.
<scripture passage="Rev 13:7" parsed="|Rev|13|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.7" />
<sup>7</sup>Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa.
<scripture passage="Rev 13:8" parsed="|Rev|13|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.8" />
<sup>8</sup>Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
<scripture passage="Rev 13:9" parsed="|Rev|13|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.9" />
<sup>9</sup>"Aliye na masikio, na asikie!
<scripture passage="Rev 13:10" parsed="|Rev|13|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.10" />
<sup>10</sup>Waliokusudiwa kuchukuliwa mateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana na hayo ni lazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu na imani."
<scripture passage="Rev 13:11" parsed="|Rev|13|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.11" />
<sup>11</sup>Kisha nikamwona mnyama mwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembe mbili kama pembe za kondoo, na aliongea kama joka.
<scripture passage="Rev 13:12" parsed="|Rev|13|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.12" />
<sup>12</sup>Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.
<scripture passage="Rev 13:13" parsed="|Rev|13|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.13" />
<sup>13</sup>Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.
<scripture passage="Rev 13:14" parsed="|Rev|13|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.14" />
<sup>14</sup>Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.
<scripture passage="Rev 13:15" parsed="|Rev|13|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.15" />
<sup>15</sup>Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.
<scripture passage="Rev 13:16" parsed="|Rev|13|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.16" />
<sup>16</sup>Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.
<scripture passage="Rev 13:17" parsed="|Rev|13|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.17" />
<sup>17</sup>Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.
<scripture passage="Rev 13:18" parsed="|Rev|13|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.13.18" />
<sup>18</sup>Hapa ni lazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 14" progress="97.12%" prev="Rev.13" next="Rev.15" id="Rev.14">
<h3 id="Rev.14-p0.1">Chapter 14</h3>
<p id="Rev.14-p1">
<scripture passage="Rev 14:1" parsed="|Rev|14|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikaona mlima Sioni, na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu mia moja arobaini na nne elfu ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
<scripture passage="Rev 14:2" parsed="|Rev|14|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.2" />
<sup>2</sup>Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama sauti ya maji mengi na kama sauti ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
<scripture passage="Rev 14:3" parsed="|Rev|14|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.3" />
<sup>3</sup>Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu mia moja arobaini na nne elfu waliokombolewa duniani.
<scripture passage="Rev 14:4" parsed="|Rev|14|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.4" />
<sup>4</sup>Watu hao ndio wale waliojiweka safi kwa kutoonana kimwili na wanawake, nao ni mabikira. Wao humfuata Mwanakondoo kokote aendako. Wamekombolewa kutoka miongoni mwa binadamu wengine, wakawa wa kwanza kutolewa kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.
<scripture passage="Rev 14:5" parsed="|Rev|14|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.5" />
<sup>5</sup>Hawakupata kamwe kuwa waongo; hawana hatia yoyote.
<scripture passage="Rev 14:6" parsed="|Rev|14|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.6" />
<sup>6</sup>Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote.
<scripture passage="Rev 14:7" parsed="|Rev|14|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.7" />
<sup>7</sup>Akasema kwa sauti kubwa, "Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji."
<scripture passage="Rev 14:8" parsed="|Rev|14|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.8" />
<sup>8</sup>Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, "Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake--divai kali ya uzinzi wake!"
<scripture passage="Rev 14:9" parsed="|Rev|14|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.9" />
<sup>9</sup>Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, "Yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake,
<scripture passage="Rev 14:10" parsed="|Rev|14|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.10" />
<sup>10</sup>yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu, ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo.
<scripture passage="Rev 14:11" parsed="|Rev|14|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.11" />
<sup>11</sup>Moshi wa moto unaowatesa kupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabudu huyo mnyama na sanamu yake, na kutiwa alama ya jina lake, hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana."
<scripture passage="Rev 14:12" parsed="|Rev|14|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.12" />
<sup>12</sup>Kutokana na hayo, ni lazima watu wa Mungu, yaani watu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
<scripture passage="Rev 14:13" parsed="|Rev|14|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.13" />
<sup>13</sup>Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, "Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana." Naye Roho asema, "Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata."
<scripture passage="Rev 14:14" parsed="|Rev|14|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.14" />
<sup>14</sup>Kisha nikatazama, na kumbe palikuwapo wingu jeupe hapo. Na juu ya wingu hilo kulikuwa na kiumbe kama mtu. Alikuwa amevaa taji ya dhahabu kichwani, na kushika mundu mkononi mwake.
<scripture passage="Rev 14:15" parsed="|Rev|14|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.15" />
<sup>15</sup>Kisha malaika mwingine akatoka Hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, "Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva."
<scripture passage="Rev 14:16" parsed="|Rev|14|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.16" />
<sup>16</sup>Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa.
<scripture passage="Rev 14:17" parsed="|Rev|14|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.17" />
<sup>17</sup>Kisha malaika mwingine akatoka katika Hekalu mbinguni akiwa na mundu wenye makali.
<scripture passage="Rev 14:18" parsed="|Rev|14|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.18" />
<sup>18</sup>Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, "Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!"
<scripture passage="Rev 14:19" parsed="|Rev|14|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.19" />
<sup>19</sup>Basi, malaika huyo akautupa mundu wake duniani, akakata zabibu za dunia, akazitia ndani ya chombo kikubwa cha kukamulia zabibu, chombo cha ghadhabu ya Mungu.
<scripture passage="Rev 14:20" parsed="|Rev|14|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.14.20" />
<sup>20</sup>Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko mrefu kiasi cha mita mia tatu na kina chake kiasi cha mita mia mbili.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 15" progress="97.49%" prev="Rev.14" next="Rev.16" id="Rev.15">
<h3 id="Rev.15-p0.1">Chapter 15</h3>
<p id="Rev.15-p1">
<scripture passage="Rev 15:1" parsed="|Rev|15|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwa saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
<scripture passage="Rev 15:2" parsed="|Rev|15|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.2" />
<sup>2</sup>Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.
<scripture passage="Rev 15:3" parsed="|Rev|15|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.3" />
<sup>3</sup>Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo: "Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makuu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
<scripture passage="Rev 15:4" parsed="|Rev|15|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.4" />
<sup>4</sup>Bwana, ni nani asiyekucha wewe? Nani asiyelitukuza jina lako? Wewe peke yako ni Mtakatifu. Mataifa yote yatakujia na kukuabudu maana matendo yako ya haki yameonekana na wote."
<scripture passage="Rev 15:5" parsed="|Rev|15|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.5" />
<sup>5</sup>Baada ya hayo nikaona Hekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hema ionyeshayo kuwapo kwa Mungu.
<scripture passage="Rev 15:6" parsed="|Rev|15|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.6" />
<sup>6</sup>Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung`aa, na kanda za dhahabu vifuani mwao.
<scripture passage="Rev 15:7" parsed="|Rev|15|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.7" />
<sup>7</sup>Kisha, mmojawapo wa vile viumbe vinne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.
<scripture passage="Rev 15:8" parsed="|Rev|15|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.15.8" />
<sup>8</sup>Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 16" progress="97.64%" prev="Rev.15" next="Rev.17" id="Rev.16">
<h3 id="Rev.16-p0.1">Chapter 16</h3>
<p id="Rev.16-p1">
<scripture passage="Rev 16:1" parsed="|Rev|16|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, "Nendeni mkamwage mabakuli hayo saba ya ghadhabu ya Mungu duniani."
<scripture passage="Rev 16:2" parsed="|Rev|16|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.2" />
<sup>2</sup>Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama, na wale walioiabudu sanamu yake.
<scripture passage="Rev 16:3" parsed="|Rev|16|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.3" />
<sup>3</sup>Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.
<scripture passage="Rev 16:4" parsed="|Rev|16|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.4" />
<sup>4</sup>Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, navyo vikageuka damu.
<scripture passage="Rev 16:5" parsed="|Rev|16|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.5" />
<sup>5</sup>Nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema, "Ewe mtakatifu, Uliyeko na uliyekuwako! Wewe ni mwenye haki katika hukumu hii uliyotoa.
<scripture passage="Rev 16:6" parsed="|Rev|16|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.6" />
<sup>6</sup>Maana waliimwaga damu ya watu wako na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; wamestahili hivyo!"
<scripture passage="Rev 16:7" parsed="|Rev|16|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.7" />
<sup>7</sup>Kisha nikasikia sauti madhabahuni ikisema, "Naam, Bwana Mungu Mwenye Uwezo! Hukumu zako ni za kweli na haki!"
<scripture passage="Rev 16:8" parsed="|Rev|16|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.8" />
<sup>8</sup>Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake.
<scripture passage="Rev 16:9" parsed="|Rev|16|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.9" />
<sup>9</sup>Basi, watu wakaunguzwa vibaya sana; wakamtukana Mungu aliye na uwezo juu ya mabaa hayo makubwa. Lakini hawakuziacha dhambi zao na kumtukuza Mungu.
<scripture passage="Rev 16:10" parsed="|Rev|16|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.10" />
<sup>10</sup>Kisha malaika wa tano akamwaga bakuli lake juu ya makao makuu ya yule mnyama. Giza likauvamia utawala wake, watu wakauma ndimi zao kwa sababu za maumivu,
<scripture passage="Rev 16:11" parsed="|Rev|16|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.11" />
<sup>11</sup>wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na madonda yao. Lakini hawakuyaacha matendo yao mabaya.
<scripture passage="Rev 16:12" parsed="|Rev|16|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.12" />
<sup>12</sup>Kisha malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ilitengenezwa kwa ajili ya wafalme wa mashariki.
<scripture passage="Rev 16:13" parsed="|Rev|16|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.13" />
<sup>13</sup>Kisha nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama, na kinywani mwa yule nabii wa uongo.
<scripture passage="Rev 16:14" parsed="|Rev|16|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.14" />
<sup>14</sup>Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita kuu Siku ile ya Mungu Mwenye Uwezo.
<scripture passage="Rev 16:15" parsed="|Rev|16|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.15" />
<sup>15</sup>"Sikiliza! Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko mbele ya watu."
<scripture passage="Rev 16:16" parsed="|Rev|16|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.16" />
<sup>16</sup>Basi, roho hao wakawakusanya hao wafalme mahali paitwapo kwa Kiebrania Harmagedoni.
<scripture passage="Rev 16:17" parsed="|Rev|16|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.17" />
<sup>17</sup>Kisha malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, Hekaluni, ikisema, "Mwisho umefika!"
<scripture passage="Rev 16:18" parsed="|Rev|16|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.18" />
<sup>18</sup>Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu.
<scripture passage="Rev 16:19" parsed="|Rev|16|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.19" />
<sup>19</sup>Mji ule mkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa na Mungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabu yake kuu.
<scripture passage="Rev 16:20" parsed="|Rev|16|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.20" />
<sup>20</sup>Visiwa vyote vikatoweka, nayo milima haikuonekena tena.
<scripture passage="Rev 16:21" parsed="|Rev|16|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.16.21" />
<sup>21</sup>Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 17" progress="97.94%" prev="Rev.16" next="Rev.18" id="Rev.17">
<h3 id="Rev.17-p0.1">Chapter 17</h3>
<p id="Rev.17-p1">
<scripture passage="Rev 17:1" parsed="|Rev|17|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.1" />
<sup>1</sup>Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli akaja, akaniambia, "Njoo, mimi nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi.
<scripture passage="Rev 17:2" parsed="|Rev|17|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.2" />
<sup>2</sup>Wafalme wa dunia wamefanya uzinzi pamoja naye; na wakazi wa dunia wamelewa divai ya uzinzi wake."
<scripture passage="Rev 17:3" parsed="|Rev|17|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.3" />
<sup>3</sup>Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
<scripture passage="Rev 17:4" parsed="|Rev|17|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.4" />
<sup>4</sup>Mwanamke huyo alikuwa amevaa vazi la rangi ya zambarau na nyekundu; alikuwa amejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa machukizo na mambo machafu yanayoonyesha uzinzi wake.
<scripture passage="Rev 17:5" parsed="|Rev|17|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.5" />
<sup>5</sup>Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo "Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani."
<scripture passage="Rev 17:6" parsed="|Rev|17|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.6" />
<sup>6</sup>Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
<scripture passage="Rev 17:7" parsed="|Rev|17|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.7" />
<sup>7</sup>Lakini malaika akaniambia, "Kwa nini unashangaa? Mimi nitakuambia maana iliyofichika ya mwanamke huyu na mnyama huyo amchukuaye ambaye ana vichwa saba na pembe kumi.
<scripture passage="Rev 17:8" parsed="|Rev|17|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.8" />
<sup>8</sup>Huyo mnyama uliyemwona alikuwa hai hapo awali, lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sana atapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa. Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uzima tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kumwona huyo mnyama ambaye hapo awali, aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena!
<scripture passage="Rev 17:9" parsed="|Rev|17|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.9" />
<sup>9</sup>"Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
<scripture passage="Rev 17:10" parsed="|Rev|17|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.10" />
<sup>10</sup>Kati ya hao wafalme saba, watano wamekwisha angamia, mmoja anatawala bado, na yule mwingine bado hajafika; na atakapofika atabaki kwa muda mfupi.
<scripture passage="Rev 17:11" parsed="|Rev|17|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.11" />
<sup>11</sup>Huyo mnyama ambaye alikuwa anaishi hapo awali lakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane, naye pia ni miongoni mwa hao saba, na anakwenda zake kuharibiwa.
<scripture passage="Rev 17:12" parsed="|Rev|17|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.12" />
<sup>12</sup>"Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme ambao bado hawajaanza kutawala. Lakini watapewa mamlaka ya kutawala kwa muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
<scripture passage="Rev 17:13" parsed="|Rev|17|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.13" />
<sup>13</sup>Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote.
<scripture passage="Rev 17:14" parsed="|Rev|17|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.14" />
<sup>14</sup>Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme."
<scripture passage="Rev 17:15" parsed="|Rev|17|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.15" />
<sup>15</sup>Malaika akaniambia pia, "Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, ni mataifa, watu wa kila rangi na lugha.
<scripture passage="Rev 17:16" parsed="|Rev|17|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.16" />
<sup>16</sup>Pembe zile kumi ulizoziona na yule mnyama watamchukia huyo mzinzi. Watachukua kila kitu alicho nacho na kumwacha uchi; watakula nyama yake na kumteketeza kwa moto.
<scripture passage="Rev 17:17" parsed="|Rev|17|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.17" />
<sup>17</sup>Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani kwa kukubaliana wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo neno la Mungu litakapotimia.
<scripture passage="Rev 17:18" parsed="|Rev|17|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.17.18" />
<sup>18</sup>"Na yule mwanamke uliyemwona ndio ule mji mkuu unaowatawala wafalme wa dunia."
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 18" progress="98.24%" prev="Rev.17" next="Rev.19" id="Rev.18">
<h3 id="Rev.18-p0.1">Chapter 18</h3>
<p id="Rev.18-p1">
<scripture passage="Rev 18:1" parsed="|Rev|18|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng`ao wake.
<scripture passage="Rev 18:2" parsed="|Rev|18|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.2" />
<sup>2</sup>Basi, akapaaza sauti kwa nguvu akisema, "Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
<scripture passage="Rev 18:3" parsed="|Rev|18|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.3" />
<sup>3</sup>Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo."
<scripture passage="Rev 18:4" parsed="|Rev|18|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.4" />
<sup>4</sup>Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, "Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
<scripture passage="Rev 18:5" parsed="|Rev|18|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.5" />
<sup>5</sup>Kwa maana dhambi zake zimekuwa nyingi mno, zimelundikana mpaka mbinguni, na Mungu ameyakumbuka maovu yake.
<scripture passage="Rev 18:6" parsed="|Rev|18|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.6" />
<sup>6</sup>Mtendeeni kama alivyowatendea ninyi; mlipeni mara mbili kwa yale aliyoyatenda. Jazeni kikombe chake kwa kinywaji kikali mara mbili zaidi ya kile alichowapeni.
<scripture passage="Rev 18:7" parsed="|Rev|18|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.7" />
<sup>7</sup>Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: `Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!`
<scripture passage="Rev 18:8" parsed="|Rev|18|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.8" />
<sup>8</sup>Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ni Mwenye Uwezo."
<scripture passage="Rev 18:9" parsed="|Rev|18|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.9" />
<sup>9</sup>Wafalme wa Dunia waliofanya uzinzi naye na kuishi naye maisha ya anasa wataomboleza na kulia wakati watakapoona moshi wa mji huo unaoteketea.
<scripture passage="Rev 18:10" parsed="|Rev|18|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.10" />
<sup>10</sup>Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake, na kusema, "Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata."
<scripture passage="Rev 18:11" parsed="|Rev|18|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.11" />
<sup>11</sup>Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumfanyia matanga, maana hakuna mtu anayenunua tena bidhaa zao;
<scripture passage="Rev 18:12" parsed="|Rev|18|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.12" />
<sup>12</sup>hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marmari;
<scripture passage="Rev 18:13" parsed="|Rev|18|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.13" />
<sup>13</sup>mdalasini, viungo, ubani, manemane, udi, divai, mafuta, unga na ngano, ng`ombe na kondoo, farasi na magari ya kukokotwa, watumwa wao na hata maisha ya watu.
<scripture passage="Rev 18:14" parsed="|Rev|18|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.14" />
<sup>14</sup>Wafanyabiashara wanamwambia: "Faida yote uliyotazamia imetoweka, na utajiri na fahari vimekuponyoka; hutaweza kuvipata tena!"
<scripture passage="Rev 18:15" parsed="|Rev|18|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.15" />
<sup>15</sup>Wafanya biashara waliotajirika kutokana na mji huo, watasimama mbali kwa sababu ya hofu ya mateso yake, watalalamika na kuomboleza,
<scripture passage="Rev 18:16" parsed="|Rev|18|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.16" />
<sup>16</sup>wakisema, "Ole! Ole kwa mji huu mkuu. Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi ya zambarau na nyekundu, na kujipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu!
<scripture passage="Rev 18:17" parsed="|Rev|18|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.17" />
<sup>17</sup>Kwa saa moja tu utajiri wako umetoweka!" Halafu manahodha wote na wasafiri wao, wanamaji na wote wanaofanya kazi baharini, walisimama kwa mbali,
<scripture passage="Rev 18:18" parsed="|Rev|18|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.18" />
<sup>18</sup>na walipouona moshi wa moto ule uliouteketeza, wakalia kwa sauti: "Hakujapata kuwako mji kama mji huu mkuu!"
<scripture passage="Rev 18:19" parsed="|Rev|18|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.19" />
<sup>19</sup>Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: "Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!"
<scripture passage="Rev 18:20" parsed="|Rev|18|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.20" />
<sup>20</sup>Furahi ee mbingu, kwa sababu ya uharibifu wake. Furahini watu wa Mungu, mitume na manabii! Kwa maana Mungu ameuhukumu kwa sababu ya mambo uliyowatenda ninyi!
<scripture passage="Rev 18:21" parsed="|Rev|18|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.21" />
<sup>21</sup>Kisha malaika mmoja mwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, "Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
<scripture passage="Rev 18:22" parsed="|Rev|18|22|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.22" />
<sup>22</sup>Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
<scripture passage="Rev 18:23" parsed="|Rev|18|23|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.23" />
<sup>23</sup>Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!"
<scripture passage="Rev 18:24" parsed="|Rev|18|24|0|0" osisRef="Bible:Rev.18.24" />
<sup>24</sup>Mji huo uliadhibiwa kwani humo mlipatikana damu ya manabii, damu ya watu wa Mungu na damu ya watu wote waliouawa duniani.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 19" progress="98.65%" prev="Rev.18" next="Rev.20" id="Rev.19">
<h3 id="Rev.19-p0.1">Chapter 19</h3>
<p id="Rev.19-p1">
<scripture passage="Rev 19:1" parsed="|Rev|19|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.1" />
<sup>1</sup>Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya umati wa watu wengi mbinguni ikisema, "Haleluya! Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Mungu wetu!
<scripture passage="Rev 19:2" parsed="|Rev|19|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.2" />
<sup>2</sup>Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!"
<scripture passage="Rev 19:3" parsed="|Rev|19|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.3" />
<sup>3</sup>Wakasema, "Asifiwe Mungu! Moshi wa moto unaoteketeza mji huo utapanda juu milele na milele!"
<scripture passage="Rev 19:4" parsed="|Rev|19|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.4" />
<sup>4</sup>Na wale wazee ishirini na wanne, na vile viumbe hai vinne, wakajitupa chini, wakamwabudu Mungu aliyeketi juu ya kiti cha enzi wakisema, "Amina! Asifiwe Mungu!"
<scripture passage="Rev 19:5" parsed="|Rev|19|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.5" />
<sup>5</sup>Kisha kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: "Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa."
<scripture passage="Rev 19:6" parsed="|Rev|19|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.6" />
<sup>6</sup>Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumo kubwa, ikisema, "Haleluya! Maana Bwana Mungu wetu Mwenye Uwezo ni Mfalme!
<scripture passage="Rev 19:7" parsed="|Rev|19|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.7" />
<sup>7</sup>Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa arusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari.
<scripture passage="Rev 19:8" parsed="|Rev|19|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.8" />
<sup>8</sup>Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung`aa!" (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watu wa Mungu.)
<scripture passage="Rev 19:9" parsed="|Rev|19|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.9" />
<sup>9</sup>Kisha malaika akaniambia, "Andika haya: Heri wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwanakondoo!" Tena akaniambia, "Hayo ni maneno ya kweli ya Mungu."
<scripture passage="Rev 19:10" parsed="|Rev|19|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.10" />
<sup>10</sup>Basi, mimi nikaanguka kifudifudi mbele ya miguu yake nikataka kumwabudu. Lakini yeye akaniambia, "Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako; sote tunauzingatia ukweli ule alioufunua Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ukweli alioufunua Yesu ndio unaowaangazia manabii."
<scripture passage="Rev 19:11" parsed="|Rev|19|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.11" />
<sup>11</sup>Kisha nikaona mbingu zimefunguliwa; na huko alikuwako farasi mmoja mweupe, na mpanda farasi wake aliitwa "Mwaminifu" na "Kweli". Huyo huhukumu na kupigana kwa ajili ya haki.
<scripture passage="Rev 19:12" parsed="|Rev|19|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.12" />
<sup>12</sup>Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe.
<scripture passage="Rev 19:13" parsed="|Rev|19|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.13" />
<sup>13</sup>Alikuwa amevaa vazi lililokuwa limelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni "Neno la Mungu."
<scripture passage="Rev 19:14" parsed="|Rev|19|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.14" />
<sup>14</sup>Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na walikuwa wamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi.
<scripture passage="Rev 19:15" parsed="|Rev|19|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.15" />
<sup>15</sup>Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Uwezo.
<scripture passage="Rev 19:16" parsed="|Rev|19|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.16" />
<sup>16</sup>Juu ya vazi lake, na juu ya mguu wake, alikuwa ameandikwa jina: "Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana."
<scripture passage="Rev 19:17" parsed="|Rev|19|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.17" />
<sup>17</sup>Kisha nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, "Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu.
<scripture passage="Rev 19:18" parsed="|Rev|19|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.18" />
<sup>18</sup>Njoni mkaitafune miili ya wafalme, ya majemadari, ya watu wenye nguvu, ya farasi na wapanda farasi wao; njoni mkaitafune miili ya watu wote: walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa."
<scripture passage="Rev 19:19" parsed="|Rev|19|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.19" />
<sup>19</sup>Kisha nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi, pamoja na jeshi lake.
<scripture passage="Rev 19:20" parsed="|Rev|19|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.20" />
<sup>20</sup>Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka, pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake.) Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa kiberiti.
<scripture passage="Rev 19:21" parsed="|Rev|19|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.19.21" />
<sup>21</sup>Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 20" progress="99.01%" prev="Rev.19" next="Rev.21" id="Rev.20">
<h3 id="Rev.20-p0.1">Chapter 20</h3>
<p id="Rev.20-p1">
<scripture passage="Rev 20:1" parsed="|Rev|20|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
<scripture passage="Rev 20:2" parsed="|Rev|20|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.2" />
<sup>2</sup>Akalikamata lile joka--nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani--akalifunga kwa muda wa miaka elfu moja.
<scripture passage="Rev 20:3" parsed="|Rev|20|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.3" />
<sup>3</sup>Malaika akalitupa Kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
<scripture passage="Rev 20:4" parsed="|Rev|20|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.4" />
<sup>4</sup>Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumtangaza Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja.
<scripture passage="Rev 20:5" parsed="|Rev|20|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.5" />
<sup>5</sup>(Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka elfu moja itimie.) Huu ndio ufufuo wa kwanza.
<scripture passage="Rev 20:6" parsed="|Rev|20|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.6" />
<sup>6</sup>Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja.
<scripture passage="Rev 20:7" parsed="|Rev|20|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.7" />
<sup>7</sup>Wakati miaka elfu mia moja itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
<scripture passage="Rev 20:8" parsed="|Rev|20|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.8" />
<sup>8</sup>Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
<scripture passage="Rev 20:9" parsed="|Rev|20|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.9" />
<sup>9</sup>Walitawanyika katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watu wa Mungu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza.
<scripture passage="Rev 20:10" parsed="|Rev|20|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.10" />
<sup>10</sup>Ibilisi, aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka moto wa kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.
<scripture passage="Rev 20:11" parsed="|Rev|20|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.11" />
<sup>11</sup>Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena.
<scripture passage="Rev 20:12" parsed="|Rev|20|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.12" />
<sup>12</sup>Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uzima, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.
<scripture passage="Rev 20:13" parsed="|Rev|20|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.13" />
<sup>13</sup>Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; kifo na kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.
<scripture passage="Rev 20:14" parsed="|Rev|20|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.14" />
<sup>14</sup>Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.
<scripture passage="Rev 20:15" parsed="|Rev|20|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.20.15" />
<sup>15</sup>Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 21" progress="99.27%" prev="Rev.20" next="Rev.22" id="Rev.21">
<h3 id="Rev.21-p0.1">Chapter 21</h3>
<p id="Rev.21-p1">
<scripture passage="Rev 21:1" parsed="|Rev|21|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.1" />
<sup>1</sup>Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya. Mbingu ile ya kwanza na dunia ile ya kwanza vilikuwa vimetoweka, nayo bahari pia haikuweko tena.
<scripture passage="Rev 21:2" parsed="|Rev|21|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.2" />
<sup>2</sup>Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
<scripture passage="Rev 21:3" parsed="|Rev|21|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.3" />
<sup>3</sup>Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, "Tazama! Mungu amefanya makao yake kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
<scripture passage="Rev 21:4" parsed="|Rev|21|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.4" />
<sup>4</sup>Yeye atayafuta machozi yao yote; maana hakutakuwako tena na kifo, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!"
<scripture passage="Rev 21:5" parsed="|Rev|21|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.5" />
<sup>5</sup>Kisha yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi akasema, "Tazama, nafanya yote mapya." Tena akaniambia, "Andika hili, maana maneno haya ni ya kuaminika na ya kweli!"
<scripture passage="Rev 21:6" parsed="|Rev|21|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.6" />
<sup>6</sup>Kisha akaniambia, "Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima.
<scripture passage="Rev 21:7" parsed="|Rev|21|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.7" />
<sup>7</sup>Yeyote atakayeshinda atapokea hiki, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
<scripture passage="Rev 21:8" parsed="|Rev|21|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.8" />
<sup>8</sup>Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili."
<scripture passage="Rev 21:9" parsed="|Rev|21|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.9" />
<sup>9</sup>Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, "Njoo! Mimi nitakuonyesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!"
<scripture passage="Rev 21:10" parsed="|Rev|21|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.10" />
<sup>10</sup>Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionyesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
<scripture passage="Rev 21:11" parsed="|Rev|21|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.11" />
<sup>11</sup>uking`aa kwa utukufu wa Mungu. Mwangaza wake ulikuwa kama wa jiwe la thamani kubwa kama yaspi, angavu kama kioo.
<scripture passage="Rev 21:12" parsed="|Rev|21|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.12" />
<sup>12</sup>Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na malaika wanangojea kumi na wawili. Majina ya wangoja milango kumi na mawili ya Israeli yalikuwa yameandikwa juu ya milango hiyo.
<scripture passage="Rev 21:13" parsed="|Rev|21|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.13" />
<sup>13</sup>Kila upande ulikuwa na milango mitatu: upande wa mashariki, milango mitatu, kaskazini milango mitatu, kusini milango mitatu na magharibi milango mitatu.
<scripture passage="Rev 21:14" parsed="|Rev|21|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.14" />
<sup>14</sup>Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya mawe hayo yalikuwa yameandikwa majina na mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
<scripture passage="Rev 21:15" parsed="|Rev|21|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.15" />
<sup>15</sup>Basi, yule malaika aliyekuwa anasema nami alikuwa na kijiti cha dhahabu cha kupimia, kwa ajili ya kuupima huo mji, milango yake na kuta zake.
<scripture passage="Rev 21:16" parsed="|Rev|21|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.16" />
<sup>16</sup>Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa na urefu, upana na urefu wa kwenda juu, kama kilomita elfu mbili na mia nne.
<scripture passage="Rev 21:17" parsed="|Rev|21|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.17" />
<sup>17</sup>Kisha akaupima ukuta wake pia; nao ulikuwa mita sitini kwa kipimo cha macho cha kibinadamu ambacho malaika alitumia.
<scripture passage="Rev 21:18" parsed="|Rev|21|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.18" />
<sup>18</sup>Ukuta huo ulikuwa umejengwa kwa mawe mekundu ya thamani, na mji wenyewe ulikuwa umejengwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
<scripture passage="Rev 21:19" parsed="|Rev|21|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.19" />
<sup>19</sup>Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili yakuti samawati, la tatu kalkedoni, la nne zamaradi,
<scripture passage="Rev 21:20" parsed="|Rev|21|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.20" />
<sup>20</sup>la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, la nane zabarijadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, la kumi na moja yasinto, na la kumi na mbili amethisto.
<scripture passage="Rev 21:21" parsed="|Rev|21|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.21" />
<sup>21</sup>Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulu moja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo.
<scripture passage="Rev 21:22" parsed="|Rev|21|22|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.22" />
<sup>22</sup>Sikuona hekalu katika mji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Uwezo na yule Mwanakondoo ndio Hekalu lake.
<scripture passage="Rev 21:23" parsed="|Rev|21|23|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.23" />
<sup>23</sup>Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.
<scripture passage="Rev 21:24" parsed="|Rev|21|24|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.24" />
<sup>24</sup>Watu wa mataifa watatembea katika mwanga wake, na wafalme wa dunia watauletea utajiri wao.
<scripture passage="Rev 21:25" parsed="|Rev|21|25|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.25" />
<sup>25</sup>Milango ya mji huo itakuwa wazi mchana wote; maana hakutakuwa na usiku humo.
<scripture passage="Rev 21:26" parsed="|Rev|21|26|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.26" />
<sup>26</sup>Fahari na utajiri wa watu wa mataifa utaletwa humo ndani.
<scripture passage="Rev 21:27" parsed="|Rev|21|27|0|0" osisRef="Bible:Rev.21.27" />
<sup>27</sup>Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.
</p>
</div3>

<div3 title="Revelation 22" progress="99.69%" prev="Rev.21" next="toc" id="Rev.22">
<h3 id="Rev.22-p0.1">Chapter 22</h3>
<p id="Rev.22-p1">
<scripture passage="Rev 22:1" parsed="|Rev|22|1|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.1" />
<sup>1</sup>Kisha malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima maangavu kama kioo yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo.
<scripture passage="Rev 22:2" parsed="|Rev|22|2|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.2" />
<sup>2</sup>Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
<scripture passage="Rev 22:3" parsed="|Rev|22|3|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.3" />
<sup>3</sup>Hapana kitu chochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katika mji huo, na watumishi wake watamwabudu.
<scripture passage="Rev 22:4" parsed="|Rev|22|4|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.4" />
<sup>4</sup>Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao.
<scripture passage="Rev 22:5" parsed="|Rev|22|5|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.5" />
<sup>5</sup>Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.
<scripture passage="Rev 22:6" parsed="|Rev|22|6|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.6" />
<sup>6</sup>Kisha malaika akaniambia, "Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
<scripture passage="Rev 22:7" parsed="|Rev|22|7|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.7" />
<sup>7</sup>"Sikiliza! Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki."
<scripture passage="Rev 22:8" parsed="|Rev|22|8|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.8" />
<sup>8</sup>Mimi Yohane, niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuona nikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliyenionyesha mambo hayo, nikataka kumwabudu.
<scripture passage="Rev 22:9" parsed="|Rev|22|9|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.9" />
<sup>9</sup>Lakini yeye akaniambia, "Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!"
<scripture passage="Rev 22:10" parsed="|Rev|22|10|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.10" />
<sup>10</sup>Tena akaniambia, "Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.
<scripture passage="Rev 22:11" parsed="|Rev|22|11|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.11" />
<sup>11</sup>Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu."
<scripture passage="Rev 22:12" parsed="|Rev|22|12|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.12" />
<sup>12</sup>"Sikiliza!" Asema Yesu, "Naja upesi, pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.
<scripture passage="Rev 22:13" parsed="|Rev|22|13|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.13" />
<sup>13</sup>Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho."
<scripture passage="Rev 22:14" parsed="|Rev|22|14|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.14" />
<sup>14</sup>Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, kwani watakuwa na haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
<scripture passage="Rev 22:15" parsed="|Rev|22|15|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.15" />
<sup>15</sup>Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.
<scripture passage="Rev 22:16" parsed="|Rev|22|16|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.16" />
<sup>16</sup>"Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!"
<scripture passage="Rev 22:17" parsed="|Rev|22|17|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.17" />
<sup>17</sup>Roho na Bibiarusi waseme, "Njoo!" Kila mtu asikiaye hili, na aseme,"Njoo!" Kisha, yeyote aliye na kiu na aje; anayetaka maji ya uzima na apokee bila malipo yoyote.
<scripture passage="Rev 22:18" parsed="|Rev|22|18|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.18" />
<sup>18</sup>Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
<scripture passage="Rev 22:19" parsed="|Rev|22|19|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.19" />
<sup>19</sup>Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang`anya sehemu yake katika ule mti wa uzima, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.
<scripture passage="Rev 22:20" parsed="|Rev|22|20|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.20" />
<sup>20</sup>Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: "Naam! Naja upesi." Amina. Na iwe hivyo! Njoo Bwana Yesu!
<scripture passage="Rev 22:21" parsed="|Rev|22|21|0|0" osisRef="Bible:Rev.22.21" />
<sup>21</sup>Nawatakieni nyote neema ya Bwana Yesu. Amen.
</p>
</div3></div2></div1>
</ThML.body>
</ThML>
